Jihad inamaanisha nini? Ni zipi Aina za Jihad?

The Answer

Dear Brother / Sister,

Jihad ni jina linaloitiwa kila shughuli na harakati katika njia ya Allah (SWT). Linamaanisha kutoa bidii ili kuinyanyua haki na kuifanya itawale. Kwa maneno mengine, jihad ni kufanya kwa vitendo katika Uisilamu; ni nguvu ya Uisilamu ili kutenda.

Neno jihad mara nyingi linafasiriwa kuwa ni “vita vitakatifu” kwa lugha za Magharibi. (1) Ufasiri huo unatokana na juhudi ili kuonesha kuwa Uisilamu ni dini inayoenea kwa mabavu ya silaha.

Hata hivyo, maana ya neno “jihad” sio “vita.” Kupigana kwa ajili ya Allah (SWT) pia ni namna ya jihad lakini, kwa maana jumla, neno hili linahusisha mchakato wowote na kitendo ili kuifanya dini ya Allah ienee kila pahala.

1- Abu’l Ala Mawdudi, Jihad katika Uisilamu, Machapisho ya Kiisilamu LTD, Lahor, uk.1; Rudolph Peters, İslam ve Sömürgecilik (Uisilamu na Ukoloni), Kilichofasiriwa na Süleyman Gündüz, Nehir Pub. ist.1989, uk.29; M.J. Kister, "Mali ya Ardhi na Jihad" , Jarida la Kiuchumi na Historia ya Kijamii ya Mashariki, Leiden, 1991, XXXIV, 276; W. Montgomery Watt, Nadharia ya Siasa ya Kiisilamu, Edinburgh, p. 14; Ahmet Özel, İslam Hukukunda Milletlerarası Münasebetler ve Ülke Kavramı (Mahusiano ya Kimataifa Katika Sheria ya Kiisilamu na Dhana ya Nchi), Marifet Pub. Ist. Uk. 64

Aina za Jihad

1. Jihad dhidi ya Ujinga: Jihad hii inamaanisha kuwafundisha watu ukweli na mambo mazuri. Allah Mtukufu anamhutubia Mtume wake katika Quran kama ifuatavyo:

“Waite waelekee kwenye Njia ya Mola wako Mlezi kwa hikima na mawaidha mema, na ujadiliane nao kwa namna iliyo bora.” (an-Nahl, 125)

Yafuatayo yanaelezwa katika aya nyengine:

“Na uwe kutokana na nyinyi umma unao lingania kheri na unao amrisha mema na unakataza maovu. Na hao ndio walio fanikiwa.”  (Aal-i Imran, 104)

Quran ni dawa ya roho inayotosha kutibu kiyakinifu na kiroho, na majeraha ya mtu mmoja mmoja na ya kijamii sio tu kwa taifa fulani mahususi bali watu wote hadi Siku ya Kiama. Wajibu wa kuwasilisha dawa hii kwa watu wamepewa Waisilamu.

2. Jihad dhidi ya Nafsi ya Mtu: Waumini wanaonywa dhidi ya njama za nafsi katika aya kama ifuatavyo: “… wala usifuate matamanio yakakupoteza kwenye Njia ya Mwenyezi Mungu.” (Sad, 26)

Mtume (s.a.w.) ameeleza yafuatayo “jihadi kubwa zaidi ni ile dhidi ya nafsi yako.” Pia amesema, “Adui mkubwa ni nafsi yako, ambayo imo ndani mwako.” (Ajluni, Kashfu’l-Khafa, Beirut, I, 143, Hadith Nambari: 413)

Mtume amevutia umakini juu ya umuhimu wa jihad hii. Kwa hakika, wakati wa kuridi mapiganoni, Mtume (s.a.w.) alisema, “Tumerudi kutoka jihad ndogo kuja kwenye jihad kubwa kabisa.” (Kanzu’l-Ummal, IV, 430, Hadith Nambari: 11260 ) Hivyo, alielezea kwa kifupi kuwa mtu kuishinda nafsi yake lilikuwa ni suala zito zaidi na muhimu zaidi kuliko kupigana na adui.

3. Jihad dhidi ya Shetani: Aya ifuatayo katika Quran inaonesha kuwa Shetani ni adui mkubwa kabisa kwa mwanadamu. “Hakika Shet’ani ni adui yenu, basi mfanyeni kuwa ni adui.” .”(Fatir, 6 ) Hivyo, umakini unavutwa kwenye ukweli kuwa jihad kubwa zaidi ni ile inayofanywa dhidi ya adui mkubwa zaidi.

4. Jihad ya Silaha: Jihad hii sio yenye kuendelea. Sio faradhi kwa kila mtu. Kama dola lina nguvu ya kutosha, jihad ni fard al-kifayah (fardhi ya kujitosheleza); yaani, kundi la watu fulani linaposimamisha jihad, watu wengine hawabebeshwi jukumu.

Maswali juu ya Uislamu

Author:
Maswali juu ya Uislamu
Subject Categories:
Read 1.608 times
In order to make a comment, please login or register
MASWALI YENYE KUFANANA