Kufunga swaumu kuna hekima gani na manufaa gani?

The Answer

Dear Brother / Sister,

Maarisho ya Allah na makatazo kwa hakika ni kwa ajili ya manufaa ya watu. Wanazuoni wa Kiislamu wamekubaliana kwamba amri zote hizi zinalenga kuwanufaisha watu. Ni ukweli usiopingika kwamba yapo manufaa makubwa kwa watu katika mambo ambayo Allah anatutaka tuyafanye na kuna madhara katika mambo Anayokataza. Kutokana na wito uliotolewa na mafundisho ya Kiislamu, wanazuoni wa Kiislamu mara zote wamekuwa wakifikiria mno manufaa na hekima ya njia mbalimbali za kuabudu na wamejaribu kuwaeleza njia za utekelezaji ili kuwasaidia watu kuzitakasa nafsi zao na kuzitukuza badala ya manufaa binafsi katika kuzitekeleza. Katika swala hili, faida na hekima ya kuabudu ambayo wanawajibishwa ziko wazi, pia ni kweli kwamba sio manufaa yote na malengo yanayopaswa kueleweka ni yakinifu.

Lengo kuu la kufunga swaumu ni kuwafanya watu wafikie uchamungu. Hili limeelezwa wazi katika Qur’an:

“Enyi mlio amini! Mmeandikiwa Saumu, kama waliyo andikiwa walio kuwa kabla yenu ili mpate kuchamngu.” (Qur’an, al-Baqarah, 2:183)

Kufunga swaumu, kunakowaongoza watu kwenye hatua ya elimu ya kiroho, kunawafanya watu waondokane na masimbi ya madhambi yaliyomo nyoyoni mwao na nafsini mwao kwa muda mfupi. Kufunga swaumu, kwa hivyo, kunawafanya wafikie siri ya aya “Hakika amefanikiwa aliye itakasa” (Qur’an, ash-Shams, 91:9). Haya ni maelezo ya ukweli kwamba wale wanaozitakasa nafsi zao ndio watakaopata uwokovu. Kama vile kutoa zaka kunavyosafisha madhambi na kusababisha kukua kwa usafi na unyoofu (Qur’an, at-Taubah, 9:103), hivyo pia ndivyo ilivyo swaumu, ambayo ni zaka ya kiwiliwili, kuwaokoa watu kutokana na kutawaliwa na nafsi zao.

Mtu anayefunga swaumu huvunja msururu wa tamaa za kimwili na kuishikilia kamba ya Allah. Ilhali tamaa za kimwili zinamfanya mtu kuwa mbinafsi na kumpelekea kuwa mkiwa, mtu anakuwa makini zaidi juu ya ukweli kwamba yeye ni mwanajamii, kwa kushikilia kamba ya Allah. Wakati wa Ramadhani, mwezi wa kufunga, sala zinazosaliwa kwa jamaa zinaleta hisia ya umoja katika nafsi. Matajiri wanasali katika safu moja na masikini, wanakula kwenye meza moja; sadaka, fitrah na malipo (fidya: kwa wale wasioweza kufunga (wazee, wagonjwa na wasiojiweza, n.k.) fidia lazima itolewe kwa kumlisha masikini kwa kila siku ambayo mtu hafungi) ni kama maji ya maisha ili kuboresha uenezaji wa pato lisilo na uwiano.

Kufunga kunaifanya tamaa ya nafsi iwe nyoofu kutokana na uumbwaji wake kwa upande mmoja, kujizuia kwa khiyari kutokana na matamanio ya nafsi na kujifunza subira kutokana na kuwafanya watu wavumilie njaa na kiu kwa upande mwingine. Kuwa na maisha ya mafanikio, mtu anahitaji kuelekea kwenye unyoofu wa tamaa za nafsi. Watu wenye imani dhaifu hawawezi kufanikiwa maishani; wanaweza pia kumalizikia vibaya kwa upande wa kiroho. Kwa sababu njia za kuabudu zina hali na namna ambazo wale tu wenye imani thabiti wanaweza kuzitekeleza. Katika nukta hii, kufunga kunafaa sana katika kuyadhibiti matamanio ya nafsi na kuitukuza nafsi kwa upande wa kuitakasa na utiifu. Vivyo hivyo, mazingatio ya swaumu kuwa ni namna ya kujinyima anasa za kimwili na taabu kwa dini mbalimbali na tamaduni licha ya kuwepo miundo tofauti yenye manufaa kwa upande wa kueleza ukweli huu.

Shukurani kwa swaumu, hali ya kukinai inaingia tena katika majumba yetu. Mtu anayevumilia njaa na kiu kutokana na swaumu anafahamu watu wenye haja na umuhimu wa mtu kukinai alichonacho. Hawezi kamwe kukifuja. Maelezo ya Mjumbe wa Allah “Mtu kukinai alichonacho ni hazina isiyo na ukomo” (Bayhaqi, Zuhd, 2:88) yanagonga katika masikio ya waumini. Kufahamu umuhimu wa chakula, mtu anakuwa ni mwenye shukurani zaidi kwa Mungu. Anafahamu lengo linalosababisha kunyimwa na kukinai kunapelekea rehema. Dalili ya dunia ya Mjumbe wa Allah “wale wanaotumia kwa busara hawatopata shida kutimiza malengo” (Ibn Abi Shayba, al- Musannaf, 5:331) kuonekana wazi wazi katika maisha yake.

Swaumu inamwezesha mtu kuwa na nidhamu katika maisha  yake pamoja na iftar (futari wakati wa mwezi wa Ramadhani) na sahur (daku) na tarawih sala na namna nyenginezo za ibada.

Ramadhani, mwezi wa swaumu, umejaa fursa na hazina mbalimbali kwa binaadamu ili arejee kwa Mola wake Mlezi na kumwomba msamaha wa madhambi yake. Mtu ana fursa ya kuzingatia mengi zaidi kwenye Qur’an. Kutokana na wingi huo kwamba Ramadhani inaleta na inaondosha utando wa madhambi kwenye moyo na ubongo, binaadamu anaanza kufahamu baadhi ya aya kwa kina.

Kama ni sadaka ya mwili, swaumu inachangia pakubwa kwenye hali ya ujengaji na uvunjaji wa kemikali mwilini kwa kuondosha sumu zilizomo mwilini. Katika mwezi huu, binaadamu anapoanza kuuzingatia mwili wake kuwa ni wa kimaajabu na mshikamano wenye mpangilio mzuri wa maada na kumaanisha kwamba uko tofauti na viumbe wengine, miili hurudia upya na ubongo huchangamka… miili yetu inakuwa na afya kama inavyohakikisha maneno ya Mjumbe wa Mungu “Fungeni mtapata afya”. (Tabarani, Mu’jamu’l-Awsat, VIII: 174; Mundhiri, at-Targhib, 2:206)

Kufunga swaumu ya Ramadhani ni wakati ambao watu hujisikia kuwa na matumaini ya msamaha. Swaumu ni mwalimu anayewafundisha watu namna ya kuwa imara dhidi ya matatizo ya ghafla. Ramadhani ni mwezi unaotoa nafasi kwa watoto wetu kujifunza na kutekeleza dini kwa msisimko…

Mjumbe wa Allah amesema madhambi ya wale wanaoitarajia Ramadhani kwa kuamini na kumtumainia Allah basi watasamehewa makosa yao. (Nasai, Imani, 21). Kwa namna hiyo hiyo, Mtume amesema na huku akimtaja Sahaba wake Mtukufu Ka’b b, Ujra: “Ewe Ka’b! Sala ni ushahidi unaothibitisha kuwa mtu ni Mwislamu. Swaumu ni ngao madhubuti. Kutoa sadaka kunayasafisha madhambi kama maji yanavyouzima moto. Ewe Ka’b! Nyama na mifupa  inayoundika kwa kulishwa na vitu vya haramu inastahiki kuingia motoni.” (Tirmidhi, Jum’a, 79).

Upo muunganiko imara kati ya  hekima na ufahamu wa amri za swaumu. Kuwa makini na kanuni zinazohusiana na sheria za swaumu kutatupa fursa ya kufunga swaumu kwa mujibu wa sunnah aliyotuachia Mtume kuwa ni hekima.

Maswali juu ya Uislamu

Author:
Maswali juu ya Uislamu
Subject Categories:
Read 526 times
In order to make a comment, please login or register
MASWALI YENYE KUFANANA