Ni upi umuhimu wa Imani kwa mwanadamu?
Submitted by on Thu, 28/02/2019 - 11:05
Dear Brother / Sister,
1. Imani ni sababu ya kuumbwa kwa mwanaadamu. Hiyo ni kusema, ameumbwa ili kumjua Muumba wake kwa Imani na kumwabudu Yeye. Kama mtu atatenda kwa mujibu wa sababu ya kuumbwa atapata furaha isiyo na mwisho ahera na kuingia peponi; Vinginevyo, ataingizwa motoni na atapata shida na huzuni zisizo kuwa na mwisho. Kwa hivyo, Imani ni njia ya kupata furaha isiyo na mwisho na ni ufunguo wa kuingia peponi. Mtu hawezi kuingia peponi bila ya Imani. Hivyo, ni muhimu kuliko kitu kingine chochote kwa mtu kuamini na kuihifadhi Imani yake bila ya kuipoteza au kuidhoofisha hadi pumzi yake ya mwisho.
Kutokana na umuhimu mkubwa wa Imani, mtume wetu amesema:
“Ifanye upya Imani yako kwa kusema la ilaha illallah : Hapana mola ila Allah”; anaelekeza umakini wetu upande wa kuifanya upya na kuihifadhi Imani. Swali kama, “Imani imetakiwa mara kwa mara kufanywa upya; Je, kuna uwezekano wa kuendelea wa kudhoofika kwa Imani na kupotea?” Linaweza kuja katika akili ya mtu.
Badiuzzaman, anafasiri jambo la kufanywa upya Imani kama ifuatavyo na kujibu swali hilo pia:
“Kwakuwa mwanaadamu na ulimwengu anaoishi ni wenye kufanywa upya kwa kuendelea, anahitajika mara kwa mara kuifanya upya Imani yake. Kwa vile kiukweli kila mtu ana watu wengi ndani yake. Anaweza kuzingatiwa tofauti kwa idadi ya miaka ya maisha yake au kwa idadi ya siku au hata idadi ya masaa ya maisha yake. Kwa vile mtu mmoja ni mwenye kuathiriwa na wakati, anakuwa kama mwana mitindo kila siku huvalishwa katika muundo wa mtu mwingine.
Zaidi ya hivyo, kama ilivyokuwa ndani ya mtu kuna uwingi na upya, pia ulimwengu anaoishi upo katika kutembea, unakwenda na ulimwengu mwingine unachukua nafasi yake. Ni wenye kubadilika kwa kuendelea. Kila siku inafungua mlango wa ulimwengu mwingine. Ama Imani, ni vyote viwili nuru ya maisha ya kila mtu ndani ya mtu huyo, na ni nuru ya ulimwengu anaoishi ndani yake. Na ama la ilaha illallah ni ufunguo wa kuwashia nuru hiyo.
Kisha, roho, matakwa, mashaka, na shetani huwa na taathira kubwa kwa mwanaadamu. Ili kuharibu Imani yake, mara nyingi wana uwezo wa kufaidika kutokana na kutojali kwake, kumuhadaa kwa ushawishi wao na kama hivyo kuzima nuru ya Imani kwa mashaka na kutokuwa na uhakika.
Pia mwanaadamu ni rahisi kutenda au kusema maneno ambayo kwa uwazi huenda kinyume na sharia, na ambayo kwa mtazamo wa baadhi ya mamlaka za kidini ni ukafiri.
Hivyo, kuna haja ya kuifanya upya Imani wakati wote, kila saa, kila siku.” (Mektubat: Letters)
Katika kifungu cha hapo juu, wajibu wa kuifanya upya Imani umeelezwa kupitia nukta tatu tofauti:
Nukta ya kwanza: Wakati na sehemu ambayo mtu huishi, hali yake ya kiroho, saikolojia, fikra, na ufahamu unaweza kubadilika mara nyingi kwa mujibu wa mazingira anayoishi. Vitu anavyokutana navyo, vitu anavyovifanya na watu anaokutana nao huacha alama chanya au hasi kwake.
Mtume wetu anasema yafuatayo kuhusu jambo hilo:
“Moyo wa muumini hapitia mabadiliko zaidi ya sufuria ichemkayo”
“Moyo ni kama ndege. Kila wakati unaelekea upande mwingine”
“Moyo ni kama ubawa wa ndege uliyotupwa. Upepo unaubadilisha; moyo upo kama hivyo.”
Kwa mujibu wa ukweli kuwa moyo wa mwanaadamu na hali yake ya kisaikolojia ni vyenye kuwa katika hatari ya kushambuliwa, na athari za nje, mtume wetu ametuamuru kuifanya upya Imani yetu mara nyingi kwa kusema la ilaha illallah.
Nukta ya pili: Ni ukweli kuwa kuna hisia hasi kama roho, matakwa, na udanganyifu ndani ya mwanaadamu, na shetani ni mwenye kujaribu kumshawishi na kumuhadaa kwa kuendelea. Katika wakati wa kutozingatia, fikra hizo hasi huenda zikamsababishia mashaka mtu kuhusu Imani. Ni wajibu kuifanya upya Imani ili kuepuka kudondoka katika hali ya hatari kama hiyo.
Nukta ya tatu: Mtu hawezi kujizuia na baadhi ya maneno na sentensi ambazo ni kinyume na dini kwa kuonekana na ambazo huzingatiwa kuwa ni ukafiri kwa baadhi ya wanachuoni. Hivyo, ni wajibu kusema la ilaha illallah na uifanya upya imani.
Njia nyingine ya kuboresha Imani na kuihifadhi ni kuiboresha kutoka katika Imani ya kuiga kwenda katika Imani ya kuchunguza. Inaweza fikiwa kwa kusoma vitabu kuhusu Imani ambavyo hufundisha ukweli wa Imani kwa kuchunguza kiundani na kujibu mashaka na udanganyifu ambao unaweza kuja katika akili na kushiriki mazungumzo kuhusu Imani. Ikiwa mtu ataiboresha Imani yake kutoka hatua ya kuiga kwenda katika hatua ya Imani ya kuchunguza kiundani, itakuwa ngumu kwake kupoteza Imani yake au kufa bila ya Imani katika pumzi ya mwisho.
Wanazuoni wa Kiislamu wanasema shetani atakuja kumuhadaa mtu na kumwondolea Imani yake kitandani pake kwa kutumia ujanja na udanganyifu wake wote. Hivyo, wanasema wanahofu ya wakati wa kifo.
Mtu anaweza kuokolewa kutokana na hatari kama hiyo kitandani kupitia Imani ya uchunguzi. Ni kwa sababu katika Imani ya uchunguzi, Imani haipo akilini tu, imetawanywa katika moyo, roho, na hisia nyingine na imekaa humo. Hata kama shetani ataharibu Imani katika akili ya mtu hataweza kuharibu Imani iliyopo katika hisia nyingine. Na kama hivyo, hubaki kuwa muumini na kufa hali ya kuwa ni muumini.
2. Imani ni chanzo kikubwa cha tabia njema na ni nukta yenye nguvu ya kusaidia. Mtu anayepata Imani ya kweli anaweza kushindana na ulimwengu wote na anaweza kumalizana na msukumo wa shida ambao anapitia kwa mujibu wa nguvu ya Imani yake.
Ushindi wetu ambao umeandika historia na kuwafanya watu waandike hadithi ni mfano mzuri wa nguvu ambayo Imani humpa mtu.
Mtu mwenye Imani, haijalishi ukubwa wa msiba ni kiasi gani unaomtokea, huweza kukabiliana na shida na huzuni kwa Imani juu ya Allah na kujisalimisha, na kwa hisia za kuridhika kwa kadari na huyakabili kwa subira na uvumilivu. Hadondokei katika kukata tamaa na mtazamo mbaya. Hadondokei katika uasi na kupiga kelele.
Inatoka katika nguvu ambayo Imani humpa mtu. Tunaona mara nyingi kuwa watu wasiyo na Imani hukata tamaa sana kiasi cha kuwafanya wafikirie kujiua wanapokabiliana na matatizo madogo. Ukweli wa kuwa takriban hatuoni watu kujiua katika nchi za Kiislamu na kuwa kujiua kunaongezeka katika nchi zilizoendelea na nchi tajiri pamoja na hatua ya juu ya maendeleo huthibitisha hilo.
Mtume wetu amegusia nguvu na kuhimili ambavyo Imani humpa mtu kama ifuatavyo:
“Muumini ni kama mmea wa kijani. Upepo wa shida ambao haumkosi humfanya ainame lakini hauwezi kumvunja. Kinyume chake, humfanya afufuke na kupona.
Mnafiki (au kafiri) ni kama mmea uliyokauka. Upepo wa shida hufanya majani yadondoke, hufanya shina kuvunjika na kuyaua.”
“Ajabu ipo katika njia za muumini kwa kuwa kuna uzuri katika kila jambo lake na hili halipatikani kwa yeyote ila muumini; kwa sababu akiwa katika hali ya kumfanya awe na furaha, humshukuru Allah, na kama hivyo, kuna uzuri ndani yake, na akiwa katika shida huonesha ustahamilivu (na huvumilia kwa subira), kuna uzuri ndani yake kwa ajili yake.”
Maswali juu ya Uislamu