Kwanini wanawake katika Uislamu wana nusu ya haki ya wanaume katika kutoa ushahidi?

The Answer

Dear Brother / Sister,

Mambo ya lazima yanayounda misingi ya sheria ya Kiislamu yanategemea ufunuo (wa Allah). Yameorodheshwa katika Qur’an. Kwa maneno mengine, mambo ya lazima yamewekwa na kuamrishwa na Muumbaji wa Ulimwengu. Zama, angahewa na mazingira yoyote mtu anamoishi, mambo hayo ya muhimu ndio chanzo cha amani na njia ya kupata faraja. Hii ni kwa sababu ya amri hizo ndio zenye kufaa zaidi kwa uumbwaji wa mwanadamu. Amri na mamlaka za kisheria katika Qur’an zinapotafitiwa, nukta inayosalia nki kwamba kuwepo kwa mwanadamu kimwili na kiroho huzingatiwa.

Katika mambo ya kutoa ushahidi, inawezekana kuliangalia hilo, pia. Tafsiri ya aya inayohusu kutoa ushahidi ni kama ifuatavyo:

“…Na mshuhudishe mashahidi wawili katika wanaume wenu. Ikiwa hapana wanaume wawili, basi mwanamume mmoja na wanawake wawili katika mnao waridhia kuwa mashahidi. Ili ikiwa mmoja wao akipotea, mmoja wao amkumbushe mwengine…” (1)

Kwa hivyo, hapa, jambo la msingi linahusiana moja kwa moja na uumbwaji wa wanawake. Hili ni sharti la sura yao ya kisaikolojia. Msingi wa silika ya mwanamke ni kusisimka na yeye anaishi kwa misisimko yake. Kwa hiyo, dhana hujikita moyoni mwake zaidi kuliko akilini mwake na kuleta athari kwa njia hiyo. Kwa hakika hawezi kutokuwa na upendeleo mbele ya matukio. Yeye huliendea jambo akiwa na welewa unaoendana na jinsi inavyotawala dhamiri na huruma yake.

Kwa sababu ya sifa yao hiyo, Qur’an inasema: “Wanawake wanaweza kusahau, kwa hiyo wanatakiwa wapewe wasaidizi katika ushahidi.” Hayo yamesemwa na Allah aliyemuumba mwanamke. Kwa hivyo, ni kanuni isiyobadilika. Je hakuna wanawake wasiosahau kirahisi na wenye kumbukumbu kali kuliko wanaume? Ndiyo, wapo, lakini kwa ujumla, hali hiyo ya kisaikolojia (kusahau) huonekana mara nyingi zaidi kwa wanawake. Ni jambo la kimaumbie tu kwamba hawezi kutunza kumbukumbu kwa muda mrefu.

Kwa upande mwingine, mwanamke ni mndani sana. Ana dunia ya kwake mwenyewe. Yeye ameshughulishwa sana na kazi za nyumbani kutwa nzima. Anawatunza watoto na kuwalea. Wanawake wachache sana huvutiwa na kazi, biashara, na siasa. Mwanamke ambaye yuko mbali sana na dunia ya nje anawezaje kujua matukio yanayotokea huko, atayajuaje na kuyahifadhi akilini mwake na kwa kiasi gani ataweza kutoa ushahidi?

Kwa kupokea ushahidi wa wanawake wawili sawa na wa mwanamume mmoja, na kwa hivyo kutokumtwisha mzigo mwanamke kwa kumpa wajibu ule wa mwanamume katika mambo ya kuutoa ushahidi, Uislamu hauharibu haki yake, kinyume chake, unamuhifadhi na kumzuia asitende dhambi. Hayo ni kwa sababu kutoa ushahidi ni jukumu zito lenye majukumu makubwa.

Katika aya ya Qur’an, yanaelezwa yafuatayo:

“…Wala msifiche ushahidi. Na atakaye ficha basi hakika moyo wake ni wenye kutenda dhambi. Na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi wa mnayo yatenda.” (2)

Katika hadithi (maneno ya Mtume) yameonesha kuwa kutoa ushahidi kuna majukumu makubwa na kuwa ushahidi wa uongo unahesabiwa ni miongoni mwa madhambi makubwa mno.

Kwa hakika, Uislamu unamhifadhi mwanamke dhidi ya madhambi makubwa na kumzuia kutenda dhambi ya ushahidi wa uongo, kwa kuhadaiwa na baadhi ya udhaifu wake kupitia msisimko au kupitia hali ya kuwa na jazba. Uislamu umechukua tahadhari dhidi ya hilo kwa kumteulia mwanamke msaidizi kando yake. Kwa sababu hii tu, katika baadhi ya mambo ya ushahidi, wanawake wawili huchukua nafasi ya mwanamume mmoja.

Wakati mwingine wanawake wanaweza kuwa na wivu katika mambo watakayoyatolea ushahidi na hisia za ushindani zinaweza kutawala. Kwa hiyo, wanaweza kuwa na dosari ya kutambua haki kwa kuficha baadhi ya vipengele vya jambo hilo. Hata hivyo, ikiwa wanawake wawili watatoa ushahidi, mashaka yatafutwa pale mmoja wao atakapofafanua nukta atakayoificha mwingine.

Kwa upande mwingine, kuwa ushahidi wa wanawake wawili huchukulika kuwa sawa na ushahidi wa mwanamume mmoja hakuna namna ya kumaanisha kuwa mwanamke ana thamani ya nusu ya mwanamume. Hili ni dalili tu kuwa umuhimu mkubwa kwa kuwepo namna zote za uhakikisho katika ushahidi. Katika madai yapi mwanamke hutoa ushahidi, ni katika madai gani hayumo, na katika yapi ushahidi wake ni nusu ya ule wa mwanamume?

Sheria ya Kiislamu imemtoa mwanamke katika ushahidi wa makosa yanayohukumiwa adhabu inayoitwa ‘had’ kama vile uzinifu, pombe na wizi na katika adhabu za ‘qisas’ (kisasi) na ushahidi wake katika hayo haupokelewi. Katika madai hayo, adhabu ya uzinifu inahitaji ushahidi wa wanaume wanne na hayo mengine ni wanaume wawili. Katika madai yanayohusiana na mambo kama ya biashara, kuuza na kununua, ndoa na talaka, yaliyomo katika kundi la mahusiano na miamala, ikiwa hakuna wanaume wawili, basi ushahidi wa mwanamume mmoja na wanawake wawili hutakiwa. Hata hivyo, katika mambo ambayo wanaume si mahiri kama vile kujua ubikira, hali za wakati wa uzazi kuhusu mama na mwana, na kuanzisha undugu wa kunyonya, ushahidi wa mwanamke mmoja unatosha. Zaidi ya hayo, Umar Ibn Al-Khattab (Allah awe radhi naye) aliona ushahidi wa mwanamke mmoja kuwa unatosha hata katika mambo ya talaka. Hayo ni kwa sababu kusudio halisi katika ushahidi ni kuhifadhi haki mbalimbali, kuendeleza haki na kuutambua ukweli. Hekima mojawapo ya kutokutumia ushahidi wa mwanamke katika adhabu za ‘had’ na katika qisas (kisasi) ni kiwango cha hisi ili kuzuia shaka hata ndogo sana katika mambo hayo. Hayo ni kwasababu katika madai ya qisas kwa kauli zisizo kamilifu, haki ingeweza kukiukwa au mtu angeweza kulipiziwa kisasi kimakosa. Mwelekeo kama vile wa usahaulivu na kuelemewa na jazba kuhusu wanawake kunaweza kulitoa jambo hilo maanani.

(1) Al-Baqarah, 282.
(2) Al-Baqarah, 283.

Maswali juuyau islamu

Author:
Maswali juuyau islamu
Subject Categories:
Read 141 times
In order to make a comment, please login or register
MASWALI YENYE KUFANANA