Kuna mantiki gani (hekima) kwa adhabu ya rajm (kupigwa mawe hadi kufa)? Kwa nini Uisilamu, ambayo ni dini ya upendo inatekeleza hukumu hiyo?

The Answer

Dear Brother / Sister,

“Mtawala ni lazima awe na hisani na huruma katika upande wake wa kulia na awe na hasira na maadilisho katika upande wake wa kushoto. Malipo ni sharti la huruma yake; na maadilisho hulazimu adhabu.”

Cheo cha mtawala hakistahiki kutowazawadia watiifu na kutowaadhibu wasiotii; yote mawili ni alama za udhaifu. Mungu Mtukufu hana kasoro kama hizo.

Tunapaswa tueleze kwa uwazi kwamba amri kama rajm ni miongoni mwa adhabu nzito za kuheshimu sheria katika Uisilamu. Moja ya malengo makuu ya binadamu na dini za mbinguni ni kuhakikisha mwendelezo wa kizazi. Uzinifu ni njia ya aibu na haramu ambayo inaharibu tabia na kuchanganyikana kwa kizazi kwa pande tofauti za kisheria na kiutu. Ni uhalifu mkubwa mno na ni utaratibu unaovutia kutenda uhalifu kwa roho. Hatuwezi kutarajia dini ya mbinguni kama ulivyo Uisilamu usiwe na mizani ya kizuizi ili kuepusha uhalifu wa fedheha namna hiyo. Kumwadhibu mhalifu sio kinyume cha kutokuwepo huruma na upendo; ni sharti la haki.

Kwa kutumia ibara “usikaribie zinaa” badala ya “usizini” kimiujiza, Quran imewakataza watu kutokaribia zinaa seuze kuifanya. Kwa kuwa, ibara “usiikaribie zinaa” ni fasaha zaidi kuliko kuliko ibara “usizini”. Kumwambia mtu “usikaribie” kuna athari zaidi kuliko kumwambia “usifanye”; ibara “usikaribie zinaa” inaelezea katazo la vitu vinavyoweza kupelekea kuzini kama vile kugusa, kubusu, kutazama na kukonyeza. Kufanya mambo yanayopelekea uzinifu kunaidhinisha uzinifu. Uzinifu ni amali mbaya na ni dhambi kubwa. Isitoshe, uzinifu ni njia mbaya mno kiasi kwamba inaondoa utando wa kivutio cha mpito, inasababisha mkanganyo wa kizazi, inapelekea kwenye amali za haramu, inakiuka haki za wengine na inaharibu vibaya safu za jumuia kwa kuiharibu familia, inaeneza vurugu, inasababisha machungu na kueneza maradhi ya ukosefu wa maadili.

Sheikhu’l-Islamu Alusi anaeleza yafuatayo kwa sababu ni kifo kwa watoto: “Kwa kuwa inafinya na kusababisha utasa wa kizazi. Mtu ambaye wazazi wake hawako kisheria ni kama mtu aliyekufa. (Alusi, Ruhu'l-Maani, Daru'l-Fikr, 8/67.) Majaribio gani na harakati zipi za watu waliokufa zinazoweza kuhusiana na masuala ya sheria ya kiisilamu?”

Baada ya kukatazwa yale yote yanayopelekea uzinifu, sheria ya Kiisilamu inaliangalia kosa la zinaa kuwa ni ukiukaji wa haki za umma na kulitolea adhabu ipasavyo; inaweka adhabu nzito na vikwazo vizito vya uzinifu ili kuwazuia watu. Kiukweli, uhalifu wa zinaa unatikisa misingi ya familia na kuitishia. Familia ndio msingi wa jumuia. Kama uhalifu wa namna hiyo unakuwa wa kiholela, utaenea katika jumuia, utasababisha kuporomoka kwa familia na kufisidika kwa jumuia na kizazi na kuporomoka kwa maadili. Hata hivyo sheria ya Kiisilamu inazingatia kutengamaa kwa jumuia kuwe juu zaidi ya kila kitu na kulipa umuhimu mkubwa suala hilo.

Kwa hivyo, sheria ya Kiisilamu inatoa adhabu kali kwa uzinifu na kukataza aina zote za uzinzi ili kuwaweka watu salama kutokana na adhari mbovu na kuilinda jumuia. Halikadhalika, sheria ya Kiisilamu haitaki waliooana ambao wanazini waishi na kuwazingatia kuwa ni mifano mibaya mno.

Wanazuoni wa Fiqh kwa pamoja wamekubaliana kwamba kapera anayezini na sio mtumwa awe mwanamme au mwanamke atalazimika kuchapwa mijeledi mia moja. Kwa kuwa, Allah anaeleza hivi: “Mzinifu mwanamke na mzinifu mwanamume, mtandikeni kila mmoja katika wao bakora mia. Wala isikushikeni huruma kwa ajili yao katika hukumu ya Mwenyezi Mungu, ikiwa nyinyi mnamuamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho. Na lishuhudie adhabu yao kundi la Waumini. (an-Nur, 24/2)

Wanazuoni wa Fiqh pia wamekubaliana kwa pamoja kwa kutoa shuhuda mbalimbali kwamba mtu aliye kwenye ndoa awe mwanamme au mwanamke kama amezini apigwe mawe mpaka afe.

Adhabu ya hadd, inayojumuisha rajm, inakuwa wazi kwenye hali mbili: kukiri (mtu aliyezini akiri kufanya zinaa) na mashahidi (4 wanaume). Mazingira ya msingi kwa adhabu hii kutolewa kwa mtu ni haya: 1. Awe na akili timamu, 2. Awe amebaleghe, 3. Awe na hiari, 4. Ajue kwamba uzinifu ni haramu.

Kama inavyoonekanwa, Uisilamu unasimama dhidi ya mtu katika kila hatua ya njia hii, unajaribu kumweka mbali na amali hii mbaya na kumnasihi aishi mazingira halali na kwenye mipaka ya kujizuia.

Hata hivyo, haijalishi ni umadhubuti gani upo kwenye mfumo husika na haijalishi sheria zilizowekwa zina uzuri gani, haitotatua sana ikiwa mtu mmoja mmoja hana dhamiri safi ya kuukubali mfumo huo na sheria hizo. Kwa hivyo, kando ya sheria nzuri na madhubuti, mtu mmoja mmoja anapaswa alelewe katika njia ya kuzitekeleza sheria hizo na zilelewe ili ziweze kuwa na dhamiri safi ili mapendekezo na ushauri usikilizwe. Quran inamchukua mtu kwenda kwenye nukta husika “Haijalishi nini unafanya wapi na lini, upo chini ya udhibiti wa Mola Mtukufu,” na kumfanya atekeleze amali zake zote katika mazingira hayo.

Maswali juu ya Uislamu

Author:
Maswali juu ya Uislamu
Subject Categories:
Read 412 times
In order to make a comment, please login or register
MASWALI YENYE KUFANANA