Haki ya Allah inamfaa kila mtu, kama Muislamu au hapana. Allah ameharamisha dhuluma na uonevu kwa watu bila ya kujalisha dini yao. Inawezekana kwa Allah, anayeharamisha dhuluma ukandamizaji, Awakandamize watu kwa kuacha haki?
Imesisitizwa na ibara “wala Mola wako Mlezi si mwenye kuwadhulumu waja.” Katika aya ifuatayo: “Anaye tenda mema basi anajitendea mwenyewe nafsi yake, na mwenye kutenda uovu basi ni juu ya nafsi yake vile vile; wala Mola wako Mlezi si mwenye kuwadhulumu waja.”(Fussilat, 41/46) kuwa hakuna atakayedhulumiwa na kwa hiyo watu wote watatendewa haki bila ya kujalisha dini yao.
Kuna aya nyingi kuhusu jambo hilo. Aya mbili zinazowaambia makafiri moja kwa moja ni kama ifuatavyo:
“Anaye geuza shingo yake ili kupoteza watu waache Njia ya Mwenyezi Mungu. Duniani atapata hizaya, na Siku ya Kiyama tutamwonjesha adhabu ya kuungua. (Ataambiwa): Hayo ni kwa sababu ya iliyo tanguliza mikono yako. Na hakika Mwenyezi Mungu si dhaalimu kwa waja.” (Hajj, 9-10)
Aya ifuatayo inaeleza kuwa hakuna amali, ndogo au kubwa, itakayopotea na kuwa kila amali itakuwa na malipo au adhabu: “Basi anaye tenda chembe ya wema, atauona! Na anaye tenda chembe ya uovu atauona!” (az-Zilzal, 99/7-8)
"Dharra" iliyotajwa katika aya inamaanisha mdudu mdogo sana au chembe inayoweza kuonekana katika mwangaza wa jua tu. Kinachomaanishwa hapa ni kueleza jukumu la mwanadamu kwenye kitu kidogo kabisa ambacho akili ya kibinadamu inaweza kuvutiwa nacho. Lengo halisi ni kueleza kuwa amali ndogo kabisa njema au mbaya haitapotea katika macho ya Allah.