Amantu ina maana gani? Ni zipi nguzo za Imani zilizo katika Amantu?

The Answer

Dear Brother / Sister,

Amantu ni neno lenye kueleza nguzo za Imani za dini ya uislamu kwa ujumla. Amantu, ambalo lipo katika muundo wa mzungumzaji mmoja wa kitenzi amana lenye maana “Nimeamini”, limetumika sehemu tatu katika Qur’an Allah alipokuwa anaielezea Imani. (Angalia Yunus, 190; Yasin, 36-25; ash-Shura, 42/15)

Katika Surat ash-Shura, Hz. Mtume (s.a.w) anaamrishwa moja kwa moja kusema “amantu”. Kwa kuegemea haya, yawezekana kusema amantu ni neno ambalo lipo katika Qur’an.

Amantu imekusanya nguzo za Imani ambazo kila muislamu anapaswa kuziamini, na kuzikubali.

Kuna nguzo 6 za Imani katika Amantu; ni kama zifuatazo:

  1. Kumwamini Allah,
  2. Kuwaamini Malaika wake,
  3. Kuamini vitabu vyake,
  4. Kuwaamini mitume wake,
  5. Kuamini siku ya hukumu (Maisha baada ya kufa),
  6. Kuamini kadari, kwamba kheri na shari ni kutoka kwa Allah.

Amantu inasomwa kama ifuatavyo:

Amantu billahi wa malaikatihi wa kutubihi wa rusulihi wal-yawmil-akhiri wa bil-qadari khayrihi wa sharrihi minallahi taala wal-ba’thu ba’dal-mawti haqqun ashhadu an la ilaha illallah wa ashhadu anna Muhammadan abduhu wa rasuluh.

Maana yake ni kama ifuatavyo:

Amantu billahi: Nimeamini katika kuwepo na umoja wa Allah, kwamba hana washirika, kwamba ana aina zote za sifa njema na ametakasika na aina zote za upungufu.

Wa malaikatihi: Na pia nimeamini malaika wa Allah.

Wa kutubihi: Na pia nimeamini vitabu vya Allah.

Wa rusulihi: Na pia nimeamini mitume wa Allah.

Wal-yawmil-akhiri: Na pia nimeamini siku ya hukumu.

Wa bil-qadari khayrihi wa sharrihi minallahi taala: Na pia nimeamini kadari, kwamba kila lionekalo baya au zuri kwetu hutokea kwa elimu, sharia, na uumbaji wa Allah.

Wal-ba’thu ba’dal-mawti haqqun: Na pia nimeamini kwa moyo maisha baada kifo (na kufufuliwa). Vyote ni kweli na sahihi.

Ashhadu an la ilaha illallah wa ashhadu anna Muhammadan abduhu wa rasuluh: Nashuhudia ya kuwa hakuna Mola ila Allah na nashuhudia kuwa Hazrat Muhammad ni mja na mjumbe wake..

Sentensi ya mwisho inaitwa neno la shahada, yaani, sentensi ya kushuhudia.

Maswali juu ya Uislamu

Author:
Maswali juu ya Uislamu
Subject Categories:
Read 1.474 times
In order to make a comment, please login or register
MASWALI YENYE KUFANANA