Je, Imani ina faida kwa afya? Je, kuna tafiti zozote za kisayansi kuhusu hilo?
Submitted by on Thu, 28/02/2019 - 10:59
Dear Brother / Sister,
Imani hupelekea mwanaadamu kuyapenda maisha na humpa hisia za kushikamana na maisha. Mtu mwenye Imani huwa na mtazamo mzuri kuhusu maisha na uwepo; huona kuwa maisha ni neema ya Allah na huona mazingira yake ya kijamii na kiasili kuwa ni kazi za sanaa na yeye mwenyewe akiwa ni sehemu kati yake. Hivyo, huona kuwa ni jukumu lake kuendelea na maisha yake mpaka jukumu lake litakapo maliza na hupambana kuishi.
Moja kati ya misingi muhimu ya kiroho ambayo inadhibiti maisha katika jamii ya Kiislamu ni Imani. Amri na makatazo ya Allah yanazingatiwa na waumini.
Kwa kuongezea, Imani humpa mtu hisia za juu za kuridhika na humwezesha kuanzisha uhusiano na vitu vya duniani. Hisia za kuridhika kwa mtu zilizosababishwa na Imani humfanya aridhike na vitu vidogo na kuwa na furaha pale mahitaji yake yanapokamilika hata kwa daraja ya chini au ya wastani. Na kama hivyo, humzuia mtu kutokana na kuanguka katika taabu na shida.
Kuna vitabu viwili vya msingi juu ya faida za imani kwa afya. Cha kwanza ni “Kitabu cha dini na afya”; ni kitabu chenye kurasa 712 kilichokusanya kazi zilizoteuliwa kutokana na tafiti ambazo zinatafuta uhusiano wa matendo ya dini na afya. Kingine ni “Mungu, Imani, na Afya”, kilichoandikwa na Dr. Jeff Levin, ambaye ni mmoja kati ya wataalamu wakubwa wanaosema kuwa makundi yenye Imani yapo katika hali nzuri kuliko mengine kiupande wa maradhi na kifo.
Dr. Levin anatilia mkazo hilo katika utafiti wake: Wafuasi wa makundi ya kidini ambao hujizuia na baadhi ya matendo na ambao huunga mkono maisha ya kiafya wana hatari ndogo ya kupata mshtuko wa moyo, shinikizo la damu na kansa. Wana maisha mazuri zaidi na marefu. Dini zinazozuia unywaji wa pombe na kuvuta sigara, zinazolazimisha milo midogo na zisizoruhusu kujamiiana nje ya ndoa zina fursa nzuri zaidi kuhusu jambo hilo. Faida hizi haziwezi kupatikana bila ya kuhudhuria sehemu za ibada na kutekeleza baadhi ya matendo ya kimwili kama ibada.
Dr. Levin anarudia kwamba maradhi ya aina tatu – moyo, kansa, shinikizo la damu – yajulikanayo kama ‘Wauaji wa Amerika ya kaskazini’ yanadhihiri kwa uchache kwa watu wa dini ukilinganisha na wasiyo na dini. Kwa mfano, anasema wanawake waliyoolewa na wanaume waliyotahiriwa ni wachache huugua kansa ya kizazi ukilinganisha na wengine. Vivyo hivyo, idadi ya wale wanaougua kansa ya kizazi kati ya Wahindus wasiyotahiriwa ni kubwa mno kuliko ya Waislamu wa kihindi, ambao takribani hawaugui maradhi haya.
Vivyo hivyo, waumini wenye subira, ambao si wenye haraka au fujo, wasiyokunywa pombe na ambao huenda sehemu za ibada mara kwa mara hufariki kwa shinikizo la damu kwa asilimia 40 chini ukilinganisha na wengine.
Hata hivyo, tunajua kuwa lengo kuu la Imani na ibada ni kuonesha uaminifu wetu kwa Mola wetu, aliyetuumba. Tafiti hizi zinatuonesha kwamba Mola wetu hatupi malipo yake hapa duniani kwa muundo wa hamasa na amani moyoni mwetu tu bali pia huboresha afya zetu.
Habari iliyotolewa na Associated Press mnamo tarehe 24 August 2007 ni yenye kuvutia. Shirika hilo la habari lilitangaza taathira chanya ya maadili ya kidini kwa vijana kwa kusema, ”Imani ni ufunguo wa furaha kwa watoto wengi.”
Kwa mujibu wa maelezo yaliyotolewa katika habari hiyo, matokeo ya utafiti huo yameonesha kuwa vijana wenye dini wana furaha zaidi kuliko wasiyo na dini. Utafiti wa kina uliyofanywa na Associated Press na MTV umeonesha kuwa kati ya vijana wenye umri kati ya 13 na 24, ambao hujitazama kuwa ni watu wa dini wana furaha zaidi kuliko wasiyo na dini. Asilimia 44 ya vijana wamesema kuwa dini na mambo ya kiroho ni muhimu kwao na asilimia 21 kati yao wamesema wameona kuwa dini ni muhimu. Kati ya jamii tofauti walioshiriki katika utafiti, Wamarekani wa Kiafrika wamesema dini ni kipengele muhimu kwao. Kati ya wale waliyosema dini ni muhimu sana kwenye maisha yao, asilimia 80 wamejieleza kuwa ni wenye furaha.
Wanasayansi ya jamii wanaelekeza umuhimu katika ukweli kuwa kuna uhusiano wa moja kwa moja baina ya furaha na kutekeleza wajibu wa kidini. Profesa wa sayansi ya jamii Lisa Pearce kutoka chuo cha South Carolina anasema, “Dini ina mchango mkubwa katika furaha”.
Amesema asilimia 68% ya vijana wamesema kuwa wametekeleza dini zao na imani zao kwa mujibu wa utafiti waliyoufanya. Asilimia 75 ya vijana waliyoshiriki katika utafiti huo wamesema Allah ana taathira katika furaha yao.
Maswali juu ya Uislamu