FAQ katika kifungu cha Mitume

1 Je Yesu (Mtume Isa) (a.s.) amekufa? Je utafafanua suala hili kwa mtazamo wa Kiisilamu?

Yesu hajafa.

Kama ilivyo kwa mitume wote, Yesu aliwalingania watu kuja kwenye ukweli na kuwaomba waamini uwepo wa Allah na kumpwekesha na kumhudumia na kumwabudu Yeye.

Hakusita hata kidogo katika wajibu wake na wala hakuogopa na kuwa na wasiwasi. Alikuwa mvumilivu na mtii kwa suala hilo. Kama Mtume Isa alivyoendelea kutimiza wajibu wake wa kufikisha ujumbe wa Allah, wivu na chuki za Wayahudi ziliongezeka. Mwishowe, walikimbilia kula njama ili wamuue; walianza kuufanyia kazi mpango wao. Walimtuma mnafiki aliyeitwa Tatianos nyumbani kwake.

Waliizingira nyumba yake na kundi la watu elfu 4. Pindi Tatianos alipoingia nyumbani humo, hakumkuta Yesu. Alipokuwa anatoka nje kuwajulisha kuwa Yesu hayupo nyumbani, Allah Mtukufu aliifananisha sura yake na ya Yesu. Pale Wayahudi walipomwona, walidhani kuwa ni Yesu na kumkamata. Ingawa alisema yeye sio Yesu, hawakumsikiliza. Kisha wakamtundika msalabani.

Ndio, Yesu yuko hai; hajafa. Zipo hadithi mbalimbali zinazoeleza kuwa Yesu atashuka ardhini wakati wa mwisho. Hadithi iliyoripotiwa na Jabir bin Abdullah katika kitabu cha Muslim inaeleza ifuatavyo: “Kundi moja la ummah wangu litaendelea kuunga mkono na kuuhudumia ukweli mpaka Siku ya Kiama. Mwishowe, Yesu, mwana wa Mariyamu, atakuja. Kiongozi wa Waisilamu atamwambia: “Njoo utusalishe.” Yesu atasema: Hapana, wamo kati yenu viongozi wa wengine kwa fadhila za Allah.”

Kufafanua na kufasiri hadithi hii na zinazofanana na hii katika kitabu chake kilichoitwa Mektubat, Badiuzzaman anavutia umakini kwa masuala yafuatayo: Katika nukta hiyo, wakati wimbi la kutokuwa na dini litakaposhika kasi, dini ya Ukristo itakaribia uasilia wake, yaani, kumpwekesha Allah; itatakaswa na ushirikina na ugeuzwaji, na itaunganika na Uisilamu.

Ukristo utaathiriwa na kubadilishwa kuwa ni namna ya Uisilamu. Kuifuata Quran, Wakati Ukristo wa kweli unaufuata Uisilamu, dini ya kweli itakuwa na nguvu kutokana na kuungana na Ukristo. Ingawa itashindwa mbele ya wimbi la kumkana Mungu ilhali ni tofauti, Ukristo na Uisilamu zitakuwa na uwezo wa kuishinda na kuifurusha kutokana na muungano wao. Zipo sifa nyingi katika hadithi kuhusu wakati wa mwisho Wakristo watatambua umoja huu.

Kama lilivyo suala la Yesu kushuka ardhini kimwili, hebu wacha tusome kuhusu suala hili kutoka Mektubat: “… Kisha nafsi ya Yesu (amani imshukie), ambaye yupo mbinguni kwa umbile lake la kibinadamu, atakuja kushika hatamu za wimbi la dini ya kweli, kuwa ni, ya kuaminika juu ya ahadi ya Mmoja Mwenye Nguvu Juu ya Vitu Vyote, Mletaji Habari za Kweli amesema. Kwa kuwa alishaliambia hilo, ni kweli, na kwa kuwa Mmoja Mwenye Nguvu Juu ya Vitu Vyote ameahidi, kwa hakika ataitimiza tu.

Kwa hakika, sio mbali na hekima ya Mwingi wa Hekima za Utukufu muda wote anatuma malaika ardhini kutoka mbinguni, wakati mwengine anawatuma kwa umbo la kibinadamu (kama Jibril atatokea katika umbo la Dihya), na kutuma viumbe wenye roho kutoka Dunia ya Kiroho kuwafanya watokee katika umbo la binadamu, na hata hutuma roho za wafu wengi watakatifu duniani zinazofanana na viwiliwili vyao, sio mbali na Hekima Yake – hata kama hayuko hai na kuwepo na kiwiliwili chake mbinguni, na akawa kweli kafa na kuwekwa kipembeni mbali zaidi ya Ahera – kumvika Yesu (amani imshukie) mwilini mwake na kumleta duniani, hivyo kuleta dini ya Yesu kwenye hitimisho jema; kutokana na matokeo hayo ya kinyakati. Kwa hakika Ameliahidi hilo kwa sababu hekima Yake inataka yatokee hayo, na kwa kuwa Ameliahidi hilo, kwa hakika Atamleta.

Yesu (amani imshukie) atakapokuja, sio lazima kwa kila mtu kumjua kuwa ndio Yesu wa kweli. Uteuzi Wake na wale walio karibu nae watamtambua kwa njia ya nuru ya imani. Hautokuwa ni ushahidi-binafsi hivyo kila mtu atamtambua.”