FAQ katika kifungu cha Haki za Watu Binafsi

1 Je, unaweza kutoa maelezo kuhusu Uislamu unavyothamini haki za mtu?

Katika dini ya Kiislamu, pamoja na maisha ya mtu, imani yake, kutokuwa na kosa, uhuru, bidhaa, mali, cheo na heshima vimehifadhiwa. Kwani, amani na furaha ya mwanadamu duniani na akhera inazingatia yaliyotajwa hapo juu.

Kukiuka haki za kiyakinifu na za kiroho za mtu ni kosa kubwa jichoni mwa Allah na hilo haliingii katika msamaha wa Allah. Maana yake, kama utakiuka haki za mtu, unaweza kusamehewa na mtu huyo huyo. Allah hasamehe kosa hilo isipokuwa mpaka mtu aliyedhulumiwa apate haki yake au asamehe haki hiyo. Kila mmoja anatakiwa aheshimu haki za wengine katika dini ya Kiislamu.

Mwanadamu ni kiumbe chenye kuishi kijamii. Kisha, kuna mahusiano mengi ya kijamii baina ya watu. Mahusiano yanahitajika kusimamishwa kwa ukweli na haki. Vinginevyo, ukiukwaji wa haki za watu na dhuluma itatokea.

Quran inahifadhi sana haki za kiroho za watu kiasi kwamba ikawakataza waumini kuwashuku vibaya watu wengine, kuwapeleleza wengine na kusengenya.

Enyi mlio amini! Jiepusheni na dhana nyingi, kwani baadhi ya dhana ni dhambi. Wala msipelelezane, wala msisengenyane nyinyi kwa nyinyi. Je! Yupo katika nyinyi anaye penda kuila nyama ya nduguye aliye kufa?(al-Hujurat, 12)

Sasa, hebu tufikirie kiuadilifu: Je, dini inayokataza kuwasengenya na kuwapeleleza wengine itaruhusu vurugu, vitisho na kuwaua wengine kwa dhuluma?