Ahl al-Kitab (Watu wa Kitabu) inamaanisha nini?

The Answer

Dear Brother / Sister,

Wafuasi wa dini za mbinguni kama vile Uyahudi na Ukristo wanaitwa “Ahl al-Kitabu” (Watu wa Kitabu). Watu wa Kitabu wametajwa kwa wingi ndani ya Quran. Watu wa Kitabu wanazingatiwa kuwa ni “makafiri” kwa sababu hawamkubali Mtume (s.a.w.) lakini sio makafiri kwa upande wa “kumkanusha Allah.”

Quran inatoa kipaumbele kwa watu wa Kitabu kuhusiana na masuala fulani ikilinganishwa na makafiri wengine. Mathalani, inaruhusiwa kuwaoa wasichana na wanawake wa watu wa Kitabu na inaruhusiwa kula nyama ya wanyama waliowachinja. (al-Maida, 5) Kipaumbele hiki wanapewa wao kwa sababu wako karibu na imani ikilinganishwa na makafiri wengine. Quran inawahutubia ifuatavyo:

Sema: Enyi Watu wa Kitabu! Njooni kwenye neno lilio sawa baina yetu na nyinyi: Ya kwamba tusimuabudu yeyote ila Mwenyezi Mungu, wala tusimshirikishe na chochote; wala tusifanye sisi kwa sisi kuwa Waola Walezi badala ya Mwenyezi Mungu.” (Aal-i Imran, 64) Yaani, tusitambuane kuwa ni Miungu. Hebu tuzitathmini amali zetu kwa kutegemea amri ya Allah na radhi zake. Hebu na tuwe waja wa Allah. Hebu na tujijue kuwa ni waja Wake. Hebu tuheshimiane kwa kutegemea kanuni hii. (1)

Quran inaeleza kuwa Watu wa Kitabu wanawafanya wanazuoni wao na Mapadri wao kuwa ni Miungu. (at-Tawba, 31) Wakati Adiy b. Haram, aliyesilimu kutoka katika Ukristu, alisema, “Ewe Mjumbe wa Allah! Hatuwafanyi kuwa ni Miungu wetu”, Mjumbe wa Allah (s.a.w.) akasema,

“Wanaharamisha alichokihalalisha Allah na kuhalalaisha Allah alichokiharamisha. Hili linamaanisha kuwafanya Miungu wao.” (2)

Kwa kweli, sio lazima kumwita mtu “Mungu” ili kumfanya awe Mungu. (3)

Aya ifuatayo inaeleza njia ya kuifuata wakati wa kutendeana na watu wa Kitabu:

Wala msijadiliane na Watu wa Kitabu ila kwa njia iliyo nzuri kabisa, isipo kuwa wale waliodhulumu miongoni mwao. Na semeni: Tumeyaamini yaliyo teremshwa kwenu. Na Mungu wetu na Mungu wenu ni Mmoja. Na sisi ni wenye kusilimu kwake.”  (al-Ankabut, 46)

Katika aya hiyo, Watu wa Kitabu wanashughulikiwa katika makundi mawili:

1. Kundi la Wajeuri.

2. Kundi la Waadilifu.

Tunaamrisha kutendeana nao kwa njia bora kabisa. Mtazamo huu utawavutia kuja katika Uisilamu na hawatopata tabu kuukubali Uisilamu kwa sababu wakiukubali hawana haja ya kumkataa Musa (Moses) na Isa (Jesus).  Hivyo, wataifuata dini ya Mtume wa mwisho na wataokolewa na kuwa ni wafuasi wa dini iliyogeuzwa.

Quran inaeleza kuwa Wakristu wako karibu na Uisilamu kuliko Wayahudi:

Hakika utawakuta walio shadidi kuliko watu wote katika uadui kwa walio amini ni Mayahudi na Washirikina. Na utawakuta walio karibu mno kwa mapenzi ni wale wanao sema: Sisi ni Manasara. Hayo ni kwa sababu wapo miongoni mwao makasisi na wamonaki, na kwa sababu wao hawafanyi kiburi.(al-Maida, 82)

Historia inaithibitisha aya ya hapo juu. Idadi ya Wayahudi walioukubali Uisilamu ni ndogo mno. Hata hivyo, Wakristu wengi wameukubali Uisilamu kutokana na utafiti wao. Idadi ya Wakristu walioukubali Uisilamu barani Ulaya ni zaidi ya mamia kwa maelfu. Makanisa mengi yamegeuzwa kuwa misikiti barani Ulaya na yanahudumia kuwa ni vituo vya Kiisilamu kwa sasa.

Matunda mema ya shughuli za Kiisilamu katika nchi za Kikristu ni ukweli; hata hivyo, ni ukweli pia kuwa wakuu wa nchi hizo wana msimamo dhidi ya Uisilamu.

Allah Mtukufu, anaetuamuru tutendeane na kundi adili la Watu wa kitabu kwa njia bora kabisa, anaeleza yafuatayo kuhusu kundi katili:

Piganeni na wasio muamini Mwenyezi Mungu wala Siku ya Mwisho, wala hawaharimishi alivyo harimisha Mwenyezi Mungu na Mtume, wala hawashiki Dini ya Haki, miongoni mwa walio pewa Kitabu, mpaka watoe kodi kwa khiari yao, hali wamet’ii.” (at-Tawba, 29)

Suala la kuwa ima sifa zilizotajwa katika aya hiyo “zinahusisha Watu wa Kitabu wote au hapana?ni kitu cha kujadiliwa. (4) Haipaswi kupuuzwa kuwa aya hiyo haisemi kuwa, “piganeni na Watu wa Kitabu wote mpaka walipe Jizyah (Kodi)” lakini inasema, “piganeni na wale miongoni mwa Watu wa Kitabu wenye sifa hizi na zile.” (5) Matendo ya Mjumbe wa Allah (s.a.w.) yalikuwa kama hivyo. Wakati wa zama za Makkah za Uisilamu, Mtume (s.a.w.) aliwatuma baadhi ya Waisilamu kwenda Ethiopia, ambayo ilikuwa ni nchi ya Kikristu, na kusema kuwa watakuwa salama wakiwa huko. Wakati wa zama za Madinah, Mtume aliingia katika mazungumzo na Wayahudi na Wakristu, akiwataarifu kuhusu dini ya Uisilamu na kujaribu kuwashawishi. Baadhi ya Watu wa Kitabu waliukubali Uisilamu kutokana na matendo haya.

Kama inavyoelezwa katika Quran, “Wote hao (watu wa Kitabu) si sawa sawa,” (Aal-i Imran, 113). Ni kinyume na Quran na ukweli wa kihistoria kuwazingatia wote kuwa ni sawasawa katika kundi moja.
 
Aya ifuatayo haizuii kutoingia katika mazungumzo na wao na kuwa na mahusiano ya kibinadamu pamoja nao. “Enyi mlio amini! Msiwafanye Mayahudi na Wakristo kuwa ni marafiki. Wao ni marafiki wao kwa wao. Na miongoni mwenu mwenye kufanya urafiki nao, basi huyo ni katika wao. Hakika Mwenyezi Mungu hawaongoi watu wenye kudhulumu.”  (al-Maida, 51) Kwa kweli, kuwaoa wasichana na wanawake wa Watu wa Kitabu kumeruhusiwa na Quran. (al-Maida, 5)

Hamdi Yazir anaeleza yafuatayo kuhusiana na aya iliyotajwa-hapo-juu: Waumini hawakatazwi kuwafanyia hisani Wayahudi na Wakristu, kuwafanya marafiki na kuwapa usimamizi; wanakatazwa kuwafanya ni marafiki zao wa ndani na wasaidizi wa uovu kwa sababu hawawezi kuwa ni marafiki wa kweli wa waumini. (6)

Inawezekana kufupisha suala hili kama ifuatavyo: Ni jambo la kuwa na mahusiano ya kiutu pamoja nao na ni jambo jengine kuishangaa dini yao, desturi zao na mila; yaliyopita hayakatazwi na Quran lakini ya baadaye ndio yanayokatazwa.

Marejeo:

1. Yazır, II, 1132
2. Razi, XVI, 37
3. Yazır, IV, 2512
4. Riza, X, 333; Qutub, III, 1631-1634
5. Ateş, III, 1133-1134
6. Baydawi, II, 211

Maswali juu ya Uislamu

Author:
Maswali juu ya Uislamu
Subject Categories:
Read 806 times
In order to make a comment, please login or register
MASWALI YENYE KUFANANA