Nini unafikiria kuhusu msiba wa tarehe 11 Septemba na jaribio la tukio hilo la kuyahusisha mashambulizi mengine ya kigaidi duniani na dini ya Uisilamu?

Submitted by on Sat, 18/08/2018 - 10:38
Dear Brother / Sister,
Mwisilamu hawezi kuwa gaidi; gaidi hawezi kuwa Mwisilamu wa kweli
Uisilamu ni dini ya uvumilivu; Uisilamu unazingatia kuwa kiumbe ni chenye thamani mno; unazingatia uvunjaji wa sheria na mashambulizi dhidi ya watu wasio na hatia ni madhambi makubwa. Kwa hakika, aya ya Quran tuliyoitaja inatangaza kwa kupaza sauti:
‘Aliye muuwa mtu bila ya yeye kuuwa, au kufanya uchafuzi katika nchi, basi ni kama amewauwa watu wote. Na mwenye kumuokoa mtu na mauti ni kama amewaokoa watu wote. Na hakika waliwajia Mitume wetu na hoja zilizo wazi. Kisha wengi katika wao baada ya haya wakawa waharibifu katika nchi.’ (5: 32).
Kwa kweli, Mwisilamu huhudumia maisha tu na sio kifo. Kwa hivyo, lazima tusisahau kanuni mbili kuu za sheria zilizowekwa na Uisilamu:
Ya kwanza: Aya ya Quran: ‘Na habebi mwenye kubeba mzigo wa mwenziwe’ (6: 164). Yaani, mtu mwengine hawezi kuadhibiwa kwa sababu ya mtenda mauaji. Katika sheria, uhalifu na adhabu ni vitu binafsi.
Ya pili: mtu huzingatiwa kuwa hana hatia hadi itakapothibitishwa kuwa ni mkosa. Yaani, hakuna anayeweza kushitakiwa isipokuwa tu ithibitike kuwa ni mwenye hatia. Haizingatiwi kuwa ni haki kumwadhibu mtu bila ya ushahidi. Mtu anazingatiwa hana hatia isipokuwa ithibitishwe kuwa ni mkosa. Yafuatayo yanaripotiwa kutoka kwa Bwana Mtume: ‘Muumini anaweza kujilinda yeye mwenyewe katika muktadha wa dini isipokuwa akiua mtu asiye na hatia kinyume na sheria.’
Kilugha, Uisilamu unamaanisha amani. Hili linaonesha kuwa amani ya kweli ya kiwiliwili na akili inawezekana tu kupitia kumtii Allah na kujisalimisha Kwake. Mwisilamu anakuwa Mwisilamu kamili ikiwa tu anaishi katika amani na maelewano katika jumuia. Maisha ya kumtii Allah na kumwabudu Yeye yataupelekea moyo kukinai na amani ya kweli itafikiwa katika jumuia. ( 13:28-29).
Mitume wote wa Allah waliwafikishia watu ukweli walipowalingania kuja kwenye njia sahihi. Ni muhimu hapa kukumbuka hadithi ya Mtume ifuatayo: ‘ vipo vitu vitatu ambavyo ndio vipengele vya msingi kuhusiana na imani: kuwasaidia watu hata kama mtu ana hali ngumu ya kiuchumi; kuomba amani kwa watu kwa shauku; kuwatendea watu haki kama yeye mwenyewe anavyotaka atendewe kwa haki.
Bwana Mtume pia amesema:
Watu ni kama kundi la mifugo; kila mmoja wa kundi hili anapaswa awe kama mlinzi na mchungaji wa wengine na anapaswa abebe jukumu la kundi zima la mifugo.’
‘Ishini pamoja, shikamaneni, msizozane; rahisishianeni; msitiliane uzito na msifanyiane ugumu.’
‘Mtu anayelala usiku tumbo lake likiwa limeshiba ilhali majirani zake wana njaa basi huyo sio muumini wa kweli.’
‘Mwisilamu ni mtu anayemwabudu Allah na hayadhuru maisha ma mali za wengine.’
Kwa kifupi, Uisilamu haubezi mtu mmojammoja au jumuia. Kwa hakika, una lengo la kuleta maelewano na uwiano kati yao. Ujumbe wa Uisilamu ni kwa watu wote. Kwa mujibu wa Uisilamu, Allah ndiye Mlezi na Muidhinishaji wa Dunia. (1:1). Bwana Mtume ni mjumbe aliyetumwa kwa watu wote. ‘Sema: Enyi watu! Hakika mimi ni Mtume kwenu nyinyi nyote, niliye tumwa na Mwenyezi Mungu’ (7:158). ‘Nasi hatukukutuma ila uwe ni Rehema kwa walimwengu wote.” (21: 107).
Katika Uisilamu, watu wote huzingatiwa kuwa ni sawa bila ya kujali rangi zao, lugha, mbari au nchi. Hatuwezi kukataa, katika zama zilizoitwa zama za mapambazuko leo, kuwa bado vipo vikwazo, ubaguzi na kutendewa tofauti kati ya watu kutokana na sababu tulizozitaja. Uisilamu umetokomeza ubaguzi wa namna zote na upendeleo, na kutangaza duniani kuwa kila mmoja ni sawa kutokana na ukweli kuwa wote ni viumbe wa Allah. Uisilamu una mashiko ya kikweli ya kimataifa; unakataa upendeleo unaogemea rangi, koo, mbari, damu na eneo. Tunakemea aina zote za mashambulizi dhidi ya wanadamu. Tunasikitika kutokana na aina zote za uvunjwaji wa sheria unaowalenga watu wasio na hatia. Uisilamu unakataza mauaji ya kutisha ya watu wengi ambapo watu wasio na hatia huuliwa pamoja na madhalimu. Kwa mujibu wa Uisilamu, hakuna atakaebebeshwa jukumu kutokana na makosa ya wengine.
Uisilamu hauruhusu kuuliwa watu wasio na hatia na wasio na hifadhi. Kama mauaji hayo ya watu wengi yamefanywa na baadhi ya Waisilamu mmoja mmoja kuwa ndio dai la kibaguzi la vyombo vya habari, tutawatangaza madhalimu wote kuwa ni wahalifu na watenda dhambi kwa niaba ya Uisilamu. Tunataka kutilia mkazo kuwa ni muhimu mno kuwaadhibu madhalimu kwa adhabu kali bila ya kumbagua yeyote kwa upande wa kidini, mbari na jinsia.
Tunapokabiliana na matukio hayo, lazima tusisahau kuhusu ukweli kuwa dola mbalimbali na mtu mmoja mmoja: Kama ukiwa ndani ya meli au nyumba na mkiwa na watu tisa wasiokuwa na hatia na mmoja ni muuaji yuko nanyi, mtajua tu ni namna gani mtu huyo anayetaka kuizamisha meli au kuiteketeza nyumba kwa moto alivyo katili. Utapiga mayowe ili kumfanya kila mtu asikie ukatili wake. Hata kama mtu asiye na hatia ni mmoja tu na tisa waliobaki ni wauaji, tena itakuwa ni kinyume na haki kuizamisha meli hiyo au kuiteketeza nyumba hiyo kwa moto. Ni hivyo hivyo kwa matukio ya aina hii, pia. Tunakemea matendo haya ya damu na yasiyo na huruma na tunataka kumkumbusha kila mtu kuwa ni hatari mno kufanya matendo hayo hayo.
Maswali juu ya Uislamu