Kwa mujibu wa Uislamu, kwanini Mhalifu huadhibiwa? Ni lipi lengo la adhabu katika Uislamu?

The Answer

Dear Brother / Sister,

Kuna mambo mengi yamezingatiwa katika kutekeleza adhabu kwenye historia; lengo la adhabu liliwekwa kwa mujibu wa mazingatio haya. Kwenye ulimwengu wa Kimagharibi, lengo la adhabu zamani (mpaka kufikia karne ya 18) ilikuwa ni kitisho, kulipa kisasi na  kutisha kwa kuhukumu. Kuchoma moto, kusulubu, kukata viungo vya mwili, kuvunjwa mifupa, kuunguza kwa kutumia chuma moto, n.k. zilikuwa ni adhabu zilizoshuhudiwa zamani.

Mbali na hayo, kulikuwa hakuna uhusiano kati ya uhalifu na adhabu kwenye zama hizo. Kwenye sheria ya uhalifu ya Uingereza, adhabu ya kifo  ilitekelezwa kwa karibia aina 200 ya makosa ya uhalifu hadi kufikia karne ya 18. Sheria za uhalifu za Ufaransa, adhabu ya kifo iliwekwa kwa makosa ya aina 215 tofauti tofauti ya uhalifu. Uhalifu mwingi uliowekewa sheria ulikuwa ni uhalifu mdogo mdogo tu.

Katika kipindi cha muda, visasi vya mtu mmoja mmoja viliondolewa na visasi vya kijamii na Kiungu. Kwenye visasi vya kijamii, vitisho vilichukua nafasi; kwenye visasi vya Kiungu, lengo ilikuwa ni upatanisho/kusuluhisha. Tangu karne ya 18, wanazuoni wa magharibi wamepambana dhidi ya adhabu za kulipiza kisasi na wakajaribu kutafuta adhabu nyingine mbadala.

MALENGO YA ADHABU KATIKA UISLAMU

Lengo la adhabu kwenye Kanuni za Kiislamu za Uhalifu si kandamizi, wala za kutesa au kulipiza kisasi dhidi ya mwalifu. Hz. Mtume (rehma na Amani ziwe juu yake) hakutumwa kuja kuwatisha na kuwadhulumu watu; alitumwa kama rehma kwa viumbe wote.

Kwa mujibu wa kinachofahamika kwenye vyanzo vya dini (aya na hadithi) na kauli za mujtahid, malengo ya Uislamu kwenye kuadhibu wahalifu ni kama ifuatavyo:

1. Kudhibiti uhalifu kwa ujumla

Utekelezaji wa adhabu kwenye sheria za kiislamu hulenga kuwa kama mfano ili kuzuia uhalifu. Hii ina maana kwamba, Adhabu za kiislamu zina lengo la kuzuia uhalifu kabla haujafanywa na kuwazuia watu wasifanye uhalifu kwa kuwaonya.

Kwa hiyo, kwenye Uislamu, adhabu hutekelezwa mbele ya umma/muhadhara. Kutekeleza adhabu kwa uwazi mbele za watu inahusiana kwa karibu sana na saikolojia ya mwanadamu.

Lengo la adhabu kuwa kama mfano na kuzuia, hutambulika  kama njia nzuri za kuitangaza adhabu na kuitekeleza mbele za watu. Hivyo basi, hisia za watu zinazohusiana na kuchukia uhalifu na kuulaani siku zote huwekewa  tahadhari. Hakuna mtu yoyote anaetaka awe sehemu ya uhalifu na kudharauliwa mbele za watu wakati huo. Inalinda nyendo za watu kufanya uhalifu.

2. Kuudhibiti uhalifu.

Moja kati ya malengo ya adhabu katika Uislamu ni kumbadili  mhalifu. Adhabu hutekelezwa ili kuboresha  maadili mema kwa mhalifu na kumtia adabu ili asirudie tena uhalifu.

Adhabu kwenye Uislamu ni kama elimu kwa mtoto kutoka kwa baba yake au matibabu kwa mgonjwa kutoka kwa daktari. Lengo si kumakandamiza, kuumiza, au kulipiza kisasi  kwa mhalifu.

3. Upatanisho/Suluhu (kufutiwa adhabu)

Adhabu kwa uhalifu ni upatanisho (suluhu), ambayo ndio utekelezaji wa haki kamili. Hivyo, alieathirika huridhika na kuburudika; Amani na ustaarabu huendelezwa kwenye jamii. Hivyo basi, Mtume wa Allah (rehma na Amani ziwe juu yake) amesema yafuatayo katika hadithi:

“Adhabu inayotekelezwa kwa kuitambulisha haki duniani ni bora zaidi kuliko mvua ya asubuhi inyeshayo kwa siku 30.” (Ibn Hanbal, Musnad, II / 402)

Kuna ulazima wa kutenda haki kulipiza kisasi dhidi ya mtu ambae amefanya jambo baya. Jambo hili limetajwa kama ifuatavyo kwenye Kur’an:

“Na malipo ya uovu ni uovu mfano wa huo. Lakini mwenye kusamehe, na akasuluhisha, basi huyo malipo yake yapo kwa Mwenyezi Mungu. Hakika Yeye (Allah) hawapendi wenye kudhulumu…” (ash-Shura, 46/40)

Kama inavyoonekana, kuna ulazima wa kutenda haki kumuadhibu mhalifu kwa kadri anavyostahiki. Hata hivyo, ni vyema kwa alieathirika kumsamehe mhalifu.

Usawa (Mumathalah) ni muhimu katika adhabu. Hii ina maana kwamba, adhabu lazima iwe sawa na inayofaa kwa uhalifu. Ikiwa adhabu itakuwa kali ukilinganisha na uhalifu, italeta ukandamizaji na kutoridhika, sio haki kwenye jamii. Tabia ya adhabu ya suluhu/upatanisho ni neema na rehma kubwa   kwa mhalifu. Kwa mujibu wa mitazamo ya wanazuoni wengi, adhabu inayolipwa kwa uhalifu duniani itatoa kafara/kufuta kosa la uhalifu; mhalifu hatoadhibiwa tena siku ya Qiyama kwa uhalifu huo.

Ukweli ni kwamba, Mtume (rehma na Amani ziwe juu yake) amesema yafuatayo:

“Mtu anapofanya uhalifu na akaadhibiwa kwasababu ya uhalifu huo, huzingatiwa kama suluhu/upatanisho kwake.” (Ömer Nasuhi Bilmen - Hukuki İslamiyye ve Istılahat-ı Fıkhiyye K., I / 33)

Kwa vile lengo la adhabu ni kuboresha, ni vyema adhabu isitekelezwe ikiwa mhalifu ametubu baada ya kutenda uhalifu. Kwasababu, lengo la adhabu itakuwa limeshapatikana.

Wakati mtu mmoja alipokwenda kukiri kwa Mtume (rehma na Amani ziwe juu yake) kwamba ameiba, Mtume alimwambia, “Sidhani kama wewe umeiba.” (1)

Vile vile, wakati Maiz, mmoja katika Maswahaba, alikiri mbele ya Mtume wa Allah kwamba amefanya zinaa ili atubu, Mjumbe wa Allah alimuambia,

 “Fikiria vizuri. Huenda hujazini; inawezekana umembusu tu au jambo jengine kama hilo.”

Hivyo, alijaribu kumfanya Maiz aachane na kukiri kwake. Hata hivyo, wakati Maiz aliposisitiza kwamba amefanya zinaa, aliadhibiwa. (2)

Ni muhimu kuelezea kwamba kwenye masuala yote mawili yaliyotajwa hapo juu, uhalifu haukuwa bayana kwasababu hakuna mtu yoyote aliyejua au kuona uhalifu huo uliofanywa. Wahalifu walitubu na kukiri uhalifu wao. Ikiwa hawakukiri, isingewezekana kuwashtaki.

Kwa hiyo, wakati Mtume wa Allah (rehma na Amani ziwe juu yake) alipoona kweli wametubu kwa uhalifu waliotenda, hakutaka uhalifu wao ujulikane kupitia kukiri kwao. Aliona inatosha kwao kutubu na kuomba msamaha kwa Allah. 

Ikiwa uhalifu umekuwa wazi kutokana na ushahidi na ushuhuda bila ya mhalifu kukiri, hali hapo ni tofauti. Kutubu kwa mhalifu katika hali hiyo hakuzingatiwi.

Kwenye kutekeleza adhabu ya hadd, maslahi ya jamii ni bora kuliko maslahi ya mhalifu. Haijalishi hali ya mhalifu, adhabu ya mhalifu hutekelezwa iwapo uhalifu  umekuwa wazi ili kudhibiti aina hizi mbaya za uhalifu zisienee kwenye jamii na ili zisisababishe utundu na kukata tamaa. Hata hivyo, qisas (kulipiza kisasi) huondolewa kwasababu kwenye kisasi, ndugu wa mtu ambae ameuliwa wana haki ya kumsamehe muuwaji. Na msamaha huu unatiliwa nguvu sana kwenye Kur’an.

Kwa kuzingatia uhalifu ambao huitwa tazir na ambao hukumu zake zinaachwa kwa hakimu aamue, hali ya mhalifu huzingatiwa. Ikiwa hakimu atashawishika kwamba mhalifu atabadilika, anaweza akaondoa au akapunguza adhabu. Hata hivyo, maslahi ya jamii lazima yazingatiwe wakati wa maamuzi.

Maelezo ya chini:

(1) Ahmad b. Hanbal, Baqi Musnad al-Ansar, 21480
(2) Muslim, Hudud, 22; ash-Shawkani, Naylul-Awtar, VII, 95,109; az-Zaylai, Nasbu'r-Raya, III, 314 n.k.

Maswali juu ya Uislamu

Author:
Maswali juu ya Uislamu
Subject Categories:
Read 290 times
In order to make a comment, please login or register
MASWALI YENYE KUFANANA