Kwa nini hajj ilifaradhishwa?

The Answer

Dear Brother / Sister,

Wajibu wa mtu, anayemwamini Allah na dini Aliyoituma, kwaMuumba wake unaitwa “ibadah” (ibada).

Ibadah, kwa maana pana, ni mtu kuratibu maisha yake kwa namna anayotaka Allah; ama (ibada) katika maana iliyo katika mipaka yake,ni kumgeukia Allah kwa mambo kama vile swala, kufunga, zakah, hajj na kuchinja mnyama. Kila ibada ina sifa na busara zake za kipekee; ikiwa mtu anaabudu huku akiyajua hayo, atanufaika zaidi. Ni muhimu sana kujua vipimo vya kihistoria, kimaadili na kitamaduni na hekima za hajj, vyenye amali za kiishara, ili kuonesha hekima za hajj na kuvutia ari cha hajj.

Kwa hakika kuna hekima nyingi kwa ajili ya maisha ya dunia na ya ahera katika kila amri ya Allah. Kutokana na ukweli huu usio na dosari, hajj ina hekima nyingi. Sehemu ya ukweli huo umeorodheshwa kama ifuatavyo:

Kila mmoja kimaumbile anatakiwa amwabudu Allah. Hajj ni ibada inayomwezesha mwanadamu kuonesha udhaifu wake mbele ya Allah, kumwabudu na kumshukuru kwa neema alizowapa. Kwa kuwa, anayehiji huachana na mambo ya kidunia kama vile pesa, mali, cheo, na hadhi, na kumgeukia Allah. Anaonesha kujisalimisha kwake na uaminifu wake mbele ya Mwenye uwezo na nguvu. Hilo humfanya apate ridhaa ya kuwa mja wa Allah.

Hajj huleta taswira changamfu ya usawa na undugu kwa kuwakutanisha mamilioni ya Waislamu wenye malengo ya namna moja pasi na kujali lugha zao, mbari, nchi, tamaduni, hadhi na cheo. Mahujaji wote, wakiwemo matajiri na masikini, wenye nguvu na wanyonge, hupata mafunzo halisi ya usawa na undugu wakiwa wamevaa mavazi ya kufanana, wakiwa na kujinyima kunakolingana, wakiwa na taabu zinazolingana na kutenda kwa wakati mmoja katika mazingira hayo hayo. Hajj humfanya tajiri na masikini waswali katika Arafat wakiwa wamevaa mavazi ya namna moja, kuzunguka Kaaba kwa pamoja; kwa hivyo, inamfundisha mwanadamu asijidai kwa hadhi yake, cheo, mali na pesa; inawafundisha mahujaji kukutana na kujuana ndani ya mfumo wa undugu wa Kiislamu na kutokusahau Sehemu ya Mkusanyiko.

Kuona ardhi tukufu ulikoanzia Uislamu, ambapo Mtume (s.a.w) na Sahaba zake walipata taabu na matatizo, na ambapo mitume wengi tangu Nabii Adam waliishi na kuzuru kutaimarisha hisia za kidini za Waislamu na kuzidisha utiifu wao kwenye Uislamu.

Maelfu ya Waislamu wenye rangi, lugha, nchi na tamaduni mbalimbali lakini ni wenye lengo moja na kutoka duniani kote huja kwa pamoja na kukutana, shukrani ziiendee hajj. Hilo huwawezesha Waislamu kuwasiliana, kutambua matatizo ya Waislamu wenzao na hata kuanzisha mahusiano ya kibiashara.

Kwa kuhiji, Muislamu anatimiza wajibu wa kushukuru neema za kidunia kama vile afya, vipaji, mali na pesa alizopewa na Allah.

Waislamu wanaohiji huzidisha maadili kama vile uvumilivu, ustahamilivu, kusahau shida, kuweza kufanya kwa pamoja jambo linalofanana katika kundi kubwa la watu, kusaidiana, mshikamano na kujizoeza kanuni mbalimbali.

Hajj humwachia muumini kumbukumbu kubwa isiyofutika maishani mwake. Kumbukumbu hizo huwasaidia Waislamu wasipotee njia katika maisha baada ya hajj. Hajj huunda tukio muhimu la kihistoria katika maisha ya muumini.

Muislamu anayekunjua mikono yake, anamwomba Allah na kufutiwa madhambi yake katika mahali kama Arafat, ambayo ni mfano wa Sehemu ya Mkusanyiko, hatakuwa mwepesi kurudia tena madhambi aliyoyatenda katika siku za nyuma.

Shukrani ziiendee hajj, athari njema zinatokea miongoni mwa Waislamu. Waumini wanafundishana sifa nzuri. Maendeleo chanya hufanyika katika fikra zao. Inapunguza fikra hasi zinazowabagua watu kama vile ubaguzi wa kimbari.

Kwa kifupi, hajj ina hekima nyingi na manufaa mengi ya kimaadili, kijamii, kiuchumi na kisaikolojia. Hapo juu yametajwa machache tu.

Maswali juuyau islamu

Author:
Maswali juuyau islamu
Subject Categories:
Read 17 times
In order to make a comment, please login or register
MASWALI YENYE KUFANANA