Moja kati ya maelezo ya Badiuzzaman Said Nursi yanayohusiana na jambo hilo la kwa nini mtu anayefariki hali ya kuwa ni kafiri analazimika kukaa motoni milele ni kama ifuatavyo:
“Swali: Dhambi ya ukafiri ni ya muda mdogo lakini adhabu yake ni ya milele na isiyoisha; vipi jambo hili linaendana na uadilifu wa kiungu? Na kama mtu atalikubali hilo, vipi litaendana na hekima ya tangu? Na hata kama mtu atalikubali hilo, vipi huruma ya kiutawala iruhusu jambo hilo?
Jawabu: Kama mtu atakubali kuwa adhabu si yenye mpaka, ni wazi kuwa ukafiri uliyofanywa katika muda wenye mpaka, kwa namna sita, ni uhalifu wenye uwiano wa kutokuwa na mpaka.
Kwanza: Mtu anayefariki kafiri atabaki hivyo hata kama ataishi milele, kwa sababu ameharibu kiini cha roho yake. Na moyo wake uliyoharibika una tabia ya kutenda uhalifu usiyo na mpaka. Kwa hivyo, adhabu yake si kinyume na uadilifu.
Pili: Hata kama ukafiri unakuwa katika muda wenye mpaka, ni uhalifu usiyo na mpaka na ni kusema uongo kwa muda usiyo na mpaka; unakana ulimwengu wote, ambao unashuhudia umoja wa kiungu.
Tatu: Kwa vile ukafiri ni utovu wa shukurani kwa neema zisizo na mpaka, ni mauaji yasiyo na mpaka.
Nne: Ukafiri ni uhalifu dhidi ya asiye na mpaka; hiyo ni, ni dhati ya kiungu na sifa zake.
Tano: Dhamiri ya mwanaadamu, kwa mtazamo wa nje ni yenye mpaka, lakini kwa nguvu ya ukweli wake, mizizi ya sura yake ya ndani imesambaa na kuenea kuelekea umilele. Kwa hivyo, haina mpaka. Hata hivyo, Ukafiri unaichafua na kuishusha hadhi yake.
Sita: Japo vyenye upinzani kwa ubishi ni vyenye kupingana, vinafanana katika mambo mengi. Na kama hivyo, kwa upande mmoja, Imani huvuna matunda ya furaha ya peponi, na kwa upande mwingine, ukafiri ni wenye kutoa adhabu na maumivu ya milele. Kwa hivyo, Inaweza kuhitimishwa kuwa kama mtu atayaweka mambo haya sita pamoja, basi adhabu ile isiyo na mpaka itaendana na uhalifu usiyo na mpaka na ni uadilifu kabisa. (Angalia Nursi, İşaratü'l-İcaz)
Una maana ya kufunika, kufunika neema ambazo mtu huzipata kwa kutozifikiria, kuonesha kutoshukuru. Kwa hivyo, usiku unaitwa kafir (wenye kufunika) katika Kiarabu kwa sababu hufunika kila kitu kwa giza lake. Kama neno, ukafiri ni kinyume cha Imani; yaani, kutokuwa na imani. Kwa maana nyingine, maana yake kukanusha uwepo na umoja wa Allah, utume na mambo aliyoyaleta Hz. Muhammad kutoka kwa Allah. Mtu asiyeamini mambo ambayo ni lazima kuyaamini katika Uislamu huitwa kafir (Kafiri) kwa sababu anafunika na kuuficha ukweli. Si lazima kukanusha mambo yote ambayo ni lazima kuyaamini ili kuwa kafiri. Ni ukafiri kutoamini moja au baadhi ya mambo hayo.
Ukafiri unaweza kupatikana kupitia moyo, maneno na matendo. Mtu anayetamka jambo litakalomfanya kafiri na ikawa hakuna ulazima kulitamka, mtu anayedharau, au kuyafanyia dhihaka mambo ambayo ni lazima kuyaamini au mtu anayefanya mambo ambayo hayaendani na Imani anakuwa kafiri.
Hata hivyo, ikiwa mtu aliyetishiwa kuuliwa akisema jambo ambalo linamfanya awe kafiri hali ya kuwa moyo wake umejawa na imani ili kuokoa maisha yake hatoki katika Uislamu. (Hamdi Yazır, Hak Dini Kur'an Dili, İstanbul 1960, Vol. 1, p. 207-208; Asım Efendi Kamus Tercümesi, Vol. 2, p. 662).
Yafuatayo yameelezwa ndani ya Qur’an kama ruhusa kwa wale waliolazimishwa kuuacha Uislamu:
“Anaye mkataa Mwenyezi Mungu baada ya kuamini kwake - isipo kuwa aliye lazimishwa na hali ya kuwa moyo wake umetua juu ya Imani, lakini aliye kifungulia kifua chake kukataa - basi hao ghadhabu ya Mwenyezi Mungu ipo juu yao, na wao watapata adhabu kubwa.” (an-Nahl, 16/106)
Sababu ya aya hii kuteremshwa ni kama ifuatavyo: Katika mji wa Makka, washirikina wa kikuraishi walikuwa wakiwalazimisha maswahaba watatu, Ammar, baba yake na Sumayya mama yake radhi za Allah ziwe juu yao kuuacha Uislamu. Walimfunga Sumayya baina ya ngamia wawili, na kuwaburura ngamia kuelekea pande kinzani na kuutawanya mwili wake vipande vipande kwa sababu ya kukataa kuuacha Uislamu. Walimuua Yasir, na kumpa adhabu aina tofauti. Walikuwa ndiyo mashahidi wa kwanza katika Uislamu. Walimtupa Ammar katika kisima. Alipokaribia kufa maji, alilazimika kukubali walichokitaka washirikina. Na kama hivyo, akaokoa maisha yake. Mtu alipokwenda kwa mtume na kusema kuwa Ammar ametoka katika Uislamu, mtume wa Allah alisema, “Hapana, Ammar ni muumini kutokea kichwani mpaka miguuni. Imani imepenya katika nyama na mifupa yake. “Wakati huo huo, Ammar akawasili, akiwa analia. Hz. Mtume alifuta machozi yake na akamwambia, “Usijali! Kama wakikulazimisha tena, jifanye unakubali kwa ulimi wanachokisema. (Ibn Kathir, Tafsiru'l-Qur'ani'l Azim, Istanbul 1985, IV, 524 ff.; Elmalılı Hamdi Yazır, ibid, İstanbul 1936, IV, 3130, 3131).
Mwanaadamu ameumbwa kumjua na kumuabudu muumba wake; kwa hivyo, si kitu kizuri kwake kuhaulishwa kutoka katika kusudio lake, kuzuiliwa kuamini na kudondoka katika dimbwi la ukafiri. Anapoona ukweli unaoumiza wakati wa umauti, kaburini, na ahera, atataka arejeshwe tena duniani; hata hivyo, ombi hili litakataliwa kwa vile maisha ya dunia anapewa mtu mara moja tu.