FAQ katika kifungu cha Jihadi

1 Je Jihad ni suala la vita tu? Unaweza kutueleza kuhusu Jihad katika mwangaza wa aya za Quran na Hadith?

Baadhi ya waandishi wa Kimagharibi kwa makusudi wanaijadili dhana ya Jihad kuwa ni kama vile suala la vita, na kuzipuuza maana nyengine.  Wakati ambapo, jihad ina maana ya ufahamu zaidi, inakubali kila aina ya mapambano kwa ajili ya Allah. Ambapo, aya za Quran, Hadith, na matendo ya Mtume Muhammad katika maudhui hii yanapewa mazingatio, ni wazi kabisa kuwa Jihad haimaanishi vita tu.

Mifano kutoka katika Hadith:

Bibi Aisha aliuliza, Ewe Mjumbe wa Allah, tunaiona Jihad kuwa ni amali bora zaidi, je tusijiunge nayo? Akajibu, Lakini, Jihad bora zaidi ni hajj timilifu (kuhiji mjini Makkah). (Sahih Al-Bukhari Jihad, 2784)

Katika hadith nyengine, inaelezwa kuwa, Kweli, maneno ya kweli na haki ni Jihad kubwa kabisa hususani inaposemwa mbele ya mtawala dhalimu. (Tirmidhi's Kitabu'l-Fitan) Hadithi nyengine ya aina yake ilisimuliwa na Abdullah bin Amr, Mtu mmoja alikuja kwa Mtume kumuomba ruhusa aende Jihad. Mtume aliuliza, “Je wazazi wako wako hai?” Akajibu ndio kwa kutilia mkazo. Mtume akasema, “Pambana na nafs yako (uovu wako) ili uwatimizie haki zao” (Sahih Al-Bukhari Jihad, Juzuu ya 4, Kitabu 52, Nambari 248)

Inasimuliwa kwenye mamlaka ya Tariq b. Shihab: Alikuwa ni Marwan aliyeanzisha (tendo la) kutoa hotuba kabla ya sala ya sikukuu ya ‘Id. Mtu mmoja akasimama na kusema: Sala inapasa iitangulie hotuba. Marwan akasema, Hili (tendo) limeshatendeka. Huku haya yakitokea Abu Sa’id akasema: Mtu huyu ameshatimiza (wajibu wake) alionao. Nimemsikia Mjumbe wa Allah akisema: Yeyote atakayeona uovu basi anapaswa ausawazishe kwa mkono wake; na kama hawezi hivyo, basi anapaswa ausawazishe kwa ulimi wake, na kama hakuweza hivyo, basi (hata) kwa kuchukia kwa moyo wake, na hii ni imani finyu kabisa. Sahih Muslim Imani, Kitabu 001, Nambari 0079-80)

Hadithi hizi zinapotegemewa, itaonekanwa kwamba Jihad ina maana pana, inayojumuisha aina zote za bidii kwa ajili ya Allah.

Jihada maana yake ni kujibiidisha au kupambana kwa Kiarabu, linatokana na mzizi Jahd.

Jihad, kwa maana pana zaidi, ni kujibidiisha kupitia njia ya Allah, kutimiza wajibu wa uja kwa Allah, kupambana na vyote viwili uovu wa nafsi na Shetani, kuishi na kuakisi roho ya mfumo wa maisha ya Kiisilamu kwa kufuata kigezo cha Mtume Muhammad, kuwalingania watu kuja katika Dini, kuutangaza Ujumbe wa Kiungu kwa watu, kuulinda Uisilamu na Waisilamu dhidi ya uadui wowote unaoweza kutokea na kupigana kwa ajili ya hayo ikilazimika. Katika muktadha huu, Jihad ina sura mbili: Kiroho na Kiyakinifu.

Namna ya Kiroho inahitaji imani kamili na kujisalimisha, unyoofu na usafi, kujitolea nafsi na juhudi kubwa katika dini. (Al-Baqarah Surah, 2:285, 286) Kwa namna hii, inawaandaaa waumini kuwa na imani thabiti na elimu ya kisayansi, ili kuwa makini na wenye kuona mbali, na kuidumisha dini kwa unyoofu wa hali ya juu kuwa ndio kigezo. (Az-Zumar Surah, 2-3) Namna ya Uyakinifu kwa upande mwengine, inachambua umuhimu wa kujiendeleza kiuchumi, kiteknolojia, kitamaduni dhidi ya uchochezi wa maadui unaoweza kutokea.

Dhana ya Jihad katika Uisilamu inarejea katika kipengele kikubwa cha wajibu na majukumu, ambayo yamebainishwa na aya za Quran na Hadithi.

1- Kujaribu kuidumisha Dini kwa ajili ya Allah kwa unyoofu

2- Kusambaza ukweli juu ya kila kitu.

3- Kujitahidi kuwalingania wengine kuja katika Uisilamu, kuwafundisha wasiouju.

4- Kuamrisha mema na kukataza maovu.

5- Kujitahidi kuvumilia matatizo yanayohusu kuwalingania watu kuja kwa Allah na matusi ya watu.

6- Kutangaza elimu ya Ujumbe wa Kiungu wa kuamrisha mema na kukataza mabaya kirafiki zaidi.

7- Kujibidiisha vilivyo ili kuwa juu katika sayansi na teknolojia.

8- Kujiendeleza kiyakinifu ili kushinda katika vita vya kiuchumi na utamaduni.

9- Kuongoza dola kwa busara ya kutoruhusu walanguzi

10- Kujitahidi dhidi ya maadui kwa kutokuwa adui yao kisiasa, kiuchumi, na kijeshi.

11- Kuchukua hatua za tahadhari dhidi ya uhaini wowote unaoweza kujitokeza na mavamizi ya maadui.

12- Pindi vita vikiwa haviepukiki, haifai kuwakimbia maadui, bali kupigana nao, na kumwamini Allah.

Uongo na tathmini za haraka-haraka juu ya Jihad kama vile ni suala la vita tu ni ukosefu, upungufu na sio sahihi kwa mujibu wa mafundisho ya Quran na Sunnah.

2 Jihad inamaanisha nini? Ni zipi Aina za Jihad?

Jihad ni jina linaloitiwa kila shughuli na harakati katika njia ya Allah (SWT). Linamaanisha kutoa bidii ili kuinyanyua haki na kuifanya itawale. Kwa maneno mengine, jihad ni kufanya kwa vitendo katika Uisilamu; ni nguvu ya Uisilamu ili kutenda.

Neno jihad mara nyingi linafasiriwa kuwa ni “vita vitakatifu” kwa lugha za Magharibi. (1) Ufasiri huo unatokana na juhudi ili kuonesha kuwa Uisilamu ni dini inayoenea kwa mabavu ya silaha.

Hata hivyo, maana ya neno “jihad” sio “vita.” Kupigana kwa ajili ya Allah (SWT) pia ni namna ya jihad lakini, kwa maana jumla, neno hili linahusisha mchakato wowote na kitendo ili kuifanya dini ya Allah ienee kila pahala.

1- Abu’l Ala Mawdudi, Jihad katika Uisilamu, Machapisho ya Kiisilamu LTD, Lahor, uk.1; Rudolph Peters, İslam ve Sömürgecilik (Uisilamu na Ukoloni), Kilichofasiriwa na Süleyman Gündüz, Nehir Pub. ist.1989, uk.29; M.J. Kister, "Mali ya Ardhi na Jihad" , Jarida la Kiuchumi na Historia ya Kijamii ya Mashariki, Leiden, 1991, XXXIV, 276; W. Montgomery Watt, Nadharia ya Siasa ya Kiisilamu, Edinburgh, p. 14; Ahmet Özel, İslam Hukukunda Milletlerarası Münasebetler ve Ülke Kavramı (Mahusiano ya Kimataifa Katika Sheria ya Kiisilamu na Dhana ya Nchi), Marifet Pub. Ist. Uk. 64

Aina za Jihad

1. Jihad dhidi ya Ujinga: Jihad hii inamaanisha kuwafundisha watu ukweli na mambo mazuri. Allah Mtukufu anamhutubia Mtume wake katika Quran kama ifuatavyo:

“Waite waelekee kwenye Njia ya Mola wako Mlezi kwa hikima na mawaidha mema, na ujadiliane nao kwa namna iliyo bora.” (an-Nahl, 125)

Yafuatayo yanaelezwa katika aya nyengine:

“Na uwe kutokana na nyinyi umma unao lingania kheri na unao amrisha mema na unakataza maovu. Na hao ndio walio fanikiwa.”  (Aal-i Imran, 104)

Quran ni dawa ya roho inayotosha kutibu kiyakinifu na kiroho, na majeraha ya mtu mmoja mmoja na ya kijamii sio tu kwa taifa fulani mahususi bali watu wote hadi Siku ya Kiama. Wajibu wa kuwasilisha dawa hii kwa watu wamepewa Waisilamu.

2. Jihad dhidi ya Nafsi ya Mtu: Waumini wanaonywa dhidi ya njama za nafsi katika aya kama ifuatavyo: “… wala usifuate matamanio yakakupoteza kwenye Njia ya Mwenyezi Mungu.” (Sad, 26)

Mtume (s.a.w.) ameeleza yafuatayo “jihadi kubwa zaidi ni ile dhidi ya nafsi yako.” Pia amesema, “Adui mkubwa ni nafsi yako, ambayo imo ndani mwako.” (Ajluni, Kashfu’l-Khafa, Beirut, I, 143, Hadith Nambari: 413)

Mtume amevutia umakini juu ya umuhimu wa jihad hii. Kwa hakika, wakati wa kuridi mapiganoni, Mtume (s.a.w.) alisema, “Tumerudi kutoka jihad ndogo kuja kwenye jihad kubwa kabisa.” (Kanzu’l-Ummal, IV, 430, Hadith Nambari: 11260 ) Hivyo, alielezea kwa kifupi kuwa mtu kuishinda nafsi yake lilikuwa ni suala zito zaidi na muhimu zaidi kuliko kupigana na adui.

3. Jihad dhidi ya Shetani: Aya ifuatayo katika Quran inaonesha kuwa Shetani ni adui mkubwa kabisa kwa mwanadamu. “Hakika Shet’ani ni adui yenu, basi mfanyeni kuwa ni adui.” .”(Fatir, 6 ) Hivyo, umakini unavutwa kwenye ukweli kuwa jihad kubwa zaidi ni ile inayofanywa dhidi ya adui mkubwa zaidi.

4. Jihad ya Silaha: Jihad hii sio yenye kuendelea. Sio faradhi kwa kila mtu. Kama dola lina nguvu ya kutosha, jihad ni fard al-kifayah (fardhi ya kujitosheleza); yaani, kundi la watu fulani linaposimamisha jihad, watu wengine hawabebeshwi jukumu.