Kafiri ni nani? Ni sababu zipi zinazompelekea mtu katika Ukafiri?

The Answer

Dear Brother / Sister,

Neno kafir (Kafiri) hutumika kumaanisha mtu anayeukanusha Uislamu, anayeonesha kutoshukuru neema, anakuwa mbali, anakwepa na kufunika. Kama neno, linamaanisha mtu asiye na Imani.

Mtu anayekanusha Qur’an, Uislamu, na Hz. Muhammad anaitwa kafiri. Kwa kweli, hilo limeelezwa katika aya ambapo Mayahudi wanaalikwa katika Uislamu.

 “Na aminini niliyo yateremsha ambayo yanasadikisha mliyo nayo, wala msiwe wa kwanza kuyakataa...” (al-Baqara, 2/41)

Kwa kweli, katika aya hizi, kumkana Allah huzingatiwa ni ukafiri pamoja na kumshirikisha na wengine, kuamini kwamba Allah ana mtoto na kukana moja kati ya sifa zake kwa makusudi.

Hilo limeelezwa kuhusu Mayahudi na Wakristo kudondokea katika hali ya ukafiri kwa Imani zao potofu.

 “Hakika wamekufuru walio sema: Mwenyezi Mungu ni Masihi mwana wa Maryamu. Sema: Ni nani mwenye kumiliki cho chote mbele ya Mwenyezi Mungu ikiwa Yeye angetaka kumuangamiza Masihi mwana wa Maryamu, na mama yake, na wote waliomo katika ardhi? Na mamlaka ya mbingu na ardhi na vilivyomo ndani yake ni vya Mwenyezi Mungu. Huumba apendavyo. Na Mwenyezi Mungu anao uweza juu ya kila kitu.” (al-Maida, 5/17)

 “Hakika wamekufuru walio sema: Mwenyezi Mungu ni Masihi mwana wa Maryamu! Na hali Masihi mwenyewe alisema: Enyi Wana wa Israili! Muabuduni Mwenyezi Mungu, Mola wangu Mlezi na Mola wenu Mlezi. Kwani anaye mshirikisha Mwenyezi Mungu, hakika Mwenyezi Mungu atamharimishia Pepo, na mahala pake ni Motoni. Na walio dhulumu hawatakuwa na wa kuwanusuru.” (al-Maida, 5/72).

 “Kwa hakika wamekufuru walio sema: Mwenyezi Mungu ni wa tatu wa Utatu. Hali hakuna mungu ila Mungu Mmoja.” (al-Maida, 5/73).

Kwamba Imani ya kiungu ya Mayahudi na Wakristo iliyokusanya kuwaiga wakanaji imetajwa kama ifuatavyo:

Na Mayahudi wanasema: Uzeir ni mwana wa Mungu. Na Wakristo wanasema: Masihi ni mwana wa Mungu. Hiyo ndiyo kauli yao kwa vinywa vyao. (katika hili) Wanayaiga maneno ya walio kufuru kabla yao.” (at-Tawba, 9/ 30).

Katika aya za hapo juu, hali ya itikadi potofu au ukanaji inayolazimu ukafiri kuhusu Allah zimeamuliwa. Kwa hivyo, kumkana Allah, kumshirikisha, kuamini kwamba Allah ana mtoto, kukana moja ya sifa zake kwa makusudi humpelekea mtu kwenye ukafiri. Kumshirikisha ni ukafiri mkubwa zaidi. Kwa kuwa Allah hana washirika. Allah anajielezea kama ifuatavyo: katika surat al Ikhlas:

 “Sema: Yeye Mwenyezi Mungu ni wa pekee. Mwenyezi Mungu Mkusudiwa. Hakuzaa wala hakuzaliwa. Wala hana anaye fanana naye hata mmoja.” (al-Ikhlas, 112/1-

Kwamba kumshirikisha Allah kumeekwa mbali na msamaha kunaelezwa kama ifuatavyo:

 “Hakika Mwenyezi Mungu hasamehe kushirikishwa, nahusamehe yaliyo duni ya hilo kwa amtakaye. Na anayemshirikisha Mwenyezi Mungu basi hakika amezua dhambi kubwa.” (an-Nisa, 4/48).

Kwa upande mwingine, hakuna shaka kwamba mtu anayeacha shirki, na kutubu, akaomba msamaha na kuimarisha itikadi yake anaweza kusamehewa. Kwa kuwa, mtu kama huyo amewekwa huru kutokana na sifa ya ushirikina na huzingatiwa kuwa ni muumini.

Kumuelezea Allah kwa namna ambayo haikubaliani na utukufu wake, kuzifanyia dhihaka sifa zake au amri zake, kumuhusisha na upungufu humfanya mtu atoke katika dini ya uislamu. (al-Fatawa'l-Hindiyya, Bulaq 1310, II, 258).

Kwa mujibu wa Abu Hanifa (d. 150/767), Sifa za Allah ni qadim (bila ya mwanzo); hazikuumbwa baadaye. Kwa hivyo, kusema kwamba sifa zake ziliumbwa baadaye na kuwa na shaka kuhusu jambo hilo humfanya mtu atoke katika dini ya Uislamu (Ali al-Kari, Sharhu'l-Fikhi'l- Akbar, Egypt 1323 h. p. 22).

Kwa mujibu wa Imam Shafii, Malik na Ahmad bin Hanbal, mtu anayekana elimu kwa Allah anakuwa kafiri.  (Ibn Taymiyya, Majmau'l Fatawa, Riyad 1381-1386 h. XXIII, p. 349)

Kwa upande mwingine, mtu anayekata tamaa katika huruma ya Allah na anayeamini kwamba bila ya shaka hataadhibiwa na Allah anakuwa kafiri, Allah mtukufu anasema yafuatayo katika Qur’an.

 “Hakika hawakati tamaa na faraji ya Mwenyezi Mungu isipo kuwa watu makafiri.” (Yusuf, 12/87),

 “Sema: Enyi waja wangu walio jidhulumu nafsi zao! Msikate tamaa na rehema ya Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu husamehe dhambi zote. Hakika Yeye ni Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu.” (az-Zumar, 39/53).

 “Je, wamejiaminisha na mipango ya Mwenyezi Mungu? Kwani hawajiaminishi na mipango ya Mwenyezi Mungu ila watu wenye kukhasiri.” (al-A'raf, 7/99).

Mtu mwenye itikadi potofu kama hiyo anakuwa muislamu pale atakapotamka kalima at-tawhid au kalima ash-shahada. Hz. Mtume amesema yafuatayo katika hadithi: “Nimeamrishwa kupambana na watu hadi waseme La ilaha illallah (Hakuna Mola ila Allah), watakapo tamka hayo, watalinda damu zao na mali zao kutokana na mimi isipokuwa katika baadhi ya hali. Ni juu ya Allah nini cha kuwafanya baada ya hapo." (ash-Shawkani, Naylu'l-Awtar, VII, 197,ffd.; Zaylai, Nasbu'r-Raya, III, 379).

Ni ukafiri kutokubali taasisi ya utume au kukana utume hata wa mtume mmoja. Kwa hivyo, Mayahudi, wanaowakubali mitume wengine kama mitume wa Allah lakini si Hz. Isa (Yesu) na Hz. Muhammad, na Wakristo, wasiyokubali utume wa Hz. Muhammad, ni makafiri. (Ali al-Kari, ibid, p. 50; al-Fatawa'l Hindiyya, II, 263; al-Ghazzali, al Iqtisad, Egypt, nd. p. 112).

Wale wanaokana taasisi ya utume hawawi waislamu kwa kutamka kalima at-tawhid, yaani, kwa kusema, “Hakuna mola ila Allah”. Wanalazimika kuongeza kalima ash-shahada (Nashuhudia kwamba Hz.Muhammad ni mja na mtume wa Allah). Kwa wafuasi wa dini nyingine kama Mayahudi na Wakristo, kwa kuongezea kutamka kalima ash-shahada kwa kuamini, ni lazima kusema kwamba hawana uhusiano na dini zilizotangulia. Haitoshelezi kwa watu hao kusema, “Mimi ni muumini; Mimi ni muislamu; Nimeamini; Nimekuwa muislamu.”

Kwa kuwa, wanaweza kutamka maneno haya na huku bado wanaendelea kubaki katika dini zao. Katika hali kama hiyo, aina ya mtu ambaye ni myahudi na muislamu au mtu ambaye ni mkristo na muislamu atatokea, jambo ambalo haliendani na kiini cha uislamu. (azl-Zuhayli, al-Fiqhu'l-Islami wa Adillatuhu, Damascus, 1404/1984, VI, 427).

Pia ni ukafiri kunasibisha sifa ya uungu kwa mtume. Kwa kweli, Wakristo huzingatiwa kuwa ni makafiri kwa sababu wanasema Hz. Isa ni mtoto wa Allah. (angalia al-Maida 5/17, 72).

Ni ukafiri kukana Qur’an yote, sura yake moja, aya yake moja, au hata sharia moja, amri na katazo lake. Ni ukafiri kukana neno moja ambalo kwa maafikiano lipo katika Qur’an, na namna ya usomaji ambao hauna shaka kwa maafikiano; ni ukafiri kuongeza kitu katika Qur’an, pia. Pia ni katika vitu vinavyomfanya mtu atoke katika Uislamu, kuifanyia dhihaka, dharau, mzaha Qur’an, sura au hata aya ya Qur’an. (Ali al-Kari, ibid, p. 151; al-Fatawa'l Hindiyya, II, 266; A.Saim Kılavuz, İman Küfür Sınırı, İstanbul 1982, p. 114-115).

Katika Uislamu, mambo ya Imani huzingatiwa ni kitu kimoja. Kukana moja kati ya misingi ambayo ni lazima kuamini maana yake ni kukana yote. Haiwezekani kabaki kuwa muislamu kwa kumtenganisha Allah na mtume wake na kwa kuamini sehemu moja ya Qur’an na kukana sehemu nyingine. (al-Baqara, 2/85). Hayo yameelezwa katika Qur’an:

Hakika wale wanao mkataa Mwenyezi Mungu na Mitume wake, na wanataka kufarikisha baina ya Mwenyezi Mungu na Mitume wake, kwa kusema: “Wengine tunawaamini na wengine tunawakataa.” Na wanataka kushika njia iliyo kati kati ya haya. - Hao ndio makafiri kweli. Na tumewaandalia makafiri adhabu ya kudhalilisha” (an-Nisa, 4/150 151).

Kwa aya ya hapo juu, Allah anawatisha Mayahudi na Wakristo wanaomkana Yeye na mitume wake. Kwa kuwa wanamtenganisha Allah na mitume wake kuhusu Imani. Wanaamini baadhi ya mitume na kuwakana wengine. Ni mitazamo isiyo na mashiko inayotokana na waham na kuwakuta wazee wao na Imani hiyo, na hisia zao. Kwa hivyo, Mayahudi hawakumuamini Hz. Isa na Hz. Muhammad. Wakristo hawakumkubali Hz. Muhammad, aliyekuja baada yao.

Hata hivyo, kuamini taasisi ya utume inalazimu kuamini juu ya mitume wote walioletwa na Allah duniani. Mayahudi waliyoishi Hijaz kipindi cha kuja kwa Uislamu walikuwa na wivu kuhusu ukweli kuwa Hz. Muhaamad ametumwa kama mtume mkuu; hivyo, walimkataa, wakamkana, na kupigana naye kipindi alichokuwepo Madina. Hata hivyo, walishindwa na kutolewa eneo la Hijaz baadaye. Kuwaadhibu kwao, kuwakandamiza na hata kuwaua mitume waliyotangulia kunaelezwa kama ifuatavyo katika Qur’an:

“Na mlipo sema: Ewe Musa! Hatuwezi kuvumilia chakula cha namna moja tu, basi tuombee kwa Mola wako Mlezi atutolee vile vinavyo mea katika ardhi, kama mboga zake, na matango yake, na saumu zake, na adesi zake, na vitunguu vyake. Akasema: Mnabadili kilicho duni kwa kilicho bora? Shukeni mjini, huko mtapata mlivyo viomba. Na wakapigwa na unyonge, na umasikini, na wakastahili ghadhabu ya Mwenyezi Mungu. Na haya ni kwa sababu walikuwa wakiyakataa maneno ya Mwenyezi Mungu, na wakiwaua Manabii pasipo haki. Hayo ni kwa walivyo asi na wakapindukia mipaka. (al- Baqara, 2/61).

Umma wa kiisalimu unaamini juu ya mitume wote waliyoletwa na Allah mtukufu duniani, majina yao yawe yametajwa katika Qur’an au la. Kwa hivyo, ni wajibu wa Imani katika Uislamu kuamini Hz. Daud, Hz. Musa, Hz. Isa, ambao ni mitume wa mbinguni kabla ya Uislamu. Na kwamba asili ya vitabu vyao, ambavyo havikupotoshwa, ni vitabu vilivyoteremshwa na Allah. Muislamu anayemkana mmoja kati yao, kwa mfano, utume wa Hz. Isa au Injili, aliyoteremshiwa, anatoka  katika Uislamu. Ina maana itikadi ya Uislamu ina sifa za kiulimwengu. Inakusanya muundo wa asili wa Uyahudi na ukristo usiyopotoshwa. Licha ya hivyo, aya nyingi katika Qur’an zinatujuza kuhusu mabadiliko yaliyofanywa kwenye Injili na Tawrat baadaye na ushirikina na Imani potofu zilizoingizwa katika dini hizi. Tunaweza kutoa aya ifuatayo kama mfano ili kuliweka wazi jambo hilo:

“Hakika wamekufuru walio sema: Mwenyezi Mungu ni Masihi mwana wa Maryamu! Na hali Masihi mwenyewe alisema: Enyi Wana wa Israili! Muabuduni Mwenyezi Mungu, Mola wangu Mlezi na Mola wenu Mlezi. Kwani anaye mshirikisha Mwenyezi Mungu, hakika Mwenyezi Mungu atamharimishia Pepo, na mahala pake ni Motoni. Na walio dhulumu hawatakuwa na wa kuwanusuru.” (al-Maida, 5/72).

Ni ukafiri kukana amri na makatazo yaliyotajwa katika Qur’an au hadithi na hakuna migogoro kuhusu mambo hayo. Kuzingatia makatazo kama ulevi, kamari, uasharati, ni halali ni moja ya mfano wa ukafiri. Hata hivyo, kutenda yaliyo haramu ambayo ni madhabi makubwa humfanya mtu atoke katika uislamu au la ni jambo lililojadiliwa na wanazuoni katika karne ya kwanza ya uislamu. Imepokelewa kutoka kwa Ibn Omar (r.a) kwamba kuna dhambi kuu tisa. Ni kama zifuatazo: Kumshirikisha Allah, kumuua mtu kwa dhulma, kumsingizia mwanamke mwema kwamba amezini, kukimbia vita, kufanya uchawi, kuchukua mali au pesa ya yatima, kuasi wazee wawili, kusisitiza kutenda haram (matendo yaliyokatazwa). Abu Huraira akaongeza kula riba na Hz. Ali aliongeza kunywa ulevi katika mambo hayo. Wakati huo huo, kuna baadhi ya wanazuoni wanaokubali kuwa kila dhambi yenye madhara kama dhambi zilizotajwa hapo juu au zaidi ni dhambi kumbwa; baadhi hukubali kuwa kila dhambi ambayo Allah na mtume wake wameiwekea adhabu kuwa ni dhambi kubwa. Kuhusiana na jambo hilo, Imamu Adh-Dhahabi (d. 748/1437) aliandika kitabu mahususi na kueleza dhambi sabini kubwa. (adh-Dhahabi, Kitabu'l-Kabair, Beirut, 1355/1933).

Kikundi cha khawariji, kilichodhihiri kipindi cha ukhalifa wa Hz. Ali, wanayakubali matendo kama sehemu ya Imani na kusema kuwa wale wanaotenda dhambi kubwa hutoka katika uislamu. Kundi la Muutazila pia wanakubali kuwa matendo ni sehemu ya Imani na kwa hivyo, kutenda dhambi kubwa hamfanya mtu aache kuwa muumini lakini hawasemi kuwa humfanya awe kafiri, kinyume na wanavyosema khawariji. Kwao wao, mtu kama huyo huitwa “fasiq” na anakuwa katika hali baina ya Imani na ukafiri mpaka atubie. Kama atatubia kabla ya kufa anakufa kama muislamu; kama hatatubia kabla ya kufa atakufa kama kafiri. (Taftazani, Sharhu'l-Aqaid, trnsl by Süleyman Uludağ, İstanbul 1980, p. 262 ff)

Kwa mujibu wa wanazuoni wa Ahl as-sunna, kutenda dhambi kubwa hakumfanyi mtu kutoka katika Uislamu labda mtu akane kuwa si dhambi. Dalali yao ni kama ifuatavyo: Imani ni kukubali kwa moyo. Kama sifa hii itabakia, dhambi kubwa iliyofanywa chini ya taathira ya vitu kama shahawa, matamanio, wivu na uvivu havikinzani na kukubali kwa moyo. Hata hivyo, ikiwa dhambi imetendwa kwa Imani na hisia ya kuzingatia haramu ni halali na kuifanyia mzaha halali, huzingatiwa ni ukafiri. Kwa upande mwingine, aya na hadithi huwaita waislamu wasi na wenye dhambi waumini. Tunaweza kutoa aya zifuatazo kama mfano:

“Enyi mlio amini! Tubuni kwa Mwenyezi Mungu toba iliyo ya kweli!” (at-Tahrim, 66/8).

“Enyi mlio amini! Mmepewa ruhusa kulipa kisasi” (al-Baqara, 2/178).

“Na ikiwa makundi mawili katika Waumini yanapigana, basi yapatanisheni.” (al-Hujurat, 49/9).

Matendo yaliyotajwa hapo juu katika aya ni dhambi kubwa. Hata hivyo, Allah mwenye nguvu anawaita wale waliotenda matendo hayo “waumini”.

Ni jambo lililokubaliwa kwa maafikiano, tokea zama za Hz. Mtume kwamba sala za Janazah za  Ahl al-Qiblah ambao wanatambulika kwa kutenda dhambi kubwa zimesaliwa na kwamba ni ruhusa kuwaombea msamaha kwa Allah.

Waumini wanaonywa dhidi ya dhambi kubwa kama ifuatavyo katika Qur’an:

Mkiyaepuka makubwa mnayo katazwa, tutakufutieni makosa yenu madogo, na tutakuingizeni mahali patukufu.” (an-Nisa 4/31; see also ash-Shura, 42/37; an-Najm, 53/32).

Katika aya hii, dhambi kubwa zinawekwa nje ya msamaha, kwa sababu kuna baadhi ya adhabu za kidunia kwa dhambi hizo kama nyongeza, toba mahususi inalazimika kwa dhambi za ulimwengu wao mwingine. Inawezekana kwa nyingi katika dhambi ndogo kusamehewa kupitia sala, funga, hija, zaka, na sadaka bila ya kuhitaji toba (Ahmad b. Hanbal, Musnad, II, 229). La ziada ni, hija huwa ni njia ya kusamehewa baadhi ya dhambi kubwa. Kwa kuwa kuna hadithi zinazoeleza kuwa Hija inayotekelezwa kwa ukamilifu inafuta dhambi zote zilizotangulia za mtu na kuwa kana kwamba amezaliwa upya. (Bukhari, Muhsar, 9, 10; Nasai, Hajj, 4; Ibn Majah, Manasik, 3; Darimi, Manasik, 7; Ahmad b. Hanbal, II, 229, 410, 483, 494).

Kwa kufupisha, ni wajibu wa Imani kukubali amri zote za Allah na makatazo na sharia zote za Kiislamu na kuuzingatia Uislamu kama mfumo. Wale wanaokataa baadhi kati ya hayo au kudai kuwa ni muhali kutekeleza Uislamu katika karne hii na kukana hata sharia moja ya Uislamu wanakuwa makafiri.

Maswali juu ya Uislamu

Author:
Maswali juu ya Uislamu
Subject Categories:
Read 7.461 times
In order to make a comment, please login or register
MASWALI YENYE KUFANANA