Ni ipi dini ya mwisho ya Mwenyezi Mungu?

The Answer

Dear Brother / Sister,

Wanazuoni wa Kiislamu wanagawanya dini katika makundi makuu mawili:

1. Dini za kweli.

2. Dini potovu.

Dini zenye msingi wa kumwamini Mungu mmoja na kuwaamuru watu kumwabudu na kumtii Yeye tu zinaitwa "dini za kweli". Dini za kweli zilizotoka kwa Allah. Kwa hivyo, pia zinaitwa dini zinazotoka mbinguni. Dini ya kweli pia huitwa "dini ya upwekeshaji" kwasababu zina msingi wa kumpwekesha Allah na kumwabudu Yeye tu. 

Dini ambazo hazikuteremshwa na Allah, zilizoundwa na watu na hazina msingi wa kumwamini Mungu mmoja zinaitwa "dini potovu".

Baadhi ya dini za kweli zilipotoshwa na watu baadaye; na ushirikina na imani potovu ambazo hapo mwanzoni hazikuwepo ziliongezwa baadaye. Dini zilizokuwa za kweli hapo mwanzoni lakini baadaye zikabadilishwa zinaitwa "dini zilizogeuzwa"; mathalani, Uyahudi na Ukristo.

Dini ya kwanza kwa wanaadamu ni ya upwekeshaji iliyokuwa na msingi wa kumwamini Mungu mmoja, iliyoteremshwa kwa Adam, mtu wa kwanza na Mtume wa kwanza. Tafiti za kielimujamii zinakubali kuwa dini ya mwanzo ya wanaadamu ilikuwa ya upwekeshaji. Kwa hakika, Schmidt, mtafiti wa historia za dini mbalimbali na mwanaelimujamii, alionesha kwamba Mbilikimo, ambao ni jamii ya kale zaidi duniani, walikuwa na imani ya Mungu mmoja. Uchunguzi wa Schmidt umekanusha madai ya Durkheim kwamba Utambikaji ulikuwa dini ya mwanzo ya wanadamu na akaondosha nadharia hiyo iliyoenea huko Magharibi.

Baada ya Nabii Adam (a.s), baadhi ya watu waliacha kuamini upweke (wa Allah), wakatoka kwenye dini za kweli na kuingiza baadhi ya imani potovu kadiri wakati ulivyosonga mbele kwa kutii nafsi zao na ushawishi wa Shetani. Hivyo, dini potovu zikaibuka. Kadiri watu walivyojitenga na dini ya kweli, Mwenyezi Mungu aliwapelekea mitume wengine na dini ili wawaite kwenye imani ya upwekeshaji. Hata hivyo, baadhi ya watu walikubali wito huo na wengine waling’ang’ania imani zao potovu. Wachilia mbali kuendelea kung’ang’ania imani zao wenyewe, walijaribu kuwazuia wale waliotaka kurejea kwenye dini ya kweli na wakawakandamiza na kuwatesa. Hivyo, mara zote kumekuwa na mapambano baina ya walioamini dini ya kweli na ambao hawakuamini, katika kila karne na enzi. Mapambano haya bado yanaendelea na hayataisha mpaka Siku ya Kiama.

Dini ya Mwisho ni Uislamu.

Leo hakuna hata kimoja katika vitabu vitukufu vilivyoshushwa kabla ya Quran chenye hali yake asili. Kadiri wakati ulivyosonga mbele, uasili wake ulipotea na vikaandikwa upya na watu. Kwa hivyo, ushirikina na imani potovu vikachanganywa ndani mwake. Mathalani, ni ukweli wa kihistoria kuwa Taurati isingeweza kudumishwa na Wayahudi baada ya Nabii Musa, kwani waliishi uhamishoni kama watumwa kwa karne nyingi na walipoteza imani yao na wakaabudu sanamu; pia ni uweli wa kihistoria kuwa Taurati iliyopo sasa iliandikwa na baadhi ya wanazuoni na ikapokelewa kana kwamba ilikuwa ile  Taurati ya asili. Ni dhahiri kuwa kitabu kilichoandaliwa baada ya kupita muda huo mrefu uliovurugika hakiwezi kuwa Taurati ileile aliyoshushiwa Nabii Musa. Kwa hivyo, ina baadhi ya madai na kashfa zisizowastahiki mitume na amri zilizo kinyume na dini yenyewe. 

Zaburi aliyopelekewa Dawud ilipatwa na hali hiyo hiyo.

Ama kuhusu Injili (Biblia), Nabii Isa (Yesu) hakupokea wahyi wa kimaandishi kwasababu alipata utume alipokuwa na umri wa miaka thelathini na kazi ya utume iliisha alipofikisha umri wa miaka thelathini na tatu.  Alikwenda kijiji hadi kijiji kingine na mji mmoja hadi mwingine ili kuwaongoza watu katika kipindi kifupi sana cha miaka mitatu. Katika siku zake za mwisho, kila mara alifuatwa na watawala wa Kirumi kutokana na uchochezi wa Wayahudi. Hakuweza kupata muda au fursa ya kuandikwa Injli. Kwa hakika, Injili zilizopo leo zimeitwa kwa majina ya watu walioziandika na zinaonekana kama wasifu wenye mahubiri, mafunzo na wongozo wa Yesu kwa mitume wake. Kando ya hayo, hazikuandikwa na mitume wake, ambao walikuwa waumini wa mwanzo, bali waliosikiliza maneno ya kiungu aliyopewa Yesu kuwafikishia.

Zipo tofauti baina ya Biblia zilizopo, kwa upande wa maudhui na masimulizi. Kwa hakika, Biblia hizo zilikubaliwa na baraza la mapadri elfu moja mnamo mwaka 325 BK huko Nicaea. Baraza lilichunguza mamia ya Biblia na kukubali Biblia 4 zilizodai kuwa Yesu alikuwa katika uungu kwa muwafaka wa wajumbe 318 na wakaziharibu Biblia zingine kwa kuzichoma moto.

Kama ilvyoonekana, kanuni ya kwamba Yesu alikuwa mwana wa Mungu – Allah atukinge dhidi ya hilo – ilipokelewa na baraza lililokutana miaka mingi baada ya Yesu. Kwa hivyo, ni muhali kusema kuwa Biblia zilizopo leo ni kama Biblia za asili

Maswali juu ya Uislamu

Author:
Maswali juu ya Uislamu
Subject Categories:
Read 2.266 times
In order to make a comment, please login or register