Katika Uislamu, mzinifu huadhibiwa kwa kupigwa mawe na mwizi huadhibiwa kwa kukatwa mkono. Jee amri hizi hazizingatiwi kama za kikatili kwa zama za sasa. Ni lipi jibu lako kwa jambo hili?
Dear Brother / Sister,
- Tunachotakiwa kufanya kama Waislamu ni kujisalimisha na kutii maamrisho ya Allah na mtume wake.
- Inajulikana kwamba katika mfumo wa sasa wa sheria, uzinifu si kosa la uhaini. Inawezekana kwa mtu mwenye akili ambae ana fikra ya heshima, ima ni muumini au si muumini, akachukulia kwamba zinaa si uhaini likifanywa kwa ndugu zake?
- Ni lazima tuielezee vizuri kwamba amri kama za kupiga mawe katika Uislamu ni adhabu kali sana. Moja katika malengo ya ubinadamu na dini zote za mbinguni ni kuhakikisha kuendelea kwa kizazi. Uzinifu ni ukatili na njia haramu ya kuzalisha na kuchanganya vizazi kwa vigezo tofauti halali vya kibinadamu. Uzinifu ni kosa kubwa sana na ni njia ya kuvutia kufanya uhaini kwa roho mbaya. Hatutegemei uislam,, ambao ndio dini ya ulimwengu,kutokuchukua tahadhari kuzuia uhaini wa kikatili wa aina hiyo.
- Kwenye hatua hizi za kinga, inasisitizwa kwamba mashuhuda wanne ni muhimu kugundua jinai ya uzinifu ingawa ni kama vile haiwezekani kwa watu wanne kuwaona watu wawili wakifanya zinaa. Zaidi ya hapo, ikiwa mtu ambae amesema amewaona watu wawili wakizini na haikuthibitishwa na watu watatu zaidi, anapigwa viboko themanini. Inamaanisha asiwepo yoyote atakaezungumzia jambo hilo.
Kwakweli, takriban matukio yote ya kupiga mawe yaliyotokea kipindi cha Mtume yalitekelezwa baada ya wakosaji kukiri wenyewe ili wajivue makosa. Na kwakweli, Mtume (rehma na Amani ziwe juu yake) alijifanya kama hawasikii waliokuja kujishtaki ili awalinde wasipigwe mawe; alijaribu njia zote kama vile kuwachunguza kama anaejishtaki ana akili timamu au laa, ima ilikuwa ni uzinifu halisi au zile tu hatua za mwanzo, n.k; ingawa, alipaswa kutekeleza adhabu mara tu walipojitambulisha.
- Amri ya Qur’an inayohusiana na kumkata mwizi mkono ni, kwa kusema ukweli, ni amri ya zama za sasa kwasababu zamani hakujawahi kuwa na wezi wengi, majambazi, wabakaji, wakabaji n.k Kila mtu isipokua wezi, anakubali kwamba adhabu ovyo ovyo kwa wezi haziwezi kuzia kabisa.
- Idadi ya kesi za kukatwa mkono katika karne tatu za kwanza katika historia ya Uislamu, wakati sheria hii inatekelezwa kwa haki, zilikuwa sita tu. (Ismail al-Fahrani, “ash-Shariatu bayna’s-salihin wa’l-Murjifin” al-Ahram, 17 Januari, 2011)
Baada ya muda, katika kila mji duniani, angalau kichwa kimoja au zaidi, sio mikono, hukatwa, wamiliki wa mali huuliwa kinyama kwa sababu ya fedha au bidhaa ambazo huibwa kupitia jinai hizi. Zama hizi zinahitaji zaidi kuliko zama zingine ili kuzuia uhaini huu kupitia kupambana na kitendo hiki.
- Ni muhimu kusikiliza maneno yafuatayo ya Badiuzzaman Said Nursi:
“Wakati fulani jangwani, mtu alikuwa mgeni wa mhamiaji ambae alikuwa mmoja katika watu wanaopenda uhalisia. Aligundua kuwa wakazi wa jangwani hawakuchukua tahadhari kulinda mali zao. Mwenyeji wake alikuwa kaacha pesa wazi wazi kwenye kipembe cha nyumba.
Mgeni akamuuliza, “Hivi huogopi wezi, kiasi kwamba umetupa tu vitu vyako kwenye kipembe kama hivyo?”
Mwenyeji wake alijibu, “Hakuna wezi hapa.”
Mgeni akasema, “Sisi tunaweka fedha zetu kwenye masunduku na kuyafunga ,lakini bado mara kwa mara zinaibwa.
Mwenyeji akamuambia, “Sisi tunakata mikono ya wanaoiba kama amri ya Mungu na tunatenda haki kwa mujibu wa shari’a.”
Palepale mgeni akaeleza kwa mshangao, “Kwahiyo si wengi kati yenu watakosa mkono!”
Mwenyeji wake akamuambia: “Nina miaka hamsini sasa, na katika maisha yangu yote nimemuona mtu mmoja tu.”
Kwakufupisha: Wakati adhabu zinapotekelezwa kwa namna ya kutekeleza maagizo ya Mungu na haki za kidominika (dominical justice), kwa pamoja kiroho, na kiakili, na kimaadili, na uwezo wa akili kindani wa mwanadamu zinaathiriwa na kushawishiwa. Ni kwa sababu hii kwamba utekelezaji wa adhabu mara moja ndani ya miaka hamsini kumekua na athari kubwa kuliko kuwafunga watu kila siku…” (Badiuzzaman Said Nursi, Hutbe-i Şâmiye (Damascus Sermon), Envar, uk. 75-78)
Maswali juu ya Uislamu
