Ni zipi shuhuda za umoja wa Allah (Tawhid)?

The Answer

Dear Brother / Sister,

- Madai ya kwamba kuna mola zaidi ya mmoja si sahihi kiakili.

Wanachuoni wa elimu ya tawhid wa Kiislamu wametaja shuhuda kadhaa ili kuthibitisha umoja wa Allah. Ushahidi muhimu kati ya hizo unaitwa ufupishaji na kutowezekana ambao unakataa madai ya kwamba kuna Mungu zaidi ya mmoja

Tunapo jaalia ya kwamba kuna miungu wawili ulimwenguni, bila ya shaka kutakua na majadiliano baina yao na migogoro baina ya matakwa yao.

Mwisho wa mgogoro kama huo, kwa mfano, pale Mungu mmoja anapotaka kitu kitokee na mwingine hataki kitu hicho kitokee, moja kati ya yumkini zifuatazo zitatokea.

1. Matakwa ya miungu hao wawili yote yatatokea

2. Matakwa ya miungu hao yote hayatatokea

3. Moja kati ya matakwa ya miungu hao wawili yatatokea na mengine hayatatokea

Uwezekano huo wote si sahihi kiakili na ni muhali.

Kama matakwa yao wote wawili yatatokea, hali ambayo jambo moja litatokea na jingine halitatokea wakati huo huo itatokea, Yaani,, mambo mawili yenye kukinzana kama uwepo na kutokuwepo vitakutana, jambo ambalo kiakili ni muhali

Kama matakwa yao wote wawili hayatatokea, itamaanisha kitu kitakua kimezuiliwa kutokana na kuuwepo na kutokuwepo, yaani, mambo mawili yenye kukinzana yatatokea, jambo ambalo pia kiakili ni muhali.

Kwa kuongezea, miungu watakabiliwa na udhaifu pale matakwa yao yanapokua hayajatimia. Dhati dhaifu haziwezi kuwa dhati za kiungu haziwezi kuumba kitu.

Katika yumkini ya tatu, matakwa ya mmoja kati ya miungu miwili yatatokea na ya mwingine yatazuiwa; hivyo mungu ambaye matakwa yake hayakutokea atakuwa dhaifu. Dhati dhaifu haiwezi kuwa Mungu.

Kwa kuongezea, tulieleza kuwa miungu watakuwa sawa, pale mmoja kati yao anapogundulika kuwa ni dhaifu, basi Yule mwingine pia atakuwa dhaifu kwa sababu walikua sawa. Kisha , wote wawili watakuwa dhaifu. Dhati dhaifu haziwezi kuwa miungu.

Na kama hivi, yumkini zote zinagundulika kuwa si sahihi na nadharia kwamba kuna miungu wawili au zaidi inathibitishwa kuwa sio sahihi.

Kisha, dhati ya kiungu ambayo imeumba ulimwengu ni moja. Na dhati hiyo ni Allah, aliyetakasika, mwenye ukamilifu, nguvu, ukubwa kama ulazima wa uwepo wa dhati yake ya tangu na ya milele.

Kuna shuhuda nyingine zenye kuthibitisha imani ya umoja. Hebu tutaje baadhi yake ambazo sisi tunaziona ni muhimu:

- Ushahidi kwamba “utawala wake haukubali washirika”:

Sheria muhimu zaidi ya ukweli wa utawala ni kujitegemea na uhuru. Yaani, kukataa kuingilia kwa wengine na ushirika katika utawala.

Ni wazi kwamba hata binadamu dhaifu ambao sehemu ndogo sana ya utawala hukataa kuingiliwa kutoka nje ili kulinda kujitegemea kwao na huwa na hasira pale wengine wanapowaingilia katika mambo yao. Katika historia, wafalme waliokua na mapenzi makubwa na huruma waliwaua watoto wao wasio na hatia na ndugu zao wapendwa ili tu wasiweze kuwaingilia katika utawala wao. Ni wazi inaonesha kwamba ukweli wa kuwa hakuna kuingiliwa katika utawala ni wenye kutawala bila ya mashaka na jambo la lazima.

Kwa vile kivuli cha hisia za utawala ndani ya wanadamu dhaifu na wenye kuhitaji zinakataa kuingiliwa kwa kiasi kikubwa sana na hazikubali ushirika katika utawala wao na hujaribu kuhami kujitegemea kwao, itafahamika kwamba Allah mtukufu ambaye ana utawala katika muundo wa kuwa mola wa limwengu, utawala kamili katika muundo wa uungu na kujitegemea kwa ukamilifu katika muundo wa umoja yupo huru kutokana na kuwa na mshirika, mwenza na adui.

Kwa hivyo, kujitegemea na upekee ni kanuni ya lazima ya utawala wa kikamilifu wa Allah.

- Ushahidi wa nidhamu:

Nidhamu kamili na mfumo uliopangika unaonekana katika viumbe juu ya mgongo wa ardhi kutokea atomu mpaka nyota kwa kimoja kimoja na vyote kwa pamoja ni dalili kubwa na ni ushahidi ulio wazi wa umoja.  Ikiwa yoyote asiyekuwa muumba ataingilia katika shughuli za kiungu na uumbaji ulimwenguni, mpangilio huo ulio makini kabisa na mlingano utaharibika na alama za vurugu zitatokea kila sehemu.

- Ushahidi wa “wepesi katika umoja na ugumu katika wingi”:

Kama uumbaji wa vitu utarejeshwa kwa muumbaji mmoja na mtengenezaji, itakua ni wepesi kama uumbaji wa kitu kimoja kama utarejeshwa katika asili, uumbaji wa nzi utakua mgumu kama uumbaji wa mbingu, ua litakua gumu kama wakati wa machipuo na tunda litakua gumu kama shamba la miti ya matunda.

Kwa vile wepesi wa tangu unaonekana katika uumbaji wa vitu ulimwenguni, inafahamika kwamba Muumba ni mmoja na wa pekee…

Maswali juu ya Uislamu

Author:
Maswali juu ya Uislamu
Subject Categories:
Read 140 times
In order to make a comment, please login or register
MASWALI YENYE KUFANANA