FAQ katika kifungu cha Sala

1 Ni ipi hekima ya kuswali swala tano kila siku?

Asubuhi na mapema, mwanadamu huwa katika hali  kana kwamba ameanza maisha mapya na huwa na nguvu za kiwiliwili ambazo ni muhimu kwa shughuli za kila siku kupata mahitaji yake ya kuendesha maisha yake. Ni Allah ndie anaempa nguvu hizi na ndie anaemfanya afaulu katika juhudi zake za kutafuta maisha. Hivyo basi, mwanaadamu anapaswa kuswali swala ya alfajiri ili amshukuru Allah kwa kumpa neema ya afya njema na ili apokee msaada kutoka kwa Allah katika juhudi zake za kidunia.

Kila siku, kutoka asubuhi hadi jioni, mwanadamu hufaidika na neema za uhai, afya na akili ambayo Allah amempa. Kuzishukuru neema hizi, mwanadamu hupata mafanikio katika mambo yake ya kidunia. Swala za mchana na jioni zimewekwa kuwa ni lazima ili mwanadamu ashukuru kwa mafanikio aliyoyapata na ili shughuli hizi ziendelee kulindwa ili zisije zikaiingiza nafsi kwenye mghafala na huzuni.   

Swala za jioni zimefanywa kuwa fardhi (lazima) ili zile kazi za kila siku na juhudi ambazo zipo karibu kukamilika kwa kadri jioni inavyokaribia zimalizwe kupitia ibada za kiroho na kwa hiyvo itakuwa ni alama ya shukurani kwa mapato na faida iliyopatikana siku hiyo.  

Baada ya hapo, mwanadamu ataingia. Ulimwengu wa usingizi. Kabla ya kufika kwenye ulimwengu huu, ambao ni mfano wa kifo na ambao huzingatiwa kama kipindi cha Amani na utulivu, inatakiwa kuimaliza siku kwa ibada tukufu, ili kuingia katika ulimwengu huo na radhi za kiungu na na mwamko wa kiroho na kumuomba Allah msamaha na huruma zake na itakuwa ni alama ya mwisho mwema; hivyo basi, swala za usiku hufanywa.

Kwa upande mwengine, ziko hatua 5 tofauti kwenye maisha ya watu na viumbe vyengine vinavyowazunguka watu: kuzaliwa (being born), kukuwa (growing up), kusimama makuzi (stagnating), kuwa mzee (getting old) na kufa (dying).

Kuendana na hatua hizo, Muumba wetu ametuagiza tutekeleze swala 5 kila siku ambazo zitaweka usawa mzuri baina ya uwepo wetu wa kimaumbile na kiroho na juhudi zetu. Hatuwezi kumshukuru Allah vyakutosha kwasababu ni Yeye ndie alietuagiza kufanya ibada hiyo ambayo ni tukufu, kivitu na ina faida nyingi sana.

Hekima iliyopo nyuma ya kuzigawa swala mara 5 kwa siku haifungwi kwenye hayo tuliyoeleza juu tu.

Maelezo yafuatayo ya mwanachuoni Badiuzzaman Said Nursi yanafafanua jambo hili:

 “Kama ulivyo mshale wa sekunde, mshale wa dakika, mshale wa saa, na mshale wa siku kwenye saa ambayo hueleza majuma kila moja humuangalia mwenzake, ni mifano ya wao kwa wao, na hufuatana, ni hivyo hivyo kwenye mabadiliko ya usiku na mchana, ambayo ni mfano wa sekunde za dunia yetu hii – saa kubwa ya Allah Mtukufu – na miaka yenye kueleza dakika zake, na hatua za umri wa mwanadamu ambazo hueleza masaa yake, na muda wa umri wa maisha ya dunia ambao hueleza siku kila moja kumuangalia mwenzake, ni mifano ya kwa wao, zinafanana , na zina kumbukana.

Kwa mfano:

Muda wa swala ya alfajiri, mapema sana asubuhi: Muda huu mpaka kuchomoza kwa jua huashiria na kukumbusha mwanzoni mwa kipindi cha masika, kipindi ambacho mwanamama hupata ujauzito, na mwanzoni mwa siku sita za uumbaji wa mbingu na ardhi; inakumbushia pia matendo ya Kiungu ndani yake…”

2 Ni nini swala? Kwanini swala, ambayo inajumuisha matendo machache tu ni muhimu sana katika Uislamu?

Mwenyezi Mungu Mtukufu hahitajii chochote; Hahitaji ibada zetu vile vile. Ni sisi ndio tunaohitaji ibada. Ibada ni aina ya tiba kwa majeraha yetu ya kiroho. Ni chakula chetu cha roho na tiba kwa maradhi yetu ya moyo. Hivyo basi, sababu ya Mwenyezi Mungu Mtukufu kutuagiza tufanye ibada ni kwa faida yetu. Wakati daktari anaposisitiza ushauri juu ya matumizi ya dawa kwa mgonjwa, hufanya hivyo kwa faida ya mgonjwa na si kwa faida yake. Ni upuuzi kumuambia daktari, “Kwanini unasisitiza matumizi ya dawa hii? Kwanini unaitaka hii?”; ni hivyo hivyo, itakuwa upuuzi na ukosefu wa fikra madhubuti kufikiri, “Kwanini Mwenyezi Mungu anatuamrisha tuabudu? Kwanini anataka ibada?”

Sababu ya kwanini Allah ameumba ulimwengu ni kuonesha ishara za majina yake na sifa zake na kuleta mambo mazuri yanayoakisi ishara na kazi zilizofanywa kwa usanii wa hali ya juu ili ipelekee kushuhudia utukufu wa uwepo Wake na watambue kwa urahisi viumbe vyenye utambuzi kama wanadamu.

Mwanadamu siku zote ameshughulishwa na mambo ya dunia; hivyo, haangalii maajabu ya Kiungu na akapata somo kutoka kwao kuhusiana na umoja wa Muumba, elimu yake isiyo mipaka, nguvu na hekima zake. Mtu anaweza akatafuta njia kwenda kwa msanii kutokana na Sanaa, na kwa mtoaji wa neema kupitia neema kwa kuachana tu na mambo ya dunia. Lakini njia pekee ya kuachana na mambo hayo ni kupitia swala.

Mwangaza, hewa, maji, chakula, ambavyo ni vyakula kwa ajili ya maisha ya kidunia na uwepo wa uhai wa kiwiliwili ni mambo muhimu; sawa na ibada hasa ya swala, ambayo ni mwangaza kwa akili, ni hewa kwa moyo na chakula cha roho, ni muhimu mno kwa mtu mwenye akili.

Swala, ambayo maana yake ni kutubu na kuomba msamaha, kutokana na makosa yetu kwa Allah, Ambaye ana ufalme wa milele kabla na baada kwa ulimwengu wote, ambae ametuumba tukiwa si chochote si lolote, ambae anatupa neema kwa maelfu, anayetuahidi maisha ya milele Peponi kwa wale watakao muheshimu, ambae tunamuhitaji kwa kila pumzi yetu na ambae ndie mfadhili wetu, swala ndio maelezo ya mwanadamu ya heshima kwa Mola wake. Si akili, moyo au dhamira inaweza kuruhusu dharau kwa Mwenyezi Mungu kwa kutokutekeleza swala.

Swala ni kama muhtasari wa ibada ambao unajumuisha nguzo zingine zote za Uislamu. Kwa mfano, mtu anayeswali vile vile hufanya aina ya Hija kwa kuelekea Qiblah; hufanya aina fulani ya funga kwa kutokula wala kunywa wakati wa swala; hufanya aina fulani ya Zaka kwa kuutoa muda wake ambao ndio mtaji wake wa maisha, kwa kutaja majina ya Allah. Kwa kuongezea, anapokuwa anaswali hufanya ibada ya viumbe vyengine ulimwenguni kwa kusimama kama miti na mimea, kwa kurukuu kama viumbe vyenye miguu minne na kusujuda kama wadudu wanaotambaa.

Sawa na hilo, baadhi ya malaika wanamuabudu Allah kwa kusimama muda wote, wengine wanaabudu kwa kurukuu na wengine kwa kusujudu muda wote. Mtu anaetekeleza swala tano hukamilisha ibada za malaika kwa kufanya kila kitendo kwa muda fulani; kwa mantiki kwamba, naye huwa kama malaika!

Swala ni ishara ya ibada ambayo ndio msingi mkuu wa dini ya Kiislamu. Maelezo yafuatayo yanapatikana kwenye hadithi: “Tofauti kubwa kati ya Muislamu na asiyekuwa Muislamu ni swala.” (Muslim, Iman, 134; Abu Dawud, Sunnah, 15; Tirmidhi, Iman, 9)

Kila mtu anayeingia anga la kiroho la Uislamu kwa misingi ya mkataba wa wa Imani anahitaji kupumua kwenye hewa hii ya ibada. Ni jukumu la kiraia kwa kila mtu ambae amekubali uraia wa kiroho wa Kiislamu la kutekeleza ibada ya swala. Roho, akili na dhamira vyote vina haki ya kufaidika na anga la kiroho la ibada. Ni ukatili wa hali ya juu kuvinyima vitu hivyo haki ya kuamiliana na Mola wao kwasababu tu eti nafsi haitaki.

Adhana inayosomwa mara tano kwa siku ni wito wa kusimama mbele ya Allah na ni kama amri ya kuwaita wanajeshi kukusanyika katika kambi za kijeshi za dunia kwa Mfalme wa milele. Mtu ambae hatotokea mara zote tano kwenye kambi za kijeshi huhesabika kama mtoro na huduma zake za kijeshi hufutwa; anapaswa aanze tena huduma hizo upya.

Hebu fikiria hali ya mtu ambae hakutokeza licha ya wito wa Allah mara tano kwa siku na hukimbia!

Swala ni mkusanyiko halisi. Wenye maana ya kupeleka shukurani kwa rafiki wa kweli anaetupa neema zisizohesabika.

Swala ni kisimamo cha kimya kimya kutambua ukubwa wa Muumba.

Swala ni kiunganisho kinachong’aa ambacho kinaunganisha ardhi na mbingu. Ni muhimu kwa milango ya fahamu kwa ambao wanahitaji mwangaza wa Amani ya kiroho hawana namna isipokuwa wakumbatie kiunganishi hichi. 

Kutekeleza swala kwa jamaa ni muhimu sana. Swala ya jamaa huzingatiwa kama moja ya sherehe kubwa za kiibada katika Uislamu. Ukweli kwamba swala ya jamaa hupewa umuhimu mkubwa inaonesha kwamba dini hii tukufu ni dini ya umoja na hivyo basi tunatarajia umoja wa kudumu baina ya Waislamu.

Swala ya jamaa hupunguza utabaka unaotokana na familia na matabaka ya kijamii. Haijalishi aina ya familia, rangi, utaifa, Waislamu wote husimama kwenye hadhi sawa wakitekeleza ibada ya swala na wote huelekea Qibla kimoja, wakimuabudu Allah mmoja wote kwa pamoja kama mwili mmoja.

Swala ya jamaa ni njia nzuri ya kuunganisha jamii. Ni fursa nzuri kwa waumini kila mmoja kujua hali ya mwenzake.

Ikiwa mawe ya jengo fulani ni madhubuti, jengo pia litakuwa madhubuti. Ni hivyo hivyo, ikiwa kila mtu, ambae ni jiwe kwenye jengo la jamii, akiwa sawa na madhubuti kiroho na kimwili kupitia ibada ya swala, basi na jengo la jamii litakuwa sawa na madhubuti. Sharti la msingi kwenye kutengemaa huku baada ya Imani ni swala.

Zipo aya nyingi na hadithi zinazoelezea umuhimu wa swala. Chache katika hizo zimeelezewa hapa chini kutoa fikra:

“Enyi mlio amini! Takeni msaada kwa subira na Sala. Hakika Mwenyezi Mungu yu pamoja na wanao subiri.” (al-Baqara, 2/153)

Kwenye aya hii, imeoneshwa kwamba ni muhimu kujifunza kuwa na subira na kufaidika na utukufu wa swala ili kufaulu mitihani duniani. Kwa kweli, swala na subira ni mfano wa magurudumu ya mashine kila moja humsaidia mwenzake. Kutekeleza ibada ya swala mara tano kwa siku hupelekea uvumilivu. Hata hivyo, mtu ambae hutekeleza swala tano hujifunza kuwa mvumilivu kwa sababu maisha yake huyaweka kwenye nidhamu maalumu. Hii ni kuwa, swala humsaidia mtu kuwa mvumilivu na uvumilivu humsaidia kutekeleza ibada ya swala.

"…Na kwa hakika jambo hilo (la swala) ni gumu isipokuwa kwa wanyenyekevu" (al-Baqara, 2/45)

Katika aya ya hapo juu, inasisitizwa kwamba kutekeleza ibada ya swala ina mnasaba wa moja kwa moja na kumjua Allah. Na ni jambo gumu kweli kwa wale waliyokosa elimu hii kuonesha subira kubwa inayohusu kutekeleza ibada ya swala.

Ulimwengu huu mkongwe umeshuhudia watu wengi waliopata kusema, “Niliswali kwa mwaka mmoja; nikagundua kuwa si jambo la kumalizika; kwa hiyo nikaachana nayo.”

“Zilindeni Sala, na hasa Sala ya katikati, na simameni kwa ajili ya Mwenyezi Mungu nanyi ni wenye kunyenyekea.” (al-Baqara, 2/238)

“Hakika Sala inazuilia mambo machafu na maovu” (al-Ankabut, 29/45)

“Hakika wamefanikiwa Waumini, Ambao ni wanyenyekevu katika Sala zao.” (al-Muuminun, 23/1-2)

Katika mkutano wa “Alastu bi rabbikum” [Mkutano ambao Allah aliwaita viumbe na akawauliza swali Je, Mimi si Mola wenu? Viumbe wakajibu “Wewe ni Mola wetu na hakuna ubishi kwenye hilo], ambao uko nje ya mipaka ya akili ya mwanadamu na ambao ni mkutano wa siri kwenye ulimwengu usiyoonekana, kila mmoja alisema “Ndio” kwa kupitia mifumo yao ya kiroho na ulimi wa hekima kupitia swali la Allah, “(Je, Mimi sio Mola wenu?) Swala ni ishara ambayo inathibitisha ahadi iliyotolewa katika ulimwengu usiyoonekana ndani ya ulimwengu wetu huu. Swala ni ngao kwa waumini.

3 Kuna hekima gani kwenye matendo ya sala?

Maana ya Matendo katika Sala: Kila nguzo na sehemu ya sala ina hekima zake mahususi,

Moja ya majina ya Allah ni al-Hakim (Mwingi wa Hekima). Yaani, kwa hakika anapangilia na kuumba hekima nyingi, mapendefu na malengo ya kila tendo ni Vyake. Ni kweli kwamba kuna maelfu ya hekima katika amri Yake na makatazo yake. Kuna maana nyingi katika kila tendo la sala, ambayo ndio ibada muhimu zaidi.

Tunaweza kuziorodhesha kama ifwatavyo:

Sala ndio nguzo ya dini. Kama tutafikiria kwamba Kaaba ndio nguzo ya ulimwengu, tutafahamu hekima ya kuligeukia Kaaba wakati wa kusali.

Kunyanyua mikono yetu tukiwa tunasema takbir (Allahu akbar) kunamaanisha tunavirusha vitu vya kidunia nyuma yetu na kusimama kusali kwa ajili ya Allah.

Tukisimama kwa miguu yetu, tunawakilisha namna miti inavyoabudu, milima na malaika ambao daima huabudu wakiwa wamesimama.

Tunapoinama, tunaiwakilisha ibada ya wanyama kama ngamia, mbuzi na kondoo namna wanavyoabudu, na malaika mara zote huabudu kwa kuinama.  

Tunaposujudu, tunaiwakilisha ibada ya mnyama anaetambaa, majani na malaika ambao daima huabudu wakiwa wanasujudu.   

Tunapoketi, tunaiwakilisha ibada ya viumbe vyote kwa Allah kwa niaba yetu wenyewe. Mwishowe, tunapotoa salamu upande wa kulia na kushoto, tunautolea salamu ulimwenu mzima.

Isitoshe, tunaposali, tunaufanya mwili wetu na kila kiungo chake kuabudu.

Kusimama na kusoma Quran kwenye sala pia kuna maana. Kuna hekima maalumu kwenye kuinama/kurukuu baada ya kusimama na kusujudu baada ya kurukuu, kunamaanisha kuwa karibu mno na Allah…

Mwanaadamu, akiwa katika hali ya kuiwakilisha ibada kuu inayotekelezwa ulimwenguni kote, anatekeleza kwa Mwingi-wa-Rehema-Mwenye-Kurehemu ibada ambayo inaendelea kuchukua nafasi mwilini mwake pamoja na kuabudu kwa viumbe hai na viumbe tunavyovizingatia kuwa sio hai mara tano kwa siku.

1. KUSIMAMA (QIYAM)

Kwanza, tunasimama, tunanyanyua mikono na kusema Allahu akbar (Allah ndio mkubwa kuliko wote). Hapo, mwanaadamu hurusha nyuma kila kitu isipokuwa Allah na kujielekeza kwa amri Yake na utashi. Utumwa na uja umewekwa hivyo. Hapo, ibada ya viumbe vyote ndio huwakilishwa.  

2. KUINAMA (RUKU)

Baada ya kumsifu Allah kama Anavyostahiki, mwanaadamu hijisikia unyonge kwenye uwepo wa kiburi anachokiinamia kukionesha na kukiinamisha kichwa chake kama ni alama ya heshima na kusema Subhana Rabbiyal-Azim (Utakasifu ni wake Mola Mlezi, Aliye Mkuu). Muumini anaiwakilisha ibada ya viumbe vyote wanaorukuu kwa kufanya hivyo.

3. KUOMBA KWA UNYENYEKEVU (DUA)

Kisha, ananyooka, na kumshukuru na kumsifu Allah kwa sababu Amemwongoza mja kwenye njia iliyonyooka. Kwa muda fulani, anatafakuri, akiwa amesimama, kiburi na utukufu wa Allah na uwepesi na uchache wa tendo lake, kisha anatishiwa.

4. KUSUJUDU (SAJDAH)

Anasujudu na kuweka paji lake la uso chini akijisikia staha na udhaifu kikamilifu na kusema,

‘Subhana Rabbiyal-Ala (Utakasifu ni wa Mola Mlezi, Aliye Mkuu).

5. KUKETI NA KUTOA SALAMU

Baada ya kurudia matendo hayo kwa mpangilio, anajikuta yuko mbele ya Allah pasi na viunganishi vyovyote na kumwomba Yeye msaada.

Vinapokutana viumbe viwili, husalimiana. Katika upande mmoja wa sala (kuketi), anaesali hurudia ibara hizo hizo za salamu ambazo zimetumika kati ya Mtume Muhammad (s.a.w.) na Allah wakati wa safari ya Miraji (kupaa mbinguni):

(Maamkizi mema yote, sala na wema ni wa Allah. Amani iwe juu yako, Ewe Mtume na rehema za Allah na baraka Zake. Amani iwe juu yetu na juu ya waja wema wa Allah!)

Matendo ya mwili katika sala:

Kuna matendo 4 katika sala. Tendo la kwanza ni qiyam, ambalo ni, kusimama. La pili ni ruku (kuinama). La tatu ni sijdah ya kwanza (kusujudu) na la nne ni sijida ya pili. (Fususulhikam,  2/476-477)

Kwenye kisimamo katika sala, kichwa kinamwashiria Mola Mlezi na miguu inawaashiria watu. Mwanaadamu, anayeyachanga matendo yote katika kisimamo, anasoma Quran (qira’ah), ambayo ni fard, katika hatua hii. Anatimiza fard mbili: qiyam na qira’ah.

Kama ilivyo ruku’, inamaanisha kuitenda hali ya wanyama katika sala. Katika hatua hii, miguu ya wanyama inatazama kwenye kitovu cha ardhi, na mwelekeo wa viwiliwili vyao viko kimlalo. Inamaanisha, wanyama husimama sambamba na mvuto wa dunia. Wakiwa wamesimama namna hiyo, kichwa cha mnyama hakitazami eneo wala mvutano wa dunia. Ni hali inayowahusu wao. Kwa nini tunatenda hivyo ilhali sisi ni wanaadamu? Swali kama, ‘Wanyama ni nani kwetu?” linaweza kuibuka. Jawabu ni ifwatavyo: mwili wa mwanaadamu, ambao ni kifupi cha wanyama 18 elfu, una roho ya kinyama inayoishi duniani. Roho hiyo, inayoitwa nafsi kwa upande wa matamanio, haiwezi kupandikizwa kwa binaadamu isipokuwa iwe imesafishwa. Atatakiwa ale kidogo, alale kidogo na ajamiiane kidogo ili awe mbali na upande wa mnyama, ambao ni karibu na dunia. Kisha, atakuwa katika hali ya kusafishwa. Salah (kusali), ambayo ni ibada inayoefahamika, inatakiwa itende uwepo wa mnyama ndani yake.

Hekima ya sajdah; mtu anaposujudu, kichwa kinakwenda chini sawa na kiwango cha miguu. Mtu hutenda hali hii ambayo ni kusujudu kwa mimea.

Kusujudu mara ya pili ni kukosa uhai. Lenyewe halina tendo. Yaani, hakuna tendo linakuja kutoka ndani yake. Inafanya kama ni matokeo ya nguvu kutoka nje. Inayojumuisha mbale ndani ya mawe na sakafu. Mbale inamilikiwa na kitu kinachoitunza isipokuwa ikiyeyushwa kwa kuwa ipo katika hali ya mtawanyiko katika vitu visivyo hai. Elementi ya kila mbale ina roho kwa upande wa atomi zake.

Kusujudu mara ya pili ni kama ya kwanza kwa sababu mimea na vitu visivyo hai viko pamoja; havina matendo kama wanyama. Kila sayari, nyota na vinavyofanana angani havina uhai. Kusujudu ni kukubwa kama kilivyo kiwango chao.

Kwa kuongezea, sala (salah) ni aina ya ibada inayojumuisha mwanaadamu, wanyama na viumbe vyote. Hata hivyo. Inafahamika kwa kutimizwa kimoyomoyo na kiroho na sio kimwonekano.