1
Je, inawezekana kupata shuhuda za Utume wa Mtume Muhammad (S.A.W) katika Biblia, Taurati na Zaburi?
Shuhuda za Utume wa Hadhrat Muhammad (S.A.W) katika Biblia iliyogeuzwageuzwa.
Ni muhimu sana kwamba tumeiita Biblia kuwa “imegeuzwageuzwa” katika kichwa cha habari. Neno imegeuzwageuzwa linamaanisha kuwa imepotoswa na kubadilishwa. Shuhuda zote tutakazozileta hapa zinamshuhudia Mtume Muhammad (S.A.W) ambazo zimeondolewa kwa umakini kutoka katika Biblia na kwa hivyo zimegeuzwageuzwa. Licha ya kazi makini na ya uangalifu ya mchakato wa kugeuzageuza kwa kuondoa kila aya iliyoeleza habari ya Mtume Muhammad (S.A.W) kutoka katika Biblia, kumebakia shuhuda nyingi sana. Kama kuna ishara nyingi sana za Mtume (S.A.W) katika Biblia iliyogeuzwageuzwa, basi kuna ishhara ngapi zilizomo katika Biblia halisi aliyoshushiwa Yesu (AS)? Hebu tafakari hilo!
Ugeuzaji walioufanya Wakristo na Wayahudi katika vitabu vyao hususani uondoaji wa aya zilizoeleza habari za Mtume Muhammad (S.A.W) umetajwa katika Qur’an kama ifuatavyo:
“Basi ole wao wanao andika kitabu kwa mikono yao, kisha wakasema: Hiki kimetoka kwa Mwenyezi Mungu, ili wachumie kwacho pato dogo. Basi ole wao kwa yale iliyo andika mikono yao, na ole wao kwa yale wanayo yachuma.” (al-Baqara, 2/79)
“Enyi Watu wa Kitabu! Amekwisha kujieni Mtume wetu anaye kufichulieni mengi mliyo kuwa mkiyaficha katika Kitabu, na anaye samehe mengi. Bila shaka imekujieni kutoka kwa Mwenyezi Mungu nuru na Kitabu kinacho bainisha. .―” (al-Maida, 5/15)
Qur’an inatueleza kuwa Wakristo wameficha habari nyingi sana alizofunuliwa Yesu (AS). Baadhi ya sehemu za habari hizo ni maneno katika Biblia kuhusu kuja Mtume Muhammad (S.A.W). Katika sehemu hii, tutachanganua maneno yanayosu kuja Mtume Muhammad (S.A.W) yaliyomo katika Biblia.
1. Yesu alisema; “Mkinipenda, mtazishika amri zangu. Nami nitamwomba Baba, naye atawapa Periklito (Msaidizi) mwingine, ili akae nanyi hata milele.” (Yohana 14:16,17)
2. Yesu alisema; “Lakini huyo Periklito (Msaidizi), ambaye Baba atampeleka kwa jina langu, atawafundisha yote, na kuwakumbusha yote niliyowaambia.” (Yohana 14: 26)
3. Yesu alisema; “Na sasa nimewaambia kabla halijatokea (Periklito), kusudi litakapotokea mpate kuamini.” (Yohana 14: 29)
4. Yesu alisema; “Lakini ajapo huyo Msaidizi (Periklito), nitakayewapelekea kutoka kwa Baba, huyo Roho wa kweli atokaye kwa Baba, yeye atanishuhudia …” (Yohana 15: 26)
5. Yesu alisema; “Lakini mimi nawaambia iliyo kweli; yawafaa ninyi mimi niondoke, kwa maana mimi nisipoondoka, huyo Msaidizi (Periklito) hatakuja kwenu; bali mimi nikienda zangu, nitampeleka kwenu.” (Yohana 16: 7)
6. Yesu alisema; “…Lakini Msaidizi (Periklito) atakapokuja, atawaongoza awatie kwenye kweli yote; kwa maana hatanena kwa shauri lake mwenyewe, lakini yote atakayoyasikia atayanena, na mambo yajayo atawapasha habari yake.” (Yohana 16: 13)
7. Yesu alisema; “…Yeye (Periklito) atanitukuza mimi, kwa kuwa atatwaa katika yaliyo yangu na kuwapasha habari.” (Yohana 16: 14)
Neno la asili la misemo ya mshabaha ya Kibiblia iliyooneshwa hapo juu kama Periklito na Mtume Yesu (S.A.W) kupewa habari njema ni “Munhamenna” katika lugha ya Sham (Ki-Syria) na “Periklytos” kwa Kigiriki. Kisawe cha neno hilo kwa Kiarabu ni “Ahmad”.
Maneno ya Kigiriki ya Periklytos wa Biblia, yaani, “Ahmad” yameoneshwa kuwa ni “Briklitus” katika baadhi ya vyanzo. Kwani “Ahmad” (S.A.W) ni jina la Mtume Muhammad (S.A.W), imeelezwa na Qur’an kuwa jina Lake ni “Ahmad” katika Biblia. (Angalia. Saff, 61/6)
Na pia sifa zote zilizotajwa hapo juu anazo Mtume Muhammad (S.A.W) peke yake. Basi, ni Mtume Muhammad (S.A.W) ndiye aliyetajwa kuwa mtu aliyesubiriwa katika Biblia na ikatolewa habari njema kumhusu yeye.
Licha ya hivyo, neno “Periklito” limeelezwa katika ufafanuzi wa Kibiblia kuwa ni "mtu sahihi atakayepambanua ukweli na uwongo"; yaani, ni jina la mtu atakayewaongoza wanadamu kwenye ukweli baada ya Yesu (AS). Je, yupo yeyote asiyekuwa Hadhrat Muhammad (S.A.W) aliyefanya kazi hiyo zaidi yake aoneshwe duniani?
8. Yesu alisema; “Lakini mimi nawaambia iliyo kweli; yawafaa ninyi mimi niondoke, kwa maana mimi nisipoondoka, huyo Msaidizi (Periklito) hatakuja kwenu; bali mimi nikienda zangu, nitampeleka kwenu.” (Yohana 16: 7)
Ni nani asiyekuwa Hadhrat Muhammad (S.A.W) aliyepo duniani na akawapa wanadamu faraja ya kweli? Ndiyo, ni Mtume (S.A.W) anayemwokoa mwanadamu kutokana na adhabu ya kifo na kuwapa faraja halisi.
9. Yesu alisema; “Mimi sitasema nanyi maneno mengi tena, kwa maana yuaja mkuu wa ulimwengu huu, wala hana kitu kwangu.“ (Yohana 14: 30)
10. Yesu alisema; “…Naye akiisha kuja, huyo atauhakikisha ulimwengu kwa habari ya dhambi, na haki, na hukumu.” (Yohana 16:8)
Baada ya Mtume Yesu (AS), ni nani aliyekuja asiyekuwa Mtume Muhammad (S.A.W) kama mkuu wa dunia na akapambanua haki na batili na kuwaonesha wanadamu njia ya kweli? Na, ni nani anayestahiki kupewa cheo cha “kiongozi wa dunia” asiyekuwa yeye? Na, ni mtume gani baada ya Hadhrat Dawud (AS) asiyekuwa Mtume Muhammad (S.A.W) aliyeeneza dini yake kutoka magharibi mpaka mashariki na akaweka mfumo wa kodi katika nchi na kupata ushindi nyoyoni mwa masultani na sehemu moja ya tano ya wanadamu wakimsifu kwa swala na kumtukuza kila siku? Ni nani asiyekuwa Hadhrat Muhammad (S.A.W) anayeweza kuoneshwa kama mtu mmoja tu aliyeyafanya hayo yote? Kwa hivyo, maneno yaliyotumika kwa ajili ya mtu baada ya Yesu (AS) katika Biblia kuwa ni “mtawala wa wa dunia” ni kwa Mtume Muhammad (S.A.W). Cheo chake mashuhuri ni “rehema ya ulimwengu”.
11 “Ushuhuda wa Yohana Mbatizaji ni kama ifuatavyo; Naye alikiri, wala hakukana; alikiri kwamba, Mimi siye Kristo. Wakamwuliza, Ni nani basi? U Eliya wewe? Akasema, Mimi siye. Wewe u nabii yule? Akajibu, La!” (Yohana 1:20-21)
Mtume Yohana (Yahya) aliulizwa maswali matatu na majibu yake kwa maswali yote matatu yalikuwa ya kukana:
a. Je, wewe ni Kristo, yaani, Yesu?
b. U Eliya wewe?
c. Wewe u nabii yule?
Hivyo, mitume watatu tofauti wametajwa katika Biblia ya Yohana. Hao ni Yesu (AS), Eliya na Mtume Muhammad (S.A.W)!
Kinachofahamika kutokana na maneno hayo ni kwamba; “Nabii yule” ni tofauti na Yesu (AS). Kwa hivyo, ni nani mtu huyo aliyefunuliwa kwa watu aliyoyasikia kutoka kwa Mungu na ambaye hakuwa hai wakati wa Mtume Yesu na aliyetajwa kuwa ni “Nabii yule” asiyekuwa Mtume Yesu? Kwa hakika ni; Mtume Muhammad (S.A.W). Kwani hakuna mwingine ghairi ya Mtume Muhammad anayeweza kuoneshwa kama aliyefuatia baada ya Yesu (AS) ambaye amefanya kazi ya Utume na kupata nafasi kubwa katika historia.
12. “Jihadharini na manabii wa uongo, watu wanaowajia wamevaa mavazi ya kondoo, walakini kwa ndani ni mbwa-mwitu wakali. Mtawatambua kwa matunda yao. Je! Watu huchuma zabibu katika miiba, au tini katika mibaruti? Vivyo hivyo kila mti mwema huzaa matunda mazuri; na mti mwovu huzaa matunda mabaya. Mti mwema hauwezi kuzaa matunda mabaya, wala mti mwovu kuzaa matunda mazuri. Kila mti usiozaa tunda zuri hukatwa ukatupwa motoni. Ndiposa kwa matunda yao mtawatambua.” (Mathayo 7:15-20)
Hakuna sehemu yoyote ya Biblia inayosema kuwa Hakuna mtume baada ya Yesu (AS). Hata hivyo, sifa ifuatayo imewekwa ili kumtambua anayedai kuwa ni mtume:
“Mtawatambua kwa matunda yao mumjue mwongo na mkweli…”
Kusingekuwa na mtume yeyote baada ya Yesu (AS), angetoa jibu fupi na la wazi wazi kama hivi: “Hakutakuwa na mtume yeyote baada yangu, Atakayedai utume baada yangu, kwa hakika ni mwongo.” Kwa hivyo, mbinu ya Yesu (AS) ya kumtambua mtume mwongo na mkweli ni ushahidi unaotosha wa kuja mtume mwingine baada ya Yesu.
Suala la kuja mtume baada ya Yesu (AS) pia linatosha kwa ajili ya Utume wa Mtume Muhammad (S.A.W) kwa sababu baada ya Yesu (AS), matokeo yenye manufaa ya kuunda jamii zilizomwamini Mungu, kumtegemea Mungu, kumpenda Mungu na kuacha kuabudu sanamu kulifanikiwa tu katika dini iliyoletwa na Mtume Muhammad (S.A.W).
13. Yesu (AS) anakuja Jerusalem. Anaanza kuhubiri kila siku. Hata hivyo, watu mashuhuri, wakuu wa nchi na viongozi wa kidini walitaka kumuua. Yesu (AS) anawapa ujumbe ufuatao:
“Ikiwa hamwamini ukweli huu, Mungu atakuleteeni juu yenu taifa litakaloamini na kuishi kwa mujibu wao …”
Katika mojawapo ya mafundisho yake, anaeleza mfano unaoelezwa hapa chini na ukweli wake kwa wakuu wa nchi;
Mfano wa Mmiliki ardhi (Mathayo 21:33-46; Marko 12:1-12; Luka 20:9-19)
“Sikilizeni mfano mwingine. Kulikuwa na mtu mwenye nyumba, naye alipanda shamba la mizabibu, akalizungusha ugo, akachimba shimo la shinikizo ndani yake, akajenga mnara. Akapangisha wakulima, akasafiri. Wakati wa matunda ulipokuwa karibu, akawatuma watumwa wake kwa wale wakulima, wapokee matunda yake. Wale wakulima wakawakamata watumwa wake, huyu wakampiga, na huyu wakamwua, na huyu wakampiga kwa mawe. Akawatuma tena watumwa wengine wengi kuliko wa kwanza wakawatenda vile vile. Mwishowe akamtuma mwanawe kwao, akisema, Watamstahi mwanangu. Lakini wale wakulima walipomwona yule mwana, wakasemezana wao kwa wao, Huyu ni mrithi; haya na tumwue, tuutwae urithi wake. Wakamkamata, wakamtupa nje ya shamba la mizabibu, wakamwua. Basi atakapokuja yule bwana wa shamba la mizabibu, atawatendaje wale wakulima?”
Wakamjibu Yesu kama ifuatavyo:
“Atawaangamiza vibaya wale wabaya; na shamba la mizabibu atawapangisha wakulima wengine, watakaomlipa matunda kwa wakati wake.”
Yesu akawauliza:
“Hamkupata kusoma katika maandiko, Jiwe walilolikataa waashi, Hilo limekuwa jiwe kuu la pembeni; Neno hili limetoka kwa Bwana, Nalo ni ajabu machoni petu? Kwa sababu hiyo nawaambia, Ufalme wa Mungu utaondolewa kwenu, nao watapewa taifa lingine lenye kuzaa matunda yake. Naye aangukaye juu ya jiwe hilo atavunjika-vunjika; naye yeyote ambaye litamwangukia, litamsaga tikitiki.” (Mathayo 21:43)
Mkuu wa makuhani na Mafarisayo waliposikia mithali yake, walitambua kuwa alikuwa anazungumza habari zao.
Wakataka kumkamata, lakini waliogopa mkusanyiko, kwa sababu mkusanyiko ulimzingatia kuwa ni mtume.
“Kwa sababu hiyo nawaambia, Ufalme wa Mungu utaondolewa kwenu, nao watapewa taifa lingine lenye kuzaa matunda yake …”
“Jiwe” lililotajwa katika sentensi hizo kwa hakika ni Mtume Muhammad (S.A.W) na watu watakaopewa mali ya Mungu ni ummah (jumuia) wa Kiislamu … Juhudi za wanazuoni wa Kikristo za kutafsiri “jiwe” kuwa ni Yesu (AS) ni bure.
a. Kwa hakika inafahamika kutokana na sentensi hizo kuwa mtu aliyeelezwa kwa taswira ya jiwe atakuwa tofauti na Yesu (AS) ambaye wengine wamedai kuwa ni mwana wa Mungu. (Allah atukinge dhidi ya hilo).
b. Kwa mujibu wa madai yao, Yesu (AS) aliuliwa na Wayahudi. Haifai kuuliza mantiki ya jiwe kuwaangukia juu yao kwa kuwa anayeangukiwa atapondekapondeka?
c. Yesu (AS) alisema katika Biblia ya Yohana, 12:47; “Na mtu akiyasikia maneno yangu, asiyashike, mimi simhukumu; maana sikuja ili niuhukumu ulimwengu, ila niuokoe ulimwengu…” kwani hili ni kinyume cha utendaji wa “jiwe” kama ilivyoelezwa hapo juu kwa sababu kwa mujibu wa maneno ya Biblia, anayeangukia juu ya jiwe hilo atavunjikavunjika, na atakayeangukiwa nalo atapondekapondeka.”
d. Zaburi, inaeleza kuwa inastaajabisha kuwa jiwe limekuwa jiwe la mingi kwa maneno, “…nalo ni ajabu machoni petu.” Kwa mujibu wa madai ya Wakristo, Daud (AS) alimheshimu sana Yesu (AS) mpaka –Alah atuepushie hilo- akawa anadhani kuwa Yesu ni Mungu. Basi kwa nini anaona ajabu kuwa Yesu ni jiwe la mingi? Kwa hivyo, mtu huyo lazima asiwe Yesu (AS) na utume wake lazima uwe wa kustaajabisha. Ukweli nyuma ya hilo ni kama ifuatavyo: Kwa kuwa wana wa Israil hawakutokana na Hadhrat Hajar na hawatokani na familia hiyo, wanaona kuwa Wana wa Ismail kuwa wako sawa nao na kwa hakika hakutokea mtume yeyote kutoka katika familia ya Ismail (AS) inawezekana ndio sababu ya kukanganyika kwao.
e. Mtume Muhammad (S.A.W) ambaye ukweli wake na kustahiki kwake kumethibitishwa na shuhuda nyingi, amesema yafuatayo katika hadithi kuwa jiwe hilo ni yeye mwenyewe:
“Tashbihi ya Mitume kabla yangu na mimi ni kama jengo lililojengwa vizuri sana lakini halina jiwe la msingi. Watu walioliangalia walivutiwa sana kwa uzuri wake; hata hivyo, walistaajabu kuhusu kutokuwepo jiwe la msingi. Hapa jengo hilo limekamilishwa nami na Utume unaishia kwangu.” (1)
14. Katika Biblia, kumeelezwa habari za Mtume atakayekuja na atakayekuwa mkuu wa ulimwengu kuwa ni “mwenye Sayf na fimbo.” (2) Neno la Kiarabu Sayf hapa linamaanisha upanga. Kwa hivyo, Mtume ana wajibu wa kupigana Jihad. Kwa hivyo, mtu huyu hawezi kuwa Yesu (AS) kwa sababu hakuteuliwa kufanya Jihad na Hakupigana vita. “Mwenye upanga” anaweza kuwa ni Mtume Muhammad (S.A.W) peke yake. Kwa kuwa Mtume Muhammad (S.A.W) na ummah Wake aliteuliwa kupigana Jihad. Licha ya hivyo, Mtume Muhammad ana fimbo na alikuwa akitembea nayo.
15. Na tena, Mtume atakayekuja baadaye ametajwa kuwa ni “Sahib-ut Taj” (mwenye taji). (3) Hili pia ni jambo lake pekee Mtume Muhammad (S.A.W). Maana ya Taj ni kilemba alichokuwa akijizungushia kichwani. Hapo kale, watu waliokuwa wakivaa kilemba (vazi la kichwani) miongoni mwa mataifa walikuwa ni Waarabu. Kwa hivyo, ‘Sahib-ut Taj’ aliyetajwa katika Biblia kwa hakika inamaanisha ni Mtume Muhammad (S.A.W).
SWALI: Kwa nini kwamba ilhali mitume wengine wanabashiri kuja kwa Muhammad (S.A.W), Yesu (A.S) anafanya hivyo kikamilifu na katika namna ya habari njema?
JIBU: Kwa sababu Ahmad (S.A.W) alimtetea Yesu (S.A.W) dhidi ya madai na kashfa za kutisha za Wayahudi, na ameokoa dini yake dhidi ya kupotoshwa. Zaidi ya hivyo, mbele ya udhia wa Shari‘a za Wana wa Israil, ambao hawakumtambua Yesu, alikuja na Shari‘a iliyoadilishwa ambayo ilikuwa nyepesi, yenye kuenea kote, na iliyoziba mapungufu ya Shari‘a ya Yesu’. Kutokana na sababu hizo, Yesu mara nyingi alitoa habari njema kuwa "mtawala wa dunia" atakuja!
[1]Sahihu’l-Bukhari, IV, 162- 163
[2]Nabhani, Hujjatullah ala’l-Alamin, 99, 114.
[3] Nabhani, Hujjatullah ala’l-Alamin, 113,114; Ali al-Qari, Sharhu’sh-Shifa, 1:739.
Shuhuda za Utume wa Hadhrat Muhammad (S.A.W) katika Taurati Iliyogeuzwageuzwa.
Qur’an inasema kuwa Wayahudi walikiuzageuza kitabu kitukufu cha dini yao, Taurati, kwa kubadilisha sehemu za maneno yake na maana zake. Hiyo ndiyo sababu juu ya ishara zilizomhusu Mtume Muhammad (S.A.W) ndizo zilizokusudiwa kugeuzwageuzwa na kubadilishwa na Wayahudi. Watu wa kitabu kitukufu, waliobadilisha maana halisi za maneno, walileta ugumu wa kufahamu ishara za maelezo ya Mtume Muhammad (S.A.W).
Aya zinazoashiria jambo hilo kutoka katika Qur’an ni kama ifuatavyo:
“Miongoni mwa Mayahudi wamo ambao hubadilisha maneno kuyatoa mahala pake, na husema: Tumesikia na tumeasi…” (an-Nisa, 4/46)
“Wao huyabadilisha maneno kutoka pahala pake. Wanasema: Mkipewa haya basi yashikeni, na msipo pewa haya tahadharini …” (al-Maida, 5/41)
Sasa tuangalie maneno ya Taurati yanayomwashiria Mtume Muhammad (S.A.W):
1. Kwa maana Bwana wa majeshi asema hivi, Mara moja tena, “Ni kitambo kidogo tu, nami nitazitikisa hizo mbingu, na hii nchi, na bahari, na nchi kavu; nami nitatikisa mataifa yote, na vitu vinavyotamaniwa na mataifa yote vitakuja; nami nitaijaza nyumba hii utukufu, asema Bwana wa majeshi.” (Agano la Kale Haggai 2:6-7)
Habari njema za kuja kwake na neno la "Himada" katika maandiko ya asili ya Taurati yanatokana na mzizi wa jina Muhammad kwa Kiarabu na herufi za maneno Ahmad kuwa ni “Ha, Mim na Dal” na hayo kwa kawaida yana maana moja. Kwa hivyo, neno linaloleta maana ya jina la Mtume Muhammad (S.A.W) limetajwa pamoja na tukio kubwa sana litakalotokea baadaye kwa mujibu wa maneno ya aya hiyo.
Kwa hivyo, lipi linaloweza kuwa kubwa zaidi ya ujio wa Mtume Muhammad (S.A.W), aliyeeneza habari ya kuwepo Mungu kwa mabilioni ya watu baada ya Agano la Kale? Kwa hiyo aya hii ya Taurati inaeleza habari za Mtume Muhammad (S.A.W) na ushindi wa Uislamu duniani kote, ambao ni jambo kubwa sana na tukufu.
2. Sehemu ya 42 ya Isaya ya Agano la Kale inaeleza ukweli kuhusu Mtume Muhammad (S.A.W) na kuja kwake… Hebu kwanza tusome sehemu inayohusiana nayo ya Agano la Kale na kisha tuchanganue maneno hayo, ambayo yapo katika Taurati:
“Tazama mtumishi wangu nimtegemezaye; mteule wangu, ambaye nafsi yangu imependezwa naye; nimetia roho yangu juu yake; naye atawatolea mataifa hukumu. Hatalia, wala hatapaza sauti yake, wala kuifanya isikiwe katika njia kuu. Mwanzi uliopondeka hatauvunja, wala utambi utokao moshi hatauzima; atatokeza hukumu kwa kweli. Hatazimia, wala hatakata tamaa, hata atakapoweka hukumu duniani; na visiwa vitaingojea sheria yake. Mungu Bwana anena, yeye aliyeziumba mbingu, na kuzitanda; yeye aliyeitandaza nchi na mazao yake; yeye awapaye pumzi watu walio juu yake; yeye awapaye roho wao waendao ndani yake. Mimi, Bwana, nimekuita katika haki, nami nitakushika mkono, na kukulinda, na kukutoa uwe agano la watu, na nuru ya mataifa; kuyafunua macho ya vipofu, kuwatoa gerezani waliofungwa, kuwatoa wale walioketi gizani katika nyumba ya kufungwa. Mimi ni Bwana; ndilo jina langu; na utukufu wangu sitampa mwingine, wala sitawapa sanamu sifa zangu. Tazama, mambo ya kwanza yamekuwa, nami nayahubiri mambo mapya; kabla hayajatokea nawapasheni habari zake. Mwimbieni Bwana wimbo mpya, Na sifa zake tokea mwisho wa dunia; Ninyi mshukao baharini, na vyote vilivyomo, Na visiwa, nao wakaao humo. Jangwa na miji yake na ipaze sauti zao, Vijiji vinavyokaliwa na Kedari; Na waimbe wenyeji wa Sela, Wapige kelele toka vilele vya milima.”
Kuna ulinganifu baina ya maneno yaliyomo katika Isaya ya Agano la Kale sehemu ya 42, na Mtume Muhammad (S.A.W). Maneno ya mambo hayo yaliyobashiriwa pia ni muhimu sana. Kwa hivyo, habari hiyo njema haikufunuliwa katika enzi za Musa (AS) au hata kabla yake. Hayo yatatokea kweli baadaye… Habari njema zilizoelezwa hapa ni Mtume Muhammad (S.A.W) na hebu tuone hayo kwa kuchanganua neno moja baada ya jingine:
a. “Tazama mtumishi wangu nimtegemezaye; mteule wangu, ambaye nafsi yangu imependezwa naye; nimetia roho yangu juu yake; naye atawatolea mataifa hukumu.” (Agano la Kale 42:1)
Sentensi hii ya Agano la Kale inamwashiria kikamilifu Mtume Muhammad (S.A.W). Kwa kuwa Mungu alimsaidia, alimridhia na alimteua miongoni mwa wanadamu. Licha ya hivyo, Mungu alimtuma kwake Jibril (AS) (Malaika mkuu) na kuweka haki miongoni mwa mataifa pamoja naye. Kwa hivyo, sifa tano za mtu huyo zilizotolewa habari njema katika maneno hayo anazo. Sentensi hii ya Taurati inatoa habari njema kikamilifu za Mtume Muhammad (S.A.W) kwa maneno yake yote.
b. “Hatalia, wala hatapaza sauti yake, wala kuifanya isikiwe katika njia kuu. Mwanzi uliopondeka hatauvunja, wala utambi utokao moshi hatauzima; atatokeza hukumu kwa kweli…” (Agano la Kale 42:2-3)
Maneno hayo, yaliyomo katika Taurati, yanaeleza kuhusu maadili ya juu ya Mtume Muhammad (S.A.W). Wakati Qur’an inaeleza sifa za Mtume Muhammad kwa maneno “Na wewe uko katika tabia bora kabisa” (1), Taurati imeeleza hilo kama ilivyooneshwa hapo juu. Kwa hivyo, mtu ambaye habari njema zinatolewa atakuwa ni mwenye maadili ya juu. Mtume Muhammad (S.A.W) ana maadili hayo ya juu sana na anakubalika kwa kila mtu.
c. “Hatazimia, wala hatakata tamaa, hata atakapoweka hukumu duniani; na visiwa vitaingojea sheria yake…” (Agano la Kale 42:4)
Maneno hayo ya Taurati pia yanafahamisha habari za Mtume Muhammad (S.A.W). Kwa kuwa Mtume Muhammad (S.A.W) alitawala ardhi alipokuwa hai na akahifadhi haki. Na kamwe hakukosa ujasiri wake. Hata pindi alipoteremshiwa aya, “Allah atakulinda dhidi ya watu (yaani fitina)” (2), aliwaondoa walinzi waliokuwa wakisubiri mbele ya hema lake na akawaambia; “Sasa Allah atanilinda, hamna haja ya kusubiria hapa.” (3) Watu na mataifa ambao walichoka mateso na dhuluma walimngojea mtu huyu. Kwa hivyo, maneno hayo yanafahamisha habari za ujasiri wa Mtume Muhammad (S.A.W), kuhifadhi kwake haki na watu wa pwani kumsubiri; kwa mantiki hii, imeashiria na hata kutoa maelezo kumhusu Mtume Muhammad (S.A.W).
d. “Mimi, Bwana, nimekuita katika haki, nami nitakushika mkono, na kukulinda, na kukutoa uwe agano la watu, na nuru ya mataifa…” (Agano la Kale 42:6)
Mtu ambaye habari njema zilitolewa kumhusu yeye katika Taurati ilisemekana kuwa amehifadhiwa na Mungu na kwa sababu hii, katika hali ngumu sana na hata katika nyakati ambapo kunusurika ilishindikana, alihifadhiwa na kufika salama kama ilivyoandikwa katika historia. Hata wakati wa kuhama, pindi uwezekano wa kukamatwa na washirikina ulipokaribia sana pangoni walipojihifadhi na pindi sahibu yake mwaminifu, Abu Bakr (RA), alikuwa akimlilia, alimweleza rafiki yake kuhusu kuwepo ulinzi imara wa kiungu kwa kusema “Usihofu, Mwenyezi Mungu yu pamoja nasi.” (4) katika kila awamu ya maisha ya Mtume (S.A.W), ulinzi huu wa kiungu ulionekana. Wale wanaoyajua maisha ya Mtume watalifahamu hilo vyema zaidi.
Licha ya hivyo, Mtume Muhammad (S.A.W) aliwafanya watu wawe wema baina yao. Uhasama wa damu ulikomeshwa na maadui wakawa marafiki waaminifu, shukrani zimwendee … na tena mataifa yalipata njia ya kweli, shukrani zimfikie na kwa kweli alikuwa chanzo cha nuru. Kwa hivyo, mtu ambaye habari zake njema zimetolewa ana sifa tatu katika Taurati: I. Mungu anamlinda, II. Atakuwa vyema na watu, III. Atakuwa kiongozi wa mataifa; hizo ni sifa zinazojulikana kwa kila mtu.
e. “kuyafunua macho ya vipofu, kuwatoa gerezani waliofungwa, kuwatoa wale walioketi gizani katika nyumba ya kufungwa…” (Agano la Kale 42:7)
Maneno hayo ya Taurati pia yanafahamisha habari za Mtume Muhammad (S.A.W). Kwa kuwa nyoyo butu na akili zenye maradhi ziliponywa, shukrani zimwendee yeye. Kwa msaada wake, nafsi zimekombolewa kutokakatika utumwa wa shari na wale wanaoishi katika giza la ushirikina wameifikia nuru ya tawhid (kumpwekesha Mungu).
f. “Mimi ni Bwana; ndilo jina langu; na utukufu wangu sitampa mwingine, wala sitawapa sanamu sifa zangu…” (Agano la Kale 42:8)
Maneno hayo ya Taurati ni muhimu. Kwa kuwa, kwa aya hii, Mungu anaeleza kuwa mtu kuhusu huyo ambaye habari zake njema zimeelezwa atauvunja ushirikina. Mapambano makubwa zaidi ya Mtume Muhammad (S.A.W) yalikuwa dhidi ya washirikina na alipopata ushindi wa mji wa Makka, jambo la kwanza kabisa alilolifanya lilikuwa ni kuyavunja masanamu.
Licha ya hivyo, katika aya hii, Mungu anasema, “hataruhusu kusifiwa masanamu” Mtume Muhammad (S.A.W) aliifanya kazi hiyo pamoja na kutamka maneno “Alhamdulillah”, alieleza kuwa kila sifa njema ni kwa Mungu. Kwa hivyo, mtu ambaye habari zake njema zinaelezwa ni Mtume Muhammad (S.A.W) kwa sababu Mtume Muhammad (S.A.W) alitimiza kwa mafanikio kazi ya mtu kuhusu ambaye habari zake njema zimeelezwa.
g. “Jangwa na miji yake na ipaze sauti zao, Vijiji vinavyokaliwa na Kedari; Na waimbe wenyeji wa Sela, Wapige kelele toka vilele vya milima.” (Agano la Kale 42:11)
Maneno hayo ya Taurati pia yanafahamisha habari za Mtume Muhammad (S.A.W). Kwa kuwa, Mtume Muhammad (S.A.W) alikuwa mwanachama wa jumuia iliyotokana na wajukuu wa Kadar, ambaye alikuwa mwana wa Ismail (S.A.W), mwana wa Abraham (AS). Kwa hivyo, maneno hayo yanaashiria mababu wa Mtume Muhammad (S.A.W).
Kwa kifupi, Sehemu hizo za Agano la Kale zinalingana kikamilifu na Mtume Muhammad (S.A.W). Licha ya hivyo, katika muendelezo wa sehemu hii ya Agano la Kale, aya ya 17, kufedheheshwa kwa washirikina ni muhimu kwa sababu ufedheheshwaji huo ulifanywa na Mtume Muhammad (S.A.W). Ndiyo, pamoja na uchambuzi wa kina zaidi, mtu anaweza kukuta ishara nyingi zaidi katika Agano la Kale. Kwa hivyo, kama zilivyo sayansi nyingi kuanzia taaluma ya maisha ya kiinitete (embriolojia) mpaka unajimu, kutoka jiolojia mpaka elimukale (akiolojia) zinathibitisha kinachosemwa na Qur’an, ishara za Agano la Kale zinathibitisha utume wake Mtume Muhammad (S.A.W).
3. “Mimi nitawaondokeshea nabii miongoni mwa ndugu zao mfano wako wewe, nami nitatia maneno yangu kinywani mwake, naye atawaambia yote nitakayomwamuru.” (Agano la Kale, kitabu kitukufu cha Kumbu Kumbu la Torati, 18:18)
4. “Kwa maana Musa kweli alisema ya kwamba, Bwana Mungu wenu atawainulieni nabii, katika ndugu zenu, kama mimi; msikieni yeye katika mambo yote atakayonena nanyi. Na itakuwa ya kwamba kila mtu asiyemsikiliza nabii huyo ataangamizwa na kutengwa na watu wake. Naam, na manabii wote tangu Samweli na wale waliokuja baada yake, wote walionena, walihubiri habari za siku hizi.” (Agano Jipya, Matendo 3:22-23)
Sasa hebu tuchanganue sentensi hizi mbili zilizochukuliwa kutoka katika Biblia:
a. Hotuba ya Hadhrat Musa (AS) kama “ndugu zako” kwa Wana wa Israil, waliokuwa wanatokana na mbari ya Ishaq (AS), ambaye alikuwa mwana wa Hadhrat Ibrahim (AS), ni ishara wa wajukuu wa Hadhrat Ismail (AS) ambaye alikuwa ni kaka yake Hadhrat Ishaq (AS), yaani, kwa wana wa Ismail. Mtume aliyetokana na wana wa Ismail ni Mtume Muhammad (S.A.W) peke yake kwa sababu Mtume Muhammad (S.A.W) peke yake ndiye aliyetokana na mbari ya Ismail. Hadhrat Joshua (AS) na Yesu (AS) hawakutokana na wajukuu wa mbari ya Hadhrat Ismail bali walitokana na wana wa Israil.
b. Usemi “mtume kama mimi”, Hadhrat Musa (AS) alimkusudia Mtume Muhammad (S.A.W). Kwa kuwa Mtume Muhammad (S.A.W) ndiye aliyeshabihiana na Hadhrat Musa mpaka sifa ishirini kama vile jihad, sheria na kanuni alizoweka, adhabu aliyoweka na utii wa jumuia kwake… lakini si Hadhrat Joshua au Yesu (AS).
c. Maneno katika aya, “Nitatia maneno yangu katika kinywa chake” ni ishara ya hali ya kutokujua kusoma na kuandika ya Mtume Muhammad (S.A.W) na ingawa hakujua kusoma na kuandika, alihifadhi neno la Mungu kiurahisi na aliwasomea watu. Habari hii ilidhihirika kweli sawa sawa na ilivyosemwa.
Na tunataka kuonesha maneno yaliyomo katika aya za 18 na 19 za Agano la Kale, kitabu kitukufu cha Kumbu Kumbu la Torati: katika sentensi hizo, kumesisitizwa kuwa “mtume huyo anazungumza neno la Bwana wake”. Sifa mojawapo muhimu ya Qur’an aliyoteremshiwa Mtume Muhammad (S.A.W) ni kuwa, surah 113 kati ya 114 zinaanza na “Basmala” yaani “B-ismi-llahi r-rahmani r-rahim” ("Kwa Jina la Allah, Mwingi wa Rehema, Mwenye Kurehemu"). Licha ya hivyo, Mtume Muhammad (S.A.W) alianza kusoma aya za Quran na kila kitu kwa Basmala na aliunasihi ummah wake kufanya hivyo. Hivyo, mtu ambaye habari zake njema zilielezwa katika Agano la Kale na yeye kuelezwa kuwa ni mwenye kuanza mambo kwa jina la Mwenyezi Mungu ni Mtume Muhammad (S.A.W).
5. “Bwana alitoka Sinai, Akawaondokea kutoka Seiri; Aliangaza katika kilima cha Parani, Akaja Meribath-Kadeshi na watukutu elfu kumi. Upande wake wa kuume Palikuwa na sheria ya moto-moto kwao.” (Agano la Kale, kitabu kitukufu cha Kumbu Kumbu la Torati, 33:2)
a. Katika maneno haya ya Taurati: “Alitoka Sinai” ni ishara inayomhusu Hadhrat Musa (AS) na ufunuo wa kiungu wa amri kwake; kwa upande mwingine, “Akawaondokea kutoka Seiri” ni ishara inayomhusu Yesu (AS) na ufunuo of Biblia kwake, na hatimaye “Aliangaza katika kilima cha Parani” ni a ishara kwa ajili ya Mtume Muhammad kuwa atatokea Makka. Kwa kuwa Paran hutamkwa Faran kwa lugha ya Kiarabu na Faran ni katika majina ya zamani ya Makka.
Licha ya hivyo, sentensi zinazosema kuwa Hadhrat Ismail anaishi katika jangwa la Paran kutoka katika Agano la Kale pia ni ushahidi wa hilo. Kwa kuwa Hadhrat Ismail (AS) alikuwa akiishi Makka. Kwa hivyo, Paran ni Makka kwa ishara ya Agano la Kale. Kwenye maneno ya Taurati, Mungu anaeleza kuwa “Aliangaza katika kilima cha Parani”. Ni nani anayeweza kuwa aliangaza hapo asiyekuwa Mtume Muhammad (S.A.W)?
b. Kinachomaanishwa kwa maneno mtukufu katika maneno yaliyomo katika maneno “alikuja pamoja na watukufu elfu kumi” ni Ahl al-Bayt wa Mtume Muhammad na swahaba zake. Katika kipindi kifupi sana, jumuia hii tukufu ilifikia mpaka idadi ya watu elfu kumi na hata mamia ya maelfu.
c. Maneno “Upande wake wa kuume Palikuwa na sheria ya moto-moto kwao” yanasimama kwa ajili ya jihad na pia ni ishara kuwa mitume wa baadaye wana jukumu la Jihad. Mtume Muhammad (S.A.W) na jumuia yake wanawajibika na jihad; kwa hivyo, mtu aliyeashiriwa katika maneno husika yanahakikisha kuwa mtu huyo ni Mtume Muhammad (S.A.W). Kwa hivyo, maneno hayo ya Taurati yanafahamisha habari za Mtume Muhammad (S.A.W) kwa alama za mara tatu.
6. Mungu akamwambia Ibrahimu, “Neno hili lisiwe baya machoni pako, kwa ajili ya huyo mwana, na huyo mjakazi wako. Kila akuambialo Sara, sikiza sauti yake, kwa maana katika Isaka uzao wako utaitwa. Naye mwana wa mjakazi nitamfanya kuwa taifa, maana huyu naye ni uzao wako. Ibrahimu akaamka asubuhi na mapema akatwaa mkate na kiriba cha maji, akampa Hajiri akimtwika begani pake, na kijana, akamruhusu; naye akatoka, akapotea katika jangwa la Beer-sheba. Yale maji yakaisha katika kiriba, akamlaza kijana chini ya kijiti kimoja. Akaenda akakaa huku akimkabili, mbali naye kadiri ya mtupo wa mshale; maana alisema, Nisimwone kijana akifa; naye akakaa akimkabili, akapaza sauti yake, akalia. Mungu akasikia sauti ya kijana.”
“Malaika wa Mungu akamwita Hajiri kutoka mbinguni, akamwambia, Una nini, Hajiri? Usiogope, maana Mungu amesikia sauti ya kijana huko aliko. Ondoka, ukamwinue kijana, ukamshike mkononi mwako, kwa kuwa nitamfanya kuwa taifa kubwa. Mungu akamfumbua macho, naye akaona kisima cha maji; akaenda akakijaza kiriba maji, akamnywesha kijana. Mungu akawa pamoja na huyo kijana, naye akakua, akakaa katika jangwa, akawa mpiga upinde. Akakaa katika jangwa la Parani; mama yake akamtwalia mke katika nchi ya Misri.” (Mwanzo 21, 12-21)
Katika sehemu hii ya Taurati, kuna maelezo kuwa taifa litaundwa kutokana na mwana wa Hadhrat Hajar. Taifa hilo ni Mtume Muhammad (S.A.W) na ummah wa Kiislamu. Hakuna mitume wengine waliokuja kutokana na wajukuu wa Hadhrat Ismail isipokuwa Mtume Muhammad (S.A.W).
7. “Kwa hakika Mungu alimwambia Ibrahim kuwa Hajar - mama yake Isma‘il- atazaa watoto. Atatokea mtoto katika wanaye ambaye mkono wake utakuwa juu ya watu wote, na mkono wa watu wote utafunguliwa juu yake kwa utukufu.” (Agano la Kale, Mwanzo, 17)
Maneno hayo ya Taurati pia yanafahamisha habari za Mtume Muhammad (S.A.W). kama tulivyoeleza hapo awali, hakuna mitume wowote maarufu na mashuhuri waliotokana na wajukuu wa Ismail (AS), ambaye alikuwa mwana wa Hajar isipokuwa Mtume Muhammad (S.A.W).
8. “Musa alisema: “Ewe Mola Mlezi! Kwa hakika nimekuta katika Taurati jumuia bora itakayoibuka kwa manufaa ya wanadamu, itakayoamrisha mema na kukataza maovu, na itakayowamini Mungu. Naomba hiyo iwe Jumuia yangu!” Mungu akasema: “Hiyo ni jumuia ya Muhammad…” (Agano la Kale, Isaya, 42)
Jina Muhammad limetajwa kuwa ni Mushaffah, Munhamanna, na Himyata, katika namna ya majina ya Assyrian kwa Kihebrania, katika vitabu vya kimbinguni. Jina Muhammad katika hali yake ya asili lilikuwepo katika sehemu chache. Na hizo chache ziligeuzwageuzwa na Wayahudi. Licha ya hivyo, sentensi alizotamka Musa katika Taurati zinazoeleza jumuia aliyoiona ni za kuvutia sana.
Musa alipoeleza sifa za jumuia hiyo, alisema, “Hao ni watu bora zaidi, iliyotokea katika historia ya wanadamu, kuamrishana mema, kukatazana maovu, na kumwamini Allah.” Maneno hayo hayo yametumika katika aya ya 110 ya sura of Aal-i Imran katika Quran:
“Nyinyi mmekuwa bora ya umma walio tolewa watu, kwa kuwa mnaamrisha mema na mnakataza maovu, na mnamuamini Mwenyezi Mungu.”
Kama inavyoonekana, Upo upatanifu kamili baina ya maneno ya Musa katika Taurati na katika Quran. Upatanifu huu unathibitisha kuwa jumuia hiyo aliyoiona Musa ilikuwa ummah wa Muhammad.
9. “Katika siku za mwisho, ya kwamba mlima wa nyumba ya Bwana utawekwa imara juu ya milima...mataifa yote watakwenda, kila moja kwa jina la mungu wake, na sisi tutakwenda kwa jina la Bwana... (Agano la Kale, Micah 4 verses 1, 2, 5)
Sentensi hiyo ya Taurati inaeleza waziwazi mlima mtukufu zaidi miongoni mwa milima, na takbira na ibada za mahujaji zinazotokea duniani kote; yaani, “ummah wa Muhammad” unaojulikana kama “ummah uliorehemewa.”
10. Agano la Kale, Daniel, sura ya 2: katika sura hiyo, Nebukadneza, aliyepindua dola ya Assyria, aliyeutengeneza mji wa Babeli kuwa ni kituo na aliyetawala kwa miaka arobaini na tatu, ndoto aliyoota na Daniel, aliyefasiri ndoto yake wametajwa. Muhtasari wa kisa hicho ni kama ifuatavyo:
Daniel, aliyekuwa katika jela ya katili Nebukadneza, alimweleza mfalme kuhusu ndoto yake kabla Nebukadneza hajamsimulia Daniel ndoto yake. Mfalme alithibitisha alichosema kwa mshangao na akasema, “Hiyo ilikuwa ndoto, na sasa nifasirie.” Daniel alisema:
“Sanamu ni utawala wa duniani. Wewe ni kichwa chake. Baada yenu, utainuka ufalme mwingine; unawakilishwa na shaba kwa kuwa ni dhaifu kwenu. Kisha, falme mbili zaidi zitakuja na kutanuka. Ufalme mwingine wa chuma utawavunjavunja wengine. Kisha, nafasi yake itachukuliwa na falme nyingine nyingi, nyingine imara na nyingine dhaifu; chuma na udongo haviwezi kuchanganyika pamoja; halikadhalika falme hizo hazitakaa pamoja na kuungana. Kisha, Mungu atazivunja falme hizo na kumpeleka sultan ambaye utawala wake utaendelea mpaka Siku ya Kiama; mtu huyo mtukufu atawapeleka watu kwenye furaha kamili duniani na ahera. Hiyo ndiyo tafsiri ya kutanuka kwa jiwe lililoanguka kutoka mbinguni katika ndoto yako na kuvunja sanamu vipande vipande.“
Sentensi hizo za Taurati, ambapo humo kumeelezwa ndoto zilizofasiriwa na Daniel, zinatufahamisha kuhusu mtu mtukufu atakayeendelea kuishi mpaka Siku ya Kiama pamoja na dini atakayoleta. Hakuna shaka kuwa mtu huyo ni Mtume wetu (s.a.w). Mtume (s.a.w) alivunja masanamu vipande vipande na kupata ushindi duniani kwa usultani yakinifu na nyoyo kwa usultani wa kiroho.
[1] al-Qalam, 68/4.
[2] al-Maida, 5/67.
[3] Tirmidhi, Tafsîr, 5/6.
[4] Abu Nuaym, Dalail, Juz. 2, uk. 328
Shuhuda za Utume wa Hadhrat Muhammad (S.A.W) katika Zaburi Iliyogeuzwageuzwa.
Zaburi, ambayo ni kitabu cha pili katika vitabu vya kiungu, imetajwa katika aya tatu tofauti za Qur’an tukufu. Aya hizo ni hizi zifuatazo:
“Hakika Sisi tumekuletea wahyi wewe kama tulivyo wapelekea wahyi Nuhu na Manabii walio kuwa baada yake. Na tulimpelekea wahyi Ibrahim na Ismail na Is-haka na Yaakub na wajukuu zake, na Isa na Ayub na Yunus na Harun na Suleiman, na Daud tukampa Zaburi.” (An-Nisa, 4/163)
“Na Mola wako Mlezi anawajua vilivyo waliomo mbinguni na katika ardhi. Na hakika tumewafadhilisha baadhi ya Manabii kuliko wengine; na Daudi tulimpa Zaburi..” (Al-Isra, 17/55)
“Na hakika tulikwisha andika katika Zaburi baada ya Kumbukumbu, ya kwamba nchi watairithi waja wangu walio wema.” (Al-Anbiya, 21/105)
Aya mbili za mwanzo katika hizo zinaeleza kuwa Zaburi, ambayo ni mojawapo ya vitabu vinne vya kiungu, alipewa Daud (AS) na aya ya tatu inaeleza kuwa Zaburi ilitumwa baada ya Taurati…
Sasa, tutaangalia katika sehemu za Zaburi, ambapo kuna ishara zinazomhusu Mtume Muhammad (S.A.W).
1. “Wewe u mzuri sana kuliko wanadamu; Neema imemiminiwa midomoni mwako, Kwa hiyo Mungu amekubariki hata milele. Jifungie upanga wako pajani, wewe uliye hodari, Utukufu ni wako na fahari ni yako. Katika fahari yako usitawi uendelee Kwa ajili ya kweli na upole na haki Na mkono wako wa kuume Utakufundisha mambo ya kutisha. Mishale yako ni mikali, watu huanguka chini yako; Imo mioyoni mwa adui za mfalme. Kiti chako cha enzi, Mungu, ni cha milele na milele, Fimbo ya ufalme wako ni fimbo ya adili. Umeipenda haki; Umeichukia dhuluma …” (Zaburi, 45:2-7)
Sasa, tuangalie jinsi maneno hayo ya Zaburi yanamkusudia dhahiri Mtume Muhammad (S.A.W):
a. “Wewe ni mbora zaidi katika watu…”
Mazuri ya dhahiri ya Mtume Muhammad (S.A.W) yaliyojumuika juu ya kiwiliwili chake kitukufu na ambayo pia yanaashiria mazuri yake ya ndani hayapo kwa yeyote. Zaidi ya hivyo, Imam Qurtubi anasimulia kuwa uzuri wa Mtume Muhammad (S.A.W) haukujitokeza kikamilifu. Kama uzuri wake wa juu juu ungeweza kuonekana kikamilifu, maswahaba wasingemudu kumwangalia. (1)
Jabir bin Samura (RA) anasimulia; “Nilimwona Mtume Muhammad (S.A.W), ambaye alikuwa ni jua la ulimwengu katika usiku wa mbalamwezi. Alikuwa amevaa joho jekundu. Nilianza kuuangalia uso wake uliokuwa uking’aa na mwezi ili kujaribu kujua kipi kilikuwa kizuri zaidi. Ninaapa kwa Allah kuwa utukufu wa uso wa Mtume Muhammad (S.A.W), ambaye alikuwa karibu yangu, ulikuwa mzuri kuliko mwezi.” (2)
Hadhrat Aisha (RA) anaeleza uzuri wa Mtume (S.A.W) kwa maneno yafuatayo: Wanawake walioona uzuri wa Hadhrat Yusuf (AS) walijikata vidole baada ya kujisahau; kama wangemwona Mtume Muhammad (S.A.W), wangejikata mikono yao.”
b. “Kazeni mapanga yenu juu ya mapaja yenu …”
Mtume Muhammad (S.A.W) anasema yafuatayo katika Hadithi yake mojawapo: “Nimetumwa pamoja na upanga katika kipindi kinachokaribiana na Siku ya Kiama…” (3) Aya hii ya Zaburi pia inaonesha kuwa Mtume atakayekuja anaitwa “Sahib as-Saif”; yaani, atakuwa mwenye upanga na atawajibika kupigana jihad. Na ummah wake pia unaitwa Sahib as-Saif; yaani, watawajibika kupigana jihad. Habari hizo za Zaburi zinaweza kuonekana katika maisha Mtume (S.A.W) na katika jumuia yake katika uhalisia wake.
c. “Kwa niaba ya ukweli, fedheha, na uadilifu. Uruhusu mkono wako wa kulia udhihirishe amali za kiuchamungu.”
Sentensi za Zaburi pia zimetaja habari za haki ya Mtume Muhammad (S.A.W). Kwa hakika, Mtume Muhammad (S.A.W) ni mwenye busara zaidi kati ya wanadamu. Yafuatayo yamesimuliwa: Mwanamke wa kabila la Mahzumi aliiba. Makuraishi hawakutaka mwanamke huyo, kutoka kabila tukufu aadhibiwe. Mtume Muhammad (S.A.W) alimpenda sana Usama bin Zayd. Walijua kuwa Mtume asingeumiza hisia zake. Kwa sababu hiyo, walimwomba Mtume asimwadhibu mwanamke huyo kwa kumweka Usama kama mhenga. Mtume (S.A.W) alimwambia Usama kama ifuatavyo:
“Wana wa Israil waliangamizwa kwa sababu tu walikuwa na upendeleo. Walikuwa wakiwaadhibu masikini kwa adhabu kali sana lakini hawakuwaadhibu matajiri na wenye ushawishi. Ninaapa kwa Allah kuwa kama binti yangu mwenyewe Fatima atatenda uhalifu huo, nitamwadhibu vivyo hivyo.” (4)
Mtume Muhammad (S.A.W) hakufanya ubaguzi wowote wa kidini pindi alipofanya maamuzi ya kisheria. Kama Myahudi alikuwa katika upande wa haki, Alimpa Myahudi huyo haki yake kwa kuichukua kutoka kwa Muislamu. Vitabu vya Sirah vimejaa visa vinavyohusu uadilifu wa kipekee wa Mtume.
c. “Mishale yako ina ncha kali. Mataifa yatakuangukieni chini yenu, kwa mishale katika moyo wa maadui wa mfalme …”
Ukweli wa habari hizi za Zaburi pia unaonekana katika maisha ya Mtume Muhammad (S.A.W). Kwa kuwa Uajemi, Byzantina, India, China na nchi nyingine nyingi zilishindwa na watu wake wengi walisilimu na kuingia katika ummah wa Mtume Muhammad (S.A.W). Na maneno hayo ya Zaburi yanaelezwa katika aya za Qur’an kama ifuatavyo:
“Mali aliyo leta Mwenyezi Mungu kwa Mtume wake kutoka kwa watu wa hivi vijiji ni kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, na kwa ajili ya Mtume, na jamaa, na mayatima, na masikini, na msafiri, ili yasiwe yakizunguka baina ya matajiri tu miongoni mwenu. Na anacho kupeni Mtume chukueni, na anacho kukatazeni jiepusheni nacho. Na mcheni Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mkali wa kuadhibu.” (Al-Hashr, 59/7)
e. “Umewapenda walio wema, na kuuchukia walio uovu.”
Sentensi hii inafahamisha kuhusu sifa mbili za Mtume Muhammad (S.A.W) kama sifa hizo zilivyoelezwa katika Qur’an kama ifuatavyo:
“Nyinyi mmekuwa bora ya umma walio tolewa watu, kwa kuwa mnaamrisha mema na mnakataza maovu, na mnamuamini Mwenyezi Mungu. Na lau kuwa Watu wa Kitabu nao wameamini ingeli kuwa bora kwao. Wapo miongoni mwao waumini, lakini wengi wao wapotovu.” (Aal-e-Imran, 3/110)
2. “Badala ya baba zako watakuwapo watoto wako, Utawafanya kuwa wakuu katika nchi zote. Jina lako nitalifanya kuwa kumbukumbu Katika vizazi vyote. Kwa hiyo mataifa watakushukuru Milele na milele.” (Zaburi 45:16-17)
Sentensi hizi za Zaburi pia zinamhusu Mtume Muhammad (S.A.W) kwa sababu, ingawa miaka 1400 imepita tangu kifo cha Mtume Muhammad (S.A.W), waumini wamekuwa wakisoma salawat kwa kusema “Swalli 'ala Muhammadin wa 'ala ali Muhammad…” hususani baada ya swala tano za kila siku kwa enzi nyingi. Kwani yupo mwingine anayetajwa sana kama Mtume Muhammad (S.A.W) juu ya ardhi? Kwa hakika hapana. Kwa hivyo, inawezekana kwamba mtu aliyetajwa katika Zaburi si Mtume Muhammad (S.A.W)?
3. “Na awe na enzi toka bahari hata bahari, Toka Mto hata miisho ya dunia. Wakaao jangwani na wainame mbele zake; Adui zake na warambe mavumbi. Wafalme wa Tarshishi na visiwa na walete kodi; Wafalme wa Sheba na Seba na watoe vipawa. Naam, wafalme wote na wamsujudie; Na mataifa yote wamtumikie. Kwa maana atamkomboa mhitaji aliapo, Na mtu aliyeonewa iwapo hana msaidizi. Atamhurumia aliye dhaifu na maskini, Na nafsi za wahitaji ataziokoa. Atawakomboa nafsi zao na kuonewa na udhalimu, Na damu yao ina thamani machoni pake. Basi na aishi; Na wampe dhahabu ya Sheba; Na wamwombee daima; Na kumbariki mchana kutwa. Na uwepo wingi wa nafaka Katika ardhi juu ya milima; Matunda yake na yawaye-waye kama Lebanoni, Na watu wa mjini wasitawi kama majani ya nchi. Jina lake na lidumu milele, Pindi ling'aapo jua jina lake liwe na wazao; Mataifa yote na wajibariki katika yeye, Na kumwita heri. Na ahimidiwe Bwana, Mungu, Jina lake tukufu na lihimidiwe milele; Dunia yote na ijae utukufu wake!” (Zaburi 72, 2-19 muhtasari)
Mwenye kusikia sentensi za Zaburi atahakikisha kuwa zinamsifia Mtume (s.a.w). Sifa zote zilizotajwa katika aya hizo za Zaburi zipo kwa Mtume (s.a.w).
Mpaka katika sehemu hii ya somo letu, tumesoma baadhi ya sehemu zilizogeuzwa za Injili, Taurati na Zaburi zilizomwashiria Mtume (s.a.w). Tumehakikisha kabisa kuwa mbili jumlisha mbili ni sawa sawa na nne kuwa vitabu vya kimbinguni vinamtaja Muhammad (s.a.w) na kutoa habari njema kuwa atafika. Ingawa vitabu hivyo vya kimbinguni vimegeuzwageuzwa sana na hususani aya zinazomhusu Mtume (s.a.w) zilijaribiwa kubadilishwa na kuondoshwa, Hadhrat Muhammad (s.a.w) anang’aa sana kama jua katika vitabu vya kimbinguni vilivyopo.
[1] Peygamberimizin Şemaili, Prof.Dr. Ali Yardım, Damla Yayınları.
[2] Darimi, Muqaddima, 10.
[3] Tirmidhi Vol. 3 p. 213; Ahmad bin Hanbal V/218.
[4] Bukhari, Anbiya 54, Hudud 12; Muslim, Hudud 8, 9.
2
Kwa nini Mtume Muhammad (s.a.w.) alioa wake wengi?
Hebu tuangazie suala hili kwa mtazamo wa haiba yake safi kabisa. Kwanza kabisa, lazima ieleweke kwamba Mtume (s.a.w.), ambae ni kilele cha juu cha maadili, hakuoa mpaka alipofikia umri wa miaka 25. Kulingana na mazingira ya nchi yenye joto kali na kuwa aliishi kwa kujizuia, ambao ni ukweli uliokubalika tangu alipokuwa akiishi, kwa miaka mingi, itaonekana kuwa amejizuia, utashi madhubuti na udhibiti imara wa nafsi yake. Kama angefanya chembe ya kosa katika suala hili, maadui zake siku za nyuma na leo wangekuwa wameshalitangaza duniani. Hata hivyo, maadui zake wote katika nyakati zilizopita na leo hawathubutu kusema jambo kama hilo licha ya kumsifu kwa mambo tele yasiyowezekana kwake.
Mtume (s.a.w.) alioa kwa mara ya kwanza akiwa na umri wa miaka ishirini-na-tano. Ndoa hii ilikuwa kati yake na mwanamke aliyekuwa na hadhi ya juu sana na wa kipekee mbele ya Allah na Mjumbe Wake bali alishaolewa mara mbili hapo kabla. Ndoa hiyo ya furaha ilidumu kwa miaka ishirini-na-tatu na kumalizikia mwaka wa nane wa utume kama pazia lililoanguka chini, likiacha machungu ya muda mrefu nyuma yake. Mtume (s.a.w.) akaachwa mkiwa tena kama alivyokuwa hadi miaka 25. Baada ya miaka-23 ya maisha ya furaha, Mtume alikuwa mzazi pekee wa watoto wao kwa miaka mine au mitano; alikuwa na umri wa miaka khamisini-na-tatu.
Alipoanza kuoa mwanamke mwingine, alishafikisha miaka 55, huku kukisalia shauku na hamu ndogo ya kuoa. Jambo lisilokubaliwa na dhamiri, akili na moyo kuizingatia ndoa baada ya umri wa miaka hamsini-na-tano katika nchi yenye ashiki kuwa ni jambo linalohusiana na matamanio na ashiki.
Suala jingine linalokuja akilini hapa ni mandhari ya utume wa Mjumbe ililazimu kuoa wake wengi.
A) Awali ya yote, ieleweke kwamba wanaozungumza namna hiyo labda ni wale wasiokubali kanuni zozote na dini au ni wale wajumbe wa dini nyingine zilizoegemea vitabu tofauti. Zama za kale hazina haki kwa vyovyote vile kutoa shutuma kwa kitu kama hiki kwa sababu wao wenyewe wamejihusisha katika mahusiano ya mpito na wapenzi kadhaa wa kadhaa wa kingono bila ya kutii sheria yoyote au kanuni; hata walikuwa na mahusiano ya kujamiaana na maharimu zao; shambulizi la baadaye pia sio la haki, ovu na la kimsukumo; ni jambo lenye kusikitisha kwao. Kuna mitume wengi watukufu waliokubaliwa na vitabu walivyo navyo na mikusanyiko inayofuata vitabu hivyo ambao wameoa zaidi ya mwanamke mmoja na wakaoa sana.
Mathalani, Mtume Suleiman na Daud wakitazamwa, itaonekana kwamba wenye kufuata dini hizo hawatendi haki wanapopinga mfumo wa wake wengi. Mtume Muhammad (s.a.w.) hakuanzisha mfumo wa wake wengi; isitoshe, mfumo wa wake wengi sio kinyume cha utume wenyewe. Zaidi ya hayo, kama itakavyoonekana baadaye, mfumo wa wake wengi ulikuwa na manufaa kuliko watu wanavyofikiria kwa upande wa wajibu wa utume.
Kwa namna fulani, mfumo wa wake wengi ni muhimu hasusani kwa mitume walioleta amri za dini mpya na shariah kwa sababu kuna masuala mengi ya dini yanayohitaji ufaragha wa familia; masuala hayo yanaweza tu kufundishwa kikamilifu na mke wa mtume. Kwa hivyo, kunahitajika walimu wanawake watakaochambua vipengele hivyo vya dini kwa uwazi bila ya kutumia vidokezo au vijembe – namna hiyo ya masimulizi inaleta ugumu kufahamika na kuyatekeleza masuala hayo kwa vitendo.
Wake wema na wanaojizuia wa nyumba ya Mtume ndio wenye jukumu la kuwaongoza na kuwafikishia wanawake; kwa hivyo, wao ni lazima kwa Mtume, utume na dunia ya kinamama.
B) Kipengele kingine inayohusiana na wake wa Mtume (s.a.w.)
1) Kwa kuwa miongoni mwa wakeze walikuwepo vijana, wa makamo, na kinamama wakongwe, hukumu za kidini zilizohusiana na utofauti wa umri wao na uzoefu zikaasisiwa. Wakafundishwa na kutekeleza kwa vitendo kwanza ndani ya nyumba ya Mtume, shukurani kwa kinamama hao waliojizuia.
2) Kwa kuwa kila mke alitoka katika ukoo au kabila tofauti, mafungamano ya kijamaa yakaasisiwa kati ya makabila hayo na baadaye kati ya Mtume na makabila hayo, yaliyowezesha kuwepo upendo wa kina na undugu katika jumiua nzima. Kila ukoo na kabila lilimzingatia kuwa ni mmoja ya wanafamilia yao na walihisi manufaa makuwa kwake kwa pande zote mbili kidini na kindugu.
3) Kila mke aliyemuoa kutoka kabila tofauti, kumethibitisha manufaa makubwa na kuuhudumia Uisilamu katika vipindi vyote viwili maishani mwake Mtume na baadaye; walifikisha sunnah thabiti na za dhahiri na hukumu za dini kwa watu wao wa karibu na wa mbali. Kwa nanma hii, koo zao, wanawake na wanaume, zilijifunza Quran, tafsir (tafsiri ya Quran) na hadithi kutoka kwao; na waliweza kufahamu roho ya dini.
4) Kupitia ndoa hizi, Mtume aliasisi mafungamano ya kindugu takribani Uarabuni kote, ambazo ziliwapa uhuru wa kuhama na kukubalika kama ni mmoja ya kila familia. Shukurani kwa mahusiano haya ya karibu, kila mmoja aliweza kumwendea yeye binafsi na kujifunza amri za dini moja kwa moja kutoka kwake. Makabila pia kwa ujumla wao kutokana na ujirani wao kwake: yalijiona kuwa yalibahatika na yakajifaharisha kwa mahusiano hayo.
Bani Makhzum kupitia kwa Umm Salama, ukoo wa Umayya kupitia kwa Umm Habiba na ukoo wa Hashim kupitia kwa Zaynab bint Jahsh walijiona kuwa wako karibu na Mtume na kujiona kuwa ni wenye bahati.
C) Tuliyoyataja hivi punde ni ya ujumla na yanaweza kuwa ni kweli kwa mitume wote katika hali kadhaa. Sasa tutashughulikia kimahususi manufaa ya kila mke wa Mtume Muhammad mmoja baada ya mwingine:
Hapa tutaona kuwa sababu na mantiki ya mtu kutii kikamilifu mbele ya maisha yaliyobarikiwa ya Mtume (s.a.w.), aliyeungwa mkono na ufunuo; kwa maneno mengine, fikra za mtu zinalazimika kunyenyekea mbele ya kipaji hiki, ambacho kipo chini ya kivuli cha ufunuo.
1) Hadhrat Khadija (Allah amridhie) alikuwa ni mke wa kwanza wa Mtume. Ndoa yake kwa mwanamke huyu tunu, aliyekuwa mkubwa zaidi ya yeye kwa miaka 15, ni mfano adhimu zaidi kwa kila ndoa. Alikuwa mtiifu kwa Hadhrat Khadija na alimheshimu wakati wa ndoa yao; hakumsahau baada ya kufariki na alimtaja karibu kwenye kila tukio.
Mtume (s.a.w.) hakuoa kwa miaka mine au mitano baada ya kifo cha Hadhrat Khadija. Ingawa alilazimika kuwalea watoto kadhaa, aliwatunza kwa mashaka na alitekeleza majukumu kama ni mama na baba kwao. Kama angekuwa na udhaifu wowote kwa wanaweke angeweza kutekeleza hayo?
2) Mke wake wa pili, licha ya kuwa si wa pili kiutaratibu wa miaka na matukio, ni Aisha (Allah amridhie). Ni binti wa Abu Bakr, rafiki wake wa ndani; licha ya kuwa ndoa hii, Mtume alitoa heshima za juu kwa mtu aliyeshirikiana naye katika nyakati zote njema na mbaya. Abu Bakr atakuwa na hadhi ya kuwa pamoja na Mtume katika siku ambayo koo zote zitaishia pamoja na ukoo wa milele. Ndio, Hadhrat Aisha na Abu Bakr walikuwa na hadhi ya kuwa karibu mno na Mtume (s.a.w.) bila ya kuacha mianya yoyote ya kiyakinifu au kiroho.
Isitoshe, Aisha, ambaye alikuwa ni mtu wa kipekee, alikuwa na nguvu za kubeba ujumbe wa kiutume. Maisha yake baada ya ndoa na huduma zake baada yake yamethibitisha kuwa angekuwa ni mke pekee wa mtume. Alikuwa ni mmojawapo katika mabingwa wa kusimulia hadithi, mfasiri mzuri zaidi, na bingwa wa kipekee katika sheria ya Uisilamu; kwa kweli aliwakilisha ubora wa ndani na wa nje na kuwa na uzoefu na Mtume Muhammad pamoja na ufahamu wake usio na kifani.
Kwa hivyo, Mtume aliambiwa ndotoni kuwa angemwoa; hivyo, alipokuwa bado kigori na hajui kitu kuhusu wanaume na mambo ya kidunia, aliandaliwa na kuingizwa katika nyumba ya Mtume.
Hivyo, angekuwa ni chanzo cha heshima kwa Hadhrat Abu Bakr na angeandaliwa kuwa ni mmoja ya wanafunzi wa kusifika zaidi wa Mtume (s.a.w.) miongoni mwa kinamama na mwalimu adhimu na mfikishaji wa ujumbe wa Uisilamu kwa kuviboresha vipaji vyake vyote na uwezo wake. Aliingia katika nyumba iliyobarikiwa ya Mtume (s.a.w.) kwa namna zote mbili mke na mwanafunzi.
3) Mkewe wa tatu, ingawa sio wa tatu kimpangilio wa kimatukio, ni Umm Salama (Allah amridhie). Umm Salama, aliyetokana na ukoo wa Makhzum na mmoja ya Waisilamu wa mwanzo waliosumbuka mno mjini Makkah, alihamia Ethiopia na kisha mji wa Madina, kuwa ni miongoni mwa wale wa daraja la kwanza.
Mumewe alimwandalia safari hizo ndefu na zenye mashaka pamoja naye. Alikuwa ni mtu asiye na kifani katika uoni wake. Alipompoteza mumewe wa kifani, Abu Salama, ambaye alisumbuka nae kwenye matatizo mengi, katika mji wa Madinah, aliachwa mkiwa na watoto wake. Abu Bakr na Umar walimpendekezea ndoa, wakifahamu fika mahitaji yake na kusumbuka kwake kama ni mjane fukara pamoja na watoto wa kusaidiwa, lakini aliwakataa kwa sababu aliamini kwamba hakuna ambaye angekuwa ni mbora zadi ya mumewe aliyefariki.
Wakati fulani baadaye, Mtume (s.a.w.) alimposa. Hili lilikuwa sahihi na la kimaumbile kwa sababu mwanamke huyu adhimu, ambaye hakuona haya kujitoa muhanga na kusumbuka kwa ajili ya Uisilamu, alikuwa mkiwa baada ya kuishi miaka mingi katika ukoo mtukufu zaidi wa Kiarabu; asingeweza kutelekezwa na kuachwa akiombaomba maishani mwake. Kutokana na uchamungu wake, utii, na alivyotaabika, kwa hakika amestahiki kusaidiwa. Kwa kumwoa yeye, Mkuu wa Ulimwengu (s.a.w.) alimsaidia. Alikuwa akifanya alivyokuwa anafanya, akiwafanya rafiki wale wasio na marafiki na kuwasaidia watoto wasio na baba. Alifanya kile kilichotakiwa na mazingira ya wakati huo.
Umm Salama alikuwa hodari na mwenye kipaji kama Hadhrat Aisha. Alikuwa na aina zote za uwezo wa kuwa mwalimu na mfikishaji wa ujumbe wa Uisilamu. Pale Mtume alipomweka kwenye himaya yake, mwanafunzi mpya ambaye wanawake wote wameshukuru mno alikuwa amekubaliwa kuingia shule ya elimu na uongofu.
Hatuwezi kufafanua ndoa ya Mtume, ambae alikuwa na umri wa karibu miaka 60, kumwoa mjane aliyekuwa na watoto tele na kudai kuwa gharama na majukumu kwa chochote kingine, na kamwe haitokuwa ashiki na kumili kwa wanawake.
4) Mke mwingine wa Mtume alikuwa ni Ramla bint Abi Sufyan (Umm Habiba). Alikuwa ni binti wa Abu Sufyan, mtu aliyewakilisha ukafiri dhidi ya utume kwa kipindi fulani. Alikuwa ni katika Waisilamu wa mwanzo waliokuwa na hadhi ya juu. Alikuwa ni mwanamke aliyehamia Ethiopia, ambapo mumewe baadaye alijiunga na Ukristo; kisha mumewe alifariki na yeye alipitia matatizo mengi.
Maswahaba, katika wakati huo, walikuwa wachache na masikini. Hawakuwa na pesa za kutosha kuwasaidia wengine. Hivyo, alichagua nini Angeweza kuritadi na kuingia katika Ukristo na akasaidiwa kwa njia hiyo au arudi nyumbani kwa baba yake, sasa ni makao makuu ya ukafiri au atangetange nyumba hadi nyumba kuombaomba. Si rahisi kwa mmoja ya mwanamke mwenye dini, mtukufu na tajiri kufanya jambo lolote kati ya hayo. Kulikuwa na jambo moja tu lililobakia: uingiliaji kati na msaada wa Mtume (s.a.w.)
Hivyo ndivyo pia ilivyokuwa katika ndoa ya Umm Habiba (Allah amridhie). Mbele ya Najjash, ndoa ya mwanamke huyu, aliyejitolea muhanga kwa namna zake zote kwa ajili ya dini yake, akaolewa na Mtume, jambo ambalo lilikuwa ni la kimaumbile kwa mwanamke aliye mbali ya nyumbani kwao kati ya watu weusi na aliyepitia misukosuko mingi wakati wa uhai wa mumewe kutokana na Uisilamu kisha kifo cha mumewe. Achilia mbali kukata tamaa, ni muhimu kulipongeza hilo kwa sababu ni kitu ambacho kimetambulika na Mtume kwa sababu imeonekana wazi kuwa ametumwa kuwa ni “ili awe rehema kwa walimwengu”.
Isitoshe, mwanamke huyu adhimu anayo mambo mengi ya kuyaleta kwenye maisha ya malezi kwa Waisilamu, hivyo, Umm Habiba aliungana na nyumba ya Mtume kuwa ni mke na mwanafunzi.
Kupitia ndoa hii, familia ya Abu Sufyan ilipata fursa ya kuingia nyumba ya Mtume, jambo lililowasababishia kubadili mawazo yao na kulainika. Ushawishi wa ndoa hii ulikuwa kwa familia ya karibu ya Abu Sufyan; ilishawishi wana Umayya wote. Hata inaweza kusemwa kuwa familia hii, iliyokuwa hasimu na karibu mno na watu wengine, imelainika shukurani kwa ndoa ya Umm Habiba na alikuwa tayari kutenda aina zote za amali njema.
5) Mmoja ya wanawake waliongia katika nyumba ya Mtume alikuwa ni Zaynab bint Jahsh (Allah amridhie). Alikuwa ni mwanamke wa uzawa tukufu na hisia za ndani kama alivyokuwa ni ndugu wa karibu wa Mtume; alikulia karibu yake. Wakati Mtume alipojitambulisha kwa wazazi wake kwamba anataka kumwoza kwa Zayd (Allah amridhie) familia yake ilisita kidogo kwa sababu familia hii ilitarajia kumwozesha mtoto wao Mtume. Hatimaye, waliridhia ndoa yake kwa Zayd bin Haritha wakati Mtume aliposisitiza.
Zayd alikuwa ni mtumwa aliyepoteza uhuru wake kipindi fulani na akawa ni miongoni mwa watumwa; kisha Mkuu wa Ulimwengu (s.a.w.) akamwokoa kutoka katika utumwa. Mtume (s.a.w.) alitaka kuanzisha usawa na uwiano kati ya watu kwa kukazania ndoa hiyo na kuanza kuitekeleza miongoni mwa jamaa zake. Hata hivyo, Zaynab, aliyekuwa na desturi ya hali ya juu, alionekana kutodumu na ndoa hii kwa muda mrefu, ambayo aliikubali kutokana na msisitizo wa Mtume. Ndoa hii haikuleta furaha kwa Zayd, pia; ilimletea machungu na tamaa tu.
Mwishowe, Zayd alimpa talaka Zaynab; lakini Mtume (s.a.w.) alikuwa akijaribu kumshawishi Zayd na kuifanya ndoa iendelee. Wakati huo huo, alishuka Jibril na kumletea amri ya kiungu ikimwamuru Mtume kumwoa Zaynab. Mtihani ambao Mtume alikuwa akipitia ulikuwa mkubwa; alikuwa anaenda kufanya jambo ambalo halikuwahi kufanywa hapo kabla; alikuwa anakwenda kutangaza vita dhidi ya mila za jadi zilizolowea. Yalikuwa ni mapambano magumu. Linaweza tu kufanyika kwa sababu ilikuwa ni amri ya Allah. Kwa kuufahamu fika utumwa, Mtume alitekeleza kile alichoamrishwa ingawa ilikuwa ni vigumu kwa hadhi ya ukoo wake. Kama Hadhrat Aisha alivyoeleza, “Kama Mtume amejiinamia kuzuia jambo lolote la yale yaliyoletewa ufunuo kwake, basi kwa hakika angeizuia aya hii.” Ndio, ilikuwa ni vigumu mno kwa Mtume (s.a.w.)…
Hekima ya kiungu imemtaka mwanamke huyo wa hadhi ya juu na mwenye kujizuia aingie katika nyumba ya Mtume (s.a.w.), kumlea na kumpa mafunzo, na kumfanya afikishe ujumbe wa Uisilamu. Mwishowe, hili lilifahamika. Alitenda kwa mujibu wa kanuni za kuwa mke wa Mtume zilivyosisitiza.
Isitoshe, katika Enzi za Jahiliyyah, mtoto wa kupanga alikuwa akitambulishwa na kuzingatiwa kuwa ni mtoto wa kumzaa na mke wa mtoto wa kupanga alikuwa akizingatiwa kuwa ni mke wa mtoto wa kumzaa. Mila hii iliyokuwepo katika zama za Jahiliyyah ilipotakiwa kuvunjwa, utekelezaji wa mwanzo ulifanyika kwa Mtume (s.a.w.). “… wala hakuwafanya watoto wenu wa kupanga kuwa ni wana wenu khasa. Hayo ni maneno ya vinywa vyenu tu…” (al-Ahzab, 33/4)
6) Mmoja ya wanawake waliopata heshima ya kuingia nyumba ya Mtume alikuwa ni Juwayriya bint Harith (Allah amridhie). Waisilamu walipigana na kabila lake na kuwateka wanawake na wanaume. Wakati mwanamke huyu, aliyeishi katika kasri la kabila lake, alipoletwa mbele ya Mtume, alikuwa katika hali mbaya na alihisi kufedheheshwa; alijawa na kinyongo na chuki.
Mtume (s.a.w.) alisawazisha tatizo hilo kwa urahisi. Alipomwoa Juwayriya, alipata hadhi ya cheo cha mama wa waumini na kupata heshima kutoka kwa Maswahaba. Na Mtume aliposema, “Jamaa wa Mtume hawawezi kufanywa watumwa” na akawaacha huru, moyo wa Juwayriya na watu wake wote ulifuzu.
Kama inavyoonekanwa, Mtume wetu ametatua tatizo hili kwa urahisi alipokuwa na umri wa karibu miaka sitini kwa kuoa; hivyo, aliweka amani ilhali kila kitu kilikuwepo kuendeleza vita.
7) Mmoja ya wanawake wenye bahati ya kuingia nyumba ya Mtume alikuwa ni Safiyya bint Huyayy (Allah amridhie), binti wa mtawala wa jadi wa Khaybar. Katika vita maarufu vya Khaybar, alimpoteza baba yake, kaka, na mume, na kabila lake likatekwa nyara; Safiya alikuwa anaungulika rohoni kulipa kisasi. Hata hivyo, alipoolewa na Mtume na kunyanyuliwa hadhi ya juu ya kuwa mke wa Mtume, Maswahaba walianza kumheshimu na Mtume alikaa nae kwa wema, jambo lililomfanya Safiyya kusahau yote yaliyotokea. Alianza kuchukua fahari ya kuwa mke wa Mtume.
Isitoshe, Wayahudi wengi walikuwa na fursa ya kumjua Mtume kwa ukaribu zaidi kupitia Safiyya na walibadilisha mwenendo wao dhidi ya Waisilamu. Kuna hekima nyingi katika tendo moja la Allah, ambaye anafanya mambo mengi kupitia kitu kimoja. Ameumba mengi mazuri katika ndoa hii kama alivyofanya katika ndoa nyinginezo.
Halikadhalika, ni vyema kusema kuwa Mtume alifundisha kitu kwa ummah wake katika jambo hilo alikuwa anazifahamu fika fikra za maadui zake. Mwanamke kama Safiyya, mwanamke wa taifa na kabila jengine kabisa, ni muhimu mno kwa ajili ya ufahamu wa mambo ya ndani ya mataifa hayo; hata hivyo, ni muhimu kuwa makini katika hali hiyo ikiwa watajaribu kupekua siri za Waisilamu katika njia hiyo hiyo.
8) Mmoja ya wanawake wenye bahati ya kuingia katika nyumba ya Mtume alikuwa ni Sawda (Allah amridhie). Alikuwa ni katika wa mwanzo kusilimu na alihamia Uhabeshi pamoja na mumewe; Kama ilivyokuwa kwa Umm Habiba, aliachwa mkiwa wakati mumewe alipofariki.
Mtume Muhammad alimwoa na kuurekebisha moyo wake; alimwokoa dhidi ya huzuni, alikuwa ni mwenza wake. Sawda, aliyetaka aolewe na Mtume (s.a.w.), hakutaka kitu chengine chochote duniani.
Mambo hayo yalikuwa ndio matukio na sababu za Mtume kuoa wake wengi. Hakuna hata ashiki iliyohusishwa. Alioa ima ili kuunganisha uhusiano wa karibu zaidi pamoja na mawaziri wake, kama ilivyokuwa alipomwoa binti wa Abu Bakr na Umar, pale alipoona vipaji na uwezo wao au kutokana na sababu nyenginezo tulizozitaja moja baada ya nyengine hapo juu; alijitolea kubeba mzigo mkubwa alipowaoa.
Ukweli kwamba Mtume wetu (s.a.w.) alimwandalia kila mke makazi, chakula, nguo kwa usawa, kwamba alikaa nao kwa uangalifu wa usawa, aliepusha matatizo yaliyoweza kujitokeza kati yao kabla hayajatokea na kwamba alitatua matatizo kwa urahisi, au kama Bernard Shaw alivyoeleza, “kama vile mtu anavyokunywa kahawa”, akionesha kwamba mtu huyu wa kipekee ni mtume.
Tunajua ni vigumu kiasi gani kwa mtu kusimamia mke mmoja na watoto wawili na sisi tunanyenyea mbele ya Mtume, aliyesimamia wanawake wengi aliyowaoa kabla na kwamba aliboresha nyenendo kadhaa ndani ya majumba ya waume waliopita kwa njia iliyopangika vizuri.
Kuna suala lingine la ziada la kulitaja: ni ukweli kwamba idadi ya wakeze ilikuwa ni zaidi ya kiwango halali kwa wanaume wa ummah huu. Yalikuwa ni mazingira maalumu. Ni sheria maalumu ambayo imebeba sababu nyingi na hekima ambazo tunaweza kuzijua au kutozijua. Ufunuo unoweka ukomo wa wake wengine umekuja baada ya yeye kuoa ndoa zote hizi. Kwa hivyo, yeye pia alikatazwa kuoa tena. (al-Ahzab, 33/52)
9) Mke mwengine wa Mtume alikuwa ni Hafsa bint Umar al-Khattab, Hafsa, binti wa Umar, alizaliwa miaka mitano kabla ya Muhammad (s.a.w.) kuwa mtume. Mama yake ni Zaynab, dada wa Uthman b. Maz’un, mmoja ya Maswahaba watukufu.
Haijulikani ni lini Hz Hafsa alisilimu. Inaweza kusemwa kuwa alisilimu baada ya baba yake Umar kusilimu kwa sababu tunajua kuwa familia nzima ya Umar na ndugu zake baadae wamesilimu.
Hazrat Hafsa aliolewa na Khunays b. Huzafa, as-Sahmi. Huzafa alikuwa ni miongoni mwa Waisilamu waliohamia Abyssinia. Kuna masimulizi yanayoeleza kuwa Hafsa pia alishiriki katika kuhama huku. Baada ya kurudi kutoka Abyssinia, Huzafa alihamia Madina pamoja na mkewe Hafsa.
Hadhrat Khunays b. Huzafa alishiriki katika vita vya Uhud na alijeruhiwa vibaya sana. Alikufa shahidi kutokana na majeraha hayo mjini Madina. Hadhrat Hafsa alijaribu kuyatibu mwenyewe majeraha ya mumewe. Alihuzunika sana alipofariki. Hadhrat Umar alimtaka Hadhrat Abu Bakr kumwoa mwanawe, Hafsa. Hata hivyo, Abu Bakr hakulijibu pendekezo la Umar. Kisha, Hadhrat Umar alimpendekeza Uthman, ambaye mkewe ni Ruqayya, mtoto wa Mtume, aliyefariki na baadaye, alikuwa mkiwa. Hata hivyo, Hadhrat Uthman, aliyetarajia kumwoa Umm Kulthum, mtoto mwengine wa Mtume, alisema, “sio busara kwangu kuoa sasa” baada ya kufikiri kwa muda.
Hazrat Umar, aliyejaribu kumwoza binti yake kwa muumini mnyoofu kwa kitendo kilichomfaa baba Mwislamu, akaenda/alienda kwa Mtume akiwa na majonzi pindi aliposhindwa kulitekeleza hilo. Akiwa anazungumza na Mtume, alisema, “Nashangazwa na tabia ya Uthman. Nimempendekeza amwoe Hafsa lakini hakukubali.” Bwana Mtume akasema, “Je naweza kukupendekezea mkwe bora zaidi ya Uthman na naweza Kumpendekezea Uthman baba mkwe bora kuliko wewe?” Umar aliposema, “Ndio, ewe Mjumbe wa Allah!”, Bwana Mtume akasema, “Niozeshe binti yako Hafsa na nitamwoza mwanangu Umm Kulthum kwa Uthman.
Hadhrat Umar alifurahishwa sana aliposikia tunu hiyo. Alitaka sana kuwa ni jamaa wa Mtume lakini hakuwa na ushujaa wa kumpendekezea amwoe Hafsa kwa sababu Hafsa alikuwa, kama alivyoeleza Bibi Aisha, “kama alivyo baba yake”, yaani, alikuwa mkali kidogo. Kwa pendekezo lake, Mjumbe wa Allah (s.a.w.) aliyaimarisha uhusiano wake na Umar na kumzawadia kutokana na kuuhudumia Uisilamu kwa kuwezesha shauku ya Umar kueleweka.
Mjumbe wa Allah (s.a.w.) alimwoa Bibi Hafsa katikati ya mwaka wa tatu wa Hijrah. Alimpa Hafsa dirham 400, yaani, gramu 118, za fedha kuwa ndio mahr (mahari).
Baada ya kufariki Mjumbe wa Allah (s.a.w.), Hafsa aliishi maisha ya staha mno na kidini. Kiasi cha hadithi sitini zimeripotiwa na yeye: baadhi ya hadithi zimetoka moja kwa moja kwake, nyingine alizisikia kutoka kwa baba yake. Hafsa, aliyejua kusoma na kuandika, alifariki mwaka wa arubaini-na-tano wa Hijrah; sala ya jeneza lake ilisalishwa na Marwan, kadhi wa Madinah. Kwa mujibu wa masimulizi mengine, alifariki mwaka wa arubaini-na-moja wa Hijrah.
3
Ni nini Sunnah? Unaweza kufafanua umuhimu wa Sunnah katika Uisilamu?
Sunnah ni kile ambacho Mtume amekifanya, amekisema na matendo yake yote na ishara. Basi, tunaweza kusema kuwa alichokifanya wakati wa uhai wake ni Sunnah.
Neno sunnah limetumiwa katika vitabu vya fiqh likimaanisha “kuna malipo kama tutalifanya lakini sio dhambi kama hatulifanyi.” Mathalani, kula kwa mkono wa kulia, kusafisha meno, kutokula hali ya kuwa umesisima, n.k.
Hata hivyo, tunapolizingatia neno sunnah katika ufahamu wake mpana, linajumuisha kila alilofanya Mtume wetu. Kwa hali hiyo, utashi, na makatazo ya Allah pia yanaingia katika Sunnah. Mathalani, je Mtume wetu amesimamisha sala? Ndio. Basi ni sunnah kusimamisha sala.
Kwa mujibu wa hayo, ni lazima kuzigawa sunnah katika makundi.
Fardh: Ni kila jambo ambalo Allah kwa hakika anatutaka tutekeleze au tuepuke. Ni Mtume wetu ambaye anaefikisha maamrisho na makatazo ya Allah kwa njia iliyo bora zaidi na ambaye anakuwa ndio kigezo. Tunapaswa kumfuata yeye ili kutekeleza kikamilifu maamrisho na makatazo ya Allah. Kama vile kusimamisha sala, kufunga swaumu, kuepuka uasherati na kutokula kitu chochote cha haram (kilichokatazwa).
Wajibu: Mambo ya wajibu katika dini yetu: kwa mfano, ni wajibu kusimamisha sala ya witr kuwa ni rakaa tatu.
Nafilah: Yale mambo mengine yasiyokuwa faradhi na wajibu ambayo yanatekelezwa kikamilifu wakati wa kusimamisha sala. Mathalani, kusoma baadhi ya aya kutoka katika Quran wakati wa kusali ni faradhi lakini kusoma dua ya subhanaka ni nafilah.
Adab: Ikiwa tutafanya harakati zetu za kila siku kama alivyofanya Mtume kama vile kula, kulala, kuingia msikitini au chooni, n.k. tutafanya kwa mujibu wa taratibu zake. Mtu asiyefanya kwa mujibu wa taratibu hizo hazingatiwi kuwa ametenda dhambi.
Hii inamaanisha tunaweza kuigawa sunnah kuwa ni faradhi, wajibu, nafilah na adab. Ni mpangilio wa ubora wa sehemu za sunnah.
Tunaweza kuifikiria kama mwili wa binadamu. Mtu ana viungo vya lazima ili aishi: mathalani, ubongo, moyo, kichwa, n.k. Kanuni ambazo ni lazima tuziamini ni kama vile moyo na ubongo kwa roho yetu.
Viwiliwili vyetu vina viungo vya hisia kama vile macho, masikio, mikono, miguu, n.k. Faradhi ni kama viungo hivyo. Faradhi ni macho, masikio, mikono na miguu kwa roho yetu. Mtu asiyetekeleza faradhi ni kama mtu asiye na mikono, miguu, macho na masikio.
Pia tuna mazuri na mapambo mengine kama vidole, nyusi na nywele katika miili yetu. Tunaweza kuishi bila ya hivyo. Hata hivyo, tukiwa navyo, tutakuwa kamilifu. Vivyo hivyo, sehemu za nafilah na adab za sunnah ni mapambo na urembo wa roho zetu. Kama tutayatekeleza, tutapata malipo mengi; kama hatuyatekelezi, hatutopata madhambi.
Kwa kuongezea, mambo ya faradhi na wajibu ni sunnah ambazo ni lazima kutekelezwa. Tutapata thawabu nyingi kama tutatekeleza nafilah na adab.
Kama ilivyo kwa haramu, lazima tuzihifadhi nafsi zetu kutokana na kuua na kutia sumu haramu kama tunavyoihifadhi miili yetu kutokana na sababu zenye kuua kama ukimwi, sumu na moto.
Umuhimu wa Sunnah
Sahihi Muslim inaeleza kwa kifupi umuhimu wa Sunnah kama ifuatavyo:
Chochote au vyovyote Mtume wa Mungu (amani imtue) alivyofanya au kusema kuhusu jambo lolote, anafanya hivyo kama ni mtume. Kila alichokifanya huwa amelifanya bila ya mkengeuko au kasoro. Maneno yake yote na matendo yamewekewa mipaka ya mpango wa Mungu. Kwa hivyo, kila mmoja analazimika kufuata na kuiga kila hatua ya maisha yake. Maisha yake ni Quran hai, na majumlisho ya Sheria za Kiungu.
Zipo aya nyingi na hadithi nyingi katika Quran na vitabu vya hadithi, ambazo kwa usahihi kabisa zinaeleza kuwa kushikamana na Sunnah ndio msingi mkuu wa dini.
Baadhi yake ni kama ifuatavyo:
Enyi mlio amini! Mt’iini Mwenyezi Mungu, na mt’iini Mtume na wenye madaraka katika nyinyi. Na mkizozana katika jambo basi lirudisheni kwa Mwenyezi Mungu na Mtume, ikiwa mnamuamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho. Hayo ndiyo bora zaidi na ndiyo yenye mwisho mwema. (an-Nisa, 4:59)
Wanazuoni wa tafsir ya Quran wamefasiri amri, “lirudisheni kwa Mwenyezi Mugu na Mtume” kuwa ni “ishaurini Quran na Sunnah”.
Badiuzzaman Said Nursi anafasiri aya hiyo, Waambie (wao, ewe Mjumbe):
“Sema: Ikiwa nyinyi mnampenda Mwenyezi Mungu basi nifuateni mimi, Mwenyezi Mungu atakupendeni na atakufutieni madhambi yenu. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kufuta madhambi na Mwenye kurehemu. (Aal-i Imran, 3:31) kuwa ni, kama mnamwamini Mungu (Mtukufu Aliyetakasika), kwa hakika mtampenda Yeye. Kwa kuwa mnampenda Mungu, mtatenda kwa namna anayoipenda Yeye. Ili kufanya hivyo, lazima mfanane na wale anaowapenda Mungu. Na anaweza kufananishwa kwa kumfuata yeye. Kila mnapomfuata, Mungu hukupendeni, pia. Isitoshe, mnalazimika kumpenda Mungu kwa ajili hiyo Atakupendeni.
Ibara hizi zinaunda ufupisho tu na maana ya aya kwa maneno machache. Inamaanisha kuwa lengo adhimu zaidi kwa binadamu ni kuyapokea mapenzi ya Mungu Mtukufu. Aya hiyo inaonesha kuwa njia ya kufanikiwa lengo adhimu ni kumfuata Mpenzi wa Mungu na Matendo yake. (Nuru, nuru ya 11)
Al Maududi anahutubia maelezo ya hapo chini kuhusu kujisalimisha kwenye Sunnah:
Kuziacha Sunnah za Mtume Muhammad hata kwa kiasi kidogo kunakupelekea kukosa mapenzi ya dhati kutoka kwa Mungu na mjumbe Wake. Hali ya kwanza ya upendo ni kujisalimisha kikamilifu. Mtu anayempenda Mjumbe wa Mungu, Mtume Muhammad (s.a.w.), anapaswa ajisalimishe kwake na anapaswa atiii maamrisho yake.
Katika muunganiko huu, napendelea kueleza baadhi ya sehemu zinazohusiana na kushikamana na Sunnah kutoka katika Mkusanyiko wa Risale-i Nur.
Vyanzo vya Matendo Adhimu ya Mtume Mtukufu ni vitatu: maneno yake, matendo yake, na ruhusa yake. Na vipo vifungu vitatu kwa kila moja ya vyanzo hivi vitatu: wajibu, kujitolea, na kusifika.
Ni sharti kuyafuata yote ya wajibu na ya lazima, na kuna adhabu kwa kuyaacha. Kila mmoja ana jukumu la kuyafuata. Kama ilivyo utaratibu wa kujitolea, na wa kusifika, waumini kwa mara nyengine tena wana jukumu la kuyafuata, lakini hakuna adhabu ikiwa yataachwa. Hata hivyo, kuna faida kubwa kuyatenda kwa mujibu wake na kuyafuata. Na kuyabadilisha ni uzushi, kutoongoka, na kosa kubwa. Kufuata na kuyaiga matendo ya desturi ya Mtume ni kusifiwa vilivyo na kwa mujibu wa hekima, na kuna manufaa kwa maisha ya mtu na jamii na kwa utu. Kwa hivyo katika matendo yote ya mwenendo wake kuna mambo mengi yenye manufaa kwa maisha, na halikadhalika, kwa kuyafuata hayo, ruhusa hiyo na matendo hayo kunakuwa ni kama ibada.
Ndio, kwa kuwa rafiki na adui wanakubaliana, haiba ya Muhammad (S.A.W.) inadhihirisha viwango vya juu vya maadili ya wema; na kwa kuwa wote wamekubaliana, yeye ndiye mtu mashuhuri zaidi na mbora zaidi katika watu; na kwa kuwa kama ilivyoorodheshwa na maelfu ya miujiza yake, na kuthibitishwa na Dunia ya Kiisilamu ambayo ameiasisi na mafanikio yake, na kutiliwa mkazo na ukweli wa Quran ya kuwa alikuwa ni mbashiri na mfasiri, alikuwa ni mtu bora zaidi na Sahihi na mwongozo bora zaidi; na kwa kuwa kama lilivyo tunda la kumfuata yeye, mamilioni ya watu wa usahihi wameboreka kupitia daraja za kuifikia furaha ya dunia zote mbili; kwa hakika Matendo yake ni mifano murua ya kufuatwa, na mwongozo salama zaidi, na sheria nzuri mno kuwekwa kuwa ni kanuni. Wenye furaha ni wale ambao ushiriki wao wa kuyafuata Matendo ya Mtume (S.A.W.) ni mkubwa. Ilhali wale wavivu na wasiyoyafuata hupata hasara kubwa, na wale wanaoyazingatia kuwa hayana umuhimu wanatenda uhalifu mkubwa, ilhali kama wanayakosoa, ambako kunaashiria kuyakanusha, ni kupotoka kikweli kweli. (kifungu cha maneno kutoka kitabuni)
Ewe Rafiki! Nilipokuwa natenda njia yangu kwa wasiwasi na kujawa na dukuduku, nimeshuhudia Sunnah ya Mtume Muhammad ikitoa msaada kama nyota na taa. Kila sunnah au sharia inang’aa kama jua linavyoangaza kwenye njia za uasi wa dhuluma dhini ya mtindo wa Mungu. Kama mtu, hata kama, ameacha walau punje na kujiweka mbali na njia hiyo iliyonyooka (njia ya Mungu) ya sunnah; anakuwa ni mwanasesere wa Shetani, hatua ambayo hofu na amali mbovu hutokea, na mzigo hujazwa kama mlima. (Mesnevi-i Nuriye)
Matendo ya Mtume (S.A.W.) ni adabu. Hakuna doa kati ya hayo ambayo chini yake kuna mwangaza, na adabu, sio ya kupekuliwa. Mtume Mtukufu (rehema na amani zimshukie) amesema:
Wale wanaomtii Mungu na mjumbe Wake watafuatana na mitume, waliojitolea, mashahidi, na wale ambao Mungu amewatunuku fadhila na tunu Zake. Ni marafiki wema walioje hao!
Mtu yeyote anayemtii mjumbe Wake, huwa anamtii Mungu.
Addabani Rabbi fa ahsana tadibi, maana yake ni: “Mola Wangu Mlezi amenifundisha tabia njema, na mafunzo yake ni mazuri mno.” Ndio, yeyote atakayeisoma tawsifu ya Mtume na kujua Matendo yake kwa hakika atafahamu kuwa Mungu Mtukufu amekusanya adabu mbalimbali kwa Kipenzi Chake na tabia njema. Yeyote atakayeacha matendo hayo basi ameacha adabu. Anathibitisha sheria, “Mtu mwenye maadili-mabaya amekosa baraka za Kiungu,” na kukosa adabu kwa namna ambayo humsababishia hasara.
Hadithi zinazothibitisha muungano usiovunjika kati ya Quran na hadithi:
Abu Dawud anasimulia kutoka kwa Irbad b. Sariya. Siku moja Mjumbe wa Allah alisalisha na kisha akatugeukia: akatoa hutuba fasaha mno kiasi kwamba nyoyo zinatetemeka na macho yanabubujikwa na machozi. Mmoja ya wasikilizaji alisema, “Ewe Mjumbe wa allah! Inaonekana kama ni hotuba ya kutuaga; sasa ni maamrisho gani unatupa?” Mjumbe wa Allah akasema, “nakuusieni kumcha Allah, na kusikiliza na kutii hata kama atakuwa ni mtumwa; kwa kuwa, wale watakaoishi baada yangu watashuhudia mfarakano mkubwa. Ni lazima mfuate sunnah zangu na za makhalifa waongofu. Zishikeni na lazimikianeni nazo. Jiepusheni na mambo ya kuzuazua, kwa sababu ni uzushi, na kila uzushi ni upotovu. Utakupelekeeni mtoni.”
Muslim anasimulia kutoka kwa Jabir (r.a.):
Wakati Mjumbe wa Allah anatoa hotuba, macho yake yalipiga wekundu, sauti yake ilikuwa kali na hasira zake ziliongezeka kwa hivyo alikuwa ni kama mtu anaetoa onyo dhidi ya adui na kusema, “adui amekushambulieni asubuhi na jioni pia.” Akasema pia, “Saa ya mwisho na nimeletwa kama hivi viwili” na akaunganisha kidole chake cha shahada na cha kati, na akaendelea kusema: “maneno mazuri zaidi ni yale yanayotoka kwenye kitabu cha Allah, na mwongozo bora zaidi ni ule uliotolewa na Muhammad. Na mambo maovu zaidi ni yale yaliyozushwa; na kila uzushi ni upotovu.”
Bukhari na Muslim wanasimulia kutoka kwa Anas (r.a.):
Mjumbe wa Allah (s.a.w.) alisema, “Hakuna yeyote miongoni mwenu atakayezingatiwa kuwa ni muumini isipokuwa anipende mimi zaidi ya nafsi yake, baba yake, watoto wake na kila mtu.”
Mtume amesema, “Rehema za Allah ziwashukie wasaidizi wangu.” Alipoulizwa, “ni nani hao wasaidizi wako?”, akasema, “Wale wanaotekeleza Sunnah zangu na kuzifundisha kwa wengine.”
Mjumbe wa Allah anahutubia ufahari na utukufu wa Sunnah na umuhimu wa kumfuata yeye kwa muhtasari kama ifuatavyo: “Kama Musa Ibn Imran angeishi katika zama zangu, asingefanya chochote zaidi ya kunifuata mimi.”
Yaani, hakuna njia nyengine isipokuwa ni kumfuata Bwana Muhammad, ambae ni mtu sahihi kabisa, hata kwa Musa, ambae ni mtume aliyepewa kitabu; ni wema ulioje na bahati kwa mtu wa kawaida na ummah wenye dhambi kama sisi kufuata Sunnah za Mtume mkarimu.
“Kama mtaacha sunnah za Mtume wenu, mtapotea.”
“Kama mtu atafuata matamanio yake binafsi badala ya yale niliyoyaleta, hatozingatiwa kuwa ni muumini wa kweli.”
“Allah na mimi tunawalaani wale wanaoacha Sunnah zangu.”
“Mtu anaezikengeuka Sunnah zangu hazingatiwi kuwa anaifuata njia yangu.”
“Amali ya mtu ambayo haiendani na njia yangu basi hukataliwa.”
Hizo ni baadhi aya na hadithi zinazohusiana na suala hili. Kuna aya na hadithi nyingi katika Qurani na vitabu vya hadithi zinazoeleza kwa uwazi kuwa kushikamana na Sunnah ni kanuni ya lazima kwa dini. Kisha, madai ya kuwa “wacha tutende kwa mujibu wa Quran tu” yako mbali ya umakini. Waisilamu wanyoofu hawayatilii maanani madai kama hayo.
4
Hadithi ni nini? Je utafafanua tofauti kati ya aya (ayah) na hadithi?
Aya maana yake ni sentensi ambayo mwanzo wake na mwisho uko wazi katika Quran. Kila aya ya Quran ni muujiza. Kila aya ni ushahidi kwa ajili ya uaminifu wa mtume aliyefikisha aya hiyo na somo la kupigiwa mfano kwa ajili ya wenye kufikiri, kutafakari na kuzingatia; kila aya ni ‘kitu cha ajabu’ kwa sababu ni muujiza na ina thamani.
Hadithi ni maneno, amali, idhinisho na sunnah za Mtume zinazojumuisha maadili yake na ubora wa kiutu ulioelezwa kwa maneno au maandishi. Kwa namna hii, hadithi ni kisawe cha sunnah.
Neno hadithi limeanza kutumiwa kuwa ni jina la jumla kwa ajili ya habari zilizoripotiwa kutoka kwa Mtume kwa mujibu wa muda.
Mjumbe wa Allah (s.a.w.) sio tu aliwapelekea watu ufunuo alioupokea kutoka kwa Allah bali pia aliwafafanulia ufunuo huo na kuutekeleza katika maisha yake yeye mwenyewe, kuwa ni mfano madhubuti kwao. Kwa hivyo, pia alikuwa akiitwa Quran hai.
Wanazuoni wa Kiisilamu kwa ujumla wanazizingatia hadithi zinazohusiana na masuala ya kidini kuwa zimefunuliwa na Allah kwa mtume na kuonesha aya ifuatayo kuwa ni ushahidi wa hilo:
“Wala hatamki kwa matamanio. Hayakuwa haya ila ni ufunuo ulio funuliwa; “(an-Najm, 53/3-4).
Kwa kuongezea, wanasema neno hikmah (hekima) lililotajwa katika aya ifuatayo linamaanisha sunnah:
“Hakika Mwenyezi Mungu amewafanyia wema mkubwa Waumini vile alivyo waletea Mtume aliye miongoni mwao wenyewe, anaye wasomea Aya zake, na anawatakasa, na anawafunza Kitabu na hikima, ijapo kuwa kabla ya hapo walikuwa katika upotovu ulio wazi.” (Aal-i lmran, 3/164)
Kwa hakika, baadhi ya masimulizi yaliyoripotiwa kutoka kwa Mtume na Maswahaba zake yameutanguliza ukweli huu. Yafuatayo yanaripotiwa kutoka kwa Mjumbe wa Allah:
“Nimepewa Kitabu kitukufu na mfano wake (sunnah)” (Abu Dawud, Sunan, II, 505).
Hassan Ibn Atiyya amefafanua yafuatayo kuhusiana na suala hili: “Jibril (Jibrilu) ameleta na kufundisha sunnah kwa Mjumbe wa Allah kama vile alivyoileta na kuifundisha Quran.” (Ibn Abdilbarr, Jamiu'l Bayani'l-ilm, II, 191).
Kama inavyofahamika kutoka kwenye aya na taarifa za hapo juu, Quran na hadithi (au sunnah kwa ufahamu mpana zaidi) ni sawasawa kwa upande wa kuwa ni ufunuo ulioteremshwa kwa Mjumbe wa Allah (s.a.w.) na Allah. Hata hivyo, Quran inatofautiana na hadithi kwa sababu ni jambo lisilowezekana kutoa kitu kama Quran kwa upande wa maana na maneno, inathibitishwa kwa maandishi katika ubao uliohifadhiwa (Lawh al-MafuzMahfudh), na sio Jibril wala Mtume (s.a.w.) anayeweza kubadilisha kitu ndani yake. Hadithi hazikuwa ufunuo kama maneno; na sio miujiza kama maneno ya Quran; inaruhusiwa kuiripoti kwa maana yake tu maadamu maana haibadiliki.
Kama ilivyo fiqh ni chanzo kinachotegemea ufunuo, hali ya hadithi kwa kulinganisha na Quran na kwa upande wa hukumu inayoileta ni kama ifuatavyo:
1. Baadhi ya hadithi zinathibitisha na kusisitiza hukumu ambazo Quran imezileta; kwa mfano, hadithi zinazokataza kuwaasi wazazi wawili, kubeba ushahidi wa uongo na kufanya mauaji.
2. Baadhi ya hadithi zinafafanua na kuzijalizia hukumu ambazo zimeletwa na Quran. Kusimamisha sala, kutekeleza hajj na kutoa zakah yote yameamrishwa katika Quran lakini haikuelezewa namna ya kutekelezwa. Tunajifunza namna gani ya kuyatimiza hayo kutoka katika hadithi.
3. Baadhi ya hadithi zimetoa hukumu kuhusu masuala ambayo Quran haikuyataja kabisa. Hadithi zilizokataza kula nyama ya punda na ndege wanaowinda na hadithi zinazothibitisha hukumu mbalimbali kuhusu diyah, n.k. ni mifano ya hadithi inayoonesha kuwa hadithi zinaweza kuwa ni chanzo cha sheria za kutegemewa.
Tulichokieleza hadi sasa kinaonesha nafasi ya hadithi (sunnah) katika dini ya Uisilamu. Ukweli kuwa ni lazima kuzipa umuhimu hadithi kama ni chanzo kinachokuja mara tu baada ya Quran kutoka katika nukta ya mtazamo wa dini ya Uisilamu na kutenda kwa mujibu wa sunnah za Mtume kumeamrishwa kwa hotuba za dhahiri na wote wawili Allah na mjumbe Wake Bwana Muhammad (s.a.w.). Aya zifuatazo zinazohusiana na suala hilo zimo ndani ya Quran.
“Sema: Ikiwa nyinyi mnampenda Mwenyezi Mungu basi nifuateni mimi, Mwenyezi Mungu atakupendeni na atakufutieni madhambi yenu.” (Aal-i Imran, 3/31);
“Sema: Mt’iini Mwenyezi Mungu na Mtume. Na wakigeuka basi Mwenyezi Mungu hawapendi makafiri.” (Aal-i Imran, 3/32);
“Na mt’iini Mwenyezi Mungu na Mtume ili mpate kurehemewa. (Aal-i Imran, 3/132);
“Na anacho kupeni Mtume chukueni, na anacho kukatazeni jiepusheni nacho. (al-Hashr, 59/7).
Kama inavyoonekana, katika aya kama hizo hapo juu, kumtii Mjumbe wa Allah (s.a.w.) kumeamrishwa pamoja na kumtii Allah; hata pia imeelezwa wazi kuwa kumtii Mtume (s.a.w.) kunamaanisha ni kumtii Allah.
Katika hadithi fulani, Mjumbe wa Allah (s.a.w.) amesema, “Jueni ya kwamba nimepewa Quran na mfano wake (sunnah). Utafika wakati mtu ameshiba juu ya kochi lake atasema: Ihifadhini Quran; mkikuta jambo la halali ndani yake lihalalisheni, na mkikuta linalokatazwa likatazeni. Bila ya shaka yoyote, lile ambalo Mjumbe wa Allah ameliharamisha ni kama vile Allah ameliharamisha.” (Abu Daawd Sunnah, 5; Ibn Majah, Muqaddima, 2; Ahmad b. Hanbal, Musnad, IV,131), akiwaonya Waisilamu dhidi ya wale wote wanaodharau sunnah na wanaotaka kuitenganisha kutokana na dini na kutilia mkazo kuwa dini haiwezi kuzingatiwa bila ya sunnah.
5
Aisha (R.A) alikuwa na umri gani alipoolewa na Mtume Muhammad (S.A.W.)?
Baada ya kuwa mtume, miaka kumi baadaye, akiwa na miaka 50, Mtume Muhammad (S.A.W.) alihitaji wake ili wamsaidie kufanya kazi za nyumbani, kutunza watoto wake, na kumsaidia kuwalingania watu kuingia katika Uisilamu. Alitaka kuwaoa wote wawili Sawda, aliyekuwa mkongwe na mjane, na binti wa Abu Bakr, Aisha.
Mtume Muhammad (S.A.W.) alitoa ombi hili miaka kumi baada ya kuanza kwa Ufunuo. Aisha alizaliwa miaka 5-6 kabla ya kuanza kwa ufunuo. Hivyo, inaonekana kuwa umri wa Aisha ulikuwa 17-18 alipoolewa na Mtume Muhammad (S.A.W.).
Nukta hii inahitimishwa kwa undani zaidi katika kitabu “Asr-ı Saadet (Zama za Bishara Njema)” cha Mawlana Shibli. (Ist. 1928. 2/ 997)
Tunaweza kuhitimisha waziwazi kutokana na tawasifu ya Asma, dada mkubwa wa Aisha, kwamba Aisha alishafikisha umri wa kuolewa wakati alipoolewa na Mtume Muhammad (S.A.W.). Vitabu vya kale vya tawasifu vinaandika kuhusu Asma kama ifuatavyo: “Asma alipofikisha umri wa miaka 100, alifariki mwaka wa sabini na tatu baada ya Kuhama (Hijrah). Wakati wa Kuhama, alikuwa na miaka 27 kwa uhakika. Kwa kuwa Aisha alikuwa mdogo kwa miaka 10 kuliko dada yake, alitaka afikishe miaka 17. Isitoshe, aliposwa na Jubair kabla ya kuolewa na Mtume Muhammad (S.A.W.). Hivyo alikuwa mwari wa umri wa kuweza kuoleka.” (Hatemu’l Enbiya (Mwisho wa Mitume) Mtume Muhammad na maisha Yake, Ali Himmet Berki, Osman Keskioğlu, uk. 210)
6
Unaweza kutoa maelezo kuhusu wakeze Mtume na mfumo wake wa wake wengi?
WAKE WA MTUME
1. Khadijah:
Maisha ya ndoa ya Mtume yanaanzia na mama yetu mtukufu Khadijah. Alipomwoa, Mtume alikuwa na umri wa miaka 25 na yeye alikuwa na miaka 40. Hivyo, tofauti ya miaka kati yao ilikuwa ni miaka 15. Alikuwa ni tofauti kidogo ikilinganishwa na wake wengine wa Mtume. Bibi Khadijah aliyekuwepo kwa ajili yake Mtume pindi akieneza ujumbe; alijumuika nae wakati watu walipomtenga na kumbeza. Tena, wakati Mtume alipopokea ufunuo wa mwanzo, uliomfanya atetemeke na kuwa na hofu, Bibi Khadijah, bila ya kusita, alisema maneno yafuatayo laini na ya kumtuliza:
“Habari njema kwako! Naapa kwa Allah kuwa Allah hatokuaibisha, kwa sababu unawatunza jamaa zako, unasema kweli, unawabeba wale wasioweza kujimudu wao wenyewe, unawaalika wageni wako kwa namna bora kabisa na unasaidia watu kwenye matukio yanayojiri katika njia ya Allah.”
Mwanamke huyu wa thamani pia ni mmoja ya Waisilamu wa mwanzo. Alifariki mnamo mwaka wa kumi wa utume, miaka mitatu kabla ya Kuhama (Hijrah). Mjumbe wa Allah alihuzunika sana kutokana na kifo cha mtukufu Khadijah. Mwaka huo uliitwa mwaka wa huzuni kwa sababu matukio ya kusikitisha yalitokea moja baada ya jengine katika mwaka huo, kama vile kifo cha Abu Talib, ambae ni mjomba wake Mtume na mtetezi wake dhidi ya washirikina, na Khadijah, ambae kwake alipata amani.
Ndoa ya Mjumbe wa Allah na Khadijah ilidumu kwa miaka 25 na watoto wake wote isipokuwa Ibrahim walizaliwa kutoka kwa bibi huyu wa thamani. Alipokufa, Mtume alikuwa na umri wa miaka 50. Hayo ni kusema kuwa, Mtume alitumia muda wake mwingi zaidi wa ndoa na pia ujana wake na miaka ya ukomavu na bibi huyu tu ambae alikuwa kamzidi kwa miaka 15.
2. Sawda bint Zam’a:
Mkewe huyu pia ni mmoja ya Wasilamu wa mwanzo. Mumewe wa mwanzo alifariki baada ya kuhamia Ethiopia na akaachwa mkiwa. Mtume alitibu majeraha ya moyo uliovunjika wa mwanamke huyu, alimwokoa kutokana na masikitiko kwa kumwoa na kuwa mwenza/mwandani wake. Baada ya yote, mwanamke huyu adhimu hakutaka chochote katika maisha ya kidunia isipokuwa kuwa ni mke wa Mtume; na alipoolewa na Mtume, alikuwa na miaka 55. Kama inavyoweza kufahamika kutokana na hili, lengo kuu la ndoa hii ni kumsaidia mwanamke aliyeachwa mkiwa na kumpa makazi salama.
3. Aisha:
Ni mwanamke wa kwanza na ndiye pekee bikira aliyeolewa na Mtume. Alikuwa ni binti wa pekee wa Hazrat Abu Bakr, ambaye alikuwa khalifa baadaye. Aidha, alikuwa ni mwanamke wa umahiri adimu na maumbile yanayoweza kumchota Mtume na kumshawishi kwa njia ya aina yake. Maisha yake baada ya ndoa na huduma zake za baadae yalithibitisha kuwa yeye, mwenye maumbile adhimu, asingekuwa mke wa yeyote isipokuwa mke wa Mtume. Kwa hakika, alijithibitisha mwenyewe kuwa ni msimulizi mzuri zaidi wa hadithi, mtolea maelezo Quran aliye sahihi zaidi na mwanachuoni wa hali ya juu wa sheria ya Kiisilamu, na alijaribu kumwakilisha Mtume kwa namna zote.
Ndoa yake na mtukufu Aisha ilikuwa ni zawadi adhimu kwa rafiki-yake-wa-pangoni Abu Bakr, ambae daima alikuwa pamoja naye na alivumilia matatizo yake pamoja naye.
4. Hafsa bint Umar:
Hafsa alikuwa mjane. Mumewe alikuwa ni mpiganaji ambaye alikufa shahidi katika vita vya Badr. Alikasirishwa na kifo cha mumewe na akaachwa mkiwa. Baba yake Hazrat Umar mwanzoni alimpendekeza Hazrat Uthman kumwoa binti yake lakini alikataa. Kisha, alimpendekeza Hadhrat Abu Bakr hivyo hivyo, lakini alikataa pia. Kwa kushuhudia hili, Mjumbe wa Allah alisema kuwa anataka kumwoa bila ya kusita hata kidogo na akamwoa. Ndoa hii pia ilitokana na wajibu na kwa ndoa hii, mtu adhimu, Hadhrat Umar alifurahishwa na ukiwa wa mwanamke, aliyesononeshwa na kifo cha mumewe na aliyeachwa mkiwa ulimalizika.
5. Zaiban bint Huzaima:
Mjumbe wa Allah (s.a.w.) alimwoa mwanamke huyu baada ya Hafsa. Mumewe wa kwanza alikuwa ni Ubaidah bin Harith ambaye alikufa shahidi katika vita vya Badr. Bibi huyu, aliyeachwa mkiwa alikuwa na umri wa miaka 60. alikuwa hohehahe akihitaji msaada katika wakati huu wa ukiwa. Mtume wa rehema na upendo aliyelielewa hitaji lake hilo alitaka kumchukua awe chini ya matunzo yake kwa kumwoa. Isitoshe, alifariki miaka miwili baada ya kuoana.
Kwa hakika, haiwezekani kwa ndoa ya mwanamke mwenye miaka-sitini kuwa na ashiki. Lengo kuu la ndoa hii lilikuwa ni kumsaidia mtu aliyeachwa mkiwa.
6. Umm Salama:
Pia alikuwa ni mmoja ya Waisilamu wa mwanzo na mmoja ya wale waliohamia Ethiopia. Baadaye, alihamia Madinah. Mumewe mpenzi, aliyefuatana nae katika taabu za safari za kuhama na ambaye hakumwacha mkono, alikufa shahidi katika vita vya Uhud. Awali, Hazrat Abu Bakr na Umar walinyoosha mkono wao wa huruma kwa mwanamke huyu, ambaye angebidi ayamudu maisha yake yeye mwenyewe na watoto wake mayatima, lakini alikataa mapendekezo yao.
Baadaye, Mjumbe wa Allah alimposa na akakubali. Hivyo, watoto wake mayatima wapate makazi yenye shamrashamra, wangeishinda huzuni ya kifo cha baba yao kwa msaada wa Mjumbe wa Allah na wangekuwa na baba ambaye asingewafanya wamtamani baba yao halisi.
Umm Salama alikuwa ni mwanamke wa uhodari wa juu na busara, pia, kama Bibi Aisha. Alikuwa na kipaji cha kuwa mnasihi na mfikishaji wa ujumbe. Kwa ndoa hii, mkono wa huruma umemchukua chini ya matunzo yake, na mwanafunzi mwengine ambaye hususani wanawake watashukuru vilivyo amekubaliwa kwenye shule ya elimu na uwongofu wa kiroho.
Kinyume na hivyo, hatuwezi kufafanua kwa namna nyengine kwa nini Mjumbe wa Allah, aliyekuwa na ya aliyefikisha takibani umri wa miaka sitini, alichukua majukumu mengi kwa kuoa mjane mwenye watoto tele.
7. Umm Habiba (Ramla bint Abu Sufyan):
Alikuwa ni binti wa Abu Sufyan aliyewaongoza makafiri mjini Makkah. Mola wetu Mlezi, ambaye ni muweza wa kuhuisha mfu na kumfisha aliye hai, alimtunuku imani, katika miaka ya mwanzo ya Uisilamu, mwanamke huyu, aliyeandikiwa na Allah kupanda hadhi ya kuwa mama wa waumini hapo baadaye.
Alilazimika kuhamia Ethiopia na mumewe kwa sababu hakuweza kuiacha imani yake chini ya mazingira magumu ya Makkah. Hata hivyo, mumewe alijiunga na Ukristo kwenye safari hii na kisha alifariki. Hivyo, Umm Habiba aliachwa mkiwa. Wakati Mjumbe wa Allah alipoyasikia haya, alituma ujumbe kwa Najjash akisema kuwa anataka kumwoa bibi huyu, aliyeachwa mkiwa. Umm Habiba alifurahi sana kusikia hivi na akaolewa na Mtume chini ya uwepo wa mbele ya Najjash.
Kama Mtume asingefanya hivyo, mwanamke huyu mkiwa na asiye na msaada ima angelazimika kurudi Makkah na kuiacha imani yake chini ya mateso makali ya baba yake na familia au kuombaomba msaada wa Wakristo au kuwa ombaomba ili aweze kuishi. Hata hivyo, ndoa hii ilikuwa ndio chaguo bora zaidi.
Kwa sababu ya ndoa hii, Abu Sufyan, aliyekuwa adui mkubwa wa Waisilamu na Mtume pia, alipunguza mateso yake kwa waumini; na kinyongo chake kwa Mtume kidogo kilipata nafuu. Aidha, uhusiano ulijengwa pamoja na wana Umayya, jambo ambalo lilisaidia kuwa ni chachu ya kuwafanya Wasilimu. Baada ya hayo, Abu Sufyan akapata fursa ya kuitembelea nyumba ya Mtume kwa urahisi na hivyo akauelewa Uisilamu vyema zaidi na mwishowe, akawa muumini.
Kama inavyoonekana bayana, lengo la ndoa hii lilikuwa ni kumsaidia mwanamke mkiwa, kupunguza mateso yaliyosumbua Waisilamu kupitia kwake na kumfanya adui mkubwa awe na imani kwa kujenga mahusiaono naye.
8. Juwairiyyah bint Haridh:
Waisilamu walishinda vita vya Muraysi na kupata ngawira nyingi, pamoja na mateka 700. Juwairiyyah, binti wa kiongozi wa kabila la Bani Mustaliq, alikuwa ni miongoni mwa mateka, pia. Juwairiyyah mwanzo aliolewa na Musafi bin Safwan. Kisha, Musafi alifariki katika vita vya Muraysi. Juwairiyyah alikwenda kwa Mtume na kumwomba amwache huru. Mjumbe wa Allah yeye mwenyewe alilipa kikombozi na kumwacha huru. Mama yake alipokuja kumchukua ili amrejeshe, alipendelea kuwa Mwisilamu na kubakia Madinah na baadaye, aliolewa na Mjumbe wa Allah.
Baada ya ndoa hii ya Mjumbe wa Allah, mateka waliomilikiwa na kabila la Abdulmuttalib wakaachiwa huru, na kisha Waisilamu wengine, kwa kuliona hili, mateka wengine wote waliachiwa huru wakidhania kwamba watu wa kabila la jamaa zake Mjumbe wa Allah hawawezi kushikiliwa watumwa.
Ndoa hii ya Mtume pia imefanyika akiwa na miaka sitini na ushee. Alikuwa na lengo la kujenga mahusiano na kabila muhimu; alikuwa na mateka wengi aliowaacha huru, na la muhimu zaidi, ni kuwasababisha Wayahudi wengi kusilimu na kumnyanyua hadhi mwanamke ambaye mumewe aliuliwa katika vita dhidi ya Waisilamu na hivyo alijawa na chuki dhidi ya Waisilamu, kwa cheo cha mama wa waumini kwa kumchukua yeye chini ya mbawa zake za huruma.
9. Safiyya bint Huyayy:
Jina lake halisi lilikuwa ni Zainab. Nyakati hizo, ngawira kwa ajili ya machifu na viongozi wa Kiarabu ilikuwa ikiitwa safiyya. Kwa kuwa bibi huyu alikuwa ni ngawira kwa Mjumbe wa Allah, aliitwa Safiyya. Wazazi wake walikuwa ni watu muhimu Wayahudi. Baba yake alikuwa ni kiongozi wa Wana wa Nadir na mama yake alikuwa ni binti wa kiongozi wa Wana wa Quraidha. Baba yake, mume na kaka waliuliwa katika vita vya Khaybar na watu wengi wa kabila lake walichukuliwa mateka. Safiyya alikasirishwa mno na kuwa na chuki dhidi ya Waisilamu.
Mjumbe wa Allah alilainisha hisia zake kwa kumwoa baada ya vita. Kutokana na ndoa hii, mahusiano pamoja na sehemu muhimu ya Wayahudi yalijengwa na kwa hivyo, wangepata kuujua Uisilamu kwa ukaribu zaidi. Aidha, kujua dhamiri mbovu za maadui mapema kumekuwa kwepesi na mipaka ya Uisilamu ikaanza kutanuka.
10. Mariyatu’l Qibtiyyah (Umm Ibrahim):
Mjumbe wa Allah alipeleka barua mbalimbali kwa tawala za nchi jirani ili kuwalingania Uisilamu. Moja ya tawala hizi ulikua ni Muqawqis, utawala wa Misri. Muqawqis alimwamkia mjumbe kwa njia nzuri na kumtumia Mtume zawadi na vijakazi wawili. Vijakazi hawa wawili walijifunza Uisilamu njiani na kusilimu. Walipofika Madina, Mjumbe wa Allah alimtwaa Mariya kwa ajili yake mwenyewe. Baadaye, alimwacha huru na kumwoa, ambaye alimzaa mwanawe Ibrahim.
Ndoa hii ilikuwa na ushawishi mkubwa kwa Wamisri wote. Wamisri hawakushiriki katika vita kati ya Waisilamu na Wabizantina wanaoishi nchini Misri na hawakuwasaidia Wabyzantinia. Moja ya sababu ya hili ni kuwa mwanamke kutoka taifa lao aliolewa na Mtume.
11. Maimunah bint Harith:
Jina lake halisi lilikuwa ni Barrah, ambalo lilibadilishwa na Mjumbe wa Allah baadae kuwa Maimunah. Ilikuwa ndio ndoa ya mwisho ya Mtume. Mwaka mmoja baada ya mkataba wa Hudaibiyyah, Mtume na Waisilamu walitembelea Makkah kwa ajili ya kuzunguka Alqaaba (tawaf). Abbas, mjomba wake Mtume, alimpendekeza Mjumbe wa Allah kumwoa Maimunah. Kwa hakika, Maimunah alikuwa ni shemeji wa Abbas na yeye Maimunah alimruhusu yeye kumchagulia mchumba wa kumwoa. Mtume alikubali pendekezo hili na kumwoa. Kutokana na hili, watu wa Makkah walisema: “Hii inamaanisha kuwa bado Muhammad anawapenda raia wake.”
Ndoa hii ilifanyika wakati Mjumbe wa Allah akiwa na miaka zaidi ya sitini. Lengo kuu la ndoa hii lilikuwa ni kumsaidia mjane, aliyeachwa kati ya waabudu masanamu mjini Makkah licha ya kuwa alikuwa ni Mwisilamu, ili amwokoe kutokana na matatizo yake na kutoa ishara njema kwa watu wa Makka.
12. Hazrat Zainab bint Jahsh:
Bibi Zainab alizaliwa miaka ishirini kabla ya kuanza utume na alikuwa ni binti wa shangazi wa Mtume. Jina lake halisi lilikuwa ni Barrah. Mjumbe wa Allah alilibadilisha na kumwita Zainab. Baba yake alikuwa ni Burrah kutoka kabila la Beni Asad na mama yake alikuwa ni Umm bnt Abdulmuttalib, shangazi yake Mtume. Alikuwa ni miongoni mwa wahamiaji wa kwanza kutoka Makka kwenda Madina. Alikuwa mwari alipohamia Madina. Mtume alimwoza kwa mwanawe wa kambo, Zaid bin Haritha.
Kama inavyoeleweka, enzi za Makkah zilikuwa ni enzi za misingi ya imani na enzi za Madina zilikuwa ni enzi za uwekaji wa kanuni. Matukio yaliyotokea wakati wa enzi hii ima ni kuondosha kanuni ya ushirikina iliyoenea katika jamii na kuota mizizi kutokea kale, ilibadilishwa kwa nyengine mpya au kuwekwa kanuni nyengine mpya.
Ukweli kwamba Bibi Zainab aliolewa na Bwana Zaid kabla ya Mtume na kwamba baadaye aliolewa na Mtume tofauti na wakeze wengine walioleta kanuni za kufuta mila na desturi za Zama za Ujinga.
Ndoa hii ya Mtume ambayo imepingwa vikali na wanafiki wa zama hizo na wajinga wa sasa ilikuwa ni ya Bibi Zainab. Pia, ilikuwa ni ndoa iliyopelekea kuasisiwa kwa sheria muhimu mno.
Matokeo yake ni sababu zifwatazo, mkataba wa ndoa hii ulikuwa ni “mkataba wa kiungu”, ikimaanisha imeidhinishwa na Allah Mtukufu wa Dhati Yake.
Dhana ya utumwa na tabaka la waheshimiwa ilikuwa na nguvu na kuota mizizi katika Zama za Ujinga. Dhana hii ni lazima ikomeshwe na lazima itiliwe mkazo kuwa watu wa juu mbele ya Allah hawatokani na matabaka yao, cheo au mbari lakini ni kutokana na taqwa. Kwa sababu hii, imani hii potofu kuhusu ndoa, ambayo ni moja kati ya masuala yenye hatari, yalikomeshwa kwa ndoa hii.
Mtume aliaka kuchukua hatua kuelekea lengo hili kwa kumwozesha mwanamke wa hadhi ya juu na mrembo kama Zainab kwa mtumishi wake Zaid, ambaye alimwacha huru. Hata hivyo, Zainab na kaka yake hawaikupendelea rai hiyo mwanzo, ambayo imelazimika kwa sababu ya imani iliyoenea katika jamii; kwa sababu haikuwa ni mila mwafaka kwa mwanamke huru na mtumishi wa hapo zamani kuoana.
Zainab alimwambia Mjumbe wa Allah maoni yake: “Ewe Mjumbe wa Allah, mimi ni binti wa shangazi yako. Sitaki kuolewa na yeye. Aidha, mimi ni kutoka kabila la Quraish.” Mjumbe wa Allah alimfafanulia kuwa Zaid alikuwa ni kipenzi mno kwake na kwa Uisilamu na kumweleza kuwa kwa hakika alikuwa ni mtukufu kwa sababu ya wazazi wake.
Kisha, aya ya 36 ya sura al-Ahzab ikateremshwa:
“Haiwi kwa Muumini mwanamume wala Muumini mwanamke kuwa na khiari katika jambo, Mwenyezi Mungu na Mtume wake wanapo kata shauri katika jambo lao. Na mwenye kumuasi Mwenyezi Mungu na Mtume wake basi hakika amepotea upotofu ulio wazi.”
Kutokana na hayo, Zainab akakubali kuolewa na yeye akisema, “sitomwasi Allah na Mjumbe wake.”
Hata hivyo, ndoa hii haikuendelea. Hakukuwa na mapenzi ya dhati na heshima kati yao. Licha ya kuwa Zainab alikuwa ni mwanamke mwenye dini aliyemwogopa Allah, bali alijisikia fakhari kutokana na uzuri wake na hadhi yake, na akimwangalia mumewe, aliyekuwa mtumwa hapo awali na kumuumiza kwa kejeli.
Bwana Zaid hakuweza kamwe kuhimili kuongezeka kwa kutowiana. Aliomba ushauri wa Mtume na kusema kuwa alitaka waachane. Mtume alikasirishwa sana kwa sababu yeye ndiye aliyetaka ndoa hii ifanyike. Alitaka kuzivunja imani potofu za jamii. Kwa sababu hiyo, alimwambia Zaid kila mara alipomjia: “Mtunze mkeo, usimpe talaka.” Hata hivyo, licha ya kila kitu, ndoa hii haikudumu zaidi ya mwaka mmoja. Mwishowe Zaid akalazimika kumpa talaka.
Baada ya muda, ikafika wakati wa kuvunja desturi nyengine lakini ada potofu zilizotokana na Enzi za Ujinga. Ilikuwa ni imani kwamba watoto wa kambo walikuwa wakizingatiwa kuwa ni watoto wa kuwazaa na hivyo, wake wa watoto wa kambo walikuwa wakizingatiwa kuwa ni mabinti wa damu wa baba wa kambo.
Uisilamu ukabadilisha kikamilifu dhana nyengine ya mtoto-wa-kambo. Aya ya Quran kuhusu maudhui hii ilikuwa iko wazi:
“Waiteni kwa baba zao, maana huo ndio uadilifu zaidi mbele ya Mwenyezi Mungu. Na ikiwa hamwajui baba zao, basi ni ndugu zenu katika Dini, na rafiki zenu.” (Sura al-Ahzab, 5)
Baada ya kuteremshwa aya hii ya Quran, Zaid alianza kuitwa Zaid bin Haritha, kwa kunasibishwa kwa baba yake. Baada ya imani hii potofu kuhusu mtoto wa kambo kukomeshwa, ikawekwa wazi kuwa wake zao hawakuwa kama mabinti wa damu wa baba wa kambo. Baadaye, hili lilibidi lithibitishwe na kutiliwa mkazo kwa mfano. Ingewezekana kupitia ndoa ya Bibi Zainab na Mtume. Hata hivyo, Mtume alikuwa na wasiwasi kuhusu uwezekano wa umbea wakati akikomesha mila hii iliyoota mizizi. Hata hivyo, kanuni hii iliyoletwa na Uisilamu ilipasa itekelezwe na yeye kabisa kabisa. Ilikuwa ni ya lazima. Kwa hakika, Quran inafafanua kama ifuatavyo:
“Na ulipo mwambia yule Mwenyezi Mungu aliye mneemesha, nawe ukamneemesha: Shikamana na mkeo, na mche Mwenyezi Mungu. Na ukaficha nafsini mwako aliyo taka Mwenyezi Mungu kuyafichua, nawe ukawachelea watu, hali Mwenyezi Mungu ndiye mwenye haki kumchelea. Basi Zaid alipo kwisha haja naye tulikuoza wewe, ili isiwe taabu kwa Waumini kuwaoa wake wa watoto wao wa kupanga watapo kuwa wamekwisha timiza nao shuruti za t’alaka. Na amri ya Mwenyezi Mungu ni yenye kutekelezwa.” (Sura al-Ahzab, 37)
Kwa kuifuata aya hii, mnamo mwaka wa tano wa Kuhama (Hijrah), Zainab aliolewa na Mtume kwa mkataba wa kiungu alipokuwa na umri wa miaka 35.
Kwa hakika, wanafiki walianza umbea kuhusu ndoa hii: “Ingawa Muhammad alilijua kwamba mwana wa mkewe alikuwa amekatazwa kwake, alimwoa mwana wa mkewe!” walisema. Kutokana na hili, ikateremshwa aya ya 40 ya sura al-Ahzaab:
“Muhammad si baba wa yeyote katika wanaume wenu, bali ni Mtume wa Mwenyezi Mungu na Mwisho wa Manabii, na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi wa kila kitu.”
Licha ya mitume kuwa ni aina ya baba kwa ummah zao na kuwalea kwa huruma zaidi na upendo kuliko hata baba zao wa damu, hii haimaanishi ubaba wa damu. Hivyo, aya hii ya Quran imeweka wazi kuwa sio mwafaka kwa upande wa mantiki, elimu na maumbile kwa mitume kuoa mwanamke kutoka katika ummah wao. Kutokana na hili, Uisilamu umetenganisha sheria ya watoto wa kambo na wale watoto wa kuwazaa. Hata hivyo, mila hii ilikuwa ni kongwe sana na madhubuti kiasi kwamba hakuna Waisilamu waliothubutu kuoa namna hiyo kwa wakati huo. Kwa sababu hiyo, wanafiki wa wakati huo walieneza umbea kuhusu ndoa hii na wakatengeneza kasumba nyingi kuhusu swala hili. Mbali na hayo, walijaribu kuionesha ndoa hii kuwa ni ushahidi wa ashiki ya Mtume (Mungu aepushe).
Maneno machache na jawabu la kunyamazisha la Badiuzzaman Said Nursi kwa wote wanaodhania kuwa ndoa hii inatokana na ashiki kama ifuatavyo:
“Mungu aepushe, mara mia kwa maelfu! Mkono wa mashaka ya kuchukiza hauwezi kumfikia yule aliyenyanyuliwa daraja! Ndio, alikuwa hivyo tokea umri wa miaka kumi na tano hadi arubaini wakati damu inapochemka na kuchangamka na ashiki ya roho inapowaka, ametosheka na kuridhika na mwanamke mmoja kama Khadijah Mtukufu (Allah amridhie) pamoja na kujizuia kikamilifu na unadhifu – kama ilivyo makubaliano ya rafiki na adui yanavyofanana. Baadaye yeye akawa na wake kadhaa baada ya umri wa miaka arubaini, yaani, wakati joto la mwili lishapoa na ashiki kutulia, ni ushahidi unaothibitisha waziwazi na unaojitosheleza kwa wale wote wenye angalau akili adilifu kwamba ndoa hizo hazikuwa ni kwa ajili ya kutosheleza tamaa za kimwili, bali zilikuwa zimeegemea kwenye mifano ya hekima.” (Mkusanyiko wa Risale-i Nur, Makala ya Saba)
Mtume, aliyemjua Zainab alipokuwa mwari bikira, angemwoa kabla ya kuolewa na Zaid. Hakukuwa na kizuizi kwenye hilo. Hivyo, ndoa hii imehitimisha mantiki muhimu kama vile kusawazisha imani potofu ambazo zilienea kati ya watu na kuwekwa sheria mpya.
7
Je inampasa Mwisilamu aongozwe na Quran au hadithi? Je Sunnah na Hadith zimegandana? Kwa kiwango gani hadithi ni za kuaminika?
Ulipotokea msambaratiko katika historia ya Uisilamu na wakati watu walipoihama Qur’an, wanazuoni wa Kiisilamu wamepekuwa na kukuta suluhisho katika Sunnah kwa sababu mwenye kuifafanua Quran bila ya shaka yoyote ni Mtume.
Wanazuoni wote wamezikubali Sunnah za Mtume (s.a.w.) kuwa ndio chanzo cha msingi cha kuifafanua Quran. Je kuna ukweli wowote ulioegemewa?
Ndio, wajibu wa utume hauishii kwa kufikisha Quran; kuifafanua, kuonesha namna itakavyotekelezwa pia ni wajibu wa Mtume. Mathalani aya zifuatazo zinachambua baadhi ya wajibu wa kiungu wa Mtume:
“Na hatukumtuma Mtume ila kwa ulimi wa kaumu yake ili apate kuwabainishia.” (Ibrahim,14-4)
“Ambao kwamba wanamfuata huyo Mtume, Nabii, asiye soma wala kuandika, wanayemkuta kaandikwa kwao katika Taurati na Injili, anaye waamrisha wema na anawakanya maovu, na anawahalalishiavizuri, na ana waharamishia viovu, na anawaondolea mizigo yao na minyororo iliyo kuwa juu yao. Basi wale waliomuamini yeye, na wakamhishimu, na wakamsaidia, na wakaifuata nuru iliyo teremshwa pamoja naye – hao ndio wenye kufanikiwa.” (al-Araf, 7-157)
“Haiwi kwa Muumini mwanamume wala Muumini mwanamke kuwa na khiari katika jambo, Mwenyezi Mungu na Mtume wake wanapo kata shauri katika jambo lao. Na mwenye kumuasi Mwenyezi Mungu na Mtume wake basi hakika amepotea upotofu ulio wazi.” (al-Ahzab ,33-36)
“La! Naapa kwa Mola wako Mlezi! Hawataamini mpaka wakufanye wewe ndiye muamuzi katika yale wanayo khitalifiana, kisha wasione uzito katika nyoyo zao juu ya hukumu utayo toa, na wanyenyekee kabisa.” (an-Nisa, 4-65)
“Mwenye kumt’ii Mtume basi ndio amemt’ii Mwenyezi Mungu. Na anaye kengeuka, basi Sisi hatukukutuma wewe uwe ni mlinzi wao.” (an-Nisa, 4-80)
“Na anacho kupeni Mtume chukueni, na anacho kukatazeni jiepusheni nacho. Na mcheni Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mkali wa kuadhibu.” (al-Hashr, 59-7)
“Sema: Ikiwa nyinyi mnampenda Mwenyezi Mungu basi nifuateni mimi, Mwenyezi Mungu atakupendeni na atakufutieni madhambi yenu. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kufuta madhambi na Mwenye kurehemu.” (Aal-e-Imran, 3-31)
Ndio, aya hizo hapo juu na mfano wa hizo zinaeleza kuwa wajibu wa Mtume wetu hauna mipaka wa kuifikisha Quran kwa watu.
Je tunaweza kulibainisha hilo?
1. Moja ya wajibu wa Mtume wetu ni kufafanua aya zilizofupishwa: Mathalani, Quran inasema, “Simamisheni sala”, lakini tusimamishe sala kwa namna gani? Inasema “Rukuuni (inamieni chini) na sajdah (sujuduni)”, lakini haitwambii kwa undani namna gani tufanye hivyo. Hakuna ufafanuni wa namna gani tufanye qiyam (tusimame wima). Mtume wetu anaifafanua ayah ii kwa muundo na maudhui, na kuonesha namna ya kutekeleza kwa kusema “Simamisheni sala kama nifanyavyo mimi”. Mtume wetu anafafanua maamrisho ya kimuhtasari ya Quran kama vile sala, funga na hajj.
2. Kufafanua aya ambazo ni ngumu kufahamika pia ni moja ya wajibu wa Mtume wetu.
Mathalani, yafuatayo yanaelezwa katika aya, “Basi waandalieni nguvu kama muwezavyo, na kwa farasi waliofungwa tayari-tayari, ili kuwatishia maadui wa Mwenyezi Mungu na maadui zenu, na wengineo ambao hamwajui, lakini Mwenyezi Mungu anawajua.” (al-Anfal,8-60). Katika aya hiyo, ibara “basi waandalieni nguvu kama muwezavyo na kwa farasi waliofungwa tayari-tayari” imetumiwa. Maswahaba wakamuuliza Mtume: “Nini nguvu?” Mtume wetu akasema, “Tambueni kwamba nguvu ni kurusha, nguvu ni kurusha, nguvu ni kurusha” mara tatu. Akatuamuru kudaka kwa kubadilisha vifaa vya kurushia kwa kila umri kwa kasi, bila ya kupoteza muda.
3. Mtume pia ameweka mipaka na kuhifadhi yasiyo na mipaka na aya jumla za Quran. Mathalani, yafuatayo yanaelezwa katika Quran, “Kakini Mwenyezi Mungu ameihalalisha biashara na ameiharamisha riba” (al-Baqara, 2-275). Kwa mujibu wa aya hii biashara ya kila kitu ni halali (imeruhusiwa). Hata hivyo, Mtume wetu ameliwekea mpaka na kukataza biashra ya nguruwe na vilevi. Hivyo, alifafanua mipaka ya biashara halali. Mfano mwengine ni aya hii: “Wale ambao wameamini, na hawakuchanganya imani yao na dhulma – hao ndio watakao pata amani na wao ndio walio ongoka.” (al-An'am, 6-82) Wakati aya hiyo ilipoteremshwa, maswahaba walimuuliza Mtume wetu: “Sote tunazidhulumu nafsi zetu. Ewe Mjumbe wa Allah, je yupo yeyote kati yetu asiyefanya kosa?” Mtume wetu (s.a.w.) akakumbusha aya “Kwa hakika shirki ndio dhambi kubwa-kabisa” na akafafanua hilo jambo ovu hapa ni shirki. Kwa hivyo, Mtume wetu anafafanua aya za Quran ambazo ni ngumu kufahamika.
3. Matukio katika Quran yalithibitishwa na kuidhinishwa na Mtume kwa kuyakariri. Hivyo, aliwafanya watu wayafahamu vizuri zaidi, ambako ndiko kulikotajwa hapa kuhusiana na suala hilo.
4. Mtume wetu pia ana mamlaka ya kisheria, yaani, anapitisha sheria ambazo hazimo ndani ya Quran. Mathalani, vyakula ambavyo ni haramu (vilivyokatazwa) vimetajwa katika aya mbili. Hata hivyo, nyama ya punda haijatajwa katika aya yoyote kati ya hizo. Mtume wetu akakataza kula nyama ya punda wa mitaani wakati wa safari ya vita vya Khaybar.
Kwa nini hazikuelezwa ndani ya Quran lakini zimeachwa kwa Mtume wetu?
Kama Quran ingetoa undani wote, kingekuwa ni kitabu chenye juzuu nyingi. Ingekuwa ni vigumu kwetu kunufaika nacho. Kwa hivyo, Quran imemwachia Mtume wetu ufafanuzi wa baadhi ya masuala. Zipo sababu nyengine za kwa nini ufafanuzi umeachwa kwa Mtume wetu. Baadhi ya masuala yalikuwa yamebatilishwa kufuatana na wakati.
Baadhi ya hadithi zimetufikia kuwa ni hadithi dhaifu. Kutekeleza kwa mujibu wa hadithi hizo dhaifu kunasababisha hitilafu. Khitilafu ni rehema kwa umma. Kama Allah ametja masuala yote kwa uhakika katika Quran, uwezekano wa hitilafu ungepungua. Unyumbukaji wa dini yetu dhidi ya mazingira ya wakati yanayobadilika na jamii ungepungua. Kwa hakika, mandhari ya juu ya dini yetu, nadhani, ni kuwa inafungua njia kwa tafsiri mpya kulingana na muda na pahala, jambo ambalo ni kitu kizuri.
Sio hayo tu. Mtume wetu ameacha mwanya kwa wanazuoni. Ndio uzuri wa dini yetu. Wanazuoni wanabainisha baadhi ya sheria za kimsingi na mitindo ya kutoa maamuzi kutekeleza kwa mujibu wa Quran na Sunnah. Wanazuoni wamefasiri masuala mapya kwa mitindo hiyo. Hivyo, tunaweza kuweka sheria zetu wenyewe kwa mazingira mapya bila ya kuhitaji sheria nyengine zozote mfumo wa kitamaduni na bila ya kuhaulisha sheria. Kwa hakika, mahitaji mapya yote yaliyotokea hadi kipindi cha mwisho cha Dola la Othmaniya yamefanywa sheria kwa kutegemea Quran na Sunnah na yamekusanywa kwenye kitabu pamoja na mfumo tunaouthamini wenyewe. Vipi watu wetu wataisoma Quran kupitia hadithi? Mathalan, sote tunasoma Sura Ya Sin kwa wingi. Kama tunataka kutambua “vipi Mtume wetu aliifasiri sura hiyo?”, tutajuaje? Kuna njia mahususi au mtindo fulani wa hilo?
Awali ya yote, Quran hufasiriwa kupitia Quran kwa sababu aya moja hufafanua aya nyengine. Suala fulani linafafanuliwa kwa namna moja katika aya fulani; katika aya nyengine, namna nyengine ya suala hilo hufafanuliwa, n.k. Hata hivyo, zipo tafsiri nyingi za Mtume wetu kuhusu Quran. Moja ya sehemu kubwa ya Bukhari ni Tafsir (tafsiri). Aidha, zipo hadithi zinazohusiana na tafsiri ambazo hazimo katika kitabu cha Bukhari wala Tirmidhi lakini zimetajwa katika vyanzo vyengine.
Kutumia sayansi ya hisabati, mimi baadhi ya wakati husema: mstari unapita kati ya nukta mbili. Vivyo hivyo, Quran ni nukta asili kuhusu maana ambayo tunaihitimisha kutokana na Quran. Kama haturejei kwenye hadithi kama ndio chanzo cha pili, kunaweza kuwa na maelfu ya mitazamo itakayoasisiwa kutoka kwenye nukta moja. Hata hivyo, ni nini dini? Ni dini ya kumpwekesha na mshikamano. Watu hawawezi kuhitimisha tafsiri tofauti kwa utashi wao kutoka kwenye aya hiyo lakini kwa kuitafsiri kwa mujibu wa ukweli. Tutapekuwa kile Mtume alichosema kuhusiana na suala hilo. Kama hakuna kitu kuhusu jambo hilo katika maneno ya Mtume, basi tutatafuta walivyosema Maswahaba wa Mtume, Tabi’in (wafwasi wa Maswahaba) na Atbaut Tabi’in (Wafwasi wa tabi’in; tutayatia akilini waliyoyasema. Wanazo fursa zaidi kuliko sisi katika kuifahamu Quran kwa mujibu wa uasili wake.
Kwa kiasi gani hadithi ni za kuaminika?
Hakuna sababu ya kwa nini tusizitegemee hadithi. Kama tulivyotaja hapo kabla, Quran inawaelekeza watu kwenye maneno ya Mtume, “Na anacho kupeni Mtume chukueni, na anacho kukatazeni jiepusheni nacho.” Yaani, mara zote Quran inaonesha kwa Mtume kuwa ndio chanzo cha pili.
Pili, Mtume anajiashiria mwenyewe; anavutia mazingatio kwa Sunnah zake na kueleza kuwa Uisilamu utaendelea kwa Sunnah zake. Mathalani, Bwana Mtume alimtuma Muadh nchini Yemen. Mtume alimuuliza, “Utashughulika vipi ukiwa huko?” Bwana Muadh akasema, “Nitashughulika kwa mujibu wa Quran”. Mtume wetu akauliza, “Itakuwaje ikiwa hukupata kitu kutoka katika Quran?” Akasema, “Kwa mujibu wa Sunnah zako na ikiwa sikupata kitu katika Sunnah zako, basi kwa jitihada yangu (kutoa sheria kutoka katika vyanzo asili)”. Mtume wetu akafurahishwa na majawabu yake. Hadithi hiyo ni ushahidi kwa ajili ya wanazuoni wa Uisilamu. Ni hoja kuwa Sunnah ni ushahidi na kwamba ijtihad ni muhimu. Hivyo, pale Mtume alipokuwa hai, Swahaba wamezijua hadithi kuwa ndio chanzo cha pili.
Bwana Umar anasimulia: “Nimefunga mkataba wa zamu kwa zamu na kaka yangu. Siku moja, alienda shambani na akalishughulikia; nikenda kwa Mjumbe wa Allah na kumsikiliza. Jioni, nikamjulisha kaka yangu kuhusu nilichokiona na kukisikia nilipokuwa pamoja na Mjumbe wa Allah. Kesho yake, nikenda shambani na kulishughulikia; kaka yangu akaenda kwa Mjumbe wa Allah na kumsikiliza. Jioni, aliniarifu kuhusu alichokiona na kukisikia alipokuwa na Mjumbe wa Allah. Hivyo, tuna fursa ya kumfuata Mjumbe wa Allah kwa karibu zaidi.”
Swahaba akasema: “Nilikuwa naandika kila nilichosikia kutoka kwa Mtume. Baadhi ya watu wakaniambia, ‘Mjumbe wa Allah ni binadamu pia. Wakati mwengine, anazungumza anapokuwa kakasirika na baadhi ya wakati, anapokuwa mtulivu. Sio sahihi kuandika kila anachokisema.’ Hapo, nikaacha kuandika. Hata hivyo, nikaanza kusahau nilichokisikia kutoka kwa Mtume. Kwa hivyo, nikenda kwa Mtume na kumwambia kuhusu suala hili. ‘Ewe Mjumbe wa Allah! Nimesikia habari nzuri kutoka kwako na nikaziandika lakini baadhi ya watu kutoka Ansar wamesema jambo. Kwa hivyo, nikaacha kuandika. Hata hivyo, nahisi sio rahisi kama siandiki. Nifanyeje? Mjumbe wa Allah akaashiria mdomo wake na kusema, ‘Hakuna chochote isipokuwa ni ukweli tu unaotoka katika kinywa hiki. Andika.’
Baadhi ya watu wamemjia Mjumbe wa Allah na kumlalamikia kuhusu hifadhi yao. Akawaambia, “Ombeni msaada wa mikono yenu ya kulia” akiwashauri kuandika.
Wacha niseme kitu kingine. Anas (Allah amridhie) amesimulia hadithi nyingi na yeye ni mmoja kati ya watu saba waliosimulia hadithi nyingi. Katika hadithi fulani nimeisoma katika Mustadrak, Bwana Anas anasema, “Nimeandika hadithi kutoka kwa Mjumbe wa Allah wakati wa mchana na kumsomea wakati wa usiku hivyo akawa anazisahihisha.” Yaani, Mtume wetu alisahihisha kile alichokiandika. Baada ya hayo, katika sayansi ya hadithi, wanafunzi huchukua hadithi walizojifunza kuzipeleka kwa walimu wao na kuwawasilishia. Wanafunzi huzisoma hadithi walizoziandika na kuzihifadhi mbele ya walimu wao; walimu huwasahihisha na kisha kuwapa wanafunzi stashahada.
Je tunaweza kusema kuwa hadithi zote ni tafsiri ya Quran?
Ndio tunaweza kusema hivyo. Mtume wetu (s.a.w.) aliitumia Quran katika maisha yake. Kwa hivyo, mfumo bora wa maisha ambao Quran unawataka watu umedhihirishwa kwa Mtume wetu (s.a.w.) Tukiuzingatia kwa mtazamo wa ibada, Mtume wetu ametuonesha namna ya kumwabudu Allah kunavotakiwa kuwe kamilifu. Mtume wetu ametekeleza aina zote za ibada kwa namna sahihi. Ibada ya Mtume wetu ni namna kamilifu ya kuabudu ambako Quran inatutaka tufanye kwa hali zote. Ni kitu hicho hicho kinafaa kwa mahusiano ya binadamu pia. Mtume wetu ametuonesha mifano bora zaidi katika uhusiano wake na watu na majirani zake. Pia ametuonesha mifano bora zaidi ya uhusiano wa mume na mke. Ametuonesha namna ya kukaa na watoto.
Hivyo, Mtume wetu (s.a.w.) amewakilisha vitendo na kuonesha mifano bora ya Quran katika hatua zote, vitengo na nyakati za maisha yake. Waisilamu wanaweza kuzichukua kama zilivyo kutoka kwa Mtume kwa kiasi kikubwa wawezacho. Katika hadithi, Bibi Aisha anaelezea maadili ya Mtume kuwa ni, “Maadili yake ni maadili ya Quran.” Kwa hivyo, Mtume wetu amefafanua maadili ya Quran kwa upande wa maadili. Labda, hakufafanua kila kitu kwa kusema kwa mdomo lakini alifanya kwa vitendo. Kila neno, tendo na ishara ya Mtume ni tafsiri ya roho ya Quran.
Kwa upande mwengine, alifafanua habari za mataifa yaliyopita. Katika hadithi, tunaweza kuona baadhi ya matukio kuhusu Bwana Ibrahim (Abraham) ambayo hayamo katika Quran. Hivyo, tunakuta masomo yote ambayo Quran inataka kuyataja, kuyaleta kwa watu kwa upande wa sheria, maadili na mfumo wa maisha katika maisha ya Bwana Mtume baadhi ya wakati kwa maneno yake, na wakati mwengine kwa amali zake na wakati mwengine kwa uchanganuo wake.
Yafuatayo yanaelezwa katika Quran,”kuleni na kunyweni: lakini msifanye israfu”. Katika aya nyengine, ufujaji umekatazwa. Ufujaji ni ndugu wa israfu. Hebu tuangalie utendaji wa Mtume ili tufahamu aya mbili hizo vizuri: Mtume wetu ameweka wazi mpaka wa israfu; mfano hai wa hilo ni wudu (udhu). Alipotia udhu, alitumia maji kwa uangalifu hivyo hakufanya israfu. Akatuamuru kuosha viungo vyetu kwa maji mara tatu-tatu tukiwa tunatawadha. Kutumia maji mengi zaidi ni makrooh (karaha). Akaweka mpaka huo. Mmoja ya Maswahaba alistaajabishwa na kuuliza: “Ewe Mjumbe wa Allah! Ni kwa ajili ya kuhifadhi maji?” Akajibu, “Hapana, hata kama ukiwa karibu na mto, utaosha viungo vyako mara tatu.”
Nimeona masimulizi kutoka kwa Abu ad-Darda katika hadithi: “Wakati mmoja, Mtume wetu aliwasili mtoni akiwa njiani kuelekea pahala fulani. Wakamletea bakuli la maji kutoka mtoni. Akatawadha kwa kutumia maji hayo na maji mengine yakabakia. Ni kawaida kwetu kuyamwaga pembezoni. Hata hivyo, Mtume wetu akasema, “Nenda kayamimine mtoni. Yanaweza kuwa ni kinywaji cha kiumbe fulani baadaye.”
Tukila zaidi ya tunavyohitaji, tukizungumza zaidi ya ulazima, tukitumia muda wetu ovyo, tunavipoteza. Ni upotevu ambao hatuwezi kuurejesha tena. Kuwasha kiberiti pia ni upotezaji. Ni makrooh. Ukweli kwamba Mtume ametwambia tusiyapoteze maji tukiwa tunatia udhu mara tano kwa siku, alitupa somo la kuheshimu uasili. Anatufundisha kwamba ufujaji ni swala hatari katika nyanja nyengine za maisha kupitia mfano wa udhu.
Sasa, hebu tuangalie ufafanuzi wa aya, “msifanye israfu”. Hivyo, tukiisoma aya hiyo, tunahitajika kurejea kwenye hadithi ili kuona namna aya hiyo inavyofafanuliwa. Utamaduni mpana wa hadithi yetu ni, kila tutakavyoielewa vyema basi tutaifahamu Quran. Je naweza kusema jambo kama hili kuwa ndio hitimisho? Tunaposoma aya katika Quran, tunapaswa tujaribu kuifahamu maana na tafsiri ya Quran. Hata hivyo, haitoshi kwetu, bali tunapaswa tuongeze utamaduni wa hadithi yetu. Tunapaswa tujifunze hadithi nyingi na kuyatengeneza maisha yetu kupitia hadithi hizo. Tunaposoma Quran kama hivyo, itakuwa kama tunajifunza maana ya Quran kutoka kwa Mtume.
Bila ya shaka. Wanazuoni wetu waliolifahamu hilo kwa namna hiyo, kwa mfano, Tabari, ameandika hadithi zote alizozikumbuka kuhusu aya. Baadhi ya watu wakamkosoa Tabari kwa sababu ameripoti hadithi nyingi. Tafsiri yake nyingi ya juzuu arubaini imejaa hadithi. Hata hivyo, tunapozirejea hadithi, tunazifahamu aya vizuri zaidi. Mwanga unaotolewa na hadithi ni tofauti na maana tunayoifasiri kwa kutafakari. Kwa maoni yangu, ni vyema zaidi kujaribu kuifahamu Quran kupitia hadithi.
Je Sunnah na hadithi ni kitu kimoja?
Je Sunnah, maisha ya Mtume wetu inamuunganisha Mwisilamu; je waifuate?
Tutalishughulikia suala hilo kwa mujibu wa hadithi na mitazamo ya wanazuoni.
1. Quran: Zipo baadhi ya aya zinaonesha kuwa Bwana Mtume anapokea ufunuo mwengine usiokuwa Quran (1) pia.
Baadhi ya hizo ni kama ifuatavyo:
1- Inafahamika kutokana na aya zifuatazo kuwa Mtume wetu alipewa hekima pamoja na Kitabu kitukufu: ‘Hakika Mwenyezi Mungu amewafanyia wema mkubwa Waumini vile alivyo waletea Mtume aliye miongoni mwao wenyewe, anaye wasomea Aya zake, na anawatakasa, na anawafunza Kitabu na hikima’, (2) ‘Na Mwenyezi Mungu amekuteremshia Kitabu na hikima’, (3).
Maneno hayo mawili yana mfanano na utofauti. Kwa mujibu wake, kwa kuwa kilichokusudiwa na Kitabu kitukufu ni Quran, hekima inalazimika kiwe ni kitu kingine. Uwezekano kwamba ni Sunnah unakubalika. (4) Ni nukta ya kutofautiana. Nukta ya kufanana ni kwamba vyote viwili vinatokana na ufunuo. (5)
2- Ahadi iliyoelezwa katika aya ifuatayo wamepewa Waisilamu lakini haikuelezwa katika aya hiyo ilikuwa ni nini: “Na Mwenyezi Mungu alipo kuahidini kuwa moja katika makundi mawili ni lenu” (6). Inathibitisha kuwa inaarifiwa kupitia namna nyengine ya ufunuo.
3- Aya ifuatayo inathibitisha waziwazi kuwa upo ufunuo mbali na Quran: “Na Nabii alipomwambia mmoja wa wake zake jambo la siri. Basi alipo litangaza yule mke, na Mwenyezi Mungu akamdhihirishia Mtume, alimjuvya sehemu na akaacha sehemu nyengine. Alipo mwambia hayo, huyo mke akasema: Nani aliye kwambia haya? Mtume akasema: Kaniambia Mjuzi Mwenye khabari zote!” (7) Licha ya kuwa hakuna ufafanuzi kuhusu kufichua siri katika Quran, Mtume anayajua hayo. Ni wazi kuwa upo ufunuo ambao haukujumuishwa katika Quran kwa kuwa hawezi kujua kivyakevyake na kwa kuwa inaelezwa kuwa Allah alimpa khabari.
2. Hadithi:
1- Kwa mujibu wa masimulizi ya Miqdad b. Ma’dikarib, Mjumbe wa Allah (s.a.w.) amesema yafuatayo: “…Nimepewa Kitabu na mfano wake”. (8)
2- Hadithi Qudsi: (9) ibara zifuatazo zilizomo katika hadithi za aina hii: “Mjumbe wa Allah ameeleza yafuatayo katika hadithi aliyoipokea kutoka kwa Mola wake Mlezi”, “Allah ameeleza yafuatayo katika hadithi kuwa Mjumbe wa Allah (s.a.w.) amesimulia” na ukweli kuwa hadithi hizo zimeanzia na maneno “Ewe mja wangu” zinathibitisha kuwa Bwana Mtume amepokea ufunuo mwengine usiokuwa Quran.
3- Tukio mashuhuri linalofahamika kuwa ni Jibiril (Jibrilu) hadithi: (10). Jibril alikuja katika umbile la binadamu, akiuliza maswali na kupokea majibu; Bwana Mtume aliwaambia maswahaba zake kuwa alikuwa ni Jibril na kwamba amekuja kuwafundisha dini.
4- Maneno ya Bwana Mtume (s.a.w.) kama vile ‘kwa uhakika Mola wangu Mlezi amenifunulia, (11) Nimeamrishwa, Nimekatazwa, (12) na ukweli kwamba alisema Jibril amemfundisha mambo fulani (13) yanathibitisha pia kuwepo ufunuo mwengine usiokuwa Quran. (14) Ukweli kwamba Bwana Mtume amesema “kwa kweli sikujua kuhusu hayo lakini Allah ameniambia” alipoyajibu maswali ya Myahudi” (15) yanaunga mkono suala hilo.
3. Mitazamo ya Wanazuoni:
Maswahaba wa Mtume walitambua kuwa Mtume wetu (s.a.w.) amepokea ufunuo mwengine zaidi ya Quran kutokana na matendo yake, ufafanuzi wake na maneno. Waliyasema hayo mara nyingi. Wanazuoni pia walitoa mitazamo yao kuhusu asili ya Sunnah inayoegemea kwenye hadithi na maneno ya maswahaba; wengi wao wameelezea kuwa chanzo cha Sunnah kiliegemea kwenye ufunuo.
Bibi Aisha (Allah amridhie) amesema kuwa kulikuwa na ufunuo kuhusu Bibi Khadija na kwamba amepewa kasri Peponi.
Maneno yaliyopo katika masimulizi: Jibril ameteremsha Sunnah kama alivyoteremsha Quran kunaonesha kwamba upo ufunuo mwengine usiokuwa Quran. (16) kwa kuongezea, ukweli kwamba Mtume amepokea habari kama kuwatendea wema majirani, kutawadha (udhu), kusimamisha sala, kutamka talbiya, kusimamisha sala kwenye Bonde tukufu la Aqiq, nyakati za sala, mlango wa pepo ambao umma wa Muhammad utaingilia, jina la Bwana Hamza (Allah amridhie) yameandikwa katika ubao na viumbe wa mbinguni (17) kunaonesha kwamba upo ufunuo mwengine usiokuwa Quran.
Tawus anasema kuwa yeye mwenyewe anayo maandishi yaliyoletwa na ufunuo kuhusu diyah (pesa ya damu, kikombozi/fidia) na kwamba hukumu kuhusu zakat na diyah zimekuja kwa ufunuo. (18)
Kwa kusema, “pindi hadithi inapotoka kwa Mjumbe wa Allah (s.a.w.) inapokufikia wewe, usitoe hukumu kinyume nayo; kwa sababu Mjumbe wa Allah (s.a.w.) alikuwa ni mfikishaji kutoka kwa Allah, Aliye Juu” (19) Awza ameeleza kuwa sunnah zimeegemea kwenye ufunuo.
Kama tulivyotaja kabla, mtu mwenye kutoa ufafanuzi muhimu kuhusu suala hilo alikuwa ni Imam Shafi. (20) Kwa mujibu wa ufahamu kuwa anaegemea kwa mtu ambaye elimu yake anaitegemea na kuwa yeye mwenyewe pia amekubali, Sunnah ima ni ufunuo, au maelezo ya ufunuo au ni kitu ambacho Allah amemkabidhi. Umeegemea zaidi kwenye utume wake ambao ni mahususi kwake na hekima kuwa Allah anamhamasisha umeegemea huko. Haijalishi ni upi kati ya vibadala hivyo ni chenye kukubalika, Allah ameamrisha watu kumtii Mjumbe wa Allah na kutenda kwa mujibu wa Sunnah. Ufafanuzi wa Quran kwa Sunnah unatokea ima kwa utume kuja kutoka kwa Allah, au kwa msukumo au kwa “amri” aliyopewa.
Ibn Hazm, anaekubaliana na mtazamo huo huo, anaelezea sunnah kuwa ni ufunuo usio-somwa (ghayr matluw) na anasema kuwa ni lazima kutii sunnah, ambazo ni ufunuo wa pili kama ilivyolazimika kuitii Quran. Vyote ni sawasawa katika hilo vyote vimeungana na vyote vinatoka kwa Allah. (21)
Ghazali anaeleza kuwa sunnah zinategemea ufunuo na kwamba ni ufunuo usio-somwa. (22)
Kama sunnah zote zinazingatiwa kuwa ni ufunuo, itakuwa ni wazi papo hapo kwamba Bwana Mtume (s.a.w.) hawezi kuzibadili Sunnah kama alivyokuwa hawezi kuibadili Quran. (23)
Hapa panaibuka suala muhimu pamoja na ufahamu kwamba sunnah zote zinategemea ufunuo kama ilivyo Quran. Kama Bwana Mtume (s.a.w.) aliusubiria ufunuo wa sunnah kama aya za Quran katika kila hali na tukio, mashauriano yake na jitihada zake zingeshughulikiwa vipi? Kwa hakika kuna baadhi ya nyakati alikuwa akisubiri ufunuo lakini kufikiria na kukubali kuwa alitenda kama hivyo katika kila hatua ya maisha yake kutasababisha matatizo.
Kutokana na hali hizo, baadhi ya wanazuoni wamekuwa na mtizamo kwamba si sunnah zote bali baadhi yake zilitegemea ufunuo na baadhi yake zilitegemea mazingira kama vile jitihada na mashauriano
Mathalani, Ibn Qutayba anasema yafuatayo, kukigawa chanzo cha sunnah katika sehemu tatu:
a) sunnah ambazo Jibri amezileta kutoka kwa Allah. (24)
b) sunnah ambazo Allah ameziacha kwa Mjumbe Wake (s.a.w.), ambazo Amemtaka kutoa mtazamo wake. (25)
c) sunnah ambazo Mjumbe wa Allah amezitekeleza kwa ajili ya adab; sunnah ambazo mtu anapata thawabu anapozifanya lakini hapati adhabu anapoziwacha. (26)
Sarakhsi wa Hanafi, aliyeupitisha mtazamo huo huo, anasema kuwa hukumu ambazo Bwana Mtume amezitoa zilizotegemea mawazo yake na jitihada ni kama ufunuo:
Ufunuo unakusanya sehemu mbili:
1- Ufunuo wa waziwazi. Umegawika sehemu tatu.
a) Ufunuo ambao unakuja kupitia ulimi wa malaika, unaodirikiwa na sikio na kwamba unatambulika kwa uhakika kuja kutoka kwa Allah. Sehemu hii ni ufunuo wa Quran.
b) Ufunuo ambao unafafanuliwa kwa Mtume na malaika kupitia ishara, bila ya hata neno moja. (27)
c) Msukumo. Ni udhihirisho wa kiungu katika moyo wa Mjumbe wa Allah (s.a.w.) bila ya kuwa na shaka yoyote. Mwangaza huchomoza moyoni mwake na hukumu kuhusu suala husika inakuwa waziwazi.
2- Ufunuo wa siri: Unaitwa “ma yushbihu’l-wahy” (unaofanana na ufunuo), Sarakhsi anasema kuwa zipo hukumu ambazo Mjumbe wa Allah (s.a.w.) zimemfikia kupitia mawazo yake na jitihada. Ukweli kwamba hakuachwa burebure kufanya makosa na kuwa mara zote alikuwa chini ya udhibiti wa ufunuo akitoa hukumu za namna hiyo kama ufunuo. Jitihada za watu wengine kutoka umma wake hazipo kama jitihada ya Bwana Mtume (s.a.w.) kwa kuwa upo uwezekano wa kufanya makosa na ni jambo lisilowezekana kusahihishwa kupitia ufunuo. (28)
Uchambuzi wa Sarakhsi unamaanisha matendo yote ya Bwana Mtume (s.a.w.) yanategemea na kusahihishwa na ufunuo. Tendo au neno la Bwana Mtume (s.a.w.) ima ni sahihi au si sahihi. Kama litabakia kama lilivyo, inakuwa wazi kwamba ni sahihi kwa sababu Allah hatoliacha tendo au neno lisilo sahihi kuendelea.
Shatbi anasema yafuatayo:
Hadithi ima ni ufunuo safi unaokuja kutoka kwa Allah au ni jitihada ya Bwana Mtume (s.a.w.). Hata hivyo, katika hali hiyo, jitihada yake ni ima inategemea ufunuo mzuri katika Kibatu kitukufu au sunnah au imeshakaguliwa. Hata kama mtazamo kuwa Bwana Mtume anaweza kukosea katika jitihaza yake inakubaliwa, kamwe hatoachwa kwenye makosa; litasawazishwa haraka. Mwishowe, litakuwa ni sahihi. Kwa hivyo, hakuna uwezekano wa makosa katika kitu chochote kinachokuja kutoka kwake. (29)
Kutenda kwa mujibu wa mitazamo hiyo, inaweza kusemwa kuwa wale wote wanaosema sunnah zote ni ufunuo hawakuzi-mambo kwa sababu sunnah zote zinakaguliwa na ufunuo; hizo ima zinaachwa kama zilivyo au kusahihishwa. Yaani, kwa kuwa hatuwezi kukubali uwepo wa utendaji ambao haujakaguliwa na ufunuo, tunaweza kusema kama ni hitimisho kuwa sunnah zote zinategemea ufunuo. Hata hivyo, tunaposema sunnah zote zinategemea ufunuo, tunamaanisha sunnah ambazo zimebainishwa wakati wa umri wa Mjumbe wa Allah na kwamba zimetufikia zikiwa sahihi.
4. Ufunuo uliothibitishwa Kimyakimya (taqrir)
Tunachomaanisha kuwa ni sunnah za taqrir tunapofafanua sunnah ni uthibitisho wa ukimya wa Bwana Mtume (s.a.w.) wa baadhi ya matendo au maneno aliyoyaona au kuyasikia. (30) Yaani, maswahaba walipofanya au kusema kitu kilichoegemea kwenye matendo ya Jahiliyya au maono yao wenyewe, Bwana Mtume baadhi ya wakati aliwasahihisha, na wakati mwengine aliwabadilishia na wakati mwengine hakusema kitu. Maswahaba walikizingatia kimya chake kuwa ni ruhusa kwa sababu isingefaa kwa mtume kuacha kosa kama lilivyo. Kwa hivyo, ukimya wake umemaanisha kuwa tendo hilo au neno halikuwa kosa.
Maswahaba walikuwa chini ya udhibiti wa Bwana Mtume (s.a.w.); vivyo hivyo, kwa Mjumbe wa Allah (s.a.w.) daima alikuwa chini ya udhibiti wa ufunuo kama ulivyo ulazima wa sifa ya ismah (kutokufanya makosa) (31). Kwa hivyo, inapaswa itambulike kwamba kosa lake lisingeachwa bila ya kusahihishwa (32) na kwamba lingetolewa onyo haraka, bila ya kusita (33). Bwana Mtume (s.a.w.) anatofautiana na mtu mwengine yeyote na kutokana na wale walioidhinishwa kujitahidi.
Inaeleweka kuwa alionywa kwa sababu ya baadhi ya matendo yake hata kabla hajawa mtume. (34)
Wakati mmoja, alipotaka kuvua izar yake (vazi la nje/seruni) ili arembee mawe alizuiliwa. Katika tukio jengine, alitaka kuivua izar yake ili amsaidie mjomba wake Abu Talib kwa ajili ya kukarabati Kisima cha Zamzam lakini alizimia. Alisema mtu mmoja aliyekuwa na nguo nyeupe alimwambia ajisitiri yeye mwenyewe alipokuja. (35)
Mwili wake ulihifadhiwa ili kumlinda asioneshe sehemu ambazo sio vyema kuwaonesha wengine; pia alihifadhiwa kutokana na baadhi ya matendo yasiyopendeza katika kipindi hicho. Kwa mujibu wa maelezo yake mwenyewe, alitaka kutazama baadhi ya michezo na burudani katika maeneo ambayo sherehe za arusi zikifanyika lakini alilala na hakutazama wala kuzisikia; baadaye, hakutenda tena mambo mabaya mpaka alipochaguliwa kuwa mtume. (36)
Je inaweza kufikiriwa kuwa mtu aliyekuwa chini ya matunzo hata kabla hajawa mtume na hajachaguliwa kuwa ni mfano kwa umma wake na utu bado asingehifadhiwa katika kipindi alipokuwa mfano katika mandhari zote kwa ajili ya umma wake na utu na kuwa makosa yake yasingesahihishwa? (37)
Kwa hakika, tunaona mifano kadhaa ya katika Quran.
Bwana Mtume (s.a.w.) alikuwa na wasiwasi kuhusu matunzo ya ufunuo na Allah, Aliyetukuka, aliuondosha wasiwasi wake kwa kusema hakuna haja ya kuwa na woga kuhusu hilo. (38)
Alionywa kuhusu masuala kama vile kuwaongoa watu, watu kutii amri ya Allah, jukumu lake lilikuwa tu ni kufikisha ujumbe wa Allah ambao uongofu huo unategemea utashi wa Allah na kwamba matokeo hayo yanategemea utashi wa Allah (39); alionywa kuhusu Abu Talib, ambaye alimwombea msamaha na akakatazwa kumwombea dua mjomba wake. (40)
Kwa upande mwengine, alisitishwa kuwalaani maadui zake baada ya Vita vya Uhud (41) kutokana na utashi wake wa kutolewa viungo kutokana na yale aliyofanyiwa Bwana Hamza (Allah amridhie) (42).
Zaidi ya hayo, alionywa kuhusu kuwaachia huru wafungwa wa vita kwa kupewa fidia baada ya Vita vya Badr (43); aliepushwa kutokana na matendo aliyoyataka ili kuzichota nyoyo za wanafiki (munafiq) (44); pia alionywa alipojiharamishia yale ambayo Allah amemhalalishia kutokana na matakwa ya wafungwa wa vita. (45)
Aya hizo hapo juu na sawa na hizo ni ishara za wazi ambazo Bwana Mtume (s.a.w.) amesawazishwa wakati kile alichokifanya hakikuendana na ridhaa ya kiungu. Allah, Mtukufu, mwanzo alimwachia tu na akamtaka ajitahidi au ashauriane na maswahaba zake. Kisha, kama iliwiana na ridhaa ya Allah, basi iliachwa kama ilivyo; kama haikuwiana, alisahihishwa. Kwa hakika, ukweli kwamba mwanzo alisema watoto wa washirikina walikuwa ni kama baba zao na kisha akasema kuwa wangeweza kwenda Peponi, kwamba mwanzo alisema mijusi wamewalaani Wayahudi na kisha akaiwacha rai hiyo kwa onyo la ufunuo. Kwamba mwanzo alisema mtazamo unaohusiana na mateso ya kaburini yalikuwa ni uovu wa Wayahudi na kisha akakubali uwepo wa adhabu kaburini kutokana na onyo lililoletwa na ufunuo na kutubia kwa Allah kutokana na hilo katika dua zake, (46) akionesha kuwa alionywa na kusahihishwa nje ya ufunuo wa Quran pia.
Kama inavyoonekanwa, ni muhali kwa Mjumbe wa Allah kuendelea na amali mbovu, tendo au neno aliloliona au aliloarifiwa kwa sababu ruhusa ya ukimya wa namna hiyo inafuatwa na umma; pia ni muhali kwa Mjumbe wa Allah (s.a.w.) kuendelea kutenda maovu au maneno katika uwepo wa Allah; lolote alilofanya wakati wa maisha yake ni mfano na ni kitu cha kufuatwa na sisi.
Kisha, Allah, ambaye ni Mjuzi-wa-Kila-Kitu, Mwelewa-wa-Kila-Jambo, Msikivu-wa-Kila-Kitu, Mwenye-Kuona-Kila-Kitu na Mwingi wa Hekima, pia aliyasahihisha maneno ya namna zote, amali na matendo ya Mtume au aliyaidhinisha na kuyawacha kama yalivyokuwa. Iwe tunayaita mambo hayo ambayo Allah hakuyabadilisha na kuyaacha kuwa ni ufunuo wa siri kama wanazuoni wa madhehebu ya Hanafi wanavyoyaita (47) au ni ufunuo uliothibitishwa kimya-kimya, tunaweza kusema kuwa sunnah za Bwana Mtume (s.a.w.) zinategemea ufunuo.
Kutenda kwa mujibu wa ukweli huo, tunafikiria kuwa tunapaswa tukubali kuwa mwendelezo wa baadhi ya ada na mila za jumuia ya Mtume zimeishi wakati zimeshakaguliwa na Allah na kwa kuwa zilikuwa ni idhinisho la kimya-kimya, sio sahihi kuyazingatia hayo kuwa ni desturi tu na mila. Isitoshe, tumeeleza kuwa yameegemea kwa Bwana Ibrahim (a.s.) au mitume wengine.
Kisha, hata kama ishara na matendo ya Mtume yalikuwepo kwa muundo sawa na wa kipindi cha Jahiliyya, yangesahihishwa na ufunuo kama yangekuwa ni kosa. Inaweza kusemwa kuwa yale yote ambayo hayakusahihishwa basi yameidhinishwa.
MASIMULIZI YALIYORUHUSU HADITHI KUANDIKWA
Kuna masimulizi mengi yanayoonesha kuwa imeruhusiwa kuziandika hadithi. Moja ya masimulizi yapo kwa Abullah Ibn Amr (Allah amridhie); hadithi alizoziandika zimepelekwa kwa kizazi kilichokuja baada yake kwa namna ya vitabu. Akasema:
“Nilikuwa nikiandika chochote nilichosikia kutoka kwa Mtume ili kukihifadhi. Makuraishi walinikataza kuandika wakisema: ‘Unaandika unachokisikia kutoka kwa Mjumbe wa Allah (s.a.w.); hata hivyo, Mjumbe wa Allah ni binadamu pia. Wakati mwengine, anazungumza akiwa na hasira na wakati mwengine, anapokuwa mtulivu. Hapo, niliacha kuandika. Hata hivyo, nilimwarifu Bwana Mtume kuhusu hali hiyo. Mjumbe wa Allah akauashiria mdomo wake uliobarikiwa na akasema, ‘Andika! Naapa kwa Allah kwamba hakuna chochote zaidi ya ukweli unaotoka kinywani mwangu.” Masimulizi haya yanathibitisha kuwa Abdullah Ibn Amr (Allah amridhie) aliandika hadithi kwa mfumo wa Abu Hurayra na umesajiliwa kwa Bukhari. Abu Hurayra (Allah amridhie) anasema yafuatayo: “Hakuna anayenishinda kwa kuzijua hadithi za Bwana Mtume isipokuwa Abdullah Ibn Amr; kwa sababu alikuwa akiandika lakini mimi sikuandika.
Masimulizi yanayoelezea ruhusa kuhusu hadithi sio tu zile tulizozitaja. Ukweli kwamba Mjumbe wa Allah (s.a.w.) aliwaambia watu waliokuwa wakilalamikia hifdhi yao: “Ombeni msaada wa mikono yenu ya kulia”, ishikeni elimu kwa kuiandika”, kwamba alitoa maandishi ya hotuba zake kwa watu waliozitaka kwa maandishi, ambapo kuna kiasi cha makala 300 (ambazo ni nyaraka zilizoandikwa) ambazo zote ni hadithi na urefu wao unatofautiana kwa mistari michache kwenye kurasa chache kunathibitisha kuwa ilikuwa ni ruhsa kuandika hadithi. Hata kama ni makala tu zilizozingatiwa, itafahamika kuwa Bwana Mtume hakupinga kimfumo na kimsisitizo kuandika vitu vyengine visivyokuwa Quran na kwamba alitoa umuhimu mkubwa kwa matumizi ya uandishi katika maisha ya kiraia.
AS-SAHIFA AS-SAHIHA (KURASA NJEMA) ZA ABU HURAYRA:
Katika baadhi ya masimulizi, inaelezwa kuwa Abu Hurayra (Allah amridhie) ameandika hadithi alizozisikia kutoka kwa Mjumbe wa Allah (s.a.w.). Jina la ukurasa huo ni as-Sahifa as-Sahiha. Al-Hasan Ibn Amr Ibn Umayya ad-Damri anasimulia: “Nimeripoti hadithi karibu na Bwana Abu Hurayra (Allah amridhie). Hata hivyo, akaikanusha kwa kusema: “hakuna hadithi kama hiyo.” Nikamwambia kuwa nimeisikia kutoka kwake. Kisha, akasema, “Kama umeisikia kutoka kwangu, lazima niwe nayo kwa maandishi” na akanichukua kwa kunikamata mkono hadi nyumbani kwake. Huko, akanionesha vitabu tele ambavyo hadithi za Bwna Mtume (s.a.w.) zimeandikwa. Akaikuta hadithi ambayo nimeiripoti na akanambia: “Sikukwambia mie kuwa kama nimesimulia hadithi, itakuwa ninayo kimaandishi?”
KUKUSANYA HADITHI:
Kipindi cha pili muhimu cha historia ya hadithi kimekusanya kazi zilizoitwa “tadwin as-sunnah” (uandikaji nyaraka na usajili wa hadithi kwa maandishi”. Inaifunika karne ya pili ya Hijria.
NINI/NI NINI TADWIN?
Katika kamusi, tadwin inamaanisha kutunga na kukusanya kwenye kitabu kimoja. Kama ulivyo msamiati wa hadithi, inamaanisha kusajili rasmi hadithi kwa njia ya maandishi na kuzikusanya kwenye kitabu kimoja. Neno “rasmi” ni muhimu mno hapa. Kama inavyoonekana katika sehemu zilizopita, usajili wa hadithi umeanza wakati wa zama za Mjumbe wa Allah (s.a.w.) na mtu mmoja mmoja na binafsi. Kwa hakika, MJUMBE WA ALLAH yeye mwenyewe ameacha nyaraka nyingi za maandishi na zote ziliitwa “sunnah”. Hata hivyo, hakuna kati ya hizo zimehusishwa katika tendo la “uandishi” ikielezwa kwa neno tadwin kwa sababu kwenye tadwin, uandishi wa hadithi zote unahusika. Kisha, tunaweza kuchambua tadwin kiusahihi kama ifuatavyo: “mchakato wa uandishi wa hadithi zote uliotekelezwa katika karne ya pili ya Hijria chini ya uangalizi wa dola”.
UMEANZAJE?
Mchakato wa tadwin umeanza na Umar bin Abdulaziz, Khalifa wa kabila la Umayya. Umar bin Abdulaziz (Allah amrehemu), ambaye ni maarufu sana kwa uchamungu wake na bidii yake kwa sunnah za Mjumbe wa Allah (s.a.w.), akaanza kupatwa na wasiwasi kuhusu hadithi kama ilivyokuwa ni/katika kazazi cha maswahaba waliojua sunnah vizuri sana na wanazuoni wakubwa walivyoanza kufariki mmoja baada ya mwengine. Akafikiria kuwafanya wanazuoni waandike hadithi ili kuepusha hatari ya kupotea kwake. Kwa hivyo, yeye kwa kuwa ni Khalifa/Halifa alipeleka mashauri na notisi za ilani kwa magavana.
Maandiko ya moja ya barua ambazo Umar bin Abdulaziz aliyapeleka yamesajiliwa na Bukhari. Ni barua aliyoituma kwa gavana/kadhi wa Madina, Abu Bakr Ibn Hazm: “Tafuta, kusanya na andika masimulizi ya Bwana Mtume (s.a.w.) katika mji wako. Nachelea kuwa sayansi (hadithi) itapotea na wanazuoni watatoweka. Ukiwa unafanya hivyo, sunnah za Mjumbe wa Allah pekee (s.a.w.) ndio zitakazokubalika. Wanazuoni wanapaswa wakae katika maeneo maarufu ya wazi kwa umma kama misikitini, kueneza elimu na kuwafundisha wasiojua. Sayansi haitotoweka labda ifanywe ni siri.” Kwa mujibu wa masimulizi ambayo Ibn Sa’d ameyasajili, Umar Ibn Abdilaziz (Allah amrehemu) anayo ibara ifuatayo ya ziada katika barua aliyoiyandika/aliyoiandika kwa Ibn Hazm:
“…sunnah zilizopo zinazojulikana au masimulizi ya Amra Bintu Abdirrahman yanapaswa yakubalike…”
Ibara ya ziada ifuatayo/ibara ifuatayo ya ziada ipo katika simulizi/masimulizi ya Darimi:
“Andika masimulizi ambayo ni hakika yamekuja kutoka kwa Bwana Mtume (s.a.w.) na kutoka kwa Bwana Umar uliyo nayo (au ambayo yapo katika eneo lako)”.
Kwa mujibu wa aliyoyasajili Abu Nuaym katika Tarikh Isfahan, Umar Ibn Abdilaziz alipeleka barua kwa miji yote ya Kiisilamu.
Hivyo, kwa kuchukua masimulizi mbalimbali yaliyotaja tadwin kwa mazingatio, tunayo rai ya jumla kuhusu suala hili. Ili kulienzi jaribio hilo la Umar Ibn Abdilaziz, tunahitaji kutaja maneno yafuatayo ya Muhammed Ibnu Shihab az-Zuhri, ambaye ni mtu aliyehudumia kwa kiwango kikubwa katika mchakato wa tadwin na ambaye ndiye aliyeupa mchakato huo jina la tadwin:
“Hatuzingatii kuwa ni mwafaka kuandika elimu mpaka watawala watulazimishe kufanya hivyo. Tukianza kufanya hivyo (kama ni matokeo ya kulazimishwa na uingiliaji kati wa watawala), tumeamini kwamba hatutakiwi tumzuie Mwisilamu yeyote kuandika.”.
SABABU ZILIZOSABABISHA KUKUSANYWA KWA HADITHI
Kutakuwa na manufaa kutazama kwa karibu sababu halisi zilizosababisha hadithi kuandikwa na kukusanywa kwenye vitabu:
1- Kwa makubaliano ya pamoja ya wanazuoni, moja ya sababu hizo ni hii ifuatayo kwamba imeelezwa katika barua ya Umar Ibn Abdilaziz: Wasiwasi kwamba hadithi zitapotea kwa sababu ya vifo vya wanazuoni: Ni suala muhimu sana. Ingawa hadithi zimeandikwa na mtu mmoja mmoja, zimeandikwa ili zihifadhiwe; zikishahifadhiwa, vitachomwa moto; au itashauriwa vichomwe moto baada ya kifo cha mmoja wao. Masimulizi ya hapo juu tuliyoyanukuu kutoka kwa Zuhri yanatosha kufahamu wasiwasi na hofu kati ya wanazuoni.
Isitoshe, kipindi hicho kilikuwa ni kipindi ambapo machafuko ya kisiasa na vurugu za wenyewe kwa wenyewe zimetokea. Kifo cha Said Ibn Jubayr, mwanazuoni mashuhuri wa hadithi wa zama hizo, ambaye aliuliwa na Hajjaj az-Zalim, ilikuwa inatosha kumtia hofu Umar Ibn Abdilaziz kuwa hadithi zingeweza kupotea. Nini chengine zaidi, matukio yanofanana/yanayofanana na hilo yamesababisha kifo cha Talq Ibnu Habib; Mwanazuoni mashuhuri, Mujahid ameponea chupuchupu kufa lakini alitupwa gerezani.
2- Ingawa haikuakisi waziwazi katika barua ya Umar Ibn Abdilaziz, sababu nyengine muhimu ambayo ilianzisha tadwin ilikuwa ni ongezeko la michakato ya uchakachuaji wa hadithi kutokana na khitilafu za kisiasa na kimadhehebu. Maneno yafuatayo ya Zuhri (Allah amrehemu) yanathibitisha na kutilia mkazo hilo: “Kama isingekuwa kwa hadithi isiyojulikana kwamba imekuja kutoka mashariki na kwamba tumeikataa, nisingeandika hata hadithi moja wala nisingemruhusu yeyote kuandika hata moja.”
Suyuti anasema yafuatayo ili kueleza mchango wa mchakato wa udanganyifu wa hadithi katika tadwin: “Katika enzi ambapo wanazuoni wametawanyika na udanganyifu na uzushi (bid’a) za Khawarija na Rafidhwa umeongezeka, sunnah zikaandikwa na kukusanywa kwenye vitabu kwa kuviunganisha na maneno ya Swahaba na fatwa za Tabi’in.”
VIPI TADWIN IMETOKEA:
Masimulizi yanaonesha kuwa Umar Ibn Abdilaziz hakukuta kuwa inatosha kutuma notisi ya ilani; alifwatilia na kukagua michakato ya tadwin kwa uangalifu. Mathalani, aliwakodi makarani maalumu kufanya kazi ya tadwin katika kituo maalum; aliwateua makarani wawili kwenda kwa Hishm Ibn Abdilmalik, na Zuhri. Waliandika hadithi za Zuhri kwa mwaka mzima.
Umar Ibn Abdilaziz, Khalifa, yeye mwenyewe alishiriki katika michakato ya tadwin; alikwenda msikitini na kalamu mkononi mwake kwa ajili ya kusali na akajiunga na masomo baada ya sala, kuandika hadithi kutoka kwa Awn Ibn Abdillah na, Yazid Ibnu’r Raqqasi.
Wakati wa tadwin, sio tu masimulizi yaliyorejeshwa katika/ya zama za Mjumbe wa Allah (s.a.w.) bali pia maneno na matendo ya Maswahaba na Tabi’in yamehusishwa na baadhi ya wanazuoni wa hadithi kuwa katika nadharia ya sunnah.
Hadithi zilizoandikwa kutokana na amri ya KhalifaHalifa zilipelekwa kwenye kituo katika muundo wa vitabu; vilitolewa nakala huko na vikapelekwa kwenye miji ya Kiisilamu. Usimulizi wa uandishi wa waraka muhimu ambao umetolewa unakuja kutoka kwa Zuhri: “Umar Ibn Abdilaziz (Allah amrehemu) ametuamuru kukusanya sunnah na tumeziandika katika vitabu. Umar Ibn Abdilaziz (Allah amrehemu) alipeleka kitabu kwa kila mji alioutawala.”
Ni hakika kuwa vitabu vilivyopelekwa vilikuwa ni nakala za vitabu asilia katika kituo.
Baadhi ya masimulizi yanaeleza kuwa hadithi zilikusanywa kituoni hapo zikakaguliwa na wanazuoni: Abu’z-Zinad Abdullah Ibnu’z-Zakwan anasimulia: nimemwona Umar Ibn Abdilaziz akiwaleta pamoja wanazuoni wa fiqh. Wanazuoni wa fiqh wamekusanya kiwango kikubwa cha hadithi. Akazisoma pamoja na wanazuoni na wakati sunnah ambayo haikutekelezwa/haikuwepo imesomwa, amesema: “Hii ni ziada; hakuna haja ya kuitegemea.”
Inaweza kusemwa kuwa nakala zilizopelekwa mijini zilitolewa nakala baada ya kuchunguzwa na kamati hiyo:
Sifa muhimu za msingi za michakato ya tadwin ni kwamba hadithi hazikuandikwa chini ya vigawanyo kama vile sunan, sahih au musnad. Jambo lililokuwa muhimu katika tadwin lilikuwa ni kuziandika, kuziweka katika maandishi sio namna nyengine yoyote au lengo/au lengolingine lolote. Kwa hivyo, masimulizi marfu (yaliyorejeshwa kwa Mtume), mawqut (yaliyowekewa wakati), maqtu (yaliyokatika) yameandikwa pamoja na hasan (yaliyohakikiwa vyema) na daif (dhaifu). Tofauti yao na vigawanyo vingeshughulikiwa katika karne ijayo iliyoitwa zama za tabwib (kugawanywa katika milango).
MCHANGO WA ABU BAKR IBN HAZM:
Hatuna waraka wowote unaoonesha kwamba gavana/kadhi wa Madinah, Abu Bakr Ibn Hazm, ameandika hadithi zozote yeye mwenyewe kutokana na amri licha ya kuwa alikuwa ni mwanazuoni mkubwa wa hadithi. Labda aliona inatosha kuwalazimisha wanazuoni wafanye kazi ya tadwin kama ni gavana/akiwa kama kadhi. Kwa hakika, Zuhri, aliyeikubali kazi ya tadwin na kutoa mchango wa msingi ndani yake, ni mwanazuoni wa Madinah na kwa hakika alianza kufanya kazi kutokana na amri ya Abu Bakr Ibn Hazm.
Ingawa maisha ya Umar Ibn Abdilaziz yalikuwa sio marefu ya kutosha kuona matunda ya michakato ya tadwin, tumeripoti hapo juu kutoka kwa Zuhri kwamba vitabu vilivyokusanywa katika kipindi chake vimefikia kiwango cha kutosha cha kutolewa nakala na kupelekwa miji mikubwamikubwa. Kwa hivyo, wanazuoni wa Kiisilamu wamekubaliana kwa kauli moja kuwa tadwin ya kwanza imeanza wakati wa zama za Umar Ibn Abdilaziz (Allah amrehemu), katika miaka ya mwisho ya karne ya kwanza ya Hijria.
Profesa Dk. İbrahim Canan
Dk. Ahmet Çolak
Tanbihi:
1- Ingawa imesemwa kuwa kilichomaanishwa na aya: “Wala hatamki kwa matamanio. Hayakuwa haya ila ni ufunuo uliofunuliwa” ni Quran, wapo wanazuoni wanaosema inahusisha sunnah pia. Mathalani, Elmalılı (mwanazuoni wa kituruki wa tafsiri) anatafsiri aya hii kuwa “Hiyo, yaani, Quran au hotuba yake, si chochote/kingine isipokuwa ni ufunuo. Haiwezekani kuelezewe/kuzieleza kwa namna nyengine yoyote. Inawezekana tu kuteremshwa kuwa ni ufunuo.” Hivyo, anaashiria kuwa sunnah ni ufunuo pia. (Yazır, Hak Dini VII, 457); Cf Qurtubî, Tafsir, XVII,84-85; Aydınlı, Abdullah, Sünnetin Kaynağı Hakkında, Din Öğretimi dergisi, Issue37, Ank, 1992, uk.48; Kırbaşoğlu, Sünnet, 236 pamoja na wengine.
2- al-Baqara, 48; Aal-e-Imran, 164.
3- an-Nisa, 113; al-Jumua, 2.
4- Kwa wale wanaosema kilichokusudiwa na neno hekima ni sunnah, tazama Hasan al-Basri, Qatada, Yahya b. Kathir, (Suyuti, Miftahu’l-Janna, s.23); Imam ash-Shaii, ar Risala, 32,78,93.
5- Ukweli kwamba Quran na sunnah vyote ni ufunuo unazusha swali kuwa tofauti kati yao ni ipi? Tunafahamu kutokana na aya hiyo kuwa hakuna tofauti kati yao kwa upande wa asili. Hata hivyo, mmoja kati yao ni wahy matluw (ufunuo unaosomwa), na mwengine ni wahy ghayr matluw (ufunuo usio-somwa). Suyuti anafafanua suala hili kama ifuatavyo: Neno la Allah lina pande mbili. Allah anamwambia Jibril, “Mwambie Mtume, Allah anakuamrisha kufanya hili na lile. Jibril anafahamu utashi wa kiungu na kufikisha kwa Mtume. Inaweza kufananishwa na mfalme anampeleka mtu wa kuaminika kama ni mjumbe kwa maudhui zake na uwasilishaji wa ujumbe kwa ujumbe kupitia maneno yake mwenyewe. Nyengine ni: Allah anamwambia Jibril, “Nenda kwa Mtume na msomee kitabu hiki.” Jibril anamsomea Mtume kitabu hiko kama kilivyo, neno kwa neno. Ufunuo wa Quran unaweza kufananishwa na huo muundo wa pili na sunnah kufananishwa na muundo wa kwanza. Kwa hivyo, inasemwa kuwa inaruhusika kuripoti sunnah pamoja na maana. Suyuti, al-Itqan, I,45; tazama Subhi es-Salih, Hadis İlimleri, s.261-262; Karaman, Hadis Usulü, uk.9-10.
6- al-Anfal, 7.
7- at-Tahrim, 3.
8- Ni muhimu kwa suala letu kwamba imeelezwa mwanzoni mwa hadithi kuwa kutaibuka watu watakaosema tutakubali kile kilichomo ndani ya Quran lakini tutakataa kisichokuwemo na kuwa sunnah zimetolewa. Tazama Abu Dawud, Sunnah, 6.
9- Hadithi zote zinazoitwa qudsi (takatifu) au za kiungu zimeeleza kwa kusifiwa Allah. Ipo mitazamo fulani ambayo maneno yote mawili na maana zake ni za Allah au maana ni za Allah na maneno ni ya Mtume kama hadithi nyengine. Tazama Al-Hadith, wa’l-Muhaddithun, s.18; Qawaidu’t-Tahdith, uk.64 pamoja na wengine.
10- Tazama, Bukhari, Eeman, 37; Muslim, Eeman, 1; Abu Dawud, Sunnah, 16; Tirmidhi, Eeman,4.
11- Muslim, Jannah, 63-64; Tazama, Aydınlı, Sünnetin Kaynağı, p.50-51; Toksarı, Sünnet, uk.98-99; Abu Dawud, Adab, 48.
12- Muslim, Eeman, 32-36; See, al-Munawi, Fayzu’l-Qadir, VI, 289-290.
13- Kwa mfano/Kwa mifano, tazama, Muslim, Janaiz, 1; Tirmidhi, Eeman, 18; Jihad, 32.
14- Ingawa baadhi ya watafiti wanadai kuwa kwa kuwa hadithi ambazo neno ufunuo limetajwa zinasimuliwa kwa upande wa maana, haziwezi kukubalika kuwa ni ushahidi kwamba hadithi kwa ujumla ni ufunuo (Erul, Bünyamin, İslamiyat, C.1, s.1, uk.55 pamoja na wengine), katika makala nyengine mtu huyo huyo anasema kuwa haiwezekani kusema kuwa Allah hawasiliani na Bwana Mtume isipokuwa kwa Quran. Pia anasema Mjumbe wa Allah ameteuliwa kwa jukumu la tabligh (kufikisha ujumbe), kufundisha na kufafanua. Hata hivyo, pia anasema kuwa itakuwa vyema kuiita ni hekima. (Erul, Bünyamin, İslamiyat, V.III, uk.1., uk.184.
15- Muslim, Hayd, 34.
16- Bukhari, Nikah, 108.
17- Tazama yanayohusika, Suyuti, Miftah, 29; Musnad, II, 85,160; Bukhari, Adab, 28; Muslim, 1,140; Abu Dawud, Manasik, 24,27; Tirmidhi, Hajj, 14; Abu Dawud, Salat, 2; Bukhari, Badu’l-Khalk, 6; Abu Dawud, Sunnah, 9; Musnad, I, 191; Ibn Hisham, Sira, III, 101-102.
18- Suyuti, Miftah, 29.
19- Abdulghani Abdulkhaliq, Hujja, 337; Inasemwa kuwa ipo ijma (makubaliano ya wanazuoni) kwamba sunnah zinategemea ufunuo. Tazama, ibid, uk.338; Inaripotiwa kuwa Hasan b. Atiyya amesema sunnah inategemea ufunuo kama Quran. Darimi, Muqaddima, 49.
20- Imam Shafii, anayesema wahy matluw ni Quran na wahy ghayr matluw ni sunnah, anaeleza kuwa sunnah ni ‘hekima’ iliyotajwa katika Quran. (ar-Risala, 3-4,10; al-Umm, V, 127,128.)
21- Ibn Hazim, al-Ihkam, 93; cf. Kırbaşoğlu, Sünnet, uk.260-261.
22- Ghazali, Mustasfa, I, 83; kwamba Kattabi ana maoni hay ohayo/hayo hayo, tazama Khattabi, Maalimu’s-Sunan, V, 10.
23- Çakan, İ.Lütfi, Hadislerde Görülen İhtilaflar ve Çözüm Yolları, Ist, 1982, uk.96.
24- Hadithi inayoeleza mwanamke na mama yake mdogo au shangazi yake hawezi kuolewa na mwanamme huyo huyo kwa wakati mmoja ni kama hiyo/hivyo. Bukhari, Nikah, 27; Muslim, Nikah, 37-38.
25- Anaeleza tukio lifuatalo kuwa ni mfano: kuvaa nguo za hariri ni haramu kwa wanaume lakini Bwana Mtume alimwachia Abdurrahman b. Awf avae nguo za hariri kutokana na ugonjwa wake. Tazama, Bukhari, Jihad, 91; Libas, 29; Muslim, Libas, 24-26.
26- Ibn Qutayba, Abu Muh. Abdullah, Ta’wilu Mukhtalifi’l-Hadith, Beirut, 1972, uk.196 pamoja na wengine.
27- ibara/Ibara kama roho mtakatifu/roho takatifu imepulizwa kifuani mwangu ni ufunuo wa aina hiyo. Ibn Majah, Tijarah, 2; Bayhaqi, Sunan, VII, 76; Suyuti, Miftah, 30.
28- Sarakhsi, Shamsuddin, Usulu’s-Sarakhsi, Beirut, 1973, II, 90-96.
29- Shatibi, Muwafaqat, IV, 19; Kwa ajili ya Mitazamo hiyo hiyo, tazama, Abdulghani, Hujja, uk.334 pamoja na wengine.
30- Tazama, Aydınlı, Istılah, 148; Pia Tazama, Bukhari, I’tisam, 24.
31- Ismah, moja ya sifa za mitume, inamaanisha kuwa mbali na ukafiri, kutokumjua Allah, kusema uongo, kufanya makosa, uovu, kutelekeza, kutokujua undani wa Shariah. Pia inamaanisha kwa kutowezekana/kushindikana kuendelea kufanya makosa. Tazama, Ghazali, Mustasfa, II, 212-214; Sabuni, Maturidiyye Akâidi, trns Bekir Topaloğlu, Ank. 1979, s.212-212; Yazır, Hak Dini, IX, 6357; Abdulghani, Hujja, 108 pamoja na wengine/pamoja na wengine.
32- Sarakhsi, Usul, II, 68.
33- Sabuni, Maturidiyya, 121; Abdulghani, Hujja, uk.222; Kwa mtazamo wa Ibn Taymiyya kwamba mitume hawatoachwa waendele kufanya makosa, tazama Abduljalil Eesa, Ijtihadu’r-Rasul, Misri, nd. uk.33.
34- Kwamba Allah alimhifadhi (s.a.w.) kutokana na uchafu wa Jahiliyya, tazama Ibn Sa’d, Tabaqat, I, 121; Abu Nuaym, Dalail, I, 129; Bayhaqi, Dalaîl, I, 313.
35- Abu Nuaym, Dalail, I, 147; Pia tazama, Bukhari, I, 96; Muslim, I, 268; Bayhaqi, Dalail, I, 313-314.
36- Tazama. Tabari, Tarikh, II, 196; Abu Nuaym, Dklail, I, 143; Bayhaqi, Dalail, I, 315; Mara, wakamchukua (s.a.w.) kwa nguvu kwenda kwenye burudani, lakini akatoweka; Kisha, akasema; mtu mwenye-ngozi-nyeupe, mrefu amenambia/aliniambia; ‘Ewe Muhammad! Usiliguse sanamu hilo. Rudi!’” Cf Musnad, II, 68-69; Köksal, İslam Tarihi, II,117-121.
37- Kwa maelezo zaidi, tazama Sarakhsi, Usul, II, 91; Ghazali, Mustasfa, II,214; Sabuni, Maturidiyya, s.121; Abdülghani, Hujja, 221-222; Abduljalil Eesa, İjtihad, uk.31-33; Çakan, İhtilaflar, uk.96,113; Erdoğan, Sünnet, 192 pamoja na wengine/pamoja na wengine.
38- Qiyamah, 16-17.
39- Tazama yanayohusika al-Ghashiya, 21-22; Hud, 12; al-Kahf, 23; al,-Qasas, 56; Yunus, 99; ash-Shuara, 3.
40- at-Tawba, 113.
41- Tirmidhi, Tafsir, sura 3/12; Aal-e-Imran, 128; Abduljalil Eesa, Ijtihad, uk.95.
42- Viungo vya Bwana Hamza kama sikio lake na pua vimekatwa na ini lake limenyofolewa. Ibn Hisham, Sira, III, 101-103. Kwa ajili ya aya tazama an-Nahl, 126-127.
43- al-Anfal, 67-68. Tazama Abdülghani, Hujja, 185.
44- at-Tawba, 88, 84; Tazama Ibn Kathir, Tafsir, II, 378; Abduljalil Eesa, uk.105.
45- at-Tahrim, 1-2.
46- Tazama Abduljalil Eesa, Ijtihad, s.59-66.
47- Tazama, Sarakhsi, II, 90-91; Tahanawi, Muh. Ali b. Ali, Kashshafu Istilahati’l-Funun, Ist, 1984, II, 1523.
8
Ni yapi malengo ya vita ambavyo Mtume Muhammad (S.A.W.) amepigana?
Ni ukweli unaojulikana kuwa sababu nyingi za vita hivi zinaweza kutajwa. Kwa mujibu wa tathmini yetu, vita vya mtume Muhammad (S.A.W.) vilitokana na sababu zifuatazo na hekima:
1. Ili kumfanya adui ahisi kwamba wanazo nguvu za kutosha za kupigana.
Baadhi ya vita vya mtume (S.A.W.), hususani vya sariyya ambavyo vilitokea kabla ya Vita vya Badr, vimelenga kuwaonesha washirikina na Wayahudi wa Madinah waliokuwa na uhasama dhidi ya Uisilamu na wafwasi wake, na washirikina wa Makkah waliokuwa wakisubiri fursa ya kuwashumbulia Waisilamu kuwa Waisilamu ni imara na kuweka eneo la uhuru kwa ajili ya kufikisha ujumbe wa Uisilamu na kuwalinda Waislamu dhidi ya mashambulizi. 1
Vita hivi vya sariyya ni mapambano yaliyofanyika ili kuonesha kuwepo kwa Waisilamu na nguvu yao na matokeo ya kuvivuka vizuizi katika njia ya tabligh. Utawala wa nguvu za kikatili wa wakati huo katika eneo hilo, kwa kumwona mwenye nguvu ndiye mwenye haki na kuwanyima wanyonge haki ya kuishi ulisababisha Mtume Muhammad (S.A.W.) kutuma makundi ya maaskari ili kuhakikisha usalama wa eneo hilo. Vita vya sariyya vya Saif al-Bahr na Rabigh pamoja na Abwa, Buwat, Hamraul Asad na Badr ndogo vimeendeshwa kwa lengo hilo. 2
2. Kuzuia vyanzo vya kifedha vya mashambulizi.
Baadhi ya vita vya mtume (S.A.W.) vilipiganwa kwa lengo la kudhibiti njia za biashara ya washirikina wa Makkah na kuwadhoofisha kiuchumi kwa kuwa walianza kuliandaa jeshi ili kupigana na Mtume Muhammad (S.A.W.) na Waisilamu kwa kutumia bidhaa za Waisilamu walizolazimika kuziacha walipohama kutoka Makkah na kushikiliwa na washirikina hapo baadaye. Maisha ya kipekee ya washirikina wa Makkah yalikuwa ni biashara. Walinzi wa misafara waliokuwa na silaha waliopelekwa Damaskas walilazimika kufuatiliwa karibu na Madina ili wasiwadhuru Waisilamu. Kwa sababu hii, Mtume Muhammad (S.A.W.) aliandaa vita hivyo vilivyotajwa vya ghazwa na sariyya ili kuifuatilia misafara ya washirikina. 3
Kwa hakika, Vita vya Badr vilipiganwa kwa lengo la kuepusha maandalizi ya vita ambavyo wangeanzisha Makuraishi kwa manufaa waliyoyapata kutokana na misafara ya kibiahara. Vita vya Uhud viliandaliwa kwa pato lililotokana na msafara wa biashara ya Damaskas ya Abu Sufyan ili kulipiza kisasi kwa Mtume Muhammad (S.A.W.). 4
Vita vya sariyya vya Saiful-Bahr, Rabigh, Harar, Nahla, Qarda na Is, vilivyokuwa dhidi ya washirikina wa Makkah, ambao daima walikuwa wakiwatishia Waisilamu, vilikuwa ni nguvu fanisi dhidi ya nguvu kubwa-kubwa katika kujiandaa kwa ajili ya vita kama vile kufuatilia misafara ya kibiashara na kukata vyanzo vya kifedha. 5
3. Kujilinda dhidi ya mashambulizi.
Wakati mapigano yote ya Mtume Muhammad (S.A.W.) yalikuwa na sifa ya kijilinda kwa upande wa sababu zake na malengo yake makuu, idadi ya mapigano ya kujilinda kwa upande wa mikakati ni ndogo. Baadhi ya vita vya Mtume Muhammad (S.A.W.) vilitokea kutokana na mashambulizi ya adui ili kuwaondoa Waisilamu na mshikamano wao wa kikanda. Katika mazingira hayo, Mtume Muhammad (S.A.W.) alitumia haki yake ya kisheria ya kujilinda. Kwa kuwa Quran imeruhusu kupigana ili kujilinda panapo shambulizi 6 na imesisitizwa kuwa mapigano yanapaswa yapiganwe kwa kutegemea sababu halali za kisheria. 7
Kipindi cha mapambano kati ya vita vya Badr na Khandaq ni majaribio ya kujilinda dhidi ya washirikina wa Makka na Wayahudi wa Madina. 8 Umuhimu wa hatua za lazima za kujiinda hususani kwa Wayahdui/Wayahudi, ambao waliishi nao pamoja, unaweza kuonekana katika kipindi cha baadaye. Kwa hakika, kutokana na uhaini uliofanywa na kabila la Quraydha, Waisilamu wamepitia vipindi vya hatari wakati wa mapigano walipolazimika kuilinda Madina dhidi ya vikosi vyenye nguvu vya Ahzab, vilivyoundwa na washirikina wa Makkah na Wayahudi wa Khaybar. 9 Katika kipindi cha Madina, Mtume Muhammad (S.A.W.) alilazimishwa kupambana na sifa za kiadui za Wayahudi dhidi ya Waisilamu na alilazimika kuwa tayari dhidi ya mashambulizi yanayoweza kutokea. 10 Kwa sababu hii, mapigano ya Badr, Uhud na Khandaq yalikuwa ni mapigano makubwa ya kujilinda kwa upande wa kisheria na mkakati ambao umelenga kujilinda dhidi ya mashambulizi.
4. Ukusanyaji wa taarifa kuhusu adui.
Baadhi ya ghazwa na sariyya ya Mtume Muhammad (S.A.W.) zilitokea ili kukusanya taarifa dhidi ya maadui waliokuwa wakivizia fursa ya kushambulia wakati wowote ule. Waisilamu walilazimika kuwa makini muda wote dhidi ya maadui wa namna zote, hususani washirikina. Kwa sababu hizi, baada ya kuhakikisha usalama wa Madina, Mtume Muhammad (S.A.W.) alilenga kuwa na hadhari zaidi dhidi ya washirikina wa Makkah kwa kuweka mikataba na makabila jirani. Vita vya mwanzo vya sariyya viliendeshwa kwa lengo la kukusanya taarifa kuhusu adui, kupeleleza kiintelijensia na kudhibiti mazingira yao ya kisiasa na kiuchumi. 11
Doria na makachero walipelekwa kabla ya vita ili kupata taarifa. Kuwa na taarifa kuhusu hali halisi ya adui kupitia mapambano ya doria, inteligensia na njia nyengine kulikuwa na umuhimu mkubwa mno wa usalama wa Waisilamu. Kwa ajili hiyo, Waisilamu ambao walisumbuka kwa kuwa na nguvu yenye mipaka dhidi ya adui mpaka pale ushindi wa Makka ulipolazimishwa kupokea taarifa kuhusu nguvu ya ya adui ya mapigano iliyojumuisha mbinu zao za kupigana, pahala na kwenye mazingira yapi wangefanya hivyo. 12 vita vya sariyya vya Nahla, Dhu’l Qassa ya mwanzo, Wadi’l Qura’, Jinab ya pili, Hunayn, Abdullah ibn Rawaha na vita vya sariyya vya Khaybar vilitokea ili kuwa na taarifa kuhusu adui ambae angevurumisha mashambulizi ya kushtukiza.
5. Uvunjaji wa mikataba na kuwaadhibu wahaini
Uvunjaji wa mikataba unajenga uhalifu kwa mahusiano ya kimataifa. Kuvunja vipengele vya mikataba kwa upande wowote ule ilikuwa ndio sababu ya baadhi ya mapigano katika kipindi cha Mtume Muhammad (S.A.W.). Uvunjaji wa katiba ya Madina (hati ya Madina) pamoja na uvunjaji wa mkataba wa Hudaybiyyah, mikataba ambayo imefungwa na Mtume Muhammad (S.A.W.) baada ya Kuhama kumepelekea sababu kuu ya baadhi ya mapigano.
Mtume wa Allah (S.A.W.) mara zote alitimiza mikataba mbali mbali kikamilifu. Mfano bora kabisa wa hili ni huu hapa: Kwa mjibu wa ibara ya mkataba wa Hudaybiyyah, “Mtu anaposilimu akiwa Makka na akataka apate hifadhi Madina, madai yake hayo hayatokubaliwa na atarejeshwa kwao Makka.” Baada ya hatua ya utilianaji saini, Abu Jandal, aliyekuwa mwana wa ujumbe wa Makka, alimjia Mtume Muhammad (S.A.W) akiburura minyororo yake na kudai hifadhi kutoka kwake. Wakati Suhayl ibn Amr, aliyetia saini mkataba kwa niaba ya watu wa Makkah, alikataa dai lake kulitetea wazo kwamba makubaliano yalishapitishwa, Abu Jandal alilia sana, “Enyi Waisilamu! Mtanirejesha tena kwa hawa Makuraishi wanaotaka kunifanya niikane dini?” Huku haya yanatokea Mtume (S.A.W.) akasema, “Ewe Abu Jandal, kuwa na subira! Tarajia malipo yako kutoka kwa Allah. Allah atakauonesha wewe na mfano wako mlango. Tumeshaweka mkataba na Makuraish. Hii ni ahadi ya pande mbili kwa ajili ya Allah na hatuwezi kuivunja. 13
Tukio hili la kusikitisha ni mfano muhimu mno wa uaminifu wa Mtume (S.A.W.) kwa ibara za mkataba.
Kipindi cha mapigano ambayo yalianza baada ya Kuhama kilimalizika kwa mkataba wa Hudaybiyyah; hata hivyo, mkataba huu ulivunjwa na Makuraish. Kwa sababu hii, Mtume Muhammad (S.A.W.) alisonga mbele kuelekea Makka ili kuwafunza nidhamu. 14 Kama ilivyo kwa mapigano yaliyoendeshwa na washirikina, mapigano ya Mtume Muhammad (S.A.W.) yaliyoendeshwa dhidi ya makabila ya Kiyahudi yaliyopo Madina yaliendeshwa kwa masuala ya kisheria kama vile kuvunja kanuni za mkataba na kuungana na maadui dhidi ya masharti ya mkataba.
6. Kuadhibu Mavamizi na Uporaji
Uporaji wa wanyama waliotegemea malisho ya kiangazi waliomilikiwa na Mtume (S.A.W.) na Waisilamu na wengine kufa shahidi kwa wakati huo huo kulizusha kisingizio cha baadhi ya mapigano ya sariyya. Ni wajibu kupambana na watu waliozoea kuwashambulia Waisilamu kwa sababu tu ya imani zao pamoja na makabila yaliyoandaa mashambulizi haya. Ulinzi alioumarisha mtu ili kulinda mali yake na maisha yake katika shambulizi la uvamizi na uporaji linazingatiwa kuwa ni kujilinda. Upotevu wa mali na uhai wakati wa kujilinda hauhitaji adhabu yoyote kwa upande wa sheria za Kiisilamu. Mapigano ya vita vya sariyya ya Harar, Dhu’l Qassa ya pili, Tarif, wana wa Fazara, Ukl, Uranis na Mayfaa pamoja na mapigano ya ghazwa ya wana wa Quraydha, Safawan / Badr ya kwanza, Sawiq na Dumatu’l Jandal yametokea kutokana na uporaji wa mali za Waisilamu na Mtume (S.A.W.) na mashahidi wa baadhi ya Waisilamu wakati wa jaribio la uporaji huu na matukio mbalimbali yakiwemo mashambulizo hayo hayo.
7. Kumzuia Adui asiungwe mkono
Mtume Muhammad (S.A.W.) alikuwa na sifa ya amani na alikuwa muwazi kwenye makubaliano katika kila hatua ya maisha yake. Alifunga mikataba pamoja na makabila yenye dini tofauti-tofauti yaliyoishi Madina katika mazingira alipofurushwa kutoka ardhi ya kwao na kulazimishwa kuhama lakini hakuachwa katika amani hata huko Madina. Katika muundo huu, baadhi ya makubaliano yalifungwa pamoja na baadhi ya makabila kabla ya adui aliyekuwepo katika njia ya biashara ya Makuraish ili kuwazuia wasiungane na adui na kuunda jukwaa la amani. 17 Mapigano ya ghazwa ya Abwa na Dhu’l-Ushayra yalitokea ili kuyayakinisha makubaliano ya amani. Mapambano ya Mtume wa Allah (S.A.W.) yanapaswa yazingatiwe kuwa ni juhudi za kumaliza migogoro kwa amani wakati wa zama za Madina, ambapo bado hakukuwa na vita vilivyopamba moto.
8. Uingiliaji kati wa Kijeshi uliofanywa pindi zilipopokelewa habari za shambulizi.
Sehemu muhimu ya vita vya ghazwa na sariyya vya Mtume Muhammad (S.A.W.) vilitokea kutokana na kupokea habari za shambulizi wakati mwingine kutoka kwa kabila moja na wakati mwingine mjumuiko wa makabila yaliyojipanga dhidi ya Mtume na Waisilamu kwa sababu tu ya imani yao. Sio kwamba mrejesho baada ya kupokea habari za njama ya kushambuliwa ungemaanisha kusalimu amri mbele ya adui. Mtume Muhammad (S.A.W.) alihama ili kuepuka pigo la kwanza ya shambulizi ambalo kwa hakika lilipangwa na adui. Wakati shambulizi la adui ndio sababu ya kisheria kwa ajili ya vita, mrejesho wake unazingatiwa kuwa ni sababu ya kisheria dhidi ya maandalizi ya mashambulizi hayo yaliyopokelewa na inteligensia. 18 Vita vifuatavyo vya ghazwa na misafara ya kijeshi ya Tabuk vilitokea kutokana na kupokea taarifa za njama za adui kutaka kushambulia; Dhul-Qassa ya kwanza, Qarqaratu’l- Kudr, Bahran, Dumatu’l Jandal, Muraysi, Wadi’l-Qura, Turaba, Najid / Hawazins, Mayfaa, Jinab, Dhatu’s-Thalathil, wana wa Bakr, Abdullah ibn Rawaha, Khaybar, Ghaba, mapigano ya sariyya ya Qutba ibn Amir pamoja na Ghatafan, Qatan, Dhatu’r-Riqa, Hunayn, Taif, Khaybar na mapigano ya vita vya ghazwa ya Fadak. Vita vingi vya ghazwa na sariyya itapozingatiwa, itaonekanwa kwamba vimetokea kutokana na kupokea habari ya shambulio.
9. Kuwasaidia Waisilamu wanaoteswa.
Viko vita vilivyokuwa na lengo la kukomesha shinikizo kwenye uhuru wa dini na imani lililowekwa na makabila fulani na dola kadhaa zilizowadhulumu na kuwatesa Waisilamu. Makabila na dola kadhaa zilizojawa na hisia za chuki dhidi ya Waisilamu walionesha chuki zao kila walipopata fursa. Chuki hii ilikuwa ikioneshwa kwa mtindo wa dhuluma na kuwatesa Waisilamu walioishi dola jengine wakiwa ni wachache.
Mwisilamu mmoja mmoja na jumuia kadhaa zilizodhulumiwa na walionyimwa uhuru wa kutekeleza imani na ibada ya dini yao wanabebeshwa jukumu kama hawatojaribu kukomesha dhuluma hii. 19
Na kwa nini basi isilazimike kupigana kwa ajili ya Allah na kwa wale, waliokuwa wanyonge, wanaotendewa vibaya (na kudhulumiwa)? – wanaume, wanawake, na watoto, ambao kilio chao ni: “Mola Mlezi wetu! Tutoe katika mji huu ambao watu wake ni madhalimu, na tujaalie tuwe na mlinzi anaye toka kwako, na tujaalie tuwe na wa kutunusuru anayetoka kwako.” 20
Aya ya hapo juu inaweza kutumiwa kuwa ni msingi kwa ajili ya kupigana kwa ajili ya kuwasaidia watu wanaodhulumiwa. Ukweli kuwa Mtume (s.a.w.) alilisaidia kabila la Khuzaa baada ya ombi lao la kutaka msaada katika kipindi cha Amani ya Hudaybiyya 21 unaweza kutafsiriwa kuwa ni kutimiza amri ya aya hii. 22 Mapigano ya sariyya ya Bi’r al-Mauna na mapigano ya ghazwa ya Dumatul-Jandal yalikuwa ni uingiliaji wa kijeshi wa Mtume (s.a.w.) uliotokea ili kuwasaidia Waisilamu walioweko matesoni.
10. Kutokomeza vikwazo vinavyozuia tabligh (kufikisha ujumbe wa Uisilamu)
Kwa kuwa tabligh ni jukumu la msingi la Mtume (s.a.w.), lengo kuu ni kumtambulisha Allah duniani kote kwa njia ya amani. Jukumu la tabligh halikupuuzwa hata katika mazingira ya wakati ambapo adui aliwalazimisha Waisilamu kupigana. 23 Kama ulivyo umuhimu wa jukumu hili, Mtume (s.a.w.) alituma wajumbe wa tabligh kwa makabila na dola kadhaa kandokando ya Madinah. Wakati sababu iliyo nyuma ya mapigano ya ghazwa na sariyya yaliyodaiwa kutokea kutokana na tabligh yakichunguzwa, itaonekanwa kuwa yametokea kwa sababu ya wajumbe hao walilazimika kujihami walipokuwa wakishambuliwa. Kwa maneno mengine, vita vilitokea kwa sababu wanaolinganiwa hawakuukubali Uisilamu bali kwa kuwa waliwashambulia Waisilamu. Kwa hivyo, Mtume (s.a.w.) alipigana ili kutokomeza vikwazo vilivyozuia tabligh na sio kuwafanya watu kuukubali Uisilamu kwa mabavu.
Miongoni mwa mapigano ya sariyya ambayo Mjumbe wa Allah (s.a.w.) ameyapeleka kwa kusudi la kulingania Uisilamu ni Dhat al-Atlah chini ya uongozi wa Ka’b b. Umayr 24, Dhat ath-Thalathil yaliyoongozwa na Amr b. As 25, Dumatul-Jandal yaliyoongozwa na Abdurrahman b. Awf, Jazima yaliyoongozwa na Khalid b. Walid 26. Mapigano ya sariyya yaliyoongozwa na Ibn Abi’l Awja kwenda kwa Wana wa Sulaym kuwalingania Uisilamu lakini walisema, “Hatutaki wito wenu.” Kisha, waliwashambulia Waisilamu kwa kufyatua mishale yao na Waisilamu wote kufa mashahidi isipokuwa Ibn Abi’l Awja. 27
Wakati mwengine Mtume (s.a.w.) alituma wajumbe kwa baadhi ya makabila na madola wakati alipoombwa na wakati mwingine alipeleka wajumbe kwa kusudi la kufikisha ujumbe wa Uisilamu bila ya kuombwa kufanya hivyo. Baadhi ya wajumbe hawa ambao hawakuwa na lengo lolote isipokuwa ni kufikisha ujumbe wa Uisilamu walishambuliwa kwa kushtukiziwa na kufanyiwa uhaini; walikufa mashahidi. Mapigano ya sariyya yafuatayo yalishambuliwa na Waisilamu walioshiriki humo walikufa mashahidi: mapigano ya sariya ya Raji’, Bi’r al-Mauna, Wana wa Sulaym, Dhat al-Atlah, Dhat ath-Thalathil, Wana wa Jazima, Uman, Bahrayn na Dumatul-Jandal.
Yapo makabila yaliyodai wajumbe wa tabligh wakieleza kuwa wameshakuwa Waisilamu na kuahidi kuwa watawalinda wajumbe hao; hata hivyo, waliwashambulia kwa kuwashtukiza na wajumbe hao kufa mashahidi; mashambulizi haya yalisababisha kuzuka baadhi ya mapigano ya sariyya na ghazwa. Wajumbe ambao hawakuwa na jukumu jingine isipokuwa ni kuwajulisha watu kuhusu dini iliyoleta wokovu kwa utu walishambuliwa kihaini na kushtukiziwa. Mtume (s.a.w.) alipambana dhidi ya watu hao walioushambulia Uisilamu ili kuulinda Uisilamu. Mapigano ya ghazwa ya Dhat ar-Riqa na mapigano ya sariyya ya Jamum, Mayfaa, Wana wa Amir, Sayf al-Bahr ya Pili na Khaybar yalizushwa ili kuzuia mashambulizi dhidi ya wajumbe wa amani.
11. Kuwaadhibu wale waliowatendea vibaya na kuwaua mabalozi
Mjumbe wa Allah alituma mabalozi kwa watawala wa nchi kadhaa katika ukanda husika baada ya Mkataba wa Hudaybiyya kwa kusudi la kuwalingania Uisilamu. Miongoni mwa watawala hao walijibu wito huo kwa vizuri; hata hivyo, wengine waliujibu kwa namna hasi/vibaya na kuwatusi mabalozi na Mtume (s.a.w.). 28
Baadhi ya mabalozi hawa waliotumwa kwa viongozi na watawala wa makabila na nchi mbalimbali ili kutimiza wajibu wa tabligh walitukanwa, kuuliwa au kushambuliwa. Hata hivyo, mabalozi na wajumbe walikuwa na dhamana ya uhai katika sheria ya kimataifa. 29 Kuwatusi, kuwashambulia na kuwauwa mabalozi waliokuwa na dhamana ya uhai ulikuwa ni uhalifu mkubwa mno. Mapigano ya sariyya ya Himsa, Wana wa Qurayt na Qurata na vikosi vya Muta yaliendeshwa kwa sababu hii.
12. Kujibu tangazo la vita lililotolewa na adui
Azimio la vita lililofanywa na adui ni moja ya sababu za Mtume (s.a.w.) kupigana. Kutokulijibu kabila au dola linaloendesha vita dhidi yako kutachochea uadui na kuwafanya wakushambulie kwa nguvu zaidi na kishupavu; kwa hivyo, ni lazima kujibu tangazo la vita lililotolewa na adui. Katika hali hiyo, kulijibu tangazo la vita kunazingatiwa ni kujilinda kwa sababu adui huyo anaonesha kuwa anakusudia khasa pindi anapotangaza vita. Wakati Mtume (s.a.w.) alipokalibiwa na azma hiyo na hatari ya kushambuliwa, alijibu tangazo hilo la vita. Mfano pekee wa vita vya namna hii ni mapigano ya Ghazwa ya Badr ndogo.
Wakati Mtume aliposhindwa na washirikina wa Makkah kwa namna fulani wakati wa Mapigano ya Uhud, alikubali pendekezo la Abu Sufyan, aliyempa changamoto iliyoegemea kwenye ufahari wa ushindi, kupigana tena karibu na viunga vya Badr mwaka uliofuata. 30 Kama ulivyo umuhimu wa kujibu azimio na kitisho cha vita kwa Makuraish, Mtume aliandaa jeshi na kwenda kwenye vikosi 31; hata hivyo, alipokwenda huko, hakukuwa na mtu. Abu Sufyan, aliyeketi nje ya Makkah na jeshi la watu elfu mbili, aliamua kurudi kabla ya kufika Badr kutokana na udhuru wa njaa. 32 Imefahamika wazi kuwa kikosi hiki kilitekeleza jukumu kutokana na tangazo la vita la Abu Sufyan.
Hitimisho
Inafahamika kutokana na somo hili, ambapo sababu za Mtume (s.a.w.) zimechunguzwa, kwamba mapigano yake na vita viliegemea kwenye sababu tofauti-tofauti. Kwa mujibu wa hayo, vita vyote vimeegemea kwenye sababu za kisheria; kwa hivyo, inaweza kuhitimishwa kuwa hakuna mapigano, vita au uingiliaji kati wa Mtume (s.a.w.) ambao si wa haki. Ikiwa sababu zote zitazingatiwa, itaonekana wazi kuwa Mtume (s.a.w.) hakushambulia kabila lolote au dola lolote kinyume na haki.
Ikiwa kanuni za Uisilamu, zinazotegemea Quran na Sunna, zimezingatiwa, itaonekanwa kuwa mahusiano kati ya mtu mmoja mmoja na dola mbalimbali yanategemea kanuni ya amani. Vita ni wajibu usiotakikana kuwa ni kitu cha mpito; vinaweza kutokea kuwa ni mapambano kwa ajili ya kuwa hai.
Kuvielezea kwa njia inayohusiana na leo hii, itaonekana kuwa sababu za vita vya Mtume (s.a.w.) ni za kisheria kama zimechunguzwa chini ya vigezo vinavyotumiwa kubainisha uhalali wa vita hapo kale na sasa.
Tanbihi
1. Khattab, Mahmud Shit, Komutan Peygamber Hz. Peygamber’in Askerî Dehası, kimefasiriwa na Ağırakça, Ahmed, İst., 1988, uk. 56.
2. Kwa maelezo zaidi kuhusu mapigano ya ghazwa na sariyya, tazama Nargül, Veysel, Kur’an ve Hz. Peygamber’in Uygulamaları Işığında Cihad, (Tasnifu Isiyochapishwa ya shahada ya Udaktari), Erzurum, 2005, uk. 111-217.
3. Ibn Hisham, Abu Muhammad Abdulmalik b. Hisham, as-Siratu’n-Nabawiyya, kilichochapishwa pamoja na uhakiki wa Mustafa Saka na marafiki, by., nd., II, 241-242, 245; Muslim, Sayd 17.
4. Ibn Sa’d, Muhammad, at-Tabaqatu’l-Kubra, Beirut, 1985, II, 37; Samhudi, Nuruddin Ali b. Ahmad, wafau’l-Wafa, Beirut, nd., I, 281. Pia tazama Ibnu’l-Athir, Abu’l-Hasan Ali b. Muhammad, al-Kamil fi’t-Tarikh, Beirut, 1965, II, 113, 116; Bukhari, Manaqib, 251, Maghazi, 2.
5. Tazama Hamidullah, Muhammad, İslam Peygamberi, kilichofasiriwa na Salih Tuğ, Ankara, 2003, II, 1036-1037.
6. al-Hajj, 22/38; al-Baqara, 2/190; ash-Shura, 42/41.
7. al-Baqara, 2/194.
8. Khattab, Komutan Peygamber, uk. 13.
9. Waqidi, Muhammad b. Umar, Kitabu’l-Maghazi, Chuo Kikuu cha Oxford, 1966, II, 459-460; Ibn Qayyim, Abu Abdillah Muhammad b. Abi Bakr, Zadu’l-Maad fi Hady-i Khayri’l-Ibad, Cairo, nd., III, 129-130.
10. al-Baqara, 2/91; Aal-i Imran, 3/183; Qasas, 28/48-50.
11. Ibn Hisham, I-II, 601, ff.; Hamidullah, İslam Peygamberi, I, 139.
12. Tazama Balazuri, Abu’l-Abbas Ahmad b. Yahya b. Jabir, Ansabu’l-Ashraf, Beirut, 1996, I, 383-384; Kattani, Abdulhay, at-Taratibu’l-Idariyya, Beirut, nd., I, 363.
13. Ibn Hisham, III-IV, 318; Bayhaqi, Ahmad b. Ali b. Husayn, as-Sunanu’l-Kubra, Hyderabad, 1344, Sunan, IX, 219-220.
14. Ibn Qayyim, Zadu’l-Maad, III, 290, 394.
15. Tazama Ibn Hisham, I-II, 501-504.
16. Ibn Sa’d, II, 28-29, 57-59, 74-78; Ibnu’l-Athir, II, 137-139; Suhayli, Abdurrahman b. Abdillah b. Ahmad, ar-Rawdu’l-Unf fi Tafsiri’s-Sirati’n-Nabawiyya li Ibn Hisham, Kairo, nd., II, 296; Samhudi, I, 277-278, 298.
17. al-Anfal, 8/58; at-Tawba, 9/12-13; Güner, Osman, Resûlullah’ın Ehl-i Kitap’la Münasebetleri, Ankara, 1997, p. 299.
18. al-Anfal, 8/58; at-Tawba, 9/12-13; Aal-i Imran, 3/146-147, 200.
19. al-Hajj, 22/39-40.
20. an-Nisa, 4/75.
21. Abu Yusuf, Yaqub b. Ibrahim, Kitabu’l-Haraj, Cairo, 1396, p. 230; Balazuri, Futuhu’l-Buldan, kimechapishwa pamoja na uhakiki wa Abdullah Anis at-Tabbaa’, Beirut, 1987, uk. 41.
22. Yaman, Ahmet, İslam Devletler Hukukunda Savaş, İstanbul, 1998, uk. 86-87.
23. Darimi, Siyar, 8.
24. Ibn Sa’d, II, 127-128.
25. Ibnu’l-Athir, II, 232.
26. Ibn Hisham, IV, 280-281.
27. Ibn Sa’d, II, 123.
28. Ibn Kathir, Ibn Kathir, Imaduddin Abu’l-Fida Ismail, al-Bidaya wa’n-Nihaya, Beirut, 1966, IV, 268 ff.
29. Shaybani, Muhammad b. Hasan, Sharhu Siyari’l-Kabir, (pamoja na ufafanuzi wa Sarakhsi), Beirut, 1997, II, 72; Turnagil, Ahmet Reşid, İslamiyet ve Milletler Hukuku, İstanbul, 1972, uk. 92-96.
30. Ibn Hisham, III, 100; Balazuri, Ansab, I, 417.
31. Tabari, Abu Jafar Muhammad b. Jarir, Tarikhu’t-Tabari Tarikhu’l-Umam wa’l-Muluk, Beirut, nd., III, 42; Ibn Hazm, Abu Muhammad Ali b. Ahmad, Jawamiu’s-Sira, kilichofasiriwa na M. Salih Arı, İstanbul, 2004, uk. 180-181.
32. Ibn Hisham, III, 220; Ibn Sa’d, II, 59-60.
Dk. Veysel Nargül
9
Ni ipi Shule Wake Safi wa Mtume (Azwaj at-Tahirat)?
Kipindi cha Madina kilikuwa ni kipindi ambapo hukumu za Kiisilamu na maamrisho yalikuwa yakiteremshwa kwa wingi na zikifundishwa kwa ummah na Mtume. Maswahaba wanaume wangeweza kumwona Mtume katika Msikiti wa an-Nabawi na kumwuliza maswali yao na matatizo. Wamejifunza kutoka kwake nini, kwa nini na vipi vya kufanya. Hata hivyo, haikuwa rahisi kwa wanawake. Wao pia walikuwa na maswali ya kuuliza. Kwa hivyo, wanawake walimwomba Mtume kutenga siku moja katika wiki kwa ajili yao nyumbani kwake. Mjumbe wa Allah akakubali pendekezo lao. Hivyo, wanawake wakaanza kwenda nyumbani kwa Mtume na kuuliza maswali yao kuhusu dini na kupokea majibu. Wakati wa mkutano huu, tukio la aina yake likatokea. Muda ambao, wanawake wameanza kuzungumza wao kwa wao kwa sauti kubwa. Walikuwa wakipiga soga. Wakati huo huo, Hazrat Umar aliyekuwa akipita alikerwa na wanawake kuzungumza kwa kelele mbele ya Mjumbe wa Allah na kugonga mlango. Alipofungua mlango, wanawake walimwona na kukatiza mazungumzo mara moja. Hazrat Umar alikerwa alipoona mandhari hiyo. Hakujizuia kuwaonya na kusema, “kinamama! Mnaniogopa mimi, lakini hamwogopi kuzungumza kwa kelele mbele ya uwepo wa Mjumbe wa Allah!” Hapo, wanawake walisema kwa utiifu, “Ewe Umar! Wewe una moyo-mgumu na mkali, lakini Mtume hayuko hivyo”
Hazrat Umar, aliyeitoa mali yake yote kwa ajili ya Mjumbe wa Allah, hakufurahishwa na hilo hakuwa kama Mtume. Mjumbe wa Allah akaligundua hilo na kusema,
“Ewe Umar! Kama utatembea njiani na shetani akakuona unakuja, anaweza kubadili njia yake” ili kumtuliza. Nyumba ya Mtume ilikuwa ni kama shule kwa wanawake. Hususani wake wa Mtume walikuwa ndio wanafunzi wa mara kwa mara na kwa namna fulani ni walimu wa shule hii. Profesa Raşit Küçük, wa Chuo Kikuu cha Marmara, Kitivo cha Theolojia, anafafanua suala hili kama ifuatavyo:
“Hukumu na maamrisho ya Uisilamu yanawahusu wote wanaume na wanawake. Hata hivyo, kuna baadhi ya hukumu na maarisho yanayowahusu wanaume tu au wanawake tu. Bwana Mtume hakupata ugumu wowote katika kufundisha hukumu na maamrisho ambayo yamewahusu wote wanaume na wanawake au wanaume watupu kwa sababu wanaume walikuwa ni jinsia moja na yeye. Alilazimika kuwahutubia wanawake kulingana na mafundisho na utekelezaji wa masuala ambayo yanawahusu wanawake na kujibu maswali yao. Wake za Mtume, waliokuwa katika umri tofauti tofauti na waliokuwa na vipaji tofauti, waliigiza kama ni walimu kwa ajili ya wanawake waumini. Mchakato wa kufundisha uliendelea na hata kuongezeka baada ya kifo cha Mtume.” (1993, İzmir, Ebedî Risalet Sempozyumu Tebliği)
Kwa hakika, shule ya Mjumbe wa Allah, iliyokuwa karibu na Msikiti wa an-Nabawi, ilikuwa na sehemu mbili. Moja ya hizo ilikuwa ni Shule ya Ashab as-Suffa, iliyowajumuisha Maswahaba wanaume, na sehemu nyengine ilikuwa ni Shule ya Wake Watakatifu, iliyowakusanya kinamama.
Kwa kweli, vyumba vya Wake Watakatifu vilikuwa kama shule na wakeze Mtume walikuwa namna zote mbili wanafunzi na walimu wa shule hiyo kwa sababu walijifunza hukumu na maamrisho ya Uisilamu moja kwa moja kutoka kwa Mjumbe wa Allah na kuyafundisha kwa ummah. Wajibu huu uliendelea baada ya kifo cha Mtume kama ulivyotajwa hapo juu. Mmoja ya wanafunzi wa kudumu na hodari zaidi wa Shule ya Ashab as-Suffa alikuwa ni Abu Hurayra, ambae alijitolea maisha yake kuhifadhi hadithi za Mtume na ambaye amepata dua ya Mtume kwa ajili ya kuimarisha uhifadhi wake ili kulibeba jukumu hili vyema; kwa upande mwengine, mwanafunzi hodari zaidi wa Shule ya Wake Watakatifu alikuwa ni Bibi Aisha, ambaye alikuwa na uwezo wa hali ya juu kama umahiri, uhifadhi na ufahamu na alikuwa ni mke wa kipekee wa Mtume. Kwa hakika, wa mwanzo katika “Mukthirun” (watu waliosimulia hadithi nyingi zaidi) alikuwa ni Abu Hurayra, aliyekuwa mwanafunzi hodari wa Shule ya Ashab as-Suffa ambaye amesimulia hadithi 5374; Bibi Aisha, aliyekuwa mwanafunzi hodari zaidi wa Shule ya Wake Watakatifu alikuwa ni mtu wa nne mingoni mwa Mukthirun; alisimulia hadithi 2210.
Ndio, Uisilamu umeleta hukumu na maamrisho yanayohusu ngazi zote za maisha pamoja na ngazi mbalimbali za umuhimu kuwa ndio dini ya mwisho na kamilifu. Upambanuzi, ufundishaji na utekelezaji wa hukumu na maamrisho hayo ulikuwa ni wajibu wa msingi na muhimu zaidi kwa Zama za Furaha Kamili kwa sababu mtindo na muundo ambao Allah angeuridhia, ambao ndio dini yenyewe, ulikuwa umechambuliwa katika kila kipindi na hatua ya maisha.
Tukiangalia vyanzo kadhaa ili tufahamu ukweli huu, tunaona hazina ya kuvutia ya hukumu, maamrisho na siri mbalimbali. Na wajibu wa kuwasilisha hazina hii kwa ummah unakuwa dhahiri kama ilivyo kwa lengo lisilo na dosari kwa ndoa hizo.
Tunaweza kusema kuwa kama tutawatoa kinamama hao hususani Bibi Aisha, ambaye ana nafasi maalumu kati yao, basi kiasi cha nusu ya maarisho na hukumu za dini ya Uisilamu zingetoweka!