Je atashuka tena ardhini kabla ya Kiama kutokea?

The Answer

Dear Brother / Sister,

Yesu Mtakatifu, aliyeumbwa bila ya baba kama muujiza, ni mmoja ya mitume wanne watukufu. Katika umri wa miaka thelathini, alipewa utume; na baada ya miaka mitatu, Allah alimpandisha mbinguni bila ya kufikwa na mauaji ya Wayahudi.

Yesu Mtakatifu, aliyeumbwa bila ya baba kama muujiza, ni mmoja kati ya mitume wanne watukufu. Alipokuwa na umri wa miaka thelathini, alipewa utume; na baada ya miaka mitatu, Allah alimpandisha mbinguni bila ya kufikwa na mauaji ya Wayahudi. Pia anakumbukwa kwa jina la Masihi. Imefafanuliwa kuwa amepewa cheo hiki kwa sababu aliwaponya wagonjwa kwa kuwapangusa, kwa sababu Zakaria alimpangusa yeye, kwa sababu ataipangusa ardhi; yaani ataifunika. Kama ilivyosimuliwa, Yesu Mtakatifu atashuka ardhini tena wakati wa mwisho na atakuwa katika umma wa Mtume Muhammad (S.A.W.)

Madai kuwa Yesu Mtakatifu alisulubiwa.

Tukiangalia Injili ya wakati wa sasa, haiwezekani kukuta mtazamo kuhusu makubaliano yaliyokuwepo. Kwa mujibu wa Agano Jipya, Yesu Mtakatifu alikumbana na vikwazo katika kazi yake ya kisheria na haki, alishutumiwa kuchochea jamhuri na kwa kung’ang’ania madai ya Wayahudi ili wamtundike msalabani, na Gavana wa sita wa jimbo la Yahudiya wa Ufalme wa Roma, Pilato walimtundika msalabani. Katika Injili ya Luka, imeelezwa kuwa Pilato alitii utashi wa Wayahudi (1) na kwamba alilazimika kumhukumu kifo Yesu Mtakatifu katika mahakama ya juu ya kidini ya Wayahudi, Sanhadrin.

Kwa mujibu wa Injili, inasimuliwa kuwa eneo la Yesu Mtakatifu halijulikani, lakini Yuda Iskariot, aliyekuwa mmoja ya Wanafunzi 12, alitaja pahala pake kwa kiwango kichache mno cha sarafu 30 za fedha na Allah alimfananisha umbo lake na Yesu Mtakatifu.

Mwisho wa Yesu Mtakatifu, hata hivyo, unabishaniwa baina ya Wakristo. Ilhali ni mtazamo mashuhuri kuwa alisulubiwa, pia wapo Wakristo wanaopinga hakusulubiwa, kama vile madhehbu ya Cerinthi na Tatianos. George Sale, aliyefasiri Quran kwa Kiingereza, anasema, “Ingawa baadhi ya Wakristo wanasema kuwa mtazamo kwamba Yesu Mtakatifu hakusulubiwa, ulibuniwa na Mtume Muhammad, hili sio kweli. Madhehebu kama vile Basilid, Cerinthi na Carpocrati walikuwa na maoni hayo hayo hapo kabla. Katika kazi yake Safari za Wajumbe, Photius alisema kuwa maelezo haya yameandikwa: ‘Yesu Mtakatifu hakusulubiwa; mtu mwengine alisulubiwa badala yake. Kwa sababu ya hili, aliwakebehi wale waliomsulubu.”

Baadhi ya Wakristo, ingawa, wakiamini kwamba alisulubiwa katika wakati wa Pilato na kisha alifufuliwa na kupandishwa hadi mbinguni. Iskariot, aliyeonesha pahala alipo, aliomba msamaha kwa usaliti wake na kufanya mauaji. Wakristo wamegawika katika makundi matatu kuhusu suala hili. Kundi linaloitwa Melkaiye linaamini kuwa Yesu Mtakatifu alisulubiwa kiwiliwili na roho, lakini kifo chake hakikuiathiri roho yake moja kwa moja, kiasi cha hisia na mguso. Kundi jengine linaitwa Yakubiya linasema kuwa asili ya Masihi liliundwa kwa asili mbili amesulubiwa; na kundi la tatu linaitwa Nasuri linaamini kuwa aliuliwa kimwili; lakini nafsi yake ilipaishwa mbinguni. (3)

Hatma ya Yesu Mtakatifu katika Qur’an:

Mitazamo ya Injili na Wakristo kuhusu mwisho wa Yesu Mtakatifu ni mifupi kama ilivyofafanuliwa hapo juu. Qur’an inaweka wazi na kuchambua ufafanuzi kuhusu suala hili. Baadhi ya aya kuhusu suala hili:

“Na Makafiri walipanga mipango na Mwenyezi Mungu akapanga mipango, na Mwenyezi Mungu ndiye mbora wa wenye kupanga.”

“Pale Mwenyezi Mungu alipo sema: Ewe Isa! Mimi nitakufisha, na nitakunyanyua kwangu, nitakutakasa na wale walio kufuru, na nitawaweka wale walio kufuata juu ya wale walio kufuru, mpaka siku ya Kiyama.” (4)

Katika aya nyengine, suala hili limefafanuliwa zaidi na inaelezwa:

“Na kwa kusema kwao: Sisi tumemuuwa Masihi Isa, mwana wa Maryamu, Mtume wa Mwenyezi Mungu – nao hawakumuuwa wala hawakumsalibu, bali walifananishiwa tu. Na hakika walio khitalifiana katika haya wamo katika shaka nayo. Wao hawana ujuzi nayo wowote, ila ni kufuata dhana tu. Wala hawakumuuwa kwa yakini.”

“Bali Mwenyezi Mungu alim-tukuza kwake, na hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu, Mwenye hikima.” (5)

Katika aya, inafafanuliwa wazi kuwa Yesu Mtakatifu hakusulubiwa, lakini mtu mwengine alisulubiwa kimakosa. Wanazuoni wamefafanua aya hii kama ifuatavyo: Wayahudi walipokwenda kwa Yesu Mtakatifu kwa kusudi la kumuua; hawakumkuta, kwa sababu Allah Mtukufu alimpaisha mbinguni. Wayahudi walipatwa na wasiwasi na kuogopa kuwa jamhuri ingeingilia kati na hivyo walimkamata mtu na kumtundika msalabani kuwa ndio Yesu Mtakatifu. Ingawa jamhuri ilimjua kwa jina mtu aliyesulubiwa, lakini hawakumjua kwa kumuona.

Kwa mujibu wa mtazamo mwengine, Wayahudi wamejifunza kuwa Yesu Mtakatifu alikuwa kwenye nyumba na walikwenda huko ili kumuua. Kiongozi wao Yahuda alimtuma mtu aliyeitwa Taytayus ndani ili kumuua Yesu. Allah Mtukufu alimpaisha Yesu Mtakatifu mbinguni na akamfanya mtu huyu kufanana naye; na Wayahudi wakamsulubu mtu huyu badala ya Yesu Mtakatifu.

Mbali na masimulizi haya, inahusishwa kuwa mmoja ya wanafunzi wa mtume ametengeneza fitina na akafanya ujasusi; na kisha Allah akamfananisha na Yesu kuwa ndio adhabu na baadaye akasulubiwa.

Masimulizi haya yanaonesha waziwazi kuwa Wayahudi waliojaribu kumuua Yesu Mtakatifu hawakufanikiwa na Allah alimwokoa kutokana na mashambulizi yao na kumpaisha mbinguni.

Kushuka kwa Yesu Mtakatifu ardhini

Umma wa Mohammad (S.A.W.) ni umma uliosifika katika namna nyingi. Wamesifiwa kote katika Quran na maandiko mengine mbalimbali.

Yesu alipoona ubora wa sifa za jumuia hii, alimwomba Allah kumfanya awe mmoja kati yao na Allah akalikubali ombi lake. Ni kwa sababu hii kwamba wakati utakapofika, atashuka ardhini kuwa ni mucaddid-mwana mambo leo wa dini. (6)

Wasomi wamehitimisha kuwa imeasisiwa kupitia Kitabu, misemo-ya-Sunnat za Mtume Mohammed (S.A.W.) na makubaliano kati ya wanazuoni kwamba Yesu Mtakatifu atashuka ardhini (7) na kwamba hili limekuwa ni suala la imani iliyoegemea kwenye hadithi bora na kuwa yeyote anayekanusha, atahukumiwa kuwa ni kafiri. (8)

Kwa mujibu wa Shawkani, hadithi zinazotangaza kushuka kwa Yesu ardhini ni kiasi cha 29 na zimefikia hadhi ya kuwa hadithi nzuri (9). Upo usajili huo huo katika Sahihi Muslim (10). Anasema:

“Kama hadithi iliyosimuliwa kuhusu Mahdi mtarajiwa na Dajjal, hadithi kuhusu kushuka kwa Yesu mwana wa Mariyamu zimefikia hadhi ya kuwa nzuri.” (11)

Katika ufafanuzi wa Quran uliofanywa na Ibn-i Kasir, ilhali ukweli kuwa Yesu Mtakatifu ni dalili ya siku ya Kiama, ambayo imetajwa katika aya ya 61 ya sura Az-Zukhruf, inafafanua; inaelezwa kuwa masimulizi yanatangaza kuwa atateremshwa kabla ya kusimama Kiama zimefikia hukumu ya kuwa ni sahihi. Sheikh Abdulfettah Abu Gudde pia anaeleza kuwa masimulizi yanayoripoti kuwa Yesu Mtakatifu atashuka ardhini na atamuua Dajjal, zimekuja kwenye hukumu ya sahihi (12). Inaonekana katika Nazmu’ul-Mutanasir kilichoandikwa na msomi Muhaddith-mwanazuoni wa hadithi- Kittani (13) kuwa anaunga mkono mitazamo hiyo hiyo.

Katika kitabu cha Fathu’ul Bari kilichoandikwa na Ibn-I Hacer, pia, kuna kisa kuwa hadithi zinazoeleza kuwa Mahdi atakuwa ni miongoni mwa jumuia hii na kwamba Yesu Mtakatifu atasali nyuma yake ni hadithi sahihi (14).

Katika utunzi wake Sherhu’l-Makasid, Sadeddin Taftazani pia anaeleza kuwa zipo hadithi nyingi kuhusu kushuka kwa Yesu na kuwa ni hadithi sahihi kimaana. (15)

Tunaona kuwa katika baadhi ya hadithi na aya, dalili za Wakati wa Mwisho zimefafanuliwa. Zimekusanywa chini ya anwani ‘Dalili za Saa ya Mwisho.’ Moja ya dalili hizi ni kushuka kwa Yesu Mtakatifu ardhini. Kwa maneno mengine, Yesu Mtakatifu atashuka ardhini kabla ya kusimama kiama. Moja ya aya zake, Allah Mtukufu anasema, “Kwa hakika (Yesu) ameletwa duniani bila ya baba, na kumpa miujiza kama vile kumfufua mfu) ni dalili ya kuijua Saa ya Mwisho.” (16) na kwa hivyo inaonesha ukweli huu. Katika hadithi nyingi, Mtume Muhammad (S.A.W.) pia amejulisha kuwa Yesu Mtakatifu atashuka ardhini. Baadhi ya hizo ni kama ifuatavyo:

“Hakitosimama Kiama mpaka muone dalili kumi… Moja ya hizo ni kushuka kwa Yesu Mtakatifu…” (17)

“Naapa kwa Allah ambaye maisha yangu yapo kwenye mkono wake wenye Nguvu kuwa ni karibu mno kwa Yesu mwana wa Mariyamu kushuka kuwa ndio mtawala mwadilifu miongoni mwenu.” (18)

Kama inavyojulikanwa, Yesu Mtakatifu yupo mbinguni katika tabaka la tatu la maisha. Hahitaji kula wala kunywa kama sisi na hahitaji mahitaji ya wanadamu wengine; na anaongoza maisha ya nuru kama nyota na malaika. Kwa mujibu wa habari njema zilizotolewa na Mtume: “Yesu Mtakatifu atakuja wakati wa mwisho; atatekeleza shari’a ya Muhammad.” (19), atakuja ardhini katika hali ya binadamu.

Kama hekima ya kiungu inavyosisitiza kuwa atashuka ardhini, hivyo lazima atimize baadhi ya majukumu muhimu. Hebu tuyaorodheshe baadhi yake:

Shughuli za Yesu Mtakatifu

a. Yeye Kumfuata Mahdi

Atakapokuja Yesu Mtakatifu, atatekeleza Shari’a za Kiisilamu. Mjumbe wa Allah, anasema, “Kama Yesu Mtakatifu angekuwa hai, asingefanya chochote isipokuwa kunifuata mimi.” (20), inaeleza waziwasi katika moja ya hadithi zake iliyohusishwa na Muslim kuwa yeye atazifuata Sunnah za Mtume Muhammad (S.A.W.). (21)

Imam-An-Nawawi anasema: “Yesu Mtakatifu hatokuja kuwa ni mtu tofauti katika jumuia ya Muhammad, lakini atakuja ili kuendeleza Shari’a ya Muhammad.” (22).

Imam Rabbani pia anasema kuwa Yesu Mtakatifu atashuka ardhini na kuifuata Shari’a ya Muhammad, mtume wa mwisho. (23)

Kadi Ilyas pia anaonesha kuwa imeasisiwa na hadithi zilizothibitishwa kuwa atakuja ili kufufua kanuni za Shari’a zilizoachwa na jamhuri ya watu. (24)

Kama inavyojulikanwa, Mtume Muammad (S.A.W.) ndio muhuri wa mitume, yaani, mtume wa mwisho. Na hii ndio hali, inaweza tu kudhaniwa kuwa Yesu Mtakatifu atakuja sio kuwa ni mtume mpya, bali kama ni mfuasi wa Mtume Muhammad (S.A.W.) na kwamba atatekeleza kwa mujibu wa Shari’a ya Muhammad. Wasomi wanasema:

 “Yesu Mtakatifu analo jukumu la kufufua na kuitekeleza Shari’a ya Muhammad. Mtume pekee wa kutekeleza Uisilamu ni Yesu Mtakatifu. Atakuja wakati ambao dini itakuwa duni na kupuuzwa; atatimiza wajibu wake kama ni mtawala mwadilifu. Kabla hajatumwa ardhini, ameshaandaliwa kwa kila uwanja wa elimu kuhusu Uisilamu chini ya hali halisi ya wakati huo na atakapokuja, atayatekeleza.” (25)

Hadithi zinazoeleza kuwa Yesu Mtakatifu atasali nyuma ya Mahdi (26) ambazo zina hadhi ya hadithi sahihi pia zinaonesha kuwa ataufuata Uisilamu. Yapo masimulizi mengi kuhusu suala hili. Baadhi ya hayo ni kama ifuatavyo:

“Mahdi atakuwa imam; na Yesu Mtakatifu atamfuata yeye, yaani, atasali hali ya kuwa Mahdi anasalisha” (27)

Katika hadithi nyengine iliyosimuliwa katika vitabu vya Bukhari na Muslim, inaeleza kuwa:

“Utafanyaje kama Yesu mwana wa Mariyamu atakuja miongoni mwenu na kumfuata yeye katika sala, ilhali imam wenu ni mtu miongoni mwenu?” (28)

Katika hadithi iliyopo katika Musnad, ambayo Ahmad amesimulia kutoka kwa Jabir, inaeleza:

Wakati Yesu Mtakatifu alipopendekezewa kusalisha akasema, “ongoza sala, ewe Roho ya Allah!” atasema: “mwacheni imamu wenu atangulie mbele na kusalisha.” (29)

Moja ya masimulizi kuhusu maudhui hii, inaelezwa:

“Katika umma huu, kwa hakika kutakuwepo na kundi linapigania ukweli mpaka wakati ambao Yesu mwana wa Mariyamu ataingia Nyumba Takatifu wakati wa alfajiri. Yesu mwana wa Mariyamu atakuja pembeni ya Mahdi. Ataambiwa, ‘tangulia mbele, ewe mtume wa Allah! Salisha!” Atajibu; ‘Hapana, kwa baraka kutoka kwa Allah, nyinyi mmefanywa ndio watawala juu ya wengine’” (30)

Katika hadithi iliyotoka kwa Ibn Maja, iliyoripotiwa na Abu Umama, inaeleza; pindi imamu atakapoongoza sala – itapendekezwa kwa Yesu Mtakatifu, atasema, “Nyinyi tangulieni mbele; jukumu hili mmepewa nyinyi”

Masimulizi mengine kuhusu suala hili ni haya:

“Wakati Mahdi anasali sala ya asubuhi pamoja na waumini, atampendekeza Yesu, ambaye hivi punde tu ameshuka, kusalisha, na Yesu Mtakatifu ataweka mkono wake katika mabega yake na atasema ‘maandalizi ya wito wa qamat kwa ajili ya kusali – yametolewa kwa ajili yenu; basi utaongoza’ na mwishowe Mahdi ataongoza sala kuwa ndio imam kwa Yesu Mtakatifu na waumini.” (31)

Katika Maelezo ya Fiqhu’l Akbar Aliyyu’l-Kari, suala hili limeelezewa wazi zaidi:

“Yesu Mtakatifu atakutana na Mahdi. Wakati huo huo, sala itasimamishwa. Mahdi atamwashiria Yesu Mtakatifu kusalisha, lakini Yesu atatoa udhuru akisema ‘Sala hii inasimamishwa kwa ajili yenu’ na atasema; Nyinyi mnastahiki kuongoza sala hii zaidi kuliko mimi.’ Ili liwe wazi zaidi Yesu Mtakatifu ataifuata Shari’a ya Mtume Muhammad (S.A.W.), atamfuata Mahdi (katika sala), na kwa hivyo watasali pamoja.” (32)

Masimulizi yote haya yanaeleza kuwa ‘Yesu Mtakatifu atamfuata Mahdi katika sala’ yanaonesha kuwa atajisalimisha kwa Uisilamu. Kwa maneno mengine, Yesu Mtakatifu hatokuja na dini mpya. Isitoshe, yanaonesha pia muunganiko kati ya Ukristo na Uisilamu; na mapatano na mamlaka ya ukweli wa Qur’an. (33)

Nukta nyengine kwa Yesu Mtakatifu kutekeleza Shari’a ya Muhammad (S.A.W.) ni hii:

“Katika zama za mwisho, Yesu (amani iwe juu yake) atakuja na atatenda kwa mujibu wa Shari’a ya Muhammad (S.A.W.),” kunaashiria kuwa wakati wa mwisho dini ya Ukristo itatakaswa na itajivua na ushirikina mbele ya sura ya ukafiri uliopo na imani ya kumkana Mungu iliyotokana na falsafa ya Uasilia, na itabadilishwa kuwa Uisilamu. Katika nukta hii, kama ilivyo haiba jumla ya Ukristo itaiua haiba jumla ya kutisha ya upingaji dini kwa Ufunuo wa upanga wa mbinguni, hivyo pia, kunawakilisha haiba jumla ya Ukristo, Yesu (amani imshukie) atamuua Dajjal, anayewakilisha haiba ya jumla ya upingaji dini, yaani, ataiua dhana ya kumkana Mungu.” (34)

b. Kuusafisha kwake Ukristo kutokana na ushirikina

Wajibu mwengine muhimu wa yesu Mtakatifu ni kuutakasa Ukristo kutokana na ushirikina, hususani utatu, na kulibadilisha hili kuwa kumpwekesha Allah. Kwa sababu haitowezekana kwa watu mbele ya maendeleo katika elimu na utu na hisia za ustaarabu, kuichukua haki na ukweli kuwa ndio msingi ili Ukristo uendelee katika muundo wake wa awali. Pia itatoweka au kurudi katika muundo wake wa asili na kutakaswa kutokana na ushirikina.

Ilhali Ukristo, ambao unapitia mageuzi kadhaa, kwanza utaangukia kwenye kuabudu masanamu na ukengeukaji uliotopea, baadhi ya watu watakuwa karibu mno na kumpwekesha Allah na wataanza kumupua. Kuanzia Vita vya Kwanza na vya Pili na kuendelea, Ukristo, uliopitia mabadiliko kadhaa hususan miaka ya mwishoni, umekuwa ukipitia maumivu ya mpito kutoka utatu kuja katika kumpwekesha Allah. Gazeti la ‘Ukweli wa Wazi’ linalotolewa na kundi la Kikristo na kuwahutubia watu milioni nane linaweza waziwazi kusema kuwa utatu uliongezwa katika Ukristo hapo baadaye. Wachamungu wengi wa Kikristo wanaweza kueleza kuwa hawakusita kuufahamu utume wa Muhammad (S.A.W.). Je hili halioneshi kuwa masafa makubwa yamezibwa kwa namna hii kwamba hata katika eneo kama Vatikani, mkuu wa Kitengo cha Mahusiano pamoja na Waisilamu, kwa jina ni Michael Lelong, anafafanua hivi waziwazi?

d. Kutokomeza kwake ukafiri

Yesu Mtakatifu ataendesha vita vyenye changamoto dhidi ya ukafiri. Ukafiri hauwezi kupata nguvu wenyewe ili kusimama wima dhidi yake. Kwa mujibu wa hadithi, “kila kafiri atakayeipata pumzi yake atakufa; na pumzi yake itafika hadi nukta ya mbali zaidi katika upeo wa macho.” (35) Kwa maneno mengine, kama alivyochukua ukweli wenye nguvu wa Uisilamu kuwa ndio chanzo chake, hakuna mtazamo wa ukafiri utakaoungwa mkono dhidi ya ukweli huu ulio sahihi, na mwishowe utalazimika kutoweka.

Yesu Mtakatifu kuufuta ukafiri kunamaanisha kuwa atamwangamiza Dajjal ambaye ndiye mwakilishi wa ukafiri na mfumo wake wa mbovu-mbovu uliogemea kwenye ukafiri na haiba yake jumla.

c. Kuanzisha kwake amani

Yesu Mtakatifu, atakayeishi ardhini kwa miaka arubaini kama ni kiongozi mwadilifu (36), pia ataanzisha amani – na kwa kuwa amani huwekwa – watu watatumia panga kama ni fyekeo. (37)

Katika zama zake, mapanga yatawekwa kwenye ala zake na hakutokuwa na haja ya kutumia silaha.

Wakati Yesu Mtakatifu anafuta ukafiri, ambao ndio chanzo cha kila aina ya uovu, akiwa anaishi ardhini, ataweka imani, ambayo ndio chanzo cha mazuri yote, katika pahala pake. Hivyo, haki, usawa, wingi wa neema, amani na furaha, ambavyo ndio nyenzo za imani, vitanawiri. Ukweli huu kila nukta imeelezwa kwenye masimulizi. Atakapokuja, “uadui, mapigano, na choyo vitatoweka” (38), mazingira ya amani ya kweli na furaha yataundwa, na “ile sijida moja tu itaonekanwa kuwa na thamani mno kuliko dunia na vilivyomo ndani yake.” (39)

Katika wakati huo, watu wataimarika, imani zao zitakuwa thabiti, na watakimbilia kufanya amali njema kwa kiasi ya kuwa watathamini zaidi sijida moja kuliko dunia na kila kilichomo ndani yake. (40)

Hadithi hii pia inavutia mno katika kuonesha mazingira ya kiroho ya wakati huo:

“Yesu mwana wa Mariyamu atakuwa ni katika umma wangu; atakuwa ni kiongozi mwadilifu na imam. Atavunja msalaba na atamuua nguruwe. Ataondosha jizya-kodi inayotozwa kwa Wasiokuwa Waisilamu chini ya utawala wa Kiisilamu-, na hatoigusa zakat- ugavi wa moja ya arobaini ya pato la mtu kuwa ndio zaka inayotekelezwa na Waisilamu (moja ya nguzo tano za imani ya Kiisilamu). Hakuna tena msimamizi wa zakat atakayesajiliwa upya kwenye mifugo ya kondoo, mbuzi na ng’ombe au ngamia. Uadui na chuki vitaondoshwa. Wanyama wote wenye sumu wataondoshwa. Halikadhalika, mtoto mdogo wa kiume ataweka mkono wake katika kinywa cha nyoka, lakini hatomdhuru. Mbwa mwitu watakuwa kama kondoo katika zizi la kondoo na mbuzi. Kama vile bakuli lililojazwa maji, hivyo ndivyo dunia itakavyokuwa na amani. Pia kutakuwa na muungano wa dini na hakuna yeyote atakaeabudiwa tena isipokuwa Allah. Zana za vita (silaha na nyenginezo) zitatelekezwa.” (41)

Masimulizi mengine yaliyopo kwa Muslim, inasemwa: “ataua nguruwe, atavunja msalaba na ataondosha jizya” (42)

Kuvunja msalaba kama ilivyoelezwa katika masimulizi haya na mengine kunaashiria kuwa Yesu Mtakatifu atautakasa Ukristo kutokana na ushirikina ambao umeichanganya mantiki, sayansi na ukweli na ambao Ukristo umegeuzwageuzwa. Hivyo, ataurejesha kwenye Uisilamu na kuuokoa dhidi ya utatu.

Ya kwamba ataondosha jizya kunaonesha kuwa katika wakati huu, kutakuwa na baraka ya mali. Atakapokuja, mali zitakithiri kwa kiwango ambacho hakutokuwa na haja ya hata kuchukua jizya. Pia baadhi wanafasiri kuwa watu wataukubali Uisilamu; kwa sababu jizya hawatozwi Waisilamu.

Maelezo hayo ni kama vile ‘sumu itatolewa kutoka kwa wanyama wenye sumu’, ‘mbwa mwitu na mwanakondoo wataranda pamoja’ ni alama za mazingira ya amani; kama ilivyo katika maneno ‘silaha na zana za vita zitatelekezwa.’

d. Kumuua kwake Dajjal

Moja ya mafanikio makubwa ya Yesu Mtakatifu ni kumuua Dajjal. Atalikamisha hili pamoja na Mahdi.

Kiasi cha kuibuka Dajjal na harakati zake ni kukubwa mno, kuuliwa kwake ni muhimu na kunafurahisha pia.

Kama inavyosimuliwa, wakati Mtume Muhammad (S.A.W.) alipopanda kwenda Miraj, alizungumza na Yesu; alipotajwa Dajjal, Yesu alisema:

“Mola wangu Mlezi ameniarifu kuwa Dajjal ataibuka. Nitachukua mishale miwili iliyotengenezwa kwa mti wa kadib. Dajjal atakapowaona, atayeyuka kama risasi.” (43)

Mtume Muhammad (S.A.W.) ameutangaza ukweli huu:

“Wakati Dajjal, ambaye ni adui wa Allah, atakapomwona Yesu Mtakatifu, atayeyuka kama vile chumvi inavyoyeyuka katika maji. Hata kama Yesu Mtakatifu atamwacha tu, atayeyuka hadi kuteketea kabisa. Hata hivyo, Allah atamuua kwa mkono wa Yesu Mtakatifu mwenyewe. (44)

Masimulizi mengine ni kama ifuatavyo:

“Yesu Mtakatifu atashuka kutoka mbinguni, atamuua Dajjal au atamsaidia Mahdi kumuua huyo Dajjal.” (45)

“Mahdi ataibuka pamoja na Yesu Mtakatifu; watamuua Dajjal katika viunga vya Palestina katika eneo la Bab-i Ludd; au atamsaidia Mahdi kumuua Dajjal.” (46)

Vipi ukweli huu utajidhihirisha wenyewe?

Kwanza, Dajjal ataibuka, na ataanza kufanya harakati zake alizozipanga hatua kwa hatua. Kisha kipindi cha machungu kitaanza. Siku za songombingo zitapitiwa. (47)

Katika zama zake, waumini watasumbuka kwa matatizo makubwa na ukame. Watalazimishwa kukimbilia Pass ya Afiq au kwenye Mlima wa Duhan mjini Damaskas. Kwa hivyo, katika kipindi hicho, Yesu Mtakatifu atakuja katika wakati wa Sala ya Asubuhi; Dajjal atakapomwona, atayeyuka kama inavyoyeyuka risasi. (48)

Pia inavutia kuwa eneo ambalo Dajjal atauliwa ni eneo la Pass ya Afiq. Yesu Mtakatifu atapigana na Shetani huko; na mwishowe kwa msaada wa Allah, atashinda. Atamshinda Dajjal katika eneo hilo hilo na kwa mtindo huo huo. (49)

Yesu mwana wa Mariyamu atashuka juu ya mnara katika Mashariki ya Damaskas, mikono yake miwili ipo juu ya mabega ya malaika. Kila kafiri ikimfikia pumzi yake tu atakufa. Pia atamsaka Dajjal na atamuua katika lango la Ludd. (50)

Kama ambavyo Ibn-i Kathir anafafanua, Yesu Mtakatifu atauwakilisha ukweli. Muda utafika; ukweli utakuwa na nguvu kupitia yeye na utaushinda u-Dajjal. Lango hilo la Ludd limetajwa mahususi katika hadith kuonesha kuwa Uisilamu utawashinda Wayahudi (Dajjal pia ni Myahudi); kwa sababu Wayahudi, katika duara kubwa, wanauwakilisha u-Dajjal na Ludd iko chini ya utawala wao. (51)

Dajjal Mkubwa, atakayesafiri maeneo mbalimbali duniani ili kuamsha fitina na kuanzisha utawala, na atakayeonesha maajabu fulani aliyotunukiwa na Allah ili kuongoza njia iliyopinda, hatoweza kumtoroka Yesu Mtakatifu.

Masimulizi yanaonesha kuwa Dajjal, atayebadilikabadilika kiroho popote atakapokanyaga na wowote atakaowatembelea na atawafanya kuwa ndio nyenzo za uharibifu kwa maisha ya kijamii na wafwasi wake hawatoweza kuendelea mbali na harakati zao na watajaribu kuyahifadhi matukio katika hatua ya nne. Yesu Mtakatifu atamshughulikia. Atamuua Dajjal Mkubwa.

Hili litatokea vipi?

Kama inavyoelezwa na Bediüzzaman, kuna namna mbili ya hili:

Namna ya kwanza: atakuwa ni mtu wa ajabu akiwa na nguvu za kimiujiza ambazo zitaweza kuua na kubadilisha njia ya Dajjal wa kutisha, atakayejihifadhi kupitia maajabu, aliyotunukiwa na Allah ili kumtoa (Dajjal) nje ya mstari, kama ulivyo uchawi nguvu za mazingaombwe, na hali ya kiroho, atamvutia kila mmoja. Na mtu huyo atakuwa ni Yesu (Amani imshukie), ambaye ni mtume wa watu wengi, na ambaye watu wengi watamfuata.

Namna ya pili ni hii: watakuwa ni wafwasi wachamungu wa kweli wa Yesu watakaoiua haiba ya mkusanyiko mkubwa mno ya uyakinifu na ukosefu wa dini ambayo Dajjal atauunda – kwa kuwa Dajjal atauliwa na Yesu’ (A.S.) upanga – na kuyaharibu mawazo yake na ukafiri, ambavyo ni kumkana Mungu. Wale wachamungu wa Kikristo watachanganya uasili wa Ukristo wa kweli pamoja na uasili wa Uisilamu na kumshinda Dajjal na nguvu zake zilizomkusanyikia, kwa kweli atamuua. Simulizi: “Yesu (amani imshukie) atakuja na atatekeleza sala za faradhi nyuma ya Mahdi na kumfuata,” kunaashiria muungano huu, na mamlaka ya Qur’an na kufuatwa kwake.  (52)

Dini ya Ukristo itasonga mbele kuelekea kwenye imani ya Mungu mmoja, itakayokuwa imeokolewa dhidi ya imani ya utatu wa Mungu; itatakaswa dhidi ya ushirikina na upuuzi, itageuzwa kuwa Uisilamu, itaitii Quran na kuufuta mtazamo wa upingaji dini kwa kufaidika na nguvu kubwa ya pamoja.

Hata hivyo, kila kitu kitatokea kutokana na mzunguko wa sababu mbalimbali; kwa sababu tunaishi katika dunia ya sababu mbalimbali. Isitarajiwe kuwa hili litatokea katika mfumo wa kawaida. Sio amali zote hata zile za Mtume Muhammad (S.A.W.) zilikuwa zikistaajabisha. Alikuwa akionesha miujiza mara moja moja na ilipohitajika, na alikuwa na tabia za kawaida katika muda mwengine. Baadhi ya wakati alikuwa na njaa, na wakati mwengine alipambana na ugumu.

Hatupaswi tutarajie harakati zote hizo za Yesu Mtakatifu zitakuwa ni matendo yasiyo ya kawaida. Ni hakika kuwa ataonesha maajabu ikihitajika. Hata hivyo, nyakati nyengine, atayachukulia matokeo yanayojiri katika nyakati kwa mazingatio na atatenda kwa njia mwafaka. Katika mtindo sahihi; na katika eneo sahihi na wakati.

Kama inavyojulikana kuwa Dajjal ni mwakilishi wa ukosefu wa dini, kwamba anayo kamati, mfumo na serikali na kuwa haya yamejidhihirisha wenyewe kuwa ni ukomunisti; isisahaulike kuwa mapambano makubwa ya Yesu Mtakatifu yatakuwa dhidi ya upingaji dini, ukafiri, na ukomunisti.

Kwa hivyo, je Yesu Mtakatifu ataondosha mfumo wa upingaji dini na nadharia yake? Hukumu kutoka katika aya ya sura An-Nisa: “Na hawi katika Watu wa Kitabu ila hakika atamuamini yeye kabla ya kufa kwake. Naye Siku ya Kiyama atakuwa shahidi juu yao.” (53) Baadhi ya wanazuoni-wafasiri waliofafanua aya za Qur’an – wanaeleza kuwa Watu wa Kitabu watamwamini Yesu Mtakatifu. Katika ufafanuzi wa aya hii, Aliyyu’l-Kari anasema kuwa Yesu Mtakatifu atakaposhuka ardhini, dunia nzima itakuwa ni jumuia moja ya Uisilamu (54). Mehmed Vehbi Efendi, pia, anasajili kuwa atakapoibuka Dajjal, Yesu Mtakatifu atashuka kutoka mbinguni na kumuua; na kisha umma zote zitamwamini Yesu Mtakatifu na dunia nzima watakuwa ni watu wa dini ya Uisilamu. (55)

Mnamo wakati wa mwisho, ambapo uyakinifu na uasili vitapopata nguvu na kuzaliana sana, na kuja kwenye nukta ya kumkana Allah na ambapo Dajjal mwenyewe ataongoza kamati hii; Yesu Mtakatifu ataanza jukumu lake. Wakati ambapo kundi hili linamkana Allah na dini; dini ya kweli ya Ukristo itakayokusanya haiba yake ya jumla ya Yesu (amani imshukie) itaanza mapambano dhidi ya wimbi hili la kotukuwa na dini. Kwa kuunganika pamoja na Mahdi, watamuua Dajjal. Kwa maneno mengine, Ukristo, utakaotakaswa kutokana na ushirikina, na Uisilamu utafikia makubaliano na kuiua nadharia ya Dajjal ya ukafiri.

Bediüzzaman anafafanua hali hii kwa maneno yake mwenywe:

“Katika nukta hiyo wimbi hilo litakapotokea kuwa na nguvu, dini ya Ukristo wa kweli, itakayokusanya haiba jumla ya Yesu (amani imshukie), itaibuka. Yaani, itashuka kutoka mbingu ya Rehema ya Kiungu. Ukristo uliopo utatakaswa mbele ya ukweli; utauweka kando ushirikina na ugeuzwaji, na kuunganika pamoja na ukweli wa Uisilamu. Ukristo wakati huu utabadilishwa kuwa ni namna ya Uisilamu. Kuifuata Qur’an, haiba jumla ya Ukristo itakuwa katika hadhi ya mfuasi, na Uisilamu, kutokana na kiongozi huyo. Dini ya kweli itakuwa na nguvu kutokana na kuunganika nayo. Ingawa kushindwa kutatokea kabla ya wimbi la kumkana mungu japo kuwa imejitenga, Ukristo na Uisilamu zitakuwa na uwezo wa kuishinda kutokana na muungano wao. Kisha Yesu (amani imshukie), ambaye yupo katika umbo lake la kibinadamu katika dunia ya mbinguni, atakuja kuongoza wimbi la dini ya kweli, kuwa ni, ya kutegemewa juu ya ahadi ya Mmoja Mwenye Nguvu Juu ya Kila Kitu, Mletaji wa Habari za Uhakika alivyosema. Kwa kuwa ameshaliambia hilo, basi ni kweli, na kwa kuwa Mwenye Nguvu Muweza wa Kila Kitu ameshaahidi, kwa hakika atalitimiza.” (56)

“Muungano unastahiki cheo cha ‘Waisilamu Wakristo’ ambayo ni taasisi ya Wakristo ya kujitolea muhanga-yenyewe itajaribu kuibua dini ya kweli ya Yesu Mtakatifu pamoja na ukweli wa Uisilamu itakuwa-chini ya amri ya Yesu Mtakatifu-kuiua na kuisambaratisha kamati ya Dajjal inayoharibu ustaarabu na thamani tukufu ya utu kwa kusudi la kumkana Allah; na itauokoa utu kutokana na kumkafiri Allah.” (57)

Maudhui ya uhakika sio kumuua Dajjal yeye mwenyewe hasa, ambaye anaweza kufa kwa sababu ya virusi; lakini kuua ustadi wake na mfumo wa ukafiri aliouzusha. Nukta hii inawekwa wazi katika Mionzi kutoka katika Mkusanyiko wa Risale-i Nur.

“Pia, kwa kuwa matukio mageni ya ajabu na harakati za kutisha za serikali ya Kumpinga Mtakatifu, na taasisi iliyojificha na serikali aliyoiasisi, vimesimuliwa kama inavyorejea kwake yeye mwenyewe, maana yao ya kweli imebakia tata. Kwa mfano, “atakuwa na nguvu kupita kiasi na ataishi-muda-mrefu ya kwamba Yesu (A.S.) pekee ndiye atakayeweza kumuua; hakuna chengine kitakachoweza.” 12 Yaani, itakuwa imefunuliwa tu, imenyanyuliwa, dini takasifu kwamba itaweza kuirudia njia yake na serikali yenye tamaa, kuitokomeza. Dini hiyo itaibuka miongoni mwa wafwasi wa kweli wa Yesu (A.S.), na itaifuata Qur’an na zitaunganika pamoja. Kuja kwa Yesu (A.S.) na kuibuka kwa dini ya kweli ya Ukristo, mfumo wa kumkana Mtakatifu usiokuwa na dini utafutwa na kumalizika kabisa. Mfumo wa Kumkana Mtakatifu ungeweza labda kuuliwa kwa kimelea tu au kwa mafua.” (58)

Yesu Mtakatifu atakapomuua Dajjal, idadi kuwa ya watu wataingia katika dini ya kweli, dini ya kweli itaonesha uwepo wake vizuri, na ukweli uliotajwa katika aya iliyoelezwa punde utajidhihirisha wenyewe.

Chini ya mwangaza wa elimu yote hii, tunaweza kusema kuwa Yesu Mtakatifu atatekeleza shuhguli zake moja baada ya nyengine, zikiegemea kwenye haiba jumla. Dajjal na kamati yake, wanaojaribu kuueneza mfumo wa upingaji dini, watayeyuka kama barafu mbele yake na Mahdi; na wataendelea kuyeyuka.

Je hiyo sio aina ya usadikishaji na udhihirishaji wa masimulizi haya kuwa ukomunisti ambao ni utawala unaomkana Allah na ulioidhulumu dunia kwa miaka sabini, uliouminya uzalishaji wa Urusi wa miaka elfu-moja kwa ghafla moja, na ambao haujaacha kitu asili takatifu kikiwa salama, mwishowe kumalizikia kwenye maangamizi ya kuridhisha?

Mfumo wa upingaji dini, ambao ni kunyume na maumbile na sheria za Allah, utakufa na imeshakuwa hivyo. Urusi yenyewe haitohimili mbele ya ukweli huu; kwa sababu, tunaona waziwazi kuwa habari hizi njema zimeanza kufahamika, “Kwa sababu ya mwamko thabiti uliosababishwa na vita viwili vibaya kabisa vya dunia, hakuna kabisa-kabisa hata taifa moja lisilokuwa na dini litaloweza kuishi, na Warusi hawawezi tena kuishi bila ya dini. Hawawezi kurudi kuwa Wakristo, pia. Wanaweza tu kuweka amani pamoja na au kujisalimisha kwa Quran, ambayo inavunja kabisa-kabisa ukafiri, ambayo inategemea ukweli na shuhuda na kushawishi akili na moyo kwa pamoja.” (59)

e. Kuwaua kwake Wayahudi

“Dajjal atakuja na Wayahudi elfu sabini pamoja na yeye mwenyewe. Wote hao watakuwa wameandaliwa na panga zilizorembwa na watavaa kashida za kijani. Dajjal atakapomtizama Yesu Mtakatifu, atayeyuka kama chumvi inavyoyeyuka katika maji na ataanza kukimbia. Yesu atamwambia: “Nitakushughulikia kwa pigo, hutoweza kutoroka.” Atamkamata kwenye lango la mashariki la Ludd na atamuua. Allah pia atawashinda Wayahudi. Hakutokuwa na kiumbe, kamwe ambacho kimeumbwa na Allah kisizungumze pale Yahudi anapojificha nyuma yake.  Hakutokuwa na jiwe, mti, ukuta, na hata mnyama, asiyesema, “Ewe Mwisilamu mja wa Allah! Njoo na umuue.” Isipokuwa tu kwa mti uitwao ‘Gharqad’. Ni mti wa Wayahudi. Hautozungumza.” (60)

Katika hadithi nyengine iliyosimuliwa kwa Muslim, inaelezwa:

“Saa ya mwisho haitofika mpaka Waisilamu wapigane dhidi ya Wayahudi na Waisilamu watawaua mpaka Wayahudi wangejificha nyuma ya jiwe au mti na jiwe au mti utasema: Mwisilamu, au mtumishi wa Allah, yupo Yahudi nyuma yangu; njoo na umuue; lakini mti Gharqad hautozungumza, kwa kuwa ni mti wa Wayahudi.” (61)

Je ukomunisti, ambao ni utawala wa mfumo wa upingaji dini, utapata kipigo kisichomaanisha kuwa Wayahudi walioeneza fitina ardhini katika historia yao yote, wenye sifa mbaya kutokana na njama zao na fitina na ambao walioanzisha ukomunisti katika ulimwengu wetu katika zama zetu kupokea kipigo?

Kwa kuwa fitina ya taifa hili ambalo, kama inavyoelezwa katika Qur’an, limestahiki adhabu ya Allah na ambalo limebandikwa nembo ya udhalili na ufukara ipo katika umbali huo kwamba ni mbali kunakovuka fitina zote zilizofanywa hapo kabla; kama tunavyochukulia, wamekuwa ni wenye kustahiki adhabu ya kiungu kama inayobidi. Muda utaonesha lini na vipi Wayahudi, waliopata kipigo kisichosahaulika na kuporomoka kwa ukomunisti, watasumbuka na adhabu nyengine watayostahiki.

f. Kuwa kwake sababu ya baraka na urutuba

Katika moja ya hadithi, Mtume Muhammad (S.A.W.) anasema: “Ni bahati ilioje kwa maisha baada ya Masihi!” na atafafanua sababu ya hili: Siku hiyo ikija, mbingu zitanyesha mvua yake, ardhi itaotesha mimea yake. Hii ni kwa kiwango ambacho hata kama utaatika mbegu katika jiwe gumu, basi itaota.” (62)

Hadithi hii inaonesha wingi wa neema (baraka) utakaokuwepo katika wakati huo wa Mahdi na bado zitaendelea hapo baadaye.

Haya ni mazuri machache yatakayofikiwa wakati wa utawala wa Yesu. Moja ya mazuri haya ni baraka ya mali kama inavyoelezwa katika simulizi (63). Kutakuwa na baraka kiasi kwamba hakutokuwa na mtu atakayekubali. (64)

Kadiri watu wanavyotangulia kutoa shukurani, Allah atawatunuku fadhila zake kwa wingi. Sababu nyengine muhimu ni kwamba pesa iliyotumika hapo kale kwa ajili ya risasi itaelekezwa kwenye huduma za umma. Pia, kama ambavyo teknolojia inayokua na kuendelea katika kilimo na viwanda vitajengwa katika wakati huo, uzaishaji utaongezeka zaidi na zaidi.

Je Yesu Mtakatifu ameshakuja?

Bediüzzaman anasema kuwa Ukristo ima utatoweka au utarudia kwenye kumpwekesha Allah kwa kutakaswa dhidi ya ushirikina, na utasitisha vita dhidi ya Uisilamu.

Maoni yake ni kuwa mwishowe itatokea. Anazihusisha awamu za Ukristo hadi leo kwenye njia ya kujitambua kwake:

“Ulichanwachanwa mara kwa mara, ukakaribia kuwa Utakaso; lakini haukufanikiwa. Pazia limechanwa tena, utaangukia kwenye mkengeuko kabisa. Baadhi, ingawa, ulikaribia kwenye kumpwekesha Allah; haitasaidia, Tayari uko tayari… Kuanza kuchanwa. Kama haukutoweka, utapata utakaso na kujumuika na Uisilamu. Ni jambo kubwa lisiloelezeka, ishara ambayo: Mtukufu wa Mitume amesema: ‘Yesu atatekeleza Shari’a yangu na atakuwa ni miongoni mwa jumuia yangu.’” (65)

Hapo juu tumetoa baadhi ya mifano kuhusu namna gani ukweli huu utatokea. Bediüzzaman anatoa mifano mingi kuhusu suala hili katika utunzi wake. Moja ya utunzi huo, anasema: “Wakati wa mwisho, dini ya kweli ya Yesu Mtakatifu (amani imshukie) itatawala; itakuja bega kwa bega na Uisilamu.” (66). Kama iliyokuwa katika Zama za Furaha- wakati wa Mtume Muhammad (S.A.W.), Qur’an inawalingania Watu wa Kitabu kuja katika neno maarufu; kumwabudu Allah na kutomshirikisha na chochote (67). Aya hii imeanza kuwa na athari zaidi katika wakati wetu ikilinganishwa na uliopita. Katika wakati wetu ambapo ujinga na uigaji wa upofu umewekwa kando, na umebadilishwa kwa mantiki, elimu, haki, na ukweli, dunia ya Kikristo pia imeanza kuisikiliza kwa makini amri hii ya Qur’an.

Inaonekanwa siku hizi kutokana na Zama za Furaha Kamili, Mjumbe wa Allah ametangaza: “Wakati wa mwisho, Wakristo wachamungu wa kweli wataanzisha ushirika pamoja na watu wa Quran-Waisilamu, na kwa hivyo utasimama dhidi ya uadui wa pande mbili: wanaomkana mungu.” (68) Hadithi nyengine kuhusu suala hili: “Siku za baadaye, mtasimamisha amani na Warumi kuanzisha usalama na mtapigana pamoja dhidi ya adui wa pande mbili.” (69)

Katika hadithi ya kutoka kwa Ibn-i Mace, inaelezwa kuwa vita vitakapozuka, jeshi lisilokuwa na asili ya kiarabu ambalo farasi wake ni wakakamavu, silaha zao ni bora zaidi watausaidia Uisilamu. (70) Je sio jeshi hili ni la dola la Kikristo ambalo lina teknolojia ya vita ya hali ya juu na ambalo litauunga mkono Uisilamu wakati wa vita vikubwa?

Bediüzzaman amezungumzia sana kuhusu kundi pinzani la ndani, lililoshughulika na pigo la kifo kwa Wajerumani na Bolsheviki, na ambalo, wakati wa Vita II vya Dunia, walipigana dhidi ya Urusi, mwakilishi wa ukomunisti, na likasema: “Kwa kumtegemea Allah, nitafanya nje ya mfumo wa upingaji dini, na litaulinda Uisilamu na Waisilamu; na kusema kuwa wao ni aina ya wawakilishi wa haiba jumla ya Yesu Mtakatifu. (71)

Sio nchi za Kiisilamu wala Kikristo zingeweza kupigana na ukomunisti peke yao, ambao umekuwa ukijishughulisha kwa niaba ya mfumo wa kumkana mungu kwa miaka sabini na nane. Kwa hivyo, muungano ulikuwa haukamatiki. Taasisi kama NATO na CENTO zimeibuka kwa mantiki hii.

Ulikuwa wakati mwafaka. Baada ya kuliona hilokwa usahihi, Bediüzzaman ameona haja ya kuwakumbusha wote wawili Waisilamu na wachamungu wa Kikristo kuhusu ukweli fulani:

“Sasa, Waumini wanapaswa waunde muungano sio tu na ndugu zao Waisilamu, lakini pia na wachamungu wa Kikristo na wasizingatie nukta wanazotofautiana na wanapaswa wasijitumbukize katika safu, kwa sababu ya mashambulizi ya ukafiri khasa.” (72)

“Sasa, watu wa dini na ukweli vinahitaji kuunda muungano aminifu sio tu na waumini wenziwao, wafanyakazi wenzao, na ndugu zao; lakini pia na wachamungu Wakristo na wanapaswa wasizingatie nukta za hitilafu kwa mujibu wa wakati na wanapaswa wasijitumbukize katika safu.” (73)

Wamishionari, wachamungu Wakristo, na watumishi wa Qur’an wangelipa umuhimu mkubwa; kwa sababu wimbi la ukafiri linaloenea kutoka Kaskazini limekuwa likijaribu kuuharibu muungano kati ya Waisilamu na wamishionari ili kujilinda dhidi ya mashambulizi ya Uisilamu na Ukristo. Wimbi hili lingeweza kulaghai na kuwapa kipaumbele na hivyo kuwavutia Waisilamu kwa kunufaika kutokana na kanuni za Uisilamu ambazo Uisilamu umeuhifadhi umma, uliofaradhisha zakat na kukataza riba, na kuwa utauepukwa ukatili. (74)

Katika Vita vya Pili vya Dunia, ulikuwepo ukomunisti katika upande mmoja, utawala wa mfumo wa upingaji dini na nchi za Kikristo katika upande mwengine. Bediüzzaman alisema katika tathmini ya vita kutokana na mtazamo huu, “…Kwa sababu ya Vita hivi vya Dunia, pamoja na tukio la dola mbili zinazodai udhibiti wa ardhi, mapigano makubwa kati ya wimbi la kutisha la mfumo wa upingaji dini na dini za mbinguni vitaanza kwa dini mbili kubwa kukata rufaa mahakamani juu ya usuluhishi wa kutafuta amani.” (75)

Mazingira yalikuwa dhaifu. Na adui alikuwa mkubwa mno. Hata hivyo upande wenye nguvu wa kutokubaliana ulikuwepo, wangekuwa ni rahisi kushindwa kwa nguvu chache. Wakati huo huo, wimbi la Dajjal lilikuwa katika utendaji. Wakristo na Waisilamu watalazimika kuwa katika muungano dhidi ya wimbi hili. Bediüzzaman alikuwa akisema:

“Wasiwasi mkubwa na maliwazo yanakuja moyoni mwangu: Wasiwasi ni kuwa mwisho wa mapigano haya, uharibifu mkubwa zaidi ya wa Vita I vya Dunia unaweza kuleta ukatili wa Dajjal barani Ulaya, chanzo na usaidizi wa ustaarabu. Faraja yangu ni kuwa mwamko kamili wa ulimwengu wa Kiisilamu, Dunia Mpya itaikubali dini ya Ukristo kuwa ni kanuni za utendaji na kuunda muungano pamoja na Uisilamu, na Injili itaunda muungano na Quran na kujisalimisha kwake utasimama dhidi ya mawimbi mawili ya kutisha yanayokuja pamoja na msaada wa kiungu na utawashinda Allah akipenda.” (76)

Wimbi hili la Dajjal halikuwa chochote isipokuwa ni ukomunisti. Kutokana na ufundi wa dunia, hakujaonekana mfumo wa pili ulioendesha vita kwa namna ambayo ni dhidi ya dini zote na mambo takatifu kuchukua upuuzi “Dini ni afyuni” kuwa ndo kanuni. Mfumo huu ulikuwa mbali kumshinda Namrudh, Firauni na Shaddat katika uharibifu umepindukia kwa kummeza yeyote aliyekaa mbele, umekua kiuwezo na umevamia sehemu muhimu ya dunia. Katika wakati huo, sio Waisilamu, ambao ni wafwasi wa dini ya kweli wala Wakristo watakaokuwa na uwezo wa kuhimili peke yao. Hakutokuwa na namna nyengine kuliko kuungana kati ya Waisilamu na Wakristo.

Hapo kale, dola za Kikristo hazikuusaidia umoja wa Uisilamu; hata hivyo, kwa kuwa ukomunisti na vurugu zimeibuka, dola zote mbili za Marekani na Ulaya zitalazimika kuusaidia umoja wa Uisilamu. (77)

Muundo wa Uisilamu unamaanisha kutambua wajibu wa tatu kati ya majukumu ya Mahdi, ikimaanisha ‘imani, maisha na Shari’a’, kwa sababu wajibu wa tatu wa Mahdi ni kuthibitisha Ukhalifa wa Uisilamu kwenye umoja wa Uisilamu na kuunda muungano pamoja na wachamungu Wakristo na hivyo kuutumikia Uisilamu. Jukumu hili lingeweza kutimizwa kwa ufalme mkubwa, nguvu, na mamilioni ya watu watakaojitoa-muhanga. (78)

Mnamo tarehe 13 Disemba 1992, Mamlaka ya Papa yametoa kitabu chenye kurasa 627. kitabu hiki, kilichosambazwa kwenye makanisa yote, kimeuzwa nakala laki 200 katika Ufaransa peke yake. Ndani ya kitabu, Ukristo umetathminiwa kwenye mwelekeo wa Uisilamu. Ndani ya kitabu, chenye Sura ya Fatiha, kimesema:

“Watu hawatakiwi kuzitii sheria zilizowekwa na binadamu, lakini watii sheria za kiungu.”

Katika kitabu kiilchojaa imani ya kumpwekesha Allah, utatu umeshughulikiwa kwa namna hii:

“Kumekuwa hakuna uwezekano wa kufafanua imani ya utatu kwa mujibu wa imani ya Mungu mmoja. Yesu Mtakatifu ni mtume pekee anayefikisha chochote kilichofunuliwa kwake na Allah.”

Tokea 1967, Ofisi ya Upapa kwa anwani ya ‘Makao Makuu ya Baraza la Mazungumzo kati ya Dini Mbalimbali’ imekuwa ikiwapongeza Waisilamu katika Maadhimisho yao ya mwezi wa Ramadhani. Tangazo walilolitoa mwaka 1992:

“Wapendwa Waisilamu madada na makaka!

Sisi Wakristo tunaoheshimu kushikamana kwenu na funga na sala tunapenda kufanya kazi pamoja ili kuanzisha amani.

Kwa hisia za hali ya juu zinazoamshwa na funga kupitia mwezi wa Ramadhani ambayo ni faradhi kwenu kama Waumini na Waisilamu, mnaelewa na kufahamu vyema kuwa haiwezekani kuanzisha amani ya kweli bila ya msaada na mwangaza ulioletwa na Allah. Huyu ni Allah ambaye ni Mola Mlezi pekee wa amani na furaha.

Tunamwomba Allah atupe faraja sote Waisilamu na Wakristo ya nguvu za kuyavumilia magumu katika kuanzisha amani kupitia msaada wa pande mbili na mazungumzo.”

Katika ujumbe huu kwa dunia ya Uisilamu kwenye tukio la Maadhimisho ya mwezi wa Ramadhani, katika mwaka 1996, Kadinali Francis Arinze aliwapongeza Waisilamu kwenye maadhimisho yao na kusema kuwa mahusiano kati ya Waisilamu na Wakristo ni lazima yaboreshwe na kwamba mahusiano yanapaswa yawe makubwa zaidi na ya kina zaidi kuliko uvumilivu. Arinze ananukuu maneno haya ya Papa Jean Paul: “Sisi Wakristo na Waisilamu tuna ukosefu wa mafahamiano na wakati mwengine tunapingana na hata kujiteketeza wenyewe kwenye mabishano na vita.” Na kusema: “Ni wakati wa kuziokoa kumbukumbu zetu kutokana na mabaki hasi yaliyopita na tuangalie maisha ya baadaye. Yeyote atakayemkasirikia mwengine lazima aombe radhi kwa majuto. Lazima tusameheane kwa sote. “ (79)

Ni kama vile Yesu Mtakatifu anatekeleza shughuli zake nyuma ya pazia. Hivyo ameshakuja. Kwa kweli kama ilivyo ulazima wa lengo la mtihani, sio kila mtu anaweza kumfahamu. Ni wale wafwasi wake wa karibu mno wataweza kumfahamu.

Tanbihi

1. Unjili ya Luka, 23
2. Matayo, 26:14-16.
3. Elmalılı, Hak Dini Kur'an Dili, 3:1517-1518.
4. Al-‘Imran Surah, 54-55.
5. An-Nisa Surah, 157-158.
6. Canan, A.g.e., 14:74.
7. Said Havva, A.g.e., 9:336.
8. A.g.e., uk. 420.
9. Ibni Mace, 10:338.
10. Muslim, 2:58.
11. Sıddık Hasan Han, es-Seyyid Muhammed Sıddık el-Kannucî, el-Izaa (Kahire: 1407/1986), s. 114; Said Havva, A.g.e., 9:335-336, 446.
12. Said Havva, A.g.e., 9:445.
13. Kittânî, A.g.e., s. 147.
14. Ibni Mâce, 10:338.
15. et-Teftazanî, Mes’ûd bin Ömer bin Abdillah, Şerhu'l-Makasıd (Istanbul: 1277), Hatime: 8; 2:307.
16. Zukhruf Surah, 61.
17. Muslim, Kitabu'l-Fiten: 39.
18. Bukharî, Spells: 102; Mezalim: 31; Mitume: 49; Muslim, Kitabu cha Imani: 242; Ebu Davud, Melahim: 14.
19. Bukhari, Ukatili: 31; Matamshi: 102; Muslim, Imani: 242-243; Ibni Mâce, Njama: 33.
20. Müsned, 3:387; el-Fıkhü'l-Ekber Aliyyü'l-Karî Şerhi Terc., uk. 284.
21. Müslim, Kitabu cha Njama: 34.
22. el-Heytemî, A.g.e., uk. 68.
23. Imam-ı Rabbanî, Mektûbât, 2:1309.
24. Ibni Mâce, 10:338.
25. Şârânî, Muhtasaru Tezkiretü'l-Kurtubî Ufasiri., uk. 500.
26. Said Havva, A.g.e., 9:338.
27. Sahih-i Bukharî Ufasiri. 1:83 (H. 1406, 5:208); el-Fethu’l-Kebîr, 2:143.
28. Bukharî, Kitabu cha Mitume (Suala la kushuka Yesu): 60, 4:324; Muslim, 2:56.
29. Ibn-i Hacer, el-Feth, 6:491.
30. Muslim, Imani: 247; Suyûtî, Celaleddin Abdurrahman, el-Havî li’l-Fetâvâ, I-II (Beyrut: 1983), 2:83.
31. el-Heytemî, A.g.e., p. 64.
32. el-Fıkhu'l-Ekber Aliyyü'l-Karî Şerhi Tafsiri., uk. 284.
33. Said Nursi Miyonzi/Mionzi, uk. 507.
34. Said Nursi, Barua, uk. 13.
35. Ibni Mâce, 10:323.
36. Musned, 2: 437; 6:75.
37. Musned, 2:482-483.
38. Muslim, Kitabu cha Imani: 243.
39. Bukharî, Matamshi: 102; Ukatili: 31; Mitume: 49; Muslim, Kitabu cha Imani: 242; Abu Davud, Melahim: 14.
40. Canan, A.g.e., (Istanbul: Feza Gazetecilik A.Ş., 1996), 14:73.
41. Musned, 2:437; Muh. Tezkiretü'l-Kurtubî, p. 498.
42. Muslim, kitabu cha Imani: 243.
43. Abdullah bin Mes'ûd, Tefsîru Ibni Mes'ûd, uk. 243.
44. Muslim, Kitabu cha Njama: 34.
45. Kittânî, A.g.e., uk. 145.
46. Kitabu cha Shuhuda, uk. 105.
47. Musned, 6:125, 435; Muslim, Njama: 110.
48. Musned, 3:368; 4:216-217.
49. Sarıtoprak, A.g.e., uk. 128.
* Ludd, ni mji wenye idadi ya wakazi elfu kumi na tano, masafa ya kilomita 68 kutoka Jerusalem.
50. Muslim, Njama: 110; Tirmizî, Njama: 59, 62; Ibni Mâce, Njama: 33; Musned, 2:66; 6:455-456.
51. Ibni Kesir, Nihayetü'l-Bidaye, 1:158.
52. Said Nursî, Mionzi, uk. 506-507.
53. An-Nisa Surah, 159.
54. el-Fıkhu'l-Ekber Aliyyü'l-Karî Şerhi Tafsiri, uk. 284.
55. Mehmet Vehbi, Hülasatü'l-Beyan, 3-4: 1109.
56. Said Nursi, Barua, uk. 54.
57. Said Nursî, Barua, uk. 413.
58. Said Nursî, Mionzi, uk. 581.
59. Said Nursî, Nyongeza ya Emirdag, 2:71.
60. Ibni Mace, Njama: 33.
61. Muslim, Kitabu cha Njama: 82.
62. el-Münavî, Feyzü’l-Kadîr, 4:275.
63. Muslim, Kitabu cha Imani: 243.
64. Tirmizî, 4:93; Ibni Mâce, 10:340.
65. Said Nursî, Maneno, uk. 723.
66. Said Nursî, Nyongeza ya Kastamonu, uk. 111.
67. Al-‘Imran Surah, 64.
68. Said Nursî, Kijarida cha Utiifu, uk. 24.
69. Tafsiri ya Tac, H. 960; Ibni Mâce, H. 4089.
70. Ibni Mâce, H. 4090.
71. Said Nursî, Nyongeza ya Kastamonu, 53-54.
72. Said Nursî, Nyongeza ya Emirdag, 1:206.
73. Said Nursî, Kijarida cha Utiifu, uk. 24; Nuru, uk. 151.
74. Said Nursî, Nyongeza ya Emirdag, uk. 159.
75. Said Nursî, Sikke-i Tasdik-i Gaybî, uk. 191.
76. Said Nursî, Nyongeza ya Emirdag, 1:53.
77. A.g.e., 2:54.
78. Said Nursî, Sikke-i Tasdik-i Gaybî, uk. 11.
79. 17 Febuari 1996, Yeni Asya.

Maswali juuyau islamu

Author:
Maswali juuyau islamu
Subject Categories:
Read 36 times
In order to make a comment, please login or register
MASWALI YENYE KUFANANA