FAQ katika kifungu cha Kiapo - Dhabihu

1 Nini maana ya qurban (kuchinja mnyama)? Kwa nini Waislamu wanachinja mnyama? Kuna hekima gani?

Kilugha qurban maana yake ni kujikurubisha. Hapo, kuchinja mnyama maana yake ni kuchinja mnyama kutokana na mema aliyoyaamuru Allah ili kujikurubisha Kwake na kupata radhi zake.

Allah anaeleza yafwatayo katika Sura al-Hajj:

“Nyama zao hazimfikii Mwenyezi Mungu wala damu zao, lakini unamfikia uchamungu wenu.” (22/37).

Kufuatana na hayo, inafahamika kuwa lengo halisi la kuchinja mnyama ni kutimiza amri ya Allah na kuonesha kwamba mtu anamwogopa Allah. Inamaanisha kwamba tunaweza kuchinja hata vitu vyetu vya thamani mno kama Allah atatuamrisha. Lengo ni kuonesha kuwa tunaweza hata kuyatoa muhanga maisha yetu kama Mtume Ibrahim (Abraham) aliyeamua kumchinja mwanawe, Ismail (Ishmael). Kwa namna fulani, qurban inamaanisha tunaweza kuondokana na hisia za kupenda anasa za kidunia na kukitoa muhanga kila kitu kwa ajili ya Allah.

Lengo halisi la qurban ni kupata radhi za Allah na kutaka kujikurubisha Kwake. Mtu anaechinja mnyama huwa anajikurubisha kwa Allah na kutafuta radhi Zake. Kuchinja mnyama pia ni mfano wa msaada wa kijamii na mshikamano. Kwa ujumla, masikini hula kiwango kikubwa cha nyama iliyochinjwa kwa ajili ya kujikurubisha. Kama inavyoonekana, ufahamu wa kujikurubisha kwa Mungu na kuwasaidia masikini upo kwenye msingi wa ibada hii. Bila ya kujali hukumu ya fiqh katika hilo, kuchinja mnyama kumekuwa na nafasi muhimu kwa karne kadhaa katika maisha yetu ya kidini kama ni aina ya ibada yenye alama ya jumuia za Kiisilamu.

Dini ya Kiisilamu ina lengo la kumfanya mtu apate hekima ya kiroho na utakasifu wa kibinaadamu; wakati huo huo, inafafanua umoja na mshikamano wa amri na matendo ya jumuia. Sifa hii ya juu ya Uislamu imekuwa wazi zaidi katika ibada za kipesa pamoja na kipimo cha kijamii kama vile zakah, hajj na kuchinja mnyama. Aina hizi za ibada zipo tokea siku za mwanzo za Uisilamu bila ya kupitiwa na badiliko lolote na uingiliaji kati wowote katika ujumla wa kanuni zake na msingi wake katika jumuia zote za Kiisilamu na zimekuwa zikihamishwa toka kizazi hadi kizazi.

Hekima za Kuchinja Wanyama  

1- kilugha qurban ni kitu ambacho mtu anaweza kukitumia ili kujikurubisha kwa Allah. Kama inavyofahamika kutokana na neno kuchinja mnyama (qurban) ni fursa ya kuwa karibu na Allah na kupata radhi Zake. Qur’an inaeleza yafuatayo”

“Na kila umma tumewafanyia mahala pa kuchinjia mihanga ya ibada ili walitaje jina la Mwenyezi Mungu juu ya vile walivyo ruzukiwa katika wanyama wa mifugo. Basi Mungu wenu ni Mungu Mmoja tu. Jisalimisheni kwake tu, na wabashirie wanyenyekevu. [Hija (Al-Hajj), 34 (22:34].”

Katika aya hiyo, imeelezwa kwamba Allah Mtukuka ameamrisha hivyo ili kuwakumbusha waja Wake kuwa Yeye ndiye mmiliki wa wanyama wote na kwamba amewatunukia wanaadamu kuwa ni ishara ya rehema na baraka Zake. Mwanaadamu, anaweza kutumbukia katika utukutu na kusahau kadiri muda unavyosonga mbele kwamba mmiliki wa kweli wa mali zake na utajiri wake ni Allah Mtukuka, aliyempa mali zote kuwa ni baraka. Kama Qarun, anaweza kudhania kwamba amejipatia vitu vyote kutokana na kazi yake mwenyewe, elimu na uwezo; na pengine aanze kujichukulia baraka za Kiungu kwa ajili yake binafsi na kujaalia kwamba ana nguvu na ushupavu. Anaweza kujihisi majigambo na kuvuka mpaka. Hivyo, amri ya kuchinja mnyama inamkumbusha kwamba mali zote na vifaa vyote, mashamba ya matunda, utajiri na pesa ni ukarimu wa Allah Mtukuka ambaye amempa zawadi vitu hivyo na kwamba Mwenyezi Mungu ndiye mmiliki wa kweli. Anamtaarifu mwanadamu kwamba hawezi kumiliki chochote isipokuwa kwa ruhusu Yake na utashi. Hivyo, binaadamu ataacha kiburi na kuwa mnyenyekevu. Ataanza kuwa na adabu kama mja halisi na kujaribu kumshukuru Allah. Mwenendo huo unakuwa ni fursa ya kujikurubisha kwa Allah na kupata radhi za Allah.

2- Alla hahitaji kuchinjiwa mnyama, wala hahitaji hata ibada moja inayotekelezwa na binaadamu. Hata hivyo, kwa amri ya kuchinja mnyama, Allah anawajaribu waja Wake, huwapima bidii yao na umakini wao mbele ya amri ya Allah na ukaribu wao Kwake. Yafuatayo yanaelezwa ndani ya Qur’an, Al-Hajj (Hija) aya 37:

“Nyama zao hazimfikii Mwenyezi Mungu wala damu zao, lakini unamfikia uchamngu wenu. Namna hivi tumewadhalilisha kwenu ili mumtukuze Mwenyezi Mungu kwa alivyo kuongoeni. Na wabashirie wafanyao mema…”.

Kama inavyoonekana katika aya pia, lengo la kuchinja wanyama ni unyoofu, bidii na kuwa karibu na Allah. Lengo  ni kumkumbuka Allah kwa fadhila Zake alizotoa na hususani kupata radhi Zake. Isipokuwa yale malengo yaliyokusudiwa, bila ya kujali ni kiasi gani cha nyama kimetolewa wala kiasi gani cha damu kimemwagwa, hayana thamani mbele ya Allah.

3- Kuchinja mnyama pia ni fursa ya wokovu wa Mtume /Ismail (amani na baraka zimshukie) kuwa ni hisani ya Allah ya kukosa kuchinjwa. Allah, Aliye juu Zaidi, alimpa mtihani Mtume /Ibrahim (a.s.) na kumtaka amchinje mwanawe wa pekee, /Ismail. Wote wawili Mtume Abraham na mwanawe Mtume /Ismail (amani iwe juu yao) walitii kwa unyenyekevu. Mtume Abraham alimlaza chini mwanawe na kuanza kumchinja kooni. Hata hivyo, kisu hakikumkata Mtume /Ismail (a.s.). Hayo yalikuwa kwa uweza wa Allah, Aliye juu, hakuwa Nabii /Ismail aliyechinjwa bali ni kuwaonesha na kuwaarifu malaika na watu watakaokuja wakati wa mwisho kuhusu kujisalimisha kwao mitume hawa watukufu kusikofikika na utii, bidii na wema. Kwa kuwa hekima hiyo ishatokea, Allah Mtukuka amekiamuru kisu kisimchinje Mtume /Ismail. Badala ya Mtume Ishmael, aliwateremshia kondoo kutoka Peponi ili achinjwe. Hivyo kuchinja mnyama ni ukumbusho wa tukio hilo adhimu la kupigiwa mfano.

4- Kila mwaka, Waislamu huchinja maelfu ya wanyama. Kwa namna fulani, ni usemi wenye ishara ambayo Mwislamu anaweza kuchinja chochote alicho nacho ili kumwabudu Allah, kutii amri Yake na kuacha chochote alichonacho kwa ajili ya Allah.

5- Amri ya kuchinja mnyama iliyoletwa na Uislamu pia ni zawadi na rehema kwa watu. Masikini wenye shida na hawajaweza kula nyama kwa mwaka mzima wanaweza kupata fursa ya kupata nyama ya kula ya kutosha wakati wa sikukuu ya al-Adhha. Hivyo, mtazamo wa Uisilamu unaofahamu usawa wa kijamii utaonekana.

2 Je, ni ukatili kuchinja wanyama?

Baadhi ya waandishi wamekubali kuwa ni ukatili kuchinja baadhi ya wanyama kwa kuwakata koo zao kwa lengo la kutekeleza wajibu wa kidini na ibada, na kwa hivyo, baadhi ya ukosoaji umeelekezwa kwenye dini ya Uislamu. Walioiweka mbele mitazamo hiyo hawakuuangalia ukweli huu: Nyama inayopatikana kutokana na kuchinja wanyama ni chanzo cha protini ya thamani ya juu ambayo kimsingi ni muhimu mno kwa watu. Hii ndio sababu, duniani kote leo hii, idadi isiyohesabika ya wanyama  huchinjwa tu kwa ajili ya chakula huko machinjioni na hutumiwa kuwa ndio chanzo cha lishe..

Hakuna chanzo cha mbadala wa nyama duniani. Kwa kuzingatia hili, kupinga kuchinjwa wanyama kama chanzo cha lishe na kuzingatia hilo kuwa ni ukatili sio tu ni upuuzi bali pia halina mantiki.  Tokea enzi za awali, wanaadamu wamekuwa wakipata chakula kwa njia hiyo.

Kutokuujali ukweli huo na kupinga kuchinja mnyama kwa sababu tu ni wajibu wa kidini kunaweza tu kuwa ni mtazamo wa kiitikadi. Ukatili wa kweli ni kuua watu. Lazima wajaribu kulikomesha hilo kadiri wawezavyo. Kujaribu kulinda haki za watu wanaochinjwa na dunia ya kisasa ni kuwajibika zaidi na ndio nukta mahususi kuliko kuzuia kuchinja wanyama, walioumbwa kuwa ni chanzo cha lishe kwa wanaadamu.