FAQ katika kifungu cha Imani

1 Je, kuamini kupo katika uwezo wa mwanaadamu?

Ni Allah ndiye huwatunuku watu Imani. Hata hivyo, huwapa katika watumwa wake anayetaka. Mtumwa hutaka uongofu kutoka kwa Allah na Allah humpatia.

Kwa mujibu wa tafsiri ya Sa'd Taftazani, Imani ni Imani ni nuru ing’aayo inayotolewa na jua la milele (Allah mtukufu) na ni mwangaza kutoka katika neema isiyo na mwisho.” (Said Nursi, İşârâtü'l-İ'câz)

2 Je, utazielezea nguzo za Imani kwa ufupi?

Imani ina nguzo sita: Ambazo ni Imani juu ya Allah, Akhera, malaika, vitabu, Mitume, na kadari. Mtu anapaswa kuamini nguzo zote hizo sita ili awe muumini. Asiyeamini moja kati ya nguzo hizo hawezi kuwa muumini. Kwa sababu nguzo za Imani zimeungana.

1. Imani juu ya Allah:

Nguzo ya kwanza ya Imani ni Imani juu ya kuwepo na umoja wa Allah. Muislamu, kwanza, huamini kuwa Allah yupo na ni mmoja; ulimwengu huu ni kazi yake. Hana washirika wala kifani katika dhati, sifa wala matendo. Sifa zake hazifanani na sifa za viumbe.   

Viumbe vyote vinaonesha yote mawili kuwepo na umoja wa Allah.

Allah pekee ndiye wa tangu na wa milele, yupo huru na wakati pamoja na sehemu, yupo huru na mabadiliko, mahitaji, udhaifu na makosa.

Sifa za Allah zimekusanya kila kitu. Kila kitu kipo chini ya utashi wake. Ana majina mazuri kama ar-Rahman (mwingi wa rehema), ar-Rahim (Mwenye kurehmu), al-Ghafur (Mwenye kusamehe) na majina ya utukufu kama al-Qahhar (Mshindi), al-Jabbar (Jabari), al-Muntaqim (mwenye kulipa kisasi). Huwapa rehema wanaomwamini, na huwaghadhibikia wasiomwamini na kuasi.

Mtu anaweza kumwabudu Allah pekee. Neema za duniani na za ulimwengu mwingine zinaweza kupatikana kwa kutii maamrisho yake na makatazo yake. Hii ni sharia ya kiungu; haiwezi kubadilika.

Akili ya mwanaadamu haiwezi kufahamu dhati ya Allah, asili na ukweli. Kwakuwa akili ni kitu ambacho kiliumbwa baadaye na ina mpaka. Dhati na sifa za Allah mtukufu hazina mpaka. Ni dhahiri kuwa kilicho na mpaka hakiwezi kukizungukia kisicho na mpaka. Maana yake ni kuwa, Allah yupo tofauti na kitu chochote ambacho mtu anaweza kukifikiria.  

Allah hana washirika katika dhati yake na wala katika matendo yake. Yeye ndiye muumbaji pekee, mmiliki na mtawala wa ulimwengu wa kuwepo. Ni Allah ndiye aumbaye vyote viwili sababu na athari; Anaumba vyote viwili mti na tunda.

Shukrani, ibada na sifa njema ni zake pekee. Waumini humuabudu Allah pekee na kuomba msaada wake tu:

“Wewe tu tunakuabudu, na Wewe tu tunakuomba msaada” (al-Fatiha, 1/5)

Wanapofanya dhambi, hutubu moja kwa moja kwa Allah. Kwakuwa, hakuna ila Allah awezaye kusamehe dhambi ambayo mwanaadamu anaifanya dhidi ya Allah.

2. Imani juu ya Malaika:

Nguzo nyingine ya Imani ni Imani juu ya malaika. Kila muislamu anaamini kuwa Allah ana viumbe wazuri ambao ni malaika. Wanamtukuza Allah na hutekeleza majukumu mengine ambayo Allah amewapa. Viumbe hawa wasiyomuasi Allah, hawakuumbwa kwa kujaribiwa kama ilivyo kwa wanadamu. Asili yao ni safi; hawana hatia na daraja zao hazibadiliki.

Allah mtukufu ambaye huumba maelfu ya hisia kama akili, kumbukumbu, kujenga picha, upendo, hofu na udadisi hutimiza majukumu, hakuuacha ulimwengu huu mtupu bali ameujaza kwa kuwaweka malaika ndani yake.

3. Imani juu ya vitabu

Nguzo nyingine ya Imani ni Imani juu ya vitabu vya mbinguni. Hata kama mtu anajua kuwepo na umoja wa Allah kupitia akili yake, hawezi kufahamu maamrisho yake na makatazo yake ni yepi, namna gani atatimiza majukumu yake ya ibada, kwa ufupi kitu gani Allah ataridhika nacho. Kwa hivyo, Allah ametuma vitabu vya mbinguni. Vitabu mia moja kati ya vitabu vya mbinguni vililetwa katika muundo wa kurasa na vinne kati yao katika muundo wa vitabu. Vitabu hivi vinne ni Taurati (Agano la kale), Zaburi, Injili (Agano jipya) na Qur’an kwa mpangilio wa kihistoria.  

Muislamu analazimika kuviamini vyote. Hata hivyo, Qur’an ilivyoteremshwa, vitabu vingine vya mbinguni vimekoma kuwa na athari. Qur’an hadi kufikia leo haijapata mabadiliko ya aina yoyote hata herufi moja. Na kama hivi, Allah amebainisha sharia yake kama ifuatavyo:  “Hakika Sisi ndio tulio teremsha Ukumbusho huu, na hakika Sisi ndio tutakaoulinda.” (al-Hijr, 15/9)

4. Imani juu ya Mitume:

Nguzo nyingine ya Imani ni Imani juu ya mitume. Ni sharia ya kiungu kwamba Allah huwaonya watu kupitia mitume ambao ni wanaadamu.

Utume ni hitajio kubwa na ni neema kubwa kwa ubinaadamu. Allah amewaonesha watu njia za uongofu kupitia walimu hawa na viongozi hawa.

Jukumu la mitume ni kufikisha maamrisho wanayoyapokea kutoka kwa Allah kupitia wahyi na msukumo kwa watu na kuwaonesha njia za furaha duniani na akhera. Mitume hawa wana vipengele viwili. Moja wapo ni utumishi (ibada) na nyingine ni utume (Utume wa kiungu). Kwa upande wa utumwa, wanatii maamrisho ya Allah na makatazo kikamilifu; huwa mfano kwa watu kuhusu jambo hilo. Kwa upande wa utume, hufikisha ukweli kwa watu.

Mitume ni watumishi na viumbe vya Allah. Muislamu anapaswa awaamini wote. Kama atakanusha utume wa yeyote kati yao, basi anatoka katika Uislamu. Kwa mfano mtu asiyemwamini Hazrat Musa (Moses) au Hazrat Issa (Jesus) hawezi kuwa muumini. Imeelezwa kwa uhakika kabisa katika Qur’an kuwa wao ni mitume. Kuwaamini wao ni ulazima wa kuamini juu ya vitabu na mitume.

Mtume wa kwanza ni Hazrat Adam na wa mwisho ni Hazrat Muhammad. Taasisi ya utume imemalizikia kwa Hazrat Muhammad (s.a.w). Kwa hivyo, Hazrat Muhammad (s.a.w) anaitwa “Khatam al-Anbiya (Muhuri wa manabii)”.

Kama ilivyoelezwa katika aya ifuatayo, Hazrat Muhammad (s.a.w) alitumwa kama mtume kwa wanaadamu wote na sio kwa taifa maalumu: “Na hatukukutuma ila kwa watu wote, uwe mbashiri, na mwonyaji. Lakini watu wengi hawajui.” (Saba, 34/28)

Kama ilivyoelezwa katika aya ifuatayo, amekuwa daima ni neema na rehema kwa viumbe wote: “Nasi hatukukutuma ila uwe ni Rehema kwa walimwengu wote.” (al-Anbiya, 21/107)

5. Imani juu ya Akhera

Moja kati ya nguzo muhimu za Imani ni Imani juu ya ufufuo baada ya kifo na maisha katika ulimwengu wa baadaye. Allah mtukufu ambaye amewapa watu neema za kimaada na za kiroho katika maisha haya ya duniani, atawatunuku watumwa wake vipenzi, ambao wamefaulu majaribio ya duniani, neema zote mbili za kimaada na za kiroho peponi.

Allah ambaye hufufua mimea yote na wanyama ambao hufa katika majira ya kupukutika majira ya machipuko, bila ya shaka, atawafufua watu wanaokufa akhera. Jambo hili ni lazima kwa rehema na uadilifu wake.

6. Imani juu ya kadari:

Moja kati ya nguzo za Imani ni Imani juu ya kadari. Kadari ina sehemu mbili: Sehemu ya kwanza ni kuwa kila kiumbe, “dhati yake, muundo, na sifa” vimekadiriwa katika elimu ya Allah na akaumbwa kwa mujibu wake. Sehemu hii sio ya majaribio.

Sehemu ya pili inahusiana na sehemu ya utashi wa mwanaadamu. Allah huumba chochote akitakacho mtu na anafanya kwa utashi wake chochote kiwe kizuri au kibaya. Mtu huhusishwa na hii sehemu ya pili. Pepo na moto ni matunda ya haki ya kuchagua aliyopewa mtu.

3 Ni upi uhusiano wa tendo na kuabudu kwa Imani?

Tendo ni mtu kufanya anachokiamini, kutekeleza amri za dini na kuepuka kinachokatazwa na dini. Tendo lina uhusiano wa karibu na Imani. Mtu huchagua jambo kwanza, huamini kuwa ni la kweli na kisha kutenda lile analoamini kuwa ni la kweli. Hata hivyo, tendo si sehemu ya Imani. Hiyo ni kusema, mtu hazingatiwi kuwa ni kafiri au ameikanusha Imani yake kama hatekelezi amri za dini na hata kama hafanyi ibada. Anakuwa ni mwenye dhambi.

Hata hivyo, tendo na ibada huitia nguvu Imani moyoni, huongeza taathira yake, na kumfanya mtu akomae. Kama mtu hatekelezi mambo yanayohitajika katika dini yake, taathira chanya ya Imani kwa tabia ya mwanaadamu hupotea baada ya muda. Wakati taathira ya Imani kwa mtu inapopotea, hisia hasi, tabia mbaya, matamanio yenye madhara hutawala katika ulimwengu wa hisia wa mtu. Baadhi ya wakati, hali hiyo yaweza kumwongoza mtu kuelekea katika ukafiri, hiyo ni, kupoteza Imani yake.

Kila shari na dhambi, kila tendo ambalo linakinzana na amri ya dini hupenya moyoni, na huweka madoa na kuzima nuru ya Imani.

Mtume wetu aliashiria jambo hilo kwa maneno yake yafuatayo:

“Ndani ya moyo wa mwanaadamu atendaye dhambi, doa jeusi hutokea.”

Kila madhambi yanapo rudiwa rudiwa, weusi katika moyo huongezeka na nuru ya Imani hupotea hatua kwa hatua. Hali hiyo huendelea hadi moyo kuwa mweusi kikamilifu na kuwa mgumu na nuru ya Imani kupotea kikamilifu na kutoweka.

Kwa hivyo, sentensi ifuatayo imesemwa, “Kuna njia ya kuelekea kwenye ukafiri katika kila dhambi.”

4 Imani ni nini?

Imani maana yake ni kuamini, kuamini kwa moyo baadhi ya habari alizopewa mtu, kumkubali anayeleta habari hizo, kuamini jambo bila ya kusita.

Kama neno la Kiislamu, “Imani” maana yake kumwamini Allah, kwamba hakuna Mola ila Yeye, kwamba Hz. Muhammad (s.a.w) ni mtumishi na mtume wa Allah, kuamini malaika wa Allah, vitabu, siku ya hukumu, kadari, na kuwa zuri na baya limeumbwa na Allah. (Bukhari, Iman, 37; Muslim, Iman, 1, 5, 7; Abu Dawud, Sunnah, 15) Hiyo ni misingi ya imani.

Kwa mujibu wa tafsiri ya Sa'd Taftazani, “Imani ni nuru ing’aayo iliyo katika moyo wa mja amtakaye Allah baada ya huyu mja kutumia sehemu yake ya utashi.”

Kwa mujibu wa Badiuzzaman Said Nursi, Imani ni mwanga wenye kung’aa unaotolewa na jua la milele (Allah mtukufu) na ni nuru kutoka katika neema isiyo na mwisho.” (İşaratü'l-îcâz, p. 44.)

5 Nini faida ya kuamini? Kwanini mtu apaswe kuamini?

“Kuamini” maana yake ni kuridhika kikamilifu na ukweli wa kitu. Mtu anayeamini jambo lililothibitishwa na hoja thabiti hana mamlaka ya kuchagua kuamini au la. Kwa mfano, ni muhali kwa mtu kulipuuza jua alionalo katika siku isiyo na mawingu; Hawezi kusita kwa kujiuliza, “Napaswa kuamini au la?”. Basi kama hivyo, kusita kuamini juu ya ukweli uliyo wazi kama jua ambao pia huonekana kwa jicho la hoja ni ishara ya ujinga.

Imani ya Uislamu imejengwa katika kumuamini Allah na ahera. Kuamini hayo kikweli huwa na manufaa tu kwa kuamini kuwa mtume Muhammad ni mjumbe wa Allah na Qur’an ni maneno ya kweli ya Allah. Kwa mujibu wa hayo, rasilimali ya msingi ni Qur’an kwa sababu Qur’an ni yote mawili kitabu tuwezacho kukishika na kukiona kwa macho yetu na pia ni hazina ya miujiza ambayo kwayo tunaweza kutambua utambulisho wake wa kiungu na wa kimbinguni kwa jicho la hoja na moyo. Katika hali hiyo, kuamini juu ya Uislamu maana yake ni kuamini juu ya yale yanayosemwa na Qur’an.

- Mwanafunzi pale anapopuuza umuhimu wa kusoma na matokeo machungu ya kushindwa kufaulu, hutumia siku zake na marafiki zake katika mchezo na burudani.

Kupuuzia ukweli na kusahau hatua ya kuhesabiwa na adhabu ianzayo baada ya kifo huenda ikampa mtu raha ya muda mfupi katika dunia hii ya mpito. Raha hizo ni kama “asali yenye sumu”. 

Qur’an inatueleza yafuatayo mara nyingi katika mamia ya aya zake kwa uhakika na uwazi: Kama mtu anayeamini juu ya dini ya Uislamu atatenda kwa mujibu wa Imani yake, atakuwa na maisha ya milele peponi, ambao ni ulimwengu wa ahera, na hatokufa tena wala kuwa na huzuni yoyote. Kwa upande mwingine, ambaye haamini juu ya ukweli wa Uislamu ataingia motoni milele.

Je, inawezekana kwa mtu anayeamini kikweli kupuuzia mambo haya mawili ya kweli: ambayo ni, matokeo ya kuamini ni kuingia peponi na matokeo ya kutoamini ni adhabu ya milele na kusema, “Sijali; mambo haya hayanivutii; Ninafurahia maisha yangu; Sitaki kujisumbua kwa kufikiria vitu hivi”?

Je, si ajabu kwa mtu kuhofia kifungo cha siku mbili na kuona kuwa ni wajibu kuacha raha muhimu na furaha za roho yake pembeni, lakini kubaki bila ya hisia katika kukabiliana na kifungo cha motoni? Ambapo hoja zake hufanya iwezekane kwa mtu kufanya kazi kwa ajili ya maisha haya mafupi usiku na mchana na kukabiliana na changamoto lakini kushindwa kufanya kazi katika njia ambayo itampatia ulimwengu wa milele kama pepo?

Ni kanuni isiyobadilika ya asili ya mwanaadamu, kutathimini na kuona matukio kwa mujibu wa hukumu ambayo inatawala katika moyo na akili yake. Kwa mfano, mtu mwenye matumaini hutathmini na kutazama kila kitu kwa mtazamo wa matumaini na maisha yake huundwa kwa mujibu wa hili. Kwa upande mwingine, mwenye kukata tamaa hutazama kila kitu kwa mtazamo wa kukata tamaa na kutathmini maisha kwa mujibu wake. Glasi nyekundu hutufanya tuyaone mazingira mekundu; vivyo hivyo, glasi nyeusi pia hutufanya tuone mazingira meusi.

Kwa vile kafiri huuona ulimwengu kuwa hauna maana, mtupu na ni mchezo wa bahati, kila kitu huonekana kibaya na chenye maumivu kwake. Na kwa kuwa muumini anafahamu kuwa kila kitu kina maana, chenye faida, na kipo chini ya udhibiti wa uangalizi wa Allah na amri yake, kila kitu huonekana chenye kupendwa na chenye amani kwake.

Kama kusingekuwa na nuru ya Imani iliyoletwa na Hz Muhammad na Uislamu, ubinaadamu usingeweza kufahamu matukio yanayojiri ulimwenguni. Na kama hivyo, ubinaadamu ungelikuwa katika giza totoro na kukata tamaa.

Kwa mfano, mtu asiyekuwa na Imani ya ahera huona umauti ni kutokuwepo. Pia huliona kaburi kuwa ni shimo la kutokuwepo. Kwa upande mwingine, mtu mwenye nuru ya Imani huona umauti ni mwanzo wa ulimwengu wa milele na kaburi kuwa ni mlango wa furaha ya milele. Hauoni umauti kuwa ni chanzo chenye kutisha cha utengano bali ni njia ya kukutana tena na marafiki pamoja na jamaa.

Kafiri huona vitu vibaya na umasikini, ambavyo vipo ulimwenguni kote, kama makaburi ambapo kuna sauti za kilio na huzuni. Humuona kila kiumbe kuwa ni adui na mgeni. Jicho la moyo ambao umeangaziwa na nuru ya Imani huuona ulimwengu si kama makaburi yenye vilio na huzuni bali kama askari mwenye furaha wa kambi ya kijeshi ambaye amekamilisha majukumu yake na kurejea katika nchi yake. Huona kila kiumbe kuwa ni askari wa Allah na ni mtumishi rasmi na siyo mgeni au adui.

Licha ya hivyo, mwanaadamu ni tegemezi kiasili. Yaani, mwanaadamu ni kiumbe wa kijamii ambaye huwa na furaha kwa furaha ya wengine na huumia kwa mateso ya wengine. Wakati ambapo kila mmoja akiwa katika mateso ni muhali yeye kupata raha ya maisha.

Hata hivyo, mtu asiye na imani huona kila kitu hakina maana na ni vitu masikini visivyokuwa na uwepo; hivyo katika mtazamo wake, ulimwengu ni kama uwanja wa makaburi. Humuona kila mtu kama yatima anayelia. Ili kuwa na furaha katika hali ya kisaikolojia kama hiyo, ni lazima kunyamazisha akili na hisia kama mnyama au kuwa na moyo baridi ambao haujali maumivu ya watu waliomzunguka. Kwa vile yote mawili hayo hayawezekani, haiwezekani kufikia furaha ya kweli kupitia ukanushaji na kutokuwa na Imani.

Mtu anayesumbuliwa na mwangaza wenye kung’aa na rangi za jua na hatimaye kufumba macho yake, humsababishia hali hiyo usiku kwake yeye tu...

6 Ni upi uhalisia wa Imani?

Imani ni baraka kubwa na ni neema ya Allah kwa wanaadamu. Allah huwapa waja wake awatakao. Hata hivyo, haiwezi kudaiwa kuwa mja hana mchango wowote katika kuipata Imani.

Kinyume chake, mja anapaswa kutumia upendeleo na utashi wake kwanza na kuwa na nia ya kuamini na kuongoka. Allah atampa Imani na mwongozo kwa matakwa yake. Hivyo, baadhi ya wanachuoni wa Kiislamu na mawalii wameieleza Imani kuwa, “Ni nuru ambayo Allah mtukufu huiweka katika moyo wa mtu amtakaye baada ya huyo mtu kutumia sehemu yake ya utashi na upendeleo katika njia hiyo.”

7 Je, Imani ina faida kwa afya? Je, kuna tafiti zozote za kisayansi kuhusu hilo?

Imani hupelekea mwanaadamu kuyapenda maisha na humpa hisia za kushikamana na maisha. Mtu mwenye Imani huwa na mtazamo mzuri kuhusu maisha na uwepo; huona kuwa maisha ni neema ya Allah na huona mazingira yake ya kijamii na kiasili kuwa ni kazi za sanaa na yeye mwenyewe akiwa ni sehemu kati yake. Hivyo, huona kuwa ni jukumu lake kuendelea na maisha yake mpaka jukumu lake litakapo maliza na hupambana kuishi.  

Moja kati ya misingi muhimu ya kiroho ambayo inadhibiti maisha katika jamii ya Kiislamu ni Imani. Amri na makatazo ya Allah yanazingatiwa na waumini.

Kwa kuongezea, Imani humpa mtu hisia za juu za kuridhika na humwezesha kuanzisha uhusiano na vitu vya duniani. Hisia za kuridhika kwa mtu zilizosababishwa na Imani humfanya aridhike na vitu vidogo na kuwa na furaha pale mahitaji yake yanapokamilika hata kwa daraja ya chini au ya wastani. Na kama hivyo, humzuia mtu kutokana na kuanguka katika taabu na shida.

Kuna vitabu viwili vya msingi juu ya faida za imani kwa afya. Cha kwanza ni “Kitabu cha dini na afya”; ni kitabu chenye kurasa 712 kilichokusanya kazi zilizoteuliwa kutokana na tafiti ambazo zinatafuta uhusiano wa matendo ya dini na afya. Kingine ni “Mungu, Imani, na Afya”, kilichoandikwa na Dr. Jeff Levin, ambaye ni mmoja kati ya wataalamu wakubwa wanaosema kuwa makundi yenye Imani yapo katika hali nzuri kuliko mengine kiupande wa maradhi na kifo.  

Dr. Levin anatilia mkazo hilo katika utafiti wake: Wafuasi wa makundi ya kidini  ambao hujizuia na baadhi ya matendo na ambao huunga mkono maisha ya kiafya wana hatari ndogo ya kupata mshtuko wa moyo, shinikizo la damu na kansa. Wana maisha mazuri zaidi na marefu. Dini zinazozuia unywaji wa pombe na kuvuta sigara, zinazolazimisha milo midogo na zisizoruhusu kujamiiana nje ya ndoa zina fursa nzuri zaidi kuhusu jambo hilo. Faida hizi haziwezi kupatikana bila ya kuhudhuria sehemu za ibada na kutekeleza baadhi ya matendo ya kimwili kama ibada.

Dr. Levin anarudia kwamba maradhi ya aina tatu – moyo, kansa, shinikizo la damu – yajulikanayo kama ‘Wauaji wa Amerika ya kaskazini’ yanadhihiri kwa uchache kwa watu wa dini ukilinganisha na wasiyo na dini. Kwa mfano, anasema wanawake waliyoolewa na wanaume waliyotahiriwa ni wachache huugua kansa ya kizazi ukilinganisha na wengine. Vivyo hivyo, idadi ya wale wanaougua kansa ya kizazi kati ya Wahindus wasiyotahiriwa ni kubwa mno kuliko ya Waislamu wa kihindi, ambao takribani hawaugui maradhi haya.

Vivyo hivyo, waumini wenye subira, ambao si wenye haraka au fujo, wasiyokunywa pombe na ambao huenda sehemu za ibada mara kwa mara hufariki kwa shinikizo la damu kwa asilimia 40 chini ukilinganisha na wengine.

Hata hivyo, tunajua kuwa lengo kuu la Imani na ibada ni kuonesha uaminifu wetu kwa Mola wetu, aliyetuumba. Tafiti hizi zinatuonesha kwamba Mola wetu hatupi malipo yake hapa duniani kwa muundo wa hamasa na amani moyoni mwetu tu bali pia huboresha afya zetu.

Habari iliyotolewa na Associated Press mnamo tarehe 24 August 2007 ni yenye kuvutia. Shirika hilo la habari lilitangaza taathira chanya ya maadili ya kidini kwa vijana kwa kusema, ”Imani ni ufunguo wa furaha kwa watoto wengi.”

Kwa mujibu wa maelezo yaliyotolewa katika habari hiyo, matokeo ya utafiti huo yameonesha kuwa vijana wenye dini wana furaha zaidi kuliko wasiyo na dini. Utafiti wa kina uliyofanywa na Associated Press na MTV umeonesha kuwa kati ya vijana wenye umri kati ya 13 na 24, ambao hujitazama kuwa ni watu wa dini wana furaha zaidi kuliko wasiyo na dini. Asilimia 44 ya vijana wamesema kuwa dini na mambo ya kiroho ni muhimu kwao na asilimia 21 kati yao wamesema wameona kuwa dini ni muhimu. Kati ya jamii tofauti walioshiriki katika utafiti, Wamarekani wa Kiafrika wamesema dini ni kipengele muhimu kwao. Kati ya wale waliyosema dini ni muhimu sana kwenye maisha yao, asilimia 80 wamejieleza kuwa ni wenye furaha.

Wanasayansi ya jamii wanaelekeza umuhimu katika ukweli kuwa kuna uhusiano wa moja kwa moja baina ya furaha na kutekeleza wajibu wa kidini. Profesa wa sayansi ya jamii Lisa Pearce kutoka chuo cha South Carolina anasema, “Dini ina mchango mkubwa katika furaha”.

Amesema asilimia 68% ya vijana wamesema kuwa wametekeleza dini zao na imani zao kwa mujibu wa utafiti waliyoufanya. Asilimia 75 ya vijana waliyoshiriki katika utafiti huo wamesema Allah ana taathira katika furaha yao.

8 Je, unaweza kumtathmini mwanaadamu kupitia vioo vya Imani na ukanushaji kwa mujibu wa pande tofauti alizonazo?

Mwanaadamu ana ujamaa na viumbe vyote. Ana namna ya kubadilishana na kila kitu. Analazimika kukutana, kuongea na kuishi karibu na vitu vilivyomzunguka kimaada na kiroho kiasili yake. Kwa namna hiyo, mtu ana pande sita: kulia, kushoto, mbele, nyuma, juu na chini. Kwa kuvaa miwani ya Imani na ukafiri, mtu anaweza kuona viumbe na hali zao katika pande hizi sita.

Upande wa kulia: Upande huu una maana ya wakati uliyopita. Wakati uliyopita unapotazamwa kupitia miwani ya ukafiri, utaonekana kana kwamba ni uwanja wa makaburi. Mtazamo huu utampa mtu hofu kubwa na kukata tamaa.

Hata hivyo, upande huu unapotazamwa kupitia miwani ya Imani, huwaona watu waliotangulia wamehaulishwa kwenda katika ulimwengu bora na wenye nuru. Huona makaburi ni njia za chini kwa chini zilizochimbwa ili kufika katika ulimwengu wenye nuru. Hivyo, Imani humpa mtu furaha kubwa, raha na amani na humfanya aseme “Ahsante Allah”.

Upande wa kushoto: Upande wa kushoto, ambao ni wakati ujao unapotazamwa kwa miwani ya ukafiri utaonekana kama kaburi kubwa baya lenye giza ambalo litatufanya tuharibike na ambalo litatuangamiza kwa kuwafanya nyoka na nge kututafuna.

Hata hivyo, unapotazamwa kwa miwani ya Imani, utaonekana kama meza iliyojaa aina tofauti za vyakula vitamu na vizuri na vinywaji vilivyoandaliwa na Allah, mwenye huruma na ambaye anamuumba mtu kutokana na si kitu. Na itamfanya aseme “ahsante Allah” mara nyingi.

Upande wa juu: Mtu mwenye kuangalia mbinguni kupitia miwani ya ukafiri huona kuwa mamilioni ya nyota na sayari hutembea kwa haraka na kufanya harakati tofauti kama farasi mwenye kukimbia au ndege ya kivita katika anga isiyo na mwisho; kwa vile hafahamu kuna anayevidhibiti, anapata hofu na woga.

Hata hivyo, muumini anapoangalia mbinguni, anafahamu kwamba ndege hizi za ajabu zipo chini ya amri na udhibiti wa mwenye amri. Huona kwamba nyota ambazo hupamba dunia na mbinguni ni taa zinawaangazia wanaadamu. Kwa vile anafahamu kwamba utawala wake upo katika mikono ya Allah, huangalia kwa mapenzi matendo ambayo ni kama farasi wanaokimbia badala ya hofu na woga. Bila ya shaka haitoshi kusema “Ahsante Allah” mara elfu kwa baraka ya Imani yenye kueleza matendo ya anga.

Upande wa chini: Ni ardhi. Mtu anayeangalia dunia kupitia jicho la ukafiri huona dunia ni kama sanamu, mnyama asiyedhibitiwa pembeni mwa jua au jahazi bila ya nahodha na kupata hofu.

Hata hivyo, kama ataangalia kupitia Imani, huiona katika muundo wa meli chini ya amri ya Allah, na vyakula vyote, vinywaji, nguo na watu, yenye kusafiri pembeni mwa jua Na anaanza kusema “Ahsante Allah” mara nyingi kwa baraka kubwa iliyotokana na Imani.

Upande wa mbele: Kafiri anapoangalia upande huu, huona kwamba viumbe hai vyote, wawe wanaadamu au wanyama, wanakwenda upande huo kwa haraka kwa makundi na kupotea. Yaani wanasimama kuwepo. Kwa vile anajua kwamba ataenda huko pia, atakaribia kwenda kuwa mwendawazimu kwa huzuni.

Hata hivyo, kwa muumini anayetazama kupitia jicho la Imani, kutembea na kusafiri kwa watu upande huo siyo kwenda katika ulimwengu wa hakuna kitu bali ni kuhaulishwa kama kuhama kwa mabedui kutoka ardhi kwenda kwenye ardhi nyingine. Ni kuhama kutoka sehemu ya muda kwenda sehemu ya kudumu, kutoka katika shamba la huduma ya kazi kwenda katika ofisi ya malipo, kutoka katika ardhi ya shida kwenda katika ardhi ya neema. Kwa vile anafahamu kuwa kuhama huku si kwa ajili ya kwenda katika ulimwengu wa hakuna kitu, hukabiliana nao kwa furaha.

Hata hivyo, shida zionekanazo kama umauti na kaburi njiani ni matukio ya furaha baadaye kama matokeo. Njia ya kufika katika ulimwengu wa nuru hupita kaburini, na matukio makubwa ya furaha ni matokeo ya mabalaa mabaya. Kwa mfano, Hazrat Yusuf aliufikia ufalme wa Misri baada ya kutupwa katika kisima na ndugu zake na baada ya kuingia jela kama matokeo ya sakata la Zulekha.

Vivyo hivyo mtoto anayekuja duniani kupitia tumbo la mama yake hupata furaha ya kidunia kama matokeo ya shida na maumivu ayapatayo njiani.

Upande wa nyuma: Ikiwa wale wanaokuja nyuma watatazamwa kwa jicho la ukafiri, maswali kama “Wanaelekea wapi na wametokea wapi? Kwanini wamekuja duniani?” Hayawezi kujibiwa na kafiri hubaki katika adhabu ya kusita.

Hata hivyo, kama mtu atatazama kwa jicho la Imani, atafahamu kuwa watu hawa wametumwa na Allah kuona miujiza ya nguvu ya ajabu inayooneshwa katika maonesho ya ulimwenguni. Anafahamu kuwa watu hawa watafikia daraja kwa kufahamu maana ambazo Allah anazitaka zifahamike ulimwenguni kwa mujibu wa kiasi wanachofahamu na kurejea kwa Allah. Atasema “Ahsante Allah” kwa baraka ambazo Imani humfanya apate baraka hii ya ufahamu.

Pande hizi sita za mwanaadamu huangaziwa shukrani kwa Imani; wakati wote na sehemu zote hugeuzwa kuwa ulimwengu mkubwa na wenye raha. Ulimwengu wote takriban huwa kama nyumba yake anayoijua, si ngeni kwake na hujisikia amani ndani yake. Na kama hivyo, anakuwa kama mfalme wa ulimwengu shukrani kwa Imani.

9 Muumini ni nani? Ni zipi sifa za muumini?

Muumini ni mtu anayemwamini Allah, ahera  na misingi ya Imani. Kama mtu atasema yeye ni muislamu atazingatiwa kuwa ni muislamu.

Tunaweza kuorodhesha sifa kuu za muislamu ambazo Allah amezitaja katika Qur’an kama ifuatavyo:

Waumini humuamini Allah pekee. Hakuna dhati nyengine isipokuwa yeye wanayoiabudu akilini mwao. (al-Fatiha, 1/1-7; an-Nisa, 4/36)

Wanamuogopa Allah. Huepuka kufanya mambo ambayo yamekatazwa na Allah au yaliyo kinyume na radhi zake. (Aal-i Imran, 3/102; Yasin, 36/11; at-Taghabun, 64/15-16; az-Zumar, 39/23)

Wanamuamini Allah pekee. (al-Baqara, 2/249; at-Tawba, 9/25-26)

Hawamuogopi yeyote ila Allah. (al-Ahzab, 33/39)

Wanamshukuru Allah. Kwa hivyo, kuwa na matatizo ya kiuchumi au kuwa katika hali nzuri haiwafanyi wasikitike au kujivuna. (al-Baqara, 2/172; al-Isra, 17/3; Ibrahim, 14/7)

Wameamini kutokana na elimu ya hakika. Hawana mawazo ya kurudi bila ya kupata radhi za Allah. Wanaendelea kuhudumia dini yao kwa ari kila siku. (al-Hujurat, 49/15; al-Baqara, 2/4)

Wanashikamana na Qur’an. Hupangilia matendo yao yote kwa mujibu wa Qur’an. Ni wenye kuacha mara moja kufanya jambo pale wanapogundua ni lenye kukinzana na Qur;an. (al-Araf, 7/170; al-Maida, 5/49; al-Baqara, 2/121)

Wanamtaja Allah daima. Wanajua kuwa Allah huona na kusikia kila kitu; Ni wenye kuweka akilini mwao daima kuwa nguvu za Allah hazina ukomo. (Aal-i Imran, 3/191; ar-Rad, 13/28; an-Nur, 24/37; al-Araf, 7/205; al-Ankabut, 29/45)

Ni wenye kufahamu udhaifu wao mbele ya Allah. Ni wapole. Hata hivyo haina maana ya kuonekana dhaifu mbele ya watu wengine na kuwa wanyonge. (al-Baqara, 2/286; al-Araf, 7/188)

Ni wenye kufahamu kuwa kila kitu hutoka kwa Allah. Kwa hivyo, hawapatwi na fazaa wanapokutwa na jambo; huwa na subira na kuegemea kwa Allah. (at-Tawba, 9/51; at-Taghabun, 64/11; Yunus, 10/49; al-Hadid, 57/22)

 

Ni wenye kutazamia maisha ya ahera; wameamua kuwa ahera ndiyo lengo lao kuu. Hata hivyo, hufaidika na neema za duniani; Ni wenye kujaribu kutengeneza mazingira ambayo ni kama pepo hapa duniani. (an-Nisa, 4/74; Sad, 38/46; al-Araf, 7/31-32)

Ni wenye kuwafanya waumini peke yao kuwa ndiyo marafiki zao na wanaowaamini. (al-Maida, 5/55-56; al-Mujadala, 58/22)

Ni wenye akili. Daima wapo makini, kwa sababu wana ufahamu wa ibada zao. Daima huwahudumia waumini na dini kwa kutumia akili. (al-Mumin, 40/54; az-Zumar, 39/18)

Ni wenye kupambana kiakili kwa nguvu dhidi ya wakanushaji kwa ajili ya Allah. Hususan wakanushaji wakubwa. Huendelea na mapambano yao bila ya hofu wala uvivu. (al-Anfal, 8/39; al-Hajj, 22/78; al-Hujurat, 49/15; at-Tawba, 9/12)

Hawana woga wa kusema ukweli. Hawana hofu ya kuuweka wazi ukweli kwa kuhofia watu. Hawaogopi wakisemacho wakanushaji dhidi yao; hawapuuzi mashambulizi na dhihaka zao; Hawaogopi kukosolewa na wale wenye kuwalaumu. (al-Maida, 5/54, 67; al-Araf, 7/2)

Kufikisha dini ya Allah kwa watu. Ni wenye kuwaita watu katika dini ya Allah kwa kutumia njia tofauti. (Nuh, 71/5-9)

Si madhalimu. Ni wenye huruma na huathirika na shida za wengine. (an-Nahl, 16/125; at-Tawba, 9/128; Hud, 11/75)

Ni wenye kujizuia na hasira; ni wenye uvumilivu na kusamehe. (Aal-i Imran, 3/134; al-Araf, 7/199; ash-Shura, 42/40-43)

Ni waaminifu. Huonyesha utu wenye nguvu na husifika kwa kujiamini. (ad-Duhan, 44/17-18; at-Takwir, 81/19-21; al-Maida, 5/12; an-Nahl, 16/120)

Wanaumizwa na ukandamizaji na ukatili. (ash-Shuara, 26/49, 167; al-Ankabut, 29/24; Yasin, 36/18; Ibrahim, 14/6; an-Naml, 27/49, 56; Hud, 11/91)

Ni wenye kuvumilia shida. (al-Ankabut, 29/2-3; al-Baqara, 2/156, 214; Aal-i Imran, 3/142, 146, 195; al-Ahzab, 33/48; Muhammad, 47/31; al-Anam, 6/34)

Hawana hofu na dhulma pamoja na umauti. (at-Tawba, 9/111; Aal-i Imran, 3/156-158, 169-171, 173; ash-Shuara, 26/49-50; as-Saffat, 37/97-99; an-Nisa, 4/74)

Ni wenye kupambana na mashambulizi na vitimbi ya wakanushaji. (al-Baqara, 2/14, 212)

Wapo chini ya himaya ya Allah. Vitimbi vyote dhidi yao hushindwa. Allah huwafanya washindi kwa kuwahami dhidi ya uzushi wote na vitimbi. (Aal-i Imran, 3/110-111, 120; Ibrahim, 14/46; al-Anfal, 8/30; an-Nahl, 16/26; Yusuf, 12/34; al-Hajj, 22/38; al-Maida, 5/42, 105; an-Nisa, 4/141)

Ni wenye umakini mkubwa dhidi ya wakanushaji. (an-Nisa, 4/71, 102; Yusuf, 12/67)

Ni wenye kuwafanya maadui shetani na wafuasi wake. (Fatir, 35/6; az-Zukhruf, 43/62; al-Mumtahina, 60/1; an-Nisa, 4/101; al-Maida, 5/82)

Ni wenye kupambana na wanafiki; hawautumii muda wao pamaja nao. (at-Tawba, 9/83, 95, 123)

Ni wenye kujikinga na udhalimu wa wakanushaji. (al-Ahzab, 33/60-62; al-Hashr, 59/6; at-Tawba, 9/14-15, 52)

Ni wenye kufanya mambo yao kwa kushauriana. (ash-Shura, 42/38)

Hawana wivu au kuiga maisha ya kifahari ya makafiri. (al-Kahf, 18/28; at-Tawba, 9/55; Taha, 20/131)

Hawaathiriki na utajiri na cheo. (al-Hajj, 22/41; al-Qasas, 28/79-80; an-Nahl, 16/123)

Ni wenye uangalifu na umakini kuhusu ibada; wanatekeleza sala, funga na ibada kwa uangalifu. (al-Baqara, 2/238; al-Anfal, 8/3; al-Muminun, 23/1-2)

Hawafuati wingi bali vipimo vilivyowekwa na Allah. (al-Anam, 6/116)

Ni wenye kupambana kwa nguvu ili kufika kwa Allah na kuwa waumini wa kupigiwa mfano. (al-Maida, 5/35; Fatir, 35/32; al-Waqia, 56/10-14; al-Furqan, 25/74)

Si wenye kutenda kwa kuegemea ushawishi wa shetani. (al-Araf, 7/201; al-Hijr, 15/39-42; an-Nahl, 16/98-99)

Hawawafuati wazee wao kwa upofu. Wanatenda kwa mujibu wa Qur’an. (Ibrahim, 14/10; Hud, 11/62, 109)

Hawapotei kwa israfu. (al-Anam, 6/141; al-Furqan, 25/67)

Wanajihifadhi kutokana na zinaa na huoa kwa njia ambayo Mwenyezi Mungu anataka. (al-Muminun, 23/5-6; an-Nur, 24/3, 26, 30; al-Baqara, 2/221; al-Maida, 5/5; al-Mumtahina, 60/10)

Hawana kupita kiasi katika dini. (al-Baqara, 2/143; an-Nisa, 4/171)

Sio wabinafsi (al-Insan, 76/8; Aal-i Imran, 3/92, 134; at-Tawba, 9/92)

Wanatilia umuhimu usafi. (al-Baqara, 2/125, 168; Muddaththir, 74/1-5)

Hawachunguzani. (al-Hujurat, 49/12)

Wanaepuka uchoyo. (an-Nisa, 4/128)

Wanaomba msamaha kwa Allah. (al-Baqara, 2/286; Aal-i Imran, 3/16-17, 147, 193; al-Hashr, 59/10; Nuh, 71/28)

10 Vipi tunaweza kuimarisha Imani yetu?

Imani ni nuru, baraka kutoka kwa Allah. Hata hivyo, Imani ni elimu wakati huo huo, ambayo ni lazima isomwe. Kuna njia mbili za kuimarisha Imani yetu:

Njia ya kwanza na ya msingi ni kanuni za Sunnah na kuchunguza kwa mujibu wa Qur’an na Hadithi, kama inavyohitajika katika wakati wetu.

Njia ya pili ni kupanda daraja katika mambo ya kiroho kupitia kutekeleza matendo mema, kuutakasa moyo na roho kwa kuepuka dhambi.

Hata hivyo, hali ya karne hii inaifanya njia ya pili kuwa ngumu kuifuata. Kwa sababu hii, ni muhimu sana kusoma vitabu vinavyofunza Imani ya kuchunguza. Pia imekuwa muhimu kusoma sayansi kama sifa ya karne yetu, ukiachia mbali kusoma masomo ya dini. Hii ni kwa sababu nuru ya akili ni sayansi kama ilivyo nuru ya moyo ni masomo ya kidini. Tunaweza kusema kuwa moja kati ya vitabu  muhimu vyenye kufundisha yote mawili ni mkusanyiko wa Risale-i Nur. Kwa kuongezea, mtu anaweza kufaidika sana na vitabu vya watu maarufu kama imamu Al-Ghazali, Imamu Al-Rabbani, Imamu Mawardi na Imamu Qushairi.

Kuilinda na kuiimarisha Imani ni jambo muhimu zaidi kwa muislamu. Ni muhimu kuipa umuhimu Taqwa (Kumcha Allah) ili kuilinda Imani. Imani inaweza tu kulindwa ndani ya ngome ya Taqwa. Bila ya Taqwa, Imani hushuka. Ni muhimu kusoma na kufanya utafiti katika vitabu vinavyohusu Imani sana ili kuiimarisha Imani. Mambo ya Imani yanayotokana na elimu hayana taathira katika hisia za mtu labda yanapochujwa kupitia hoja. Kwanza, akili lazima iridhike.

Kutafakari ni muhimu sana. Ukweli wa mtume Ibrahim kumtambua Mola wake kwa kuangalia mwezi na nyota na kutafakari umeelezwa katika Qur’an. Imani huboreka kwa tafakuri. Kwa sababu hiyo, imeelezwa katika Qur’an kuwa

“Kutafakari kwa muda wa saa moja ni bora kuliko sala za sunna za mwaka mzima.”

Mazingira yana taathira kubwa kwa wanadamu. Dhambi hushauri watu ukafiri. Shauri lina taathira kubwa kwa wanaadamu. Linaingiza ukafiri ndani ya sehemu ya kutojitambua ya mtu bila ya watu kutambua. Kwa sababu hiyo, mtu anapaswa kuwa mbali na sehemu za dhambi kwa kadiri itakavyowezekana. Dhambi zinazotendwa bila ya mazingatio hushawishi watu kuwa hakuna akhera wala kuadhibiwa. Ili kulindwa na taathira hasi za mashauri kama hayo, mtu anapaswa kuwa mbali na sehemu za dhambi kadri awezavyo na kujaribu kuwashauri watu kuhusu wema na kuwakinga na shari kadri awezavyo. Mtu anapaswa kusoma mambo kuhusu Imani sana na kuwa makini na ujumbe unaotolewa ili kufidia uharibifu wa mashauri hasi aliyopewa. Ni muhimu kukutana na watu ambao wanajali kuhusu matendo mema na wanaishi kwa mujibu wa Taqwa. Katika hali kama hiyo, umuhimu wa jamii unadhihirika zaidi. Kama ilivyo dhambi kuwa inashauri hiana, matendo mema yanashauri Imani.

11 Imani imegawika sehemu ngapi?

Imani imegawika sehemu mbili:

  1. Imani ya jumla.
  2. Imani ya kuhakiki.

Imani ya jumla ina maana gani?

Ina maana kuamini kiujumla yote ambayo Mtume wetu ametufikishia kutoka kwa Allah.

Ikiwa mtu atasema:

“La ilaha illallah muhammadun rasulullah” kwa kutambua maana yake na kukubali, basi atakuwa ameamini kwa ujumla.

Sentensi hii inaitwa tawhid. Maana yake ni kama ifuatavyo:

La ilaha illallah: Hakuna Mola ila Allah.

Muhammadun rasulullah: Muhammad ni mjumbe wake.

Imani ya kuhakiki ina maana gani?

Ni kujua kwa kina na kwa ushahidi aliyotueleza mtume wetu kutoka kwa Allah. Kwa maana nyingine, ni kusoma na kukubali elimu ya lazima kuhusu dini kwa kina.

Ni elimu gani ya lazima ya dini ambayo inahitajika kusomwa?

Elimu ya lazima ya dini ambayo inahitajika kusomwa ni nguzo sita za Imani zilizokusanyika katika Amantu, ibada ya wajibu kama sala, funga, hija, zaka na matendo kama kuua mtu, kunywa kilevi, na zinaa, ambayo ni haramu katika dini.

Ni wajibu kwa kila muislamu kuyafahamu kwa kina na kuyaamini.

12 Je, kuzidi na kukuwa kwa Imani ni jambo lenye utata?

Mbegu huota na kukua sana hadi kufikia kuwa mti; Imani ni kama mti pia.

Wasomi wa Kiislamu wameigawa Imani katika hatua mbili kwanza:

1– Imani ya Taqlid (kuiga)

2– Imani ya Tahqiq (kuhakiki)

Imani ya kuiga: Ina maana ya kushikamana na misingi ya Imani kiada bila ya kuwa na hoja juu ya jambo hilo kama vile mtu kusikia kutoka kwa wazazi wake, walimu na mazingira. Kwa vile Imani ya kuiga ni aina ya kuamini ambayo haiegemei katika Imani kwa undani Zaidi juu ya misingi ya Imani na ufahamu wake, yaweza kupata na baadhi ya mashaka na udanganyifu na kupatwa na hatari ya kupotea na kuvunjika hasa katika zama hizi.

Imani ya kuhakiki: Ina maana kutambua mambo yote ya Imani kwa hoja na kwa undani zaidi, kuyakubali na kuamini bila ya kusita. Imani kama hiyo inaweza kujihami dhidi ya kupotea na kuvunjika inapokabiliwa na mashaka pamoja na udanganyifu.

Kuna ngazi kadhaa za Imani ya kuhakiki. Wasomi wa Kiislamu wamezigawa ngazi hizo katika makundi matatu:

1 - Uhakika katika kiwango cha elimu: Ina maana kufahamu na kuamini mambo ya Uislamu kielimu na kwa maelezo zaidi.

2 - Uhakika katika kiwango cha kushuhudia: Ina maana kufahamu na kuamini mambo ya Uislamu kana kwamba unayaona au kana kwamba unaangalia ukweli wake mwenyewe. Kuona kwa macho na kufahamu kielimu ni tofauti katika upande wa kumpa mtu fikra. Mtu anaweza kufahamu kitu kwa uhakika, bila ya kusita lakini anapokiona kwa macho, Imani yake huongezeka. Kwa mfano kufahamu uwepo wa Marekani na kuiona Marekani mwenyewe. Uhakika katika kiwango cha kushuhudia ni kuamini juu ya misingi ya Imani kama vile unaiona kwa macho.

3 - Uhakika halisi: Ina maana kukubali na kufahamu mambo yanayohusu Imani kwa kuingia ndani yake na kuyajaribu mwenyewe. Mfano unaofuata unaweza kuelezea ngazi tatu za Imani: Moshi unapoonekana sehemu fulani hujulikana kuwa kuna moto hapo, Kujua uwepo wa moto kwa kuona moshi ni uhakika katika kiwango cha elimu. Kwenda karibu na moto na kuja uwepo wa moto kwa kuuona ni uhakika katika kiwango cha kushuhudia. Kwenda karibu na moto na kuweka mkono wako katika moto na kuihisi sifa ya moto ya kuunguza na kujua uwepo wa moto kwa namna hiyo ni uhakika halisi.

13 Je, jeni zina taathira yoyote juu ya kuamini kwa mtu au kutoamini? Je, kadhia hii inaondoa jukumu la mtu?

Kuwa mwenye akili au la hakusababishi mtu kuamini au kukufuru. Ikiwa ni hivyo basi ingelikuwa dhulma. Hivyo, wale wenye akili sana wangeliamini na wasiyo na akili sana wangekufuru.

Kuwa na Imani au la kunaungana moja kwa moja na utashi wa mtu. Watu wenye akili, wawe na akili sana au kidogo. Wanabebeshwa jukumu. Wajibu unahusu kuwa na akili au la. Ni juu ya utashi wa mtu kuamini au la. Mtu hukubali au kukataa Imani kwa utashi wake.

Shetani aliasi japo alikuwa na akili sana na alimfahamu Allah. Uasi hautokani na uendawazimu wa shetani. Sababu ulizozitaja zinaweza kuathiri kuamini kwa mtu au la lakini sababu ya kweli ni utashi wa mtu. Hamna katika sababu hizo zenye kuathiri kuwajibika kwa mtu. Wendawazimu na wale wasiyopata ujumbe wa Uislamu hawa hawawajibiki.

Mfumo wa maumbile hauathiri katika utashi wa mwanaadamu asilimia mia moja. Unaweza tu kuwa moja ya sababu. Kama wajibu wa kujaribiwa, bila ya shaka kutakua na baadhi sababu zenye kuathiri katika Imani ya mtu. Hata hivyo, hakuna kati ya hizo itakayoweza kumuathiri asilimia mia moja. Kama mfumo wa maumbile ungelikuwa unaathiri asilimia mia moja, kila mtu angeliamini kama Hz. Adam (a.s). Mtoto wa Nabii Nuhu aliangamizwa katika gharika kabla ya kumuamini baba yake. Jambo linaloonesha kuwa mfumo wa maumbile hauna taathira katika imani. Mwanaadamu kiasili ana tabia ya kuamini au kutoamini. Hata hivyo, mambo mawili hayo yapo katika ngazi moja.

Kwa mujibu wa Badiuzzaman Said Nursi, “Imani ni mwanga wenye kung’aa unaotolewa na jua la milele (Allah mtukufu) na ni nuru kutoka katika neema isiyo na mwisho.” (Said Nursi, İşârâtü'l-İ'câz)

14 Kuna tofauti gani kati ya Imani na Ukafiri?

Neno Kufr (Ukafiri) pekee lina maana ya “kuziba”.  Katika istilahi ya kidini, maana yake ni kukataa alichokileta Hz. Mtume (s.a.w) kutoka kwa Allah na kukana moja au zaidi kati ya misingi ya kidini ambayo kwa hakika ameileta.

Iman (Imani) maana yake ni kumwamini Allah, kwamba hakuna Mola ila Yeye, kwamba Hz. Muhammad ni mja na mjumbe wa Allah, kuamini Malaika na vitabu vya Allah, kuamini akhera, kuamini kadari na kwamba kheri na shari vimeumbwa na Allah. (Bukhari, Iman, 37; Muslim, Iman, 1, 5, 7; Abu Dawud, Sunnah, 15)

Imani maana yake ni kukubali chochote alichokuja nacho mtume (s.a.w), na ukafiri maana yake ni kukana alichokileta. Kwa hivyo, kinacho tofautisha kati ya Imani na ukafiri ni kukubali kwa moyo. Hata hivyo, kukubali kwa moyo hakuwezi kufahamika na watu wengine; hivyo, kutamka Imani na kutimiza wajibu wa kidini unao onesha kile kilichotamkwa na ulimi, ambayo ni matendo, huzingatiwa kama ishara ya Imani moyoni.

Alama kuu ya kutofautisha Imani ni kukataa moja au misingi yote ya Imani au kuichukia, kuipuuza, au kutoiheshimu.

15 Jee, ni lazima kutamka Imani kwa ulimi?

Kutamka Imani kwa ulimi si wajibu wa Imani. Kama mtu hakueleza Imani yake kwa ulimi, atazingatiwa kuwa ni muumini kwa kukubali kwa moyo. Hata hivyo, vipi tutaweza kujua kuhusu Imani ya mtu moyoni mwake kama hataitangaza kwa ulimi wake?

Kwa hivyo, ni lazima kuitangaza Imani kwa ulimi ili Waislamu waweze kushuhudia Imani yake na kuushughulikia mwili wake mfu kama muislamu atakapofariki. Kwa hivyo, misingi miwili ya Imani inawekwa wazi kama hivi “Kukubali kwa moyo na kutamka kwa ulimi”

Hapa, kutamka kwa ulimi si msingi wa lazima lakini ni lazima kushuhudia Imani ya mtu na kumkubali kama muumini. Kusali kwa jamaa, kutekeleza wajibu wa kidini ni kama kutamka kwa ulimi; Kwa kweli ni vyenye nguvu zaidi kuliko kutamka. Mtume wetu ameyasema yafuatayo kuhusu jambo hilo:

“Shuhudia Imani ya mtu ahudhuriaye msikitini kwa sababu Allah anasema, “ Misikiti ya Allah itahifadhiwa na wale wenye kumwamini Allah na siku ya mwisho, wenye kusimamisha sala, na wenye kutoa zaka.” (at-Tawba, 18).

Haikatazwi na dini kukataa Imani au kutamka maneno kinyume na Imani katika hali ya kulazimishwa au kwa udhuru unaofanana na huo kwa ulimi na si kwa moyo kwa vile kutamka kwa ulimi si msingi muhimu wa Imani. Mtu anayelazimishwa kufanya hivyo hawi kafiri; anazingatiwa kuwa ni muumini kwa vile amehifadhi kukubali kwake kwa moyo.

Kwa hivyo, kipindi cha zama za furaha, swahaba wa mtume, Ammar Bin Yasir, hakuweza kuhimili dhulma na mateso, na akaikataa Imani yake kwa ulimi; hivyo akajinusuru na mateso aliyokuwa akiyapata.

Mtume wetu alikubali alichokifanya; mtume akasema kwamba kukataa Imani kwa ulimi katika hali ya dhulma na vurugu haiwezi kudhuru Imani ikiwa moyo utakuwa umejawa na Imani.

Imeelezwa katika Qur’an kuwa kukanusha kwa kulazimishwa hakumfanyi mtu kuwa kafiri. (an-Nahl 16/106)

16 Nini anapaswa kukifanya mtu anayetenda dhambi ili asipoteze Imani yake?

Anapaswa daima kukumbuka kuwa kutotekeleza wajibu ambao unalazimishwa na Imani yake ni kosa na ni dhambi na anapaswa ajisikie vibaya. Anapaswa aombe subira na msaada kutoka kwa Allah ili atekeleze amri za dini na kufanya yanayolazimishwa na Imani yake; anapaswa atubu na aape kutotenda dhambi tena.

Hapo tu ndiyo mtu ataweza kuihami Imani yake kutokana na taathira hasi za dhambi. Na kama hivyo, anaweza kuepuka hatari ya kupoteza Imani yake.

17 Imani ni kitu cha aina gani?

Imani ni kitu chenye kukusanya moyo na dhamira. Mtu anayeamini kwa moyo na kushikamana na misingi ya Imani huzingatiwa kuwa ni muumini. Kilicho muhimu katika Imani ni kukubali kwa moyo.

18 Imani humfanya mtu apate nini?

Mwanadamu hufika kilele cha juu kabisa kwa nuru ya Imani na kupata thamani ya kumfanya astahiki pepo. Hushuka chini kabisa ya vilivyo chini kwa giza la ukafiri na kufikia hali ya kustahiki moto. Imani ni mahusiano. Ni uhusiano unaomuunganisha mwanadamu na Allah. Kujenga uhusiano na Allah inawezekana tu kupitia Imani. Thamani ya kweli ya mtu inategemea uhusiano na ukaribu wake na Allah. Heshima na hadhi ya mtu huongezeka kwa mujibu wa ukaribu wake na Mfalme; vivyo hivyo thamani ya mtu huongezeka kwa mujibu wa ukaribu wake na Allah.

Katika ulimwengu huu, kama mtu ataungana na Allah, na kuwa chini ya hifadhi yake, hapo anaweza kuwa kiongozi wa Allah ardhini, afisa wake, mgeni wake au hata rafiki yake shukrani kwa Imani. Uhusiano huu wa urafiki na Allah unaweza kufahamika kwa nuru ya imani tu. Imani ni nuru ambayo mtu huona ukweli wa kila kitu shukrani kwa nuru hiyo. Huona sababu na maana zilizojificha za viumbe na kufahamu kwamba havikuumbwa bure.

Hisia nzuri zaidi kwa mwanaadamu ni upendo. Kama Imani isingekuwepo, upendo huu ungelimuweka mtu katika matatizo na hiyo ni kwa wingi wa sehemu zake. Kwa mfano mama ambaye mtoto wake mzuri na wa pekee anapofariki atahisi adhabu hii ya kiroho yote kama hatakuwa mwenye kuamini ahera.

Moja kati ya hisia muhimu za mwanadamu ni mapenzi. Mapenzi yaliyopata nuru ya Imani hufanya viumbe vyote kuwa ni marafiki wa mwanaadamu. Uhusiano wa mapenzi kisha huanzishwa kati ya mwanaadamu na mazingira yake. Hisia za kuwa pamoja na watu awapendao milele humfanya awe na furaha. Kwa mfano, mtoto anapokaribia kufariki na daktari kumpa baadhi ya dawa na hatimaye mtoto kupona, mama atakuwa na furaha sana na mwenye faraja.

Vivyo hivyo, mamilioni ya watu tuwapendao na ambao tunawajali kama mtoto huyo tunatenganishwa nao na umauti. Kama tutaliangalia jambo kwa nuru ya Imani, tutafahamu kwamba hawapotei moja kwa moja. Hivyo adhabu na huzuni hugeuka kuwa furaha isiyo na mpaka na faraja.

Kama mwanadamu atazuiwa kuamini, wasiwasi wa kutenganishwa na awapendao milele humpa adhabu kama moto. Kwa mfano kitu cha thamani zaidi kwa mwanaadamu ni akili yake. Kama akili itadondoka katika shirki na ukafiri, hupeleka maumivu na adhabu zinazokuja kutoka wakati uliopita na ambazo zimesababishwa na kupotea kwa milele kwa watu awapendao moyoni mwake. Kwa kuongezea, wasiwasi kuhusu kupotea kwake katika wakati ujao hubadilisha akili kuwa ni kifaa cha adhabu. Kwa hivyo, mtu mwenye dhambi kiujumla hujiingiza katika matumizi ya pombe au burudani ili aweze kukimbia adhabu ambazo hupewa na akili yake.

Kama akili itapata nuru ya Imani, mawazo ya kuwa pamoja na jamaa zake na marafiki zake peponi hutawala katika dunia yake. Humfanya apende maisha na viumbe. Upendo wake kwa mola wake, ambaye atakayefanya iwezekane kwake kuungana tena na awapendao na ambaye atampa yeye na wao furaha isiyo na mwisho, utaongezeka. Akili huwa akili hasa na hupata thamani yake halisi kwa nuru ya Imani.

Kama jicho la mwanadamu litapata nuru ya Imani, huona ulimwengu wote kama pepo iliyopambwa kwa maua. Huona kazi za sanaa, baraka na msaada wa Allah katika kila kiumbe akionacho. Hutazama kwa kutafakari na kupata masomo. Hufahamu ushahidi unaoonesha kuwepo na umoja wa Allah katika kila kitu na kujifunza ili aimarishe Imani yake. Ulimwengu unakuwa kama kitabu kikubwa machoni mwake. Huzisoma maana zilizojificha katika kitabu hiki cha ulimwengu.

Masikio yanapopata nuru ya Imani, husikia sauti za kiroho zinazokuja kutoka  ulimwenguni. Hufahamu kutukuzwa kwa Allah kunakofanywa katika lugha ya hali. Husikia nyimbo za upepo, vilio vya mawingu na sauti nzuri za mawimbi ya bahari shukrani kwa nuru ya Imani. Husikia maneno ya kiungu na kutukuzwa kwa Allah kutoka katika kila kiumbe kama sauti ya matone ya mvua, sauti za ndege na maongezi ya wadudu. Ulimwengu huwa kama mkusanyiko wa muziki wa kiungu. Roho na moyo wa mwanaadamu kama huyu vimejawa na ladha nzuri na raha.

Hata hivyo, masikio yanapozibwa na ukafiri, yanazuiwa kusikia sauti hizo tamu za kiroho. Sauti zenye kutoa raha hubadilishwa kuwa sauti za kilio. Maana nzuri na zenye hadhi katika moyo hubadilishwa kuwa huzuni. Sauti zinazokuja kutokana na hali ya kuwa mpweke milele zilizosababishwa na kushindwa kupata marafiki wa kweli hutawala dunia yake. Husikia sauti za huzuni na machungu zilizosababishwa na hali ya kuhisi kutokuwa na umiliki na kutolindwa. Hali hii humfanya aishi maisha ya adhabu sana.

Hivyo, Imani humfanya mtu apate furaha kubwa, baraka, ladha, raha na daraja ya heshima ambayo haiwezi kuelezeka. Fikra ya muumini kuhusu ulimwengu ni chanya. Huona kila kitu kizuri, ana fikra njema na hupata raha ya maisha. Huona viumbe vyote ulimwenguni kuwa ni marafiki zake na nduguze. Hana ugeni na kitu chochote. Kila kitu kina uhusiano na kingine kwa vifungo vya umoja kwa wingi wa majina ya Allah. Dunia ni kama sehemu ya undugu kwake.

Nuru ya Imani huangaza ulimwengu wa mwanaadamu na kuangazia ulimwenguni. Huokoa wakati uliopita na ujao kutoka katika giza. Humpa heshima mwanaadamu na huleta ukamilifu katika kiini cha ulimwengu. Huongeza thamani juu ya thamani yake. Viumbe vyote ulimwenguni hupata maana shukrani kwa Imani. Yanayojiri husimama kuwa ya bahati. Kila kitu kitaonekana kuwa huwepo kwa mpango na programu ya Allah.

Muumini huona athari ya kiini na sura ya rehema ya Allah ndani ya yote yaonekanayo kuwa upuuzi shukrani kwa fikra nzuri na chanya aliyoipata kupitia nuru ya Imani. Kwa mfano huangalia mambo mabaya kama maradhi kwa upande chanya. Hufikiri kuwa yatapelekea kusamehewa dhambi zake, huifunza roho yake, humfanya afanye matendo mazuri na kuzidisha daraja yake, na hatimaye kuifariji nafsi yake.

Kafiri huuangalia ulimwengu na yanayojiri kwa upande hasi na kwa mashaka. Ukafiri ni kama glasi nyeusi huonesha kila kitu kuwa ni kibaya na giza. Ukafiri huona viumbe kuwa ni matokeo ya bahati na bila ya sababu. Kwa fikra ya kafiri kila kitu ni upuuzi kisichokuwa na lengo. Viumbe vyote ni wageni na ni maadui wao kwa wao. Hudhani kuwa viumbe vyote huenda kwa kasi kwenye ulimwengu wa kutokuwepo. Hofu na wasiwasi wa kuwa yeye pia atadondokea katika giza la milele hufanya ulimwengu kuwa gereza kwake. Dunia yake imejawa na giza na shida. Roho yake imezungukwa na giza la hasadi, chuki, uasi badala ya nuru ya mapenzi na upendo. Mtu kama huyo anaishi maisha ya motoni kabla ya kuingia motoni.

19 Vipi muumini na kafiri huutazama ulimwengu?

Ulimwengu hutazamwa kupitia vioo viwili Kimoja ni kioo cha Imani na kingine ni kioo cha ukafiri.

Mtu anayeutazama ulimwengu kupitia vioo vya ukanushaji, ambavyo ni vioo vya ukafiri, ambavyo havikubali uwepo wa muumba huona kila kitu ulimwenguni kuwa ni bila ya mpango, bila ya mwenyewe, bila ya makusudio. Hajui na hawezi kufahamu kwa nini viumbe vimeumbwa na ni yepi majukumu yao ni kama mfano wa mtu aliyeachwa mlimani kwenye giza usiku ambaye chochote akionacho hudhani ni nyoka au dubwana na ambaye hafahamu majukumu ya viumbe hawa na wapoje.

Malengo na makusudio yake yote ni maisha ya kidunia. Hatambui maisha mingine yoyote zaidi ya maisha ya duniani. Kwa hivyo, anataka kutosheleza hisia zake zote katika dunia hii.

Hata hivyo, mwanaadamu amepewa hisia kwa mujibu wa ulimwengu wa ahera. Kila hisia ni kunjufu bila ya mpaka. Ni muhali kutosheleza hisia hizi hapa duniani. Kwa mfano, matakwa ya kuishi milele na matakwa ya kuwa na mali nyingi ni kunjufu bila ya mpaka. Hisia kama upendo na huruma hazina mpaka. Hatusemi “Napenda kiasi hiki cha watu. Hakuna nafasi ya kumpenda mtu mwingine moyoni mwangu.” Hata tukimpenda kila mtu, ukubwa wa hisia hii haujai.

Hata kama mtu anayeutazama ulimwengu kupitia vioo vya ukafiri ataona viumbe vingi kuwa ni vyenye maana, hekima na kusudio, hawezi kuvifahamu. Kwa vile kwa mtu kama huyo watu waliyotangulia wamekufa na kupotea. Watu watakaokuja pia watapotea na kuharibika. Kwa hivyo, hujiona baina ya makaburi mawili na kama kiumbe ambaye atakaye haribika na kupotea karibuni. Mtu kama huyo hawezi kupata raha wala ladha yeyote kutoka duniani kwa kuogopa kwake umauti ni kama mtu aliyehukumiwa kifo anasubiri kunyongwa. 

Mtu anayeuangalia ulimwengu kupitia vioo vya ukanushaji hutegemea akili yake na kupima kila kitu kwa akili yake kana kwamba akili yake imechaguliwa kuwa ni mhandisi wa ulimwengu; ana utajiri wa tajiri na umasikini wa masikini. Hupinga pale anaponyimwa nafasi nzuri zaidi na wepesi.

Katika Qur’an utajiri wa Karun umeelezwa, ambao utaangazia jambo hilo. Karun alikuwa tajiri kiasi cha kushindwa kubeba funguo za hazina yake mwenyewe. Watu waliuangalia utajiri wake na kusema, “Tunatamani tungelikuwa na utajiri kama huo.” Hata hivyo, Karun hatimizi wajibu wake wa kuwa tajiri na hatoi zaka, ambayo ni haki ya masikini, na halipi mishahara ya wafanya kazi wake kwa ukamilifu. Anadai kuwa ameupata utajiri wake kutokana na elimu yake.

Allah alipomfukia yeye na mali yake chini ya ardhi, watu waliyotaka kuwa kama yeye walisema, “Tunamshukuru Allah kwa kutotupa utajiri kama huo. Hatutaki kuwa katika nafasi ya Karun.”

Mtu anayeichukulia akili yake kuwa ni mhandisi wa kuamua muundo wa ulimwengu na ambaye ana uadui dhidi ya Allah kwa sababu hakupewa vitu fulani hapaswi kupuuza hadithi hizi zilizoelezwa katika Qur’an. Anapaswa kuwa na furaha na sio huzuni kwa sababu hakupewa vitu ambavyo majukumu yake asingeweza kuyatimiza. Kwa kuwa, Allah anatueleza kuwa kila mmoja ataulizwa kwa kila neema aliyonayo, hata maji anayokunywa mtu na hewa anayovuta.

Mtu anayeuangalia ulimwengu kupitia vioo vya Imani huona ulimwengu ni kama nyumba nzuri ya wageni na sehemu iliyopambwa kwa maua ambapo aina zote za neema na chakula hupatikana. Anahisi shukrani kubwa kwa Muumba wake, aliyembadilisha kutoka maumbile kwenda katika maumbile mingine kuanzia wakati ambapo alikuwa katika fuko la uzazi, aliyemuumba mwanaadamu na sio jiwe, mmea, au mnyama, aliyempatia vipawa kama akili, kufikiri, na kumbukumbu na aliyemkabidhi viumbe vyote vilivyo hai na visivyo na uhai ulimwenguni.

Anapoangalia wakati uliopita, anafahamu kuwa safari iliyoanza kwa baba zake Hz. Adam na Hz. Hawa (Eve) itaishia peponi, kwamba atakuwa pamoja na watu wote awapendao na jamaa huko milele na atakuwa mwenye kupewa aina zote za neema na Muumba wake kwa kuendelea. Anafahamu kwamba dunia si kituo kikuu bali ni chumba cha kusubiria na kituo cha mtihani njiani kuelekea ahera.

Anafahamu kwamba misiba kama maradhi na tetemeko la ardhi ni lazima ili kujaribiwa na hushukuru kwa kuonesha subira na kufikiri kuwa shida na matatizo anayokabiliana nayo hapa yatampa malipo kesho ahera.

Anapokabiliwa na matukio ambayo maana yake hasa hawezi kufahamu husema kama Ibarahim Haqqi anayesema,

“Allah huubadilisha ubaya kuwa uzuri, (Yaani, kuna kitu kizuri nyuma ya kila kitu tukionacho ni kibaya au shari. Allah hukifanya tukionacho kibaya kizuri kwa ajili yetu.)

Usifikirie Allah anafanya jambo jingine, (Yaani, kuna wema na uzuri katika kila kitu akiumbacho Allah. Akiumbacho si vingine ila ni kizuri.)

Mtu mwenye akili hukiangalia, (Mwenye akili, yaani, mtu mwenye elimu hukiangalia tu. Hajaribu kupinga vitu ambavyo sababu na maana zake hafahamu.)

Hebu tuangalie atakalolifanya Allah,

Lolote alifanyalo, hulifanya vyema.

Usiseme kwa nini lipo hivi,

Lipo kama linavyotakiwa liwe,

Kuwa na subira na tazama mpaka mwisho,

Hebu tuangalie atakalolifanya Allah,

Lolote alifanyalo, hulifanya vyema.

Hata kama akili yake haiwezi kuelewa, anajua kuwa Allah hufanya jambo katika njia iliyo bora zaidi.

20 Watu wamegawika sehemu ngapi kiupande wa Imani na ukafiri?

Wamegawika sehemu tatu:

1 - Waumini

2 - Makafiri

3 - Wanafiki

- Mtu anayeamini misingi muhimu ya dini ya Kiislamu ambayo ni wajibu kuiamini bila ya kusita na anazikubali huitwa muumini.

- Mtu asiyeamini moja kati ya misingi  ya Imani iliyojumuishwa katika Amantu na haamini lolote katika maamrisho au makatazo ya Allah huitwa kafiri.

- Mtu anayeonekana ameamini lakini anakanusha moyoni mwake huitwa mnafiki.

21 Ni ipi hali ya mtu asiyeukubali msingi mmoja tu kati ya misingi ya Imani?

Imani haiwezi kugawanywa” Hiyo ni kusema, nguzo (misingi) ya Imani huzingatiwa kuwa ni kitu kimoja; mtu asiyeamini moja kati ya misingi hiyo hutoka katika dini ya Kiislamu.

Vivyo hivyo, mtu asiyeamini yoyote kati ya nguzo sita za Imani hupoteza Imani yake. Anapaswa kutubu na kuamini tena.

22 Je, Imani ya kuiga ni yenye kutosha leo?

Kama tulivyoeleza hapo juu, leo, Imani ya kuiga inakabiliwa na udanganyifu mashaka mengi na yamedhihirishwa kwa ajili ya kupondwa na kuvurugwa. Ali Fuad Başgil anaeleza kwa nini Imani ya kuiga ilitosha zamani lakini haitoshi leo kama ifutavyo:

“Watu walihitaji nguvu ya dini na mambo ya kiroho katika kila kipindi. Hata hivyo, haja imekuwa ya wajibu leo. Katika wakati uliyopita, mababu zetu waliishi kwa raha kwa elimu ndogo ya dini na Imani ya kuiga katika mfumo wa mila kwa sababu mazingira yote yalikuwa ya kiroho. Leo hali imebadilika kabisa. Hisia za dini zimedhoofika; heshima ya mwanzo ya kidini imewekwa sehemu yake dharau ya kiburi. Familia zimesambaratika na mafungamano ya kifamilia yamedhoofika. Mzigo wa familia umewekwa katika mabega ya baba na mama; wao wameshindwa kuwa waangalifu wa masomo ya kidini kwa watoto wao kutokana na mahitaji ya kiuchumi. Kwa upande mwingine shule na vyuo vimekuwa vituo vya propaganda zenye kupambana na dini. Katika mazingira ambayo yamezibwa na dhihaka na ukaidi wa wakanaji wakaidi, elimu nyepesi ya dini haitoshi leo.

Maswali kama “Dini ni nini? Ni upi uhusiano wake na sayansi? Nini dini inapaswa kufanya mbele ya sayansi na inapaswa iwe na mtazamo wa aina gani kuhusu sayansi? Yamekuwa yakitawala akilini kwa muda mrefu. Na hususan vijana wasomi wanapaswa kujua majibu ya maswali hayo.” (Din ve Lâiklik: Religion and Laicism)

Bila ya shaka, elimu ya kidini na somo la Imani litolewalo leo linapaswa liwe na maudhui yenye kuchunguza ambayo yataifanya akili kukubali mambo ya Imani. Vinginevyo, somo jepesi la dini, na baadhi ya elimu kuhusu Imani katika mfumo wa kimila hautatosheleza kwa watu, na hususan vijana wa leo.