Je, Unaweza kuthibitisha kuwepo wa Allah kupitia hoja za kiakili?
Submitted by on Fri, 01/03/2019 - 14:57
Dear Brother / Sister,
Kuthibitisha kuwepo kwa kitu ni rahisi kuliko kuthibitisha kutokuwepo kwake. Tunaweza kuthibitisha kuwepo kwa aina ya tufaha kwa kuonesha tufaha moja tu. Hata hivyo, mtu anayedai kwamba aina ya tufaha kuwa haipo anaweza tu kuthibitisha kwa kusafiri duniani kote na hata ulimwenguni kote. Hili ni jambo gumu kabisa takribani ni muhali. Hivyo, tunaweza kusema kutokuwepo kwa kitu hakuwezi kuthibitishwa.
Mambo mawili yaliyothibitishwa hufadhilishwa kuliko maelfu ya mambo ambayo ni ya kukataa na ya kukanusha. Ikiwa watu watakubaliana juu ya ukweli mmoja, ukanushaji wa jambo hilo kwa mawazo ya maelfu ya watu kupitia madirisha yao membamba hauna manufaa.
Ikiwa mageti 999 ya kasri yamefunguliwa na moja wapo limefungwa, hakuna anayeweza kudai ni muhali kuingia ndani ya kasri hilo. Mkanushaji daima hutaka kuonesha geti lililofungwa. Kiukweli hata geti hilo lililofungwa ni kwa ulimwengu wake wa kiroho na wale ambao ni kama yeye kutokana na kizuizi mbele ya macho yao. Hakuna geti lililofungwa kwa muumini labda afumbe macho yake… Licha ya hivyo, mageti 999 yako wazi kwa kila mmoja. Hili hapa ni geti hilo na baadhi ya hoja;
1. Ushahidi wa uwezekano
Ulimwengu huzingatiwa kama jambo lenye kuwezekana. Hiyo ikiwa na maana kuwepo kwake na kutokuwepo kwake ni sawa, ina uwezo wa kuwepo au kutokuwepo. Inapokuwepo, inawezekana kwake kuwepo katika muundo mmoja kati ya yumkini zisizo kuwa na ukomo za kuwepo. Hiyo ni kusema, kisicho kuwepo kina uwezekano wa kuwepo kama ilivyokuwa kilichokuwepo. Kila chenye kuwezekana ni chenye kutegemea sababu nje yake. Na kama hivyo, kuna dhati yenye kuchagua vitu viwepo, kisha hufadhilisha muundo na hali ya kuwepo kutokana na kutokuwepo na kwa miundo mengine yenye kuwezekana pamoja na hali. Na dhati hiyo ni Allah.
2. Ushahidi wa kutokea (kuumbwa baadae)
Ulimwengu unakubali mabadiliko. Ni wenye kuendelea kubadilika. Kila chenye uwezo wa kubadilika kimeumbwa baadaye. Kwa hivyo, jambo haliwezi kuwa la tangu. Ndio, matukio kama mwendo wa kuendelea wa kitu kuelekea katika kutokuwepo kwa mujibu wa sharia ya thermodynamic (Uhusiano wa joto na nishati nyingine), kupanuka kwa kuendelea kwa ulimwengu, na mwendo wa kuendelea wa jua kuelekea kuisha kunaonesha kuwa kuwepo kuna mwanzo. Kila kiumbe ambacho kimeumbwa baadae kina muumbaji; hakuwezi kupatikana kwa taathira bila ya sababu. Na hakuna Sanaa bila ya msanii. Sababu haziwezi kwenda bila ya kuingiliwa daima. Kisha ulimwengu wa maada, ambao ni wenye kuendelea kubadilika ambao si wa tangu, ambao umeumbwa baadaye na ambao unahitaji sababu ya kwanza, unahitaji Muumba. Na muumba huyo ni Allah.
3. Ushahidi wa maisha
Maisha ni ni siri iliyo wazi. Ndio, ni vigumu kuelezeka kupitia sababu zenye kuonekana na macho na ni yenye kuonesha wazi wazi kwa vile yanaashiria nguvu ya muumba. Ndio, moja kwa moja yanamuonesha na kumtangaza muumba. Ni jambo la maajabu lenye kuwashagaza wataalamu kwa usiri wake na watu wa kawaida huwashangaza kwa uwazi wake. Maisha kwa maneno yanasema kwa lugha ya silika ni Allah pekee ambaye ameniumba na amenifanya niwepo”
4. Ushahidi wa nidhamu
Kila kitu kinaendana na sehemu zake; Vivyo hivyo, ulimwengu unafanana na viumbe ambavyo huunda ulimwengu. Hii ni dalili isiyozingatiwa ambayo inatueleza kuhusu kuwepo kwa nidhamu na mfumo na inaonesha mpangaji huyo ni Allah.
5. Ushahidi wa Sanaa
Sanaa nzuri na yenye kuvutia huvuta umakini wa watu kwenye ulimwengu kutoka atomu kwenda kwa mwanadamu na kutoka kwa seli mpaka galaxy. Ndio, kila Sanaa ulimwenguni kote ina sifa zifuatazo;
Ina thamani kubwa ya Sanaa.
Ni yenye thamani sana.
Imetengenezwa ndani ya muda mdogo na kwa wepesi sana.
Ipo kwa wingi.
Ipo aina nyingi.
Ipo kwa kuendelea.
Hata hivyo, vitu ambavyo huonekana kutengenezwa ndani ya muda mdogo, kwa wingi, urahisi, na kwa aina nyingi havipaswi kuwa ni vya kisanaa na vyenye thamani. Hata hivyo, ikiwa anayevitengeneza ni Allah, vitu hubadilika na vitu vilivyokuwa kinyume hukutana.
6. Ushahidi wa hekima na lengo.
Kila kiumbe kina lengo, kusudio, faida, na matokeo, maalumu kwa ajili yake, hakuna kinachoweza kuzingatiwa kama upuuzi, kisicho kuwa na lengo, maana, na chenye fujo kinachoweza kupatikana hata katika kitu kidogo. Hata hivyo, ulimwengu wa maada, ulimwengu wa mimea na wanyama na vitu visivyo na ufahamu wala utambuzi haviwezi kupita katika mnyororo huu wa makusudio. Basi, tunaweza kuzingatiwa kuwa ni wenye akili ikiwa tutaegemeza operesheni ya ufahamu hekima hii na makusudio haya kwa Allah.
7. Ushahidi wa huruma na rehema.
Mahitaji ya viumbe hasa mwanadamu hayana mpaka. Na utashi wao ni takribani haupo. Mahitaji ya wahitaji wote hufikiwa kutoka sehemu zisozotarajiwa bila ya kutarajiwa. Mahitaji ya viumbe wote yanafikiwa katika kiwango wanachohitaji, katika ubora na idadi. Kutumwa kwa msaada na msaada huo kuyafikia mahitaji kama yalivyo kwa uwazi inathibitisha kwamba mahitaji haya yamefikiwa na dhati yanye huruma ambaye yupo karibu na mwanadamau kuliko nafsi yake. Huruma hii na rehema pamoja na riziki ambazo zinafanya kazi ulimwengini kote na ambapo utashi unafanya kazi daima, unatujuza kuhusu na kuthibitisha uwepo wa dhati tukufu, ambaye amejawa na sifa za kufanya kazi hizi zote na ambaye ametakasika na sifa pungufu.
8. Ushahidi wa kusaidiana
Viumbe vyote kutokea yule aliyekaribu na mwenzake mpaka yule aliyembali na mwenzake husaidiana. Aina tofauti ambazo hazina uhusiano zenyewe kwa zenyewe huungana pamoja kana kwamba ni sehemu za kitu kimoja na kusaidiana zenyewe kwa zenyewe. Tunapaswa kufikiri kwamba bakteria, minyoo, udongo huungana pamoja kwa lengo moja na kusaidia mimea; na msaada huu hutokea kwa kurudia rudia. Matendo haya ya viumbe hawa ambayo yanakosa akili na utambuzi na yenye kushangaza akili na utambuzi yanaonesha matendo ya hekima ya uwajibu wa kuwepo nyuma ya pazia. Hiyo ni kusema ulimwengu wote husema “Allah” kwa ulimi wa kusaidiana.
9. Ushahidi wa usafi
Usafi ulimwenguni kote kutoka katika ardhi mpaka mbinguni unatujuza kuhusu dhati pamoja na jina lake la Al-qudus, ni kweli kwa jina lake.
Ndio, bakteria anayesafisha udongo, wadudu, wadudu chungu, ndege wengi wa kuwinda, upepo, mvua, theluji, barafu katika bahari na samaki, hewa angani, mashimo meusi mbinguni, oksijini yenye kusafisha damu katika miili yetu, upepo mwanana wa kiroho ambao huiweka huru roho kutokana na shida vinatueleza kuhusiana na jina la Al-qudus na dhati tukufu nyuma ya jina hilo.
10. Ushahidi wa nyuso
Hebu tuanze na kuiangalia sura ya mwanadamu tu, ambayo ni sifa au kipengele muhimu chenye kumtafautisha mtu mmoja kutokana na wanadamu wengine, kulifanya jambo la aina moja japo kuwa linawezekana kusambazwa kwa viumbe wote.
Uso wa mwanadamu haufanani na uso wa yeyote katika mabilioni ya watu waliowahi kuishi kabla yake kwa namna yoyote. Kanuni hii inafanya kazi pia kwa watu watakaokuja katika mustakabali. Kuchora mabilioni ya picha ambayo hufanana katika upande mmoja lakini tofauti katika upande mwengine katika eneo dogo sana na kutofautisha kila mmoja kati yao kutokana na mabilioni ya picha ambayo ni muhali kuwa kama yeye na kukiweka kila kitu katika muundo wenye njia zisizo kuwa na mpaka za uwezekano ni tangazo lenye nguvu kutoka kwa Allah mtukufu ambaye anakifahamu kwa kina kila kiumbe akiumbacho, ambaye nguvu yake na elimu yake vinatosha kumuunda kiumbe hicho katika namna yoyote aitakayo, hata kwa watu ambao ni viziwi. Ndio, huumba viungo katika uso tofauti kutokana na viungo vyengine katika sura nyengine, kulipatia kila jicho sifa yenye kulitofautisha na macho mengine litamuonesha jambo hilo kila mtu ambaye ana ufahamu dhati ambayo imeviumba na kuvipa hekima isiyokuwa na mwisho.
11. Uthibitisho wa Ushawishi wa Mungu
Bata anapotoka kutoka katika yai, anaweza kuogelea. Wadudu chungu wanatoka kutoka katika kakao na kuanza kuchimba vichuguo mara moja. Nyuki huweza kuzalisha asali, ambayo ni sanaa ya ajabu, haraka sana; buibui inaweza kuunganisha mtandao mzuri sana. Tunaelewa kutokana na mifano ya hapo juu kwamba wao na wanyama wengine hufanya mambo kutokana na kile ambacho hufundishwa katika ulimwengu mwingine na uwezo wao wa kuzaliwa. Hata hivyo, mtu anapaswa kujifunza kila kitu katika ulimwengu huu ingawa yeye ni kiumbe mwenye vipaji na kamilifu. Yaani, dhati ambayo huwapa viumbe wengine sifa hizi sio wenyewe bali ni dhati yenye hekima, ambaye huwapa vipaji hivi.
Watoto wa mkunga ambao mama yao anataga mayai kilomita nyingi mbali mara tu wanapotoka kutoka katika mayai wanawapata mama zao kwa urahisi sana. Tunawezaje kuelezea hilo kama si kupitia motisha ya Mungu? Ikiwa hali hii ya ajabu ambayo tunayoona katika wanyama inaelezwa kama zawadi ya Mwenyezi Mungu, basi inaweza tu kuonekana kama maelezo ya busara na mantiki. Vinginevyo, tafsiri nyingine yoyote inazingatiwa kama upuuzi.
12. Ushahidi wa roho na dhamiri
Njia ambayo roho yetu, ambayo hakuna mwenye mashaka juu ya kuwepo kwake hata hivyo asili yake halisi haijulikani, ni miongoni mwa shuhuda zenye kutueleza kuhusu Allah mtukufu. Dhati yenye kuwakilisha ulimwengu wa nidhamu duniani ni roho na imekuja katika dunia hii kwa ajili ya kupiga hatua na kuwa bora. Taathira ya hekima katika matokeo si maudhui yetu, tunaona sahihi kutaja nukta inayoashiria tu. Ukweli wa kwamba roho ambayo haina uhusiano na ulimwengu wa kimaada katika asili yake, imeletwa katika dunia hii kutoka katika ulimwengu wake kwamba ni yenye kukomaa hapa na kwamba iliyofanywa kupitia programu ni moja kati ya ushahidi muhimu wenye kutangaza kuwepo kwa Allah mtukufu.
Kwa upande mwingine, hisia ya ziada ndani ya mwanadamu, kurejea kwa Mola pale panapokesekana sababu ya wazi wazi, na kukariri kwa matukio yenye kufanana mara milioni kunathibitisha kwa uwazi kwamba dhamiri, ambayo imewekwa ndani ya mwanadamu na ambayo ni njia ya kumtambua Allah, kwa mapenzi ipo katika mapenzi na Muumba wake na inawasiliana naye kikamilifu. Licha ya hivyo, je dhamiri si shahidi wa kweli wa siku ya Alastu? Dhamiri inasema “Allah” kupitia ulazima wa haki ya ushahidi huu?
13. Ushahidi wa asili na historia
Kuwepo kwa mapenzi ndani ya kila mtu kwa uzuri na kuwepo kwa hisia ya chuki kuelekea ubaya ni ukweli ambao hakuna awezaye kukana. Kwa kutenda kimaadili na kufanya matendo mazuri na asili yao ya kuepuka tabia mbaya na matendo mabaya, hisia hizi zinaonesha kuwa dhati inayomuamuru mtu kutenda jema na mambo mazuri na inayomuamuru kuepuka baya na matendo mabaya ni dhati hiyo hiyo inayompa hisia hizi. Dhati hii bila ya shaka ni Allah.
Historia ya dini inashuhudia kwamba ubinadamu haukuwahi kuwa na kipindi bila ya dini. Daima waliamini juu ya dini hata kama ilikuwa ni ya kipuuzi na walifuata mfumo wa kiroho. Licha ya hivyo, Imani ni lazima kwa sababu ipo katika asili ya mwanadamu. Dhati iliyoweka haja hii katika asili ya mwanadamu ndiyo dhati hiyo hiyo yenye kutuamuru kuamini. Dhati hii ni Allah.
14. Ushahidi wa hisia
Mwanadamu amepewa maelfu ya hisia. Kila hisia ina asili ya kubeba ujumbe kutoka katika ulimwengu zaidi ya ulimwengu wa maada. Hata hivyo, mwanadamu ana hisia nyingine inayomueleza kuhusu Allah mtukufu moja kwa moja. Hisia hii ni hisia ya umilele na kutokuwa na mpaka. Kwa hisia hii mwanadmau daima hujitahidi na kufanya kazi kwa ajili ya umilele. Hakuna kilicho na mpaka chenye kumtosheleza kwa ukamilifu. Na hisia hii haiwezekani kupewa mwanadamu kupitia taathira ya dhati nyingine inayokufa. Hakuna katika sababu zenye kufa zenye kuweza kuwakilisha kinywaji cha umilele. Hata hivyo, kuwepo kwake ni ukweli; ni muhali kuukana. Hivyo, hisia hii tumepewa na dhati ambayo imetuumba pamoja na hisia hiyo. Dhati itakayotupa maisha ya milele pia ni dhati hiyo.
15. Ushahidi wa Makubaliano
If ten liars came to us and said that our house was on fire, we would believe them saying "perhaps" though we had never heard them telling the truth. For, there is a case of agreement. However, the agreement that we mention is an agreement formed by thousands of prophets, hundreds of thousands of saints, and millions of believers. The first point that these people who lived at different times and in different places agree on is the reality, “Allah exists”. How can a person who believes the lie that ten liars agree on but does not believe the agreement of the prophets, who never told lies, and millions of saints be called a human? How can he be called sane?
Ikiwa waongo kumi watatujia na kusema kuwa nyumba yetu inaungua, tungeliwaamini tukisema “huenda” japokuwa hatukuwahi kuwasikia wakisema ukweli. Kwakuwa kuna jambo la makubaliano. Hata hivyo, makubaliano tuliyoyataja ni makubaliano yaliyoundwa na maelfu ya mitume, mamia ya maelfu ya mawalii, na mimilioni ya waumini. Nukta ya kwanza wanayokubaliana watu hawa waliyoishi muda tofauti na sehemu tofauti ni uhalisia wa kuwa, “Allah yupo”. Vipi aitwe mwanadamu mtu awezaye kuamini uwongo wanaokubaliana waongo kumi na haamini makubaliano ya mitume, ambao hawakuwahi kusema uwongo, na mamilioni ya mawalii? Vipi aitwe mwenye akili?
16. Ushahidi wa Qur’an
Shuhuda zote zenye kuthibitisha kwamba Qur’an ni maneno ya Allah pia zinathibitisha kuwepo kwa Allah mtukufu. Kuna mamia ya shuhuda zenye kuthibitisha kuwa Qur’an ni maneno ya Allah na zimeelezwa kwa kina katika marejeo ya Qur’an kuhusu jambo hilo. Tunarejesha ushahidi wa jambo hilo katika kazi hizo. Ndiyo, shuhuda zote zinasema kwa ndimi zenye kuendana nazo, “Allah yupo”.
17. Ushahidi wa mitume
Shuhuda zote zenye kuthibitisha utume wa mitume na hususan utume wa Hz. Muhammad (s.a.w) zinapaswa pia kuingizwa katika shuhuda zenye kumuashiria Allah mtukufu. Kwakuwa lengo la kuwepo kwa mitume ni umoja, yaani, kutangaza kuwepo na umoja wa Allah. Kisha, shuhuda zenye kuthibitisha utume wa kila mtume pia zinathibitisha kuwepo kwa Allah. Hata hivyo, Kuorodhesha shuhuda zenye kuthibitisha utume wao ni nje ya mada kwa sasa; Hatutataja mmoja baada mwingine. Tunaona ni sahihi kusema kwa sasa kuwa shuhuda zote zenye kutangaza kwamba mtume ni mtume wa kweli zinasema kwa nguvu zaidi kuwa Allah yupo na ni mmoja.
Shuhuda za kimantiki kuhusu kuwepo kwa allah
1. Ikiwa gari linasukumwa na gari lingine, ni nani anayeliongoza la kwanza? Basi, lazima kuwe na muumba wa ulimwengu huu.
2. Hata herufi haiwezi kuwepo bila ya mwandishi; vipi tufikiri wanadamu na ulimengu kuwa bila ya mmiliki? Kwa kuongezea, Mmiliki yeyote wa kitu chochote hawezi kufanana na kitu anachokitengeneza. Kwa mfano, aliyetengeneza saa hafanani na saa, na mwandishi hafanani na herufi. Na kama hivi, Muumba anayetuumba sisi na ulimwengu hapaswi kufanana na sisi na ulimwengu.
3. Je, kukana kuwepo kwa Allah kunaweza kutupa faraja? Kinyume chake, ufahamu huu utatupeleka chini kwenye shimo la kina . Kwanini, kwa ajili gani, vipi, kwa ajili ya nani tunaishi? Nini kitatokea baada ya sisi kufariki? Kama hakuna maisha mengine, wapi tunaweza kupata itikio la hisia ya kutokuwa na ukomo na kutamani kuishi milele? Katika hali hiyo, kwanini tumepewa hisia hizi?
Sayansi zinamzungumziaje Allah?
Uislamu hauendi kinyume na sayansi katika jambo olote; kinyume chake, unahimiza sayansi. Vyanzo wa kidini vimejaa mifano ya haya. Kuna vitabu viwili vya Allah mtukufu; kimojwapo ni Qur’an, ambacho kinakuja kutokana na sifa yake ya kuongea, kingine ni ulimwengu, ambacho kinakuja kutokana na sifa yake ya Nguvu.
Wanasayansi wawe wanamwamini Allah au la, wanasoma kitabu cha ulimwengu na kufasiri Sanaa za Muumba kama wafanyakazi wanaofanya kazi bila ya kumjua anayemiliki shamba! Kila tawi la sayansi, kwa ulimi wake wa kipekee, daima unamtaja Allah. Kwa mfano, sayansi ya mimea inatueleza asili ya miti. Inaonesha namna miti inavyopokea chakula kutoka katika udongo, namna inavopeleka katika majani, na namna matunda yanavyoundika, na namna ukuaji unavyopatikana. Katika njia hii, tunaweza kugundua mashine nzuri yenye seli, mizizi, stem, matawi, majani, maua na matunda. Licha ya hivyo, ni kitu chenye uhai.
Sasa hebu tufikiri kwa makini: Vipi kitu kama udongo ambao hauna akili, haujielewi, hauna elimu, utashi na nguvu utengeneze mashine hii ya ajabu? Ambapo mtaalamu wa sayansi ya mimea hawezi kutengeneza hata jani moja la mti katika maabara kubwa, vipi mti uweze, katika maneno mengine mbao, kutengeneza maua na matunda haya ya kimaajabu? Je, kila mti na maajabu ya uumbwaji wake, haumuoneshi mmoja ambaye hana mpaka pamoja na majina na sifa zake?
Pia sayansi ya wanyama imefungua katika hoja zetu milango ya ulimwengu wa ndani wa mnyama. Tumefahamu kuwa kila mnyama ni mmea wa kimaajabu. Mdudu mwenye sumu hutengeneza asali. Mdudu asiye na mikono anatoa hariri; kondoo asiye na ulimi anatoa maziwa. Sayansi imetuonesha kwamba sio kazi ya kondoo asiye na akili kutengeneza chakula kizuri; kwa kutaja, maziwa kutokana na nyasi na maji. Kondoo, nyuki, mdudu hariri, na wanyama wote kama wao ni zana kama brashi ya mpaka rangi, kalamu ya mwandishi, nyundo ya seremala. Bila ya shaka mtendaji wa tendo la uumbaji ni Mola wetu, Mmiliki wa uliwengu huu.
Kwa kuangalia kupitia dirisha la sayansi ya anga, tumegundua nafasi ya dunia katika sehemu ya nje: ndege kubwa yenye kuruka kulizunguka jua kwa kasi. Haina mbawa wala mashine, na ni kubwa mno na japo inaruka bila ya rubani, inazunguka kwa ukimya bila ya kelele. Na bado katika dunia hii, wasafiri husafiri kwa amani na bila ya kusumbuliwa. Mara nyingi, hawajui kama wanaruka. Kwa upande mwingine, dunia huzunguka katika njia yake. Usiku na mchana na misimu ni mazao ya mzunguko huu na mageuko. Ni hatari tukikaribia katika jua au tukiwa mbali nalo. Si dunia tu yenye kuzunguka jua; sayari nyingine pia hufanya mzunguko kama huo. Ni jambo rahisi kwa dunia kugongana na moja wapo. Hata hivyo, hatuoni kosa lolote, na kila kitu kipo sawa. Mfumo huu haujabadilika kwa mamilioni ya miaka.
Je, haiwi lazima kwa mwanafunzi yeyote wa sayansi ya anga kufikiri juu ya haya na kutafuta majibu ya maswali yafuatayo?
Nani ameweka uwiano huu? Nani ameifanya dunia kuwa sehemu ya kuweza kuishi? Wakati ambao baadhi ya ndege zinaweza kugongana japokuwa zina rubani, ni elimu gani na nguvu iwezayo kuvifanya vitu hivi kuzunguka na kuruka bila ya kugangana?
Zaidi ya hayo, kuna kiumbe baina ya viumbe, ni muujiza wa kushangaza; tunamwita mwanadamu.
Anafikiria, anajenga taswira, anatafuta, anafahamu, anapenda, anahurumia na kuchukia…. Amepewa maelfu ya uwezo. La muhimu zaidi ni mwenye utambuzi wa kuwepo kwake. Ulimwengu umeangaziwa kwa ufahamu wake. Licha ya roho yake, moyo, akili na taswira, muundo huu wa kimaada hai mzuri pia ni kiwango cha juu cha Sanaa; macho mazuri, mikono mizuri, nywele nzuri, muundo uliyo katika uwiano, urefu wa wastani, kwa ufupi, amepewa vizuri zaidi katika kila kitu.
Imefahamika kwa sayansi ya udaktari kuwa sehemu za ndani za mwili wa mwanadamu pamoja na sehemu zake za nje ni za maajabu. Ni kazi kubwa ya Sanaa ya pekee kwa moyo wake unaosukuma toni za damu, na tumbo lake lenye kumengenya chakula kwa wepesi, na mapafu yake ambayo ni mashine ya kusafisha damu, na mishipa ambayo ni yenye kupimwa kwa kilomita, na kuendelea… wakati sanamu humuonesha mchongaji wake, je inawezekana kwa mwili wa mwanadamu ambao uzuri wake umefahamika na sayansi ya matibabu usioneshe mmiliki wake?
Na kama hivi, japo wanasayansi wa sayansi hizi hawarejeshi vyanzo vya sayansi hizi kwa Muumba, kila tawi la sayansi, kwa ulimi wake wa pekee, daima unamtaja Allah. Katika hali hiyo, ni lazima kusikiliza matawi haya ya sayansi.
Maswali juu ya Uislamu