Nini ibada ya hija (hajj)? Ni ipi amri ya hajj katika Uisilamu?
Submitted by on Fri, 10/08/2018 - 14:43
Dear Brother / Sister,
Ibada ya Hajj
Kilugha Hajj ni kukusudia na kulielekea jambo. Katika istilahi ya kidini, inamaanisha kutembelea sehemu maalumu katika wakati maalumu pamoja na matendo maalumu.
Pahala Maalumu ni Kaaba na Arafat.
Muda maalumu ni miezi ya Shawwal na Dhul-Qada na siku 10 za mwanzo za mwezi wa Dhul-hijja.
Vitendo maalumi ni vinavyohusiana na hajj kama kuzunguka Kaaba, waqfa kwenye Arafat na sa’y.
Amri inayohusu Hajj
Ibada ya hajj ni moja ya nguzo 5 za Uislamu. Ni ibada inayotekelezwa kimwili na kifedha.
Imefaradhishwa mwaka wa 9 wa Hijra. Kwa hakika Hajj ni fardh kwa mujibu wa Kitabu (Quran), sunnah na makubaliano ya wanachuoni.
Aya ya Quran inayoelezea kuwa hajj ni fardh ni inayofuata:
Na kwa ajili ya Mwenyezi Mungu imewajibikia watu wahiji kwenye Nyumba hiyo, kwa yule awezae njia ya kwendea. (Aal-i Imran, 97).
Hajj ni fardh kwa kila Mwislamu muumini mwanamume na mwanamke mwenye kutimiza masharti muhimu ya kuhiji. Suala hili linaelezwa katika hadith kama ifuatavyo:
“Enyi watu! Mmefaradhishiwa ibada ya hija. Kisha, timizeni ibada ya hajj.”
Swahaba mmoja akauliza,
- Ewe Mjumbe wa Allah! Ni fard kila mwaka?
Mtume (s.a.w.) alinyamaza mpaka yule mtu akauliza swali hilo hilo kwa mara ya tatu. Kisha akasema,
“- Kama ningelisema ‘ndio’ ingeliwajibika kuwa ni fardh kwenu kila mwaka na msingeliweza.”
Maswali juu ya Uislamu