Aya ifuatayo inakataza ubaguzi wa kimbari:
“Enyi watu! Hakika Sisi tumekuumbeni kutokana na mwanamume na mwanamke. Na tumekujaalieni kuwa ni mataifa na makabila ili mjuane. Hakika aliye mtukufu zaidi kati yenu kwa Mwenyezi Mungu ni huyo aliye mchamngu zaidi katika nyinyi. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua, Mwenye khabari.” (Surah Al-Hujuraat, 13)
Katika surah hiyo hiyo, yanaelezwa yafuatayo:
“Waumini ni ndugu: Basi fanyeni amani na upatanishi baina ya ndugu wawili (wanaopingana).”
Kama inavyofahamika kutokana na aya za hapo, Allah anawachukulia waumini tu ndio ndugu na si watu wa mataifa mengine. Kwa mujibu wa Uislamu, mtu asiye muumini hawezi kuwa mrithi wa baba yake muumini. Kusipokuwepo imani, basi mahusiano ya kidunia, kimfumo na ya kimbari hukosa umuhimu wake.
Mtume wa Allah (s.a.w), ambaye amesema, “Hakuna muumini wa kweli isipokuwa humpendelea nduguye anachokipenda kwa ajili yake mwenyewe”, anatuelekeza jinsi aya hii ilivyo na mwangaza katika amali zetu na msisimko.
Nini kifanyike pindi chuki na uadui unapotokea kati ya waumini ilhali walitakiwa wapendane? Mwendelezo wa aya hiyo unaagiza yafuatayo: “fanyeni amani na mapatano baina ya ndugu wawili (wanaogombana).” Uhasama wao ugeuke kuwa urafiki, upendo na undugu.
Ndiyo, kwa mujibu wa amri ya Qur’an, waumini wote ni ndugu kwa kila mmoja. Wao ni familia moja. Juu ya mstari mmoja. Watu wanaowatenganisha huchukuliwa kuwa wamewafanyia kazi maadui kwa kujua au kutokujua.
Fundisho la Allah kutoka katika surah Hud: katika tukio la gharika ya Nuh, pindi Nuh aliposema, “Ewe Allah! Mwanangu pia ni wa familia yangu. (Uzao wangu)” Ewe Nuh, yeye si wa familia (uzao) yako.” Hivyo mtoto kafiri na mwasi hahesabiki kuwa ni katika uzao wake. Kisha, kafiri kutoka katika mbari yake hawezi kuwa rafiki au ndugu yake. Hapa kunahusiana na aya kutoka kwa Allah ambako hakuna nafasi ya upotoshaji wa tafsiri kwa makusudi:
“Enyi mlio amini! Msiwafanye baba zenu na ndugu zenu kuwa vipenzi vyenu ikiwa wanastahabu ukafiri kuliko Imani. Na katika nyinyi atakaye wafanya hao ndio vipenzi vyake, basi hao ndio madhaalimu.” (Surah at-Taubah, 23)
Aya hii pia inatoa maelezo ya aya, “Waumini ni ndugu mmoja” ambapo kuna ufahamu mzuri na wa kina.
Baba yako au kaka yako asiyeamini si rafiki yako.
Wale wanaofanya urafiki nao wanachukuliwa kuwa wamesaliti ukweli na wamedhulumu.
Anazingatiwa kuwa ametumia hisia yake ya upendo, aliyozawadiwa na Allah, katika sehemu isiyosahihi na amedhulumu …
Amejipeleka mwenyewe Motoni kwa maamuzi yake yasiyo sahihi. Ameidhulumu nafsi yake.
Kwa kufanya hivyo, kafiri anapata nafasi bora zaidi moyoni mwake kuliko muumini na anakuwa mkandamizaji kwa dhuluma yake kubwa.
Allah ambaye ndiye “Malik Yawm ad-Din” (Mwenye Kumiliki Siku ya Malipo.) anaeleza yafuatayo: “Siku ambayo kwamba mali hayato faa kitu wala wana. Isipo kuwa mwenye kumjia Mwenyezi Mungu na moyo safi...” (Surah ash-Shuara, 88-89)
Je, uhusiano baina ya mwana na baba si hatua ya kwanza na ya kiwango cha juu cha ukaribu wa kimbari? Aya hii inatujulisha kuwa ukaribu huo hauna thamani kabisa katika Siku ya Hukumu. Kwa hivyo, ubaguzi wa kimbari una thamani gani katika nukta hii? Katika siku hiyo, si mali wala idadi ya watoto wa mtu yeyote watakaokuwa na thamani yoyote.
Katika siku hiyo, kitu pekee kitakachokuwa na thamani ni nafsi iliyojisalimisha. Moyo safi wa mtu uliojisalimisha na kuwa mtumwa wa amri za Muumbaji wake. Nafsi ambayo haikuathiriwa na chochote kingine isipokuwa Yeye. Nafsi hii ina thamani kubwa bila ya kujalisha mwenye kuimilki. Na Peponi ni mahali ambapo malipo yatatolewa kwa nafsi zilizojisalimisha. Kila muumini atapewa nafasi kulingana na ikhlas (unyoofu) yake, amali, maadili na lengo lake huko. Nafasi zote zilizo huko ni kulingana na thamani hizo. Huko hakuna nafasi tofauti kwa ajili ya mbari mbalimbali.