Kwa nini Uislamu ni dini ya kweli?

The Answer

Dear Brother / Sister,

“Bila ya shaka Dini mbele ya Mwenyezi Mungu ni Uislamu. Na walio pewa Kitabu hawakukhitalifiana ila baada ya kuwajia ujuzi, kwa sababu ya uhasidi ulio kuwa baina yao. Na anaye zikataa Ishara za Mwenyezi Mungu basi hakika Mwenyezi Mungu ni Mwepesi wa kuhisabu.” Qur’an, Familia ya Imran (Aal-i Imran); 19 (3: 19)

Dini inamaanisha “malipo kwa mtindo wa malipo au adhabu” na inaeleza uhusiano kati ya mfuasi na kiongozi mwenye madaraka. Kama neno lenyewe lilivyo, umetolewa ufafanuzi kadhaa wa neno dini. Zipo tofauti za kimsingi kati ya fafanuzi zinazotolewa na wanasayansi wa Kimagharibi (Ulaya) na wanazuoni Waislamu. Bado, kuna tofauti za kimsingi kati ya rai za pande zote mbili kuhusu chanzo cha dini na njia yake ya kimsingi ya kutokea. 

Kwa mujibu wa rai ya Kiislamu, dini inamaanisha ukamilifu wa kanuni unaomwongoza mwanadamu ili aweze kuishi kulingana na lengo aliloumbiwa na ili atambue lengo hilo katika nidhamu mahusussi. Dini ni msingi unaorekebisha uhusiano unaozingatia amri tukufu na utawala wa upande mmoja na utii na ufuasi wa upande wa pili, isipokuwa inafahamika kutokana na aya ambayo kwa mujibu wa Qur’an, thamani ya dini na kujitolea kumewekwa ili kuzingatie utii wa hiari. Kwa maneno mengine, kwa mujibu wa ufahamu wa Kiislamu, dini ni msingi unaoelekeza watu wenye kufahamu waelekee kwenye mema (kwa vitendo) na furaha kwa matakwa yao, na sheria ya kiungu inayorekebisha vitendo vya watu kwa kuzingatia uchaguzi wao.

Aya hiyo ndio sehemu ya kwanza ambayo neno Uislamu limetajwa katika Qur’an Tukufu. Maana ya Uislamu katika kamusi ni “kuwa mwaminifu, kutii, kujisalimisha na kuwa katika mwelekeo na amani”. Kama neno, Uislamu linamaanisha “kukubali kuwepo kwa mambo yote aliyotangaza Mtume Muhammad (s.a.w) kwa niaba ya dini na kuwa katika utii unaoidhihirisha hayo”. Jina la dini ya kweli aliyotumwa Mtume ni Uislamu. Bado, katika lugha ya Kiarabu, Uislamu ni hali isiyo na kikomo inayoonesha kuitii dini hiyo. Mtu anayefuata dini ya Uislamu ametajwa kuwa ni Muslam katika lugha ya Kiarabu na kama musalman katika lugha ya Kiajemi. Katika lugha ya Kituruki, maneno Islamiyet na Muslumanlik hutumika kwa ajili ya dini hiyo na neno musluman hutumika kwa mtu anayefuata dini hiyo.

Kuna uhusiano mkubwa kati ya maana ya neno Uislamu kwenye kamusi. Kwa mujibu wa ufahamu wa Kiislamu, dini ni sheria inayoeneza muwafaka kwa kuzuia kutoafikiana na ukinzani kati ya viumbe wenye matakwa na akili. Dini inaeleza muwafaka si miongoni mwa watu tu isipokuwa pia kati ya watu na Allah. Kwa njia hii, ukubalifu kati ya matakwa ya Muumba na matakwa ya viumbe huenezwa.     

Kwa kuwa dini zote za kimbinguni zina msingi wa kumpwekesha Allah, dini ya Uislamu aliyoijulisha Mtume Muhammad na dini zingine zilizotangazwa na mitume wengine kimsingi zinalingana. Hata hivyo, kwa mujibu wa baadhi ya wanazuoni wa Kiislamu, maneno kama vile dini ya Uislamu na jamii ya Kiislamu yanaweza tu kutumika kwa ajili ya dini aliyotummwa Mtume Muhammad na wafuasi wake. Ingawa Uislamu unaafikiana na dini za kweli zilizotangulia, dini hiyo ina baadhi ya sifa mahususi na baadhi ya maamrisho mahususi ya kipekee kwa jamii inayoifuata. Kwa mujibu wa kundi jingine la wanazuoni, pia inawezekana kwa dini zilizotangulia za mbinguni kuweza kuitwa Uislamu. Wanaeleza kuwa, katika Qur’an Tukufu kuna aya kadhaa zenye kuunga mkono rai hiyo: maneno ya majibu ya mitume wa Yesu kuwa “Shuhudia kuwa sisi ni Waislamu”, maelezo kuhusu Ibrahim kuwa “Alikuwa Muislamu hanif” na tena kutoa nafasi ya sifa ya ujumla kama vile “Amekupeni jina ‘Waislamu’ hapo kabla na hata sasa” ni mifano ya hilo. Kulingana na mtu kuwa na mitazamo kinzani, maelezo kama hayo yanawahusu Mitume.

Kwa mtazamo wetu, katika vitabu vitukufu isipokuwa Qur’an Tukufu, neno dini halikutajwa kwa ajili ya wafuasi wa vitabu hivyo na kama tutaona maneno kama vile Uyahudi na Ukristo yalitokea baadaye na yakatumiwa kwa ajili ya wafuasi wao baadaye, maana ya maneno “Bila ya shaka Dini mbele ya Mwenyezi Mungu ni Uislamu” yanaweza kufahamika kirahisi. Ingawa dini ilitangazwa na Mtume Muhammad ina kanuni mahususi, huku Qur’an ikithibitisha kwa msisitizo tamko la mitume waliotangulia linaloonesha kuwa walchotangaza kimsingi lilikuwa katika Uislamu; hata hivyo, kwa mujibu wa hekima ya kiungu, njia kamilifu zaidi ya imani hiyo inaweza tu kufikiwa kwa kutumwa Mtume Muhammad.

Kwa hali hiyo,njia pekee ya kuweza kupata radhi za Mtukuka Allah ni kuamini yote Anayoyasema. Kutokana na hayo, kwa kuanzia katika uhalisia, ingawa majina ya dini hizo zingine yanaweza kuwa yalitajwa ili kueleza itikadi fulani, muwafaka wa watafutaji ndani ya mipaka ya Allah Mtukuka unathibitisha lengo la msingi na haliepukiki kwa wakati uliotakiwa kwa ajili ya matamko ya Kiungu ili kuingiza fikra hiyo katika akili na dhamiri ya wanadamu. Wanazuoni wa Kiislamu wameeleza ufahamu huo kama “jamii tiifu” na “jamii iliyolinganiwa”; neno la kwanza hapo linaeleza watu wanaoendea matakwa yao ya utii kwenye yale haswa yaliyotangazwa na kudhihirishwa na Mtume Muhammad; na la pili linaeleza kundi linalowezekana kuwa hivyo ambalo bado halijafikia kiwango hicho isipokuwa katika kipindi cha tafakuri kilichotajwa hapo. Kwa hivyo,kwa kulinganisha na majina kama vile “Uyahudi” na “Ukristo”, baadhi ya waandishi wa Kimagharibi wanaouita Uislamu kwa kulifinya ina kuwa ni “Umuhammadi” halifai kwa sababu liko mbali na ukweli na pia lina sifa ya kuzuia mawasiliano pamoja na yaliyotajwa hapo juu.

Kuifahamu aya kwa njia hiyo katika nukta ya lengo kuu haikinzani na fikra kuwa kilammoja aliyeishi katika wakati wowote au mahali popote na akaacha kumshirikisha Allah na kuweza kujielekeza katika imani hiyo anaweza kuitwa “Muislami” kwa mujibu wa ufahamu wa Qur’an’. Kwa hakika, katika aya kadhaa, inaweza kuonekana kuwa vigezo hivyo vimezingatia kukokoka watu katika ahera.

Kwa maana pana, Uislamu (kuwa Muislamu) unaeeza utii moyo, ulimi na tabia. Utii muhimu zaidi na wa thamani kubwa kati ya hayo ni wa moyo. Katika Qur’an, kunaonekana kuwa neno Uislamu pia linatumika kwa ajili ya utii ambao haujafikiakiwango cha imani.

Maneno “Waliopewa vitabu” limefahamika kwa ujumla kuhusiana na yaliyomokwenye maneno “Watu wa Kitabu”. Neno elimu limeelezwa kama “ufunuo na shuhuda waziwazi”. Katika aya, matamshi ya watu wa Vitabu wanaoangukia katika ridhaa baada tu ya elimu kuja ni kwa ajili ya kuonesha kuwa walijulishwa kiasi cha kutosha kuhusu matamshi ya Kiungu na ingawa hawana udhuru kwa hilo, wanaangukia katika vurugu na kugombana kwa sababu ya makosa yao na kwa kufikiria manufaa yao na tamaa za kibinadamu. Kwa kuanzia na “Kwa sababu ya dhuluma miongoni mwao”, baadhi ya maelezo yalitolewa na watu yaliyodokezwa hapa yalikuwa yanawahusisha Wayahudi au Wakristo au makundi yote mawili. Nuru ya elimu ya kihistoria, hapa, inaweza kusemwa kuwa badala ya kusonga mbele katika njia ya amani na ustaarabu kwa kutumia ufunuo mwongofu uliowekewa, jamii, zilizoambiwa kwa ufunuo wa kiungu, huku akili ya kawaida ikiwekwa mbali kwa sababu ya matakwa ya kibinafsi na hususani kutenganisha katika makundi ya kidini kwa kuzingatia kuwa matakwa yao kinzani yamekosolewa. Licha ya onyo hilo, kukariri kosa hilohilo kwa wanaoamini Qur’an kumesababisha kizuizi muhimu katika kutimiza Mpango wa kufikisha ujumbe wa Kiungu kwa wanadamu kwa njia bora zaidi na kuchukua nafasi wanayostahiki katika the mashindano ya ustaarabu.

Maswali juu ya Uislamu

Author:
Maswali juu ya Uislamu
Subject Categories:
Read 3.806 times
In order to make a comment, please login or register