FAQ katika kifungu cha Elimu

1 Je unaweza kuelezea kuhusu umuhimu unaowekwa na Uislamu kwenye sayansi na teknolojia? Je, dini ya Uislamu ndio sababu ya ujinga na kutokuendelea kwa dunia ya Kiislamu hivi leo?

Chanzo cha maendeleo ni elimu na sayansi. Adui mkubwa zaidi wa watu ambaye lazima wamwepuke ni ujinga kwa sababu kikwazo cha maendeleo yote na mageuzi na chanzo cha mwinamo ni ujinga. Katika mamia ya aya, Quran tukufu inawahimiza wanadamu wajifunze sayansi zinazohusiana na dini na dunia. Tutazinukuu mbili kati ya hizo:

"Ati watakuwa sawa wale wanao jua na wale wasio jua?" (Az-Zumar, 9)

"Basi waulizeni wenye ukumbusho kama nyinyi hamjui." (An-Nahl, 43)

Mtume wetu Mohammad (S.A.W) ana Hadithi nyingi zenye kuwahimiza watu wajifundishe sayansi. Baadhi yake ni kama ifuatavyo:

"Tafuteni elimu tangu utotoni mpaka mfikwe na mauti.
Kila kitu kina njia. Njia ya kwenda Peponi ni elimu na sayansi.
Tafuteni elimu hata mpaka China."
(Bayhaqi, Shuabul-Eeman, Beirut, II. 254)

"Hekima ni mali iliyopotea ya muumini. Huichukua popote anapoikuta." (Tirmidhi, Ilm 19)

"Kutafuta elimu ni faradhi kwa kila Muislamu mwanamume na mwanamke." (Ibn Majah, Muqaddima, 17)

Kama inavyojulikana, Mtume wetu Mohammad (S.A.W) alipofika Madinah, kwanza alijenga madrasah pamoja na msikiti wake. Wanafunzi waliosoma katika madrasah hiyo kwa wakati huo waliitwa watu wa Sofa (Suffa). Watu hao wote walijitolea maisha yao katika elimu na ufahamu. Madrasah ya Sofa ndio msingi wa madrasah zote za Kiislamu na shule zilizofikia leo.

Kama dini ingekuwa ndio kikwazo cha maendeleo, je maendeleo katika enzi za upeo wa furaha, ukamilifu katika Andalusia iliyokuwa mkuu wa Ulaya, ustaarabu wa dola za Seljuk na Uthman zilizoitatanisha dunia ungekuwepo? Je, maelfu ya wanazuoni na wanafalsafa wa kidini kama vile Imamu Ghazali, Ibn-i Sina, Farabi, Imamu Rabbani, Mawlana Jalal-ud-Din Rumi wangeibuka katika dunia ya Uislamu! Badiuzzaman anaeleza kuwa Uislamu hauwezi kuchukulika kuwa unapinga sayansi kama ifuatavyo:

"Mtumwa, mtumishi, mtoto anawezaje kuwa adui na mpinzani wa mkuu wake, kiongozi na baba mtawalia? Kwa hakika, Uislamu ni mkuu na kiongozi wa sayansi na mkuu na baba wa elimu ya kweli." (Muhakemat,10)

Ni kweli kuwa Waislamu leo hawako katika kiwango kinachotakiwa katika nyanja za sayansi na teknolojia lakini si sahihi kudai kuwa Uislamu unahusika na kuwa nyuma huko kimaendeleo.

Baadhi ya duru zainadai kila uvumbuzi wa sayansi kuwa ni ushindi uliopatikana dhidi ya Uislamu. Inaweza kuwa ni kweli kwa dini batili zinazokana sayansi. Hata hivyo, Muislamu huchukulia maendeleo ya namna hiyo kuwa ni "uvumbuzi wa kimwujiza kutoka katika ulimwengu ambao ni kitabu cha uwezo wa Allah". Uvutiwaji na mastaajabu yake kwenye elimu na hekima ya Allah huzidi anaposikia kuhusu vumbuzi mpya.

Kipengele kimoja muhimu cha jambo hilo ni hiki: hakuna kanuni inayowazuia watu dhidi ya sayansis katika Quran, kitabu cha mwisho na kikamilifu miongoni mwa vitavu vya kweli. Hivyo, madai ya baadhi ya watu kuwa Uislamu ni dhidi ya sayansi na teknolojia hayana msingi kabisa na ya makusudi.

Kwa kuangalia karne iliyopita tu ambapo Waislamu waliacha misingi yao - kwa hakika, waliacha misingi yao katika namna iliyopangwa - kutoka katika ari ya Uislamu, na kupuuzia mafanikio na maendeleo yote ya karne kumi na nne si haki.