Je, ni ukatili kuchinja wanyama?
Dear Brother / Sister,
Baadhi ya waandishi wamekubali kuwa ni ukatili kuchinja baadhi ya wanyama kwa kuwakata koo zao kwa lengo la kutekeleza wajibu wa kidini na ibada, na kwa hivyo, baadhi ya ukosoaji umeelekezwa kwenye dini ya Uislamu. Walioiweka mbele mitazamo hiyo hawakuuangalia ukweli huu: Nyama inayopatikana kutokana na kuchinja wanyama ni chanzo cha protini ya thamani ya juu ambayo kimsingi ni muhimu mno kwa watu. Hii ndio sababu, duniani kote leo hii, idadi isiyohesabika ya wanyama huchinjwa tu kwa ajili ya chakula huko machinjioni na hutumiwa kuwa ndio chanzo cha lishe..
Hakuna chanzo cha mbadala wa nyama duniani. Kwa kuzingatia hili, kupinga kuchinjwa wanyama kama chanzo cha lishe na kuzingatia hilo kuwa ni ukatili sio tu ni upuuzi bali pia halina mantiki. Tokea enzi za awali, wanaadamu wamekuwa wakipata chakula kwa njia hiyo.
Kutokuujali ukweli huo na kupinga kuchinja mnyama kwa sababu tu ni wajibu wa kidini kunaweza tu kuwa ni mtazamo wa kiitikadi. Ukatili wa kweli ni kuua watu. Lazima wajaribu kulikomesha hilo kadiri wawezavyo. Kujaribu kulinda haki za watu wanaochinjwa na dunia ya kisasa ni kuwajibika zaidi na ndio nukta mahususi kuliko kuzuia kuchinja wanyama, walioumbwa kuwa ni chanzo cha lishe kwa wanaadamu.
Maswali juu ya Uislamu
