Je, haja ya kuamini ipo katika maumbile?

The Answer

Dear Brother / Sister,

Katika kazi yake inayoitwa "the Sense of Religion and the Child Psychology", mwanasaikolojia wa kiswizi Pierre Bovet anaandika kuwa watoto wote katika umri maalumu huwa na dini ya asili ambayo ni maalumu kwao, kwa lugha nyingine, dini, ambayo ipo katika asili yao ya ndani. Katika kujiunda kwa Imani hizi, dhamira za watu binafsi, ufahamu, na mawazo huchukua nafasi na hata jamii yenyewe. Mtoto mwenyewe huchagua dhana za kidini ambazo huzipata kutoka katika jamii. Na bado baada ya muda, anaona tofauti kati yake na jamii, na anatwaa njia mpya. Kama mtume wetu (s.a.w) alivyosema, “Watoto wote wamezaliwa katika asili ya Uislamu; baada ya hapo wazazi wao humfanya atwae dini hii au ile.”

Wanasayansi na wataalamu wengi wamefanya utafiti kuhusu dini ya asili ya watoto. Mmoja kati yao ni mwanafalsafa wa kimarekani William James. Ili kupata hisia za kidini za asili kutoka kwa mtoto bila ya kuingiliwa na kitu chochote, alichunguza kumbukumbu na tabia za mtoto kiziwi na mjinga aliyekuwa akiitwa Ballard, ambaye hadi kufikia umri wa miaka kumi na moja, hakupokea maelekezo ya aina yoyote. Mtoto ambaye alipata elimu nzuri baadaye, alifupisha mawazo yake ya metafizikia kabla ya kupata elimu na hisia zake kama ifuatavyo:

“Tulikuwa tukienda kutembea na Baba. Mandhari ilikuwa ikinipendeza. Sikuwa na uwezo wa kuongea wala sikuwa na weledi wa kuandika. Nilikuwa nikijiuliza: “Dunia imekujaje kuwepo?”, “Vipi mwanaadamu alianza kuishi?”, “Vipi mimea na viumbe vingine vimekuja kuwepo?”, “Nini kinasababisha dunia, jua, na mwezi viwepo?”, ”Vipi ulimwengu wa viumbe umekuwepo?”, Nani anayenifanya mimi nivifikirie vitu vyote hivi? Vipi mwanaadamu wa kwanza, mnyama, mmea bila ya mbegu umekuja katika uwepo? Tunatokea wapi na tunaelekea wapi?”, Vipi ulikuwa mwanzo wa ulimwengu? Mimi hasa sikuwa na uwezo wa kupata majibu ya maswali haya. Nilikuwa nayafikiria tena kisha nakata tamaa, na baada ya muda narejea tena kwenye jambo hili hilo la kufikiria.” (See. Pierre Bovet, the Sense of Religion and the Child Psychology, p: 71-72).

Wanasaikolojia wengi wengine walifanya utafiti kuhusu suala hili na takriban walipata matokeo yenye kufanana. Na kama hivyo, ni wazi kuwa watoto wamekuwa wakielekeza umakini wao kutazama ulimwengu na asili tokea umri mdogo na kuuliza maswali ambayo mfano wake ni hayo tuliyoyaweka juu. Hii ni asili ya mwanaadamu. Kama inavyoonekana haya maswali si wataalamu na wanafalsafa tu bali hata watoto, vijana, na watu wazima huwafanya kufikiria.

Qur’an tukufu inaelezea vizuri kabisa hadithi ya mtume Ibrahim (a.s), ni namna gani kama mtoto alivyoelekeza umakini wake kwa asili na ulimwengu ili kumtambua muumba wake kwenye nyota, mwezi, na kwenye jua, na baadaye kuchukua mbawa “na kwenda juu zaidi.” (gerçeğe doğru c.3, zafer yayınları)

Maswali juu ya Uislamu

Author:
Maswali juu ya Uislamu
Subject Categories:
Read 35 times
In order to make a comment, please login or register
MASWALI YENYE KUFANANA