FAQ katika kifungu cha Uislamu na Dini Nyingine

1 Ni zipi tofauti kuu kati ya Uisilamu na Ukristo wa leo?

1. Katika Ukristo, ipo imani ya utatu lakini katika Uisilamu, kuna imani ya kumpwekesha Allah.

2. Uisilamu unahusisha dini zote za mbingu na mitume; Ukristo unaikubali Biblia tu kuwa ndio kitabu cha kweli; hauikubali Quran kuwa ndio kitabu kilichotegemea ufunuo.

3. Ukristo unadai kuwa binadamu ni mwenye dhambi ya kuzaliwa nayo na kwa ajili hiyo, lazima abatizwe ili atakaswe; Uisilamu unaeleza kuwa watu wote wanazaliwa wakiwa hawana makosa na kwamba hakuna mtu anayebeba dhambi ya mtu mwengine.

4. Katika Ukristo, mapadri na viongozi wa dini wana mamlaka ya kusamehe makosa ya watu wanapokiri; katika Uisilamu, madhambi husamehewa na Allah pekee.

5. Katika Ukristo, maneno ya Yesu yanazingatiwa kuwa ni maneno ya Mungu; katika Uisilamu, amri za kiungu zinafikishwa kupitia ufunuo na Jibril.

6. Kwa mujibu wa Wakristo, Yesu alisulubiwa. Kwa mujibu wa Uisilamu, alipaishwa mbinguni, kwa Allah.

7. Ingawa Wakristo wa leo wanadai kuwa dini yao ndio dini ya mwisho, dai hilo si halali kwa mujibu wa Uisilamu kwa sababu yafuatayo yanaelezwa katika Quran:

“Bila ya shaka Dini mbele ya Mwenyezi Mungu ni Uisilamu…” (Aal-i Imran, 3/19);

“Na anaye tafuta dini isiyo kuwa Uislamu haitakubaliwa kwake. Naye Akhera atakuwa katika wenye kukhasiri.” (Aal-i Imran, 3/85).

(tazama. Şamil Insaiklopidia ya Uisilamu, Ukristo)

2 Je Ukristo na Uyahudi ni dini za kweli kwa sasa? Au, hizo sio tena dini za kweli kutokana na mabadiliko yaliyozikumba kadiri wakati ulivyosonga mbele?

Misingi ya Dini ya Kweli na Dini Zilizo Kuu

Dini ya kweli ni sheria ya Allah na huo ni mkusanyiko mtukufu wa baadhi ya ukumu bora. Allah aliituma kama hiba kwa watu kupitia kwa mitume Wake. Sheria hiyo inamwongoza mwanadamu kwenye heri. Kadiri watu wanavyotii amri za sheria ya Allah kupitia utashi na matakwa yao, watakuwa katika njia iliyonyooka na kupata uongofu. Watapata furaha na uokovu duniani na ahera. 

Dini zimegawanyika katika sehemu tatu:

Kwanza ni dini za kweli. Ni dini zenye kutangamana na sifa za hapo juu. Ni dini zilizowekwa na Allah na kutumwa kwa  watu kupitia kwa mitume. Pia hizo huitwa dini za "kiungu au za kutoka mbinguni".

Dini zote zinazotoka mbinguni kimsingi zinalingana. Hata hivyo, kuna tofauti chache miongoni mwazo ziko katika baadhi ya ibada na kanuni za kisheria. 

Dini zote walizofikishiwa watu kupitia mitume tangu Nabii Adam mpaka Nabii Isa kimsingi zilikuwa sawa; ziliegemea katikakumwamini mungu mmoja, Allah; hata hivyo, zilibadilishwa baadaye na asili zake zikapotea. Allah alimtuma mtume wake wa mwisho na mtukufu zaidi, Nabii Muhammad (s.a.w), kuwa ni mtume wa watu wote. Alituma dini ya kweli ya mwisho na kamilifu, Uislamu, kwa watu kupitia kwa Nabii Muhammad (s.a.w). Kwa sasa, dini pekee ya kweli iliyopo na itakayoendelea kuwepo mpaka Siku ya Kiama ni dini ya Uislamu.  

Pili ni dini ambazo asili zake zmrvurugwa na kubadilishwa. Kama ilivyoelezwa hapo juu, mwanzo zilikuwa dini ya kweli isipokuwa zilibadilishwa baadaye na kupoteza sifa zake za kiungu; mathalani, Ukristo na Uyahudi. Hizo sio tena dini ya kweli kwa sababu baadhi ya kanuni zake zimebadilshwa.

Tatu ni dini potovu. Hizo ni dini ambazo asili zake haziuniani na dini ya kweli. Ni dini zilizobuniwa na baadhi ya mataifa. Zinaweza kuwa na baadhi ya hukumu zinazofaa isipokuwa hizo si dini za kiungu kwa upande wa asili zao; kwa hivyo, hazina sifa tukufu. Dini za mataifa yanayoabudu moto, nyota na masanamu ni mfano wa dini hizo.

3 Kama Allah angetaka, angepeleka dini moja tu; kwa nini aliachilia ziwe dini tatu tofauti?

Neno Uislamu hutumika katika ufahamu wa namna nyingi. Hata hivyo, jina mahususi la dini aliyotumwa kuileta Mtume Muhammad (s.a.w) pia ni Uislamu. Kwa hivyo, jina la dini alitumwa Mtume wetu na aliyotumwa Ibrahim ni tofauti. Dini hizi zina majina tofauti lakini mambo yake ni ya namna moja. Hata hivyo, kuna tofauti katika yaliyomo.

Mitume wote, tangu Adam mpaka Muhammad (s.a.w), waliwafikishia watu dini ya kweli. Kanuni za imani, ambazo ni misingi ya dini, mara zote zilibakia zilezile a namna moja. Hata hivyo, masuala ya kiibada na mambo ya kidunia, tunayoyaita shari’ah, na baadhi ya hukumu zilibadilika kwa kuzingatia mahitaji muhimu ya kilakipindi na watu kuanzia kwa Adam mpaka kwa Muhammad (s.a.w). Allah Mtukuka alittuma shari’ah tofauti kwa kila ummah kwa kuzingtattia mitindo ya kimaisha na matakwa ya watu wa kila enzi. Yafuatayo yameeleza katika aya ya 48 ya sura al-Maida:

“…Kila mmoja katika nyinyi tumemwekea sharia yake na njia yake...”

Mathalani, Wayahudi waliabudu katika masinagogi tu na Wakristo makanisani tu; hata hivyo, sisi, Waislamu, tunaweza kufanya ibada popote. Shahamu ya ng’ombe na kondoo iliharamishwa katika shari’ah ya Musa lakini ni halali katika dini yetu.

Suala hili limeelezwa kama ifuatavyo katika Mkusanyiko wa Risale-i Nur:

“Sheria takatifu zunabadilika kwa mujibu wa enzi mbalimbali. Kwa hakika, katika enzi moja huenda kukawa na Mitume zaidi ya mmoja, na hayo yalitokea. Kwa kuwa baada ya Muhuri wa Mitume, Shari'a yake tukufu inatosha kwa watu wote katika kila enzi, hakuna haja tena ya kuwa na Sheria tofauti. Hata hivyo, kwa mambo mengine baada ya hapo, haja ya madhehebu imebakia kwa kiasi.” (Sözler (Maneno), uk. 485)

“Mengi katika hayo yana manufaa kwa wakati fulani na kuleta madhara katika wakati mwingine, na dawa nyingi zilimfaa binadamu wakati wa utotoni na zikaacha kumponya katika wakati wa ujana. Hii ndio sababu Qur’an ilifuta baadhi ya matamko yake ya baadaye. Yaani, ilipitishwa hukumu kuwa wakati wake umekwisha na kwamba umewadia wakati wa hukumu zingine.” (İşarât-ül İ’caz (Alama za Kimiujiza), uk. 50)

Hukumu kuu ni zie zile kwa mitume wote; hazibadliki na wala hazifutwi. Mathalani, kanuni za imani ni zilezile kwa dini zote za kimbinguni, na ibada ipokatikazote hizo. Hata hivyo, kuna tofauti chache katika hukumu za upili (undani) za ibada. Kulikuwa na mabadiliko katikahukumu kama muundo na nyakati za swala na mwelekeo wa qiblah.

Kwa kuwa jina la dini ya wafuasi wa vitabu hivyo halikutajwa katika vitabu vya kiungu isipokuwa Quran na kwa kuwa majina ya Uyahudi na Ukristo yalitungwa baadaye na kwa kuwa wafuasi wa mitume hao waliitwa hivyo baadaye, tunadhani kuwa maana ya ibara “dini mbele ya Allah ni Uislamu (kujisalimisha Kwake)” katika Quran inafahamika vyema. Dini ambayo Mtume Muhammad (s.a.w) aliwafikishia watu ina amri za kipekee isipokuwa ukweli unaotiliwa mkazo katika Quran kuwa kitabu hiki pia kinathibitisha walicholeta mitume waliotangulia inaonesha kuwa walichofikisha kwa ujumla kilikuwa katika Uislamu isipokuwa, kutokana na hekima ya kiungu, muundokamilifu wa mafunzo hayo ulipatikana pindi alipotumwa Muhammad (s.a.w) kama mtume. Kisha, njia pekee ya kupata radhi za Allah ni kuamini yote aliyotuletea.

4 Ni ipi dini ya mwisho ya Mwenyezi Mungu?

Wanazuoni wa Kiislamu wanagawanya dini katika makundi makuu mawili:

1. Dini za kweli.

2. Dini potovu.

Dini zenye msingi wa kumwamini Mungu mmoja na kuwaamuru watu kumwabudu na kumtii Yeye tu zinaitwa "dini za kweli". Dini za kweli zilizotoka kwa Allah. Kwa hivyo, pia zinaitwa dini zinazotoka mbinguni. Dini ya kweli pia huitwa "dini ya upwekeshaji" kwasababu zina msingi wa kumpwekesha Allah na kumwabudu Yeye tu. 

Dini ambazo hazikuteremshwa na Allah, zilizoundwa na watu na hazina msingi wa kumwamini Mungu mmoja zinaitwa "dini potovu".

Baadhi ya dini za kweli zilipotoshwa na watu baadaye; na ushirikina na imani potovu ambazo hapo mwanzoni hazikuwepo ziliongezwa baadaye. Dini zilizokuwa za kweli hapo mwanzoni lakini baadaye zikabadilishwa zinaitwa "dini zilizogeuzwa"; mathalani, Uyahudi na Ukristo.

Dini ya kwanza kwa wanaadamu ni ya upwekeshaji iliyokuwa na msingi wa kumwamini Mungu mmoja, iliyoteremshwa kwa Adam, mtu wa kwanza na Mtume wa kwanza. Tafiti za kielimujamii zinakubali kuwa dini ya mwanzo ya wanaadamu ilikuwa ya upwekeshaji. Kwa hakika, Schmidt, mtafiti wa historia za dini mbalimbali na mwanaelimujamii, alionesha kwamba Mbilikimo, ambao ni jamii ya kale zaidi duniani, walikuwa na imani ya Mungu mmoja. Uchunguzi wa Schmidt umekanusha madai ya Durkheim kwamba Utambikaji ulikuwa dini ya mwanzo ya wanadamu na akaondosha nadharia hiyo iliyoenea huko Magharibi.

Baada ya Nabii Adam (a.s), baadhi ya watu waliacha kuamini upweke (wa Allah), wakatoka kwenye dini za kweli na kuingiza baadhi ya imani potovu kadiri wakati ulivyosonga mbele kwa kutii nafsi zao na ushawishi wa Shetani. Hivyo, dini potovu zikaibuka. Kadiri watu walivyojitenga na dini ya kweli, Mwenyezi Mungu aliwapelekea mitume wengine na dini ili wawaite kwenye imani ya upwekeshaji. Hata hivyo, baadhi ya watu walikubali wito huo na wengine waling’ang’ania imani zao potovu. Wachilia mbali kuendelea kung’ang’ania imani zao wenyewe, walijaribu kuwazuia wale waliotaka kurejea kwenye dini ya kweli na wakawakandamiza na kuwatesa. Hivyo, mara zote kumekuwa na mapambano baina ya walioamini dini ya kweli na ambao hawakuamini, katika kila karne na enzi. Mapambano haya bado yanaendelea na hayataisha mpaka Siku ya Kiama.

Dini ya Mwisho ni Uislamu.

Leo hakuna hata kimoja katika vitabu vitukufu vilivyoshushwa kabla ya Quran chenye hali yake asili. Kadiri wakati ulivyosonga mbele, uasili wake ulipotea na vikaandikwa upya na watu. Kwa hivyo, ushirikina na imani potovu vikachanganywa ndani mwake. Mathalani, ni ukweli wa kihistoria kuwa Taurati isingeweza kudumishwa na Wayahudi baada ya Nabii Musa, kwani waliishi uhamishoni kama watumwa kwa karne nyingi na walipoteza imani yao na wakaabudu sanamu; pia ni uweli wa kihistoria kuwa Taurati iliyopo sasa iliandikwa na baadhi ya wanazuoni na ikapokelewa kana kwamba ilikuwa ile  Taurati ya asili. Ni dhahiri kuwa kitabu kilichoandaliwa baada ya kupita muda huo mrefu uliovurugika hakiwezi kuwa Taurati ileile aliyoshushiwa Nabii Musa. Kwa hivyo, ina baadhi ya madai na kashfa zisizowastahiki mitume na amri zilizo kinyume na dini yenyewe. 

Zaburi aliyopelekewa Dawud ilipatwa na hali hiyo hiyo.

Ama kuhusu Injili (Biblia), Nabii Isa (Yesu) hakupokea wahyi wa kimaandishi kwasababu alipata utume alipokuwa na umri wa miaka thelathini na kazi ya utume iliisha alipofikisha umri wa miaka thelathini na tatu.  Alikwenda kijiji hadi kijiji kingine na mji mmoja hadi mwingine ili kuwaongoza watu katika kipindi kifupi sana cha miaka mitatu. Katika siku zake za mwisho, kila mara alifuatwa na watawala wa Kirumi kutokana na uchochezi wa Wayahudi. Hakuweza kupata muda au fursa ya kuandikwa Injli. Kwa hakika, Injili zilizopo leo zimeitwa kwa majina ya watu walioziandika na zinaonekana kama wasifu wenye mahubiri, mafunzo na wongozo wa Yesu kwa mitume wake. Kando ya hayo, hazikuandikwa na mitume wake, ambao walikuwa waumini wa mwanzo, bali waliosikiliza maneno ya kiungu aliyopewa Yesu kuwafikishia.

Zipo tofauti baina ya Biblia zilizopo, kwa upande wa maudhui na masimulizi. Kwa hakika, Biblia hizo zilikubaliwa na baraza la mapadri elfu moja mnamo mwaka 325 BK huko Nicaea. Baraza lilichunguza mamia ya Biblia na kukubali Biblia 4 zilizodai kuwa Yesu alikuwa katika uungu kwa muwafaka wa wajumbe 318 na wakaziharibu Biblia zingine kwa kuzichoma moto.

Kama ilvyoonekana, kanuni ya kwamba Yesu alikuwa mwana wa Mungu – Allah atukinge dhidi ya hilo – ilipokelewa na baraza lililokutana miaka mingi baada ya Yesu. Kwa hivyo, ni muhali kusema kuwa Biblia zilizopo leo ni kama Biblia za asili

5 Kwanini dini zingine zisizokuwa Uislamu hazizingatiwi kuwa ni halali?

Allah, ambaye aliwatuma mitume na dini tofauti kwa wanaadamu katika enzi mbalimbali katika historia, aliuleta Uislamu uwe dini ya mwisho na Nabii Muhammad (s.a.w) awe mtume wa mwisho. Kwa kuja Uislamu, uhalali wa dini zilizotangulia kama Uyahudi na Ukristo ulifikia tamati.

Hiyo inalingana na hali ifuatayo: sheria mpya inapotungwa, iliyotangulia inakuwa haifai. Dini na sheria ya Allah ilipoletwa, uhalali wa dini na sheria zilizotangulia za Allah umefikia tamati.

Sababu kuu zinazolazimisha dini zingine zizingatiwe kuwa si halali ni kama ifuatavyo:

1- Awali ya yote, dini zilizotangulia ziliwahutubia watu mahususi wa enzi mahususi. Kwa upande mwingine, Uislamu unawahutubia watu wote. Ujumbe wake ni wa jumla na wa wote.

2- Dini zilizotangulia ziliwahutubia watu waliokuwa hai tu katika kipindi zilipoletwa. Sifa za watu waliokuwa wakiishi katika nyakati hizo zilikuwa za kifidhuli na tabia zao zilikuwa za kishenzi. Hawakuwa na maendeleo kwa upande wa sayansi, ustaarabu, fikra na ufahamu. Njia za usafiri na mawasiliano zilikuwa duni sana. Tamaduni, imani na desturi za kila sehemu na sehemu zilitofautiana. Kubadilishana fikra na tamaduni kulikuwa dhaifu sana. 

Kwa hiyo, ikawa ni lazima kutuma mitume tofauti na dini tofauti kwenda katika sehemu tofauti. Muda ulivyosonga mbele na wanaadamu kupata maendeleo katika sayansi, fikra, utamaduni na ustaarabu, dini zilizotangulia za wenyeji zilibakia nyuma na zikashindwa kutimiza haja za watu. Kwa sababu hiyo, Mwenyezi Mungu Mtukuka aliuleta Uislamu, dini ya mwisho, kwa wanaadamu.  

Dini ya Uislamu ina rasilimali ya kuweza kumwambia kila mmoja, tokea watu wa miaka 1400 iliyopita, mpaka watu wa leo na watu wa baadaye. Kwa hiyo, uhalali wake ni wa kudumu na hautaisha mpaka Siku ya Kiama.

3- Muda ulivyozidi kusonga mbele, imani za kishirikina na potovu zilipenya na kuingia katika dini zilizotangulia. Kanuni ya kuamini u-moja wa Allah, yaani, imani ya tawhid, ilipotea. Uislamu bado unaendelea kuwepo huku ukiwa na upya wake na usafi bila ya badiliko lolote.

Kwa kuhitimisha, tunaweza kusema yafuatayo:

Dini zisizokuwa Uislamu ni kama taa za kandili zinazoangaza mtaa. Uislamu ni kama jua linaloangaza dunia nzima.

Je, kuna haja yoyote ya kuwepo taa ya mtaani linapochomoza jua?

Je, kufaa (uhalali) kwa taa ya mtaani kunaweza kuwepo pindi linapokuwepo jua?