FAQ katika kifungu cha Vitabu Vitakatifu

1 Kwa kuwa vitabu vya kiungu visivyokuwa Qur’an viligeuzwageuzwa, kwa nini dini ya Kiislamu inatuamuru tuviamini?

Sisi Waislamu, tunawaamini Hadhrat Musa, Hadhrat Dawud na Hadhrat Isa (Yesu) na vitabu vya kiungu walivyoteremshiwa; Taurati, Zaburi na Biblia na hatuna shaka kuwa havitoi kanuni iliyo kinyume na dini ya kweli ya upwekeshaji. Hata hivyo, vitabu hivyo havikuhifadhiwa na kwa hivyo viligeuzwageuzwa.

Kwa sasa, hatuwezi kusema kuwa vitabu vitukufu walivyo navyo Wayahudi na Wakristo havina sehemu zinazohusiana na ufunuo walioteremshiwa Mitume hao. Hata hivyo, pia hakuna shaka kuwa vitabu hivyo vina ushirikina na imani potofu ndani mwake. Hivyo, daima tunashughulika na vitabu hivyo kwa uangalifu. Tunakubali hukumu za vitabu hivyo zinazoafikiana na Qur’an kuwa ni zinatokana na ufunuo. Tunazingatia kuwa hukumu zilizo kinyume na Qur’an kuwa ni nyongeza zilizoingizwa baadaye. Tunanyamaza kimya pindi iliyomo katika vitabu hivyo haiafikiani wala haipingani na Qur’an. Katika hali hiyo, hatutaipokea wala kuikataa. Kwa kuwa, inawezekana habari iliyomo katika vitabu hivyo ikawa ni ufunuo au laa.   

Abu Hurayrah (RA) alisema yafuatayo juu ya jambo hili: «Watu wa kitabu kitukufu walikuwa wakisoma Taurati kwa lugha ya Kihebrania. Na wakawa wanawatafsiria Waislamu kwa Kiarabu. Kutokana na hilo, Mtume Muhammad (S.A.W) aliwaambia maswahaba zake yafuatayo: Msikubali au kukataa maneno ya watu wa kitabu kitukufu.

“Semeni nyinyi: “Tumemuamini Mwenyezi Mungu na yale tuliyo teremshiwa sisi, na yaliyo teremshwa kwa Ibrahim na Ismail na Is-hak na Yaakub na wajukuu zake, na waliyo pewa Musa na Isa, na pia waliyo pewa Manabii wengine kutoka kwa Mola wao Mlezi; hatutafautishi baina ya yeyote katika hao, na sisi tumesilimu kwake.” (al-Baqara, 2/136)