Ni zipi haki za wanawake katika Uislamu? Una majibu gani juu ya madai kuwa Uislamu unawashinikiza na kuwawekea vikwazo wanawake?

The Answer

Dear Brother / Sister,

Katika nyakati za kabla ya Uislamu, wanawake hawakuwa wakitaamwa kuwa ni wanadamu. Dini ya Kiislamu imewainua wanawake mpaka katika hadhi wanayoistahiki. Uhuru haumaanishi kuweza kuishi kwa matakwa ya nafsi ya mtu au Shetani. Kinyume chake, unamaanisha kuishi kama anavyotaka Muumbaji. Kwani mtu asiyetii matakwa ya Allah anatii matakwa ya nafsi na Shetani.

Sasa tutaeleza haki za ujumla za wanawake kwa kifupi:

“Na mmoja wao akibashiriwa kwa msichana, uso wake unasawijika, naye kajaa chuki....” (an-Nahl, 16/58 )

Katika aya hiyo, Allah anaeleza jinsi watu wa Jahiliyyah walivyowatazama wanawake. Hata hivyo, Quran  imeeleza yafuatayo: 

“Anaumba apendavyo (na anapanga), anamtunukia amtakaye watoto wa kike, na anamtunukia amtakaye watoto wa kiume.” (ash-Shura, 42/49)

Mwnamke huzaliwa sawa na anavyozaliwa mwanamume; yeye pia ni mtoto kama alivyo wa kiume. Wazazi watawajibishwa ikiwa watawabagua kwa huruma na zawadi; pia watazingatiwa kuwa wamepuuza nasaha za Mtume na hawatapewa uombezi wa Mtume. Kwa kujua kuwa hisia za Jahiliyyah zitakuwa zinajirudiarudia, Mtume (s.a.w) alisisitiza umuhimu wa kuwaelimisha wasichana kama ifuatavyo:

“Baba anayewalea mabinti zake watatu au wawili atakuwa pamoja nami peponi, hata mtoto mmoja.” (Ibn Majah, Adab 3)  

Mtoto wa kike anapozaliwa, mnyama (aqiqa) huchinjwa kama ilivyo kwa mtoto wa kiume. Inatakiwa apewe jina zuri na aelimishwe na mama yake. Apewe elimu ya kijinsia kutoka kwa mama yake. Hakuna aya au hadithi inayohimiza sayansi na elimu huku ikiwabagua wanawake. Kinyume chake, Mtume (s.a.w) alinasihi elimu mahususi kwa wanawake na aliwaamuru wanaume kuhifadhi haki zao. Wanawake Mujtahid walikwezwa katika wakati wa uhai wake. (Mathalani, Aisha, mke wa Mjumbe wa Allah (s.a.w) ni mmoja wao.)

Mwanamke amenyanyuliwa bila ya ubaguzi wowote na anapofikia wakati wa kuolewa, ni haki yake na sunnah kumwona mtaradhia wake. Asipompenda mtaradhia, ana haki ya kumkataa; mkazo wa wazazi, walezi au mtaradhia wake hautabadili chochote.

Anapoamua kuolewa, anaweza kusisitiza apokee kiasi cha mahr anayotaka. Mahr ni haki yake ya kimaumbile na dhamana ya maisha aliyoiweka Allah. Anaweza kuitumia atakavyo madam ni halali. Anaweza kutumia mahr yake na mali zingine kwa kuitoa sadaka au biashara; anaweza kuanzisha makampuni, kununua hisa, n.k.; anaweza kupata pesa na kuitumia anavyotaka. Matumizi yote ya nyumbani na ya mwanamke yafanywe na mwanamume. Mwanamume hana haki ya kumwambia, “jinunulie mwenyewe mapambo yako, nguo na vipodozi”. Anapaswa ampe matumizi yake kulingana na kipato chake. Kama mwanamume hawezi kumtimizia matumizi baada ya ndoa, mwanamke akidai talaka itakubalika.

Mumewe hawezi kumdhalilisha; asisahau kuwa mkewe ni mwandani wake. Hawezi kumkasirikia na kumwacha peke yake nyumbani.

“Mwanamume bora ni yule anayewatendea vyema wanawake.” (angalia Bukhari, Nikah 43; Muslim, Fadhail 68)

Kutaniana na kujiburudisha kati ya wanandoa ni jukumu la mume.

Mwanamume asimpige mkewe isipokuwa pindi akiasi, kukiuka sheria. (angalia aya 34 ya sura an-Nisa na tafsiri yake kuhusu kuwapiga wanawake. Mathalani, angalia Ibn Kathir IV/257; Qurtubi VI/170,172,173; Elmalı IV/1351; Abu Dawud, Manasik 56; Ibn Majah, Manasik 84; Muslim, Hajj 147; Tirmidhi, Rada'11; Abu Dawud, Manasik 56; Halabi Saghir uk. 395; Halabi Kabir uk. 621; Canan, Terbiye uk. 391;) Mwanamume asimsumbue mkewe kwa kurejea ghafla kwa sababu ya wivu wake.

Katika hadithi, Mtume (s.a.w) amewakataza wanaume walio mbali na nyumba zao kwa muda mrefu wasirejee nyumbani usiku ghafla. Sababu mojawapo ni kumpa mwanamke muda wa kunyoa nywele za kwapani na za siri na kujipamba na kuchana nywele. Hadith inayohusu jambo hilo ni hii ifuatayo:

“Unaporejea nyumbani usiku, usimwendee moja kwa moja; mpe fursa ya kunyoa na kuchana nywele zake.” (Bukhari, Nikah 121,122; Muslim, Rada' 58, Imarah 181,182; Darimi, Nikah 32, Jihad 163; Musnad NI/298)

The scholars who explain the hadith state that coming home suddenly at home might mean that the man suspects of his wife.

Maulamaa wanaoifasiri hadithi hiyo wanasema kuwa kurejea nyumbani ghafla kunaweza kumaanisha kuwa mwanamume anamshuku mkewe.

Mume pia ana wajibu wa kumtosheleza mkewe. Mtume (s.a.w) alimfananisha mwanamume aliyemaliza upesi tendo la kujamiiana kuwa ni kama majogoo, yaani, kama wanyama. Pia aliwanasihi wanaume kutokuanza kujamiiana na wake zao bila ya kuwapapasa wanawake. (Kutoka katika Daylami, Ghazzali, Ihya N/52 (Tafsiri. N/129); angalia pia Suyuti, al Jamiu's-Saghir (pamoja na Fathu'I-Qadir) VI/323) kwani, mwanamume anaweza kuamshwa hisia zake kwa kutazama tu lakini mwanamke huwa tayari kujamiiana baada ya kupapaswa kwa muda mrefu. Mwanamume mzuri ni yule anayemudu kumwandaa mkewe kwa ajili ya kujamiiana na kumtosheleza kama anavyotosheka yeye. Waanaume wanaojijali wenyewe tu wakati wa kujamiiana wasisahau kuwa wanawadhulumu wanawake na wanastarehe kwa kuwatesa wake zao.

Mwanamke ana haki ya kudai talaka kutoka kwa mwanamume asiyeweza kujamiiana naye kwa mwaka mmoja baada ya ndoa.   

Mwanamke ana haki ya kukataa kujamiiana kabla ya kutanguliziwa mahr yake.

Matumizi ya mwanamke, kutunzwa na tiba zifanywe na mwanamume. Ikiwa mwanamke hawezi kuoka mkate, mumewe anunue mkate. ikiwa mwanamke anataka kujipamba, mwanamume alipie vifaa na manukato. Mume anunue gauni mbili au suti mbili kila mwaka, moja kwa ajili ya majira ya joto (kiangazi) na nyingine kwa ajili ya majira ya baridi (kusi). Ikitokea kutoelewana, sifa ya mavazi huamuliwa na mamlaka za mahali husika. Mwanamke anaweza kutaka matumizi pindi mumewe anapokwenda kuvinjari kwa siku asizokuwepo. Akitaka anaweza kudai kitanda kingine cha kulala pindi anapokuwa katika hedhi zake.

Anaweza kutaka mtumishi kulingana na hali ya mumewe. Mshahara wa mtumishi ulipwe na mume. Mwanamke hawajibiki kufanya kazi yoyote ya nyumbani isipokuwa zile ambazo kwa desturi hufanywa na wake katika eneo husika.  

Akitaka, anaweza kuafikiana na mumewe juu ya kiasi maalumu cha matumizi. Ikiwa kiasi hicho kitageuka kuwa hakitoshi, anaweza kutaka kiongezwe; kama mumewe hataafiki, anaweza kushitaki mahakamani.  

Ikiwa mwanamke hataki ndugu wa mumewe, mume anatakiwa kukodi au kununua nyumba nyingine kwa ajili yake. Sababu ya amri hiyo ni ukweli kuwa watamzuia kutaniana na kujamiiana na mumewe. Zaidi ya hayo, mwanamke ana haki ya kudai chumba kingine ikiwa ana watoto isipokuwa watoto wadogo wasiotambua mambo ya kujamiiana.

Mwanamke ana haki ya kuwatembelea wazazi wake mara moja kwa wiki; mume hawezi kulizuia hilo.

Mwanamke ana haki ya kufanya kazi katika biashara halali isiyoingilia haki za mumewe.

Ikiwa mwanamke anataka kwenda katika hamamu baada ya hedhi na uzazi, mumewe atalipia hamamu hilo, hata hivyo, ikiwa itajulikana kuwa mwanamke hajisitiri mwili wake inavyotakikana katika hamamu, hatapelekwa katika hamamu hilo.

Mume anatakiwa alipie matumizi ya mkewe aliyempa talaka rejea au isiyo rejea katika wakati wa iddah.

Mpaka sasa tumetaja mifano michache tu iliyomo katika vitabu vya fiqh kuhusu haki za wanawake juu ya wanaume. Huo si ushauri bali ni haki za kisheria zenye adhabu. Wanawake wakilazimishwa kufanya kazi na wakafanya kazi ngumu ambazo wanaume peke yao ndio wenye kuweza kuzifanya katika baadhi ya sehemu, si kosa la Uislamu bali ni kosa la wale wanaoishi kinyume na Uislamu.

Maulama wengi wa Kiislamu wanasema kuwa mwanamke ana haki ya kupiga kura kunapokuwa na uchaguzi. Kwani, hakuna ushahidi unaoeleza kuwa hawana haki hizo. Mbali na hayo, maana ya uchaguzi ni kutii. Mtume (s.a.w) alipokea utii kutoka kwa wanawake. (Angalia al-Mumtahina (60) aya 12 na maelezo yake) Rai ya kila mmoja wakiwemo wasichana wadogo iliulizwa kwa ajili ya halifa aliyetarajiwa kuteuliwa baada ya Hadhrat  Umar (ra). [angalia Muhammed Hamidullah, Islam Müesseselerine Giriş Ist.1981, uk. 112 (imechukuliwa kutoka kwa Ibn Kathir)]

Mwanamke anapofariki, sanda yake inunuliwe na mumewe.

(Kwa maelezo zaidi kuhusu vipengele vilivyoelezwa katika muhtasari wa hapo juu, angalia Ibn Abidin, Raddu'l-Mukhtar, Misri 1380 (1960) NI/571 n.k.. angalia pia sehemu zinazohusu nafaqa katika vitabu vyote vya fiqh, hususani Sarakhsi, Mabsut V/180, n.k..)

Kama inavyoonekana, mwanamke hana wasiwasi juu ya matumizi; yaani, ana dhamana kamili ya kijamii. Hizo zote ni haki za kisheria zinazotumika mahakamani pindi kunapokosekana maelewano. Katika Uislamu, mume na mke si maadui ambao kila mara hujaribu kupata haki za mwenzake. Wao ni nusu mbili zinazokamilisha kitu kizima, kusaidiana wao kwa wao; mathalani, Mtume (s.a.w) aliwasaidia wake zake kufanya kazi za nyumbani; Hadhrat  Ali (ra) na mkewe Fatima (ra) walifanya kazi kwa pamoja.

MWANAMKE KATIKA FAMILIA:

Uislamu unaeleza kuwa mwanaume na mwanamke waliumbwa kwa usawa:

“Enyi watu! Hakika Sisi tumekuumbeni kutokana na mwanamume na mwanamke...” (al-Hujurat, 49/13).

Uislamu pia unaeleza kutokufanya ubaguzi baina ya mwanamume na mwanamke na kuwa hakuna aliye mbora kwa mwenzake katika kuzaliwa, kufa na kuishi baada ya mauti. Kwani, mwanamume atasimama na kuhesabiwa peke yake mbele ya Allah. (Maryam, 19/93) Hali ya wanawake waumini wanaotenda amali njema na kutokuiacha njia ya Allah imeelezwa kama ifuatavyo: Mwenye kutenda mema, mwanamume au mwanamke, naye akawa ni Muumini, tutamhuisha maisha mema; na tutawapa ujira wao kwa bora ya waliyo kuwa wakiyatenda.” (an-Nahl, 16/97).

Tofauti kati ya mwanamume na mwanamke ipo katika viwiliwili vyao; inaelezwa kuwa wanawake ni viumbe dhaifu na laini. Kwa hiyo, tofauti zipo katika shughuli za maisha ya mtu mmoja mmoja na kijamii; inaonekana kwamba wanawake wamehifadhika hapo. Uislamu haukuwashusha wanawake kama ilivyokuwa katika imani za maisha ya Jahiliyya; pia haukuwafanya wanawake watawale kama ilivyo katika familia ambazo mkuu ni mama. Uislamu umeanzisha familia ya kuigwa ambapo kila mwanafamilia ana majukumu yake na hakuna dhuluma katika majukumu hayo. Uislamu umeweka mfano bora wa familia ulioanzisha enzi mpya, kuondosha mitazamo yote ambayo ingeweza kuwakandamiza wanawake katika familia na kuiharibu familia.

Uislamu unamwajibisha mwanamume kubeba majukumu ya mkuu wa familia.

Wanaume ni wasimamizi wa wanawake, kwa kufadhiliwa (nguvu) na Mwenyezi Mungu baadhi yao juu ya baadhi, na kwa mali yao wanayo yatoa...” (an-Nisa, 4/34)

Allah anaeleza yafuatayo katika aya nyingine kwa kumpa mwanamume wajibu wa kuwa mkuu wa familia:

“...Nao wanawake wanayo haki kwa Sharia kama ile haki iliyo juu yao. Na wanaume wana daraja zaidi kuliko wao. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu na Mwenye hikima.” (al-Baqara, 2/228)

Mwanamume anatakiwa akabili mahitaji ya familia na kuhifadhi familia dhidi ya athari zote za nje; ana majukumu muhimu sana. Mwanamume hawezi kuingilia mali binafsi ya mwanamke katika familia; hawezi kumtwisha mwanamke mzigo. Zaidi ya hayo, ikiwa mwanamke hataki kumtunza mwanaye, anaweza kumwomba mumewe aweke mtumishi; mwanamke hahitajiki kufanya kazi za nyumbani, pia. Hata hivyo, majukumu ya nyumbani kama hayo ni ishara ya taqwa ya wanawake; kwa hiyo, Mtume (s.a.w) anawahimiza hayo wanawake. Mwanamke anatakiwa kutii amri halali za mumewe. (Abu Dawud, Nikah, 40).

Muendelezo wa maisha ya familia ya Kiislamu unawezekana tu kwa kuhifadhiana hazi za kila mmoja.

“Mnazo haki juu ya wanawake na wanawake wana haki zao juu yenu.” (Tirmidhi, Rada, 11).

Maana ya kujisalimisha na kutii haki za kila mmoja kwa upande wa mwanamke ni kumtimizia mumewe majukumu ya halali.  

HAKI ZA MWANAMKE JUU YA MUMEWE:

Kwa kuwa mwanamume amewajibishwa kuleta chakula, anatakiwa akabili mahitaji yakinifu ya mwanamke na kulifanya hilo kiuhalali. (an-Nisa, 4/34). Mwanamume anatakiwa amtendee wema mwanamke na kulinda haki zake:

“... Na kaeni nao kwa wema, na ikiwa mmewachukia, basi huenda mkakichukia kitu, na Mwenyezi Mungu ametia kheri nyingi ndani yake. (an-Nisa, 4/19).

Uislamu unamkataza mwanamume kufanya ubadhirifu wa “mamlaka ya usimamizi na kuongoza familia”. Inamaanisha kuweka mpangilio katika familia. Kwa hiyo, mwanamume haruhusiwi kutumia fadhila hiyo kwa kumwonea mwanamke. Ni kwa kanuni hii tu ndipo mahusiano kati ya mwanamume na mwanamke yataweza kuendelea katika hali ya kawaida.

Uislamu unawapa wanawake fursa ndogo sana na katika mipaka halali, kutumia vipawa na ufanisi wao katika mambo ya mahusiano ya kijamii. Katika mfumo huu wa kijamii, Uislamu unawaruhusu wanawake kufanya kazi, kushiriki katika shughuli mbalimbali na kujifunza ili kuwasaidia Waislamu. (Bukhari, Ilm, 36; Ibrahim Jamal, Müslüman Kadının Fıkıh Kitabı, kilichotafsiriwa na Beşir Eryarsoy, İstanbul 1987, uk. 483, ff)

“Mwanamke ni kama ubavu. Kama utajaribu kuunyoosha, utauvunjika. Kama unataka kuwa na furaha, uache kama ulivyo.” (Bukhari, Nikah, 79).

“Mbora wenu ni yule anayemtendea mkewe vyema zaidi.” (Tirmidhi, Rada, 11; Ibn Majah, Nikah, 50).

Tunajifunza kutokana na hadithi hizo hapo juu kuwa Mtume (s.a.w) kila mara aliwaonya Waislamu kuhusu wanawake na kuwa aliwanasihi wanaume wawatendee wema. Wanawake wasipigwe; wapewe mawaidha. Hata hivyo, wakikaidi, wakawaasi waume wao, wakakaa na wanaume wasio mahram, wakufuja mali za wanaume na kufichua siri za familia, kwanza wakemewe; kisha, wakaripiwe vikali; kusipokuwepo mabadiliko, wanaweza kupigwa kidogo ili kuwaonya. (an-Nisa, 4/34). Kama kuwapiga kidogo hakusaidii, wasipigwe kwa nguvu.

HAKI ZA MUME JUU YA MKE:

“Wanaume ni wasimamizi wa wanawake, kwa kufadhiliwa (nguvu) na Mwenyezi Mungu baadhi yao juu ya baadhi, na kwa mali yao wanayo yatoa.(an-Nisa, 4/34).

Basi wanawake wema ni wale wenye kut'ii na wanao jilinda hata katika siri kwa kuwa Mwenyezi Mungu ameamrisha wajilinde...” (an-Nisa, 4/34).

Wanawake wawatii na kuwaheshimu waume wao ili waume wao wabebe vyema majukumu yao nyumbani. Mwanamke anatakiwa kumtii mumewe kwenye mambo ya halali. Mbali na hayo, kazi za nyumbani anazozifanya mwanamke na kuwatunza watoto zitazidisha taqwa ya mwanamke. Kwani, Uislamu haukuyawajibisha hayo kwa wanawake; umewahamasisha wanawake wayafanye hayo ili wapate radhi za Allah.

Wanaume ni bora kwa wanawake kwasababu ya kuwa na baadhi ya sifa za kimaumbile na uwezo wasiokuwa nao wanawake. Hata hivyo, haimaanishi kuwa wanaume ni bora kwa heshima na utukufu. (Mawdudi, Tafhimu'l Qur'an, I, İstanbul 1986, uk. 317, 318).

“Mwanamke akiswali swala tano za kila siku, akifunga katika mwezi wa Ramadhani, akihifadhi tupu yake na kumtii mumewe, milango ya Pepo itakuwa wazi kwa ajili yake.” (Bukhari, Misqat, II/202).

Hata hivyo, utii uliotajwa katika hadithi hiyo unahusu mambo yanayolingana na amri za Allah; ikiwa mume atataka jambo lililo kinyume na amri za Allah, mke hatakiwi kumtii. Kwani, kumtii Allah ni bora zaidi kuliko kumtii mume.

Kutoshelezeana kijinsia ni jambo muhimu katika familia; kwa hiyo, haifai kwa yeyote kati yao kupuuza hilo. Mwanamke anatakiwa aujue ukweli huo na amheshimu mumewe kuhusu jambo hilo. Uislamu unaeleza kuwa wanaume na wanawake wako sawa katika kuumbwa. Hakuna tofauti ya adhabu za kidunia katika usawa wa wanawake na wanaume. Adhabu za uhalifu unaofanyika dhidi ya wanaume na wanawake ziko sawa. Ukweli kuwa mwanamke hupokea nusu ya fungu katika mirathi ikilinganishwa na mwanamume si jambo la kudhalilisha au kutokuwepo usawa. Inapozingatiwa kuwa mume ana wajibu wa kumtunza mke, kuwa amtimizie mahitaji, kuwa wazazi wa mwanamke au mlezi wanatakiwa kumtunza na kukidhi mahitaji yake kabla ya kuolewa na kuwa mumewe ayafanye hayo baada ya ndoa, ltadhihirika alilokusudia Allah katika amri hiyo.   

Mwanamke hatakiwi kumpa mwanamume chochote kutoka katika mirathi aliyopata kama hataki kufanya hivyo. Hata hivyo, mwanamume anatakiwa kukidhi mahitaji yake. Kwa hivyo, inawezekana kwa mwanamke kupokea mirathi bali kutoitumia. (Ibrahim Jamal, sawa na rejea ya hapo juu uk. 485).

Allah amemuumba mwanamke awe mwenyeji wa nyumba. Mwanamume anawajibika kupata mali kwa ajili ya familia; mwanamke awajibika kutumia mali vyema kwa ajili ya kaya. Kwani, mwanamke ni mwenye kuchunga nyumba ya mumewe. Uislamu haumwajibishi mwanamke kwenye mambo mengine yoyote. Quran inamhimiza mwanamke kubakia nyumbani kwa aya ifuatayo:

“Na kaeni majumbani kwenu...” (al-Ahzab, 33/33)

Hata hivyo, katika baadhi ya hali, anaweza kutoka. Mathalani, kama hakutakuwepo mwanamume wa kuitunza kaya, ikiwa atahitajika kufanya kazi kwa sababu ya shida ya fedha, ikiwa mwanamume hawezi kupata mali ya kutosha, ikiwa mwanamume ni mgonjwa na hawezi kufanya kazi, n.k., mwanamke anaweza kutoka na kufanya kazi.

“Allah anawaruhusu wanawake kutoka ili kukidhi mahitaji yao.” (Bukhari-Muslim).

Hata hivyo, hali ya maisha ya leo ikizingatiwa, Mwanamke wa Kiislamu hawezi kujihifadhi dhidi ya macho ya wanaume waovu sokoni, mitaani na maisha ya kibiashara mbali na kwamba ni mwangalifu sana. Kwa hiyo, wanawake wajiepushe mitaani hata kama wana shida ya kifedha.

Uislamu unawapa wanawake majukumu ya nyumbani na unaondoa haja ya kufanya kazi. Uislamu utainusuru roho ya mwanamume aliyefanyiwa usaliti katika wakati wa vita na amani.

Rejea:

- Seyyid Kutub, İslâm Kapitalizm Çatışması, İstanbul 1988, uk. 129;
- Said Havva, Uislamu, Tafsiri na Said Şimşek, Ankara nd., uk. 197, ff;
- Mustafa Sibai, Kadının Yeri, İstanbul 1988, uk. 57 ff.;
- Abdullah Nasuh Ulvan, İslâmda Aile Eğitimi, I, uk. 221 ff.;
- Ömer Ferruh, İslâm Aile Hukuku Tafsiri na Yusuf Ziya Kavakcı, İstanbul 1976, uk. 228 ff;
- Hadhrat  Peygamber ve Aile Hayatı, Komisyon, İstanbul 1989, uk. 171 ff;
- M. Ali Haşimi, Kur'an ve Sünnette Müslüman Şahsiyeti, Tafsiri ya Resul Tosun, İstanbul 1988, uk. 63 ff.
 (Şamil İslam Ans, Kadın item)

Maswali juu ya Uislamu

Author:
Maswali juu ya Uislamu
Subject Categories:
Read 6.402 times
In order to make a comment, please login or register