Ni ipi hekima ya kuswali swala tano kila siku?
Dear Brother / Sister,
Asubuhi na mapema, mwanadamu huwa katika hali kana kwamba ameanza maisha mapya na huwa na nguvu za kiwiliwili ambazo ni muhimu kwa shughuli za kila siku kupata mahitaji yake ya kuendesha maisha yake. Ni Allah ndie anaempa nguvu hizi na ndie anaemfanya afaulu katika juhudi zake za kutafuta maisha. Hivyo basi, mwanaadamu anapaswa kuswali swala ya alfajiri ili amshukuru Allah kwa kumpa neema ya afya njema na ili apokee msaada kutoka kwa Allah katika juhudi zake za kidunia.
Kila siku, kutoka asubuhi hadi jioni, mwanadamu hufaidika na neema za uhai, afya na akili ambayo Allah amempa. Kuzishukuru neema hizi, mwanadamu hupata mafanikio katika mambo yake ya kidunia. Swala za mchana na jioni zimewekwa kuwa ni lazima ili mwanadamu ashukuru kwa mafanikio aliyoyapata na ili shughuli hizi ziendelee kulindwa ili zisije zikaiingiza nafsi kwenye mghafala na huzuni.
Swala za jioni zimefanywa kuwa fardhi (lazima) ili zile kazi za kila siku na juhudi ambazo zipo karibu kukamilika kwa kadri jioni inavyokaribia zimalizwe kupitia ibada za kiroho na kwa hiyvo itakuwa ni alama ya shukurani kwa mapato na faida iliyopatikana siku hiyo.
Baada ya hapo, mwanadamu ataingia. Ulimwengu wa usingizi. Kabla ya kufika kwenye ulimwengu huu, ambao ni mfano wa kifo na ambao huzingatiwa kama kipindi cha Amani na utulivu, inatakiwa kuimaliza siku kwa ibada tukufu, ili kuingia katika ulimwengu huo na radhi za kiungu na na mwamko wa kiroho na kumuomba Allah msamaha na huruma zake na itakuwa ni alama ya mwisho mwema; hivyo basi, swala za usiku hufanywa.
Kwa upande mwengine, ziko hatua 5 tofauti kwenye maisha ya watu na viumbe vyengine vinavyowazunguka watu: kuzaliwa (being born), kukuwa (growing up), kusimama makuzi (stagnating), kuwa mzee (getting old) na kufa (dying).
Kuendana na hatua hizo, Muumba wetu ametuagiza tutekeleze swala 5 kila siku ambazo zitaweka usawa mzuri baina ya uwepo wetu wa kimaumbile na kiroho na juhudi zetu. Hatuwezi kumshukuru Allah vyakutosha kwasababu ni Yeye ndie alietuagiza kufanya ibada hiyo ambayo ni tukufu, kivitu na ina faida nyingi sana.
Hekima iliyopo nyuma ya kuzigawa swala mara 5 kwa siku haifungwi kwenye hayo tuliyoeleza juu tu.
Maelezo yafuatayo ya mwanachuoni Badiuzzaman Said Nursi yanafafanua jambo hili:
“Kama ulivyo mshale wa sekunde, mshale wa dakika, mshale wa saa, na mshale wa siku kwenye saa ambayo hueleza majuma kila moja humuangalia mwenzake, ni mifano ya wao kwa wao, na hufuatana, ni hivyo hivyo kwenye mabadiliko ya usiku na mchana, ambayo ni mfano wa sekunde za dunia yetu hii – saa kubwa ya Allah Mtukufu – na miaka yenye kueleza dakika zake, na hatua za umri wa mwanadamu ambazo hueleza masaa yake, na muda wa umri wa maisha ya dunia ambao hueleza siku kila moja kumuangalia mwenzake, ni mifano ya kwa wao, zinafanana , na zina kumbukana.
Kwa mfano:
Muda wa swala ya alfajiri, mapema sana asubuhi: Muda huu mpaka kuchomoza kwa jua huashiria na kukumbusha mwanzoni mwa kipindi cha masika, kipindi ambacho mwanamama hupata ujauzito, na mwanzoni mwa siku sita za uumbaji wa mbingu na ardhi; inakumbushia pia matendo ya Kiungu ndani yake…”
Maswali juu ya Uislamu
