Uislamu unaipa haki umuhimu gani?

The Answer

Dear Brother / Sister,

Allah anaeleza yafuatayo katika aya:

Hakika Mwenyezi Mungu anaamrisha kufanya uadilifu, na hisani, na kuwapa jamaa; na anakataza uchafu, na uovu, na dhulma...” (An-Nahl 90) 

Yaani, Allah Mtukuka haridhii dhuluma na uasi.

Allah, ambaye kwa hakika ni Mwenye kuhukumu kwa haki, si mwenye kukosa kujua wanayoyafanya wanaodhulumu; wanaodhulumu na wasaliti pasi na shaka watahesabiwa kwa vitendo vyao mbele ya haki ya Allah.

Katika aya nyingine, hatari ya kuwategemea wenye kudhulumu na kustahamili dhuluma yao, achilia mbali kuwaunga mkono, inaelezwa kama ifuatavyo:

Wala msiwategemee wanao dhulumu, usije ukakuguseni Moto. Wala nyinyi hamna walinzi badala ya Mwenyezi Mungu, wala tena hamtasaidiwa..” (Hud, 113)

Katika aya nyingine, yanaelezwa yafuatayo:

Hakika Mwenyezi Mungu anakuamrisheni mzirudishe amana kwa wenyewe. Na mnapo hukumu baina ya watu mhukumu kwa uadilifu...” (an-Nisa, 58)

Nukta ya kuvutia hapa ni kwamba neno "watu" si "waumini" hutumika inapotajwa haki. Kufuatana na hayo, ni muhimu kila mmoja kumtendea haki ikiwa ni marafiki au maadui.

Kwa hakika, aya ifuatayo inatufundisha jambo hilo hilo:

Basi anaye tenda chembe ya wema, atauona! Na anaye tenda chembe ya uovu atauona!(az-Zilzal, 7-8)

Mojawapo katika mambo muhimu ya haki katika Uislamu ni kwamba marafiki, ndugu, taifa na dola haviwezi kuwajibishwa kwa kosa la mtu huyo. Allah Mtukuka anaeleza yafuatayo katika Quran;

Na mbebaji habebi mzigo wa mwingine(Fatir, 18)

Kila mmoja ataadhibiwa kutokana na makosa yake. Mtu anayeua, si yeyote mwingine, atakayeadhibiwa kwa mauaji hayo. Hata hivyo, kama mtu atamsababisha mwingine atende dhambi, wote wawili, mtenda dhambi na msababishaji wataadhibiwa.

Allah Mtukuka amebainisha mipaka katika Quran ili watu wasikiuke haki za wengine; Amezitaja kuwa ni "mipaka ya Allah". Anatuambia kuwa wenye kuvuka mipaka hiyo watakuwa wenye kudhulumu na anawaonya kuwa watapata adhabu ya Allah.

Mtume (s.a.w) anaeleza yafuatayo katika hadithi: “Allah anawaadhibu wenye kuwatesa wengine duniani.

Katika Quran, Allah Mtukuka anaeleza kuwa mataifa jeuri yasiyotawala kwa haki yatakuwa na mwisho wa kuhuzunisha. Tutatoa aya mbili kama mfano:

Miji mingapi tuliiangamiza iliyo kuwa ikidhulumu, ikawa imebaki magofu, na visima vilivyo achwa, na majumba yaliyo kuwa madhubuti?(Hajj, 45)

Na mingapi katika miji iliyo kuwa ikidhulumu tumeiteketeza, na tukawasimamisha baada yao watu wengine!.” (al-Anbiya, 11)

Dini ya Uislamu inatuamuru tuheshimu haki za watu wa dini zingine, pia. Katika nyakati za amani, haki zao hudhaminiwa na kuhifadhiwa kama zile za Waislamu. Kwa hakika, kwa mujibu wa madhhab ya Hanafi, “Muislamu anayemuua asiye Muislamu kwa dhuluma katika kipindi cha amani hunyongwa.” Yaani, yeye pia huuliwa.

Mtume anawatishia watu kama hivyo katika hadithi kama ifuatavyo:

“Mimi ni adui wa mtu anayemtesa dhimmi. Nitawaita maadui zangu kwenda kuhesabiwa huko ahera.” (Kashfu’l Khafa, II, 218, hadithi na: 2341)

Huu ndio ukweli kuhusu Uislamu. Kisha, ni muhimu kutafuta sababu za kwa nini baadhi ya Waislamu walio mbali na moyo wa Uislamu wanajihusisha na vitisho na uonevu katika ujinga wao na nafsi badala ya katika dini ya Uislamu.

Inafahamika kuwa mtu anaweza kufanya kosa; ni yule tu aliyetenda kosa ndiye huwajibiswa nalo, si wengine. Si haki kuiwajibisha dini ya mtu kwa kosa binafsi analofanya mtu huyo.

Ni muhimu kutaja nukta muhimu sana hapa:

Vituo vinavyowazuia Waislamu wasijifundishe Uislamu halisi kutoka katika rasilimali zake na kuutekeleza kivitendo, kufanya hivyo kunawatenganisha na dini yao na kuwapeleka katika upotovu na hilo husababisha Waislamu wawe masikini kwa kuwajibishwa Waislamu wanaoangukia katika vurugu. Ni vyema vituo hivyo vingejiangalia na kujiuliza dhamira yao wenyewe badala ya kulaumu wengine.

Maswali juuyau islamu

Author:
Maswali juuyau islamu
Subject Categories:
Read 15 times
In order to make a comment, please login or register
MASWALI YENYE KUFANANA