Ukristo ni nini? Utatoa maelezo kuhusu Ukristo uliotajwa ndani ya Quran?

The Answer

Dear Brother / Sister,

Ukristo ni dini ambayo kiasili imetegemea ufunuo, yenye kitabu kitukufu na ambayo kiasili ni dini ya kumwamini Mungu mmoja; hata hivyo, iligeuzwa kuwa imani ya utatu hapo baadaye. Kuna dhana ya kidini kama mitume, malaika, ahera na qadar (majaaliwa) katika dini hii lakini hayafahamiki na kufafanuliwa kwa namna sawa kama ilivyo katika Uisilamu.

Kwa uhakika, Ukristo ni dini inayoegemea kwenye imani ya Mungu mmoja. Yapo maelezo yenye kutilia mkazo ukweli huu katika Biblia na vyanzo vyengine. Kumpwekesha Allah kumetajwa (Yohana.V / 44). Hata hivyo, baadhi ya ibara na maelezo ya kuunda katika maandishi hayo hayo yamesababisha kuibuka kwa imani ya utatu. Baadhi ya waandishi wa Biblia na muda kati ya Yesu na muda wa kuandikwa Biblia una mchango mkubwa katika ufahamu huu. Kwa upande mwengine, utatu hauelezewi waziwazi popote pale katika kitabu kitakatifu cha Ukristo. Hata hivyo, baadhi ya maelezo kama “mimi na Baba ni kitu kimoja”, roho ya baba yako”, “roho ya Mungu” kumepelekea kwa baadhi ya tafsiri zinazomzingatia Yesu na roho mtakatifu kuwa ni Mungu pamoja na Mungu.

Mtu wa mwanzo kuanzisha tafsiri hizi alikuwa ni Paul, ndiye aliyeunganisha wanafunzi baadaye. Paul, anaetambulika kuwa ni “mwanathiolojia mkubwa wakati wa zama za Yesu Isa”, anajulikanwa kuwa ndio mwasisi wa Ukristo leo. Kwa mujibu wa wanazuoni wa kisasa, Ukristo wa leo unajumuisha ufasiri wa Paul kuliko mfumo uliotambulishwa na Yesu. Hata pia inaweza kusemwa kuwa karne zilizofuata zimetegemea imani yao ya kidini kwa tafsiri ya Paul kuliko Biblia. Mapendekezo ya Paul yamelenga kwenye Yesu Masiya kuliko Mungu. Kwa mujibu wake, Yesu hakuwa ni mtu tu bali pia alifufuliwa kwa uwezo wa Mungu.

Kama inavyoonekana, Ukristo wa leo umeegemea kwenye tafsiri ya Paul. Mifumo yote miwili ya dini hii ya asili na Biblia, kitabu chao kitakatifu, kimegeuzwageuzwa. Ukristo ni dini iliyogeuzwageuzwa. Hata hivyo, Ukristo uliogeuzwageuzwa na Wakristo wanaoishi leo na ukristo uliotajwa ndani ya Quran ni tofauti kabisa.

Katika Quran, neno “Nasrani” linatumiwa kwa Mkristo na neno “Nasara” kwa Wakristo. . (Aal-i Imran, 3/67; al-Baqara, 2/62, 111, 113, 135, 140; al-Maida, 5/14, 18, 51, 69, 82; at-Tawba, 9/30; al-Hajj, 22/17). Wakristo pia wametajwa na aya zilizokuwemo ibara “Ahl al-Kitab” (Watu wa Kitabu) kama aya ifuatayo:

“Sema: Enyi Watu wa Kitabu! Njooni kwenye neno lilio sawa baina yetu na nyinyi: Ya kwamba tusimuabudu yeyote ila Mwenyezi Mungu, wala tusimshirikishe na chochote.” (Aal-i Imran, 3/64)

Kwa mujibu wa Quran, kama vile Wayahudi, Wakristo hawakutimiza ahadi yao; kwa hivyo, uadui na kinyongo vitawatawala hadi Siku ya Kiama. Bwana Muhammad (s.a.w.) ni mjumbe aliyetumwa kwao, pia. Aliwafafanulia mambo mengi yaliyofichwa na Watu wa Kitabu. Hata hivyo, Wayahudi na Wakristo walisema wao walikuwa ni “watoto wa Allah na vipenzi vyake”; hivyo, walimpinga Bwana Muhammad (s.a.w.). Wayahudi walimzingatia Uzayr na Wakristo walimzingatia Yesu kuwa ni mwana wa Mungu. Wamekuwa ni makafiri tokea walipomfanya binadamu kuwa ni mungu. (al-Maida, 5/12-18; at-Tawba, 9/20) Walitenda kinyume na asili ya dini ya upwekeshaji kwa kuwasifia watoto kuwa ni Mungu. Hata hivyo, yafuatayo yanaelezwa katika Quran:

Sema: Yeye Mwenyezi Mungu ni wa pekee. Mwenyezi Mungu Mkusudiwa. Hakuzaa wala hakuzaliwa. Wala hana anaye fanana naye hata mmoja.” (al-Ikhlas, 112/1-4).

Quran inaeleza kuwa Yesu ni mja wa Allah na mjumbe na kwamba anafikisha ujumbe wa kumpwekesha Allah. (al-Maida, 5/46-47, 62-69, 72-77). Kwa hali hiyo, Wakristo waliomfanya Yesu kuwa ni mungu wanasema, “Mwenyezi Mungu ni wa tatu wa Utatu.” (al-Maida, 5/73); hivyo, wameikengeuka njia ya kweli na kwenda nje ya mstari wa upwekeshaji. Allah anawaita Wakristo walio nje ya kanuni ya upwekeshaji kuja kwenye uasili wa dini, kuja kumpwekesha Allah na kwenye njia ya Uisilamu. (al-Maida 5/46).

Kama inavyoelezwa hapo juu, Ukristo asili yake ni dini ya kweli. Mtume wake ni Yesu na kitabu chake ni Biblia. Yesu, aliyeunda nukta ya mazingatio ya Ukristo wa leo na misingi ya thiolojia ya Paul, ni mja wa Allah na mjumbe wake. Yesu yeye mwenyewe anaeleza hayo kama ifuatavyo:

(Mtoto) akasema: Hakika mimi ni mtumwa wa Mwenyezi Mungu. Amenipa Kitabu, na amenifanya Nabii. Na amenijaalia ni mwenye kubarikiwa popote pale niwapo. Na ameniusia Sala na Zaka maadamu ni hai, Na nimtendee wema mama yangu. Wala hakunifanya niwe jeuri, mwovu. Na amani iko juu yangu siku niliyozaliwa, na siku nitakayo kufa, na siku nitakayo fufuliwa kuwa hai.(Maryam, 19/30-33).

Isitoshe, Wakristo waliomfanya Yesu na mama yake kuwa ni mungu, wanaounda imani ya utatu watakumbana na Yesu Siku ya Kiama; hivyo, uongo uliosemwa na Wakristo utafunuliwa mara moja. Suala hili linaelezwa katika Quran kama ifuatavyo:

Na pale Mwenyezi Mungu atakapo sema: Ewe Isa bin Maryamu! Ati wewe uliwaambia watu: Nifanyeni mimi na mama yangu kuwa ni miungu badala ya Mwenyezi Mungu? (Na Isa) atasema: Subhanaka, Wewe umetakasika! Hainifalii mimi kusema ambayo si haki yangu. Ikiwa nilisema basi bila ya shaka umekwisha yajua. Wewe unayajua yaliyo ndani ya nafsi yangu, lakini mimi siyajui yaliyo katika nafsi yako. Hakika Wewe ndiye Mjuzi mkubwa wa yaliyo fichikana. Sikuwaambia lolote ila uliyo niamrisha, nayo ni: Muabuduni Mwenyezi Mungu, Mola wangu Mlezi na Mola wenu Mlezi. Na mimi nilikuwa shahidi juu yao nilipokuwa nao. Na ulipo nifisha ukawa Wewe ni shahidi juu ya kila kitu.” (al-Maida, 5/116, 117).

Ukristo katika zama za Mtume (s.a.w.) ulikuwa ushageuzwageuzwa kama ulivyo Ukristo wa leo.

Kisha, Ukristo wa leo sio sawa na Ukristo uliofikishwa na Yesu. Wao wenyewe walitunga sentensi kama vile “Na Wakristo wanasema Masihi ni mwana wa Mungu.” (at-Tawba, 9/30) na “Wamewafanya makuhani wao na wamonaki wao kuwa ni marabi badala ya Mwenyezi Mungu, na pia Masihi bin Maryamu.” (at-Tawba, 9/31).

Vivyo hivyo, Ukristo wa leo hauna uhusiano na Biblia iliyoletwa na Yesu. (al-Maida, 5/68) Kwa kuwa, kama vile wanazuoni wa Kiyahudi, mapadri wa Kikristo walibadilisha maamrisho ya Kitabu walichoteremshiwa na Allah kwa sababu ya manufaa ya kupata kitu. (at-Tawba, 9/34)

Maswali juu ya Uislamu

Author:
Maswali juu ya Uislamu
Subject Categories:
Read 2.565 times
In order to make a comment, please login or register
MASWALI YENYE KUFANANA