1
Ni lipi lengo na fikra kuu ya Quran? Quran ni kitabu cha namna gani?
"QUR’AN ni Maandiko yaliyoteremshwa yenye muhtasari wa vitabu vitukufu vya Mitume wote, ambao nyakati zao zilikuwa tofauti kabisa, maandiko ya watawa wote, ambao njia zao zilikuwa ni tofauti kabisa, na kazi za wanazuoni wote watakatitfu zilikuwa ni tofauti kabisa, ambao njia zao zilikuwa ni tofauti kabisa. Sura zake sita ni nzuri sana na zimetakaswa mbali na giza la mashaka na hali ya kushuku; nukta yake ya kusaidia kwa hakika ni ufunuo wa kimbinguni na Neno la milele; kusudio na lengo lake linajidhihirisha kuwa ni furaha ya milele; sura yake ya ndani ni dhahiri kuwa ni uongofu halisi; sura yake ya juu kimsingi ni nuru ya imani; sura yake ya chini ni ushahidi na uthibitisho usiopingika; sura yake ya juu inadhihirika wazi kuwa ni kuusalimisha moyo na utambuzi; sura yake ya kushoto inaonekana wazi kuwa ni kutiisha mantiki na akili; matunda yake hayabishaniwi kuwa ni Rehema ya Mwingi wa Rehema na ulimwengu wa Peponi; na daraja lake na kufaa kwake kiuhakika kumepokewa na malaika na wanadamu na majini." (Badiuzzaman Said Nursi, Sözler (Maneno))
Quran ni kitabu cha aina gani?
Umuhimu wa kuigeukia Quran na kuifanya iwe juu katika maisha yetu leo, ardhi inapovamiwa na fitina na vurugu, uko dhahiri. Kama watu wamejiingiza katika upuuzi na kutumia muda wao juu ya hilo, kama watarejea na kutii kazi za watu badala ya kitabu kitukufu cha Allah, kama wale wanaodai kuuwakilisha Uislamu wanawaita watu kwenye chama chao, dhehebu na kikundi badala ya Quran, kama Waislamu wanazingatia vitabu vilivyojaa ushirikina, na si Quran kuwa ni kitabu chao cha mwongozo, kama ummah umeiacha Quran kama ambavyo Mjumbe wa Allah analaumu katika aya ya 30 ya sura al-Furqan:
"Kisha Mjumbe atasema: ‘Ewe Mola wangu Mlezi! Kiukweli watu wangu wameifanya hii Qur'an kuwa ni kitu cha kipuuzi.'"
ikiwa Waislamu wako katika hali kama hiyo ya watu wa kitabu kitukufu na wanafikwa na mgogoro wa utambulisho unaoweza kuelezwa kuwa hauna nafasi ya kusimama juu yake na kutokusimama imara katika Sheria, Injili, na Quran kama inavyoelezwa katika aya ya 68 ya sura al-Maidah:
"Sema: Enyi Watu wa Kitabu! Hamna lenu jambo mpaka muishike Taurati na Injili na yote mlio teremshiwa kutokana na Mola wenu Mlezi. Na hakika ulio teremshiwa wewe kutokana na Mola wako Mlezi yatawazidishia wengi katika wao uasi na ukafiri. Basi usiwasikitikie watu makafiri. '"
basi, umuhimu wa kuigeukia Quran, kuifahamu na kuisaidia unakuwa lazima. Ni muhimu kuijua vyema Quran, kuisoma na kuifahamu ili kuifanya itawale maisha yetu.
Kitabu cha Kipekee, Kisicho na Kifani na cha Aina Yake Kinachopita Viwango vya Kibinadamu:
Jambo la kwanza ambalo msomaji ambaye mara tu ndio amaeanza kusoma Quran anahitaji kukizingatia ni hiki: si kitabu kilichoandikwa na wanadamu na kimegawanyika katika sura kadhaa chini ya vichwa vya habari au kitabu chenye sehemu za utangulizi, mwili na hitimisho. Quran si kitabu cha fasihi au itikadi tulivyovizoea; si kitabu cha historia, unajimu, elimu-jamii au hata tiba; pia si kitabu cha dini ya Wayunani na Warumi wa zamani. Kinavuta nadhari kwenye masuala mengi yaliyo katika mawanda ya matawi ya sayansi yaliyotajwa hapo juu, lakini ni kitabu tofauti na cha kipekee kabisa kwa upande wa malengo, mtindo, lugha, mpangilio na mtindo wa kushughulikia mambo. Ni kitabu cha ajabu kisichoweza kupimwa na tawi lolote la sayansi; kama Mawdudi anavyoliweka wazi hilo, "ni kitabu pekee cha aina yake duniani".
Quran haikuteremshwa ili kuwajulisha wasomaji wake kuhusu masuala kadhaa au kuwahamasisha kufanya utafiti wa kisayansi. Hata hivyo, lengo lake la kipekee ni kuwafanya watu na majini, ambao wamewajibishwa kwa sababu wana akili na utashi, wapatet utambuzi wa utumishi kama inavyoelezwa katika aya ifuatayo:
"Nami sikuwaumba majini na watu ila waniabudu Mimi. " (adh-Dhariyat, 51/56)
na kupata furaha kamili kote duniani na ahera. Quran si kitabu kisicho na lengo:
“Wala si mzaha.” (at-Tariq, 86/14)
Ni mkusanyiko kamili wa vigezo na kaida zenye kubainisha ukweli mbali na uwongo, jema mbali na ovu na zuri mbali na baya.
Ni sifa ya kipekee kabisa ya Quran, ambayo lengo lake la kipekee ni uongofu na furaha ya wanadamu, kutumia mtindo unaoafikiana na lengo hilo, wakati mwigine kuiambia akili, wakati mwingine hisia, wakati mwingine dhamiri na wakati mwingine moyo wa msomaji wake, kuvuta nadhari kwenye mataifa yaliyopita, mbingu na ardhi, ufalme wa mimea na wanyama, ukweli mwingi wa kisaikolojia, kisosholojia, kifalsafa na kimaadili na kuwaomba wasomaji wake wafikirie juu ya masuala hayo.
Kwa hiyo, Quran inaonekana kana yenye utata na iliyovurugika kwa upande wa mambo inayoyashughulikia ingawa imepangika katika muundo wa sura na aya. Ni umuhimu wa mtindo wa kipekee wa Quran kuliendea jambo linaloonekana kutokuhusika huku ikishughulikia suala husika, kuzuia mambo mara kwa mara, kutaja ufumbuzi wa matatizo ya kiutendaji ya jamii hasa wakati wa hatua ya miaka –ishirini-na-mitatu ya kuteremshwa na matatizo ya wanadamu yaliyoenea kote kwa ujumla, kuwahimiza watu wafanye amali njema na kutii kanuni za kimaadili, kuwapa habari njema za Pepo, kuwaonya wasifanye amali mbaya na kuwaonya dhidi ya Jahanamu.
Quran inaposomwa tena na tena, inaonekana bora zaidi kiasi cha kuwepo mshikamano na msimamo miongoni mwa mada zake, maneno na dhana, ambapo hakuna sentensi inayotumika bila ya umuhimu na kwamba kitabu chote kimejikita juu ya lengo moja: kumfanya mwanadamu apate uongofu na furaha kamili. Kama Muhammad Asad anavyoliweka wazi hilo, "Kamwe hakuna kitabu chochote - ikiwemo Biblia – kimeenezwa kwa wengi, na kwa muda mrefu sana, jibu lenye kufahamika la swali hili, "Mwenendo wangu uwe vipi ili nipate maisha mema duniani na furaha katika maisha yajayo?"
Kitabu cha Kweli, Kamilifu, Kisicho na mikingamo, Kisichobadilishwa, Kimetumwa na Allah:
Hakuna shaka kuwa Quran ni kitabu cha kweli alichoteremshiwa Mtukufu Mtume Muhammad (s.a.w) kutoka kwa Allah, Mola Mlezi wa Ulimwengu." Quran hii haiwezi kusanifiwa au kuandikwa na yeyote isipokuwa Allah. Inathibitisha sehemu za kweli za ufunuo uliofikia mpaka leo hii na inaeleza ufunuo ambao bila ya shaka unatoka kwa Mola Mlezi wa ulimwengu kikamilifu:
“Na haiwezekani Qur'ani hii kuwa imetungwa na haitoki kwa Mwenyezi Mungu. Lakini hii inasadikisha yaliyo tangulia, na ni mfafanuo wa Kitabu kisicho na shaka ndani yake, kutokana na Mola Mlezi wa viumbe vyote. " (Yunus, 10/37)
Quran inaeleza ukweli huu kuwa ni jibu la madai kama yafuatayo:
“Haya si chochote ila ni uzushi alio uzua, na wamemsaidia kwa haya watu wengine… Hivi ni visa vya watu wa kale alivyo viandikisha. " (al-Furqan, 25/4, 5),
"... Wala si kauli ya mtunga mashairi. Ni machache sana mnayo yaamini. Wala si kauli ya kuhani...." (al-Haaqqa, 69/41, 42)
na inawapa changamoto wale wote wenye kutoa kashfa za kipuuzi:
"Na ikiwa mna shaka kwa hayo tuliyo mteremshia mja wetu basi leteni sura moja ya mfano wake, na muwaite mashahidi wenu badala ya Mwenyezi Mungu, ikiwa mnasema kweli. Na mkitofanya - na wala hamtofanya kamwe - basi uogopeni moto ambao kuni zake ni watu na mawe walio andaliwa hao wanao kanusha." (al-Baqara, 2/23, 24)
"Je! Ndiyo wanasema ameizua? Sema: Hebu leteni sura moja mfano wake na muwaite (kukusaidieni) muwawezao, isipo kuwa Mwenyezi Mungu, ikiwa nyinyi mnasema kweli. " (Yunus, 10/38)
Mtu anayeiangalia Quran kwa umakini kwa hakika atagundua katika mtizamo wa kwanza kuwa haiwezi kuwa imeandikwa na mwanadamu. Haiwezekani kuona udhaifu wowote binafsi wa mtunzi unaoweza kuonekana katika kitabu au dondoo zozote zinazohusiana na masharti ya njia ya mawasilianao ambamo mtunzi anaishi. Mathalani, kama Abdullah Draz anavyoonesha kuwa Quran inaendelea kuwa juu ya sifa za kibinadamu kama vile jiografia na mbari; haitoi majina kamili ya watu na sehemu inazozitaja; inatoa mafunzo kwa ajili ya elimu ya ujumla ya watu kwa kuwataja. Jambo hili peke yake linatosha kuthibitisha kuwa Quran ni neno la Allah.
Licha ya hivyo, inawezekana kukuta baadhi ya makosa na dosari kutokana na uchunguzi wa kina hata katika kitabu kizuri kilichoandikwa na mwanadamu. Hakuna mtu yeyote anayeichunguza Quran kutokana na sababu mbalimbali kwa mamia ya miaka walioweza kukuta kosa hata dogo au ukinzani. Haiwezekani kukuta hali ya upogo au kosa katika Quran:
“Kuhimidiwa ni kwa Mwenyezi Mungu, ambaye amemteremshia mja wake Kitabu, wala hakukifanya kina upogo." (al-Kahf, 18/1)
Kitabu kitukufu cha Allah kinawapa watu changamoto kuhusu jambo hilo:
"Hebu hawaizingatii hii Qur'ani? Na lau kuwa imetoka kwa asiye kuwa Mwenyezi Mungu bila ya shaka wangeli kuta ndani yake khitilafu nyingi." (an-Nisa, 4/82)
Yeyote mwenye kuisoma Quran kwa kuzingatia na kujaribu kuifahamu ataiona kuwa si neno la mwanadamu lililotamkwa kwa utukizi na bila ya lengo lolote:
"Wala si mzaha." (at-Tariq, 86/14).
"Hiki ni Kitabu kisichokuwa na shaka ndani yake." (al-Baqara, 2/2)
“Hayo ni kwa sababu Mwenyezi Mungu ameteremsha Kitabu kwa haki. Na wale walio khitilafiana katika Kitabu wamo katika upinzani ulio mbali na haki (lengo)." (al-Baqara, 2/176).
"Ni mfafanuo wa Kitabu kisicho na shaka ndani yake, kutokana na Mola Mlezi wa viumbe vyote." (Yunus, 10/37; as-Sajda, 32/2; Yasin, 36/5; az-Zumar, 39/1)
Ni kitabu ambacho hata herufi yake moja haiwezi kubadilishwa na Allah, mwenye uwezo juu ya kila kitu, ameamua kukilinda. {6/115; 15/9}.
Ni Mwongozo Unaowapeleka Wanadamu kwenye Njia Sahihi na Nuru Inayowatoa Gizani Kuwapeleka katika Mwangaza:
Quran ni mwongozo wa wokovu kwa watu wote katika kila zama na mahali kwa ujumla. Ni mwongozo unaoonesha njia za majibu kwa waumini walio katika mgogoro na matatizo. Dhana ya uongofu (hidayah kwa Kiarabu) linalomaanisha njia ya kutokea kwa wale wasiojua mwelekeo wa kwenda jangwani linalingana na nafasi ya Quran kwa wanadamu wote.
Quran, inayoeleza kuwa mwanadamu yuko katika hasara kwa kuapa kwa kutumia istilahi zama {al-Asr, 1-2}, ni "mbinu ya wokovu" na "chelezao " kwa mwanadamu, ambaye ametatizika kutokana na migogoro ya kiroho, mmomonyoko wa kimaadili na matatizo ya kijamii katika siku zilizopita na hata leo.
"Kitabu tulicho kiteremsha kwako ili uwatowe watu kwenye giza uwapeleke kwenye muwangaza, kwa idhini ya Mola wao Mlezi, uwafikishe kwenye Njia ya Mwenye nguvu, Msifiwa." (Ibrahim, 14/1)
Njia pekee ya ufumbuzi kwa ajili ya jumuia iliyopoteza fadhila zake na sifa nzuri na ambayo hali yao ya sasa na ijayo imekuwa na giza la kupata ustawi na furaha inaoneshwa katika kitabu kitukufu cha Allah kama ifuatavyo:
"… Bila shaka imekujieni kutoka kwa Mwenyezi Mungu nuru na Kitabu kinacho bainisha. Mwenyezi Mungu huwaongoa wenye kufuata radhi yake katika njia za salama, na huwatoa katika giza kuwapeleka kwenye nuru kwa amri yake, na huwaongoa kwenye njia iliyo nyooka. " (al-Maida, 5/15, 16)
Itikadi za kibinadamu, zinazoletwa na madai kuwa watatatua matatizo hayo ya wanadamu, hupunguza matatizo hayo kwa majibu ya muda mfupi na yasiyokamilika; kwa upande mwingine, Quran analeta njia kamili za wokovu na za milele zinazofaa kwa kila zama na mahali. Quran inamfananisha mtu anayejaribu kutatua matatizo kwa majibu yaliyotolewa na wanadamu kuwa ni kama mtu asiyejiweza anayechukua hatua chache pindi radi inayong’aza macho inayoyapiga katikati ya giza na kisha anayesimama {2/20}. Quran inaongoza kwenye lililo sahihi zaidi. {17/9}. Kwani, ni ukweli mtupu {13/1; 17/105}.
Rehema, Ukarimu, Ponyo na Mwongozo kwa Wanadamu:
"Enyi watu! Yamekujieni mawaidha kutoka kwa Mola wenu Mlezi, na poza kuponyesha yaliyomo vifuani, na uwongofu, na rehema kwa Waumini. Sema: Kwa fadhila ya Mwenyezi Mungu na rehema yake! Basi nawafurahi kwa hayo. Haya ni bora kuliko hayo wanayo yakusanya." (Yunus, 10/57-58)
Quran ni ponyo na faraja, na matokeo ni rehema, kwa namna zote za vurugu na matatizo ya kiroho. Nyoyo zilizopata weusi kwa sababu ya uchafu wa kiroho na madhambi na kuwa ngumu kwa kuugua maradhi {2/10; 6/43; 8/49} zinaweza kutakaswa, kulainishwa na kuponywa kwa Quran peke yake:
"Husisimua kwacho ngozi za wenye kumkhofu Mola wao Mlezi. Kisha ngozi zao na nyoyo zao hulainika kwa kumkumbuka Mwenyezi Mungu." (az-Zumar, 39/23)
“Wale walio amini na zikatua nyoyo zao kwa kumkumbuka Mwenyezi Mungu. Hakika kwa kumkumbuka Mwenyezi Mungu ndio nyoyo hutua." (ar-Rad, 13/28)
Hivyo, Quran inakuwa ponyo na rehema kwa ajili ya wale ambao nyoyo na akili zao zinavurugwa kutokana na hadaa za Kishetani. Nyoyo za watu wanaoondokewa na matatizo ya namna hiyo na maradhi zinaelimika na busara ya kuganga yajayo hufanya kazi.
"... hii (Qur'ani) ni hoja zinazo toka kwa Mola wenu Mlezi, na uwongofu na rehema kwa watu wanao amini." (al-A'raf, 7/203; al-Jashiya, 45/20)
Quran ni aina ya kitabu kitukufu ambacho {6/155}, kama Swahaba Umar (ra) anavyoliweka wazi hilo, "Allah hufungua macho yaliyofumba, masikio yasiyosikia na nyoyo zilizofungwa kwa kutumia Qur’an."
Ushauri na Onyo Ambalo Huwafanya Watu Wawe na Ufahamu na Kuwajibika:
Jina mojawapo la Quran ni "dhikr", yaani, mawaidha; na jina jingine ni "tadhkira" yaani mwonyaji na mkumbushaji. Quran ni mkusanyiko wa mawaidha na maonyo yanayomfundisha na kumkumbusha mwanadamu juu ya majukumu yake na yanayomwongoza kwenye heri na ukweli:
“Hili ni Tangazo liwafikie watu, liwaonye, na wapate kujua kuwa hakika Yeye ni Mungu Mmoja, na wapate kukumbuka wenye akili." (Ibrahim, 14/52)
Quran inamfahamisha mwanadamu kuhusu majukumu yake kwa upande wake yeye mwenyewe, Mola wake Mlezi, watu wengine na maumbile. Inawafundisha wale wasiotambua majukumu yao na inawakumbusha wale wanaoyasahau majukumu yao. Inawaonya vikali wale wasiotimiza majukumu yao kwa makusudi.
Kama, mshairi, As Mehmet Akif, anavyoliweka wazi hilo, Quran haikuteremshwa ili wasomewe wale wanaokufa au ili kuagua. Iliteremshwa ili kuwapa mawaidha watu walio hai, kuwakumbusha wale wasiozingatia ukweli na kuwaonya dhidi ya majanga duniani na ahera yanayoweza kuwakumba. Hivyo, hakuna udhuru ulioachwa kwa wale wasiozingatia maonyo na mawaidha. {36/5-6, 69-70; 6/155-157}.
"Uteremsho wa Mwenye nguvu, Mwenye kurehemu. Ili uwaonye watu ambao baba zao hawakuonywa , basi wao wamekuwa wenye kughafilika." (Yasin, 36/5, 6)
"Wala hatukumfundisha (Muhammad) mashairi, wala hayatakikani kwake hayo. Haukuwa huu ila ni ukumbusho na Qur'ani inayo bainisha." (Yasin, 36/69)
“Ili imwonye aliye hai, na neno litimie juu ya makafiri..." (Yasin, 36/70)
“Na hichi ni Kitabu tulicho kiteremsha, kilicho barikiwa. Basi kifuateni, na mchenimngu, ili mrehemewe." (al-Anam, 6/155)
"Msije mkasema: Hakika mataifa mawili kabla yetu yameteremshiwa Kitabu; na sisi tulikuwa hatuna khabari ya waliyo kuwa wakiyasoma. Au mkasema: Lau kuwa tumeteremshiwa sisi Kitabu tungeli kuwa waongofu zaidi kuliko wao. Basi imekufikieni bayana kutoka kwa Mola wenu Mlezi, na uwongofu, na rehema. Basi nani aliye dhaalimu mkubwa zaidi kuliko yule anaye kanusha Ishara za Mwenyezi Mungu, na akajitenga nazo? Tutawalipa wanao jitenga na Ishara zetu adhabu kali kabisa kwa sababu ya kujitenga kwao.' (al-Anam, 6/156, 157)
Rejea Pekee kwa Ajili ya Waumini, Nyenzo Pekee na Kigezo Kinachopambanua Ukweli Mbali na Uongo:
Rejea kuu kwa kila Muislamu anayeuchagua Uislamu kuwa ni dini yake na anajisalimisha kwa Allah ni Quran. Atajifundisha kanuni za maisha zitakazomletea furaha duniani na ahera kutokana na Quran. Atajifundisha anachohitajika kuamini na anachohitajika kukataa, kipi ni chema na halali na kipi ni kiovu na haramu, anachotakiwa kufanya na anachotakiwa kukiepuka kutokana na Quran. Atautakasa moyo wake, kuimarisha kujisalimisha kwake kwa Allah na kuhuisha imani yake na msisimko wake pamoja nayo. {9/124; 16/102}
“Na inapo teremshwa Sura wapo miongoni mwao wasemao: Ni nani miongoni mwenu Sura hii imemzidishia Imani? Ama wale walio amini inawazidishia Imani, nao wanafurahi. " (at-Tawba, 9/124)
"Sema: Ameiteremsha hii Roho takatifu kutokana na Mola wako Mlezi kwa haki, ili awathibitishe wale walio amini, na kuwa ni uwongofu, na ni bishara kwa Waislamu." (an-Nahl, 16/102)
Atajifundisha mazuri ya Peponi na kitisho cha mateso ya Jahanamu kutoka katika kitabu kitukufu cha Allah; Hivyo, atafanya jitihada ya kuendesha maisha bora na atatenda zaidi kwa umakini ili kuepuka madhambi na amali mbaya. Kwa kifupi, muumini atapata kila kitu kuhusu jinsi ya kufanya ili apate radhi za Allah kwa ujumla katika Quran:
“Na tumekuteremshia Kitabu hiki kinacho bainisha kila kitu, na ni uwongofu, na rehema, na bishara kwa Waislamu.” (an-Nahl, 16/89)
Hata hivyo, mtu asihitimishe kutokana na aya hii kuwa Quran ni ensaiklopidia au kitabu cha sayansi. Si kitabu kinachotaja nadharia za muda mfupi za kisayansi; ni mwogozo wa maisha. Ni kitabu cha mwongozo kilichotumwa na Allah, aliyetuumba sisi na anayeyajua zaidi maumbile yetu kuliko sisi; kinatuonesha jinsi ya kutumia viwiliwili vyetu vya kupita katika dunia hii ya mpito:
“Si maneno yaliyo zuliwa, bali ni ya kusadikisha yaliyo kabla yake, na ufafanuzi wa kila kitu, na ni uwongofu na rehema kwa kaumu yenye kuamini." (Yusuf, 12/111)
Quran ni neno sahihi la mwisho la Allah. Wanadamu, waliohutubiwa kwa njia ya ufunuo tangu Hadhrat Adam (as), mtu wa kwanza, ambaye Quran, ambayo ni hazina bora inayothibitisha yaliyo ya kweli katika mafundisho yaliyotangulia ya upwekeshaji yaliyosahaulika, yaliyopotea au kubadilishwa na inayosahihisha makosa yaliyomo ndani mwao. Wanadamu wanaweza kujua kipi ni ukweli wa kiungu na kipi si sahihi na ushirikina, shukrani ziiendee Quran, ambayo ni "Furqan" (Kipambanuzi baina ya heri na shari).
Quran kwa hakika ni kipimo kwa ajili ya Waislamu. Akili ya Muislamu, mtizamo wa kidunia na mwenendo unapaswa uundwe na Quran. Anapaswa kuangalia kila kinachomjia kwa jina la elimu na utamaduni wa Kiislamu kwa utumia Quran, moja baada ya kingine; na anapaswa apambanue baina ya lililosahihi na lisilosahihi, la kweli na la kishirikina, lilo bora na lililobuniwa.
Isisahaulike kwamba fursa adhimu ya Uisilamu ni kwamba wafuasi wake wanayo Furqan, (mpambanuzi) kitabu ambacho hakijakumbwa na mabadiliko yoyote, kilichopo chini ya hifadhi ya Allah na kitakachobakia kuwa ni kigezo kisicho na doa kinachopambanua baina ya ukweli na uongo. Ni kitabu kisicho na kasoro hata chembe.
Waumini hufanya rejea kwenye Quran ili kujifundisha siri za dunia na ahera; pia hurejea kwenye Quran na sunnah bora ya Mjumbe wa Allah, ambaye ni Quran hai, kuhusu masuala wasiyoafikiana.
Kwa kifupi, Quran ni kitabu kitukufu cha rejea ambacho thamani yake kamwe haitapungua mpaka Siku ya Kiama kwa ajili ya waumini. Kitabu hiki cha hazina ndicho rejea pekee ambayo waumini watafanya rejea ili kutatua namna zote za matatizo ya kiroho yakiwemo masuala ambayo wao hawaafikiani.
Kitabu cha Vitendo na si Nadharia:
Quran si kitabu kinachoshughulikia baadhi ya mambo ya kihistoria, kijamii, kifalsafa na kimaadili kwa njia ya kinadharia. Hata hivyo, kinalenga katika kuweka jumuia iliyoundwa kwa maadili ya kidunia na kanuni za kiroho inazoziweka. Inalenga kwenye kuondoa kila kinachohusiana na ukosefu wa fadhila na shari na kuwafanya wanadamu wote wajisalimishe kwa Allah, yaani, Uislamu, kama ilivyobadili mojawapo kati ya jamii za kijinga zaidi duniani na kuwa jamii bora zaidi {2/193}; ni kitabu cha kimapinduzi. Quran iliteremshwa ili itekelezwe kivitendo na watu waitii.
"Fuateni mliyo teremshiwa kutoka kwa Mola Mlezi wenu, wala msifuate rafiki au walinzi wengine badala yake. Ni machache mnayo yakumbuka." (al-Araf, 7/3)
Kila anayeiamini Quran, kimsingi, Mtume (s.a.w), anaitii na kushikamana na kanuni ilizoziweka:
"Basi wewe yashike yaliyo funuliwa kwako. Hakika wewe uko kwenye Njia Iliyo Nyooka. Na hakika haya ni ukumbusho kwako na kwa kaumu yako. Na mtakuja ulizwa. " (az-Zukhruf, 43/43, 44)
Quran "ni kitabu kitukufu cha Allah ambacho hamtapotea kamwe kama mtashikamana nacho." {Ibn Majah} ni kamba imara ya Allah itakayokupelekeni kwenye mwangaza, ukomavu, na heshima kama mtaishikilia; Hakuna kulazimishana katika dini. Ukweli utajitokeza dhahiri mbali na uongo; mwenye kukataa Uovu na akamwamini Allah atakuwa amekamata kishikizo cha kutumainia, kisichovunjika.”
“Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusikia, Mwenye kujua." (al-Baqara, 2/256); {al-Baqara, 2/256, 257; Aal-i Imran, 3/103}
“Na shikamaneni kwa Kamba ya Mwenyezi Mungu nyote pamoja, wala msifarikiane. Na kumbukeni neema ya Mwenyezi Mungu iliyo juu yenu: vile mlivyo kuwa nyinyi kwa nyinyi maadui naye akaziunganisha nyoyo zenu; kwa neema yake mkawa ndugu. Na mlikuwa ukingoni mwa shimo la Moto, naye akakuokoeni nalo. Namna hivi Mwenyezi Mungu anakubainishieni Ishara zake ili mpate kuongoka." (Aal-i Imran, 3/103)
Jamii inayoshikamana na kamba ya Allah na kutii kanuni za ufunuo inakuwa na furaha duniani na ahera. Wale wanaoupa mgongo ukweli wa kiungu na kukiacha kitabu kitukufu cha Allah kwa kutokukitii watakosa furaha katika sehemu zote mbili za ulimwengu.
Kanuni za kimaadili, nasaha na mapendekezo yaliyo katika Quran yanakuwa muhimu yanapotekelezwa kivitendo. Mathalani, nasaha zifuatazo za kiungu hazitakuwa na manufaa yoyote kama hazitafanyika kivitendo:
“Wala msikaribie uzinzi. Hakika huo ni uchafu na njia mbaya."
"Wala msiuwe nafsi ambayo Mwenyezi Mungu amekataza isipo kuwa kwa haki..."
"Wala msiyakaribie mali ya yatima..."
“na timizeni ahadi. Kwa hakika ahadi itasailiwa. (katika Siku ya Hesabu)."
"Na timizeni kipimo mpimapo. Na pimeni kwa mizani zilizo sawa..."
"Wala usiyafuate usiyo na ujuzi nayo. Hakika masikio, na macho, na moyo - hivyo vyote vitasailiwa. (katika Siku ya Hesabu)."
"Wala usitembee katika ardhi kwa maringo. Hakika wewe huwezi kuipasua ardhi wala kufikia urefu wa milima."
"Haya yote ubaya wake ni wenye kuchukiza kwa Mola wako Mlezi. " (al-Isra, 17/32-38)
Kitabu cha Wazi Wazi, Chenye Kufahamika, Kilichorahisishwa:
Kama inavyoonekana katika aya za 32-38 za sura ya al-Isra tulizozinukuu kama ni mfano hapo juu, aya za Quran zina kanuni zenye kutendeka zinazoweza kufahamika hata kwa jumuia yenye ujinga mwingi. Quran haina utatanishi, wala kutokufahamika, wala kitabu cha kale kinachoweza kufahamika kwa wataalamu, wanasayansi na maulamaa tu au chenye alama za siri zinazoweza kutafsiriwa nao peke yao. Hukaririwa mara kwa mara kwa ujumla mwanzoni mwa sura za Quran ambapo Quran na aya zake viko wazi na vyenye kufahamika.
Katika Quran, kila kitu kimeelezwa "kupitia mifano mbalimbali" {18/54; 20/113} na kwa kina {6/55, 56, 126; 41/2-3}. Quran imerahisishwa ili ifahamike kupitia sitiari na mifano:
"Na bila ya shaka Sisi tumeifanya Qur'ani iwe nyepesi kufahamika. Lakini yupo anaye kumbuka?" (al-Qamar, 54/17, 22, 32, 40)
"Kwakuwa wale wa mwanzo waliohutubiwa na Quran hawakujua kusoma na kuandika, Shari'ah tukufu za Uislamu zilikuwa rahisi. Shari'ah iliteremshwa katika mfumo ambao ungefahamika na kutekelezwa kwa urahisi na wale wanaohutubiwa bila ya kuhitajika elimu yoyote au ubobezi. Kudai kinyume chake ni kinyume na msingi wa Shari'ah. Watu wa mwazo kuhutubiwa hawakujua kusoma na kuandika; kwa hivyo, shari'ah iliyoteremshwa ilikuwa nyepesi. Vinginevyo, wangesema, "Iko juu ya kiwango chetu; haifanani na maneno yetu; hayo ni maneno tusiyoyajua au kuyafahamu, n.k..." {41/44}.
Licha ya hivyo, Allah anaeleza, "Mwenyezi Mungu haikalifishi nafsi yoyote ila kwa kadiri ya iwezavyo." {2/286}; "Wala (Allah) hakuweka juu yenu mambo mazito katika dini" {22/78}. Kwa sababu za kiutekelezaji, Shari'ah ilibidi iteremshwe katika lugha na mtindo ambao ungeweza kufahamika kwa kila mtu." Shatibi
Quran imeelezewa kama ifuatavyo katika hadithi:
“Baadhi ya watu ni watu wa Allah. Mjumbe wa Allah alipoulizwa, 'Ni kina nani hao?', Alisema, 'Hao ni watu wa Quran; hao ni watu wa Allah na marafiki zao." (Tirmidhi)
"Rehema na wingi humiminikia mahali na malaika na utulivu huzingira mahali ambapo muumini anasoma Quran kwa unyoofu na kwa kutaka radhi za Allah." (Tirmidhi)
Harith al-Awar anasimulia: "Pindi tulipokuwa tunapita njia ya msikitini, niliwakuta watu wameacha kumtaja Allah na kuingia katika mazungumzo yasiyofaa. Kwa hivyo, nilimwendea Hadhrat Ali (ra) na kumwambia niliyoyaona.
Akaniuliza, 'Unasema kweli, ni hivyo?'
Nilipomhakikishia kuwa hivyo ndivyo ilivyokuwa, alisema: 'Nilimsikia Mjumbe wa Allah akisema,
"Tazama! Mfarakano utatokea! Hapohapo nikamuuliza: ‘Ni ipi njia ya kujinusru nao? Ewe Mjumbe wa Allah! Alijibu: Ni kutii kitabu kitukufu cha Allah.
Kina habari zote kuhusu yaliyowatokea jumuia za kabla yenu, habari za mifarakano na misukosuko itakayotokea baada yenu na ishara za Siku ya Kiama.
Pia ina hukumu kuhusu mambo yatakayotokea miongoni mwenu (kuhusu mambo kama vile imani-ukafiri, utii-uasi, kilichoruhusiwa-kilichokatazwa, n.k.). Ni kipambanuzi baina ya ukweli na uwongo.
Iko makini katika kila inachokitaja, Hakuna neno ndani mwake ambalo ni la kupita bure tu au la nje ya mada. Mwenye kuangukia katika upuuzi kwa kutokukizingatia na kutokutenda kulingana nacho, Allah atamwangamiza. Kama yeyote atatafuta uongofu mahali pengine Allah atamwacha apotee.
Ni kamba madhubuti ya Allah. Ni ukumbusho wa hekima, na ni njia iliyonyooka kabisa. Inahifadhi nafsi zinazoitii zisiharibiwe na upotovu na ndimi zenye kuisoma dhidi ya kutatizika. Wanazuoni wa Qur’an daima hutamani zaidi yaliyomo ndani mwake. Kukisoma mara kwa mara hakumchoshi msomaji wake; wala msomaji hapotezi ladha kwa kurudiarudia kukisoma. Mastaajabu yake makubwa yanayowashangaza wanadamu hayaishi kamwe.
Ni aina ya kitabu ambacho, pindi walipokisikia, majini iliwabidi wakiri kuwa, 'Hakika sisi tumeisikia Qur'ani ya ajabu. Kwa hakika Inaongoza kwenye uwongofu, kwa hivyo tumeiamini.' (Surah al-Majini, 72/1-2) Mwenye kukitamka, atakuwa anasema ukweli. Mwenye kutenda kulingana nacho atalipwa. Mwenye kuhukumu kulingana nacho, atakuwa mwadilifu. Mwenye kuwalingania watu kukiendea, atawaongoza kwenye njia iliyonyooka. Oh Awar! Jifundishe vyema maneno haya mzuri." (Tirmidhi)
Kwa muhtasari, Quran, “kitabu cha muujiza", kitakachokomesha siku za giza tunazoishi ndani mwake na matatizo na machungu tunayoumia na kitakachowaongoza wanadamu wote kwenye "furaha ya wote", kiko katika utumiaji wetu kama hazina isiyo na kifani. Tunachohitajika kufanya ni kusoma hii "mbinu ya wokovu" kwa macho maangalifu ili tupate majibu ya maswali ya leo na kuwa na nguvu na msisimko uliokuwepo katika siku za mwanzoni mwa Uislamu.
Nyenzo:
A. Yıldız-Ş. Özdemir, Kur'an Nedir, Nasıl Okunmalıdır, Pınar Yayınları.
2
Kuna tofauti gani kati ya Qur’an na vitabu vingine vya kiungu?
Katika vitabu vya kiungu kwa sasa hakuna kilicho katika katika nakala ya asili ile waliyoteremshiwa Mitume wa Allah, isipokuwa Qur’an iliyo. Nakala za asili za vitabu hivyo zimepotea katika nyakati balimbali na zikaandikwa upya na wanadamu. Hivyo, vipengele vya ushirikina viliingizwa. Mathalani, Taurati haikuweza kuhifadhiwa na Wayahudi kwa sababu walikamatwa mateka na wakaishi uhamishoni kwa muda mrefu baada ya Nabii Musa (AS) na hata walifuata upagani kwa kupoteza imani yao; na pamoja na ukweli huo wa kihistoria, nakala iliyopo sasa ya Taurati iliandikwa na baadhi ya watu wa dini kwa muda mrefu baada ya Nabii Musa na kikakubalika kuwa ni kitabu cha kidini kama ilivyokuwa nakala ya mwanzo. Ni dhahiri kuwa Taurati haiwezi kuwa nakala ile ile aliyoteremshiwa Nabii Musa (AS) baada ya kipindi hicho kirefu chenye utata. Kwa hivyo, ina baadhi ya madai na kashfa zisizoweza kusemwa na mitume na kuna hukumu zilizo kinyume na dini ya upwekeshaji.
Zaburi ya Nabii Dawud pia ilipatwa na yale yale yaliyopatwa na Taurati.
Ama kuhusu Biblia, Nabii Isa (Yesu) hakutoa mwanya wa kuandikwa wahyi. Kwa kuwa, alipata utume alipokuwa na umri wa miaka thelathini na kazi ya utume iliisha alipofikisha umri wa miaka thelathini na tatu. Alijitahidi kuonesha njia ya kweli kwa muda mfupi sana wa miaka mitatu kwa kwenda kijiji hadi kijiji kingine na mji mmoja hadi mwingine. Kuelekea mwishoni, kila mara alikuwa akifukuzwa na watawala wa Kirumi kutokana na uchochezi wa Wayahudi. Kwa hivyo, hakuweza kupata muda au fursa ya kuandikwa Biblia. Kwa hivyo, Biblia zilizopo leo zimeitwa kwa majina ya watu walioziandika na zina hotuba, mafunzo na uongofu wa Yesu (AS) na zinaonekana kama tawasifu yake. Licha ya hivyo, hazikuandikwa na wafuasi wa mwanzo wa Yesu (AS) na waumini wake bali watu waliowaona wafuasi wa Yesu (AS); kwa hivyo walikuwa ni wasikilizaji.
Zipo tofauti baina ya Biblia zilizopo, kwa upande wa maudhui na usimulizi. Kwa hakika, Biblia hizo zilikubaliwa na baraza la kiroho lililokutana mnamo mwaka 325 BK huko Nicaea. Baraza hilo lilichunguza mamia ya Biblia na kukubali Biblia nne, zilizotamka fikra ya kipengele cha uungu wa Yesu, kwa muwafaka wa wajumbe 318 kwa kuziharibu Biblia zingine zilizosalia.
Kama ilivyoonekana, hekima ya dhana ya Yesu ya kuwa mwana wa Mungu ilikubaliwa na baraza baada ya Yesu kuondoka.
Kwa hakika, baadhi ya makanisa ya Kikristo hayakukubaliana na uamuzi huu. Hivyo, haiwezekani kusema kuwa Biblia nne zilizopo sasa zinalingana na Biblia aliyoteremshiwa Yesu (AS).
3
Ni upi umuhimu wa Quran; unaweza kutoa maelezo gani kuhusu Quran?
Quran ni kitabu kitukufu cha mwisho ambacho Allah aliwateremshia watu. Quran iliteremshwa kwa Mtume Muhammad (s.a.w) kupitia kwa Jibril na ikafika leo kwa njia ya kuandikwa na kusimuliwa.
Quran ni mwongozo wa kiyakinifu na kiroho kwa mtu mmoja mmoja na jumuia, matabaka yote ya watu wanaoishi mahali popote au wakati wowote na kwa maisha yote ya mwanadamu. Kila mtu, kuanzia rais mpaka mtu wa mtaani, anapata yanayowahusu wao katika Quran. Wanachukua elimu na mafunzo yaliyo muhimu kwa ajili ya amani na utulivu duniani na ahera.
Ubora na sifa za Quran zimeelezwa kama ifuatavyo katika aya nyingi na hadithi:
* “Na hichi ni Kitabu tulicho kiteremsha, kilicho barikiwa. Basi kifuateni, na mcheni mungu, ili mrehemewe." (Al-Anam, 6/155).
* " Na hiki ni Kitabu tulicho kiteremsha, kilicho barikiwa, chenye kuhakikisha yaliyo tangulia, na ili uuwonye Mama wa Miji na walio pembezoni mwake. Na wenye kuamini Akhera wanakiamini hichi, nao wanazihifadhi Sala zao." (Al-Anam, 6/92).
* “Hebu hawaizingatii hii Qur'ani? Na lau kuwa imetoka kwa asiye kuwa Mwenyezi Mungu bila ya shaka wangeli kuta ndani yake khitilafu nyingi." (An-Nisa, 4/82).
* “Qur’ani kuwa ni uwongofu kwa watu, na hoja zilizo wazi za uwongofu na upambanuzi...." (Al-Baqara, 2/185).
* "(Qur’an) ni uwongofu na bishara njema kwa Waumini." (Al-Baqara, 2/97).
* “Na hiki Kitabu, tumekuteremshia wewe, kimebarikiwa, ili wazizingatie Aya zake, na wawaidhike wenye akili." (Sad, 38/29).
* Masimulizi yafuatayo yamesimuliwa kutoka kwa Harith bin Awar: Wakati fulani, Swahaba Ali alisema:
"Nilimsikia Mjumbe wa Allah akisema:
' Tazama! Utatokea mfarakano.' Kwa sababu hiyo, nilimuuliza,
‘Ewe Mjumbe wa Allah! Ni ipi namna ya kuondokana nao?' Alisema,
'Ni kutii kitabu kitukufu cha Allah.' (Kisha Mtume akaeleza sifa bainifu za Quran kama ifuatavyo:
'Ina maelezo yote kuhusu kilichowakuta jamii za kabla yenu, habari za mifarakano na misukosuko itakayokutokeeni na dalili za Siku ya Kiama. Ni kipambanuzi baina ya ukweli na uwongo. Kama yeyote anatafuta uongofu mahali pengine Allah atamwacha apotee. Ni kamba imara ya Allah. Ni ukumbusho wenye hekima, na njia iliyonyooka. Inazilinda nyoyo zinazoitii dhidi ya kuvurugwa na kupotoshwa na ndimi zenye kuisoma dhidi ya utata.
Wanazuoni wa Qur’an daima huwa wana shauku nayo. Kuisoma tena na tena kamwe hakumchoshi mwenye kuisoma; wala msomaji hapotezi ladha yoyote kwa kukariri kuisoma. Mastaajabu yake makubwa yaliyowashangaza watu hayataisha kamwe, " wakasema: Hakika sisi tumeisikia Qur'ani ya ajabu!" (Al-Jinn 1). Mwenye kuitamka, husema ukweli. Mwenye kutenda kulingana nayo, atalipwa. Mwenye kuhukumu kulingana nayo, atakuwa mwadilifu. Mwenye kuwaita watu kwenye Qur’an, atawaongoza kwenye njia iliyonyooka.'" (Tirmidhi, Thawabu"l-Qur'an 14, 2908)
* "Quran ni nuru ya waziwazi, dhikr yenye hekima na njia ya kweli."
* "Quran ni kamba ya Allah iliyorefushwa mpaka ardhini kutoka mbinguni."
* "Ubora wa Quran juu ya maneno mengine ni kama ubora wa ar-Rahman juu ya viumbe Wake."
* "Ikiwa mtu atasoma aya moja katika kitabu kitukufu cha Allah, itakuwa ni nuru inayomwangazia katika Siku ya Kiama."
* "Zitieni nuru nyumba zenu kwa kuswali na kusoma Quran."
Quran ilitremshwa moyoni mwa Mtume (s.a.w) kwa hali zote, maana na maneno yake pia. Hiyo ndiyo sababu, Quran inaitwa wahy al-matluww (ufunuo unaosomwa). Kwa hiyo, Quran si maana yake tu, bali ni pamoja na maneno pia. Quran haikuteremshwa yote kwa Mtume (s.a.w) kwa mara moja; ilikuwa ikiteremshwa aya baada ya aya na sura baada ya sura.
Muujiza wa Quran
Quran ina namna zote za kanuni za imani, amali na maadili yatakayomfanya mwanadamu apate furaha kamili ya halisi. Ni muujiza mkubwa wa kifasihi kwa upande wa maneno na maana. Mtume (s.a.w) amesema yafuatayo kuhusu jambo hilo:
"Kila Mtume alipewa miujiza iliyowafanya watu waamini, lakini nilichopewa mimi, ni Msukumo wa Kiungu alionifunulia Allah. Kwa hivyo ninatumaini kuwa idadi ya wafuasi wangu itawazidi wafuasi wa Mitume wengine katika Siku ya Kufufuliwa." (Bukhari, Fadhailu'l-Qur'an, 1)
Kwa hakika, miujiza ya mitume wengine iliisha baada ya kuisha muda wao. Muujiza wa Quran utaendelea kuwepo mpaka Siku ya Kiama. Katika aya kadhaa za Quran, kumeelezwa kwa msisitizo kuwa Quran ni muujiza:
“Sema: Wangeli kusanyika watu na majini ili walete mfano wa hii Qur'ani basi hawaleti mfano wake, hata wakisaidiana wao kwa wao...." (al-Isra, 17/88).
Kwa hakika, hakuna aliyeweza wala atakayeweza kuleta aya moja inayofanana na aya za Quran kwa mtindo na ufasaha. Quran ni muujiza kwa kulingana maneno yake na maana yake. Mtume (s.a.w) hakuwa mwenye kusoma na kuandika. Hakujifundisha chochote kutoka kwa yeyote. Kwa hiyo, alizingatiwa kuwa asiyejua kusoma na kuandika. Hata hivyo, kitabu kitukufu alichokuja nacho kilikuwa na ukweli wa hali ya juu na kilifahamisha mengi ya ukweli wa kisayansi ambayo sayansi na uzoefu viliweza kuyapata katika miaka elfu moja na mia nne iliyopita. Hili linathibitisha kuwa Quran ni neno la Allah moja kwa moja. Mathalani, ukweli kuwa jua linazunguka lenyewe na linakwenda katika kituo maalumu kilichopangwa pamoja na sayari zingine zinazolitegemea, kufunguka mapiramidi na miili ya maiti za Mafarao zilizohifadhiwa kwa dawa zimegunduliwa katika karne iliyopita.
Hata hivyo, Quran ilitueleza kuhusu hayo na mengine kama hayo katika karne nyingi zilizopita. Haijalishi sayansi inaendeleaje, haiwezi kuipinga Quran. Hata hivyo, maendeleo ya sayansi yataleta urahisi kwa Quran kufasiriwa na kuelezwa. Kama Badiuzzaman Said Nursi anavyoliweka wazi hilo,
"Kadiri muda unavyozidi kusogea, Quran inazidi upya; ukweli mwingi iliyo nao unadhihirika zaidi."
Kipengele kingine cha kimiujiza cha Quran ni kuwa imebashiri matukio mengi yaliyotokea baadaye. Chochote ilichobashiri kilitokea sawa na kilivyobashiriwa.
Baadhi ya fafanuzi na maelezo ya Quran ni kama ifuatavyo:
- Qur'an Yenye Hekima Nyingi, inayomfahamisha kwetu Mwenye kuturuzuku, ni mfasiri wa milele wa Kitabu kikuu cha ulimwengu...
Ulimwengu umelinganishwa na kitabu kikuu kilichoandikwa kwa kalamu ya uwezo. Katika kitabu kidogo, ibara inayosema ishara za uumbwaji (ayat at-takwiniyya) imetumika kwa ajili ya viumbe duniani. Ishara ya uumbwaji inamaanisha kilichoumbwa kutokana na amri "kuwa" (kun), inayoonesha uwepo, upweke, majina na sifa za Allah na kinachokuwa ushahidi juu ya hayo. Aya (ishara) zilizo katika Quran zinatokana na sifa za Allah zinazoitwa kauli na ishara za ulimwenguni zinatokana na sifa Zake zinazoitwa uwezo (qudrah).
Kitabu hiki cha ulimwengu hufanya Allah atambulike pamoja na ishara zake zote lakini wanadamu hawajaweza kukisoma na kukitathmini kwa usahihi. Yaani, hawakufahamu lugha ya kitabu kitukufu. Quran Yenye Hekima Nyingi imekitafsiri kitabu kitukufu cha ulimwengu, imewajulisha wanadamu kuhusu kitabu hicho na kueleza sifa za Mola wetu Mlezi, ambaye ndiye mwandishi wa kitabu hicho, kwetu. Kimetueleza kuhusu sifa Zake, majina na amali.
- kidhihirisho cha hazina za Majina ya Kiungu zilizofichwa katika kurasa za ardhi na mbingu...
Maana zilizofichwa, zimesitiriwa, ambazo zimekuwa hazionekani na hazijulikani. Tunaishukuru Quran, kwa kutafsiri kitabu kitukufu cha ulimwengu, udhihirishaji wa majina ya Allah yaliyokuwa yamefichikana duniani na mbinguni yameanza kuweza kusomwa. Katika sentensi hii, majina ya Allah yamefananishwa na hazina. Mathalani, jina al-Khaliq (Mumbaji) ni a hazina; viumbe wote ni kama vito vya hazina hiyo. Jina al-Muhyi (Mwenye Kuhuisha) ni hazina nyingine; uhai wote unatoka kwenye hazina hiyo.
- ufunguo wa kuyaendea ya kweli yaliyofichikana upo chini ya mistari hiyo ya matukio...
Katika kitabu hiki cha ulimwengu, kila jambo, kama vile kila kiumbe, ni kama neno au mstari. Ni muhimu kuyasoma kwa usahihi. Ukweli uliofichikana chini ya mambo unaweza kusomwa kwa usahihi kwa kutumia uongofu na maelekezo ya Quran tu.
Usiku na mchana, afya na maradhi, furaha na huzuni, uzee na umauti ni katika ya kweli iliyoandikwa katika kitabu hicho. Miongoni mwa matukio muhimu zaidi kwa watu ni kifo. Wanaozingatia kifo kuwa ni "kuto-kuwa, kuto-kuwepo, kuingia kaburini na kupotea hawawezi kufahamu ukweli wa kifo na kutathmini vibaya tukio hilo. Ukweli wa kifo unafahamika kwa uongofu wa Quran. Maana ya kuzaliwa ni kuja duniani kutokea katika jeraha; halikadhalika, kifo kinamaanisha kwenda katika ulimwengu wa barzakh kutoka duniani. Kisha, kuzaliwa kwingine kunakoitwa ba'th kutafuatia; watu watakwenda katika mahali pa Kukusanywa kutoka katika ulimwengu wa kaburi kupitia humo.
Kuna maelezo ya kina zaidi kuhusu ukweli wa kifo katika Mkusanyiko wa Risale-i Nur. Hebu tukumbuke baadhi yake: Kifo ni “kubadilisha makazi, kupumzika kutoka katika wajibu, roho kupewa uhuru”. Kaburi ni “mlango wa kuingia katika ulimwengu ulio bora zaidi ya dunia hii.”
- hazina ya fadhila za Mwingi wa Rehema na hotuba za milele, zinazotoka katika Dunia ya Ghaibu nyuma ya pazia la Dunia Bayana...
Ibara inayosema dunia ya ghaibu iliyotajwa hapo juu inaweza kufahamika kuwa ni kiti kikubwa cha enzi ambapo ulimwengu huu wenye kuonekana unadhibitiwa na kutawaliwa, kama ulimwengu wa tashbihi ambapo hupigwa mifano ya kila kitu, na kama ulimwengu usiojulikana kama Ubao Uliohifadhiwa (Lawh al-Mahfudh) ambapo kila kitu kimeandikwa na kuhifadhiwa.
Maneno fadhila na hotuba yanakamilishana yenyewe na kuashiria kwenye lengo lile lile moja. Kuhutubiwa na Allah Mtukufu ni fadhila kubwa kwa waja Wake. Kujulishwa kuhusu amri Zake na makatazo Yake, kupata radhi Zake, na kuoneshwa njia za kwenda Peponi ni rehema kubwa na zawadi ya Allah.
- jua, msingi, na mpango wa dunia ya kiroho ya Uislamu...
Chanzo cha mazuri yote, fadhila, manufaa na maadili ya juu, imani ya kimsingi, ni jua la Quran. Msingi wa dini yetu ni ukweli mwingi wa Quran. Jengo la uongofu na uthabiti litakaoendelea daima limejengwa na hadithi, ambazo ndizo fasiri za mwanzo za Quran, juu ya msingi huu.
Neno mpango linaweza kutafsiriwa kuwa ni ijtihad na fatwa zilizotokana na nuru ya Quran na hadithi ili kujibu mahitaji mapya yanayoibuka katika jengo linalokua la Uislamu.
- na ramani ya dunia za ahera...
Katika Quran, ramani ya barabara ya maisha ya ahera inayonzia katika Mahali pa Kukusanywa na kuendelea kama vile “kusimama, mizani (Mizan), daraja (Sirat) na Pepo au Jahanamu" umechorwa; sura nzuri za Peponi na adhabu za Jahanamu pia zimeoneshwa kwa mwanadamu kama picha.
- kifasili cha kipekee, ufafanuzi halali, ushahidi wa kueleweka, na mfasiri dhahiri wa Dhati ya Kiungu, sifa, na amali...
Chanzo pekee cha maelezo mazuri kuhusu dhati, sifa, na amali za Allah ni Quran. Akili na fikra za kibinadamu haziwezi kufanya chochote kuhusu ukweli huo mwingi usiojulikana na wa milele. Kwa kuwa Allah anajitambulisha Mwenyewe katika Quran, Hakuna haja ya ukisiaji usio na msingi maalumu wa mwanadamu na fikra zisizofaa.
Tunajifundisha kutokana na aya za Quran na wanazuoni wetu walioidhinishwa ukweli ufuatao na yaliyo kama hayo: “Kuwepo kwa Allah ni lazima; Yeye hana mwanzo wala Hana mwisho; Hahitaji wakati wala nafasi; Ana sifa zisizo na ukomo; hakuna mabadiliko wala upungufu utakaojitokeza katika sifa hizo bila ya kujalisha idadi ya viumbe Anaowaumba; Kuwepo Kwake na sifa, rehema Zake na ghadhabu, neema zake na wivu na matendo Yake mengine yote hayawezi kulinganishwa na hali na uwezo wa viumbe Wake.
Viumbe wa ulimwenguni wanatangaza kuwepo kwa Allah na sifa Zake kwa hali zao lakini watu kwa ujumla hupuuza misemo hiyo ya kiroho au kutokuifahamu. Kwa hiyo, burhan an-natiq (ushahidi wenye kueleweka) ni muhimu. (Pindi ibara burhan an-natiq inapotumika kwa ajili ya Mjumbe wa Allah (s.a.w), inamaanisha anayefikisha ujumbe wa Quran kwa watu.)
Ibara inayosema mfasiri dhahiri inamaanisha Quran inawatafsiria watu maneno ya kitabu kitukufu cha ulimwengu yale wasiyoyafahamu; ina maana inayolingana na ibara inayosema ushahidi wenye kueleweka.
mwalimu, hekima ya kweli, mwelekezaji, na kiongozi wa dunia ya utu...
Quran ilishushwa ili kuzifundisha roho za watu, kuzikamilisha nyoyo zao kwa njia ya imani na akili zao kupitia sayansi na elimu, kuwafundisha hekima ya kweli, kuwatoa watu kutoka katika njia potovu na kuwaonesha njia ya uongofu. Hekima ya kweli, yaani, habari sahihi kuhusu lengo la kuumbwa wanadamu na viumbe wengine na majukumu yao linaweza kufundishwa kutoka katika Quran kwa sababu aya za Quran ni maneno ya Muumbaji aliyewaumba viumbe hao.
Kama inavyojulikana, neno "hekima" pia hutumika kwa ajili hekima. Kivumishi "-a kweli" kilichotumika hapa kinaashiria kuwa falsafa si hekima ya kweli.
Hekima ina fafanuzi kadhaa. Mojawapo ni "amali pamoja na elimu" (mtu kufanya anayoyajua na anayojifundisha) Yaani, kama fikra inayomfanya mtu afanye amali njema, ina hekima. Fikra zinazozungumzwa tu lakini hazifanywi kwa vitendo ni fikra binafsi; haziwezi kuwa njia ya uongofu kwa ajili ya watu.
ni kitabu cha yote mawili hekima na sheria, na kitabu cha swala na ibada, na kitabu cha amri na mawaidha, na kitabu cha maombi na elimu ya Kiungu - ni kitabu kwa ajili ya mahitaji yote ya kiroho; nacho ni maktaba tukufu inayotoa vitabu vinavyofaa katika njia za watawa wote na wasema kweli, watakatifu na wanazuoni, ambao njia zao zote ni tofauti...
Quran ni kitabu cha hekima kwa sababu kinamfundisha mwanadamu lengo na mambo ya wajibu kwa viumbe wote; ni kitabu cha shari'ah (sheria) kwa sababu kinamjulisha mwanadamu kuhusu amri na makatazo kuhusu maisha ya mtu mmoja mmoja na ya kijamii.
Pia ina "swala, ibada, amri na miito", ambayo ni misingi ya shrai'ah, pamoja na vipengele vyote.
Quran ni kitabu cha dhikr inayomfanya mwanadamu apate angalau thawabu kumi kwa herufi yake moja anapoisoma; pia ni kitabu cha elimu ambapo kinamtambulisha Allah pamoja na majina Yake na sifa Zake.
Misingi ya njia zote za kweli ipo katika Quran. Kila mti wa matunda unatambua matunda mbalimbali kwa kuzingatia maumbo yao ulimwenguni; halikadhalika, kila mwanazuoni wa tafsiri hutambua maana mbalimbali katika Quran, anapata milango ya elimu mbalimbali, anafunuliwa udhihirisho wa majina tofauti ya Allah na inaleta njia tofauti ya uongofu. Kwa kipengele hiki, Quran inakuwa kama maktaba ingawa ni kitabu kimoja. (angalia Badiuzzaman Said Nursi, Sözler (Maneno) , Yirmi Beşinci Söz (Neno la Ishirini na Tano).
4
Ni ipi miujiza ya Qur’an? Unaweza kutupa mifano?
Kila aya ya Qur’an ni muujiza. Kwahiyo haiwezekani kuelezea miujiza yote iliyomo katika Qur’an hapa. Baadhi ya miujiza hiyo ni kama ifuatayo:
1- Katika aya “Mwenyezi Mungu ndie aliye ziinua mbingu mnazo ziona bila ya nguzo” (ar-Ra’d, 2) inapinga dhana potofu kwamba mbingu zimeeinuliwa kutokana na uwepo wa milima
2- Uumbaji wa ulimwengu unaelezwa kama ifuatavyo katika Qur’an: “Yeye ndiye Muumbaji wa mbingu na ardhi bila ya ruwaza” (al-An’am, 101). Aya hii inatueleza ukweli juu ya uumbaji wa ulimwengu miaka 1400 iliyopita, kutokana na mapitio ya muda na mahala, ikafanyika dunia kutokana na mripuko unaojulikana kama big bang, ambayo ndiyo nukta ya mwisho iliyofikiwa na Sayansi leo.
3- Ukweli kwamba dunia inatanuka kila uchao ni matokeo ya uvumbuzi kisayansi ambao ulimwengu wa sayansi unakubali sasa. Qur’an inalionesha jambo hilo kwa aya ifuatayo: “Na mbingu tumezifanya kwa nguvu na uwezo na hakika Sisi bila ya shaka ndio wenye uwezo wa kuzitanua.” (adh-Dhariyat, 47)
4- Uvumbuzi mwengine katika karne ya 20 ni kwamba kila nyota na kila kilicho mbinguni kinatembea katika njia yake inayojulikana kama ‘orbit’. Qur’an inalieleza jambo hili kama ifuatavyo: “Na Yeye ndiye aliye umba usiku na mchana na jua na mwezi, vyote katika anga vinaogelea (katika njia zake maalum).” (al-Anbiya, 33)
5- Zamani, ilifikiriwa kwamba jua halizunguki. Ingawa Qur’an inaeleza kwamba jua halijasimama; kinyume chake, inaeleza kuwa jua ni ni kati ya maumbo ya mbinguni ambalo hutembea kwa kasi maalumu. Sayansi imeyathibitisha yaliyoelezwa na Qur’an baada ya karne nyingi. Aya inayohusiana na hilo ni hii: “Na jua linakwenda kwa kiwango chake. Hayo ni makadirio ya Mwenye nguvu, Mwenye kujua.” (Ya Sin, 38)
Miujiza ya kijiolojia ndani ya Qur’an:
Kupungua kwa kiwango cha ardhi:
Allah anatufahamisha baadhi ya siri zake katika uumbaji ndani ya Qur’an ambayo aliiteremsha karne 14 zilizopita. Siri hizo zinathibitisha yote mawili kuwa Qur’an ni neno la Allah na inatoa mwanga kwa maendeleo ya sayansi za kimaumbile.
“Je! Hawakuona kwamba tunaifikia ardhi tukiipunguza nchani mwake?...” (Ar-Raad, 41)
“…. Je, hawaoni ya kwamba Sisi tunaifikia ardhi tukiipunguza ncha zake?...” (al-Anbiyaa, 44)
Kutokana na ongezeko la joto duniani ‘global warming’, tabaka la barafu katika ncha za dunia zinayeyuka na kiwango cha bahari kinaongezeka. Kiwango cha maji kinachobaki hufunika eneo la ardhi. Kwa kadri fukwe za bahari zinavyofunikwa na maji, kiwango cha ardhi kinapungua. (Dr. Mazhar U. Kazi, 130 Miujiza dhahiri ndani ya Qur’an, Crescent Publishing House, New York, USA, 1998, s. 115). Inawezekana kabisa maneno yanayosema “Sisi tunaifikia ardhi tukiipunguza ncha zake “ yaliyotajwa katika Qur’an yanataja jinsi fukwe za bahari zinavyofunikwa na maji.
Habari inayohusu hilo iliyochapishwa kwenye gazeti la New York Times iko kama ifuatavyo:
Katika karne iliyopita, kiwango cha hali joto cha dunia kimeongezeka kwa kiwango cha nyuzi joto 1, na kiwango cha joto kimeongezeka kwenye robo ya mwisho ya karne iliyopita. Wanasayansi walilinganisha takwimu kutoka uchunguzi uliofanywa kupitia nyambizi (submarines) kati ya miaka ya 1950 na 60 pamoja na uchunguzi uliofanywa miaka ya 90, unaoonesha kuwa tabaka la theluji (barafu) kwenye ukanda wote wa Arctic umeliwa kwa asilimia 45. Picha za satalaiti zimeonesha kuwa kiwango cha tabaka la barafu kimepungua kwa kasi katika miaka ya hivi karibuni. (www.planetwaves.net/polar_NYT.html; New York Times, 19/08/2000)
Uvumbuzi uliofanywa mwishoni mwa karne ya 20 ulitusaidia kufahamu hekima ya aya ya 44 katika suratu Al-Anbiya na aya ya 41 katika suratu Ar-Rad.
Mgawanyo wa mabara
Dunia inatembea juu ya tabaka linalojulikana kama ‘mantle’, ambalo ni zito zaidi, kama ambavyo imeweza kuhimili dunia kuogelea juu yake. Mwanasayansi wa Kijerumani anaejulikana kwa jina la Alfred Wegener aligundua kwa mara ya kwanza kwamba mwanzoni mwa karne ya 20 mabara yote yalikuwa kitu kimoja mwanzoni kabisa na hatimae yakaparaganyika kwenye uelekeo tofauti na kila moja likamkimbia mwenzake.
Kwa takriban miaka milioni 500 iliyopita, mabara yote yalikuwa yameungana, na ardhi hiyo ilijulikana kwa jina la kitaalamu kama pangea ilipatikana ncha ya Kusini mwa dunia. Kwa takriban miaka 180 iliyopita, pangea ikagawanyika kwenye mapande mawili makubwa. Moja katika mapande hayo makubwa, yaliyogawika mabara mawili makubwa yalielekea sehemu tofauti, na kufanya Afrika Australia, Antarctica na India; na lile bara la pili likazaa, bara Ulaya, Amerika ya Kaskazini na bara la Asia isipokuwa India.
Ilikadiriwa kuwa utembeaji wa mabara ulikuwa ni tabkriban sentimita 1 hadi 5 kwa mwaka. Kwa kadri ambavyo tabaka zikitembea hivyo, kulitokea mabadiliko kwenye jiografia ya dunia. (nyaraka za Carolyn, Robert Gardner, Samuel F. Howe, General Science, Allyn na Bacon Inc.Newton, Massachusetts, 1985, uk. 305)
Allah ametaja utembeaji wa milima kama mpasuko wa mabara ‘drifting’. Neno la Kiingereza ambalo wanasayansi hulitumia kwa utumbeaji huo wa mabara ni “continental drift”
“Na unaiona milima unaidhania imetulia; nayo inakwenda kama mwendo wa mawingu.” (An-Naml, 88)
Ardhi imeundwa kwa tabaka saba:
Baadhi ya taarifa zinazotolewa na Allah katika Qur’an kuhusu dunia ni kwamba dunia ina tabaka saba sawa na mbingu: “Mwenyezi Mungu ni yule ambaye ameziumba mbingu saba, na ardhi kwa mfano wa hizo…” (at-Talaq, 12) Mola wetu ameelezea kwamba ardhi na mbingu zina tabaka saba saba. Ambapo matokeo ya sayansi kupitia tafiti zilizofanywa baada ya karne kadhaa zimegundua vile vile.
Tabaka za dunia ambazo wanasayansi wameziorodhesha ni: Tabaka maji (Hydrosphere), Lithosphere, Asthenosphere, Mantle ya juu, Mantle ya chini, kiini cha nje (outer core) na kiini cha ndani (Inner Core):
Hysdrosphere inajumisha sehemu za juu za bahari na fukwe za ardhini zinazoathiriwa nazo. Lithosphere ni tabaka la mwamba mgumu ambao hufanya sehemu ya juu ya ardhi. Iikilinganishwa na tabaka zingine, ni jembamba, baridi na gumu zaidi; na kwa mantiki hiyo, hufanya kazi kama jabali la dunia.
Chini ya Lithosphere, kuna tabaka linaloitwa Asthenopshere. Tabaka hili lina vitu ambavyo vina joto na ugumu wa kati na kati kiasi cha kuweza kuyayuka vinapopata joto kali, na mgandamizo. Inafikiriwa kuwa tabaka hilo gumu la Lithosphere huelea au kutembea juu ya tabaka lijulikano kama Asthenosphere, tabaka ambalo hutembea taratibu sana. Chini ya tabaka hili, kuna tabaka jengine ambalo lina miamba ambayo ina ugumu wa kati na kati na ni joto sana; na lina upana wa kilomita 2.900 ambalo hujulikana kwa jina la kitaaluma kama Mantle. Mantle, ambayo ina madini chuma, magnesium na calcium kuliko tabaka la crust, ni joto zaidi na zito kwasababu hali joto na mgandamizo kwenye ardhi huongezeka kwa kadri ya ongezeko la kina cha urefu.
Katikati ya dunia kuna tabaka jengine lijulikanalo kama Core, ambalo ni zito mara mbili zaidi ya Mantle. Kinachosababisha uzito huu ni ukweli kwamba lina madini chuma aina ya metals (mchanganyiko wa iron-nickel) tofauti na majabali. kiini cha ardhi lijulikanalo kama Core limeundwa na sehemu mbili tofauti. Moja ni sehemu ya nje ya maji maji ijulikanayo kama liquid outer core, yenye upana wa kilomita 2.200; ambapo jengine ni tabaka gumu lijulikanalo kama solid outer core, lenye upana wa kilomita 1.250. Kwa kadri dunia inavyozunguka, sehemu ya maji kuwa sehemu yenye mvutano wa sumaku wa dunia.
Jambo la muhimu sana katika yote ni kwamba ukweli huu wa kisayansi ambao unaweza kujulikana kwa kutumia teknolojia tu ya karne ya 20 ulishaelezwa ndani ya Qur’an, ambapo ni mifano michache ya miujiza mingi ndani ya Qur’an.
Mpasuko wa ardhi:
“Naapa kwa mbingu yenye marejeo! Na kwa ardhi inayo pasuka!” (At-Tariq, 11-12)
Neno la kiarabu ‘sada’ limetajwa katika aya likimaanisha nyufa, kupasuka, kutengana n.k. Ukweli kwamba Allah anaapa juu ya kupasuka kwa ardhi ni muujiza mwengine ndani ya Qur’an.
Kwa mara ya kwanza wanasayansi mwaka 1945-46 walikwenda kwenye kina kikubwa chini ya bahari ili kutafiti rasilimali. Moja katika nukta za msingi za tafiti ilikuwa ni nyufa na mipasuko kwenye muundo wa ardhi. Tabaka la mwamba mgumu kwenye sura ya dunia ilikuwa na mwelekeo wa kaskazini-kusini na mashariki-magharibi na lilikuwa limefanya nyufa kwenye maeneo mengi kwa masafa ya maelfu ya kilomita. Shukrani kwa nyufa katika muundo wa ardhi, kiwango kikubwa cha joto kinapunguzwa na kiasi kikubwa cha miamba iliyoyeyuka inafanya vijimilima baharini. Lau kama dunia haikuwa na muundo ambao unaruhusu kiwango kikubwa cha joto kutolewa nje, maisha duniani yasingewezekana kwasababu, kwa hali kama hii, joto ambalo lisingepata sehemu nyengine ya kutokea chini ya ukonde wa ardhi ingesababisha kiasi kikukbwa cha athari hasi za nyuklia.
5
Kwanini Quran iliteremshwa?
Quran iliteremshwa ili kuwafanya watu na majini, waliowajibishwa kwasababu wana akili na utashi, wafahamu ibada kama ilivyoelezwa katika aya ifuatayo: [Nami sikuwaumba majini na watu ila waniabudu Mimi.” (adh-Dhariyat, 56)] na kupata furaha kamili duniani na ahera. Quran si neno lisilo na malengo: [Wala si mzaha.”(at-Tariq, 14)] ni vigezo na kaida timilifu zinazobainisha ukweli mbali na uongo, jema dhidi ya ovu na zuri dhidi ya baya.
Ni sifa ya bainishi ya Quran, ambayo lengo lake la kipekee ni uongofu na furaha kwa wanadamu, kutumia mtindo unaolingana na lengo hilo, wakati mwingine kuiambia akili, wakati mwingine hisia, wakati mwingine dhamiri na wakati mwingine nyoyo za wasomaji wake, ili kuvutia nadhari zao kwenye mataifa yaliyotangulia, mbingu na ardhi, himaya ya mimea na wanyama, ukweli mwingi wa kisaikolojia, kifalsafa na kimaadili na kuwaomba wasomaji wake wayatafakari masuala hayo.
Kama Muhammad Asad anavyoliweka hilo, “Kamwe kitabu chochote - ikiwemo Biblia – kilichosambazwa kwa watu wengi, na kwa muda mrefu sana, hakijatoa jibu lenye kufahamika la swali hilo:
“Nifanyaje ili nipate maisha mema duniani na furaha katika ahera?”
Quran inaendelea kuwa juu ya sifa zote za kibinaadamu kama vile jiografia na mbari; haitaji majina kamili ya watu na mahali inapopataja; inawapa watu mafundisho ya elimu ya ujumla kwa kuyataja hayo.
Quran ni kielekezi cha uokovu wa wanadamu wote katika zama zotena mahali kwa ujumla. Ni kielekezi chenye kuonesha njia za ufumbuzi kwa waumini na hususani walio katika mgogoro na matatizo. Dhana ya kuongoza (hidayah kwa Kiarabu) inayoashiria njia ya kutokea kwa wale wasiojua upande wa kwenda jangwani inatangamana na nafasi nya Quran kwa ajili ya wanadamu wote.
Quran, inayosema kuwa mwanadamo yupo katika hasara kwa kuapa kwa neno zama {al-Asr, 1-2}, ni “mbinu ya uokovu” na “chelezo” kwa ajili ya mwanamume, aliyevurugikiwa kwasababu ya migogoro ya kiroho, mmomonyoko wa kimaadili na matatizo ya kijamii katika nyakati zilizopita na leo.
“Hiki ni Kitabu tulicho kiteremsha kwako ili uwatoe watu kwenye giza uwapeleke kwenye mwangaza, kwa idhini ya Mola wao Mlezi, uwafikishe kwenye Njia ya Mwenye nguvu, Msifiwa!” Ibrahim, 1
Njia pekee ya ufumbuzi kwa jamii iliyopoteza maadili yake na sifa zake nzuri na ambayo hali yake ya sasa na ya ijayo imepata giza la kukosa ustawi na furaha imeoneshwa katika Kitabu cha Allah kama ifuatavyo:
“Bila shaka imekujieni kutoka kwa Mwenyezi Mungu nuru na Kitabu kinacho bainisha. Mwenyezi Mungu huwaongoa wenye kufuata radhi yake katika njia za salama, na huwatoa katika giza kuwapeleka kwenye nuru kwa amri yake, na huwaongoa kwenye njia iliyo nyooka.“ (al-Maida, 15, 16)
Itikadi za kibinadamu, zinazokuja pamoja na tamko kuwa zitatatua matatizo ya wanadamu, hupunguza matatizo kwa majibu yake ya muda mfupi na yasiyokamilika; kwa upande mwingine, Quran inatoa njia za kudumu na kamilifu za uokovu zinazofaa katika kila zama na mahali. Quran inamfananisha mtu anayejaribu kutatua matatizo kwa kutumia majibu yaliyotolewa na wanadamu kama mtu asiyejiweza anayetembea hatua chache pindi radi yenye mwanga mkali wa kufifisha macho inapopiga katikati ya giza na kisha anasimama {2/20}. Quran inaelekeza kwenye lililo sahihi zaidi. {17/9}. Kwa kuwa, ni ukweli kamili. {13/1; 17/105}.
“Enyi watu! Yamekujieni mawaidha kutoka kwa Mola wenu Mlezi, na poza kuponyesha yaliyomo vifuani, na uwongofu, na rehema kwa Waumini. Sema: Kwa fadhila ya Mwenyezi Mungu na rehema yake! Basi nawafurahi kwa hayo. Haya ni bora kuliko hayo wanayo yakusanya.” (Yunus, 57-58)
Quran ni ponyo na faraja, na kwa hivyo ni rehema, kwa ajili ya maradhi na matatizo yote. Nyoyo zilizofifia kwasababu ya uchafu wa kiroho na madhambi na zilizogeuka sugu na kupata maradhi {2/10; 6/43; 8/49} zinaweza kutakasika, kulainika na kuponywa kwa Quran:
“Kisha ngozi zao na nyoyo zao hulainika kwa kumkumbuka Mwenyezi Mungu.” (az-Zumar, 23)
“Wale walio amini na zikatua nyoyo zao kwa kumkumbuka Mwenyezi Mungu. Hakika kwa kumkumbuka Mwenyezi Mungu ndio nyoyo hutua!“ (ar-Rad, 28)
Kwa hivyo, Quran inakuwani ponyo na rehema kwa ajili ya watu ambao nyoyo na akili zao zimevurugika kwasababu ya ghiliba za kishetani. Nyoyo za watu wenye kuondokana na matatizo na maradhi hayo zinaongoka na uoni wao unakuwa hai.
“Hii (Qur'ani) ni hoja zinazo toka kwa Mola wenu Mlezi, na uwongofu na rehema kwa watu wanao amini. “ {7/203; 45/20}
Quran ni kitabu kitukufu ambacho {6/155}, kama Hadhrat Umar (ra) anavyoliweka hilo, “Allah hufungua macho yaliyofumba, masikio yasiyosikia na nyoyo zilizofungwa kwa kutumia Qur’an.”
Jina mojawapo la Quran ni “dhikr”, yaani, mawaidha; na jina jingine ni “tadhkira” yaani mwonyaji na mkumbushaji. Quran ni mkusanyiko wa mawaidha na maonyo yanayomfundisha na kumkumbusha mwanadamu juu ya majukumu yake na yanayomwongoza kwenye heri na ukweli:
“Hili ni Tangazo liwafikie watu, liwaonye, na wapate kujua kuwa hakika Yeye ni Mungu Mmoja, na wapate kukumbuka wenye akili.” (Ibrahim, 14/52)
Quran inamfahamisha mwanadamu kuhusu majukumu yake kwa upande wake yeye mwenyewe, Mola wake Mlezi, watu wengine na maumbile. Inawafundisha wale wasiotambua majukumu yao na inawakumbusha wale wanaoyasahau majukumu yao. Inawaonya vikali wale wasiotimiza majukumu yao kwa makusudi.
Rejea kuu kwa kila Muislamu anayeuchagua Uislamu kuwa ni dini yake na anajisalimisha kwa Allah ni Quran. Atajifundisha kanuni za maisha zitakazomletea furaha duniani na ahera kutokana na Quran. Atajifundisha kinachohitajika kuamini na cha kukataa, kipi ni chema na halali na kipi ni kiovu na haramu, anachotakiwa kufanya na anachotakiwa kukiepuka kutokana na Quran. Atautakasa moyo wake, kuuimarisha na kujisalimisha kwa Allah na kuhuisha imani yake na msisimko wake kwa Qur’an. {9/124; 16/102}
“Na inapo teremshwa Sura wapo miongoni mwao wasemao: Ni nani miongoni mwenu Sura hii imemzidishia Imani? Ama wale walio amini inawazidishia Imani, nao wanafurahi.“ (at-Tawba, 9/124)
“Sema: Ameiteremsha hii Roho takatifu kutokana na Mola wako Mlezi kwa haki, ili awathibitishe wale walio amini, na kuwa ni uwongofu, na ni bishara kwa Waislamu.” (an-Nahl, 16/102)
Atajifundisha mazuri ya Peponi na kitisho cha mateso ya Jahanamu kutoka katika kitabu kitukufu cha Allah; Hivyo, atajitahidi kuendesha maisha bora na atatenda kwa umakini zaidi ili kuepuka madhambi na amali mbaya. Kwa kifupi, muumini atapata kila kitu katika Qur’an kuhusu jinsi ya kufanya ili apate radhi za Allah:
“Na tumekuteremshia Kitabu hiki kinacho bainisha kila kitu, na ni uwongofu, na rehema, na bishara kwa Waislamu.” (an-Nahl, 16/89)
Hata hivyo, mtu asihitimishe kutokana na aya hii kuwa Quran ni ensaiklopidia au kitabu cha sayansi. Si kitabu kinachotaja nadharia za muda mfupi za kisayansi; ni mwogozo wa maisha. Ni kitabu cha mwongozo kilichotumwa na Allah, aliyetuumba sisi na anayeyajua zaidi maumbile yetu kuliko sisi; kinatuonesha jinsi ya kutumia viwiliwili vyetu vya kupita katika dunia hii ya mpito:
“Si maneno yaliyo zuliwa, bali ni ya kusadikisha yaliyo kabla yake, na ufafanuzi wa kila kitu, na ni uwongofu na rehema kwa kaumu yenye kuamini.” (Yusuf, 12/111)
Quran ni neno sahihi la mwisho la Allah. Wanadamu, waliohutubiwa kwa njia ya ufunuo tangu Hadhrat Adam (as), mtu wa kwanza, ambapo Quran, ambayo ni hazina bora inayothibitisha yaliyo kweli katika mafundisho yaliyotangulia ya upwekeshaji, yaliyosahaulika, yaliyopotea au kubadilishwa na inasahihisha makosa yaliyomo ndani mwao. Wanadamu wanaweza kujua upi ni ukweli wa kiungu na lipi si sahihi na ushirikina, shukrani ziiendee Quran, ambayo ni “Furqan” (Kipambanuzi baina yake na shari).
Quran kwa hakika ni kipimo kwa ajili ya Waislamu. Akili ya Muislamu, mtizamo wa kidunia na mwenendo unapaswa ufundishwe na Quran. Anapaswa kuangalia kila kinachomjia kwa jina la elimu na utamaduni wa Kiislamu kwa utumia Quran, moja baada ya kingine; na anapaswa apambanue baina ya lililo sahihi na lisilo sahihi, la kweli na la kishirikina, lilo bora na lililozushwa.
Isisahaulike kwamba fursa adhimu ya Uislamu ni kwamba wafuasi wake wanayo Furqan, (mpambanuzi) kitabu ambacho hakijakumbwa na mabadiliko yoyote, kilichopo chini ya hifadhi ya Allah na kitakachobakia kuwa ni kigezo kisicho na doa kinachopambanua baina ya ukweli na uongo. Ni kitabu kisicho na kasoro hata chembe.
Waumini hufanya rejea kwenye Quran ili kujifundisha siri za dunia na ahera; pia hurejea kwenye Quran na sunnah bora ya Mjumbe wa Allah, ambaye ni Quran hai, kuhusu masuala wasiyoafikiana.
Kwa kifupi, Quran ni kitabu kitukufu cha rejea ambacho thamani yake kamwe haitapungua mpaka Siku ya Kiama kwa ajili ya waumini. Kitabu hiki cha hazina ndicho rejea pekee ambayo waumini watafanya rejea ili kutatua namna zote za matatizo ya kiroho yakiwemo masuala wasiyoafikiana.
Quran si kitabu kinachoshughulikia baadhi ya mambo ya kihistoria, kijamii, kifalsafa na kimaadili kwa njia ya kinadharia. Hata hivyo, kinalenga katika kuiweka jumuia iliyoundwa kwa maadili ya kidunia na kanuni za kiroho zinazoziweka. Inalenga kwenye kuondoa kila kinachohusiana na ukosefu wa fadhila na shari na kuwafanya wanadamu wote wajisalimishe kwa Allah, yaani, Uislamu, kama ilivyobadili mojawapo kati ya jamii za kijinga zaidi duniani na kuwa jamii bora zaidi {2/193}; ni kitabu cha kimapinduzi. Quran iliteremshwa ili itekelezwe kivitendo na watu waitii.
"Fuateni mliyo teremshiwa kutoka kwa Mola Mlezi wenu, wala msifuate rafiki au walinzi wengine badala yake. Ni machache mnayo yakumbuka." (al-Araf, 7/3)
Kila anayeiamini Quran, kimsingi, Mtume (s.a.w), anaitii na kushikamana na kanuni ilizoziweka:
“Basi wewe yashike yaliyo funuliwa kwako. Hakika wewe uko kwenye Njia Iliyo Nyooka. Na hakika haya ni ukumbusho kwako na kwa kaumu yako. Na mtakuja ulizwa. “ (az-Zukhruf, 43/43, 44)
Quran “ni kitabu kitukufu cha Allah ambacho hamtapotea kamwe kama mtashikamana nacho.” {Ibn Majah} ni kamba imara ya Allah itakayokupelekeni kwenye mwangaza, ukomavu, na heshima kama mtaishikilia; Hakuna kulazimishana katika dini. Ukweli utajitokeza dhahiri mbali na uongo; mwenye kukataa Uovu na akamwamini Allah atakuwa amekamata kishikizo cha kutumainia, kisichovunjika.”
“Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusikia, Mwenye kujua.” (al-Baqara, 2/256); {al-Baqara, 2/256, 257; Aal-i Imran, 3/103}
“Na shikamaneni kwa Kamba ya Mwenyezi Mungu nyote pamoja, wala msifarikiane. Na kumbukeni neema ya Mwenyezi Mungu iliyo juu yenu: vile mlivyo kuwa nyinyi kwa nyinyi maadui naye akaziunganisha nyoyo zenu; kwa neema yake mkawa ndugu. Na mlikuwa ukingoni mwa shimo la Moto, naye akakuokoeni nalo. Namna hivi Mwenyezi Mungu anakubainishieni Ishara zake ili mpate kuongoka.” (Aal-i Imran, 3/103)
Jamii inayoshikamana na kamba ya Allah na kutii kanuni za ufunuo inakuwa na furaha duniani na ahera. Wale wanaoupa mgongo ukweli wa kiungu na kukiacha kitabu kitukufu cha Allah kwa kutokukitii watakosa furaha katika sehemu zote mbili za ulimwengu.
Kanuni za kimaadili, nasaha na mapendekezo yaliyo katika Quran yanakuwa muhimu yanapotekelezwa kivitendo. Mathalani, nasaha zifuatazo za kiungu hazitakuwa na manufaa yoyote kama hazitafanyika kivitendo:
“Wala msikaribie uzinzi. Hakika huo ni uchafu na njia mbaya.”
“Wala msiuwe nafsi ambayo Mwenyezi Mungu amekataza isipo kuwa kwa haki...”
“Wala msiyakaribie mali ya yatima...”
“na timizeni ahadi. Kwa hakika ahadi itasailiwa. (katika Siku ya Hesabu).”
“Na timizeni kipimo mpimapo. Na pimeni kwa mizani zilizo sawa...”
“Wala usiyafuate usiyo na ujuzi nayo. Hakika masikio, na macho, na moyo - hivyo vyote vitasailiwa. (katika Siku ya Hesabu).”
“Wala usitembee katika ardhi kwa maringo. Hakika wewe huwezi kuipasua ardhi wala kufikia urefu wa milima.”
“Haya yote ubaya wake ni wenye kuchukiza kwa Mola wako Mlezi. “ (al-Isra, 17/32-38)
Kitabu cha Wazi Wazi, Chenye Kufahamika, Kilichorahisishwa:
Kama inavyoonekana katika aya 32-38 za sura ya al-Isra tulizozinukuu kama mfano hapo juu, aya za Quran zina kanuni zenye kutendeka zinazoweza kufahamika hata kwa jumuia yenye ujinga mwingi. Quran haina utatanishi, wala kutokufahamika, wala kitabu cha kale kinachoweza kufahamika kwa wataalamu, wanasayansi na maulamaa tu au chenye alama za siri zinazoweza kutafsiriwa nao peke yao. Hukaririwa mara kwa mara kwa ujumla mwanzoni mwa sura za Quran ambapo Quran na aya zake viko wazi na vyenye kufahamika.
Katika Quran, kila kitu kimeelezwa “kupitia mifano mbalimbali” {18/54; 20/113} na kwa kina {6/55, 56, 126; 41/2-3}. Quran imerahisishwa ili ifahamike kupitia sitiari na mifano:
“Na bila ya shaka Sisi tumeifanya Qur'ani iwe nyepesi kufahamika. Lakini yupo anaye kumbuka?” (al-Qamar, 54/17, 22, 32, 40)
“Kwakuwa wale wa mwanzo waliohutubiwa na Quran hawakujua kusoma na kuandika, Shari'ah tukufu za Uislamu zilikuwa rahisi. Shari'ah iliteremshwa katika mfumo ambao ungefahamika na kutekelezwa kwa urahisi na wale wanaohutubiwa bila ya kuhitajika elimu yoyote au ubobezi. Kudai kinyume chake ni kinyume na msingi wa Shari'ah. Watu wa mwazo kuhutubiwa hawakujua kusoma na kuandika; kwa hivyo, shari'ah iliyoteremshwa ilikuwa nyepesi. Vinginevyo, wangesema, “Iko juu ya kiwango chetu; haifanani na maneno yetu; hayo ni maneno tusiyoyajua au kuyafahamu, n.k...” {41/44}.
Licha ya hivyo, Allah anaeleza, “Mwenyezi Mungu haikalifishi nafsi yoyote ila kwa kadiri ya iwezavyo.” {2/286}; “Wala (Allah) hakuweka juu yenu mambo mazito katika dini” {22/78}. Kwa sababu za kiutekelezaji, Shari'ah ilibidi iteremshwe katika lugha na mtindo ambao ungeweza kufahamika kwa kila mtu.” Shatibi
Quran imeelezewa kama ifuatavyo katika hadithi:
“Baadhi ya watu ni watu wa Allah. Mjumbe wa Allah alipoulizwa, 'Ni kina nani hao?', Alisema, 'Hao ni watu wa Quran; hao ni watu wa Allah na marafiki zao.” (Tirmidhi)
“Rehema na wingi humiminikia mahali na malaika na utulivu huzingira mahali ambapo muumini anasoma Quran kwa unyoofu na kwa kutaka radhi za Allah.” (Tirmidhi)
Harith al-Awar anasimulia: “Pindi tulipokuwa tunapita njia ya msikitini, niliwakuta watu wameacha kumtaja Allah na kuingia katika mazungumzo yasiyofaa. Kwa hivyo, nilimwendea Hadhrat Ali (ra) na kumwambia niliyoyaona.
Akaniuliza, 'Unasema kweli, ni hivyo?'
Nilipomhakikishia kuwa hivyo ndivyo ilivyokuwa, alisema: 'Nilimsikia Mjumbe wa Allah akisema,
“Tazama! Mfarakano utatokea! Hapo hapo nikamuuliza: ‘Ni ipi njia ya kujinusuru nao? Ewe Mjumbe wa Allah! Alijibu: Ni kutii kitabu kitukufu cha Allah.
Kina habari zote kuhusu yaliyowatokea jumuia za kabla yenu, habari za mifarakano na misukosuko itakayotokea baada yenu na ishara za Siku ya Kiama.
Pia ina hukumu kuhusu mambo yatakayotokea miongoni mwenu (kuhusu mambo kama vile imani-ukafiri, utii-uasi, kilichoruhusiwa-kilichokatazwa, n.k.). Ni kipambanuzi baina ya ukweli na uwongo.
Iko makini katika kila inachokitaja, Hakuna neno ndani mwake ambalo ni la kupita bure tu au la nje ya mada. Mwenye kuangukia katika upuuzi kwa kutokukizingatia na kutokutenda kulingana nacho, Allah atamwangamiza. Kama yeyote atatafuta uongofu mahali pengine Allah atamwacha apotee.
Ni kamba madhubuti ya Allah. Ni ukumbusho wa hekima, na ni njia iliyonyooka kabisa. Inahifadhi nafsi zinazoitii zisiharibiwe na upotovu na ndimi zenye kuisoma dhidi ya kutatizika. Wanazuoni wa Qur’an daima hutamani zaidi yaliyomo ndani mwake. Kukisoma mara kwa mara hakumchoshi msomaji wake; wala msomaji hapotezi ladha kwa kurudiarudia kukisoma. Mastaajabu yake makubwa yanayowashangaza wanadamu hayaishi kamwe.
Ni aina ya kitabu ambacho, pindi walipokisikia, majini iliwabidi wakiri kuwa, 'Hakika sisi tumeisikia Qur'ani ya ajabu. Kwa hakika Inaongoza kwenye uwongofu, kwa hivyo tumeiamini.' (Surah al-Majini, 72/1-2) Mwenye kukitamka, atakuwa anasema ukweli. Mwenye kutenda kulingana nacho atalipwa. Mwenye kuhukumu kulingana nacho, atakuwa mwadilifu. Mwenye kuwalingania watu kukiendea, atawaongoza kwenye njia iliyonyooka. Ewe Awar! Jifundishe vyema maneno haya mazuri.” (Tirmidhi)
Kwa muhtasari, Quran, “Ni kitabu cha muujiza”, kitakachokomesha siku za giza tunazoishi ndani mwake na matatizo na machungu tunayoumia na kitakachowaongoza wanadamu wote kwenye “furaha ya wote”, kiko katika utumiaji wetu kama hazina isiyo na kifani. Tunachohitajika kufanya ni kusoma hii “mbinu ya wokovu” kwa macho maangalifu ili tupate majibu ya maswali ya leo na kuwa na nguvu na msisimko uliokuwepo katika siku za mwanzoni mwa Uislamu.
Nyenzo:
(Kur'an Nedir, Nasıl Okunmalıdır, A. Yıldız-Ş. Özdemir, Pınar Yayınları)
6
Jee Qur’an imetaja uvumbuzi wa zama za sasa? Unaweza kutoa mifano?
Elimu ya falaki (Astronomy)
Haijulikani kabisa jinsi umbo la kwanza la ulimwengu lilivyopatikana. Inaweza isijulikane milele. Ingawa kuna baadhi ya nadharia ambazo zinaweza kuwa na ukweli na misingi fulani ya uhakika. Maelezo kwenye Qur’an kuhusu jambo hili yanaeleweka vyema pamoja na nadharia hizi:
“Je! Hao walio kufuru hawakuona kwamba mbingu na ardhi zilikuwa zimeambatana, kisha Sisi tukazibabandua? Na tukajaalia kwa maji kila kilicho hai? Basi je, hawaamini? “ (al-Anbiya, 21/30)
“Kisha akazielekea mbingu, na zilikuwa moshi…” (Fussilat, 41/11)
Mtazamo wa ujumla ambao upo kwa wataalamu wa fizikia ya kifalaki ni sawa na msingi ulioelezwa kwenye aya hizo.
Kuna dalili mbali mbali kwamba dunia ni duara.
“Ameumba mbingu na ardhi kwa Haki. Hufunika usiku juu ya mchana, na hufunika mchana juu ya usiku…” (az-Zumar, 39/ 5)
Neno takwir (yukawwiru) “kuingiliana” limetajwa katika aya likimaanisha kufunika kitu kilicho katika umbo la duara; kwa mfano kuzungushia kilemba kwenye kichwa.
Kwa mujibu wa Mahmud as-Sawwaf, hakuna ushahidi wa wazi kuhusu ima kuzunguka au kuto kuzunguka kwa dunia kwenye Qur’an au Sunnah. Ingawa, zipo dalili zinazoonesha kwamba dunia inazunguka:
“Na unaiona milima unaidhania imetulia; nayo inakwenda kama mwendo wa mawingu…” (an-Naml, 27/88)
Anazizingatia aya za hapo juu kama ni aya zinazoonesha kuwa dunia inazunguka.
Fizikia (Physics)
Kwa kadri mtu anavyopaa kwenda juu mawinguni, kiwango cha hewa ya oxygen angani kinapungua na mgandamizo wa hewa hushuka kufikia kiwango cha degree moja kila baada ya mita 100; hivyo basi, hupunguza uwezekano wa kupumua, na tatizo la kuona, na kutokea kwa kuzimia. Mtu akipanda juu kwa mita 20 000, hawezi kupumua ikiwa hana kifaa maalumu; na hatimae, atakufa. Qur’an imeutaja ukweli huu kwenye aya ifauatayo:
“Basi yule ambaye Mwenyezi Mungu anataka kumhidi humfungulia kifua chake kwa Uislamu. Na anaye taka apotee hukifanya kifua chake kina dhiki, kimebana, kama kwamba anapanda mbinguni…” (al-An’am 125)
Jiolojia (Geology)
Sayansi ya miamba imethibitisha kwamba milima ina ujazo kwenda chini sawa na ule unaoonekana juu ya ardhi.
“Kwani hatukuifanya ardhi kama tandiko? Na milima kama vigingi?” (an-Naba’, 78/6-7)
Katika aya ya hapo juu, Qur’an imeifananisha milima na vigingi ambavyo nusu yake huchomekwa ardhini. Aya ifuatayo pia imeelezea:
“Na milima akaisimamisha” (an-Naziat, 79/32)
Aya ifuatayo inaonesha kwamba milima, inayoelea kwenye bahari ya atmosphere, inaweka uzani sawa wa dunia:
“(…) na Ameweka katika ardhi milima ili ardhi isikuyumbisheni…” (Luqman, 31/10)
Katika sayansi ya miamba, inafahamika kuwa milima ni jambo muhimu sana katika kanuni ya kuweka usawa ijulikanyo kama isostasy katika karne hii. Kwa mujibu wa geophysics, kuna mapande mazito ya milima takriban 110 yajulikanayo kama “hot spots”. Mapande hayo ni matope mazito makubwa ya mchanganyiko ujulikanao kwa jina la kitaalamu “basalt compound” ambao huituliza ardhi kama vile rivets; yanatoka chini kabisa ya ardhi kwenye tabaka lijulikanalo kama mantle, hupenya ardhini na kuifanya kuwa ngumu sehemu ya nje ya ardhi, ili kuzuia ardhi isitembee. Mnasaba uliopo baina ya kile kinachoelezwa na aya [ndani ya Qur’an] na kile kinachoelezwa na sayansi, ambacho ni kama tafsiri tu ya aya zinazoelezea uumbaji ambapo imetajwa wazi kabisa.
Botany
Sayansi ya mimea
Jambo la mbolea (fertilization) kwenye miti limejulikana kwa muda mrefu ila uhusiano uliopo baina ya upepo na utoaji mbolea (fertilization) haukujulikana hadi siku za hivi karibuni.
“…Na katika kila matunda akafanya dume na jike…” (ar-Ra’d, 13/3)
Baada ya ukweli ulioneshwa kwenye aya hapo juu kugunduliwa na ikaonekana kwamba miti yote ina chembe chembe za kiume na kike na kwahivyo basi matunda huzaliwa kama matokeo ya mbolea (fertilization) kati ya dume na jike, ikafahamika kwamba mbolea (fertilization) pamoja na pollination hufanywa na upepo.
Urithi (Genetics)
“Na pale Mola wako Mlezi alipo waleta katika wanaadamu kutoka migongoni mwao kizazi chao, na akawashuhudisha juu ya nafsi zao, akawaambia: Je, Mimi si Mola Mlezi wenu? Wakasema: Kwani! Tumeshuhudia. Msije mkasema Siku ya Kiyama sisi tulikuwa tumeghafilika na hayo.” (al-A'raf, 7/172)
Wakati anaielezea aya hii, Sayyid Qutb ameandika, “Qur’an inakunjua pazia kwa kuelezea ukweli mzito, ambao ndio unaotaja asili ya mwanadamu. Maelezo haya ya Qur’an yalitolewa karne 14 zilizopita, wakati mwanadamu hakuwa na jicho lolote la kutambua ukweli wa uumbwaji wa mwanadamu, ukiachilia mbali dhana zisizo kuwa na msingi wowote. Sasa baada ya karne zote hizi, wanadamu sasa wametambua baadhi ya ukweli wa jambo hilo. Leo sayansi ya viumbe hai (biological science) inatueleza kuwa chembe hai (genes) zinahifadhi kumbukumbu ya kila mwanadamu, zikionesha sifa au tabia zake hali ya kuwa bado wako tumboni kwa mama zao. Chembe hai (genes) hizi, ambazo zinaweka kumbukumbu si chini ya wanadamu bilioni 3, zinaweza kuwekwa pamoja kwenye eneo ambalo halizidi kipimo cha cubic sentimita moja. Kupitia ukweli huu ulioelezwa kipindi hicho, ungalikumbana na dharau na shaka.
Allah anasema, Allah, who says,
“Tutawaonyesha Ishara zetu katika upeo wa mbali na katika nafsi zao wenyewe mpaka iwabainikie kwamba haya ni kweli. Je! Haikutoshi kwamba Mola wako Mlezi kuwa Yeye ni Shahidi wa kila kitu?” (Fussilat, 41/ 53)
Kwa hakika inaeleza ukweli mtupu
Sayansi ya alama za vidole (Dactyloscopy)
Tawi hili la sayansi linachunguza athari za vidole (fingerprints). Athari za vidole zinatofautiana kati ya binadamu mmoja na mwengine. Qur’an ilipoelezea kwamba mwanadamu atafufuliwa akiwa amekusanyiwa taarifa zake zote, inaashiria jambo hili.
“Anadhani mtu kuwa Sisi hatutaikusanya mifupa yake?. Kwani! Sisi tunaweza hata kuziweka sawa sawa ncha za vidole vyake!” (Qiyama, 75/3-4)
Biolojia (Biology)
Profesa mmoja wa masuala ya tiba, alizichunguza aya za Qur’an zinazohusu masuala ya uzazi, hasa aya ya 5 katika Suratu al-Hajj na aya ya 12 katika Suratu al-Muuminun na kuzilinganisha na taarifa za tafiti za sayansi ya viumbe katika zama zetu leo, na kusema kwamba zilikuwa sawa sawa na yale yanayozungumzwa na Qur’an ambazo hazikujulikana kabla ya karne ya 19 popote ulimwenguni. Akamalizia maneno yake kama ifuatavyo:
“Qur’an inaelezea ukweli kuhusu uzazi wa mwanadamu ambao wanadamu wataugundua kwa mamia ya miaka kwa kutumia njia rahisi sana”
Aya ambazo profesa alizitaja ni kama zifautazo:
“Enyi watu! Ikiwa nyinyi mna shaka ya kufufuliwa basi kwa hakika Sisi tulikuumbeni kutokana na udongo, kisha kutokana na manii, kisha kutokana na kipande cha damu ilio gandana, kisha kutokana na kipande cha nyama chenye umbo na kisicho kuwa na umbo, ili tukubainishieni. Nasi tunakiweka katika matumbo ya uzazi tunacho kitaka mpaka muda ulio wekwa. Kisha tunakutoeni kwa hali ya mtoto mchanga, kisha mfikie kutimia akili. Na wapo katika nyinyi wanao kufa, na wapo katika nyinyi wanao rudishwa kwenye umri wa unyonge kabisa, hata mtu awe hajui kitu baada ya kuwa anakijua. Na unaiona ardhi imetulia kimya, lakini tunapo yateremsha maji juu yake husisimka na kututumka, na kumea kila namna ya mimea mizuri (jike na dume).” (al-Hajj, 22/5)
“Na kwa yakini tumemuumba mtu kutokana na asli ya udongo. Kisha tukamjaalia awe tone ya mbegu ya uzazi katika kalio madhubuti. Kisha tukaiumba tone kuwa damu iliyo ganda, na tukaiumba damu kuwa pande la nyama, kisha tukaliumba pande la nyama kuwa mifupa, na mifupa tukaivika nyama. Kisha tukamfanya kiumbe mwengine. Basi ametukuka Mwenyezi Mungu Mbora wa waumbaji.” (al-Muminun, 23/12-14)
Usafi (Hygiene)
Kupitia maeleo yaliyotolewa katika Nyanja zote, Qur’an inamuwezesha mwanadamu kulinda usafi wa mwili na wa kiroho; na imeeleza sheria kamili za usafi, ambazo zimefahamika karne kadhaa baada ya kushushwa.
Qu’an inataja tasattur (kustiri mwili), ambalo ni jambo muhimu sana katika kanuni za usafi, kuvaa nguo safi, kupumzika vya kutosha, mlo kamili, kujiepusha kula vyakula vilivyooza na vibaya, vilevi, usaha, damu na nyama ya nguruwe na madhara ya zinaa, ambayo ndio chanzo cha magonjwa hatari sana.
7
Ikoje Taswira ya Quran kwa watu wa kitabu kitukufu (Wayahudi na Wakristo)?
Dini ya Kiislamu haioni kuwa washirikina (wanaomshirikisha Allah) wako sawa na watu wa kitabu kitukufu, ambao ni Wakristo na Wayahudi. Katika Surah Al-Maidah, Allah (SWT) anatangaza, Na chakula cha walio pewa Kitabu ni halali kwenu, na chakula chenu ni halali kwao. (Al-Maidah Surah, 5:5). Kunaweza kuwepo kufungamana nao kiuchumi na kibiashara. Sehemu ifuatayo ya aya inasomeka kuwa baadhi ya Waislamu wanaume wanaweza kuwaoa wanawake mabikra kutoka kwa watu wa kitabu kitukufu. Lakini Muislamu haruhusiwi kumwoa mshirikina.
Tunaona kuwa inafaa kuzionesha aya hizi za Qur’an zinazowahusu watu wa kitabu kitukufu:
Sema: “Enyi Watu wa Kitabu! Njooni kwenye neno lililo sawa baina yetu na nyinyi: Ya kwamba tusimuabudu yeyote ila Mwenyezi Mungu, wala tusimshirikishe na chochote; wala tusifanyane sisi kwa sisi kuwa Waola Walezi badala ya Mwenyezi Mungu.” (Al-i-Imran Surah, 3:64)
Wala msijadiliane na Watu wa Kitabu ila kwa njia iliyo nzuri kabisa, isipo kuwa wale walio dhulumu miongoni mwao. Na semeni: "Tumeyaamini yaliyo teremshwa kwetu na yaliyo teremshwa kwenu. Na Mungu wetu na Mungu wenu ni Mmoja. Na sisi ni wenye kusilimu kwake." (Al-Ankabut Surah, 29:46)
Hakika utawakuta walio shadidi kuliko watu wote katika uadui kwa walio amini ni Mayahudi na washirikina. Na utawakuta walio karibu mno kwa mapenzi ni wale wanao sema: “Sisi ni Manasara.” (Al-Maidah Surah, 5:82)
8
Je ni ishara kuwa Quran ilinakiliwa kutoka katika Taurati inapotaja majina ya Mitume waliotumwa katika Mashariki ya Kati?
Imesimuliwa katika hadithi kuwa mitume 124 000 walitumwa katika historia nzima ya mwanadamu. Kwa hakika, imeelezwa katika Quran kuwa mitume walitumwa kwenda katika ummah na jumuia zote.
“Hakika Mwenyezi Mungu hawadhulumu watu kitu chochote; lakini watu wenyewe wanajidhulumu nafsi zao.” (Yunus 44)
“Na kwa hakika kwa kila umma tuliutumia Mtume kwamba: Muabuduni Mwenyezi Mungu, na muepukeni Shetani." (an-Nahl 36)
Majina machache sana ya mitume hao yametajwa katika Quran. Mitume hao waliotajwa kwa majina waliishi Mashariki ya Kati.
Haiwezekani Quran itaje majina ya mitume 124 000. Kwa hakika, ingawa kulikuwa na mitume wengi walioishi Mashariki ya Kati mbali na ambao majina yao yametajwa katika Quran, majina yao hayakutajwa katika Quran.
Mitume waliotajwa katika Quran walikuwa ni wale waliokuwa wakijulikana katika jumuia hususani kwa Wakristo na Wayahudi. Malengo ya Quran ni kuwafundisha watu kwa kuwapa mifano kutokana na maisha ya Mitume ambao watu walioishi katika wakati huo waliwajua.
Ukweli kuwa Mitume waliotajwa katika Injili na Taurati pia wametajwa katika Quran unaonesha kuwa vitabu vyote hivyo ni neno la Allah na kwamba vyote vinatoka katika chanzo kile kile kimoja. Suala la kwamba yale yaliyotajwa hayakunakiliana kwa sababu kumwamini Allah, Mitume na Vitabu ni mambo yaliyomo katika vitabu vyote vya kiungu. Vitabu vyote vya kiungu na mitume viliteremshwa ili kuwajulishe watu kuhusu jambo husika.
9
Qur’an imesalimika vipi dhidi ya kugeuzwageuzwa?
Qur’an, maandiko matakatifu ya Allah na hutuba Zake za kiungu kwa wanadamu, iliteremshwa aya baada ya aya na sura baada ya sura katika miaka 23. Mtume alikuwa akizisoma aya na sura alizoteremshiwa kwa kuwasomea maswahaba zake, na wao wakawa wanazihifadhi na baadhi yao walikuwa wakiziandika. Licha ya hivyo, Mtume alikuwa na waandishi wa ufunuo. Wao hususani walikuwa na kazi ya kuandika aya na sura zilizoteremshwa.
Mtume alijulishwa kupitia kwa Malaika mkuu Jibril kuhusu mahali pa kuwekwa aya na sura zilizoteremshwa, pamoja na mpangilio wake katika Qur’an, na kisha Mtume akawa anawaeleza waandishi kuhusu ufunuo na kuweza kufanyika yaliyokuwa muhimu kufanyika. Qur’an yote iliandikwa katika muda alioishi Mtume na ilipangwa kipi kiwekwe mahali gani. Zaidi ya hivyo, Jibril alikuwa akija katika kila mwezi wa Ramadhani na alikuwa akimsomea Mtume aya na sura zote zilizoshushwa tangu mwanzo. Katika mwezi wa Ramadhani wa kabla ya Mtume hajafariki, Jibril alikuja tena, na kwa wakati huu waliisoma Qur’an mara mbili. Awali, Jibril alisoma, na Mtume alisikiliza; na baada ya hapo, Mtume alisoma na Jibril alisikiliza. Hivyo, Qur’an ilichukua umbo lake a mwisho.
Hata hivyo, katika wakati wa uhai wa Mtume Qur’an ilikuwa bado haijakusanywa katika kitabu kimoja. Ilikuwa imesambaa miongoni mwa maswahaba kama kurasa na ilihifadhiwa na maswahaba wengi. Hata hivyo, ilifahamika dhahiri na kwa hakika namna ya mpangilio wake wote.
Hatimaye, kutokana na kulazimika, katika wakati wa Halifa Abu Bakr, iliundwa kamati kutokana na waandishi wa ufunuo na mahafidhi hodari chini ya uongozi wa Zayd bin Thabit. Kamati hiyo iliteuliwa kwa ajili ya kuikusanya Qur’an katika kitabu kimoja. Kila swahaba alikuja na kukabidhi kurasa alizokuwa nazo za Qur’an. Kutokana na mgawanyo wa kazivya mahafidhi na waandishi wa ufunuo, kurasa, sura na aya zilipangwa kama alivyoeleza Mtume. Hivyo, Qur’an ilipangiliwa katika kitabu kimoja kilichoitwa Mushaf.
Matokeo yake, Qur’an imesalimika mbali na hali ya kusahaulika, kupotea, kugeuzwa au kubadiliswa, kwa kuwa iliandikwa sawa sawa na ilivyoteremsha kwa Mtume.
Kutokana na ulazima, katika wakati wa Halifa Uthman ibn Affan zilichapishwa nakala nyingi kutokana na kitabu hiki na kupelekwa katika sehemu mbalimbali. Nakala za Qur’an zilizopo sasa zinatokana na Qur’an hii.
Kutokana na ubora wa uimara wake, tofauti na Maandiko mengine Matakatifu, Qur’an iliwekwa katika hali ile ile ya ufunuo bila ya kugeuzwa kokote kwa hali yoyote wala kubadilishwa, na imetufikia kwa kuhifadhi uhalisi wake kwa miaka 1400. Ni dhahiri kuwa mtindo wa balagha na ufasaha wa Qur’an, hali yake ya kimuhtasari, wepesi wa kuihifadhi, kutokushabihiana na mhadhara wa kibinadamu, watu kushindwa kuiiga na kufikia kiwango chake cha umbuji, na uangalifu wa hali ya juu kabisa uliotumika katika kuihifadhi umechangia sana katika kutunza uhalisia wake. Hata hivyo, sababu halisi ni kwamba Allah aliiweka Qur’an katika hifadhi Yake na kwamba Ameahidi kuidumisha kama muujiza mpaka Siku ya Kiama kwa umbo na maana. Kwa hakika yafuatayo yanaelezwa katika Qur’an:
“Hakika Sisi ndio tulio teremsha Ukumbusho huu, na hakika Sisi ndio tutao ulinda.” (Qur’an, Al-Hijr, 15:9)
Leo, nakala zote za Qur’an zilizoko duniani ni za namna moja. Hakuna tofauti au ubadilishwaji. Licha ya hivyo, imehifadhiwa na mamilioni ya mahafidhi na inasomwa na mamilioni ya watu kwa wakati wote. Ubora huu haupo katika kitabu kingine chochote isipokuwa Qur’an, wala maandiko mengine yoyote ya kiungu. Ni muhimu kabisa kuwa Qur’an, ambayo ni maandiko ya mwisho ya Allah, ambayo kufaa kwake kunaendelea mpaka kiama, iwe na hadhi hii ya kipekee.
(Mehmed Dikmen, Islam Ilmihali, Cihan Yayinlari, Istanbul, 1991, uk. 94-97.)