Je, unaweza kutoa maelezo ya kina kuhusu kuwepo kwa Allah?

The Answer

Dear Brother / Sister,

Mamia ya dalili zenye kubainisha kuwepo na umoja wa Allah zimetajwa katika Quran.

Kwa mfano, “Je! Hawamtazami ngamia jinsi alivyo umbwa? Na mbingu jinsi ilivyo inuliwa?  Na milima jinsi ilivyo thibitishwa? Na ardhi jinsi ilivyo tandazwa? (al-Ghashiya, 17-20)

Mwanadamu ameamrishwa kuangalia viumbe vilivyomzunguka kwa makini na kumfahamu na kumtafuta muumba wa viumbe hivyo kwa kuviangalia. Katika baadhi ya aya imeelezwa kwamba ni muhali kwa watu wenye kuona viumbe kukanusha kuwepo kwa Allah.

Aya na maana yake:

“Hakika katika kuumbwa kwa mbingu na ardhi, na kukhitalifiana usiku na mchana, na marikebu ambazo hupita baharini kwa viwafaavyo watu, na maji anayo yateremsha Mwenyezi Mungu kutoka mbinguni, na kwa hayo akaihuisha ardhi baada ya kufa kwake, na akaeneza humo kila aina ya wanyama; na katika mabadiliko ya pepo, na mawingu yanayo amrishwa kupita baina ya mbingu na ardhi, bila shaka zimo Ishara kwa watu wanao zingatia.” (al-Baqara, 164).

Katika aya nyingine maana kama hiyo imeashiriwa:

 “Na ukiwauliza; Nani aliye umba mbingu na ardhi na akafanya jua na mwezi kuti'ii amri yake? Bila ya haka, watasema: Mwenyezi Mungu. Wapi basi wanako geuzwa? (Al-Ankaboot, 61).

Na ukiwauliza ni nani aliye waumba? Bila ya shaka watasema: Mwenyezi Mungu! Basi ni wapi wanako geuziwa?

Kwa vile vitu vipo na vipo katika Sanaa ya hali ya juu bila shaka vina muumbaji na mtengezaji. Ulimwengu unaweza kufananishwa na kitabu chenye maana katika muktadha huo na unaweza pia kufananishwa na mji mzuri uliokamilika katika muktadha mwingine na pia unaweza kufananishwa na kazi ya Sanaa iliyokuwa nzuri katika muktadha mwingine pia. Kama ilivyokuwa kitabu kina mwandishi pia kitabu cha ulimwengu kina mwandishi. Na yeyote atakayekuwa mwandishi wa kitabu hicho yeye pia ni mwandishi wa kila herufi. Yeyote atakaye kuwa muumbaji wa ulimwengu basi yeye pia ni muumbaji wa viumbe vyote, kutoka atomu mpaka sayari za kitabu cha ulimwengu. Kwa hivyo, mmiliki wa ulimwengu ndiye mmiliki wa viumbe vyote ndani yake, Yeyote mwenye kumiliki shamba humiliki na mazao pia. Yeyote ambaye ni mtengenezaji na muumbaji wa mti humiliki matunda yake pia. Ikiwa ulimwengu ni mti, basi mwanadamu, ambaye ni tunda la mti huo ni kazi yake Allah. Ambaye hawezi kuumba mti hawezi kuumba tunda lake pia. Hivyo, yeyote ambaye ni muumbaji wa ulimwengu ni muumbaji wa mwanadamu pia.

Allah ambaye ameliumba jicho la mwanadamu na akalipa uwezo wa kuona, ameumba jua pia. Jicho lisingeweza kuona kama jua lisingekuwepo. Kwa hivyo, ambaye ameliweka jicho katika uso wa mwanadamu ndiye huyo huyo aliyeliweka jua, ambalo ni jicho la mbingu, sehemu yake.

Kama ilivyokuwa kuna mtengenezaji wa pini vivyo hivyo kutakuwa na mtengenezaji na msanii wa viumbe vyote. Kila kimoja kati ya hivyo ni kazi ya Sanaa iliyo mahiri, ulimwenguni.

Kama ulimwengu utafananishwa na mji mzuri, kuna mkuu wa mji katika kila mji; vivyo hivyo, kutakuwa na mkuu wa mji katika mji huu wa ulimwengu, ambao upo katika mfumo na nidhamu, ambao unawekwa safi na upo chini ya uangalizi. Na huyo anayeweza kuwa hivyo ni Allah pekee.  

Akili na maarifa ya mwanadamu yanakubali kuwepo kwa muumbaji, na elimu inalithibitisha hilo. Pale tunapokiingiza kiumbe hai katika mazingatio;

  • Sababu huenda zikawa zimekiunda.
  • Kuimbe hiki yawezekana kimejiunda chenyewe.
  • Asili huenda imekiunda.
  • Au dhati tukufu huenda ikawa imekiumba kitu hicho.

Hakuna njia nyengine ya kiumbe kuja katika kuwepo zaidi ya hizo zilizotajwa hapo juu. Inaweza kuelezwa kwa mfano wa famasia kwamba njia tatu za mwanzo ni muhali kiakili na kielimu na njia ya mwisho inalazimisha kuwepo kwa Allah:

"Fikiria kuna duka la dawa ambalo kuna mamia ya chupa zinazojazwa vitu tofauti kabisa. Mchanganyiko hai na dawa hai huhitajika kutoka kwa dawa hizo. Kwa hiyo tunaenda kwa maduka ya dawa na kuona kwamba zinapatikana huko kwa wingi, na kwa aina nyingi. Sisi tunachunguza kila moja ya kati ya michanganyiko na kuona kwamba viungo vimechukuliwa kwa kiasi tofauti lakini sahihi kutoka kila chupa, wakia moja kutoka kwa hii, tatu kutoka ile, saba kutoka kwa nyingine, na kadhalika. Ikiwa wakia moja imezidi au kupungua kwa kupunguzwa, mchanganyiko usingekuwa hai na usingeonyesha sifa yake maalum. Kisha, tunajifunza dawa hai. Tena, viungo vimechukuliwa kutoka kwenye chupa nyingi kwa kipimo maalum ili kwamba ikiwa hata kiasi kidogo kabisa au chache kidogo kimechukuliwa, dawa hiyo ingekuwa imepoteza sifa yake maalum. Sasa, ingawa chupa ni zaidi ya hamsini, viungo vimechukuliwa kutoka kwa kila moja ambazo ni tofauti kulingana na vipimo na kiasi. Je, kwa namna yoyote inawezekana au huenda kwamba chupa kuwa zimegongwa na bahati mbaya ya ajabu au upepo wa ghafla na kwamba kiasi sahihi tu, ingawa tofauti, ambacho kilichochukuliwa kutoka kila moja kuwa ndicho kilichomwagika, na kisha kujipanga wenyewe na kuja pamoja ili kuunda dawa? Je, kuna upotovu, muhali na upuuzi kuliko huu?

Vivyo hivyo, kila kiumbe hai anaweza kulinganishwa na dawa za uzima kwa mlingano wa hapo juu, na kila mmea unalingana na dawa ya uzima; zimeundwa na kitu ambacho kimechukuliwa kwa kipimo sahihi kabisa kutoka kwa vitu mbalimbali. Ikiwa hizi zinahusishwa na sababu na elementi na inadaiwa, "Sababu zimeunda hizi," ni kinyume na akili, haiwezekani na ni upuuzi mara mia moja zaidi, kama vile kudai kuwa dawa katika duka la dawa imekuja kuwepo kwa njia ya ajali." (Nursi, B. Said. (Lem’alar) Flashes. Rnk Neşriyat. Istanbul, 2006, p.2002 etc.)

Sasa hebu tutumie mfano huo kwa mwanadamu, mnyama au mmea. Matofali ya kiumbe hai huyu ni seli. Seli hizi huungana pamoja katika idadi maalum na huanzisha tishu tofauti, na tishu huasisi viungo, mifumo na mwisho kiumbe huja katika kuwepo. Kuna maelfu ya molekuli tofauti hata katika seli ya umbile jepesi zaidi, kila moja ya molekuli hufanya kazi tofauti. Elementi za msingi zipo katika seli zote; Hata hivyo, seli tofauti, nafsi tofauti na mwisho hata aina tofauti hudhihiri kwa mipangilio tofauti ya idadi tofauti ya elementi hizo. Kwa mfano, kuundwa kwa viumbe kama nyuki na wadudu chungu ni muhali kutokana na elementi hizo ambazo si zenye akili si zenye kujielewa, pofu, ziwi, na jinga, zenyewe au kwa kushirikiana na sababu kama upepo au kimbunga; Kwa sababu elementi na sababu zenyewe huhitaji kuundwa.

Dawa zilizo andaliwa katika famasia kwa idadi sahihi huonesha mkemia bingwa au mfamasia ambaye amezitengeneza. Vivyo hivyo, uumbaji wa kila kiumbe hai huonesha kuwepo kwa muumbaji mahiri, anayejua, kuona, na ana ufahamu na hekima.

Maswali juu ya Uislamu

Author:
Maswali juu ya Uislamu
Subject Categories:
Read 816 times
In order to make a comment, please login or register
MASWALI YENYE KUFANANA