FAQ katika kifungu cha Uislamu

1 Uislamu ni nini? Unaweza kutoa maelezo ya kina kuhusu Uislamu?

UISLAMU NI NINI?

Maana ya Neno Uislamu Kilugha

Kilugha, Uislamu unamaanisha kujisalimisha, kunyenyekea na kutii. Dini hii ndio inaitwa Uislamu kwa sababu ni dini yenye msingi wa kusalimu amri za Allah na kuzitii.

Maana Yake Kiistilahi

Ni njia ya maisha, mfumo wenye misingi ya imani na matendo ya kuwafanya watu wapate furaha kamili duniani na ahera, iliyotumwa na Allah na kufikishiwa watu kupitia kwa mitume. Uislamu ni sheria ya kiungu inayowaongoza watu wenye akili kuelekea mambo mazuri kulingana na hiari zao. 

Yaliyomo katika Uislamu

Maana ya Uislamu ni kujisalimisha: kujisalimsha kwenye amri na makatazo ya Allah. Uislamu hautakuwepo bila ya kujisalimisha kwenye hukumu za Allah. (Angalia al-An'am, 162 na an-Nisa, 65) Mwanadamu ni mja aliyeumbwa na Allah.

Kwa kuwa Allah amekizingira kila kitu kwa elimu Yake na kwa kuwa Yeye ana hekima, sharti la utumwa ni kujisalimisha Kwake. Sheria za uhai humshurutisha mwanadamu kujisalimisha kwa Allah kwa sababu Allah ndiye anayezijua zaidi sheria hizo na anamjua zaidi mwanadamu.

Ulimwengu na kila kilichomo ndani mwake hutii sheria za Muumbaji huyo. Kwa hivyo, dini ya ulimwengu wote ni Uislamu. Jua, mwezi na nyota, vyote hivyo vinafuata Uislamu. Kwa kuwa Uislamu unamaanisha kumtii Allah na kujisalimisha Kwake, tunaona kwamba viumbe vyote hivyo vinamtii Allah bila ya kuasi. Yaani, tunashuhudia kwamba vinajisalimisha na kwamba vyote vinafuata Uislamu.

Je, wanataka dini isiyo kuwa ya Mwenyezi Mungu, na hali kila kilichomo mbinguni na katika ardhi kimesilimu kwa kumtii Yeye kikipenda kisipende, na kwake Yeye watarejeshwa?" (Aal-i Imran, 3/83)

Katika aya hiyo hapo juu, kujisalimisha kwa viumbe angani na ardhini kumetolewa kama mfano na mwanadamu ameambiwa yafuatayo: "Ewe Mwanadamu! Jisalimishe kama wao." Kama Ali (ra) anavyosema, "Uislamu ni utii na kujisalimisha." Mtu asiyejisalimisha kwa Allah hazingatiwi kuwa ni Muislamu. Mtu huzingatiwa kuwa ni mtumwa wa yule anayejisalimisha kwake. Uislamu ni alama na taswira ya imani. Je kujisalimisha bila ya imani, yaani, Uislamu bila ya imani unawezekana? Hata ikiwezekana, haikubaliki. Munafikuna (wanafiki) ni watu wanaojisalimisha bila ya imani. Leo, watu wanaojitambulisha kuwa ni Waislamu huku hawaamini kuwa ni lazima, hao hawajapokea hukumu za Allah kwa moyo na wanafuata itikadi (dini) zingine wanaingia katika kundi hili. Uislamu (kujisalimisha) thabiti, ni lazima kujisalimisha katika Sharia'ah ya Allah bila kusita, kikamilifu na bila ya masharti yoyote.

Kama mtu atajisalimisha kwa Allah kwa hiari yake mwenyewe, na akaishi kama Muislamu kwa kuuchagua Uislamu, ataishi kwa amani na kwa kutangamana na ulimwengu tangu alipojisalimisha kwa yule yule ambaye ulimwengu umejisalimisha kwake. Basi, mtu wa namna hiyo anakuwa mwakilishi wa Allah juu ya ardhi.

UISLAMU NI NINI?

Haiwezekani kufafanua maana ya dini ya Uislamu kwa kifupi bali kwa urefu. Maana yake pana inaweza kufanyika tu kwa ufafanuzi wa Quran na Sunnah kwa sababu yaliyo katika Uislamu na mipaka yake yanabainishwa na Quran na Sunnah. Uislamu unaweza kufundishwa kutoka katika Quran na Sunnah. Allah ameifanya dini hii kuwa kamilifu na pana kwenye vipengele vyote. Hakuna jambo lisilokuwa na ufafanuzi katika Uislamu. Imebainishwa iwapo jambo ni halali, haramu, makruh (lenye kuchukiwa), sunnah, au wajibu; hukumu ya kila tendo au imani imebainishwa. Katka Uislamu kuna hukumu mahususi kuhusu imani, ibada, siasa, masuala ya kijamii, uchumi, vita, amani, sheria na yote yenye kumhusu mwanadamu; au, msingi wa mujtahid kufanya hukumu ni Quran na Sunnah. Allah anaeleza rasilimali hii ya Quran kama ifuatavyo:

“Na tumekuteremshia Kitabu hiki kinacho bainisha kila kitu." (an-Nahl, 16/89 na pia angalia Yusuf, 111)

Wanazuoni ambao ni Mujtahid huwa wanahukumu masuala ambayo hukumu zake hazikufafanuliwa waziwazi katika Quran na Sunnah kwa kuegemeza maamuzi yao juu ya Quran na Sunnah.

Mtume (s.a.w) aliufafanua Uislamu kwa njia nyingi. Mmojawapo ni huu ufuatao:

"Uislamu umejengwa juu ya kanuni tano: Kushuhudia kuwa hakuna mwenye haki ya kuabudiwa isipokuwa Allah na kwamba Muhammad (s.a.w) ni Mjumbe Wake, kuswali, kulip zaka, kufanya Hajj na kufunga katika Mwezi wa Ramadhani." (Bukhari, Iman 1; Muislamu, Iman 22; Nasai, Iman 13; Tirmidhi Iman 3)

Hadithi hiyo hapo juu inaeleza kuwa Uislamu una misingi mitano. Tunachotakiwa kuzingatia ni ukweli kuwa misingi hiyo mitano ndiyo nguzo za Uislamu isipokuwa zenyewe peke yake haziundi Uislamu wote. Hatuwezi kusema kuwa nyumba huwa na msingi tu; halikadhalika, si sahihi kusema kuwa Uislamu una kanuni tano tu. Mwenye kusoma Quran ataona kuwa maadili, uchumu, masuala ya kijamii, amani, vita, wema, uovu n.k. ni mambo yaliyotajwa pamoja na kanuni hizo tano katika Quran. Uislamu una msingi na jengo. Msingi una kanuni hizo tano. Jengo lina hukumu zingine za Uislamu zinazohusu maisha ya kibinadamu. Wajibu wa Muislamu ni kuujua Uislamu wote kwa ujumla na kuutekeleza wote kwa ujumla.  

Chini ya nuru ya hadithi maarufu hapo juu, tunaweza kugawanya misingi ya Uislamu katika makundi mawili: imani, iliyoelezwa kifupi kwa maneno ya shahada na amali njema, zilizotajwa kama amali nne kutokana na umuhimu. Uislamu ni imani inayoanzia katika kalima ash-shahada (maneno ya shahada) na kanuni za imani. Uislamu ni ibada inayojitokeza pamoja na swala, zakah, saumu na hajj. Hizo zinaitwa kanuni au misingi ya Uislamu. Sehemu zilizosalia za Uislamu ni jengo lililowekwa juu ya misingi hiyo. Mambo yanayounda jengo hilo ni mifumo ya kimaisha ya Uislamu: mfumo wa kisiasa, mfumo wa kiuchumi, mfumo wa kijeshi, mfumo wa kijamii,mfumo wa elimu, n.k. Uislamu pia una vibali ili kuhakikisha mamlaka yake. (Vibali vinamaanisha kwamba ni nguvu ya kuhakikisha kuwa sheria na amri za kimaadili zinatekelezwa; inamaanisha desturi zinazohusu ushurutishaji). Vibali hivyo ni jihad, kuamrisha wema na kukataza uovu, adhabu asilia na adhabu za kiungu anazotoa Allah duniani na ahera. Hivyo, Uislamu ni imani, ibada, mifumo ya kimaisha na vibali. 

UISLAMU NI NINI?

Maana ya Uislamu ni hali ya mtu kujisalimisha kwa Allah kwa nafsi yake ya ndani na ya nje, kwa moyo na mwili, akili na dhamiri, matakwa na chuki, hisia na nia. Maana ya Uislamu ni kuokoa moyo wa mtu, akili, mwili, nafsi ya ndani na ya nje dhidi ya vyote isipokuwa Allah. Uislamu ni mfumo wa ujumla, mpango wa vitendo vya kibinadamu wenye kuamuru kwa njia ya sheria na ufunuo unaohusu vipengele vyote vya maisha na uliotangazwa na kufikishwa na Mtume.  Wenye kuutii mpango huu watapata malipo na wasiotii wataadhibiwa. Uislamu ni ukamilifu wa hukumu zilizoshushwa na Allah, itikadi, ibada, maadili, muamalat (miamala) na yote yaliyo katika Quran na Sunnah.

Kinyume cha Uislamu ni Jahiliyya (ujinga). (Jahiliyya ni jina linalokusanya namna zote za ukafiri kama ndio imani na mtindo wa kimaisha. Maana yake ni ukafiri.) Ujinga ni dhahiri kabisa uko kinyume cha kila sehemu ya Uislamu.  Kama Swahaba Umar anavyoeleza, "Wanapojitokeza wasiojua Uislamu na Ujinga, mafundo ya Uislamu hufunguka moja baada ya jingine." Uislamu ni kinyume cha Ujinga katika vipengele vyote kwa sababu kila sehemu ya Uislamu ni kazi ya ujuzi wa Allah inayokizingira kila kitu.  Kila rai na mwenendo ulio kinyume na Yeye ni Ujinga kabisa kwa sababu ni kazi ya elimu ya mwanadamu yenye mipaka.  Aidha, fikra na matakwa ya mwanadamu vinaweza kumwelemea na kuifanya wema uonekane kama uovu na shari kama vile ni heri.

"Je, wao wanataka hukumu za Kijahiliya? Na nani aliye mwema zaidi katika kuhukumu kuliko Mwenyezi Mungu kwa watu wenye yakini?” (al-Maida, 5/50)

Baadhi ya watu wanapoona uzuri na ukomavu katika matendo, mtindo wa kimaisha au baadhi ya mifumo ya baadhi ya watu wanaofuata njia ya Ujinga, wanakuwa na mashaka. Hayo ni kwa sababu jambo la Kiislamu wakati mwingine linaweza kuwepo kwa watu wenye mfumo wa Ujinga, pia. Jambo hilo la Kiislamu linaonekana zuri huko, pia. Mjinga hutwaa mfumo huo kwa sababu hajui ukweli wa Uislamu. Kama angejua ukweli, basi angefahamu kuwa tendo jema lisilo na ukamilifu aliloliona katika Ujinga ni la Uislamu na litageukia upande wa chanzo chake na asili.

Kuna Uislamu na Ujinga katika imani mbalimbali. Upo Uislamu na Ujinga katika maadili, siasa, mafunzo, vita, amani na masuala ya kijamii. Upo Uislamu na Ujinga katika masuala yote yanayomhusu mwanadamu, katika sheria na kanuni zote. Ujinga katika imani na ibada ndio ujinga wa hatari zaidi. Kwa hivyo, Allah anawasamehe watu wanaofanya baadhi ya matendo ya ujinga wakiwa na imani thabiti isipokuwa Hasamehe watu ambao imani yao na ibada zao ni za Ujinga hata kama wana maadili kamili ya Kiislamu.

"Hakika Mwenyezi Mungu hasamehe kushirikishwa, na husamehe yaliyo duni ya hilo kwa amtakaye.” (an-Nisa, 4/48)

Allah ameuleta Uislamu ukiwa kamili. Mtu anayeuchukua wote ni Muislamu. Mtu anayeuchukua baadhi yake na akaacha sehemu yake nyingine anachanganya Uislamu na Ujinga.

“Kisha nyinyi kwa nyinyi mnauwana, na mnawatoa baadhi yenu majumbani kwao, mkisaidiana kwa dhambi na uadui. Na wakikujieni mateka mnawakomboa, na hali kuwatoa mmekatazwa. Je! Mnaamini baadhi ya Kitabu na mnakataa baadhi yake? Basi hana malipo mwenye kutenda hayo miongoni mwenu ila hizaya katika maisha ya duniani, na Siku ya Kiyama watapelekwa kwenye adhabu kali kabisa. Na Mwenyezi Mungu si mwenye kughafilika na yale mnayo yatenda.” (al-Baqara, 2/85)

Ni lazima kila Muislamu atakasike dhidi ya desturi na kanuni zote za Ujinga na kuuchukua Uislamu wote. 

Lengo la dini ya Uislamu

Hukumu zilizowekwa na Uislamu zinalenga furaha ya watu. Wenye kutenda kwa kufuata hukumu hizo watapata furaha kamili duniani na ahera. Uislamu unamfanya mtu apate furaha kwa kuboresha moyo wake, fikra na matendo. Kwa kuwa furaha ya jamii hutegemea furaha ya mtu mmoja mmoja, furaha ya mtu mmoja mmoja inamaanisha furaha ya jamii. Uislamu umeweka baadhi ya hukumu ili kufikia lengo hili. Zinaitwa hukumu za Shari'ah.  

Hukumu za Dini ya Uislamu

Hukumu za dini ya Uislamu zimegawanyika katika makundi manne.

a) Imani (Hukumu zinazohusu imani): Ni hukumu zinazohusu masuala ambayo mwanadamu anahitaji kukubali au kukataa katika dini ya Uislamu. Hukumu hizi humfundisha mwanadamu anachotakiwa kukubali na kukataa. Kwa kuamini kanuni za imani, mwanadamu anachukua chakula chake cha kiroho, anatakasa moyo wake dhidi ya imani potovu na anapata thamani yake halisi. 

b) Vitendo: Vitendo ni mambo anayoyafanya mwanadamu. Ni vitendo vinavyotakiwa kufanywa au kutokufanywa. Hukumu zenye kueleza amali gani zifanyike chini ya hali zipi na namna amali hizo kuwa ni amali zenye kufaa huitwa amali za kivitendo; mathalani, kuswali, kutoa zakah, kufanya jihad, kutafuta elimu.

c) Maadili: Hizi ni hukumu zenye kufafanua hali na vitendo, mitizamo na uhusiano wa Kiislamu na wa kibinadamu. Ni hukumu zenye kuhusu kuyapendezesha maadili na kuelimisha dhamira; mathalani, kutokutukana au kudanganya, mtu kutaka vitu ambavyo hutaka kwa ajili ya nafsi yake, kwa ajili ya wengine pia.

d) sheria [Muamalat (Miamala), Uqubat (Adhabu)]: Hizi ni hukumu zilizo nje ya masuala kama ya imani, maadili na vitendo binafsi na vyenye kuhusu kuongoza dola, utawala wa jamii, masuala ya kiuchumi, ndoa, talaka, mirathi, mambo ya kibiashara na kisiasa; kwa kifupi, ni hukumu zote zenye kuamua sheria na kanuni za dola ya Kiislamu. 

Uislamu si sehemu tu ya maisha ya mwanadamu bali ni wote kikamilifu pamoja na vipengele vyake vyote. Uislamu umeyazingira na kuyaainisha masaa ishirini na nne ya mwanadamu na masuala mengine yote tangu kuzaliwa mpaka kufa.  Uislamu ndio maisha yote ya mwanadamu. Ni wote kikamilifu pamoja na imani yake, ibada na sheria. Hauwezi kugawanywa au kuambatanishwa na kitu kingine. Haukubali kupunguzwa au kuongezwa, na ushirikina.  Ni mfumo kamilifu uliokamilishwa na Allah.

Sifa Bainifu za Ujumla za Uislamu

1) Uungu: (Ni wa Mola Mlezi; hali ya kuwa mungu) Uislamu ni dini ya kweli na ya kiungu. Uislamu unategemea ufunuo. Malengo na madhumuni yake ni ya kiungu. Radhi za Allah ndiyo malengo ya msingi ya Muislamu. Chanzo na mtindo wa Uislamu ni wa kiungu, pia.

2) Ubinadamu: (Kutangamana na hali ya kibinadamu) Quran ilishushwa kwa watu, na mitume waliteuliwa kutoka miongoni mwa watu. Uislamu unampa umuhimu mkubwa mwanadamu na akili ya kibinadamu; na umeweka hukumu.  Kwa mujibu wa Uislamu, mwanadamu aliumbwa juu ya ardhi kwa namna bora kabisa na kama mwakilishi; alifanywa kiumbe wa kipekee mwenye sifa muhimu ya kiroho; na ulimwengu umetiishwa kwake.  Uislamu hauyapuuzi makundi yoyote yenye uwezo na nguvu. Unawaongoza wote hao kwenda kwenye kutengemaa, kazi na maendeleo.  Kwa kushughulikia mizigo anayomudu kuibeba, mwanadamu anaendelea katika njia yake kwa amani, usalama na utulivu.  Majukumu hayo yanatangamana na hulka ya mwanadamu.  Yanaunganishwa na uthabiti wa moyo na dhamiri ya mwanadamu. Uislamu unalenga katika kustawisha hulka yake.  Hukumu zote za Uislamu zimeelekezwa kwenye furaha ya duniani na ahera.. 

3) Upana na kuenea: Uislamu ni wa milele wa kuwepo daima, mpana wa kuwajumuisha watu wote na wa kina kirefu cha kujumuisha mambo ya duniani na nje dunia. Ujumbe na hukumu zake ni zinauhusu ulimwengu wote na wanadamu. Uislamu unapanga hatua zote za maisha ya mwanadamu, tokea kuzaliwa mpaka kufa na nyanja zote za kimaisha. Mafunzo ya Uislamu pia ni mapana. Upana huo hudhihirika katika imani, ibada, tafakuri, maadili na fadhila, na utaratibu na sheria. 

4) Wastani na usawa:  Uislamu ni dini yenye nguvu za kimsingi kama vile usawa, kati upole, haki na wastani. Ni njia ya kuepuka ubadhirifu na upungufu.  Uislamu hauna mambo ya msimamo mkali. Haumwachi mwanadamu apotee na kukandamizwa. Uwezo wa mwanadamu hautoshi kuweka mfumo wa usawa. Tunaweza kuona kirahisi vipengele vya wastani (haki na usawa) katika imani, ibada, maadili na utungaji sheria. Kuna mizani kati ya dunia na ahera, maada na roho, tajiri na masikini.  Uislamu huweka kwa usawa ndani na nje ya mwanadamu, roho na mwili, mtu mmoja mmoja na jamii, wanawake na wanaume, familia na taifa. Uislamu unapambanua haki zao kwa kila mmoja kwa usawa na utangamano.

5) Uwazi: Kanuni za imani na fikra za Uislamu ziko wazi na bayana. Ni nyepesi kuzifahamu, kueleza na kukubali.  Hazikataliwi na akili na mantiki.   

6) Dini Safi: Ni dini isiyoweza kuvurugwa kwa kuwa hairuhusu uchambuzi na usanisi (uunganishaji), kupunguzwa na kuongezwa na kwa kuwa chanzo chake ni kamili na kisichobadilika. Haiingiliwi na ushirikina. Ni dini pekee ya kweli iliyokamilishwa na kukubaliwa na Allah. 

7) Upwekeshaji (Tawhid): Uislamu kimsingi ni dini ya upwekeshaji. Katika Uislamu ndiko kwenye kumwamini Allah kwa usahihi.  Katika Islam, sifa za Allah haziwezi kuhusishwa na watu na viumbe wengine.  Uislamu unasisitiza kuwa Allah hafanani na yeyote. Watu na viumbe wengine hawawezi kufanywa miungu. Haiwezekani kumwabudu yeyote mwingine isipokuwa Allah.

8) Kuwakubali Mitume wote: Muislamu anawaamini mitume wote waliotumwa na Allah. Hambagui yeyote miongoni mwao. Anawakubali kuwa ni wajumbe na waja wa Allah kwa kutokuwafanya miungu na kutokuwapa sifa za Allah wasizozistahiki.

9) Mamlaka ni ya Allah: Allah ndiye mwenye maamuzi, sheria na kanuni na kuweka sheria. Uislamu umejenga jamii ambapo hukumu, utawala, amri na mamlaka ni ya Allah na ambapo hakuna wenye kudhulumu, kudhulumiwa na watumwa wa watumwa.

10) Chanzo kamili: Chanzo kikuu cha Uislamu ni Quran. Quran ni kitabu ambacho hakitageuzwa-geuzwa mpaka Siku ya Kiama. Nakala zote za Quran duniani ni sawasawa.

11) Kutangamana na ulimwengu: Ulimwengu na kila kilichomo huzingatiwa kuwa kinafuata Uislamu kwa kuwa kinajisalimisha kwa Allah na kumtii. Mwenye kuupokea Uislamu na kujisalimisha, anatii kanuni zilezile katika kutangamana na ulimwengu. Hivyo, jitihata na nguvu za mwanadamu huunganika na nyezo za ulimwengu. Uislamu haumfanyi mwanadamu ashindane na kupigana na nguvu za asili ulimwenguni.

12) Uislamu unajenga jamii moja (umma): Uislamu unajenga jamii (umma) yenye utangamano na uaminifu na kutenda kwa mshikamano. Nguvu za msingi za jamii hii, inayounganishwa na kifungo cha imani na isiyobagua mbari, rangi, nchi na matabaka ni undugu, mshikamano, usawa, haki, kunasihiana ukweli na subira, kueneza heri na kupambana na shari. Ni jamii bora yenye maadili ambapo desturi mbaya kama vile uzinifu, ukahaba, wizi, dhuluma na riba vimeondshwa, ambapo matakwa yaliyovuka mipaka wa mwanadamu kwa ajili ya kula, kunywa, makazi na ngono umezuiwa. Makafiri hutazamwa kama ni umma mmoja; halikadhalika, Waislamu wote ni umma mmoja ambapo wao kwa wao huangaliana kama ndugu. 

13) Wepesi na bishara: Uislamu humwangalia yeyote mwenye kutamka kalima ash-shahada na kuishi nayo maishani kuwa ni Muislamu pasi na kujali kuwa hapo nyuma alikuwa vipi. Uislamu umejikita juu ya kanuni ya usawa na haki. Haumruhusu yeyote kushurutishwa kuwa Muislamu. Unalenga katika kuenea kwa kuzishinda nyoyo. Hukumu zake ni nyepesi zinazoweza kutekelezeka. Mengi mepesi yamewekwa kuhusu ibada kwa kuzingatia ustahamilivu wa mtu (Mengi mepesi kuhusu ibada yameelezwa kuuchukua uthabiti wa mtu kwenda kwenye umakini). Majukumu magumu hayajaamrishwa na Uislamu. Kwa rehema ya Uislamu, ruhusa na bishara ni nyingi. Uislamu unaangalia mahitaji ya kiroho na kimwili ya binadamu kwa ustahamilivu na kuzitafutia ufumbuzi mwepesi na rahisi. Hata hivyo, wote wenye kupuuza kumwabudu na kumtii Allah licha ya wepesi wote huo kwa sababu ya uvivu na kuipenda sana dunia wanaonywa juu ya adhabu ya Allah.

14) Uislamu unaipa umuhimu the akili na elimu: Uislamu ni dini ya ufunuo lakini unaipa umuhimu akili. Uislamu pia unaipa umuhimu mkubwa sayansi na na elimu, kwa kueleza kuwa elimu ni faradhi kwa Waislamu wote; unayapa umuhimu masuala kama kazi, mafunzo na fikra. Isisahaulike kuwa Uislamu si dini ya kufikirika bali ya kiakili.

15) Haki za kibinadamu: Uislamu, ambao unajali haki za kibinadamu kwa namna ambayo hawataweza kuiona katika mfumo (dini) wowote mwingine, unalinda haki zifuatazo za mwanadamu:

     a. Usalama wa dini: Uislamu unalinda haki ya dini na uhuru wa kuitekeleza dini.

     b. Usalama nafsi: Uislamu unahakikisha haki ya kuishi.

     c. Usalama wa akili: Uislamu, unaoamuru sayansi na tafakuri, unakataza vyenye kudhuru akili kama vile ulevi na madawa; unachukua kila hatua ili kulinda akili dhidi ya namna zote za kuchanganyikiwa. 

     d. Usalama wa kizazi: Unachukua hatua zote za lazima ili kuhakikisha adabu na heshima na makuzi ya kizazi chenye afya.   

     e. Usalama mali: Uislamu unaziba njia zinazoelekea kwenye uhalifu kama vile wizi ili kuhifadhi mali; zaidi ya hayo, humpa mwanadamu haki na fursa ya kuwa na njia za kutosha za kutafuta riziki.

Kwa ujumla, Uislamu unatoa dhamana kwa heshima, adabu, uhuru, dini, uhai, utafutaji riziki na kazi ya kila mtu.  

Kuhusu suala la haki za binadamu, Uislamu bado upo katika kiwango cha juu sana ambacho hakiwezi kufikiwa. Unahimiza kanuni za undugu wa wanadamu. Uislamu unakataa ubaguzi wa kimbari na kutambua ubora wa mtu isipokuwa kwa taqwa (uchamungu). Amri za Uislamu, makatazo, hukumu, ibada, ufahamu wa adhabu, n.k vinahakikisha usawa.  Kiasi hiki kikubwa cha usawa hakipo katika mifumo mingine hata kwa nadharia. Uislamu haujaacha kutilia maanani dhuluma kwa ajili ya usawa. Hauruhusu unyanyasaji wa kijinsia kwa kutoona tofauti za kijinsia kwa kisingizio cha usawa wa wanawake na wanaume na kuvuka mipaka kutakakopelekea kwenye kuwanyonya na kuwakandamiza watu. Kuhusu suala la haki za kibinadamu, Uislamu bado upo katika kiwango cha juu sana ambacho hakijawahi kufikiwa. Unahimiza kanuni za undugu wa wanadamu. Uislamu unakataa ubaguzi wa kimbari na kutambua ubora wa mtu isipokuwa kwa taqwa. Amri za Uislamu, makatazo, hukumu, ibada, ufahamu wa adhabu, n.k vinahakikisha usawa.  Usawa wa kiasi hiki haupo katika mifumo mingine hata kwa nadharia. Uislamu haujaacha kutilia maanani dhuluma kwa ajili ya usawa. Haupuuzi tofauti za kijinsia kwa kisingizio cha usawa wa wanawake na wanaume na kuruka mipaka kutakakopelekea kwenye kuwanyonya na kuwakandamiza watu. 

Uhusiano wa Uislamu na Shari'ah za Mitume Waliotangulia

a) Uislamu ni jina la dini zote zilizoshushwa kupitia kwa mitume wote. (angalia al-Baqara, 130 - 133). Utu uliletwa duniani na mtume (Adam). Allah aliwatuma mitume kuleta shari'ah (sheria) tofauti zilizoegemea mazingira ya wakati huo na mahitaji ya wanadamu; hata hivyo, imani ilikuwa ileile kwa mitume wote.

b) Dini zilizofikishwa na mitume waliotangulia zilipelekwa kwa baadhi ya mataifa. Dini aliyotumwa Mtume Muhammad (s.a.w) ni ya wote. Yaani, Allah aliileta ulimwenguni kote na kwa watu wote; ni njia ya maisha itakayokuwa halali mpaka Siku ya Kiama.

c) Dini ya Uislamu, aliyofikisha Nabii Muhammad (s.a.w), ilifuta hukumu (shari'ah) za dini zilizofikishwa na mitume waliotangulia. Yaani, iliyo hai kwa sasa ni shari'ah ya Nabii Muhammad (s.a.w).

d) Dini ya Uislamu inathibitisha vitabu vyote na mitume wote waliotumwa na Allah kabla ya Nabii Muhammad (s.a.w).

Baadhi ya Aya Zinazoeleza Uislamu

Bila ya shaka Dini mbele ya Mwenyezi Mungu ni Uislamu.(Aal-i Imran, 3/19)

Na anaye tafuta dini isiyo kuwa Uislamu haitakubaliwa kwake. Naye Akhera atakuwa katika wenye kukhasiri.(Aal-i Imran, 3/85)

Na mwenye kuuelekeza uso wake kwa Mwenyezi Mungu, naye akawa anafanya wema, basi huyo hakika amekwisha kamata fundo lilio madhubuti. Na mwisho wa mambo yote ni kwa Mwenyezi Mungu.(Luqman, 31/22)

“…Leo nimekukamiliishieni Dini yenu, na nimekutimizieni neema yangu, na nimekupendeleeni UISLAMU uwe ndiyo Dini....” (Al-Maida, 5/3)

Misingi ya Islam

Misingi (nguzo) za Uislamu ni mitano: Kushuhudia kuwa hakuna mwenye haki ya kuabudiwa isipokuwa Allah na kwamba Muhammad (s.a.w) ni Mjumbe Wake, kuswali, kulipa, kufanya Hajj na kufunga wakati wa mwezi wa Ramadhani.

Katika hadithi ambayo Mtume anafafanua Uislamu, inayojulikana kama hadithi ya Jibril, tuliyoitaja mwanzoni na inayoeleza kuwa Uislamu umejengwa juu ya nguzo tano (ambazo wajinga kimakosa huziita masharti ya Uislamu), nguzo hizo tano zimeorodheshwa. Tutashughulikia kanuni za msingi za imani tunazoziita kalima ash-shahada au kalima at-tawhid kwa kina tutakapoeleza suala la upwekeshaji (tawhid).  Hapa, tutataja kwa kifupi kanuni (nguzo) zinazoeleza kama mifano ya kifani kutokana na umuhimu wa aina hizi za ibada na tunazoweza humo humo kueleza matendo hayo mema pamoja na ibada nyengine kama hizo zinazohusiana na imani. Namna ya kuzifanya ibada hizi imeelezwa kwa kirefu katika vitabu vya maswali na majibu na katika somo la fiqh.  

Ni nini amali njema (amal salih)? Amali njema ni vitendo anavyovipenda Allah. Amali njema ina sifa mbili: Ya kwanza ni kuafikiana na shari'ah ya Uislamu; ya pili ni nia iwe kwa ajili ya Allah na kulenga kumwabudu. Kama amali haina sifa hizo mbili, haizingatiwi kuwa ni amali njema kwa Allah. Amali hiyo haina faida wala malipo. Mola wetu Mlezi anasema ifuatavyo:

“…Mwenye kutaraji kukutana na Mola wake Mlezi basi naatende vitendo vyema, wala asimshirikishe yeyote katika ibada ya Mola wake Mlezi..” (al-Kahf, 18/110)

Nafasi ya amali njema katika Uislamu ni muhimu sana kwa sababu vitendo hivyo ni matunda ya kumwamini Allah na akhera. Maana ya kalima ash-shahada (tawhid) inadhirika kwa kufanya matendo mema na kuendelea kufanya hivyo. Tunapokumbuka kuwa maana ya Uislamu ni kujisalimisha na utii, na kwamba kujisalimisha huko kunamaanisha kutii na kujisalimisha kwenye amri za Allah, inadhihirika wazi kuwa Uislamu hauwezi kuwa bila ya vitendo, utii na ibada. Aya nyingi zinasifu amali njema kutokana na umuhimu wake katika Uislamu. Baadhi ya aya hizo huzitazama kama ziko karibu na imani; baadhi hutaja malipo yake na nyingine hutaja manufaa yake katika akhera.

Naapa kwa Zama! Hakika binaadamu bila ya shaka yumo katika khasara, Ila wale walio amini, na wakatenda mema, na wakausiana kwa haki, na wakausiana kusubiri...” (al-Asr, 103/1-3)

Kuhusu baadhi ya aya zingine, angalia al-Maida, 9 ; ar-Ra’d, 29 ;an-Nahl, 97 ; al-Kahf, 30; Maryam, 76; al-Ankabut, 7, 9.

Ni lazima kuufata Uislamu ili amali iweze kukubaliwa. Kwa hivyo, Allah anataja imani na amali njema kwa pamoja. Kama mtu atafanya jema lenye kufikiana na shari'ah ya Uislamu na kwa ajili ya Allah, jambo hilo litakataliwa na Allah isipokuwa akiukubali na kuufuata Uislamu wote kikamilifu. Amali hiyo haitakuwa na malipo. (angalia Aal-i İmran, 3/85)

Kuna namna nyingi za amali njema. Hayo ni mambo yote anayoamuru Allah, ambayo ama yanahusu ibada au miamala. Muislamu anapofanya jema kwa lengo la kumtii Mola wake Mlezi, anajisalimisha kwenye shari'ah na atakuwa anatafuta radhi za Allah, hapo atakuwa mtu wa amali njema.

Kwanza kabisa, matendo mema (kwa mtazamo finyu) ni matendo ya ibada. Vitendo vikuu vya ibada swala za kila siku, hajj na zakah. Hiyo ni misingi ya Uislamu. Hairuhusiwi hata kidogo kupuuza au kutweza umuhimu wake. Kwa hivyo, imeelezwa waziwazi katika hadithi mashuhuri zenye kuufafanua Uislamu.   

Umuhimu wa ibada katika Uislamu ni mkubwa. Ibada huratibu uhusiano wa mtu na Mola wake Mlezi na kuonesha kumtumikia kwake Allah. Ibada ni haki maalumu ya Allah kutoka kwa waja Wake. Ni lazima kuchunga ibada na kuwaita watu wengine kwenye kanuni za imani na kisha ibada. Ibada isipokamilika, imani ya mtu haiwezi kuimarika na haitatulia moyoni mwake. Zaidi ya hivyo, leo hii, kwa vile mamlaka ya ukafiri yamefika kila mahali, imani ya watu wanaotekeleza ibada kivivu na kuacha baadhi ya ibada hususani swala za kila siku ni jambo la hatari. Yaani, ni vigumu sana mtu kundelea kuwa muumini bila ya kuswali na kufanya ibada nyengine. Ibada ni kama vile maji kwa samaki na hewa kwa mwaadamu.

Miongoni mwa ibada hizo, swala za kila siku zina umuhimu maalumu katika sharti la imani. Uislamu unaeleza swala kama sifa inayotofautisha kati ya Muislamu na kafiri. Hairuhusiwi kupuuza swala hata safarini, vitani, au mtu anapougua. Ni tabia ya wanafiki kuacha swala na kupuuza unapowadia wakati wa kuswali. Mtu anaporejea kwa Mola wake Mlezi, jambo la kwanza atakaloulizwa ni swala. Swala ni ibada ambayo mara kwa mara humkumbusha mtu kuhusu utumishi wake kwa Allah na maana ya kalima at-tawhid. Swala humzuia mtu kufanya vitendo vyote vibaya, uzinifu na uovu. Baadhi ya aya za Quran zinazohusu umuhimu wa swala ni hizi zifuatazo: ar-Rum, 31; al-Baqara, 1-3, 153 na 238; an-Nisa, 103; 142; al-Ankabut, 45...

Muislamu huitwa kwenye swala kwa tamko “Allahu Akbar”; anaanza swala kwa maneno hayo; anayakariri wakati anaposwali kwa sababu Allah ni mkubwa kuliko kila aliye mkubwa na Yuko juu kuliko kila mfalme mwenye nguvu. Kama mtu atasikamana na Allah, ambaye ni mkubwa na mwenye nguvu kuliko kila kitu, hatamwogopa yeyote. Ataacha kuwaabudu wengine.

Saumu, hajj, zakah na ibada zote zingine huimarisha imani, hutakasa roho ya uovu na kumfanya mtu amng’ang’anie Mola wake Mlezi. Katika saumu, mtu hutanguliza kumpenda Allah kuliko mahitaji ya mwili wake. Humfanya Muislamu awe mnyoofu, kuthubutu na matakwa na subira. Zakah ni ibada kwa upande wa mali inayomwezesha Muislamu kutakasika dhidi ya ugonjwa wa ubahili. Shukrani kwa nia ya zakah, anaifahamu vyema kuwa Allah ndiye mmiliki halisi wa mali na kwamba yeye amepewa dhamana tu ya mali hiyo. Zakah inamaanisha kutanguliza radhi na kumpenda Allah kuliko kupenda mali. Inamaanisha mtu kutenga fungu la mali yake na kuwapa masikini katika jamii na kwa hivyo kuchangia ustawi wa kijamii. Hajj ni mafunzo ya kivitendo kwa Muislamu. Tunaona kuwa Muislamu anatumikia kwa vitendo na waziwazi kwa njia ya ibada ya hajj. Maamrisho kama vile kutafuta elimu, kufanya jihad, kuamrisha wema, kukataza uovu, kuwa na subira na tawakkul, kuwa na taqwa, kumpenda Allah na kuhofu adhabu Zake ni katika matedo mema yanayosisitizwa sana katika Quran. 

Kufikisha ujumbe wa Uislamu

Uislamu lazima ufikishwe kwa kila mmoja kadiri mwanadamu anavyokuwepo. Lengo halisi la kulingania na kufikisha ni kuwaokoa watu dhidi ya kuwa watumwa wa watu wengine na kuwafanya wamwelekee Allah peke yake, ambaye ni Mmoja. Lazima kila mara kuwe na watu wenye kutekeleza wajibu huo.

Na uwe kutokana na nyinyi umma unao lingania kheri na unao amrisha mema na unakataza maovu. Na hao ndio walio fanikiwa.” (Aal-i Imran, 3/104)

Aya hiyo inathibitisha wajibu huu. Uislamu lazima ufikishwe kwa kila mtu lakini hususani kwa wenye kutenda matendo ya kijuujuu kama Waislamu kwa sababu wanaouona kama Uislamu si Uislamu halisi. Hali hii lazima ibadilishwe kabisa na waoneshewe ukweli.  

Lengo mojawapo la kuwaita watu kwenye Uislamu ni kuunusuru usihodhiwe na watu wasiomfikishia yeyote na kumjulisha kila mmoja kuhusu Uislamu. Hakuna anayeweza kuuhodhi Uislamu. Hakuna anayeweza kuwa na amri juu ya ibada na kuwataabisha Waislamu kuifanya. Wenye kufanya hivyo, ikiwa wanaifanya kwa niaba ya Uislamu au ya Ujinga, wanamvunjia heshima Allah kwa sababu Allah anataka viondoshwe vikwazo vyote vyenye kuwazuia watu kumfikia. Zaidi ya hivyo, Amefaradhisha kufanya jihad dhidi ya vizuizi hivyo ili watu wajue, wajifundishe na waupokee Uislamu, ulio msafi na wenye kufahamika kirahisi, wenye kutangamana nao. Kuwanusuru watu dhidi ya utawala na uonevu wa watu wengine, dhidi ya mabwanyenye, wenye mamlaka, wahenga, mababa, mabwana na desturi wanazozing’ang’ania, na kuwawezesha kuufikia Uislamu, ambao ni mfumo na utukufu wa Allah, katika namna zote za maisha... Hivi ndivyo Uislamu ulivyo; mitume wote walitumwa kwa ajili ya hilo.

Kuupa Mamlaka Uislamu Maishani

Kanuni ambayo ni msingi mkuu wa Uislamu katika historia nzima ya mwanadamu ni ya “La ilaha illallah”. Yaani, kanuni ya kuuweka uungu, ubwana, utawala na mamlaka kwa Allah peke yake. Kanuni hii inapasa idhihirike kwa njia ya imani moyoni, ibada katika hisia, na vitendo na sheria na mfumo maishani. Kama mtu hashuhudii kuwa hakuna mwenye haki ya kuabudiwa isipokuwa Allah kwa njia inayofaa, huzingatiwa kuwa anamkosea heshima Allah na Uislamu.

Kanuni hii hutumika kikamilifu pindi mwanadamu anapomgeukia Allah kikamilifu katika maisha yake. Hivyo, mwanadamu anatazama hukumu za Allah katika mambo yote na hatua zote za maisha yake; anapokea na kutanguliza amri za Allah kuliko rai zake mwenyewe.

Mtu mwenye kutoa khabari na kuwafikishia watu hukumu za Allah ni Mjumbe wa Allah (s.a.w). Kanuni hii ndio inayounda sehemu ya pili ya kalima ash-shahada.

“Muhammad ni Mjumbe wa Mwenyezi Mungu.” (al-Fath, 48/29)

Hii ni sehemu ya pili ya kanuni ya msingi inayoegemewa na Uislamu. Kanuni hii itakapotekelezwa kikamilifu katika vipengele vyote vya kimaisha, mfumo kamili utaajitokeza. Huo ni mfumo anaouridhia Allah. 

Lengo la Uislamu ni kuondoa Ujinga. Ni lazima kuweka wafanyakazi wapya tendaji wa kuweza kuutambua. Hili ni kundi la watu wanaofuata mbinu ya Kiislamu katika mtindo wao wa kimaisha, hali ya akili, mfumo wa kijamii, kiwango cha hukumu na njia, kwa kifupi, kila kitu. Ni hao tu ndio wanaoweza kuujenga tena umma wa Kiislamu na kustahiki kuwa ndio wanaotambulishwa na aya zifuatazo:

Nyinyi mmekuwa bora ya umma walio tolewa watu, kwa kuwa mnaamrisha mema na mnakataza maovu, na mnamuamini Mwenyezi Mungu.(Aal-i Imran, 3/110)

Na vivyo hivyo tumekufanyeni muwe Umma wa wasitani, ili muwe mashahidi juu ya watu, na Mtume awe ni shahidi juu yenu...” (al-Baqara, 2/143)

2 Nini unafikiria kuhusu msiba wa tarehe 11 Septemba na jaribio la tukio hilo la kuyahusisha mashambulizi mengine ya kigaidi duniani na dini ya Uisilamu?

Mwisilamu hawezi kuwa gaidi; gaidi hawezi kuwa Mwisilamu wa kweli

Uisilamu ni dini ya uvumilivu; Uisilamu unazingatia kuwa kiumbe ni chenye thamani mno; unazingatia uvunjaji wa sheria na mashambulizi dhidi ya watu wasio na hatia ni madhambi makubwa. Kwa hakika, aya ya Quran tuliyoitaja inatangaza kwa kupaza sauti:

Aliye muuwa mtu bila ya yeye kuuwa, au kufanya uchafuzi katika nchi, basi ni kama amewauwa watu wote. Na mwenye kumuokoa mtu na mauti ni kama amewaokoa watu wote. Na hakika waliwajia Mitume wetu na hoja zilizo wazi. Kisha wengi katika wao baada ya haya wakawa waharibifu katika nchi.(5: 32).

Kwa kweli, Mwisilamu huhudumia maisha tu na sio kifo. Kwa hivyo, lazima tusisahau kanuni mbili kuu za sheria zilizowekwa na Uisilamu:

Ya kwanza: Aya ya Quran: ‘Na habebi mwenye kubeba mzigo wa mwenziwe’ (6: 164). Yaani, mtu mwengine hawezi kuadhibiwa kwa sababu ya mtenda mauaji. Katika sheria, uhalifu na adhabu ni vitu binafsi.

Ya pili: mtu huzingatiwa kuwa hana hatia hadi itakapothibitishwa kuwa ni mkosa. Yaani, hakuna anayeweza kushitakiwa isipokuwa tu ithibitike kuwa ni mwenye hatia. Haizingatiwi kuwa ni haki kumwadhibu mtu bila ya ushahidi. Mtu anazingatiwa hana hatia isipokuwa ithibitishwe kuwa ni mkosa. Yafuatayo yanaripotiwa kutoka kwa Bwana Mtume: ‘Muumini anaweza kujilinda yeye mwenyewe katika muktadha wa dini isipokuwa akiua mtu asiye na hatia kinyume na sheria.

Kilugha, Uisilamu unamaanisha amani. Hili linaonesha kuwa amani ya kweli ya kiwiliwili na akili inawezekana tu kupitia kumtii Allah na kujisalimisha Kwake. Mwisilamu anakuwa Mwisilamu kamili ikiwa tu anaishi katika amani na maelewano katika jumuia. Maisha ya kumtii Allah na kumwabudu Yeye yataupelekea moyo kukinai na amani ya kweli itafikiwa katika jumuia. ( 13:28-29).

Mitume wote wa Allah waliwafikishia watu ukweli walipowalingania kuja kwenye njia sahihi. Ni muhimu hapa kukumbuka hadithi ya Mtume ifuatayo: ‘ vipo vitu vitatu ambavyo ndio vipengele vya msingi kuhusiana na imani: kuwasaidia watu hata kama mtu ana hali ngumu ya kiuchumi; kuomba amani kwa watu kwa shauku; kuwatendea watu haki kama yeye mwenyewe anavyotaka atendewe kwa haki.

Bwana Mtume pia amesema:

Watu ni kama kundi la mifugo; kila mmoja wa kundi hili anapaswa awe kama mlinzi na mchungaji wa wengine na anapaswa abebe jukumu la kundi zima la mifugo.’

‘Ishini pamoja, shikamaneni, msizozane; rahisishianeni; msitiliane uzito na msifanyiane ugumu.’

‘Mtu anayelala usiku tumbo lake likiwa limeshiba ilhali majirani zake wana njaa basi huyo sio muumini wa kweli.’

‘Mwisilamu ni mtu anayemwabudu Allah na hayadhuru maisha ma mali za wengine.’

Kwa kifupi, Uisilamu haubezi mtu mmojammoja au jumuia. Kwa hakika, una lengo la kuleta maelewano na uwiano kati yao. Ujumbe wa Uisilamu ni kwa watu wote. Kwa mujibu wa Uisilamu, Allah ndiye Mlezi na Muidhinishaji wa Dunia. (1:1). Bwana Mtume ni mjumbe aliyetumwa kwa watu wote. ‘Sema: Enyi watu! Hakika mimi ni Mtume kwenu nyinyi nyote, niliye tumwa na Mwenyezi Mungu’ (7:158). ‘Nasi hatukukutuma ila uwe ni Rehema kwa walimwengu wote.” (21: 107).

Katika Uisilamu, watu wote huzingatiwa kuwa ni sawa bila ya kujali rangi zao, lugha, mbari au nchi. Hatuwezi kukataa, katika zama zilizoitwa zama za mapambazuko leo, kuwa bado vipo vikwazo, ubaguzi na kutendewa tofauti kati ya watu kutokana na sababu tulizozitaja. Uisilamu umetokomeza ubaguzi wa namna zote na upendeleo, na kutangaza duniani kuwa kila mmoja ni sawa kutokana na ukweli kuwa wote ni viumbe wa Allah. Uisilamu una mashiko ya kikweli ya kimataifa; unakataa upendeleo unaogemea rangi, koo, mbari, damu na eneo. Tunakemea aina zote za mashambulizi dhidi ya wanadamu. Tunasikitika kutokana na aina zote za uvunjwaji wa sheria unaowalenga watu wasio na hatia. Uisilamu unakataza mauaji ya kutisha ya watu wengi ambapo watu wasio na hatia huuliwa pamoja na madhalimu. Kwa mujibu wa Uisilamu, hakuna atakaebebeshwa jukumu kutokana na makosa ya wengine.

Uisilamu hauruhusu kuuliwa watu wasio na hatia na wasio na hifadhi. Kama mauaji hayo ya watu wengi yamefanywa na baadhi ya Waisilamu mmoja mmoja kuwa ndio dai la kibaguzi la vyombo vya habari, tutawatangaza madhalimu wote kuwa ni wahalifu na watenda dhambi kwa niaba ya Uisilamu. Tunataka kutilia mkazo kuwa ni muhimu mno kuwaadhibu madhalimu kwa adhabu kali bila ya kumbagua yeyote kwa upande wa kidini, mbari na jinsia.

Tunapokabiliana na matukio hayo, lazima tusisahau kuhusu ukweli kuwa dola mbalimbali na mtu mmoja mmoja: Kama ukiwa ndani ya meli au nyumba na mkiwa na watu tisa wasiokuwa na hatia na mmoja ni muuaji yuko nanyi, mtajua tu ni namna gani mtu huyo anayetaka kuizamisha meli au kuiteketeza nyumba kwa moto alivyo katili. Utapiga mayowe ili kumfanya kila mtu asikie ukatili wake. Hata kama mtu asiye na hatia ni mmoja tu na tisa waliobaki ni wauaji, tena itakuwa ni kinyume na haki kuizamisha meli hiyo au kuiteketeza nyumba hiyo kwa moto. Ni hivyo hivyo kwa matukio ya aina hii, pia. Tunakemea matendo haya ya damu na yasiyo na huruma na tunataka kumkumbusha kila mtu kuwa ni hatari mno kufanya matendo hayo hayo.

3 Ni thamani zipi za msingi ambazo dini ya Uislamu inaamuru zihifadhiwe?

Kuna haki nyingi ambazo Uislamu unawapa watu. Tunaweza kuorodhesha thamani nyingi zinazozingatiwa kuwa ni haki za msingi kama ifuatavyo: Uhai, dini, akili, mali na kizazi.

1- Haki ya Kuishi:

Dini ya Uislamu unamzingatia mtu kuwa ni kiumbe bora zaidi na unachukulia kuwa kulinda haki za kibinadamu ni katika kanuni za msingi. Imeelezwa katika Quran kuwa kumuua mtu bila ya haki ni kosa kubwa sana kama kuwaua watu wote na kuwa kuhifadhi uhai wa mtu ni kitendo cha thamani ya juu sana kama vile kuwahifadhi watu wote.

Mtume (s.a.w) aliwahutubia Waislamu wote kama ifuatavyo katika Hajj ya Kuaga: "Kama mnavyouchukulia mwezi huu, siku hii, mji huu kuwa ni Tukufu, basi chukulieni kuwa uhai na mali ya kila Muislamu kuwa ni dhamana tukufu " (Bukhari, "Ilm", 37, "Hajj", 132, Muslim, "Hajj, 147), kwa kueleza kuwa haki ya kuishi ya kibinadamu si yenye kuguswa. Katika hadithi nyingine, yameelezwa yafuatayo: "Epukeni mambo saba yenye kuangamiza. Mojawapo ni kumuua mtu, ambako kumeharamishwa na Allah isipokuwa kwasababu za haki." (Bukhari, "Wasaya", 23; "Tib", 48; "Hudud", 44; Muslim, "Iman", 144; Abu Dawud, "Wasaya", 10).

Kuwaua watu kama vile wanawake, watoto, wazee na viongozi wa dini kumeharamishwa hata katika wakati wa vita. Kumuua mtu na hata kujiua kumeharamishwa na kunazingatiwa kuwa ni katika madhambi makubwa.

2- Haki ya dini:

Kila mtu ana uhuru wa kuchagua dini. “Hapana kulazimisha katika dini.” (al-Baqara, 2/256), “Nyinyi mna dini yenu, nami nina Dini yangu...” (al-Kafirun, 109/6). Jambo hili limesisitizwa katika aya hizo hapo juu. Wasio Waislamu wanaoishi katika mamlaka ya dola ya Kiislamu wamepewa haki ya kutekeleza dini zao wenyewe.

3- Akili:

Akili ndio sifa bora zaidi ya mwanadamu kwa sababu dhamana za Allah ni shukurani zinazokubaliwa na akili na mwanadamu anaweza kupata radhi na kuridhika kwa Allah, hilo ni la kushukuru. Chanzo na mzizi wa elimu ni akili. Uhusiano kati ya elimu na akili ni kama uhusiano kati ya tunda na mti, mwangaza na jua, kuona na jicho. Akili ndiyo inayombainisha mwanadamu na viumbe wengine hai na wasio hai ulimwenguni na kumfanya awe bora zaidi.

Maonyo katika Quran yaliyosababisha watu kufikiri kama vile “Fikiri!”, “Je hamfikiri?”, “Je, hawafikiri”, “Angalia!”, “Je, hawaoni?”, “Pateni onyo, Enyi wenye macho!” inaonesha umuhimu unaopewa akili.

Badiuzzaman Said Nursi anaeleza akili kuwa ni muhtasari wa hali ya dhamiri iliyochujwa kutokana na hisia, kitu cha thamani kubwa kwa mwanadamu, hali ya nuru, ufunguo wa kufungulia hazina za ulimwengu, kifaa kinachoangalia majina na sifa za Allah yanayojidhihirisha duniani, mtafiti anayetafutia ufumbuzi mafumbo ulimwenguni, mwongozo wa kiungu unaomwandaa mtu kupata furaha ya maisha ya milele, zawadi ya thamani kubwa inayotenda kazi juu ya ushahidi na kumwonesha mtu malengo makubwa na ya matunda ya kudumu, na kitu cha msingi kilichoachanishwa na mada na kinahusiana na mada katika utendaji wake.

Dini ya Uislamu imeharamisha ulevi, unaolewesha watu, ili kuuhifadhi msingi huo muhimu na umeweka adhabu juu ya wenye kukiuka uharamishwaji huo. Katika sheria ya Kiislamu, vitu vyote vyenye kumduwaza mtu na kumwondolea uwezo wake wa kufikiri na kuwa na mantiki huzingatiwa kuwa ni haramu pamoja na vinywaji vyenye kulewesha.

4- Mali:

Dini ya Uislamu inahakikisha haki ya kupata mali. Uislamu unamtaka mtu aishi maisha yenye kufaa heshima ya binadaamu. Uislamu haupingani na mali. Uislamu hautaki mali kuwa ni nguvu inayomilikiwa na sehemu ya jamii; unataka mali ienee baina ya watu.

Dini yetu inazingatia kuua kuwa ni katika madhambi makubwa; halikadhalika unauzingatia wizi na unyang’anyi kuwa ni dhambi kubwa na unaweka adhabu kali sana kama vile kukatwa mkono wa mwizi katika kesi ya wizi.

5- Kizazi:

Desturi ya ndoa ni lazima kwa ajili ya kudumisha na kuendeleza kizazi cha binadamu. Kudumu na kustawi kwa kizazi cha biadamu kunawezekana tu kupitia kuanzishwa kwa familia, ambayo inaunda jamii ambayo ni muhimu sana katika jamii. Desturi ya ndoa imeegemea juu ya mkataba wa ndoa unaounda msingi wa jumuiya ya Kiislamu.

Katika kulipa umuhimu jambo la kuiimarisha jamii ya Kiislamu, dini ya Uislamu imetumia na imehimiza kuwa na watoto na kuongeza idadi ya watu. Kwa hakika, Mtume Mtukufu (s.a.w) amesema, "Oeni wanawake wapenzi na wenye kuzaa kwa sababu nitajifaharisha kwa wingi wenu katika hadhara ya ummah zingine katika Siku ya Kiama." (Ahmad b. Hanbal, I, 412).

Nabii Zakariyya (s.a.w) alimwomba Allah dua ifuatayo ili kuendeleza kizazi chake: "Na hakika mimi nawakhofia jamaa zangu baada yangu: na mke wangu ni tasa. Basi nipe mrithi kutoka kwako. Atakaye nirithi mimi na aurithi ukoo wa Yaaqub. Ewe Mola wangu Mlezi! Na umjaalie awe mwenye kuridhisha! " (Maryam 19/5-6)

Katika Uislamu, kuwa na watoto na kuendeleza kizazi huzingatiwa kuwa ni ibada. Kutokana na umuhimu wake, kumdhuru mtoto katika mji wa mimba, kuharibu mimba na kutoa mimba huzingatiwa kuwa ni kuua. Kumeharamishwa kuua  kijusi ambacho viungo vyake vimeshadhihirika. Mjumbe wa Allah (s.a.w) alipopokea ahadi ya utii kutoka kwa wanawake, aliamuru “kutowaua watoto wao kwa njia yoyote” kama ni sharti. Sharti hili ni muhimu sana. Mtoto yuko chini ya udhibiti wa mama yake kabla hajazaliwa. Hata hivyo, baada ya kuzaliwa, baba, sio mama, ndiye anayewajibika. Kisha, sharti la “kutowaua watoto wao kwa njia yoyote” linahusiana na kijusi katika mji wa mimba.

"Ewe Nabii! Watakapo kujia wanawake Waumini wanakuahidi ya kwamba hawatamshirikisha Mwenyezi Mungu na chochote, wala hawataiba, wala hawatazini, wala hawatawauwa watoto wao, wala hawataleta uzushi wanao uzua tu wenyewe baina ya mikono yao na miguu yao, wala hawatakuasi katika jambo jema, basi peana nao ahadi, na uwatakie maghfira kwa Mwenyezi Mungu..." (al-Mumtahina, 60/12).

4 Ni zipi nguzo za Uislamu?

Dini ya Uislamu imejengwa juu ya nguzo tano. Nazo ni: saumu, salah (kuswali), Hajj (kuhiji Makka), Zakat (Kutoa zaka), kushuhudia Upweke (tauhidi ya) wa Allah na utume wa Mtume Muhammad (Shahadah).

Nguzo mojawapo ya Uislamu ni kufunga katika Mwezi wa Ramadhani. Kwa njia ya saumu, Waislamu wanajikinga dhidi ya kutawaliwa na nafsi yenye uovu kwa kuitia nidhamu na kuitakasa. Na hapo inakuja hisia ya kuwahurumia masikini katika nyoyo zao kwa kuhisi maumivu yao ya kuwa na njaa.

Nguzo nyingine ya Uislamu ni kuswali. Inamaanisha kusimama mbele ya Allah mara tano kwa siku kwa mtu kujifahamu udhaifu wake na upungufu kwa kuinama na kusujudu na kuonesha utumwa Kwake. Swala za faradhi ni ibada ya wote na shukrani ya wote. Kila Muislamu ni lazima atekeleze. Mtume Muhammad (s.a.w) aliamuru: Swala ni nguzo ya dini (Tirmidhi, Iman-8)

Nguzo nyingine ya Uislamu ni Hajj (Kwenda Hija katika mji mtakatifu wa Makka). Wameamrishwa Waislamu wenye uwezo wa mali na wa kiafya kulingana na sheria ya Kiislamu, kwenda Hajj angalau mara moja maishani katika msimu mahususi uliopangwa na sheria (Shariah) ya Kiislamu. Mojawapo ya hekima za ibada hii, ambayo ni ya lazima, ni Waislamu wa dunia nzimakuweza kukutana na kudhihirisha kuwa watu wote wako sawa mbele ya Allah (SWT) pasi na kujali utaifa, lugha, rangi ya ngozi, na hadhi ya kijamii.

Nguzo nyingine ya Uislamu ni kutoa zaka (Zakah), ambayo ni nguzo ya mwisho ya Uislamu. Allah Mtukuka amewafaradhishia Waislamu matajiri, kwa ajili ya Allah, kwa kuwapa, Waislamu masikini kiasi (2.5 %) katika mali zao, kilichopangwa na Uislamu. Mali hii, ambayo tajiri humpa masikini, huitwa Zakah. Kwa mujibu wa sheria ya Kiislamu, hii ni haki ya maskini. Uislamu unawahimiza Waislamu kuwasaidia masikini hata kwa njia isiyokuwa ya Zakah pia. Nazo huitwa sadaqah (sadaka).

Ili kuweza kuwa Muislamu, ni lazima mtu atamke kalima ash-shahada. Maana ya kalima ash-shahada ni kama ifuatavyo "Ninashuhudia kuwa hakuna mwenye haki ya kuabudiwa isipokuwa Allah na kwamba Nabii Muhammad ni mja Wake na mjumbe Wake."

Sehemu ya kwanza ya shahada inaeleza kuwepo kwa Allah na upweke (tauhidi Wake na kuwa Hana washirika au washindani. Sehemu ya pili inaeleza kuwa Nabii Muhammad (s.a.w) ni mja wa Allah na kwamba aliteuliwa na Allah kuwafikishia watu Misingi ya imani na nguzo za Uislamu.

5 Kwa nini Uchaguliwe Uislamu?

Dini zote zina kanuni kuu za namna moja na zinasisitiza mambo ya namna moja. Kila Mtume aliyetumwa na Allah alikuja kuendeleza na kutimiza yale ya mtume aliyemtangulia, alikariri ujumbe wa mtangulizi/watangulizi wake, aliutimiza kulingana na hali na mazingira, alifafanua masuala yaliyohitaji ufafanuzi, alifanya upya mambo yaliyohitajika kufanywa upya na kuunganishwa na mambo yenye kufanana nayo katika upande wa nidhamu - katika kukubaliana na mazingira ya kipindi hicho na mahitaji ya kipindi hicho. Masuala haya ya upwekeshaji, utume, kufufuliwa baada ya mauti na ibada yalikuwa mambo ya msingi kwa mitume wote. Ndiyo, kanuni zilizotajwa hapo juu ziliunda msingi wa ujumbe wa mitume wote huku kukiwa na tofauti ndogondogo katika mtindo, maneno na mitazamo.

Ujumbe wa Quran ni muendelezo wa ufunuo ulioanzia kwa Nabii Adam (as), mtu wa kwanza na mtume wa kwanza. Hivyo, msingi wa dini zote hizo mbele ya Allah ni mmoja:  Uislamu.

“Bila ya shaka Dini mbele ya Mwenyezi Mungu ni Uislamu (utii kwa Matakwa yake). ” (Aal-i Imran, 3/19)

Mitume waliotumwa katika enzi na mahali tofauti hawakupingana; Nabii Muhammad (s.a.w) pia, hakumkana yeyote katika wao.

Mtume ameamini yaliyo teremshwa kwake kutoka kwa Mola Mlezi wake, na Waumini vile vile. Wote wamemuamini Mwenyezi Mungu, na Malaika wake, na Vitabu vyake na Mitume wake. Hatutafautishi baina ya yeyote katika Mitume wake, na (Waumini) husema: Tumesikia na tumet'ii. Tunakutaka maghfira Mola Mlezi wetu! Na marejeo ni kwako.." (al-Baqara, 2/285)

Sema: Tumemuamini Mwenyezi Mungu, na tuliyo teremshiwa sisi, na aliyo teremshiwa Ibrahim, na Ismail, na Is-haak na Yaakub na wajukuu zao, na aliyo pewa Musa na Isa na Manabii wengine kutoka kwa Mola wao Mlezi. Hatubagui baina yao hata mmoja, na sisi ni wenye kusilimu kwake." (Aal-i Imran, 3/84)

Kwa upande wake, Nabii Muhammad (s.a.w) ni kama muendelezo na ukamilishaji wa mitume wote waliotangulia. Hata hivyo, kuna tofauti; yeye ni mtume wa mwisho; hakuna mtume atakayekuja baada yake; kwa hivyo, yeye ndiye aliyeleta Ujumbe wa Kiungu kwa wote.     

Allah, aliyemuumba mwanadamu, anayemjua kwa kina na ndiye anayempa mahitaji yake, alipeleka ujumbe kwa watu katika kila enzi na kuishia kwa Nabii Muhammad (s.a.w). Hivyo, hakutakuwa na mitume baada yake; hakutakuwa na mabadiliko katika ufunuo; na watu watafuata ufunuo wa misho.  

“…Leo nimekukamiliishieni Dini yenu, na nimekutimizieni neema yangu, na nimekupendeleeni UISLAMU uwe ndiyo Dini...” (al-Maida, 5/3)

Na anaye tafuta dini isiyo kuwa Uislamu haitakubaliwa kwake. Naye Akhera atakuwa katika wenye kukhasiri…(Aal-i Imran, 3/85)

Muhammad si baba wa yeyote katika wanaume wenu, bali ni Mtume wa Mwenyezi Mungu na Mwisho wa Manabii, na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi wa kila kitu.(al-Ahzab, 33/40)

Dini ya Uislamu ina kanuni zote zinazomkamilisha mwanadamu kimwili na kiroho na zinazohakikisha furaha yake na uokovu. Uislamu humwongoza mtu na jamii wenye kuifuata kwenda kwenye furaha, kutoka katika uzuri na kwenye ukamilifu kutoka katika furaha. Uislamu unaipa umuhimu hifadhi ya maisha. Unawaadhibu vikali wale wanaojaribu kuvuruga amani katika jamii. Huamuru umoja, kusaidiana na mshikamano. Unalinda uhai wa kijamii dhidi ya vurugu na kitisho.   

Dini ya Uislamu ina kanuni zote zinazomkamilisha mwanadamu kimwili na kiroho na zinazohakikisha furaha yake na uokovu. Uislamu humwongoza mtu na jamii wenye kuifuata kwenda kwenye furaha, kutoka katika uzuri na kwenye ukamilifu kutoka katika furaha. Uislamu unaipa umuhimu hifadhi ya maisha. Unawaadhibu vikali wale wanaojaribu kuvuruga amani katika jamii. Huamuru umoja, vipawa na mshikamano. Unalinda uhai wa kijamii life dhidi ya vurugu na hofu.   

Uislamu unawapa watu maadili makubwa watu na huwanufaisha katika vipengele vyote. Masuala yake yote yana manufaa mengi sana, na huponya maradhi ya kimwili na kiroho. Dini ya Uislamu inazingatia elimu na busara; Hivyo, unawaelekeza watu wenye akili kwenye matendo mema na furaha kwa kuwafanya watumie utashi wao wenyewe. Huutazama ujinga kuwa ni adui mkubwa; huwapeleka watu kwenye tafakuri. Ni lazima kuzingatia hali ya dunia kabla na baada ya Enzi za Upeo wa Furaha ili kufahamu namna dini ya Uislamu ilivyokuwa ni rehema kubwa kwa utu.

Kabla ya Uislamu, dunia nzima ilikuwa katika ujinga na upotovu, kitisho na vurugu. Ushenzi huu na hofu iliyoathiri sana dunia pia iliikumba Rasi ya Uarabuni. Watu walikuwa wakijivuna kwa kuwazika mabinti zao. Waliamini ushirikina, waliabudu masanamu waliyoyatengeneza kwa mikono yao na kuyaomba msaada.

Katika kipindi cha giza, nuru ya Quran iliibuka kama jua kutoka katika pembe ya Rasi ya Uarabuni. Ilivunjavunja matabaka ya ukafiri na ukandamizaji. Iling’aza macho kwa ufunuo wa juu, ilisafisha roho kwa rehema na uongofu, ilichangamsha Akili na kuziongoza dhamiri. Iliondoa ushirikina na kuweka upweke (wa Allah) nyoyoni. Ilondoa uonevu na kuweka haki. Iliondoa chuki na uadui kutoka nyoyoni na kuweka mapenzi, huruma na upole nyoyoni.

Athari hii ya Quran sio finyu kwa kuishia katika Enzi za Upeo wa Furaha pekee. Taifa lolote lililopokea Uislamu na kuutekeleza baada ya hapo lilipata maendeleo katika sayansi, biashara, na kuwa ni mifano ya kuigwa na mataifa mengine. Mfano mzuri zaidi ni maendeleo ya ustaarabu wa Andalusia, wa-Seljuki na wa-Ottoman.

6 Unawezaje kueleza amani hiyo ambayo utu unaitafuta ipo katika Uislamu?

Katika kitabu chake Dhana za Baada ya Mambo ya Sasa, Prof. Dr. Ibrahim Ozdemir anaeleza kwa kifupi kuhusu matendo ya Kiislamu chini ya anwani ya undugu wa Kiislamu pamoja na Utu. Ninakuachieni hakikisho hili muhimu. Ni amani, ndiyo inayotafutwa na utu katika Islam?

Kwa mujibu wa Quran, mwanadamu ni kiumbe bora zaidi kuliko vyote. Yeye ni Khalifa (kiongozi wa umma wa Waislamu) wa Allah (swt) ardhini. Kwa sababu ya hilo, imeambatanishwa umuhimu mkubwa kwake na amepewa heshima. Kuua asiye na hatia kunazingatiwa kuwa ni kuwaua watu wote.

Mtume Muhammad (s.a.w) aliyaheshimu mazishi ya wasio-Waislamu, kwa hiyo hilo lilisisitiza jinsi kulivyo na umuhimu mkubwa wa kuwa mwanadamu kuliko kuwa katika dini yoyote. Dhana hii ina fungu kubwa kwa Waislamu kuwastahamilia watu wengine wa dini tofauti na kuwa na desturi ya kujadiliana nao.

Kwa upande mwingine, kwakuwa dhana ya Kiislamu kuhusu dini zingine inategemea hukumu za Quran, kamwe hawajawashurutisha watu kubadili dini chini ya kuyumba kwao. Inapaswa ionekane kuwa ni tokeo la kiasili la kanuni (la Quran), Hakuna kulazimishana katika dini. (Baqarah Surah, 2:256)

Hapo, watu waliokuwa katika eneo lililopigwa vita kamwe hawakukumbana na ushurutishaji, mbali na sharti la kulipa kodi maalumu (jizya); wameachwa huru kuchagua imani yao.

Baadhi ya kauli za Mitume (s.a.w) zimeleta nuru kuhusu suala la watawala wa Kiislamu. Nazo ni;

“Mwenye kuwadhuru raia Wasio-Waislamu raia katika dola ya Kiislamu ananidhuru mimi, na anayenidhuru mimi anamuudhi Allah." (Sahih Bukhari, Hadith)

"Mwenye kuwadhuru raia Wasio-Waislamu katika dola ya Kiislamu, mimi ni adui yake, na nitakuwa adui yake katika Siku ya Kiama." (Bukhari)

Kulazimishwa katika dini kulikatazwa tangu siku ya kwanza ya Uislamu kwa sababu tu ni kinyume na msingi wa dini. Imeelezwa waziwazi katika Quran Tukufu kuwa mpango wa Mtume Muhammad ni kufikisha maagizo ya Allah na uongofu na si kuwashurutisha kuwa Waislamu.

Utendaji wa Mtume Muhammad (s.a.w) kwa hakika umefanyika kulingana na kanuni za Quran. Kama inavyoeleweka, Mtume Muhammad (s.a.w) alianza kuishi pamoja na Wayahudi baada ya kuhama kutoka Makka kwenda Madina. Mtume (s.a.w) aliacha waraka (hati) ulioandikwa kuhusu mahusiano yake na Wayahudi. Mkusanyiko wa sheria zilizopangwa katika mfumo maalumu, ambazo Mtume Muhammad (s.a.w) aliziweka pamoja na vipaumbele vya kiraia vya Madina zinapaswa zikubalike kuwa ni katiba ya kwanza ya kimaandishi ambayo haikuwahi kufanywa hapo kabla na dola tawala.

Katika katiba hii ya kimaandishi, yenye ibara hamsini ilieleza kuwa Wayahudi wanaweza kuendelea na dini yao. Kwa kueleza hayo, Wayahudi na marafiki zao walikuwa wamepewa uhuru wa kidini.

Eneo la Najran lilikuwa katika upande wa kusini mwa Makka, palikuwa ndio kitovu cha Ukristo. Mtume Muhammad (s.a.w) pamoja na mkataba maarufu aliowekeana pamoja na Wakristo wa Najran aliwaekea uhuru wa kidini kujitawala. Juu ya hayo, haki za kinga ya maradhi ilitolewa kwa madhabahu yao na kwa viongozi wao wa kidini.

Kanuni hizi za msingi zilizoelezwa kwa uangalifu katika Quran na Sunnah (Vitendo adhimu vya Mitume), baadaye zikatumiwa na watawala wa Kiislamu. Kwa muktadha huu maagizo ya Abu Bakr (as) [Halifa wa kwanza (kiongozi wa umma wa Waislamu)] baada ya kifo cha Mtume Muhammad (s.a.w) aliyowapa makamanda wake watendaji na mkataba alioweka Omar (as) wakati wa ushindi wa Jerusalem unaakisi mtazamo huo huo. Juu ya hayo, Abu Bakr katika maagizo yake kwa mmoja wa makamanda wake, msikate mitende, miti yenye matunda, na msiue wanyama kama kondoo, ngamia, na mbuzi isipokuwa [mkimhitaji] kwa ajili ya chakula, kwa kuyapa umuhimu maskani ya kiasili hata katika nyakati za vita.

7 Je, kuna kanuni kama vile "Hakuna kuulizana katika dini" katika Uislamu? Kama ipo, inamaanisha nini?

Kuna namna mbili za amri za shari'ah:

1. Amri na makatazo yanayokuja moja kwa moja kutoka kwa Allah; tunaziita “taabbudi”, yaani, sababu (hekima) zake hazijulikani.

2. Sehemu ambayo sababu (hekima) zake zinapatikana katika amri za Allah na makatazo ya Allah; tunaziita “maqul al-mana”.

Tunaweza kuangalia swali lako katika sura tofauti. "Kwa nini swala ya asubuhi iwe na rak'ah nne na si kumi au ishirini?" (Rakaa nne ni mjumuiko wa rakaa mbili za faradhi, na mbili za sunna ) Jibu ni "kwasababu Allah ametuamrisha kufanya hivyo."

Swala ya adhuhuri ilipangwa na Allah iwe ya rak'ah 10 (Nne za faradhi na sita za sunna kabliya na baadiya). Kutafuta hekima yake hakutafanikiwa. Jawabu sahihi la swali hilo ni kwa sababu Allah ameamrisha hivyo. Hata hivyo, baadhi ya kanuni za shari'ah zinaweza kufafanuliwa kwa hekima, lakini hizo si sababu halisi. Sababu za uhakika ni amri za Allah na makatazo.

Mathalani, "Kwa nini Allah ameamrisha salah (swala)?" Mtu anaweza kuorodhesha hekima na madhumuni ya jambo hilo katika vitabu vikubwa-vikubwa. Mtu anaweza kujibu kwa nini tunafunga saumu kwa kutafuta hekima na sababu zake. Hata hivyo, sababu (hekima) na manufaa hayawezi kushika nafasi ya Amri za Allah. Mathalani, sababu mojawapo ya kufunga ni kuhisi namna watu wanavyoumizwa na njaa na kuwaendea kwa huruma.

Hivyo, mtu anaweza kusema “Ninaweza kuhisi njaa zaidi na kuzidisha huruma yangu na ninaweza kumsaidia masikini zaidi na zaidi.” Ingawa wakati wa imsak (muda wa kuanza kufunga) ni saa kumi alfajiri, kama mtu anakusudia kufunga saa tano usiku, lakini kama atafungua dakika 5 kabla ya iftar (kufuturu wakati wa magharibi), je, funga yake itakubaliwa? Hapana kwa hakika. Kuna wakati maalumu uliopangwa wa kufuturu. Na ingawa mtu anabakia na njaa kwa muda mrefu zaidi, funga yake haikubaliki. Hiyo inamaanisha kuwa, hekima ya kufunga inayotakiwa imetumika (kwa kubakia na njaa), lakini kwa sababu ya kufungua katika wakati asiouruhusu Allah, funga yake haikubaliwi.

Hivyo, tuziangalie amri zote na makatazo yote kwa namna hiyo. Hiyo inamaanisha kuwa, tunaitekeleza kwa sababu Allah ametuamrisha tufanye hivyo. Kwa hakika, zinaweza kuwepo sababu (hekima) zake, pia. Na sababu hizi zinaweza kutafutwa. Hiyo pia ni elimu na ibada. Hata hivyo, hekima na manufaa kwa hakika si sababu halisi, bali ni ufafanuzi.

8 Nini kifanyike ili kuujua na kuutekeleza vyema Uislamu?

Mtu anapaswa ategemeze maisha yake ya kidini juu ya Sunnah ya Mtume, si katika akili yake na mantiki. Maana yake, anapaswa ajue namna Mtume alivyotekeleza dini na alichounasihi ummah wake.

Je Uislamu ni dini ya kinadharia tu bila ya kutekelezwa kivitendo? Inapaswa utafute majibu ya maswali haya hapo juu na ujaribu kuutekeleza Uislamu kwa kujisalimisha kwa Allah. Kunaweza kuwepo tofauti kadhaa katika maisha ya mtu katika hatua fulani za maisha kutokana na athari za umri wake.

Tunapotaja Uislamu, jambo la kwanza linalokuja akilini ni Quran na maisha ya Mtume. Allah alishusha kitabu chenye amri na makatazo na Mtume aliyetekeleza yaliyomo ndani ya kitabu hicho. Basi, njia ya kuwa Muislamu mzuri ni kutii Quran na Mtume (s.a.w). Kumfanya Mtume, ambaye ni Quran hai, kama mfano ni jambo analolipenda sana Allah. Kwa hakika, Allah anaeleza yafuatayo katika Quran: “Sema: Ikiwa nyinyi mnampenda Mwenyezi Mungu basi nifuateni mimi, Mwenyezi Mungu atakupendeni na atakufutieni madhambi yenu.'” (Aal-i Imran, 31)

Katika hadithi iliyosimuliwa na Abu Dawud, Mtume amesema, “Tahadhari! Katika wakati mfupi ujao, baadhi ya watu watasema Quran inatutosha. Hata hivyo, nimepewa elimu kiasi au mara mbili ya kiasi cha Quran.” Hivyo, akaeleza kuwa Quran haiwezi kufahamika kikamilifu bila ya Mtume.

Ama kuhusu amri ambazo wanazuoni wa Kiislamu wamezitoa kutoka katika Quran, tuna aya ifuatayo, ambayo iko waziwazi, kuhusu jambo hilo: “…Na lau kuwa wangelilipeleka kwa Mtume au kwa wenye mamlaka kati yao, wale wanao chunguza wangelilijua...” (an-Nisa, 83)

Kama inavyoweza kuonekana, tumeombwa tuwaendee wale waliopewa mamlaka baada ya Mtume. Kuwepo kwa madhhab manne ndio ufafanuzi wa aya hiyo.
Kwa kuhitimisha, njia ya kujifunza vyema Uislamu na kuutekeleza ni kulingana na Quran, Sunnah na hukumu zilizotolewa na wanazuoni wa Kiislamu kutokana na vyanzo hivyo viwili. 

Ama kuhusu kutafiti dini zingine na rai zilizo kinyume na Uislamu, ni muhimu kwetu kujifunza sana dini yetu na kwa usahihi kwanza. Inafaa kutafiti vitu vizuri jaani katika maeneo ya jirani nasi kabla hatujajenga misingi na kuta za jengo letu kwa uimara? 

Msinielewe vibaya; sitaki kusema kuwa hakuna jema huko bali kama tunataka kupita katika chumba chenye sumu, tunahitajika kuvaa kichuja hewa madhubuti. Vinginevyo, tutadhurika na sumu. Kama tunataka kutafiti baadhi ya mambo yanayodhuru dini na yenye sumu, tunahitaji kichuja hewa kizuri kitakachozuia gesi za namna zote, maana yake, tunahitaji imani nzuri na ya kweli ya kidini ili rai hizo zisitudhuru.

Ndiyo, njia pekee ya kumpata Allah na ukweli ni kuiamini Quran na kutenda kulingana nayo kwa sababu Quran ni kitabu kitukufu kilichoteremshwa na Allah ili kuwaongoza wanadamu kwenye kheri na ukweli. Quran ndiyo itakayomwonesha mwanadamu furaha kamili ya kidunia na ya ulimwengu mwengine na itakayoitengeneza hulka ya mwanadamu. Inamwita mwanadamu kwenye imani na upwekeshaji, ibada na utumishi, undugu na upendo. Inaweka vigezo bora kabisa kuhusu imani na amali njema. Uislamu umejengwa kwa kuegemea juu ya vigezo vya Quran. Hakuna ukweli nje ya kanuni imara na adhimu za Uislamu na hakuna haja ya kutafuta. Chochote ambacho Quran inakiona chema na kukisadikisha ni kweli; chochote inachokiona kibaya na kukikataa ni batili. Uislamu, uliowekwa na Quran, unazikataa imani potofu za zamani, ushirikina, fedheha na umalaya. Kisha, Waislamu wote wanahitajika kutathmini mambo halisi matukufu yanayohusiana na itikadi, ibada, maadili, halali, haramu, kumtaja Allah, fikra na upendo unaotegemea Quran.

Aya za Quran zina nguvu ya kutosha kumshawishi kila mmoja. Watu wa kawaida wanapenda uwazi wa mtindo wake; wasomi na wanasayansi wanavutiwa na ufasaha wake na balagha yake. “Bila ya shaka, katika kumkumbuka Allah nyoyo hupata kuridhika.” Watu wenye fikra nyingi wa ngazi zote hutosheleza haja yao kwa ajili ya imani kwa Quran na wanakomaa kwa kuifuata. 

Quran imemhimiza mwanadamu atafakari na imempa vigezo kwa ajili ya hili. Watu wameweza kusoma kitabu cha ulimwengu kupitia vigezo ilivyofundisha, wamevumbua ukweli mwingi uliojificha ndani mwake na wamempata Muumbaji na Mola wao. Ni nuru ya Allah iliyowekwa akilini ili kumulika gizani na katika njia za maisha zenye dhoruba. Jua linaangazia dunia yakinifu na Quran imeteremshwa ili kuangazia dunia ya kiroho.

Yafuatayo yameelezwa katika Quran: “Hakika hii Qur'ani inaongoa kwenye ya yaliyo nyooka kabisa.” (al-Isra, 9)

Ni muhimu kufuata sheria za sayansi ili kufanikiwa katika sayansi hiyo; halikadhalika, ni muhimu kukubali kanuni za Quran na Sunnah ili kuupata ukweli.

Ndiyo, mwanadamu anaweza kujua nafsi na sifa za Allah Mtukuka kwa njia ya uongofu wa Quran na Sunnah tu. Anaweza kufahamu anapotoka na anapokwenda, ana jukumu gani duniani, maumbile na uhalisi wa dunia nyengine, na kitakachokubaliwa na kukataliwa huko kwa kupitia njia hizo mbili. Atajifunza aina ya amali, vitendo na mitazamo itakayovutia radhi za Allah Mtukuka na amali zipi, vitendo na mitazamo itakayovutia ghadhabu Zake, kipi ni kweli na kipi si sahihi, kipi ni kosa na kipi ni sawa kutoka katika kitabu cha Allah na Mtume Wake. Kila Muislamu ana wajibu wa kutambua dunia yake ya imani na kuabudu chini ya uongofu wa viwili hivyo halisi.

Pia atajifundisha kutokana na misingi hiyo miwili, Quran na Sunnah, jinsi atakavyoingia katika wigo wa Uislamu na kuamini kanuni mahususi na jinsi atakavyodumu katika wigo wa Uislamu (kwa kutenda amali fulani na kuacha amali fulani). Kwa kuwa vigezo vya Waislamu wote ni Quran na Sunnah, Muislamu anatakiwa kutathmini rai zote za kibinadamu, madai, imani na itikadi zinazoegemea juu ya Quran na hadithi, ambazo ni tafsiri ya Quran.

Mosi, Quran inatufundisha kanuni za imani, "kumwamini Allah, kadhalika na kuwaamini malaika, vitabu vya kiungu, mitume, akhera, qadar (kwamba Allah ameumba kila kitu, iwe kheri au shari). Mtu anakuwa muumini pindi tu anapoamini ukweli wa imani kama ulivyoelezwa katika Quran.

Quran imefundisha Uislamu ambao una maamrisho na makatazo yote ya Allah, kwa waumini. Muumini anapotii hayo mamrisho na makatazo, anakuwa ni Muislamu kamili.

9 Ni yapi masharti ya msingi ambayo dini ya Uislamu inayomshurutisha mtu?

Ili kuweza kufahamu umuhimu unaopewa haki za kibinaadamu katika Uislamu, ni lazima tuangalie hali ya dunia kabla ya Uislamu.

1. Dola zote za duniani zilikuwa zikitawaliwa na tawala za kifalme. Mfalme, mtawala au dola ilikuwa na mamlaka kamili juu ya watu aliowatawala. Aliweza kumnyonga yeyote kwa matakwa yake na hakuwajibika kwa yeyote.

2. Watu waligawanyika katika matabaka. Watu waliomzungua mfalme, ndugu zake na waheshimiwa walikuwa katika daraja la upendeleo. Kwa upande mwingine, kulikuwa na watu wengi waliotwezwa na ambao haki zao zilikiukwa, hao waliunda tabaka jingine. Kulikuwa na tofauti kubwa baina ya matabaka.

3. Utumwa ulitumika katika hali ya unyama mkubwa. Heshima ya mwanadamu ilikandamizwa.

4. Watu walikuwa wakitendewa kulingana na mbari zao na rangi, ubora wa ukoo ulizingatiwa kuwa ndio kigezo pekee. Watu hawakuthaminiwa kwa akili zao, elimu, uwezo, maadili na wema.

5. Hakukuwa na haki za msingi na uhuru. Haki za msingi kama vile uhuru wa dini na dhamiri, haki ya kumiliki mali, uhuru wa kupata makazi, uhuru wa fikra haukumhusu raia wa kawaida. Watu walikuwa wakidhulumiwa na kuteswa kutokana na imani zao na fikra.

6. Kanuni za msingi za sheria zilikandamizwa chini ya miguu. Haikuwezekana hata kufikiria dhana za sheria za msingi kama vile usawa mbele ya sheria, utawala wa sheria, haki ya kutoingiliwa (faragha) na uhalali wa adhabu. Hakukuwa na mahakama huru na isiyopendelea. Matakwa binafsi na amri ziliiweka kando sheria; watu waliotenda uhalifu uliofanana waliadhibiwa adhabu tofauti kwa kuzingatia matabaka yao.

Dunia ilipokuwa hatika hali hii, dini ya Uislamu ilikuja na kufanikisha mapinduzi makubwa katika historia ya mwanadamu.

Ikiangaliwa kwa macho yasiyo na upendeleo, itaonekana kuwa malengo makuu ya kibinadamu yanayoamuliwa sasa yalishaamuliwa katika Quran na katika Sunnah za Mtume Mtukufu kwa karne nyingi kabla ya matamko ya haki za kibinaadamu kutolewa katika ulimwengu wa Magharibi.

Kwa hakika, kanuni zinazohusu haki za kibinadamu zilizomo katika hotuba (Hotuba ya Kuaga) aliyohutubu Mtukufu Mtume (s.a.w) wakati wa Hajj ya Kuaga ni mfano wa wazi juu ya hilo.

Hotuba hiyo iliyosomwa katika hadhara ya Waislamu zaidi ya 100.000 mnamo mwaka 632 BK; yaani, miaka 1157 kabla ya Tamko la Haki za Mwanadamu na  Raia kutolewa mwaka 1789, linalozingatiwa kuwa ni waraka wa kwanza wa kimaandishi unaohusu haki za kibinaadamu.

Kanuni hizo mpya zilizowekwa na Uislamu kuhusu haki za kibinaadamu zilikuwa ni zenye kuvutia mno juu ya kupigania haki za kibinaadamu huko Magharibi.

Mwanadamu ana thamani zaidi ya kipekee kuliko viumbe wengine. Thamani hiyo huongezeka anapomwamini Allah na kutii amri Zake. Hivyo, mwanadamu anakuwa mgeni mheshimiwa zaidi ulimwenguni. Mwanadamu anapata thamani ya utu anapozaliwa au hata kabla yake, kwa kuumbika kwake katika mji wa mimba, na anakuwa nayo katika maisha yake yote.

Thamani inayoanzia tokea kuwa mwanadamu inamwenea kila mmoja. Huruma hii imemzingira kila mmoja, mwanamume au mwanamke, mzee au kijana, mweusi au mweupe, mnyonge au mwenye nguvu, masikini au tajiri pasi na kujali dini, taifa, mbari na rangi zao.

Hivyo dini ya Uislamu inahifadhi damu ya kila mmoja isimwagwe, heshima isivunjwe, mali isiporwe, nyumba isiingiliwe bila ya ruhusa, ukoo usivunjwe na dhamiri kutokandamizwa. Inahakikisha heshima na hadhi ya kibinadamu.

Haki za msingi na uhuru ulioleta utu kutokana na Uislamu ni kama ifuatavyo:

1. Uislamu umemaliza ubaguzi wa kimbari na rangi. Watu wote wanatokana na Adam. Haiwezekani mtu kujichagulia mbari na rangi. Ni kudura ya Allah. Ni makosa makubwa na madhara makubwa kwa Uislamu na utu kuwabagua watu kwa rangi na mbari na kudharau baadhi ya mbari na rangi na kuwatazama wengine kuwa ni bora.

Allah anaeleza katika Quran kuwa amewaumba watu kutokana na mwanamume mmoja na mwanamke mmoja, na akawafanya mataifa na makabila wanapoongezeka ili waweze kujuana. (al-Hujurat, 13)

Kama ilivyoonekana, sababu ya watu kutofautiana kwa mbari na rangi ni kujuana na kusaidiana wala si kudai kuwa ni bora.

Tukio litakaloangazia ufahamu huu wa Uislamu ni kama ifuatavyo:

Swahaba Abu Dharr, siku moja alimkasirikia Bilal al-Habashi na akamtukana kwa kumwita, “mtoto wa mwanamke mweusi”. Abu Dharr alimdharau kwa sababu ya rangi ya mama yake. Mtume (s.a.w) alipoambiwa hayo, Mtume alikasirika na akamwambia Abu Dharr kama ifuatavyo:

— Ewe Abu Dharr! Umemshutumu Bilal kwa sababu ya rangi ya mama yake? Inamaanisha kuwa bado una fikra za Jahiliyya!"

Abu Dharr, ambaye alitamka maneno hayo kutokana na kushikwa na ghadhabu za ghafla bila ya kukusudia, alisikitikia sana alichofanya na akatubu. Alianza kulia, akalala chini na kuweka uso wake chini; kisha, akasema,

 “Sitainua uso wangu kutoka ardhini isipokuwa mpaka Bilal aje kunikanyaga shavuni.” Akakariri kumwomba msamaha Bilal.

2. Uislamu umekomesha jambo la kujifaharisha kwa koo na mababu. Katika mkutano ambao Maswahaba walikuwepo, Sa'd bin Abi Waqqas aliwaomba baadhi ya Maswahaba mashuhuri wawaorodheshe wahenga wao. Wakati huo huo, aliwaorodhesha wahenga wake tokea mwanzo mpaka mwisho. Salman al-Farisi (Mwirani) pia alikuwepo hapo. Hakuwa na wahenga wa kujifaharisha nao kama wa-Qurayshi. Hakuwajua wahenga wake kwa kina, pia.

Sa'd bin Abi Waqqas alipomwomba awaorodheshe wahenga wake, hakupendezwa na ombi hilo na akasema, “Mimi ni Salman; mwana wa Uislamu. Siwajui wahenga wangu kama mlivyo nyinyi. Ninajua jambo moja tu. Allah amenitukuza kupitia Uislamu.”

Swahaba Umar pia aliudhiwa na jambo hilo lisilo la lazima la Sa’d lililoleta hisia za Jahiliyya. Alilipenda sana jibu hili lenye maana kubwa la Salman; akasema, “Mimi ni Umar; mwana wa Uislamu.” Hivyo, alitoa jibu sawa na la Salman.

Mtume (s.a.w) aliposikia habari za tukio hilo, alilipenda sana jibu la Salman. Akasema, “Salman ni katika mimi; anatoka katika familia yangu.”

Mtume aliwaozesha mabinti wa familia mashuhuri za wa-Quraysh kwa baadhi ya watumwa waliopewa uhuru miongoni mwa Maswahaba; hivyo, aliondosha fikra za Jahiliyya zilizoegemea ubora wa koo.

3. Uislamu umewapa watu haki ya kuangalia na kuwakagua watawala wao. Unalenga kumaliza vitendo vya kidikteta, uonevu, dhuluma na uhalifu.

Swahaba Abu Bakr alipoteuliwa kuwa Halifa, aliwahutubia watu kama ifuatavyo:

"Enyi watu! Nimeteuliwa kuwa ni kiongozi wenu ingawa mimi si mbora zaidi baina yenu. Kama nitatekeleza jukumu langu kulingana na Uislamu, nitiini. Kama nitaiacha njia sahihi, nionyeni."

Siku moja, wakati wa Ukhalifa wake, Swahaba Umar aliwauliza Waislamu msikitini, "Mtafanyaje kama nitaiacha njia sahihi? Wakasema, "Tutakusahihisha kwa mapanga yetu." Swahaba Umar akafurahi baada ya kusikia jibu hilo.

4. Uhuru wa fikra na dhamiri. Uhuru wa fikra na dhamiri ni haki muhimu zaidi baada ya haki ya kuishi. Kumnyima mtu haki hii kunamaanisha kumtoa katika utu wake na kumshusha mpaka katika kiwango cha wanyama. Kwa hiyo, Uislamu hauruhusu kukandamizwa fikra na dhamiri. Huku kukiwa na kanuni, “kusiwe na kulazimishana katika dini”, Uislamu haukuzingatii huko kufaa kuwafanya watu wakubali kanuni za imani kwa nguvu.

5. Uislamu umeshughulikia desturi ya utumwa kwa uangalifu sana na kulipa hilo ngazi ya kisheria.

Dini ya Uislamu ilipokuja, utumwa ulikuwa umeenea kote duniani pamoja na vitendo vyake viovu sana na vya kinyama. Uislamu kwa kawaida haukutarajiwa kuukomesha mfumo huo kikamilifu, ambao ulienea duniani kote. Kwa hivyo, haukukomesha utumwa kisiasa kali na kwa ghafla lakini ulirekebisha sana masharti na kuupa hali ya utu na ustaarabu zaidi. Licha ya hayo, Uislamu uliongeza na kurahisisha njia za uhuru na kuingiza kanuni ambazo zingekomesha utumwa kwa njia isiyo dhahiri.

6. Uhuru wa Mali. Kupenda vitu na tamaa ili kupata mali ni miongoni mwa hisia kadhaa ambazo Allah alimpa mwanadamu. Hili limeelezwa wazi katika Quran.

Uislamu umempa kila mtu haki ya mali na kuwaandalia namna ya kutimiza haja hii kihalali. Haki iliyowekwa na Uislamu kwa kila mmoja kuweza kumiliki mali kamwe haiwezi kuingiliwa bila ya idhini ya mwenyewe.

7. Usawa wa Kisheria. Uislamu unawatazama watu wote kwa usawa mbele ya sheria kama yalivyo meno ya kitana. Hauruhusu upendeleo unaozingatia hali ya kijamii na koo za watu.

Katika Uislamu, utawala wa sheria na sheria hiyo kuwa juu ni lazima. Mkuu wa dola na watu wa kawaida  hutendewa sawa. Mhalifu kwa hakika huadhibiwa hata kama ni mkuu wa dola.

Kesi ya Fatih Sultan Mehmet na msanifu majengo wa Kigiriki, Swahaba Ali na Myahudi, Salahaddin al-Ayyubi na Mwarmenia katika hadhara ya makadhi ni mifano yenye kuvutia sana kuhusu jambo hili.

Katika siku ya ushindi wa Makkah, mwanamke mmoja kutoka familia mashuhuri ya kabila la Makhzum aliiba na kukamatwa nacho. Alipaswa kuadhibiwa. Hata hivyo, kwa kuwa alikuwa ni wa familia mashuhuri, hawakutaka familia hiyo kuaibika; kwa hivyo, walitaka mwanamke huyo asamehewe. Wangelifanyaje hilo? Wangemweleza nini Mtume kuhusu hilo? Hatimaye, waliamua kumtuma Usama, ambaye Mtume alimpenda sana, kwenda kwa Mtume. Usama alikwenda mbele ya Mtume na kumweleza suala hilo. Akamwomba Mtume amsamehe mwanamke mwenye hatia. Mtume alikasirika sana. Akatoka na kutoa hotuba ifuatayo ya kihistoria: “Enyi watu! Mnajua sababu za umma za kabla yenu kuangamizwa? Mtu wa hadhi ya juu alipotenda uhalifu, wao, walimwachilia. Mtu wa kawaida alipotenda kosa, kwa hasira walimtaka mtu huyo aadhibiwe. Ukandamizaji huu ulisababisha kuangamizwa kwao. Naapa kwa Allah, kama Fatima, binti wa Muhammad, angeiba, ningemwadhibu bila ya kusita.

Hapo, adhabu ilitimizwa.

Maneno yaliyo katika hotuba ya Swahaba Abu Bakr alipoteuliwa kuwa Khalifa hayana kifani.

"Walio dhaifu miongoni mwenu ndio wenye nguvu zaidi machoni mwangu mpaka wapate haki zao; wenye nguvu ni dhaifu sana machoni mwangu mpaka nichukue haki za wengine kutoka kwao."

8. Kutoingiliwa na Uhalali wa Adhabu. Katika Uislamu, hakuna adhabu bila ya sheria, na haiwezekani kumwadhibu mwingine badala ya mhalifu.

Kanuni ya kutoingiliwa na uhalali wa adhabu imeelezwa kama ifuatavyo katika sura al-Anam: "Na kila nafsi haichumii ila nafsi yake. Na habebi mwenye kubeba mzigo wa mwenziwe." (Aya: 164)

9. Uhuru na Uadilifu wa Mahakama. Katika Uislamu, mahakama, ambazo ni taasisi za haki, zimeepushwa na kila namna ya msukuko kutoka nje, chuki binafsi na kinyongo, na matendo ya kidikteta; mahakimu hawaruhusiwi kupoteza uadilifu wao. Katika mahakama za Kiislamu, wakuu wa dola wameshitakiwa sambamba na raia wa kawaida; walikuwa wakiadhibiwa ikiwa walikutwa na hatia.

10. Kinga ya Makazi na Kutoingiliwa. Katika Uislamu, hakuna mwenye haki ya kumwingilia mtu na kuingia katika makazi yake bila ya idhini. Katika Uislamu kumekatazwa kupeleleza mambo ya faragha ya watu.

11. Uhuru wa Kusafiri. Uislamu unazingatia kuwa safari humsaidia mtu kujifunza mambo na kupona maradhi. Kwa hiyo, watu wanahamasishwa kusafiri.

12. Haki ya kuishi na kuhakikisha ulinzi wa uhai, mali na heshima. Hili limeelezwa vyema na Mjumbe wa Allah katika Hotuba ya Kuaga:

"Enyi Watu!, kama mnavyoutazama mwezi huu, siku hii, na mji huu, Makkah, kuwa ni mtukufu, basi utazameni uhai, mali na heshima ya kila Muislamu kuwa ni dhamana takatifu. Hayo yamehifadhiwa dhidi ya namna zote za ukiukwaji."

13. Hifadhi ya Kijamii. Dini ya Uislamu inamlinda mtu ili asipate tabu na asidhuriwe kwa uzee, ugonjwa, majanga, na ajali; unamhakikishia maisha mema ya baadaye wa masikini kwa njia za hifadhi ya kijamii ilizoziweka. Uislamu unawahimiza watu kufanya kazi kwanza ili waweze kujitunza wenyewe kifedha. Kwa kuongezea, umeweka hifadhi ya kipekee katika familia na baina ya majirani na shukrani ziende kwenye taratibu kadhaa ilizoziweka. Taratibu hizo zote za hifadhi zisipotosheleza, dola yenyewe inahakikisha hifadhi ya kila mmoja. Utaratibu wa zakah na taasisi zingine ndizo hifadhi za uhakika za kijamii.

14. Uhuru wa kazi, mishahara, haki na usawa. Kufanya kazi na kufanya juhudi kunatambuliwa na kuhimizwa katika Uislamu. Hakupendezi kuombaomba na kuwa ni mzigo kwa wengine. Kufanya kazi ili kupata riziki kwa njia halali kunazingatiwa kuwa ni ibada kama mtu huyo atakamilisha majukumu yake ya faradhi. Aya inayosema "Mtu huyo hatakuwa na kingine isipokuwa kile anachokipigania" inaonesha umuhimu ambao Uislamu umeweka kwenye bidii na kazi.

Kwa kuhakikisha uhuru wa kazi — kwa sharti kuwa imepatikana kihalali —, Uislamu unapanga mahusiano baina ya waajiriwa na mwajiri katika njia bora kabisa.

Kanuni ya "Mlipe mfanyakazi mshahara wake kabla jasho lake halijakauka" inahakikisha haki ya mfanyakazi katika njia kamilifu.

Kama ilivyo kanuni, mfanyakazi atajitaidi kufanya kikamilifu kazi aliyopewa na kwa namna bora zaidi na kustahiki mshahara anaoupata.

15. Ulinzi wa Watoto. Uislamu unawatunza watoto tangu kuzaliwa kwao, unawasaidia wazazi katika matumizi yao ya chakula na mavazi na unatenga mali kwa ajili yao kutoka hazina. Leo, dola zote tajiri huwapa ruzuku wazazi kwa ajili ya watoto. Mjumbe wa Allah alilisisitiza jeshi lake kutowaua wanawake na hususani watoto wakati wa vita.

16. Elimu ya Msingi ni Lazima na Bure. Hadithi inayosema, "Kutafuta elimu ni faradhi kwa kila Muislamu, mwanamume na mwanamke" inaweka elimu ya lazima. Mtaala wa elimu ya msingi umeandaliwa kwa uangalifu katika Uislamu.

Pamoja na, elimu ya kidini, elimu ya kimaadili na ya kujua kusoma na kuandika, elimu ya ufundi imejumuishwa katika elimu ya msingi. Uislamu unaona kuwa ni lazima mtoto ajifundishe elimu ya ufundi pamoja na elimu ya dini.

10 Kwa nini Allah amefanya dini nne za lazima? Je isingekuwa sawa kama ungepelekwa Uislamu tu?

Kila kitu ni bora katika mazingira kilipokuwepo. Hata hivyo, kwa ujumla kuna jambo ambalo ni bora zaidi na zuri zaidi ya mambo yote.

Kwa mfano, katika Qur’an tukufu, kumeelezwa kuwa mwanadamu aliumbwa kwa udongo bora mwusi. Kwa ulinganifu, vitu vingine viliumbwa kwa dosari? Hapana. Hivyo pia ni viumbe vizuri sana katika mazingira yao wenyewe.

Kwa mfano, jua ni zuri mno katika mazingira yake lenyewe. Kwa maneno mengine, hakuna watu ambao wangeweza kuishi kama Jua lisingekuwepo. Hata hivyo, mwanadamu ni Mzuri sana kwa ujumla, na Jua ni Zuri sana kwa upande wa kuwepokwake, na kwa upande wa Kazi linayofanya. Tunaweza kutoa mifano mingine zaidi. Kondoo, ardhi, miti ya matunda, malaika, n.k. vyote ni viumbe wazuri sana na wakamilifu kabisa katika mazingira yao wenyewe.

Kwa hali hiyo, ukweli kuwa mwanadamu ni mkamilifu zaidi haimaanishi kuwa viumbe wengine si wakamilifu na kuwa wameumbwa wakiwa na kasoro.

Hakuna kondoo wengine walio wakamilifu kuliko wale kondoo waliopo wanaweza kufikiriwa. Hakuna ngamia wengine zadi walio wazuri zaidi kuliko ngamia hao au hakuna jua zuri zaidi kuliko Jua linavyoweza kufikirika. Kwa namna hiyo hiyo, vitabu vitukufu vilivyoshushwa vilikuwa vikamilifu zaidi vilivyopelekwa katika nyakati hizo.

Kumfundisha mwanafunzi mwanafunzi wa shule ya msingi jedwali la kuzidisha namba si ziada wala upungugufu. Hata hivyo, si jedwali lakuzidisha namba bali mada za masomo ya juu hufundishwa mwanafunzi wa chuo kikuu. Halikadhalika, vitabu vitukufu vilivyotumwa kabla ya Qur’an vilikuwa bora sana katika wakati wao na kuvituma katika wakati huo kulifaa na si upungufu. Kwa mtazamo huo, kila mtume na kila ufunuo waliopelekewa ni bora na ulifaa sana kwa wakati wake.

Hata hivyo, kwa maneno mengine, Qur’an ilishushwa pindi watu wote walipokuwa katika kiwango sawa na cha wanafunzi wa chuo kikuu ambao wanaweza kuchukua masomo yao kutoka katika kitabu kimoja na kutokakwa mtume mmoja.

Kwa kutazama kuwa sayansi nyingi zilizosonga mbali hufundishwa katika vyuo vikuu, je tunaweza kusema sayansi inayofundishwa katika chuo kikuu inapaswa wafundishwe watoto wa shule za msingi? Wanadamu pia kama taasisi ya elimu. Kila kipindi ni kama idara za shule na wahadhiri wa idara hizo ni Mitume.

Kwakuwa tangu wakati wa Adam (amani iwe juu yake), wanadamu wamefikia mpaka katika kiwango cha chuo kikuu na wamepata uwezo wa kuchukua mafunzo kamili ya dini ya Uislamu. Kwa hivyo, dini kamilifu zaidi ilibakishwa kuwa ndio ya mwisho. Umuhimu wa hisabati pia upo hata katika shule ya msingi. Hata hivyo, somo hilo hufundishwa kulingana na kiwango cha wanafunzi wa shule ya msingi na mwalimu hafundishi kila anachokijua bali hufundisha mada wanazoweza kuelewa.

Vivyo hivyo, mitume wengine waliwafundisha watu kulingana na viwango vyao na wakawaelimisha. Mwishowe, walipofikia kiwango cha kuweza kufundishwa katika vipengele vyote, dini ya Uislamu na Mtume mtukufu (s.a.w) aliletwa.

-Kwa nini Allah aliachilia Injili na Taurati kugeuzwa-geuzwa na Akailinda Qur’an? Kwa nini Allah aliachilia maneno Yake kubadilishwa hapo kabla?

1. Kumtegemea Allah juu ya yale tusiyojua sababu (busara) zake kunadhihirisha ukamilifu wa imani yetu na uaminifu wetu kwa dini yetu.

2. Viumbe alivyoviumba Allah duniani havilingani. Yeye huviambatanisha baadhi kwa kuwepo sababu na kuumba baadhi yao bila ya sbabu au maana. Kwa mfano, ingawa kila mtu anatokana na mama na baba, alimuumba Adam (s.a.w) bila ya mama na baba, Isa (s.a.w) bila ya baba na Hawa bila ya mama. Inamaanisha kuwa wakati mwingine huwa Anatenda nje ya sheria za ujumla.

Aidha, kwa mujibu wa sheria, moto huunguza, Mwezi haupasuki katika vipande viwili, miti haitembei na fimbo hazigeuki nyoka. Hata hivyo, kwa amri na utashi wake Allah, Ibrahim (s.a.w) hakuunguzwa na moto, Mwezi ulipasuka vipande viwili, mti ulitembea kwa amri ya Mtume (s.a.w) na fimbo ya Musa (s.a.w) iligeuka nyoka.

Aidha, wakati baadhi ya mitume walikuja na wakauliwa na kaumu walizotumwa kwao, Allah aliwahifadhi baadhi ya mitume Wake kama vile Musa, Ibrahim na Muhammad (s.a.w).

Hali sawa na hiyo inaweza kuwa ilijitokeza kuhusu vitabu. Allah, ambaye aliachilia vitabu vingine vibadilishwe, alizuia Qur’an Tukufu kutobadilishwa kwa ukarimu Wake mahususi. Kwa sababu hiyo, Ameashiria kuwa Qur’an iko chini ya Hifadhi Yake binafsi. Allah, aliyemhifadhi Ibrahim (s.a.w) asiungue katika moto, pia ameihifadhi Qur’an kubadilishwa.

Roho zetu na mashetani haziwezi kuuliza kwa nini Hakuzuia mitume Wake wengine wasiuliwe lakini akamhifadhi Ibrahim; haziwezi kutoa rai zao juu ya jambo hilo, pia.

3. Kama Adam asingetolewa Peponi, watu wengi wasingeongezeka. Mbegu hutoka ghalani na kufika mashambani ili zigeuke kuwa miti; halikadhalika, watu wameshuka katika shamba laDunia kutoka ghala la Pepo ili waweze kuongezeka kama miti.

Halikadhalika, kama vitabu vingine visingebadilishwa, basi, ufunuo wa Qur’an usingekuwepo. Vilipaswa kubadilishwa ili ije fursa ya kuja ufunuo Qur’an. Hata hivyo, wale tu waliovibadilisha ndio wanaowajibika na ubadilishwaji huo.

4. Hadhi ya Mtume (s.a.w) miongoni mwa mitume wengine iko dhahiri. Alitumwa ili iwe rehema kwa ulimwengu wote na utume wake haufungamani na wakati au kipindi fulani isipokuwa ni wa nyakati zote na vipindi vyote. Na ametumwa kwa watu na majini. Mitume wengine hawana sifa hizo.

Kwa hivyo, Kitabu cha mtume (s.a.w) ni cha nyakati zote na sehemu zote. Kama kitabu hicho kisingekuwa na muhuri kuwa hakibadilishiki, watu wangekibadilisha. Muhuri huo umekihifadhi.

5. Hakuna anayweza kufanya chochote tofauti na anavyotaka. Hayo, Ameyaonesha kwa kuiifadhi Qur’an.

11 Je, Uislamu ni rai au mtindo wa kimaisha?

Uislamu ni dini pekee aliyoshusha Allah kwa mwanadamu tangu mwanzo wa uumbaji. Nuh, Ibrahim, Musa na Isa wote walifanya kazi ya kueneza dini hiyo hiyo moja. Mtume wetu, Muhammad (s.a.w), alifikisha ujumbe wa mwisho wa Allah kwa kuwa alikuwa ni mtume wa mwisho.

Uislamu ni dini yenye kutambulika kikamilifu.  Uislamu unawakilisha mfumo wa kimaadili unaomwongoza mtu katika kila hatua yake.

Dini ambayo Allah aliwachagulia wanadamu kuwa inawafaa katika maisha yao ni dini ya Uislamu. Allah aliirahisisha sana dini Yake ili watu waitekeleze kwa vitendo.

Kumtumaini na kumtegemea Allah, ambaye ni mmiliki wa viumbe wote na matukio yote yanayofanyika ulimwenguni, na kumfanya Yeye rafiki, inamaanisha mwisho wa hofu zote za mtu, wasiwasi, matatizo na taabu.  Huu ni urahisi mmojawapo muhimu na katika mazuri yaliyoletwa na dini ya Uislamu kwa anayetekeleza maadili ya Quran kwa vitendo. Kwa kuongezea, Allah aliwajulisha watu kuhusu amri Zake na hukumu Zake zote, zinazowafaa kwa umbile lao na ambazo si ngumu.

Allah anaeleza katika Quran kuwa maadili ya dini ni rahisi na kuwa mambo yatakuwa mepesi kwa wafuasi wa dini ya Allah kama ifuatavyo:

"Na tutakusahilishia yawe mepesi.." (al-A'la, 87/8)

"…Yeye amekuteueni. Wala hakuweka juu yenu mambo mazito katika Dini. Nayo ni mila ya baba yenu Ibrahim..." (al-Hajj 22/78)

Sambamba na aya za hapo juu, Mtume (s.a.w) amesema,  

"Dini ni wepesi." (Bukhari, Iman: 29; Nasai, Iman: 28; Musnad, 5:69)

Hivyo, aliwaita watu kwenye kuitekeleza dini.

Ni kweli kuwa dini ya Uislamu ni namna bora ya maisha kwa ajili ya asili, amani na furaha ya mwanadamu na kuwa maisha yaliyoongozwa na maadili ya Quran ni maisha bora zaidi kwa mwanadamu.

12 Je Uislamu, uliokuja miaka 1400 iliyopita, unajibu maswali ya zama zetu na kutosheleza haja zake?

Lengo la Qur’an katika Mkusanyiko wa Risale-i Nur limejadiliwa katika nyanja mbili:

Kufundisha ukweli wa Uwanja wa Kimamlaka na maadili ya Uwanja wa utumishi (ibada). Tunaposema Uwanja wa Kimamlaka, tunamaanisha mtu, sifa, vitendo, na majina ya Allah (SWT). Qur’an imemtambulisha Allah (SWT) kwa wanadamu katika njia hii na ikawalinda dhidi ya kila namna ya ushirikina (imani potovu). Inapokuja kwenye uwanja wa utumishi, inamaanisha majukumu ya wanadamu kwa Allah (SWT). Alichoamrisha Allah (SWT) na kukataza ni nini? Vitendo gani na amali gani zinazomvutia radhi Zake na kinachosababisha ghadhabu Zake? Majibu ya maswali haya yamejibiwa vizuri sana katika Qur’an.

Katika nyanja zote mbili, akili ya binadamu haina hata neno moja la kusema. Katika nyanja zote mbili hakutakuwa na athari ya muda. Allah (SWT) bado ana nafsi Yake na sifa kama zilivyokuwa hapo tangu. Mkondo wa kibinadamu aliouweka Allah (SWT) unathibitisha yaleyale kama ilivyokuwa hapo tangu na tangu.

Hapa ni kweli kuwa katika zama za mitume waliotangulia, katika karne mbalimbali, kulifanyika njia tofauti kwenye mitazamo. Na mabadliko haya yamefikia kikomo pale mwanadamu anapokuwa amefikia mahali ambapo kila mmoja anaweza kujifunza kutoka kwa mtume mmoja na akapata nidhamu kutokana na Kitabu kimoja.

Mijadala au upingaji wa namna hii hufanyika zaidi kwenye njia zinazohusu mitazamo na maadili, bado kinyume cha njia hizo hakiwezi kupatikana. Pingamizi huletwa na watu waliozoea uharibifu; na kuona kuwa njia za Qur’an hazitafaa katika jamii yenye ufisadi wa namna hii, wanajaribu kuleta madai ya aina hii.

Ukweli haubadiliki kwa kufuata idadi ya watu. Ukweli uko pale pale. Umma unapaswa uutafute na kuufuata, sio kuuweka ukweli uwategemee wao.

Hebu tutoe mifano miwili. Qur’an imekataza pombe na riba. Si mwingine bali wenye waraibu ndio wanaoweza kudai kuwa mambo hayo ni mazuri na yana manufaa. Katika nchi au katika karne, kama watu wengi wanakunywa pombe au wanajihusisha na riba, hii isingemaanisha kuwa Qur’an haikusudii kuiambia nchi hiyo au karne hiyo. Badala yake, hiyo itamaanisha kuwa wao wako nje ya wanaoambiwa na Qur’an, kwamba wako nyuma sana na kwamba wamepotoka.

Njia nyingine ziko kama hivyo.

13 Je, Uislamu ni dini ya kimantiki?

Hukumu na kanuni za dini ya Uislamu zinafaa kwa umbo la mwanadamu na mantiki yake. Tathmini hii ni sahihi. Isipokuwa kwa sehemu ndogo ya kanuni ambazo ni “ta'abbudi” (zinahitaji utii bila ya kuhitaji kujua mantiki yake), kanuni zote katika Uislamu ni "ma'qul al-mana" (zinafahamika kiakili na kimantiki).

Ukweli kuwa amri na makatazo ya Uislamu yanawafaa watu waliobaleghe na wenye akili timamu na hawawajibishwi watu wasio na akili timamu unaonesha kuwa Uislamu huipa umuhimu akili na kuiambia akili na pia inaonesha kuwa Uislamu ni “dini ya mantiki”. 

Kwa mfano, desturi ya zaka katika Uislamu ni mpango uliowekwa kwa matajiri kuwasaidia masikini na kuweka usawa wa kijamii, kuzuia migogoro baina ya masikini na matajiri na kuigeuza migogoro hiyo kuwa suluhu, mapenzi-heshima na huondoa dhuluma inayochochea chuki baina ya matabaka katika jamii. Kazi hii ya zaka inaweza kufahamika kirahisi na pia ni ya kiakili sana.

Kwa kuongezea, sharti la kwanza katika kusilimu ni kumwamini Allah na kuamini mitume Wake. Imani iko moyoni. Moyo una nafasi ya kutosha ya kuwa na hisia, msukumo, hadithi na akili kuhusu Allah. Ni ishara dhahiri ya ukweli huu kuwa mtu asiye na akili timamu hawajibiki kuwa na imani.

Mtindo wa Qur’an umejaa shuhuda za kimantiki zinazotakiwa kwa ajili ya kuthibitishwa na akili ya mtu. Humo kila mara   kuna shuhuda na mifano ya kimantiki inapoeleza kuwepo kwa Allah, kwamba Nabii Muhammad (s.a.w) ni mtume wa kweli, kwamba Qur’an ni neno la Allah, na kuhusu kuwepo kwa ufufuo baada ya kufa.

Kwa kweli, kama amri au adhabu yoyote ya Allah haitoshelezi mantiki ya mwanadamu, basi haitaweza kusemwa kuwa hapa lipo jaribio lisilo na upendeleo. Kama mtu anamwajibisha mwanafunzi wa shule ya awali kwa maswali ya sayansi yanayofaa kwa ajili ya shahada za chuo kikuu au za udaktari wa falsafa, basi mtu huyo atakuwa ameonewa. Ndio sababu, mara zote akili na fikra za kibinadamu zinatiliwa mkazo katika Qur’an na kuna maneno kama ifuatavyo: “Je hamfahamu? Je hamfikiri?”  

Pili, maneno “Uislamu ni dini ya mantiki” hutilia mkazo falsafa ya mtu anayeziegemeza fikra zake kwenye sababu na mantiki yake yeye mwenyewe. Hayo si sahihi. Kwa mujibu wa mtu huyo, “Fikra za akili zilizo bora hufanana”, kwa hivyo mambo asiyoweza kuyafahamu hayako sahihi. Kwa hiyo, kile ambacho Uislamu unacho na kile unachokipinga katika mtazamo wake kinakuwa si sahihi.

Ni kwasababu Uislamu ni dini ya mantiki. Kisichokuwa na mantiki hakina nafasi katika dini.

Watu wa namna hii wenye falsafa kama hii hawawezi kufahamu dhana ya “mantiki” kwa sababu mantiki yenyewe peke yake haiwezi kushika kila kitu bila ya hali za nje; kinyume chake, inajaribu kwenda katika mwelekeo wa elimu na fikra alizopewa hapo kabla. Ni uthibitisho bora kabisa wa ukweli huu kuwa mtu mwenye akili ya juu sana lakini ambaye si lazima awe msomi hawezi kufahamu na kufanya mambo anayoyafanya mhandisi, daktari au mufti ambaye si hodari.

Nukta muhimu zaidi ya kuitaja hapa ni hii: Haifai kwa baadhi ya watu wasiofahamu jambo fulani kusema jambo hilo “halina mantiki.” Wengi wetu hatujui kuhusu fizikia, kemia, unajimu, hisabati, n.k. na hatuyafahamu hayo lakini hakuna anayesema kuwa hayo hayana mantiki kwasababu watu wengine hawayafahamu. Akili peke yake haiwezi kugundua kila kitu. Kama ingewezekana, kusingekuwa na haja ya mitume. Kila jambo lina uwanja wa kitaaluma unaoweza kufahamika kwa wataalamu peke yao. Wataalamu hao wanaweza kufahamu kwa urahisi  masuala ambayo watu wengine hawawezi kuyafahamu. Halikadhalika, ukweli kuwa baadhi ya watu hawawezi kufahamu ukweli wa Quran haimaanishi kuwa ukweli huo si wa kiakili na usio na mantiki. 

Nukta nyingine muhimu ni hii: Kuwepo kwa baadhi ya mambo yanayoitwa ta’abbudi na kwamba hayawezi kufahamika kwa akili kunahusu kujaribiwa mwanadamu. Kanuni za imani ni za kisayansi na zimeegemea mantiki. Kanuni chache za Uislamu zipo ili kuijaribu imani na kujisalimisha sio kuiridhisha akili. Kuna haja ya kuwepo baadhi ya mambo ambayo akili haiwezi kuyafahamu kwa urahisi ili idhihirike kama mtu anaamini akilini mwake tu au anaamini na anajisalimisha kwenye Uislamu.

Kwa kuhitimisha, mtu anayesema, “Kwa kuwa Quran ni neno la Allah, kila kilichomo ndani mwake ni sahihi – hata kama akili yangu haiwezi kufahamu “anafaulu jaribio. Anayesitasita na huku akisema, “Jambo kadha katika Quran halina mantiki; akili yangu haiwezi kulifahamu” anafeli jaribio kwa sababu ama si mnyoofu au ni mjinga sana.

Mathalani, ukweli kuwa swala ya subuhi ina rak'ah mbili lakini swala ya adhuhuri ina rak'ah nne haihusiani na akili. Hata hivyo, masuala kama vile kuharamishwa kwa nyama ya nguruwe na ulevi kunaweza kuelezwa na sayansi na mantiki. Mambo ya kimantiki ni zaidi kuliko mambo ya ta’abbudi.

14 Kama Uislamu ni dini ya kweli, kwa nini ni kuna watu wengi wanaoukataa na ambao ni watu wa dini zingine duniani? Nani anayewazuia watu kuwa Waislamu?

Awali ya yote, tusisahau kuwa huenda idadi ya Waislamu ni ya kwanza kwa wingi au angalau ya pili. Kama ingekuwa dini ya kweli inategemea idadi ya wafuasi wake, dini za Ukristo na Uislamu ni za kweli. Mmoja kati ya watu watatu duniani ni Muislamu kwa sasa. Wingi huu wa idadi ni dalili ya ukweli muhimu.

Katika historia nzima, hakuna dini iliyoweza kuwafanya watu wote duniani waifuate. Kama nukta hii itapozingatiwa, italazimu kuamini kuwa hakuna dini ya kweli. Fikra hii si sahihi hata kidogo.

Wale wasiokubali dini ya Uislamu wamegawanyika katika makundi matatu:

Kundi la kwanza: Hawaukubali Uislamu bila ya ushahidi wowote wenye kuupinga. Huko kunaitwa kukataa bila ya kukubali. Yaani, hao ni watu wasiojihangaisha kutaka kujua kama Uislamu ni sahihi au laa, wanaopendelea starehe zao tu, wasiotaka kuukataa Uislamu kwa kuegemea ushahidi wowote au wasiofikiria kutumia juhudi zozote za kukubali Uislamu kwa ushahidi wowote.  Watu wengi wasioukubali Uislamu ni kama hao. Hawataki kuacha starehe zao kwa kuukubali Uislamu, unaolenga kuadabisha maisha ya watu kwa kuwabebesha mizigo na majukumu. Kundi hili, lililotofautiana na Uislamu, likokatika ujinga kabisa.

Kundi la pili: Ni watu wenye mzio wa kuuchukia Uislamu bila ya sababu, wasiosikia ushahidi wowote unaoupendelea Uislamu na wanaozingatia kila dalili dhaifu kuwa ni ushahidi ulio kinyume na Uislamu. Hao ni wachache na hawakumudu na kamwe hawataweza kuukataa ukweli wa Uislamu kupitia ushahidi wa kisayansi au wa kimantiki bila ya chuki. Kinyume chake, wengi wasio Waislamu wameukubali Uislamu kupitia sayansi na mantiki katika historia yote. Hata leo, maelfu ya watu, miongoni mwa ambao kuna mamia ya wanasayansi na wahudumu a kanisa, ambao waliuwa Wakristo, ambayo ni dini inayodai kuwa ya wote, wamesilimu na kuendelea kusilimu.

Kwa mujibu wa Nursi, kuna vizuizi vinavyozuia Uislamu, ambayo dini ya wote na inayofanya masuala yake yote yakubaliwe na Akili, dhidi ya kuenea duniani kote. Orodha yake ni kama ifuatavyo:

1. Ujinga wa wageni/wasio-Waislamu. Hata watu wa Kitabu hawakuweza kutofautisha kati ya rangi nyeupe na nyeusi kwa sababu walikuwa wajinga sana.

2. Wanaishi maisha yasiyo ya ustaarabu. Kwa hivyo, walishindwa kabisa kufahamu uzuri wa ustaarabu wa Kiislamu.

3. Hususani watu wa Kitabu, walionekana kung’ang’ania sana dini yao. Ung’ang’anizi huo kiliwazuia kuuona ukweli wa Uislamu.    

4. Utawala na udikteta wa wahudumu wa kanisa na viongozi wa kidini. Udikteta huu haukuwaruhusu watu kuwa na uhuru wa kuhoji na kufanya uamuzi.

5. Watu waliwatii na kuwafuata wahudumu wa kanisa na viongozi wa kidini bila ufahamu. Ukweli kuwa Akili za watu zilinyakuliwa na hazikuwaruhusu watu kufikri uwezekano kuwa ukweli ungeweza kuwa mwingine.

6. Mtu mmoja mmoja na utawala wa kijamii na mamlaka waliyo nayo Waislamu. Udikteta huu umeharibu mazuri ya Uislamu na ustaarabu wa Quran kimamlaka na kusababisha mandhari yaliyoonekana kutowafurahisha wageni.

7. Maovu mengi miongoni mwa Waislamu yaliyoanzia kwenye vitendo vilivyokuwa kinyume na Uislamu. Maovu haya yasiyo ya Uislamu yaliharibu mvuto wa jua la Uislamu na kuzuia jua hilo angavu kama mawingu mazito lisizifikie Akili. Vizuizi hivyo viwili vilianza kupotea kwa kuibuka fikra ya uhuru miongoni mwa wanadamu, na Matakwa ya kutafuta ukweli.

8. Kizuizi cha nane kilikuwa kuwepo kwa hadaa kuwa kulikuwa na mabishano katika baadhi ya masuala katika Quran na yaliyothibitishwa na sayansi. Kutokana na hadaa hii, wanasayansi wengi walijitenga na Uislamu, wakifanya kosa kubwa sana.

Kwa mujibu wa Nursi, kikwazo cha kwanza, cha pili na cha tatu vimevunjwa kwa neema ya elimu na ustaarabu, na vimeanza kupotea.

Kikwazo cha nne na cha tano vimeanza kutoweka kwa kuwa fikra ya uhuru na hali ya kutafiti na kutafuta ukweli imejitokeza miongoni mwa watu. 

Kikwazo cha sita na cha saba vitatoweka kama udikteta utaondoshwa na upande mbaya wa uovu utaonekana. Ukweli kuwa nguvu ya kimamlaka inayoshikiliwa na mtu mmoja mmoja imeanza kuporomoka inaashiria kuwa udikteta wa kutisha wa makundi makubwa katika jamii na wa kamati pia utaporomoka katika kipindi cha miaka thelathini au arobaini. Na ghadhabu kubwa katika bidii ya Kiislamu, pamoja ma ukweli wa matokeo mabaya ya uovu unadhihirika wazi kuwa vikwazo hivyo viwili vinakaribia kuporomoka; kwa kiasi, vimeanza kuwa hivyo. Inshaallah, vitatoweka kabisa hapo baadaye.

Kikwazo cha nane kinaelekea kwenye kutokomea kwani inadhihirika kuwa hakuna ubishani kati ya ukweli wa Quran uliofahamika kwa usahihi na uvumbuzi uliofahamika vyema wa kisayansi. Hapo nyuma, wanasayansi na wanafalsafa waliupinga Uislamu kwa sababu hawakujua vyema kuhusu uhakika wa Uislamu. Hali hiyo imebadilika kabisa kwa sasa.

“Katika Muhtasari wa Miujiza ya Quran, Risale-i Nur inaonesha nuru za hali ya kimiujiza ya miujiza iliyopo chini ya aya zote zinazoshambuliwa na sayansi, na inadhihirisha ukweli mtukufu, usioweza kufikiwa na sayansi, katika sentensi hizo na ibara za Quran tukufu kuwa lengo la wanasayansi wanalodhani kuwa linaonesha ukosoaji; inamlazimisha hata mwanafalsafa mbishi sana kujisalimisha. Ni ushahidi unaojidhihirisha wenyewe, yeyote anayetaka anaweza kuona.”

“Wakati ujao utakuwa mzuri kwa Uislamu peke yake. Na mtawalawake atakuwa mambo ya kweli ya Quran na imani… Sisi, Waislamu, ambao ni wanafunzi wa Quran, tunafuata ushahidi; tunaendea mambo ya ukweli wa imani kwa njia yay mantiki, ingawa, na nyoyoni mwetu. Hatuachi ushahidi unaopendelea utii usio na fikra na uigaji wa mhudumu wa kansa kama wanavyofanya baadhi ya wafuasi wa dini zingine. Kwa hivyo, siku za baadaye, pindi akili, sayansi na teknolojia itakapoenea, kwa hakika, huo utakuwa wakati Qur'an itakapopanda juu, inayoegemea shuhuda za kimantiki na kuiachia akili ithibitishe.” [Hutbe-i Şamiye (Hotuba ya Damaskas)]

15 Je, Uislamu ni dini ya hofu?

Kunaweza kuwepo baadhi ya dini potovu zinazoegemea hofu lakini si sahihi kusema kuwa msingi wa dini zote ni hofu. Hususani wanaoitizama dini ya Uislamu kuwa ni dini ya hofu, hawako sahihi. Quran inatoa habari njema na maonyo. Maonyo hayalengi katika kuwatisha watu; bali badala yake, yanalenga katika kuwalinda watu dhidi ya kufanya makosa. Kuwajulisha watu kuhusu hatari wanazoweza kuzikabili na yanalenga katika kuwaonya dhidi ya kuchukua hatua; hayalengi katika kuwatisha. 

Uislamu hautaji Jahannamu tu, bali pia Pepo. Kabla ya kuja Uislamu, watu walikuwa wakiishi bila ya kuamini imani ya ufufuo; walikuwa wakiamini kuwa wangepotea baada ya kufa. Uislamu uliondosha imani hii na ukawapa waumini habari njema kuwa watakwenda Peponi. Kwa hakika, hadithi ifuatayo ya Mtume (s.a.w) ni mfano mzuri wa hayo:

"Rahisisheni, msifanye ugumu; toeni habari njema, msiifanye ngeni." (Bukhari, 3/72.)

Dini ya Uislamu ni msaada wa Muumbaji kwa wanadamu na elimu ya kuujua ukweli unaolenga katika kuwafanya wawe na furaha duniani na kupata wokovu katika akhera. Tunamjua Muumbaji wetu na sisi wenyewe tunashukuru kwa Uislamu; pia tunafahamu lengo la msingi la kuwepo na kupata amani na utulivu katika dunia yetu ya ndani na ya nje tunashukuru kwa hilo. Mitume wote tokea Nabii Adam mpaka Nabii Nuh, tokea Nabii Ibrahim mpaka Nabii Musa, tangu Nabii Isa mpaka Nabii Muhammad (s.a.w) walikuwa wajumbe na viongozi wa wito huu wa amani, mapenzi na wokovu.

16 Je, njia fanisi zaidi ya kueneza Uislamu ni vita au tabligh (kulingania)?

Ni muhimu kujibu maswali "Mtume ni nani?", "Wajibu wake ni upi?" Ili kuweza kutathmini dhana ya jihad kwa usahihi. Huku akiwafanya watu wote waende katika ulimwengu wa ahera, Allah Mtukuka aliwatuma mitume ili wawaongoze watu katika safari yao ya kuwapeleka Peponi au Motoni. Wajibu mkuu wa wajumbe hao wa Allah ni kuwafanya watu wamjue Allah, kuwafundisha ibada, halali na haramu, na kuwafundisha namna ya kumshukuru Allah kwa neema Zake zisizo na ukomo. 

Mtume Muhammad (s.a.w), ambaye ni Mtume wa zama za mwisho, alitimiza wajibu huu kikamilifu; aliwajulisha watu kuhusu Allah huko Makkah, aliwafundisha amri Zake na makatazo na aliwaambia kuwa kuabudu masanamu ni kumshirikisha Allah. Alivumilia namna zote za mateso na ukatili wa watu waliopinga ujumbe wake kwa miaka kumi na mitatu na kisha alihamia Madinah kwa kufuata amri na idhini ya Allah; aliendelea na wajibu wake huko. Washirikina waliotaka kumzuia asitekeleze wajibu huu wa juu kabisa waliendelea kumsumbua huko Madinah pia lakini hawakuweza kuuzuia Uislamu kufuatwa na watu wa huko. 

Kitu muhimu sana cha Mtume (s.a.w) wa zama za mwisho kilichotajwa katika vitabu vyote vya mbinguni ni kwamba yeye ni “sahib-us sayf” (mmiliki wa upanga); yaani, pamoja na uongofu wa kiroho, anaruhisiwa kupigana (anapozuiwa kufikisha ujumbe wake). Baadhi ya mitume waliotangulia, kama vile Nabii Dawud na Nabii Suleiman, waliendesha jihad zao kwa mapanga pindi ilipolazimu.

Historia inapochunguzwa bila upendeleo, itaonekana kuwa jambo kubwa lililofanya Uislamu uvutie nyoyo na ari halikuwa vita bali kufikisha ujumbe, yaani, kuwaambia watu kuhusu uhalisia wa Uislamu na kuwaonesha mazuri ya Uislamu. Wanahistoria wanakubali kuwa makundi mawili ya watu yalikuwa na mchango mkubwa zaidi katika kuenea kwa Uislamu. La kwanza ni wanazuoni na walimu waliojitolea maisha yao kwa kufundisha Uislamu na wakahamia nchi za mbali sana ili kufanya hivyo. Kundi la pili ni wafanyabiashara waliokwenda katika baadhi ya nchi ili kufanya biashara na wakawaonesha watu wa huko mazuri ya Uislamu.

Aya zifuatazo zinaonesha waziwazi kuwa Uislamu umeenea kwa njia ya kufikisha ujumbe na wito wala si kwa njia ya upanga:

 “Hapana kulazimisha katika Dini. Kwani Uwongofu umekwisha pambanuka na upotofu.” (surat al-Baqara, 256)

“Basi kumbusha! Hakika wewe ni Mkumbushaji. Wewe si mwenye kuwatawalia.” (al-Ghashiya, 21-22)

Kuna shuhuda nyingi zinazoonesha kuwa Uislamu umeenea kwa njia ya kufikisha ujumbe wake. Tutataja baadhi yake: Mtume (s.a.w) alipoanza kufikisha ujumbe wa Uislamu katika mji wa Makkah, hakuwa na mali au nguvu. Ingawa washirikina wote wa hapo walimfanyia uadui, alizishinda nyoyo za watu kwa kufikisha ujumbe na ushawishi. Watu wengi, kuanzia Abubakr mpaka Umar, walisilimu kama hivyo na wakamtamkia kila mmoja kuwa Uislamu ulikuwa ni nguvu isiyoshindika. Kama Maswahaba wangetaka, wangewaua washirikina wote wa Quraysh, wa kwanza Abu Jahl, kwa ghafla moja. Hata hivyo, hawakufanya hayo. Waliendelea kufikisha ujumbe wa Uislamu kwa kustahamili mateso na taabu za aina zote; hawakutumia kitisho na vurugu.

Waislamu waliohamia Madinah kabla ya Mtume waliwaingiza watu wengi katika Uislamu huko kwa kufikisha ujumbe wa Uislamu na kuwalingania Uislamu. Hivyo, misingi ya Uislamu iliwekwa kwa njia ya kufikisha ujumbe kote Makkah na Madinah.

Katika miaka iliyofuata, Uislamu uliimarika Madinah. Washirikina wa Makka waliwakubali Waisilamu kuwa wana nguvu na wakasaini nao mkataba huko Hudaybiya. Kipindi cha mkataba kilikuwa ni miaka kumi lakini kilidumu kwa miaka miwili na kikavunjwa na washirikina wa Makka. Hata hivyo, idadi ya watu waliosilimu katika kipindi cha miaka hiyo miwili ilikuwa ni zaidi ya idadi ya watu walioufuata Uislamu katika kipindi cha miaka ishirini tangu Uislamu ulipoibuka.

Katika karne zilizofuatia, Wa-Mogul waliumaliza ukhalifa wa ukoo wa Abbas; wakachoma na kuharibu rasilimali za Kiislamu. Hata hivyo, baada ya muda, walianza kusilimu kwa hiari yao wenyewe. Ni ukweli wa kihistoria kuwa panga halikuwa na lolote katika kusilimu kwa Wa-Mogul. 

Kuenea kwa Uislamu katika maeneo ya Indonesia, Malaysia na Africa kulifanyika kwa njia ya ufikishaji ujumbe na si kwa njia ya upanga. 

Baada ya kuiangalia historia hiyo kwa kifupi, hebu tuangalie hali ya leo: Waislamu wamepoteza uwezo wao wa kimali katika karne iliyopita lakini Uislamu umeendelea kuenea na kuendelea kiroho. Watu wengi waliosilimu katika nchi za Ulaya kwa kuanzia na Ujerumani na Uingereza, na katika Amerika ni wanasayansi; wengi wao wamesilimu baada ya kuuchunguza tu, bila ya hata kufikishiwa ujumbe wa Uislamu. 

17 Je inaweza kuthibitishwa kupitia ushahidi wa Quran kuwa Uisilamu sio dini ya ugaidi bali ni kinyume chake inakataza gaidi, vurugu na fitina?

Quran imekemea vikali ugaidi na kuzielezea vurugu na fitina kuwa ni mambo maovu mno.

Uisilamu umekataza aina zote za ugaidi, dhuluma, na usaliti na kupinga aina zote za vurugu na tabia mbaya. Uisilamu haujibu uovu kwa uovu. Dini ya Uisilamu imeletwa na Allah Mtukufu ili kusimamisha haki, kuvunja udikteta na dhuluma za kiholela za uovu wa kikatili na kuifanya dhamiri ya mtu kuchemka. Hivyo, Uisilamu uko makini mno kuhusu hilo. Quran unayazingatia mauaji ya mtu asiye na hatia kuwa ni mauaji mabaya kabisa yaliyofanywa dhidi ya watu wote.

Allah Mtukufu anatangaza “… aliye muuwa mtu bila ya yeye kuuwa, au kufanya uchafuzi katika nchi, basi ni kama amewauwa watu wote. Na mwenye kumuokoa mtu na mauti ni kama amewaokoa watu wote… (al-Maidah, 32) Quran pia inalaani aina zote za fitina. Quran inatutanabahisha juu ya vichochezi na kueneza fitina ya wale wanaoanzisha mfarakano, wanaosababisha uhasama katika maisha ya jamii, na kueneza uhasama akiwa katika madaraka, na pia inaonesha bayana kitisho cha kueneza ufisadi, na uzito wa uhasama: “Na anapo tawala hufanya juhudi katika nchi kwa kufisidi humo na kuteketeza mimea na viumbe. Na Mwenyezi Mungu hapendi ufisadi.” (al-Baqarah, 205)

Quran imekataza fitina, katika sura al-Baqarah, 217, Allah Mtukufu anatangaza: “Na fitina ni mbaya zaidi kuliko kuuwa.” (Al-Baqarah, 217)

Ndani ya nafsi ya Mwisilamu, anayezitumia aya hizi za Quran kwa kiwango kikubwa, mnakuwa hamna uadui, chuki na ukatili. Umo undugu fulani hata kati ya adui yake mkubwa. Mwisilamu anaukubali ukweli, ambao, “tunamvumilia kiumbe kwa sababu tu ya Muumbaji.” Mwisilamu ni mtetezi wa upendo. Hana muda wa uhasama. Katika Quran Tukufu, Allah Mtukufu amewazindua waumini wajiepushe na madhara ya sehemu za ibada, kwa kuashiria kuwa sehemu za ibada zimehifadhiwa dhidi ya watu fulani kutokana na uingiliaji kati wa watu wengine: “… Na lau kuwa Mwenyezi Mungu hawakingi watu kwa watu, basi hapana shaka zingeli vunjwa nyumba za wat’awa, na makanisa, na masinagogi, na misikiti, ambamo ndani yake jina la Mwenyezi Mungu linatajwa kwa wingi.” (al-Hajj, 40) 

Mtume Muhammad ni mtume wa huruma na upendo. Katika Quran Tukufu, Allah Mtukufu anaeleza: “Nasi hatukukutuma ila uwe ni Rehema kwa walimwengu wote.” (al-Anbiya, 107) Mtume (S.A.W.) ameonesha maadili yote mema kwa namna bora zaidi katika maisha yake na kuinasihi jumuia yake kujiepusha na fitina. Aliwaamuru kujiweka mbali na fitina kwa uzito usio na kifani na kwa umakini:

Jihadharini na fitina! Kwa kuwa, wakati ule ule, ulimi ni kama pigo la upanga. (Ibn Majah, Fitan, 24)

 “Hapa pana uhakika kuwa kutatokea fitina, mfarakano na mgogoro. Itakapotokea hali hii, nenda Uhud na upanga wako. Upige jiwe kubwa mpaka livunjike vipande vipande. Kisha bakia nyumbani kwako. (Usitoke nje) hadi utakapokufikia mkono wa dhambi au kifo kikufikie nyumbani kwako.” (Ibn Majah, Fitan, 24) Ni kabla ya Siku ya Kiama, kutakuwa na fitina kama vipande vya usiku wa giza. Wakati wa fitina hiyo, mtu ataamka asubuhi hali ya kuwa ni muumini, lakini ataishia kuwa kafiri ifikapo usiku; ikifika usiku atakuwa muumini lakini ikifika asubuhi atakuwa kafiri. Wakati wa fitina hiyo, mwenye kukaa atakuwa bora zaidi ya mwenye kusimama wima. Hivyo vunjeni pinde zenu, vurugeni mishale yenu na mapanga yenu yapigeni kwenye mawe. Kama itaingia ndani ya nyumba ya mmoja wenu, uwe yule mbora zaidi kati ya wana wawili wa Adam (kuwa utakayeuliwa sio muuaji). (Abu Dawud, Fitan 2, Tirmidhi, Fitan 33)