Maarisho ya Allah na makatazo kwa hakika ni kwa ajili ya manufaa ya watu. Wanazuoni wa Kiislamu wamekubaliana kwamba amri zote hizi zinalenga kuwanufaisha watu. Ni ukweli usiopingika kwamba yapo manufaa makubwa kwa watu katika mambo ambayo Allah anatutaka tuyafanye na kuna madhara katika mambo Anayokataza. Kutokana na wito uliotolewa na mafundisho ya Kiislamu, wanazuoni wa Kiislamu mara zote wamekuwa wakifikiria mno manufaa na hekima ya njia mbalimbali za kuabudu na wamejaribu kuwaeleza njia za utekelezaji ili kuwasaidia watu kuzitakasa nafsi zao na kuzitukuza badala ya manufaa binafsi katika kuzitekeleza. Katika swala hili, faida na hekima ya kuabudu ambayo wanawajibishwa ziko wazi, pia ni kweli kwamba sio manufaa yote na malengo yanayopaswa kueleweka ni yakinifu.
Lengo kuu la kufunga swaumu ni kuwafanya watu wafikie uchamungu. Hili limeelezwa wazi katika Qur’an:
“Enyi mlio amini! Mmeandikiwa Saumu, kama waliyo andikiwa walio kuwa kabla yenu ili mpate kuchamngu.” (Qur’an, al-Baqarah, 2:183)
Kufunga swaumu, kunakowaongoza watu kwenye hatua ya elimu ya kiroho, kunawafanya watu waondokane na masimbi ya madhambi yaliyomo nyoyoni mwao na nafsini mwao kwa muda mfupi. Kufunga swaumu, kwa hivyo, kunawafanya wafikie siri ya aya “Hakika amefanikiwa aliye itakasa” (Qur’an, ash-Shams, 91:9). Haya ni maelezo ya ukweli kwamba wale wanaozitakasa nafsi zao ndio watakaopata uwokovu. Kama vile kutoa zaka kunavyosafisha madhambi na kusababisha kukua kwa usafi na unyoofu (Qur’an, at-Taubah, 9:103), hivyo pia ndivyo ilivyo swaumu, ambayo ni zaka ya kiwiliwili, kuwaokoa watu kutokana na kutawaliwa na nafsi zao.
Mtu anayefunga swaumu huvunja msururu wa tamaa za kimwili na kuishikilia kamba ya Allah. Ilhali tamaa za kimwili zinamfanya mtu kuwa mbinafsi na kumpelekea kuwa mkiwa, mtu anakuwa makini zaidi juu ya ukweli kwamba yeye ni mwanajamii, kwa kushikilia kamba ya Allah. Wakati wa Ramadhani, mwezi wa kufunga, sala zinazosaliwa kwa jamaa zinaleta hisia ya umoja katika nafsi. Matajiri wanasali katika safu moja na masikini, wanakula kwenye meza moja; sadaka, fitrah na malipo (fidya: kwa wale wasioweza kufunga (wazee, wagonjwa na wasiojiweza, n.k.) fidia lazima itolewe kwa kumlisha masikini kwa kila siku ambayo mtu hafungi) ni kama maji ya maisha ili kuboresha uenezaji wa pato lisilo na uwiano.
Kufunga kunaifanya tamaa ya nafsi iwe nyoofu kutokana na uumbwaji wake kwa upande mmoja, kujizuia kwa khiyari kutokana na matamanio ya nafsi na kujifunza subira kutokana na kuwafanya watu wavumilie njaa na kiu kwa upande mwingine. Kuwa na maisha ya mafanikio, mtu anahitaji kuelekea kwenye unyoofu wa tamaa za nafsi. Watu wenye imani dhaifu hawawezi kufanikiwa maishani; wanaweza pia kumalizikia vibaya kwa upande wa kiroho. Kwa sababu njia za kuabudu zina hali na namna ambazo wale tu wenye imani thabiti wanaweza kuzitekeleza. Katika nukta hii, kufunga kunafaa sana katika kuyadhibiti matamanio ya nafsi na kuitukuza nafsi kwa upande wa kuitakasa na utiifu. Vivyo hivyo, mazingatio ya swaumu kuwa ni namna ya kujinyima anasa za kimwili na taabu kwa dini mbalimbali na tamaduni licha ya kuwepo miundo tofauti yenye manufaa kwa upande wa kueleza ukweli huu.
Shukurani kwa swaumu, hali ya kukinai inaingia tena katika majumba yetu. Mtu anayevumilia njaa na kiu kutokana na swaumu anafahamu watu wenye haja na umuhimu wa mtu kukinai alichonacho. Hawezi kamwe kukifuja. Maelezo ya Mjumbe wa Allah “Mtu kukinai alichonacho ni hazina isiyo na ukomo” (Bayhaqi, Zuhd, 2:88) yanagonga katika masikio ya waumini. Kufahamu umuhimu wa chakula, mtu anakuwa ni mwenye shukurani zaidi kwa Mungu. Anafahamu lengo linalosababisha kunyimwa na kukinai kunapelekea rehema. Dalili ya dunia ya Mjumbe wa Allah “wale wanaotumia kwa busara hawatopata shida kutimiza malengo” (Ibn Abi Shayba, al- Musannaf, 5:331) kuonekana wazi wazi katika maisha yake.
Swaumu inamwezesha mtu kuwa na nidhamu katika maisha yake pamoja na iftar (futari wakati wa mwezi wa Ramadhani) na sahur (daku) na tarawih sala na namna nyenginezo za ibada.
Ramadhani, mwezi wa swaumu, umejaa fursa na hazina mbalimbali kwa binaadamu ili arejee kwa Mola wake Mlezi na kumwomba msamaha wa madhambi yake. Mtu ana fursa ya kuzingatia mengi zaidi kwenye Qur’an. Kutokana na wingi huo kwamba Ramadhani inaleta na inaondosha utando wa madhambi kwenye moyo na ubongo, binaadamu anaanza kufahamu baadhi ya aya kwa kina.
Kama ni sadaka ya mwili, swaumu inachangia pakubwa kwenye hali ya ujengaji na uvunjaji wa kemikali mwilini kwa kuondosha sumu zilizomo mwilini. Katika mwezi huu, binaadamu anapoanza kuuzingatia mwili wake kuwa ni wa kimaajabu na mshikamano wenye mpangilio mzuri wa maada na kumaanisha kwamba uko tofauti na viumbe wengine, miili hurudia upya na ubongo huchangamka… miili yetu inakuwa na afya kama inavyohakikisha maneno ya Mjumbe wa Mungu “Fungeni mtapata afya”. (Tabarani, Mu’jamu’l-Awsat, VIII: 174; Mundhiri, at-Targhib, 2:206)
Kufunga swaumu ya Ramadhani ni wakati ambao watu hujisikia kuwa na matumaini ya msamaha. Swaumu ni mwalimu anayewafundisha watu namna ya kuwa imara dhidi ya matatizo ya ghafla. Ramadhani ni mwezi unaotoa nafasi kwa watoto wetu kujifunza na kutekeleza dini kwa msisimko…
Mjumbe wa Allah amesema madhambi ya wale wanaoitarajia Ramadhani kwa kuamini na kumtumainia Allah basi watasamehewa makosa yao. (Nasai, Imani, 21). Kwa namna hiyo hiyo, Mtume amesema na huku akimtaja Sahaba wake Mtukufu Ka’b b, Ujra: “Ewe Ka’b! Sala ni ushahidi unaothibitisha kuwa mtu ni Mwislamu. Swaumu ni ngao madhubuti. Kutoa sadaka kunayasafisha madhambi kama maji yanavyouzima moto. Ewe Ka’b! Nyama na mifupa inayoundika kwa kulishwa na vitu vya haramu inastahiki kuingia motoni.” (Tirmidhi, Jum’a, 79).
Upo muunganiko imara kati ya hekima na ufahamu wa amri za swaumu. Kuwa makini na kanuni zinazohusiana na sheria za swaumu kutatupa fursa ya kufunga swaumu kwa mujibu wa sunnah aliyotuachia Mtume kuwa ni hekima.
Kufunga swaumu ni kutokula, kunywa na kutoshiriki kitendo cha ngono katika muda kati ya wakati wa fajr sadiq (adhana ya pili/alfajiri ya kweli; wakati wa mchana kunapokuwa na mwangaza kwenye upeo wa macho kabla ya kuchomoza jua) na kati ya kuchwa kwa jua.
Kufunga swaumu pia kunaitwa imsak. Maana ya Imsak ni kuiweka roho/nafsi mbali na inayoyatamani na kutoyafanya. Kinyume cha imsak ni iftar, yaani kufutari.
Amri ya Kidini ya Kufunga Swaumu
Kufunga swaumu ni moja ya nguzo tano za Uislamu. Wakati huo huo, ni moja ya alama kubwa za Uislamu. Imefaradhishwa (wajibu) katika mji wa Madinah, mwaka mmoja na nusu baada ya Hijra (Kuhama Makka kwenda Madinah) na siku ya tarehe 10 mwezi wa Shaban. Uwajibu wake umeanzishwa na Kitabu (Qur’an), Sunnah (mwenendo wa Mtume) na Ijma’ (makubaliano ya ummah/jumuia au ulama/wanazuoni wa Uislamu).
Katika Qur’an yanaelezwa yafuatayo:
Enyi mlio amini! Mmeandikiwa Saumu, kama waliyoandikiwa walio kuwa kabla yenu… (Qur'an, Al-Baqarah, 2:183)
Kufunga swaumu pia ni ibada ya kimwili kama wajibu sala ya faradhi. Sifa maarufu ya ibada hii ni kwamba inawaepusha mbali na maovu, na hilo linadhibiti matamanio ya ziada na kuihimiza nafsi. Katika hadith, inaelezwa hivi:
Kufunga swaumu ni ngao (inawakinga binadamu kutokana na matamanio na maovu). Aliyefunga hatakiwi kutamka maneno machafu kutokana na ujinga. Aliyefunga asiwajibu wanaotaka kupigana na kupambana naye kwa kusema tu: mimi nimefunga.’
Kwa kuwa kufunga swaumu kunawakinga wanaadamu dhidi ya kuinikia maovu, Mjumbe wa Allah (S.A.W.) amewashauri vijana, makapera kufunga swaumu ili kupunguza msongo wa matamanio ya ashiki. Pia ni ukweli unaokubalika kisayansi kwamba kufunga swaumu kunatuliza hisia za matamanio ya ashiki.
Mwezi wa Ramadhani unapoingia, kunakuwa na upungufu mkubwa wa matukio ya uhalifu yanayofanyika katika jumuia. Maovu hufifishwa hadi kiwango cha chini. Matokeo yake, matendo mema huongezeka. Kunakuwa na makaribishano kunjufu na upendo. Kusaidiana kwa pande mbili pamoja na mshikamano huongezeka. Mjumbe wa Allah (S.A.W.) anafafanua sababu ya athari ya kijamii iliyomo kwenye kufunga swaumu katika hadith ifuatayo:
Inapoingia Ramadhani, mwezi wa kufunga swaumu, milango ya Pepo hufunguliwa; milango ya Moto hufungwa na mashetani wote hupigwa pingu.
Thamani kubwa iliyomo katika kufunga swaumu mbele ya Allah inaelezewa katika hadith qudsi ifuatayo:
Matendo mema yote na ibada wanazozifanya wanadamu ni kwa ajili yao wenyewe (upo wasiwasi wa starehe na manufaa kwao). Hata hivyo, kufunga swaumu sio hivyo. Kufunga swaumu ni ibada inayofanywa kwa ajili ya ridhaa Yangu. Na Nitaitolea malipo.
Katika hadith qudsi nyingine, inaeleza:
Kwa kila tendo jema, kuna malipo yake mara kumi hadi mara mia saba. Hata hivyo. Malipo ya kufunga swaumu hayatolewi kwa kigezo hicho. Kwa kuwa ni kwa ajili Yangu. Ni Mimi Pekee nitayoilipa.
Kama inavyofahamika kutokana na sentensi hizo, licha ya kuwa kila jema na ibada kuna thawabu zake (malipo ya matendo mema yatakayohisabiwa siku ya qiyamah/siku ya kiama) zilizoambatishiwa kuanzia thawabu 10 hadi 700, kwa upande wa funga thawab zake hazihesabiki. Na Allah hakuyaacha malipo yake yahesabiwe na malaika Wake bali Ameyaweka kwake Yeye Mwenyewe kuyalipa. Kwa sababu hii, Siku ya Kiama, waumini watakuta thawabu nyingi kutokana na swaumu zao ambazo hawakuzitarajia.
Mjumbe wa Allah (S.A.W.) amesisitiza suala hili kama ifuatavyo:
Zipo furaha mbili kwa mtu anayefunga: Ya kwanza ni wakati wa kufutari (anapofungua baada ya kuzama jua); ya pili ni furaha ya kufunga swaumu (malipo yake) atapokutana na Mola wake Mlezi.
Katika baadhi ya hadith, fadhila za juu na hadhi ya heshima wanayoipata wanaofunga inaelezewa kama ifuatavyo:
Upo mlango Peponi unaitwa Rayyan. Siku ya Kiama, wale waliofunga tu ndio wataoweza kuingia (Peponi) kupitia mlango huo. Hakuna mwingine atayeweza kuingia kupitia mlango huo. (Siku ya Kiama), kutanadiwa: Wako wapi waliofunga? Waliofunga simameni na ingieni. Baada ya kuingia, mlango huo unafungwa; kuanzia hapo, hakuna atayeweza kuingilia mlango huo.
Naapa kwa Allah kwamba harufu ya njaa ya kinywa kilichofunga inaridhisha zaidi kuliko harufu ya uturi, ni msafi zaidi na maridhia mbele ya Allah.
Dua ya watu wa aina tatu haitokataliwa:
Aliyefunga mpaka afutari (mlo unaoliwa baada ya kuchwa jua ili mtu kufutari)
Mtenda haki/mkuu wa dola mwadilifu
Aliyetendewa uovu/aliyedhulumiwa.
Yafuatayo yanaelezwa katika Quran:
“Enyi mlio amini! Mmeandikiwa Saumu, kama waliyo andikiwa walio kuwa kabla yenu ili mpate kuchamngu.” (al-Baqara, 2/183).
It is known that the Messenger of Allah said,
Inatambulika kuwa Mjumbe wa Allah amesema,
“Kufunga swaumu ni ngao inayomkinga mtu na Moto wa Jahanamu kama ngao inayokukinga na hayo wakati wa vita.” (Nasai, Sawm, IV, 167)
Kufunga swaumu ni aina ya ibada inayomkinga mtu anayefunga kutokana na aina zote za matamanio ya ashiki na inamwongezea unyoofu. Ni muhimu sana kujizuia na njaa, kiu na matamanio mengine ya nafsi. Waumini wanaomwamini Allah na wanaopigana jihad kwa ajili Yake watakuwa na imani thabiti shukurani kwa swaumu.
Ramadhani hutangulia kwa siku kumi au kumi na moja kila mwaka kwa kuwa kalenda ya Hijri inategemea mwandamo wa mwezi. Kwa hivyo, wakati mwingine mtu hufunga katika kipindi cha baridi kali ya wakati wa kipupwe wakati mwingine wakati wa joto kali msimu wa kiangazi. Kwa namna fulani, muumini ananuia: “niko tayari kutimiza amri za Allah hata katika baridi ya kuganda au joto la kubabua.”
Vilevile, ni tukio muhimu sana kwa muumini kuyaacha matamanio ya nafsi yake kwa mwezi mmoja ili apate radhi za Allah.
Unafiki hauna nafasi katika kufunga swaumu. Kwa hakika, asili na sifa za kufunga swaumu na muumini anayefunga zinaelezwa kama ifwatavyo:
“Kinga ni ngao (au stara au hifadhi). Hivyo, mtu anayefunga swaumu anatakiwa ajiepushe kuingiliana na mkewe na anatakiwa asiwe na tabia za kipumbavu na kifidhuli, na kama mtu anatapigana naye au kumtukana, anatakiwa amwambie mara mbili, ‘nimefunga.” Mtume ameongezea kusema, “Naapa kwa Yule Ambaye nafsi yangu iko Mikononi Mwake, harufu inayotoka kinywani mwa aliyefunga ni bora mbele ya Allah kuliko harufu ya uturi. (Allah anasema kuhusu mtu aliyefunga), Ameacha chakula chake, kinywaji chake na matamanio yake kwa ajili Yangu. Swaumu ni Yangu. Hivyo basi nitailipia (kwa aliyefunga) na malipo ya amali njema ni mara kumi.” (Bukhari, Siyam)