Je Uislamu, Agano la Kale na Agano Jipya vimeathiriwa na Wasumeria?

Submitted by on Wed, 08/08/2018 - 14:24
Dear Brother / Sister,
Kwa kweli, suala kwamba baadhi ya habari na mambo mazuri yaliyopo leo katika umma au utamaduni yapo pia katika mojawapo ya dini za kweli haioneshi kuwa dini hiyo iliathiriwa na utamaduni huo; badala yake, inaonesha kuwa chanzo chake pia kilikuwa ni ufunuo. Wakati muda ukiendelea mbele, uhusiano wake na ufunuo ulisahaulika na kutazamwa kuwa ni utamaduni wa umma huo kwa sababu Allah aliwatuma mamia kwa maelfu ya mitume kwenda kwa wanaadamu. Mtu wa kwanza pia ni mtume wa kwanza. Kuwa baadhi ya habari zilizoelezwa na dini pia zipo katika utamaduni zinaonesha kuwa zilitokana na ufunuo. Hata hivyo, ufunuo ulisahaulika kadiri wakati ulivyosonga mbele na ilidhaniwa kuwa ilitokana na utamaduni au mtu.
Habari ya Nabii Musa (s.a.w) kuwekwa katika kikapu imetajwa katika aya nyingi. Kisa cha maisha ya Nabii Musa (s.a.w) kinaposomwa, itaonekana waziwazi. Mitume wengi waliishi katika Mashariki ya Kati; kwa hiyo, baadhi ya vidokezi vya habari njema vya dini za Mwenyezi Mungu vinaweza kuwepo katika utamaduni wa ki-Sumeria. Inamaanisha kuwa baadhi ya mitume walioishi kabla ya Musa (s.a.w) walitoa habari njema kuwa angekuja. Kwa hakika, habari njema kuhusu Mtume wetu (s.a.w) upo katika vitabu vitakatifu vilivyotumwa kabla yake.
Baadhi ya watu wasio na imani hutumia maandiko kwa namna hiyo ili kuikana dini. Hata hivyo, Quran inatuambia kuwa hakuna umma ulioachwa bila ya mtume, mwonyaji au mwongozaji. Matukio sawa na hayo katika historia ya dunia yanathibitisha habari hii ya Quran.
Inajulikana kuwa Waarabu wa Zama za Jahiliyya walikuwa na dalili za dini ya Hanif ya Nabii Ibrahim zilizosalia tokea maelfu ya miaka iliyopita. Kuwepo kwa Kaaba, Waarabu wakiizingatia kuwa ni tukufu na walikuwa wakiizunguka, kulingana kwa vitendo vya ibada zao kunazua kusema kuwa hayo yameingizwa kutoka katika dini zingine; kuwepo kwa sheria zenye kufaa heshima ya mwanaadamu au kuwepo kwa maandiko ya kale kuhusu habari za kale ni ushahidi wa kuwepo dini, lakini hayo ni mambo ya kihistoria yaliyopinduliwa na wayakinifu na wakanamungu wanaotumia uyakinifu wa Dajjal.
Ikiwa baadhi ya visa kama cha Nabii Ayyub (s.a.w) – kama vilikuwa ni kweli – vilisimuliwa katika zama za kabla hajaishi, vinaweza kuwa ubashiri mwema kumhusu yeye au vinaweza kuwa na maana ifuatayo:
Huenda wapo wengi waliopata majaribio makubwa kama Nabii Ayyub katika historia. Upambanuzi wa Quran unalenga katika kutoa mifano ya matukio ya kuenea kote na yanawakilisha maisha ya mashujaa wenye subira walioishi na watakaoishi kuwa ni mifano hai ili watu wapate mazingatio.
Kwa kuhitimisha, matukio yanayotajwa na Quran na wahusika katika matukio hayo kwa hakika ni matukio ya kihistoria. Hata hivyo, kunaweza kuwa na matukio mengine yenye kulingana nayo.
Maswali juu ya Uislamu