Ni zipi Sifa Bainifu za dini ya Uislamu?

Submitted by on Wed, 08/08/2018 - 11:38
Dear Brother / Sister,
Sifa kuu bainifu za Uislamu zenye kuubainisha na dini zingine ni kama ifuatavyo:
1- Uislamu unawahutubia watu wote na karne zote; kanuni zake zinatimiza mahitaji yote za kiutu.
Sifa hii ya Uislamu ya kuenea kote, nyakati zote na kwa wote imetajwa kama ifuatavyo katika Quran:
"Na hatukukutuma ila kwa watu wote, uwe mbashiri, na mwonyaji." (Saba', 28)
"Sema: Enyi watu! Hakika mimi ni Mtume kwenu nyinyi nyote, niliye tumwa na Mwenyezi." (al-A'raf, 158).
2- Uislamu ni dini ya wepesi na urahisi.
Katika Uislamu, watu hawatakiwi kufanya wasiyoyaweza au yale wanayotaabika kuyafanya.
Kanuni za wepesi na urahisi za Uislamu zimeelezwa kama ifuatavyo katika Quran:
"Mwenyezi Mungu haikalifishi nafsi yoyote ila kwa kadiri ya iwezavyo..." (al-Baqara, 286).
"Usitutwike tusiyo yaweza..." (al-Baqara, 286).
“Mwenyezi Mungu anakutakieni yaliyo mepesi wala hakutakieni yaliyo..." (al-Baqara, 185).
Wakati Quran inabainisha kuwa Uislamu ni dini ya wepesi na urahisi, Mtume anaeleza kanuni zifuatazo katika hadithi zake:
"Nimetumwa niwe rehema kwa viumbe wote. Sikutumwa kukuteseni wala kusababisha taabu..."
"Allah hakunituma kama mtu wa kusababisha taabu na shida au mtu wa kuwatakia hayo. Amenituma kuwa ni mwalimu na kurahisisha mambo..."
"Lililo bora katika dini yenu ni lililo jepesi zaidi. Bila ya shaka kuwa dini ni wepesi..."
"Jiepusheni na niliyoyakataza na fanyeni niliyokuamrisheni kadiri muwezavyo. Mataifa ya kabla yenu yaliangamizwa kwa sababu ya wingi wa matatizo yao na kuwapinga mitume wao."
"Fanyeni amali njema kadiri muwezavyo. Allah hatachoka kukulipeni mpaka mchoke kuabudu."
"Rahisheni mambo; msiyafanye magumu. Toeni habari njema; msiwaogopeshe watu."
Bi. Aisha alisimulia kitendo cha Mjumbe wa Allah (s.a.w) kuhusu hilo kama ifuatavyo:
"Pindi Mjumbe wa Allah (s.a.w) alipopewa hiari ya kuchagua kati ya mambo mawili, alichagua lililokuwa jepesi zaidi isipokuwa la dhambi. Kama jambo hilo lilikuwa dhambi, bila ya shaka aliliepuka zaidi kuliko watu wote."
Hadithis hapo juu inaonesha amri zilizo nyepesi kutekeleza zilizomo katika Uislamu. Wepesi huu ni nafasi kubwa katika kudhihirisha kuwa ni dini ya wote na itaendelea kuwepo mpaka Siku ya Kiama.
Baadhi ya mifano kutoka katika nyendo za Uislamu zinaonesha kuwa dini hiyo ni nyepesi:
Katika dini yetu, ni lazima kuchukua udhu kwa kutumia maji. Hata hivyo, yanapokosekana maji au kunapokuwa na hatari ya kuugua kwa sababu maji ni ya baridi sana, tayammum hufanywa kwa udongo. Udongo huchukua nafasi ya maji.
- Dini yetu huwapa manufaa wasafiri na kuwaruhusu kuswali swala za rak'ah 4 kuwa rak'ah 2 kutokana na baadhi ya sababu kama vile uchovu, kukosa muda, n.k.
- Ni faradhi kusimama wima wakati wa kuswali. Hata hivyo, wasioweza kusimama wanaweza kuswali wakiwa wamekaa kitako.
- Inaweza kuwa vigumu kwa wagonjwa na wasafiri kufunga kufunga katika mwezi wa Ramadhani. Kwa hivyo, dini yetu inaweka uhuru wa kufunga au kula. Si dhambi kama hawatafunga. Wanaweza kufunga watakapopona au kurejea kutoka safarini.
- Kama kuna hatari kama vile magonjwa ya mlipuko, vita, n.k, Waislamu wanaofanya hajj wanaweza kuahirisha hajj zao mpaka hatari iishe.
3- Hukumu zote za Uislamu ni za weledi. Hakuna chenye kutofautiana na mantiki katika Uislamu.
Mali muhimu zaidi ya mwanadamu inayomtofautisha na viumbe wengine ni akili. Mwanadamu hufikiria mambo mengine, hubainisha heri na shari na huchagua kati ya haki na batili akilini mwake.
Kwa hivyo, akili na watu wenye hekima wametajwa takribani katika aya 70 katika Quran. Ibara "Je hawasikii?", "Je hawaelewi?" yametumika mara nyingi.
Kuwa na akili timamu ni lazima ili kuweza kuwajibika katika dini yetu; kwa hivyo, wasio na akili timamu hawawajibishwi.
Watu wasiomwamini Mtume (s.a.w) walimwambia, "Tuoneshe baadhi ya miujiza ili tumwamini Allah na kukukubali wewe kuwa ni mtume", Allah hakuyapenda waliyoyasema na akawataka watizame adhi na mbingu na kuzitafakari ili waamini kuwepo Kwake badala ya kutaka kuona miujiza. Jambo hilo limeelezwa katika Quran kama ifuatavyo:
"Hakika katika kuumbwa kwa mbingu na ardhi, na kukhitalifiana usiku na mchana, na marikebu ambazo hupita baharini kwa viwafaavyo watu, na maji anayo yateremsha Mwenyezi Mungu kutoka mbinguni, na kwa hayo akaihuisha ardhi baada ya kufa kwake, na akaeneza humo kila aina ya wanyama; na katika mabadiliko ya pepo, na mawingu yanayo amrishwa kupita baina ya mbingu na ardhi, bila shaka zimo Ishara kwa watu wanao zingatia." (al-Baqara, 164)
Anas, mmojawapo kati ya Maswahaba mashuhuri, alimsifu mtu mbele ya Mjumbe wa Allah (s.a.w) huku akimtaja. Mjumbe wa Allah akamuuliza Anas:
- Akili yake iko vipi?
Anas akasema:
- Ewe Mjumbe wa Allah! Ibada yake, maadili na fadhila ni nzuri. Mjumbe wa Allah akauliza tena:
- Akili yake iko vipi? Anas akasema:
- Ewe Mjumbe wa Allah! Sisi tunataja ibadayake, ihsani isipokuwa wewe unauliza akili yake. Hapo, Mjumbe wa Allah alisema:
- Mfanya ibada mpumbavu anaeza kuhadaiwa na Shetani kirahisi na kutenda madhambi zaidi kuliko anayefanya dhambi kutokana na ujinga wake. Watu wanaweza kumkaribia Allah kwa mujibu wa akili zao.
Hadithi hiyo hapo juu, iliyosimuliwa katika "Adabu'd-Dunya wa'd-Din" cha Mawardi ni mfano mzuri sana na tukio lililokera linaonesha umuhimu wa akili katika Uislamu.
Baadhi ya hadithi zingine zinazohusu akili ni kama ifuatavyo:
"Mtu asiye na akili hana dini."
"Allah hampendi muumini asiyetafakari."
"Kama akili ya mtu si timamu, dini yake haitakuwa timamu..."
"Pepo ina daraja 100. Daraja 99 ni kwa ajili ya wenye akili timamu; daraja 1 ni kwa ajili ya wengine..."
"Ewe Ali! Watu wanapojikurubisha kwa Allah kwa amali mbalimbali njema, wewe jikurubishe kwa akili yako."
"Allah hakuumba kitu chochote chenye thamani kubwa na utukufu zaidi kuliko akili."
4- Uislamu ulikomesha na kuondoa tofauti za kimatabaka, dhuluma na upendeleo uliokuwepo katika kila enzi na kuweka kanuni zilizoondoa tofauti zilizozingatia asili.
Yafuatayo yameelezwa katika Quran:
“Enyi watu! Hakika Sisi tumekuumbeni kutokana na mwanamume na mwanamke." (al-Hujurat, 13).
Mtume amesema yafuatayo:
"Watu ni wana wa Adam. Allah alimuumba Adam kutokana na mavumbi ya ardhi." Hivyo, Uislamu unaeleza kuwa watu wote wanatokana na baba mmoja na mama mmoja na kwamba kwa kuangalia asili hakuna atakayedai kuwa mbora kuliko wengine.
5- Uislamu unawatazama watu kuwa wanalingana kama vile meno ya kitana katika mbele ya sheria. Uislamu hauzipi umuhimu tofauti za kimbari, rangi na lugha; unaeleza kuwa kinachomfanya mwanadamu kuwa na thamani na kumfanya mbora kwa watu wengine ni uchamungu moyoni mwake na kiwango cha imani yake. Mtume anaeleza yafuatayo kuhusu jambo hilo:
"Enyi watu! Msisahau kuwa Mola wenu Mlezi ni mmoja (huyo huyo) na kuwa baba yenu ni mmoja. Mwarabu si mbora kwa asiye Mwarabu, asiye Mwarabu si mbora kwa Mwarabu, mweupe si mbora kwa mweusi na mweusi si mbora kwa mweupe kwa chochote isipokuwa taqwa (kumhofu Allah)."
Hivyo, dini yetu inamtazama kila mtu kwa usawa mbele ya sheria; haiupi umuhimu ubora wa kidunia na vyeo vya muda mfupi; inazingatia moyo wa mwanadamu badala ya mwonekano wake.
Uyahudi huzipa umuhimu starehe za kimwili na kunufaika kwa njia ya mali. Unawahamasisha wafuasi wake wazipe umuhimu tamaa za kidunia. Dini ya Ukristo na Uhindu huyapa umuhimu Maendeleo ya roho, kwa kudhoofisha Matakwa ya roho kwa kutia maumivu juu ya Mwili na kupuuzia maisha ya kidunia. Hata hivyo, Uislamu umeweka usawa kati ya the roho na Mwili, dunia na ahera. Unayapa usawa yote mawili; unalenga katika kutimiza mahitaji ya yote mawili kilakimoja kivyake.
Aya ifuatayo ya Quran inaeleza uwiano kati ya dunia na ahera katika Uislamu kwa namna bora kabisa: “Mola wetu Mlezi, tupe mema duniani na Akhera."
Islam hauipi umuhimu dunia kwa kuleta hasara ya ahera au (kuipa umuhimu) ahera kwa hasara ya dunia.
Uislamu unaeleza kuwa ahera itapatikana humu duniani na kuwataka watu waitumikie dunia kama vile hawatakufa na kuitumikia ahera kama vile watakufa kesho.
6- Hakuna tabaka la wahudumu wa kidini katika Uislamu. Kila mtu anapaswa ajifundishe dini yake kadiri anavyoweza. Katika Uislamu, hakuna tabaka la watu maalumu wenye kupendelewa linalofanya kazi kama kiunganishi kati ya mja na Muumba kwa ajili ya ibada na kuwafanya watu watubu madhambi yao.
7- Uislamu ni dini ya maadili na fadhila na inalinda sayansi, elimu na ukweli kikamilifu.
Maswali juu ya Uislamu