Kwanini nyama ya ngurume imeharamishwa katika dini ya Kiislamu?

The Answer

Dear Brother / Sister,

Dini ya Kiislamu imeruhusu kula nyama za baadhi ya wanyama lakini imekataza kula baadhi ya nyama za wanyama wengine. Wakati wanyama wakiruhusiwa au wakikatazwa huchunguzwa, ikionekana nyama zao hazina matatizo ya kiafya huruhusiwa na zile zenye madhara hukatazwa. Nyama ya nguruwe imekatazwa kutokana na aina ya ulaji wake, muonekano, maumbile yake mabaya na kuwa na vitu vyenye madhara ambavyo vitamuathiri mwanadamu kama uwepo wa mnyoo anaojulikana kama trichina (kwenye nyama).

Kwenye Qur’an, nguruwe ametajwa sehemu tano. Aya ambazo zimetaja ni kama zifuatazo:-

Yeye amekuharimishieni mzoga na damu na nyama ya nguruwe na kilicho tajiwa, katika kuchinjwa kwake, jina la asiye kuwa Mwenyezi Mungu.” (al-Baqara, 2/173; an-Nahl, 16/115)

“Mmeharimishiwa nyamafu, na damu, na nyama ya nguruwe, na mnyama aliye chinjwa si kwa ajili ya Mwenyezi Mungu,...” (Surah al-Maeda, 5/3)

“Sema: Sioni katika yale niliyo funuliwa mimi kitu kilicho haramishwa kwa mlaji kukila isipo kuwa kiwe ni nyamafu, au damu inayo mwagika, au nyama ya nguruwe, kwani hivyo ni uchafu; au kwa upotofu kimechinjwa kwa jina la asiye kuwa Mwenyezi Mungu.” (al-Anaam, 6/145)

Ubaya wa hali ya nguruwe umeoneshwa kwenye aya ifuatayo:

“…Ni yule ambaye Mwenyezi Mungu amemlaani na amemkasirikia, na amewafanya miongoni mwao manyani na nguruwe, na wakamuabudu Shet'ani. Hao ndio wenye mahali pabaya na wamepotea zaidi njia iliyo sawa!” (al-Maeda, 5/60)

Inasimuliwa na Jabir b. Abdillah kwamba Mjumbe wa Allah alisema maneno yafuatayo kipindi makka imevamiwa:

“Kwa hakika Allah na Mjumbe wake wameharamisha kununua na kuuza ulevi, kula nyama za mizoga, nyama ya nguruwe na kuabudu masanamu.” (Bukhari, Buyu'; kwenye tafsiri ya Tajrid as-Sarih Vl / 537,538)

Kula nyama ya nguruwe kumekatazwa na dini zingine vile vile. Kwa mfano, yafuatayo ni maelezo yanayotokana na Kumbukumbu La Torati, kwenye kitabu cha Wayahudi:

“…na nguruwe, kwakuwa amepasuliwa ukwato lakini hacheui, huyu ni najisi kwenu; msile nyama zao, wala msiiguse mizoga yao.” (Kumbukumbu La Torati, 14/8)

Allah amewaamrisha watu wale vizuri, chakula safi na Wamshukuru kwa neema hizo. Kula chakula cha halali kunafungua njia kukubaliwa kwa maombi na ibada. Vyakula vya haramu vinasababisha ibada na dua kukataliwa. Mtume wa Allah (rehma na Amani ziwe juu yake) amesema yafuatayo:

 “Enyi watu! Hakika Allah ni Msafi na Hakubali tu kilicho safi. Kwa hakika, Allah amewaarisha waumini yale aliyowaamrisha mitume wake.” Allah anasema yafuatayo:

 “Enyi Mitume! Kuleni vyakula vizuri na tendeni mema. Hakika Mimi ni Mjuzi wa mnayo yatenda.” (al-Muminun, 23/51)

Vile vile Anasema,

“Kuleni katika vitu vizuri hivyo tulivyo kuruzukuni…” (Taha, 20/81)

Kisha, Mjumbe wa Allah alimtaja mtu ambae alikuwa kwenye safari ndefu, ambae nywele zake na nguo zake zilikuwa ovyo ovyo na akaomba, “Ewe Mungu! Ewe Mungu!”:

“Anachokula mtu huyu, anachokunywa na anachovaa ni haram. Iweje dua yake ikubaliwe?” (Muslim, Tirmidhi, Ahmad b. Hanbal)

Yafuatayo yameelezwa kwenye aya:

“Anaye waamrisha mema na anawakanya maovu…” (al-Araf, 7/157)

Imeelezwa na wataalamu wa afya kwamba nyama ya nguruwe ina madhara kwa mwanadamu. Daktari  Glen Shepherd aliandika yafuatayo kwenye hitimisho la Makala aliyoiandika kwenye gaziti la Washington Post, la tarehe 31/05/1952: 

“Mmoja kati ya watu sita Marekani na Canada wana minyoo ijulikanao kama trichina katika misuli yao (muscles) kwasababu wanakula nyama ya nguruwe ambayo huwa imeathiriwa na minyoo hiyo trichinosis. Watu wengi ambao wameathirika hawaoneshi dalili. Wengi katika hao, wenye minyoo hiyo, (wakiacha) afya hutengamaa taratibu. Baadhi yao hufa; baadhi yao hupata ugonjwa wa kupooza (paralyze) kwenye upande wa kushoto.Wote huwa ni walaji wa nyama ya nguruwe bila kuwa makini. Hakuna mwenye kinga kutokana na ugonjwa huu na hauna tiba. Hakuna dawa za kuua vijisumu (antibiotics) wala dawa zingine au chanjo ambayo inaweza kuathiri uwepo wa vijidudu hivi vinavyoonekana kama vile vimekufa. Kujilinda na maambukizi ndio suluhisho la kweli…Dalili za ugonjwa zinazosababishwa na aina hii ya minyoo (trichinas) ni sawa na zile za magonjwa zaidi ya hamsini. Njia kama vile kutia chumvi nyama ao kuvuta sigara haiwezi kabisa kuwaua trichinas. Kudhibiti sehemu za kuchinjia haitoshi kugundua nyama ipi imeathirika na trichina.”

Watafiti wengi wanasema kwamba kuendelea kula nyama ya nguruwe kunadhoofisha kiwango cha wivu kwa mwanamme kwasababu nguruwe ni mnyama pekee aliyekosa wivu kwa mwenzake wa kike. 

Kwa upande mwengine, nguruwe hutoa harufu mbaya kwavile hula aina zote za vyakula vichafu; pia nyama yake ina thamani ndogo sana kulingana na kiwango kidogo cha protini kilichomo. Kisayansi imeelezwa kuwa ni jambo lisilowezekana kuiondoa minyoo aina ya trichina kwenye nyama ya nguruwe. Profesa Hirsch, mmoja katika mamlaka ya usafi duniani, ameuelezea ukweli huo kwa uzuri kabisa.

Kula nyama ya nguruwe, ambapo baadhi ya madhara yameelezwa na wataalamu wa tiba, imekatazwa katika Uislamu kama zilivyokataza dini zingine. (Tafsiri ya Tajrid as-Sarih, VII, 537 ff.; Yusuf al-Qardawi, İslâm'da Helal ve Haram, iliyotafsiriwa na Mustafa Varlı, Ankara 1970, 50-53)

HEKIMA NYUMA YA KATAZO LA NYAMA YA NGURUWE

UMUHIMU WA KUTAHINIWA

Ikiwa jambo limefanywa kuwa halali au haramu inategemea na amri ya Allah. Ikiwa Allah Ametangaza jambo fulani ni halali, litakuwa halali; ikiwa Ametangaza jambo fulani ni haramu, litakuwa haramu. Maana yake ni kwamba, dini ni mtihani; uliopelekwa kwa watu. MwenyeziMungu Mtukufu huwajaribu watu ili kuwafanya wastahiki kupata Pepo. Hivyo basi, Ametangaza baadhi ya maamrisho na makatazo. Jambo la msingi ni kuyatii maamrisho na kuyaacha makatazo haya. Kanuni hizi zina manufaa makubwa kwa maisha ya mtu na maisha ya jamii. Hivyo, kanuni hizo hutufanya kutii maamrisho tukiwa hadhiri kabisa. Moja katika mambo tuliyokatazwa na dini yetu ni nyama ya nguruwe. Katazo hili lina sababu nyingi na hekima. Tutataja baadhi tu hapa.

 [KUWA NA] VITU VYENYE SUMU

Nyama ya nguruwe ina mafuta mengi sana. Ikiwa italiwa, mafuta huchanganyika na damu. Kwahiyo, damu huchanganyika na chembechembe za mafuta. Kiwango hiki kikubwa cha mafuta husababisha magonjwa yanayojulikana kama, arteriosclerosis, presha (hypertension) na magonjwa ya moyo (heart infarct). Zaidi ya hayo, vitu vyenye sumu vijulikanavyo kama sutoxines vinapatikana kwenye siagi (lard). Matezi ya limpathik (Lymphatic glands) hulazimika kufanya kazi ngumu ili kuondoa chembechembe hizo za sumu ambazo huingia mwilini. Husababisha maambukizi na kunyonya tezi zijulikanazo kama lymph nodes hasa kwa watoto. Koromeo la mtoto humeza na kuonekana kama la nguruwe. Hivyo basi, maradhi haya yanajulikana kama scrofulosis (maradhi ya nguruwe). Kama maradhi yataongezeka, tezi zote za lymph huathiriwa na kumezwa. Hali joto huongezeka; maumivu huanza na hali ya hatari sana hujitokeza.

KIWANGO KIKUBWA CHA SALFA

Tishu zijulikazo kama kolageni (collagen tissue) zilizopo katika mfumo wa majimaji kamasi (mucus) ambazo zinapatikana kwa wingi kwenye nyama ya nguruwe, zina kiwango kikubwa sana cha salfa (sulfur). Hivyo, kiwango kikubwa cha salfa huchukuliwa na kuingizwa mwilini. Kiwango hiki cha ziada cha salfa hubaki kwenye misuli (muscles) na mishipa ya neva (nerves), na kusababisha maambukizi kwenye viungio (joints), calcification na ngiri (hernia) kwenye viuno (loins). Ikiwa mtu atakuwa na mazoea ya kula nyama ya nguruwe, sehemu ngumu  (hard cartilage) kwenye mwili itaondolewa na tishu za kolageni zenye mfumo wa majimaji (kamasi) kutoka kwa nguruwe. Hatimae, fuvu gumu linalainika; haliwezi sasa kuhimili uzito wa mwili na huvunjika. Hivyo basi, uharibifu kwenye viungo huanza kujitokeza. Miili ya wanaokula nyama ya nguruwe huwa legevu kama jeli; tabaka za mafuta hutengenezeka. Kwa mfano, mwanamichezo akila nguruwe, huwa mchovu, mvivu na kutokuwa madhubuti. Baadhi ya wachezaji wa mpira hufikia hatua ya kukata tamaa kwasababu ya matumizi ya nyama ya nguruwe.

UKUAJI KUPINDUKIA

Kiwango cha vichocheo vya makuzi (growth hormone) kwenye nguruwe ni vingi kupita kiasi. Kitoto cha nguruwe ambazo kina uzito wa gramu mia kadhaa anapozaliwa huwa na kilo mia kwa miezi sita tu. Kwa kiwango hicho cha makuzi ni kutokana na kiwango kikubwa cha vichocheo vya makuzi (growth hormone). Homoni ya makuzi inayobebwa na nyama ya nguruwe husababisha kumezwa kwa tishu na maambukizi kwenye mwili. Husababisha pua, kidevu, mkono na mifupa ya miguu kukuwa katika hali isiyo ya kawaida na mwili kuganda mafuta. Jambo la hatari zaidi kwenye homoni hii ya makuzi ni uwezekano wa kufungua njia ya kupata saratani (cancer). Kwakweli, wachinjaji wa nguruwe wanaeleza kwamba nguruwe dume hupata saratani baada ya umri fulani.

MARADHI YA NGOZI

Chembe chembe zinazojulikana kama histamine na imidazole kwenye nyama ya nguruwe husababisha maumivu kupita kiasi. Pia hurahisisha kutokea kwa maradhi ya kuambukiza ya ngozi kama vile ugonjwa unaojulikana kama eczema, damatiti (dermatitis) na nyurodamatitis (neurodermatitis). Chembechembe hizi huongeza hatari ya kutokea majipu (boils),  kidole tumbe (appendicitis), magonjwa ya kibofu (gall bladder diseases), venali (venal) na maambukizi ya ateri (arterial infections). Kwa sababu hiyo, madaktari huwashauri wagonjwa wa moyo wasile nyama ya nguruwe.

KUMBUKUMBU

Daktari wa Ujerumani, Profesa, Dr. Reckeweg, anaelezea kumbukumbu ya hadithi fulani katika kitabu chake kinachoitwa “Nyama ya nguruwe na Afya ya mwanadamu”:

 “Nilikwenda kwenye shamba la familia ambalo liko nje kidogo ya barabara kwa ajili ya uchuguzi wa kitabibu. Baba alikuwa ana ugonjwa hatari sana unaojulikana kama arthrosis (ugonjwa mbaya sana wa viungo) na ugonjwa ujulikanao kama coxarthrosis (ugonjwa kwenye viungio vya kiuno). Pia alikuwa ana ugonjwa wa ini. Mwanamke alikuwa na ugonjwa wa mishipa ujulikanao kama varicose veins na eczema,  ambao husababisha maumivu makali ya kuvuta (harassing itching). Mtoto wa kike alikuwa anaumwa na tatizo la moyo lijulikanalo kama cardiac insufficiency na rheumatism. Mtoto wao wa kiume, alionekana mwenye afya njema zaidi kuliko wao aliyekuwa anaumwa na tatizo la moyo cardiac insufficiency baada ya angina na futi (furuncle). Mtoto mwengine wa kiume alikuwa na nywele kama nguruwe na acute pleurisy; pia alikuwa anakabiliwa na tatizo la kutokwa na fistula mara kwa mara.

Katika kipindi changu cha uchunguzi wa kidaktari kwenye nyumba ambayo ipo kwenye shamba ambayo wakazi wake na maradhi yao niliyoyataja hapo juu, nilishuhudia jambo moja la ajabu sana. Nguruwe mkubwa aliegemea tawi la mti na akawa anajikuna karibu na wanafamilia. Nikawaambia, “Hivi mnamuona yule nguruwe pale? Mnakula vitu ambavyo vinamsababishia nguruwe maumivu na ambavyo husababisha maambukizi mnapokula nyama ya nguruwe. Na sababu pekee ya maradhi yenu ni vitu hivyo.”

 “Baadhi ya wakuliwa hao wanaishi karibu na msitu mkubwa wenye kiza unaoitwa Dark Woods ambao wamejipatia maradhi mengi, waliuchukua ushauri wangu na kuacha kula nyama ya nguruwe. Kwasasa kuna makundi mengi ya kondoo kama yanayopatikana katika nchi za Kiislamu kwenye mashamba yanayozunguka maeneo yao ya kilimo”

NYAMA YA NGURUWE NA MNYOO UJULIKANAO KAMA TRICHINA

Moja ya maradhi hatari sana ambayo yanaaambukizwa kwa mwanadamu kupitia nyama ya nguruwe ni trichina. Ingawa, trichina hausababishi tatizo kubwa kwa nguruwe mwenyewe. Hata hivyo, mnyoo huu unasababisha maradhi hatari sana kwa wanadamu. Mnyoo wa trichina humezwa kupitia nyama ya nguruwe na kwenda kwenye damu kupitia utumbo mkubwa na utumbo mdogo. Hivyo basi, hutapakaa mwili mzima.

Minyoo ya trichina hukaa hasa kwenye tishu za misuli kwenye magego, ulimi, shingo, koo na maeneo ya kifuani. Husababisha kupooza kwenye kutafuna, kuzungumza na misuli ya kumezea. Pia husabisha vikwazo kwenye mishipa, tatizo la meningitis na athari kwenye ubongo. Na hatari zaidi zinaweza kusababisha kifo. Jambo la hatari katika maradhi haya ni kwamba hayana tiba sahihi. Ugonjwa wa trichina ni maarufu hasa kwenye nchi za Ulaya. Mripuko wa maradhi ya trichina umeshuhudiwa kwenye nchi kama vile Uswidi (Sweden), Uingereza, na Poland, licha ya udhibiti wa mifugo. Uturuki, mripuko wa ugonjwa wa trichina haujawahi kuonekana isipokuwa kwenye jamii za Wakristo wanaoishi Uturuki.

CHAKULA NA TABIA YA MWANADAMU

Wanadamu na wanyama huathiriwa na vyakula wanavyokula kwa kiasi fulani. Kwa mfano, inajulikana kwamba wanyama wanaokula nyama (carnivorous) kama paka, mbwa na simba ni wakali na wanyama wanaokula majani (herbivorous ) kama kondoo, mbuzi na ngamia ni watiifu na wapole. Na hivyo hivyo kwa wanadamu. Imeonekana kwamba watu wanaokula mboga kwa ujumla wao ni wapole, na wale wanaokula nyama na yatokanayo na nyama ni wakali. Nguruwe ni mnyama pekee ambae hana wivu kwa mwenza wake wa kike. Imegundulika kuwa hisia za wivu zinadhoofika au kuisha kabisa kwa wanaotumia nyama ya nguruwe. Katika kulipa umuhimu jambo la athari za chakula kwenye tabia, Savorin, mwanafalsafa wa Kifaransa amesema “Niambie unachokula, ntakuambia wewe ni nani.”

CHAKULA CHA HALALI KINATOSHA KWA MAHITAJI YA MWANADAMU

Mola wetu ametuumbia aina nyingi za vyakula kwa ajili yetu. Ingawa, Ametukataza tusile na tusinywe aina za vyakula vyenye madhara kwasababu Ana ukarimu na huruma isiyo na ukomo. Hamtwishi mja wake mzigo mzito ambao ni nje ya uwezo wake. Maamrisho na makatazo yake ni rahisi kutekelezwa. Kwani mtu atapoteza nini akiacha kunywa pombe na ikiwa hali nyama ya nguruwe?

Makala haya yameandikwa na Prof. Dr. Selahattin Salimoğlu, kili yalivyonukuliwa kwenye kitabu "Merak Ettiklerimiz 1 (Prof. Dr. Adem Tatlı)". Cihan Yayınları, ISTANBUL; ISBN 975 - 7486 - 13 - 2)

Maswali juu ya Uislamu

Author:
Maswali juu ya Uislamu
Subject Categories:
Read 4.225 times
In order to make a comment, please login or register