Quran Imeamrisha kwamba anayeiba akatwe mkono wake. Je, siyo adhabu kali hiyo kwa upande wa haki za binadamu?
Dear Brother / Sister,
Wizi, unaomaanisha “kuchukua kitu cha mtu mwingine pahala kilipowekwa bila ya mwenyewe kujua’, ni moja kati ya uhalifu mkubwa dhidi ya mali na haki miliki. Kuzitunza mali zilizolishwa kutokana na kazi ngumu na chumo halali ni miongoni mwa kanuni za msingi za Uisilamu. Uisilamu unazingatia kazi na mali kuwa ni vitu vitakatifu na huadhibiwa wale wanaoshikilia mali za wengine kwa dhuluma. Hivyo, kama hali ilivyo kwa dini zote za mbinguni na mifumo ya kisheria, wizi unazingatiwa kuwa ni dhambi kubwa na uhalifu kisheria na kidini na kimaadili katika Uisilamu.
Wizi ni hiyana kubwa inayojeruhi moyo wa mmiliki mali na ni uharibifu usioweza kukubaliwa na dhamiri. Uharibifu huu umeshatokea na unatokea katika kila karne na popote pale. Kwa hivyo, dini ya Uisilamu imeweka adhabu kali kwa wale wenye kutenda uhalifu huu mkubwa ili kutoa adhabu stahiki. Ikiwa hukumu hii itatekelezwa, kesi za wizi zitapungua kwa kiwango cha chini.
Wizi umekatazwa kwa ushahidi wa Quran, sunnah na makubaliano ya wanazuoni wa Uisilamu. Yafuatayo yanaelezwa katika Quran:
“Na mwizi mwanamume na mwizi mwanamke, ikateni mikono yao” (al-Maidah, 38).
Mtume ameeleza:
“Watu wa kabla yenu waliangamizwa kwa sababu alipoiba mheshimiwa walimwacha huru na alipoiba masikini walimwaadhibu.” (ash-Shawkani, Naylu’l-Awtar, VII, 131,136).
Wizi unapothibitishwa kutokea, adhabu ya mwizi kukatwa mkono hutekelezwa. Kama zilivyo kesi ambazo hukumu hii sio ya lazima, basi mwizi huyo hulipa fidia kwa alichokipoteza.
Majaji wa kiisilamu wamejadiliana jinai na adhabu, chini ya masharti yapi uhalifu wa wizi utazingatiwa kuwa umefanyika ili kuandaa haki na jinai, mazingira ambayo adhabu gani inafaa kutolewa, athari za hali kama vile kurudiarudia, kutezwa nguvu na kusamehe kwenye adhabu, moja baada ya nyingine; wameanzisha msingi wa sheria wenye kujitosheleza. Kwa kifupi, wameamua kwamba, ili uhalifu wa wizi uwe umethibitika, ni sharti kusiwe na udhuru kama vile wajibu, kutezwa nguvu na ukame ambavyo vingepoza kufanya uhalifu wa wizi kwa sehemu fulani au kikamilifu. Ni sharti kuwa uhalifu uwe umefanyika kwa khiyari na kwa uhuru, maudhui hii ina uwajibikaji kisheria katika makosa ya jinai, mali iliyoibiwa kuwa chini ya hifadhi na kuwa zaidi ya kiwango maalum.
Adhabu katika sheria ya Kiisilamu imeainishwa kuwa ni hatua ya mwisho na uingiliaji kati wa lazima ambao unaweza kutekelezwa baada ya tahadhari za kimsingi kutolewa ili kuzuia uhalifu. Katika hali hii, lazima itiliwe maanani kuwa lengo kuu la Uisilamu sio kuwaadhibu watu bali, kinyume chake, kuchukua tahadhari ambako kutawazuia watu kufanya uhalifu wa wizi, kuwaelimisha na kuwapa mwongozo. Pia ni muhimu sana kwamba, ili wale wote wanaojitolewa katika jamii wafanikiwe, malezi ya kidini, hadhi ya maadili jumla ya jamii na taratibu za sheria za ziada na sera rasmi ziwe kwa maelewano ya pamoja.
Allah, Aliye Juu Zaidi, ameamuru mwizi kuadhibiwa. Katika mazingira haya ya jumla, ni lazima kuukata mkono wa mtu anayethubutu kuiba kama ni kiungo hatari cha taasisi ya jamii ya Kiisilamu.
“Enyi mlioamini! Kateni mikono ya mwizi mwanamme na mwanamke, ambao uhalifu wao umethibiti na bila ya shaka yoyote wala udhuru, kuwa ni adhabu kwa yale waliyoyatenda, kuwa ni adhabu chungu kutoka kwa Allah, kuwa ni kizuizi mwafaka, kama ilivyo kupiga pingu mikononi hivyo hawatothubutu kuiba tena. Bila ya shaka, Allah ndiye aliye juu zaidi na mwenye hekima.” Maamrisho yake hayawezi kubishiwa. Anahukumu kwa busara. Haki iko salama kwa ukuu wa ulinzi Wake na adhabu Zake zimejaa hekima kikamilifu. Allah hakubali dhuluma, kero na fitina. Ametutunuku mikono na nguvu za kufanyia kazi kwa ajili ya heri na haki. Allah anaamuru tumwogope Yeye, tujitahidi kwa ajili ya mafanikio ya dini, kuwahifadhi masikini, kuwajali wahitaji na kuwasaidia walio madhaifu, kama alivyoeleza katika aya nyingi za Quran. Pia amewawajibisha matajiri kutoa zaka na sadaka kwa masikini na watu dhaifu kwa maamuzi Yake yanayohusu kusaidia, kutoa zaka na hisani. Mwisilamu wa kweli lazima atii maamrisho hayo ya Allah na kuyatekeleza maishani mwao. Kama mtu hamwogopi Allah, hana sababu nzuri ya kumkaribia Allah, hawezi kujinyima matamanio yake ya chini kabisa na hujaribu kuchukua mali ya mwingine kisirisiri, kwa namna ambayo hana haki kabisa, kama vile Allah hamwoni akifanya hivyo, kwa hakika anaishambulia heshima ya Allah, na ni vita vya siri alivyovianzisha dhidi Yake. Basi, mkono wa mtu huyo unastahiki kukatwa kuwa ndio adhabu.
Kwa namna hii, isidhaniwe kwamba hakuna usawa kati ya uhalifu na adhabu hiyo. Kwa hakika, adhabu hiyo sio tu ni malipo ya mali iliyoibiwa. Bali pia ni kwa ajili ya uhaini wa kisirisiri na kuishambulia heshima ya Allah. Ni kama vile mtu huyo kaweka mkono wake kwenye moto au ameugongesha kwenye upanga. Adhabu hiyo ni, kwa wote wawili yeye na atakayefuata njia yake iliyopotea, kama pingu isiyofunguka. Pamoja na hilo, wote wawili mwizi na wengine husafishwa kutokana na fitina. Halikadhalika, Allah huwachukulia wale wanaoishambulia heshima Yake kwa njia hii wanastahili adhabu hiyo sio tu kwa sababu ya hasira Zake bali pia kwa sababu ya kuwepo hekima ndani yake. Katika jamii ambamo adhabu hii hutekelezwa, wizi unakuwa umekomeshwa. Hakutokuwa tena na mkono utakaostahili kukatwa. Adhabu hii ni lazima itekelezwe kiuadilifu na bila ya mashaka yoyote hivyo hakutoibua dhuluma yoyote. Kinyume na hivyo, heshima na busara za Allah zitaonekana hazifai. Ikiwa adhabu ya mkono ulioiba kitu ni kukatwa, hebu fikiria adhabu ya mtu aliyeiba mkono bila ya haki (anaekata mkono wa mtu bila ya haki) itakuwaje!
Hivyo, kama mwizi, awe mwanamme au mwanamke, waliosababisha mikono yao kukatwa kwa sababu wameiba kitu, watatubu baada ya kutenda uhalifu huo na kurekebisha tabia zao, Allah atapokea toba yao kwa sababu Yeye ni mwingi wa rehema na mwingi wa kusamehe. Na wala hatowaadhibu Ahera, atawahurumia na kuwasamehe. Katika hali hii, wale waliokatwa mikono yao na baadaye wakatubia wasidhaniwe kuwa ni waovu kwa sababu waliiba hapo kabla; ni vyema wasaidiwe.
Maswali juu ya Uislamu
