Ni zipi sifa za Allah? Zimegawika katika makundi mangapi?

The Answer

Dear Brother / Sister,

Sifa za kiungu zimegawika sehemu mbili sifat dhatiyah (sifa za kidhati) and sifat subutiyah (sifa chanya).

Sifat Dhatiyah (Sifa za kidhati):

1- Wujud (Kuwepo)
2- Qidam (Utangu),
3- Baqa (Kubakia),
4- Wahdaniyyah (Umoja),
5- Qiyam bi Nafsihi (Kuwepo kwa kujitegemea),
6- Mukhalafa lil-Hawadith (Hakuna mfanano na viumbe)

Sifa za Allah za kidhati ni za Allah peke yake; hazimilikiwi na dhati nyingine yoyote. Kwa mfano, sifa ya qidam haipo kwa dhati nyingine yoyote. Sifa za kidhati hazina uhusiano na dhati nyingine.

Kuwepo (Wujud):

Sifa hii inaeleza kwamba Allah yupo. Kuwepo kwa Allah hakutegemei dhati nyingine yoyote; ni sifa ya lazima kwake. Hiyo ni kusema, kuwepo kwake kunategemea dhati yake mwenyewe na ni sifa ya wajibu kwa dhati yake. Kwa hivyo, sifa ya dhati ya wajibu hutumika kwa Allah. Baadhi ya wanazuoni wa elimu ya Al-Kalam huiita sifa ya kuwepo sifa ya kidhati.

Kinyume cha kuwepo, ni kutokuwepo (adam), haiwezi kufikiriwa kuhusu Allah.

Kudai kutokuwepo kwa Allah kunalazimu kukana ulimwengu na vilivyomo ndani yake kwasababu ni yeye ndiye anayeumba kila kitu.

Qidam (Utangu):

Ina maana Allah, aliyetukuka, hana mwanzo. Allah, aliyetukuka, ni wa tangu. Daima alikuwepo. Hakuumbwa baadaye.

Ni muhali kuufikiria wakati ambao Allah alikua hayupo. Kwa kweli, ni yeye ndiye aliyeumba wakati na sehemu. Allah yupo nje ya wakati na sehemu. Yeye ni Mola wa tangu mtukufu.

Kuzuka (kutokea katika wakati) ambako ni kinyume na utangu hakuwezi kufikiriwa kwa Allah, aliyetukuka.

Baqa (Kubaki milele):

Kuwepo kwa Allah hakuna mwisho; Daima yupo.

Kama kuwepo kwa Allah kulivyokua hakuna mwanzo, hakuna mwisho. Yeye ni wa tangu na wa milele. Kwa kweli, dhati ambayo imethibiti kuwa ya tangu ni lazima iwe ya milele.  

Kinyume cha baqa, ni fana, maana yake kuwa na mwisho. Haiwezekani kwa Allah.

Mukhalafa lil-Hawadith (Kutofanana na viumbe):

Ina maana kutofanana kwa Allah na viumbe ambao waliumbwa baadaye.

Allah hafanani na yeyote katika viumbe vyake katika dhati au katika sifa zake.

Vyovyote tufikiriavyo kuhusu Allah, yeye yupo tofauti na vyovyote tuwazavyo. Kwakuwa tuviwazavyo ni vitu tulivyovitengeneza baadaye kutokana na si kitu. Allah ni Mungu na dhati takatifu ambaye kuwepo kwake ni wajibu, wa tangu na wa milele, asiyehitaji kitu chochote au yeyote, ambaye ametakasika na kasoro zote na mwenye sifa zote za ukamilifu.

Bila ya shaka, dhati tukufu kama hiyo haifanani na viumbe ambao walikuwa hawapo lakini baadaye wakaumbwa na ambao watatoweka tena.

Kwa kweli, Allah anaielezea dhati yake kama ifuatavyo katika Qur’an:

 “Hapana kitu kama mfano wake. Naye ni Mwenye kusikia Mwenye kuona (vitu vyote).” (ash-Shura 11)

Mtume wetu anasema uthibitisho ufuatao wenye maana:

 “Allah yupo tofauti na kinachofikiriwa akilini”

Qiyam bi Nafsihi (Kuwepo kwa kujitegemea):

Ina maana kuwa Allah anaendelea kuwepo bila ya kuhitaji dhati nyingine au sehemu.

Viumbe vyote vilitokea baadaye. Kwa hivyo, wanahitaji Muumba na sehemu. Hata hivyo, kuwepo kwa Allah, ambaye ni muumba wa kila kitu, ni wajibu wa dhati yake; Hategemei kitu.

Kama Allah alihitaji dhati nyingine ili awepo, basi, angelikua kiumbe na asingelikuwa muumba wa kila kitu.

Hata hivyo, yeye ni Muumba wa kila kitu. Kila kitu isipokuwa yeye ni kiumbe. Muumba hawezi kuhitajia viumbe vyake.

Wahdaniyyah (Umoja):

Ina maana ya umoja wa Allah.

Umoja ni sifa muhimu Zaidi za Allah za ukamilifu. Kwakuwa sifa hii inaeleza kuwa Allah ni mmoja katika dhati yake, sifa na matendo na kwamba hana washirika katika utawala wake na shughuli zake.

Kinyume cha sifa hiyo ni taaddud (kuwa zaidi ya mmoja) and tasharruk (kuwa na washirika) haiwezi kufikiriwa kuhusu Allah.

Katika Uislamu na hata katika dini zote za kweli, Imani ya umoja wa Allah inaunda msingi wa Imani za kidini. Hakuna Imani au tendo litakuwa sahihi labda liambatane na Imani ya umoja katika moyo wake. Kwa hivyo, kabla ya yote Uislamu unatoa kwa wanaadamu Imani ya umoja na kuwalingania kukubali kwamba Allah ni mmoja na kumtakasa na washirika wowote. Nukta muhimu ambayo dini za kweli hutofautiana na dini za uongo ni nukta hii kwa sababu dini batili pia hukubali kuwepo kwa Allah lakini wanakosea katika sifa za kiungu, hususan sifa ya umoja; hujaalia washirika pamoja na Allah.   

Katika muktadha huu, ukweli muhimu Zaidi baada ya kukubali kuwepo kwa Allah ni Imani ya umoja. Imani juu ya Allah haina maana na thamani bila ya Imani ya umoja.

Baadhi ya aya zinazoeleza umoja wa Allah na Imani ya tawhid katika Quran ni kama ifuatavyo:

Sema: Yeye Mwenyezi Mungu ni wa pekee.” (al-Ikhlas, 1).

Ati yupo muumba mwingine asiye kuwa Mwenyezi Mungu anaye kupeni riziki kutoka mbinguni na kwenye ardhi? (Fatir, 3).

“Wala hanaye mungu mwingine. Ingekuwa hivyo basi kila mungu angelichukua alivyo umba, na baadhi yao wangeliwashinda wengine.” (al-Mu’minun, 91)

“Lau wangelikuwamo humo miungu wengine isipo kuwa Mwenyezi Mungu basi bila ya shaka hizo mbingu na ardhi zingelifisidika.” (al-Anbiya, 22)

Sifat Subutiyah (Sifa chanya):

1- Hayah (Allah yupo hai)
2- Ilm (Allah anajua kila kitu tokea tangu)
3- Irada (Allah yupo huru kufanya atakalo)
4- Qudrah (Allah ana uwezo juu ya kila kitu.)
5- Sam' (kusikia) (Allah anasikia kila kitu.)
6- Basar (kuona) (Allah anaona kila kitu)
7- Kalam (Allah anaongea bila ya kuhitaji kiungo chochote au sauti)
8- Takwin (Kuumba) (Allah anaumba kutokana na si kitu)

Tofauti na sifa zake za kidhati, Sifa chanya za Allah sio tofauti kabisa kutokana na dhati nyingine na ni juu ya dhati katika ulimwengu wa kuonekana. Kwa mfano, sifa ya Hayah ipo pia katika wanaadamu lakini ni tofauti kiupande ilivyo na asili yake. Allah ana utashi na mwanaadamu ana utashi, pia. Hata hivyo, kuna tofauti kati ya sifa hizo mbili. Utashi wa Allah hauna ukomo na hauna shaka; utashi wa mwanaadamu una mpaka. Utashi wa mwanaadamu umekuwepo kama matokeo ya utashi wa Allah. Sifa chanya zote nyingine zimegawanywa kwa malaika, majini na wanaadamu.

Hayah (Uhai):

Ina maana Allah mwenye nguvu ana uhai na ana sifa ya uhai.

Sifa hiyo, ambayo ni wajibu kwa Allah mtukufu, sio ile inayotokana na muunganiko wa kitu na roho unaoonekana kwa viumbe na ni ya tangu nay a milele. Ni uhai halisi ambao ni asili ya uhai wote.

Sifa ya uhai imeungana kwa karibu na sifa ya ukamilifu kama elimu. Utashi na nguvu. Dhati yenye sifa hizo lazima iwe na uhai kwa sababu dhati mfu haiwezi kuwa na sifa kama elimu, utashi na nguvu.

Kwa hivyo, sifa ya uhai inaelezwa kama ni sifa ya tangu ambayo inamwezesha Allah mtukufu kusifikana na sifa kama elimu, utashi na nguvu.

Kinyume cha sifa ya uhai ni umauti. Ni muhali kwa Allah.

Ilm (Elimu):

Ina maana Allah anajua kila kitu na elimu yake imekizungukia kila kitu.

Muumba aliyeumba dunia hii katika namna bora na nidhamu kamili na anayeutawala lazima ajue vitu alivyoviumba kwa kina sana. Vipi kitu kisichojulikana faida yake, ulazima wake na hekima yake kiumbwe? Hivyo, ni wajibu kwa muumba kwanza kukijua kitu kisha kukiumba kwa mujibu wa wajibu wa elimu ili kukiumba. Kwa kuongezea, kuwalipa watu kwa Imani na matendo mema na kuwaadhibu watu kwa kutofuata amri na kupotea inawezekana tu kupitia utambuzi wa kina wa kile wakifanyacho watu hao.

Kinyume cha elimu ni ujinga, kupuuza na kusahau. Haziwezi kufikiriwa kuhusu Allah.

Iradah (Utashi):

Ina maana Allah anataka jambo litokee kama vile na sio kama hivi; ina maana  yeye huamua kila kitu vile atakavyo.

Allah ana utashi kamili. Ameuumba ulimwengu huu kwa mujibu wa utashi wake wa tangu.

Kila kitu ambacho kimetokea na kitatokea ulimwenguni kimetokea au kitatokea kupitia matakwa na utashi wake. Lolote alitakalo hutokea; lolote asilolitaka haliwezi kutokea. Haya yameelezwa katika Qur'an kuhusu jambo hilo.

“Mwenyezi Mungu huumba apendacho. Anapo hukumu jambo, huliambia: Kuwa!Likawa.” (Aal-i-Imran, 47)

Katika hadithi yameelezwa yafuatayo: “Lolote alilolitaka Allah limetokea na lolote asilolitaka halikutokea.”

Hakuna sifa nyingine ya kujitegemea zaidi ya utashi inayoitwa kutamani.

Kwa kuwa utashi ni sifa yenye maana sawa na kutamani. Kwa kweli, Kutamani kunatumika kwa mfanano na utashi katika Qur’an na Hadithi.  

Qudrah (Nguvu):

Nguvu ina maana kwamba Allah mtukufu hufanya vitu kwa viumbe kwa mujibu wa utashi na elimu; ina maana ana nguvu ya kufanya na kuumba kila kitu.

Ulimwengu tuuonao na uzuri na nidhamu isiyo na makosa iliyokuwepo ni dalili yenye nguvu kwamba Allah ana nguvu isiyo na ukomo na ana nguvu juu ya vitu vyote.

Takwin (Kuumba):

Takwin maana yake ni kuvumbua na kuumba. Takwin huelezwa kuwa ni kuumba kitu kutokana na si kitu, kuleta katika kuwepo.

Sam’ (Kusikia) and Basar (Kuona):

Zina maana kwamba Allah anasikia kila kitu na anaona kila kitu.

Mambo kama umbali - ukaribu, usiri - uwazi, giza – nuru haviwi vizuizi kwa kusikia na kuona kwa Allah.

Anasikia minong’ono yetu na dua tuziombazo ndani ya mioyo yetu. Anazijibu kwa mujibu wa hekima yake.

Imeelezwa mara nyingi katika Qur’an kuwa Allah mtukufu ni Sami’ (msikivu wa yote) na Basir (mwenye kuona yote).

Kinyume cha sifa ya kusikia na kuona ni upofu na uziwi, ambazo ni muhali kwa Allah.

Kalam (Kuongea):

Ina maana kwamba Allah, mtukufu, anaongea bila ya kuhitaji herufi na sauti.

Allah ana sifa ya kuongea, hiyo ni kusema, kusema, kuongea. Sifa hiyo ni ya tangu nay a milele. Kwa hivyo, Allah pia huitwa al-Mutakallim (Mzungumzaji). Qur’an imeitwa Kalamullah, ikiwa na maana maneno ya Allah.

Wahay ambao Allah ameuteremsha kwa mitume wake, vitabu vya kiungu alivyowatumia na misukumo aiteremshayo kwa viumbe vyake yote ni madhihirisho ya sifa yake ya kalam.

Maswali juu ya Uislamu

Author:
Maswali juu ya Uislamu
Subject Categories:
Read 1.204 times
In order to make a comment, please login or register
MASWALI YENYE KUFANANA