Ni vitu vyote ambavyo vimekatazwa na dini yetu kutendwa, kutumia, kula, au kunywa basi hivyo ni haramu; kwa mfano, kunywa vilevi, kamari, kufanya uzinzi, kuua mtu, kusengenya, kuzua… Ikiwa kitu au kitendo kimefanywa kuwa haramu kutokana na madhara, uovu na uchafu ambao unapatikana katika kitu au kitendo hicho, kinajulikana kama haramu kwa hali yake (haram liaynihi ) au kwa dhati yake (kilivyo) [haram lidhatihi]; kwa mfano, nyama ya nguruwe na pombe. Ikiwa kitu kitaitwa haramu si kwa sababu ya kilivyo au hali yake lakini ni kwasababu zilizo nje ya kitu au kitendo hicho kama vile njia ya kukipata, basi hujulikana kama haramu kwa kinyume chake (haram lighayrihi); kwa mfano, mkate ulioibwa, fedha iliyoporwa …
FAQ katika kifungu cha Halali - Haramu
Tunaweza kuwaambia ndugu zetu wanaouliza maswali haya kwetu lakini si wale wanaouliza maswali kwa kupinga yafuatayo: Amri alizozitoa Allah zinaakisi Elimu yake isiyo na ukomo wa maarifa na hekima. Kikanuni, kila amri ina thamani ndani yake. Hakuna amri ya Kiungu inayoweza kutolewa muhanga kwa nyengine isipokuwa pawepo na umuhimu huo.
Kwa mfano, uwepo wa vita hauifanyi pombe na nyama ya nguruwe kuwa halali. Mtu anaepinga hili anapaswa kujua kwamba anapokunywa pombe nyumbani, vita haitokwisha na wala Amani haitopatikana. Ikiwa anafikiri hivyo kwa sababu za kibinadamu, ni kinyume na ubinadamu na maadili kwa kunywa pombe mezani na kujifurahisha binafsi wakati watu wengi wanakufa vitani.
Ni sawa sawa, wakati watu wanapouliwa vitani, hivi kula nyama ya nguruwe kunapelekea kupatikana kwa Amani?
Mbali na hayo, Allah ameshughulikia na anashughulikia vita. Ndio, Allah anatuamrisha tusipigane na na badala yake anataka tulete Amani kupitia Kur’ani na mafundisho ya Mjumbe wake.
Hapa kuna baadhi ya aya hizo:
“Enyi mlio amini! Ingieni katika Uislamu kwa ukamilifu, wala msifuate nyayo za She'tani; hakika yeye kwenu ni adui aliye wazi.” (al-Baqara, 2/208)
“Isipokuwa wale walio fungamana na watu ambao mna ahadi baina yenu na wao, au wanakujieni na vifua vyao vina dhiki kupigana nanyi, au kupigana na watu wao. Na lau angelipenda Mwenyezi Mungu angeliwasaliti juu yenu wakapigana nanyi. Basi wakijitenga nanyi, wasipigane nanyi, na wakakuleteeni amani, basi Mwenyezi Mungu hakukupeni njia kupigana nao.” (an-Nisa, 4/90)
“Kwa sababu ya hayo tuliwaandikia Wana wa Israeli ya kwamba aliye muuwa mtu bila ya yeye kuuwa, au kufanya uchafuzi katika nchi, basi ni kama amewauwa watu wote. Na mwenye kumuokoa mtu na mauti ni kama amewaokoa watu wote. Na hakika waliwajia Mitume wetu na hoja zilizo wazi. Kisha wengi katika wao baada ya haya wakawa waharibifu katika nchi.” (al-Maida, 5/32)
Aya ambayo imewaruhusu Waislamu kwa mara ya kwanza kwa takriban miaka 15 baada ya ufunuo wa kwanza ni hii ifuatayo:
“Wameruhusiwa kupigana wale wanao pigwa vita kwa sababu wamedhulumiwa - na kwa yakini Mwenyezi Mungu ni Muweza wa kuwasaidia” (al-Hajj, 22/39)
Waumini walinyanyaswa na kuteswa sana na makafiri kwa miaka 15: miaka 13 wakiwa Makkah na miaka 2 wakiwa Madinah. Licha ya hayo, walikuwa hawaruhusiwi kupigana kwasababu Uislamu ni dini ya Amani. Neno Uislamu limetokana na neno silm, ambalo lina maana ya Amani. Hivyo basi, wakati Allah aliporuhusu Waislamu kupigana vita kwa mara ya kwanza, Alitumia maneno ya kati na kati na sio maneno makali. Kwa mfano:
a. Badala ya kutumia maneno makali kama vile “piganeni mara moja”, kauli inasema, “ruhusa ya kupigana imetolewa” na maneno haya yametumika mwanzoni mwa aya. Maelezo “ruhusa ya kupigana imetolewa” badala ya “mmeamrishwa kupigana” kwakweli ni maneno ya huruma na ya kati na kati.
b. Vile vile, ukweli kwamba maneno yalopunguzwa ukali kama “ruhusa ya kupigana imetolewa” yametumika badala ya kutumia maneno makali kama vile “nimewaruhusu kupigana”, inakusudia kuonesha kuwa vita ni jambo ambalo halipendelewi katika Uislamu isipokuwa tu pale patakapokuwa na umuhimu.
c. Waislamu hawakuruhusiwa wapigane walipohitaji kupigana lakini ruhusa ilitoka kwa sharti kwamba pale tu watakapotangaziwa vita, ambao ni ushahidi wa wazi kwamba vita si lengo halisi la Uislamu. Tamko “ruhusa ya kupigana imetolewa kwa vile wamewakosea” katika aya iliyotajwa ni ushahidi wa ukweli huu.
d. Zaidi, ukweli kwamba sababu ya kutolewa ruhusa ya kupigana inaelezwa kwamba “kwa vile wamewakosea” katika aya inaonesha kwamba Waislamu hawawezi kutangaza vita dhidi ya maadui bila ya sababu yoyote – kwa mawazo ya kibabe.
Vita ya kwanza baada ya ruhusa hii ilikuwa ni vita ya Badr. Makafiri walikuja Makkah kutoka Madina na wakafika sehemu iitwayo Badr karibu na Madinah; tamko “Allah ni mwenye nguvu kuwapa msaada”, ambalo linapatikana mwisho wa aya iliyotajwa juu na ambalo ni taa ya miujiza lanatoa taarifa kuhusu mambo yajayo inayoonesha wazi kwamba makafiri watashindwa na Waumini; na kweli walishindwa.
Basi ikiwa hivyo linamaanisha nini swali “Kwanini Allah hajihusishi na vita” ni “Kwanini basi Allah hasimamishi vita?’, jibu la swali hili ni jepesi sana:
Allah ameuumba ulimwengu huu kama sehemu ya mtihani na Anawajaribu watu sehemu hii. Amewapa watu uhuru kwamba wanaweza wakatumia wanavyopenda na nguvu ambayo wangalitumia kwa uhuru ili mtihani adilifu uchukue nafasi yake. Kila mtu anajaribiwa kwa usawa ili pawepo na washindi na walioshindwa kwenye mtihani huu.
Hivyo basi, Allah hawazuii ambao wanataka kufanya vitendo vyema na ambao wanataka kufanya vitendo vibaya. Vyenginevyo, Angaliwaadhibu wanywao pombe kwa kuondosha akili zao na akawashusha hadhi zao kufikia kiwango cha wanyama na angaliwabadili wanaokula nyama ya nguruwe akawafanya nguruwe. Angaliwafuta kabisa wanaofanya ukatili, wauawaji ambao wanampigana vita dhidi ya Allah na angalikata ndimi zao wale wanaotamka maneno maovu.
Hivyo, haingilii ukatili wa watu kwasababu ni muhimu pawepo na uadilifu kwenye mtihani.
Ndivyo ilivyo. Vyote, pepo na moto vipo kwa ajili ya watu.
Pepo si rahisi; Jehanam sio lazima..
Dhamira halisi ya ubinadamu inasema, “Pepo ya milele!” hasa kwa wanaodhulimiwa “Jehanamu ya milele” hasa kwa wanaodhulumu.
Ukweli kwamba kuna wanaodhulumu na wanaodhulumiwa katika uwanja wa mitihani wa ulimwengu huu, ambapo wanaodhulumu huishi na kufa wakiwa matajiri na wanaodhulumiwa huishi na kufa maskini inathibitisha uwepo wa mahkama kuu ya Allah siku ya hukumu ambayo itaonesha haki isiyo na mwisho.