Sharia ni nini, Sharia imeishi vipi, je, Sharia inafaa katika karne hii?

Submitted by on Wed, 08/08/2018 - 15:33
Dear Brother / Sister,
Uislamu umetanguliza rai zake kuhusu utaratibu wa kiutawala kama ulivyofanya kwenye masuala mengine. Uislamu umeweka kanuni kadhaa kwa ajili ya usimamizi wa dola. Dola inatakiwa iongozwe kwa kuzingatia kanuni kama vile haki, sheria, kutokiuka haki za binadamu, kutotumia vibaya uongozi wa dola, n.k.
Sharia ni jina la hukumu za ujumla na sheria zilizoletwa na Uislamu. Inajumuisha uongozi wa dola, pia.
Lazima tufikishe na tuishi maisha ya Uislamu wa kweli na ukweli unaokubaliana na Uislamu. Kwa hivyo, baadhi ya matumizi yenye kufanyika kwa jina la Uislamu lakini hayakubaliani na Uislamu yana madhara kwa Uislamu na Waislamu.
Unakutana na mtu. Anasema kuwa anaswali na anafunga. Unaendelea kuzungumza na unagundua kuwa mtu huyo anayetekeleza amri hizo mbili muhimu zaidi anapinga Sharia na unapatwa na mshangao.
Unakutana na mtu mwingine. Anaitetea Sharia kwa shauku kubwa. Unapoingia kwa kina katika maisha yake ya ndani na ufanyaji ibada, unagundua kwamba hana hata 1% ya shauku yake anayoionesha katika kutumia sheria ya adhabu ya Kiislamu kwenye ibada yake. Unapatwa na mshangao tena.
Unakuwa na rai inayofanana kuhusu watu hao wawili: Hawaijui Sharia!
Nini sharia na isiyo sharia?
Sharia inamaanisha “dini”, “amri ya Allah”, “amri na makatazo ya Allah”.
Mtu anapaswa kujua maana ya dhana pindi anapoikataa au kuikubali. Kuiunga mkono au kuipinga ni jambo jingine.
Dhana mojawapo inayojadiliwa zaidi ni Sharia. Watu wengi wana kiwewe kuhusu jambo hilo. Kila mmoja anaizungumzia, haijalishi kama wanajua maana yake au hapana.
Kwanza, hebu tuangalie kamusi inayozingatiwa kuwa ni kamusi muhimu zaidi katika lugha yetu, “Qamus” ya Shamsuddin Sami:
Sharia inafafanuliwa kuwa ni, “sheria ya Allah inayotegemea amri na makatazo ya Allah, na kanuni za aya, hadithi na ijma (muafaka) wa ummah.”
Mambo mawili yanavuta hisia katika ufafanuzi huo. Moja ni ukweli kuwa Sharia ni “amri na makatazo ya Allah”. Jingine ni kuwa, sheria hizo za Allah zinategemea juu ya “aya, hadith, na ijma ya ummah.”
Ömer Nasuhi Bilmen anaeleza neno hilo katika kazi yake ya uhakika: “Hukuk-u İslamiyye ve Istılahat-ı Fıkhiyye Kamusu” kama ifuatavyo kwa kirefu:
“Katika lugha ya dini, Sharia ni hukumu zote za kidini na za kidunia, sheria alizoziweka Allah Mtukuka kwa waja Wake. Kwa hivyo, Sharia ni usawe wa dini na inajumuisha kanuni za imani zinazoitwa sheria za msingi, na ibada, maadili na sheria za madai zinazoitwa hukumu za kinaganaga.”
“Sharia inamaanisha sheria ya Allah iliyofikishwa na Mtume kwa mujibu wa maana yake ya ujumla. Inapotamkwa ibara ‘sheria za Sharia’, ni muhimu kufahamu hukumu za sheria ya Allah. Na, kinachomaanishwa na hiyo ni hukumu ambazo zinategemea Quran, hadithi na ijma.”
Nukta kuu zifuatazo zimeorodheshwa kitaalamu katika ufafanuzi wa kinaganaga hapo juu:
1. Allah ameweka Sharia kwa ajili ya Waja Wake.
2. Sharia ni ukamilifu wa hukumu za kidini na kidunia.
3. Sharia ni kisawe cha neno “dini”.
4. Kuna hukumu zote kuhusu maadili, ibada na maisha ya kila siku pamoja na hukumu kuhusu kuamini dhana ya Sharia.
5. Kwa ujumla, sheria ya Allah iliyotambulishwa na kila Mtume inaitwa Sharia.
6. Kinachokusudiwa na Sharia ni dhahiri kuwa ni hukumu zinazotegemea Quran, hadithi na ijma.
Mfasiri (mufassir) mmojawapo wa zama zetu, Elmalılı Hamdi Efendi anaeleza Sharia kama ifuatavyo katika tafsiri yake adhimu iitwayo, “Hak Dini Kur'an Dili”:
“Katika kamusi, Sharia inamaanisha njia inayofuatwa ili kuteka maji mtoni au katika chanzo cha maji. Hutumika kisitiari kwa ajili ya sheria maalumu na njia nyoofu iliyowekwa na Allah kwa wanadamu ili kuwawezesha wafikie maisha ya milele na furaha halisi, inayomaanisha dini.”
There are also some important points that attract attention in that definition, too:
Pia kuna baadhi ya nukta muhimu zinazovutia kutokana na ufafanuzi huo, pia:
1. Allah ameweka Sharia na kuwawajibisha waja Wake.
2. Allah ameshusha Sharia ili Waja Wake wafikie maisha ya milele na furaha halisi.
3. Sharia ni jina la njia ya hukumu nyoofu na sheria mahususi.
4. Sharia inamaanisha dini.
Mwanazuoni mashuhuri mwenye fikra nyingi wa zama zetu, Badiuzzaman, anaeleza yafuatayo alipokuwa akifafanua Sharia:
“Sharia inamaanisha mambo mawili. La kwanza ni Sharia inayoratibu vitendo na hali za mtu, ambaye ni dunia ndogo, inayokuja kutoka katika sifa ya maneno. La pili ni Sharia kubwa ya kimaumbile inayoratibu utendaji na utulizano wa dunia, ambayo ni mtu mkubwa, inayotokana na sifa ya utashi, ambayo wakati mwingine kimakosa huitwa maumbile.”
Kuna nukta kadhaa muhimu katika ufafanuzi huo, pia. Badiuzzaman anaieleza Sharia kwa kuigawanya katika sehemu mbili na kufafanua dhana ya maumbile.
1. Sharia tunayoijua, inayoratibu vitendo na hali za mtu, ambaye ni “dunia ndogo”, inayotokana na sifa ya Allah ya kusema.
2. Sharia inayoratibu utendaji na utulizano wa dunia, ambayo ni “mtu mkubwa”.
3. Ni makosa kuziita sharia katika dunia yakinifu kuwa ni “maumbile” kwa sababu dhana hiyo haidokezi kuhusu Allah. Hata hivyo, Allah ndiye anayeweka na kutumia sheria za kimaumbile.
Maelezo hayo yanadokeza maana nyingine: Dunia hii imepangwa vizuri na kamilifu kwasababu viumbe wa ulimwenguni wanatii sheria za asili za Allah bila ya kuasi. Hakuna dosari hata chembe. Maana yake, kama wanadamu watatii sheria ya Allah bila ya kuasi, watafikia upatanifu walioukosa na furaha wanayoitafuta. Sababu ya kutokupatana na kutokutulia ni uasi na uchupaji mipaka. Ufunguo wa kupata amani duniani upo katika Uislamu kama ilivyo furaha ya ahera.
Kutokana na maelezo hayo yote, mtu anayesema, “Sharia” anasema, “kanuni za kidini”. Mwanadamu ni kiumbe huru.
Anaweza kukubali au kukataa.... “Hakuna kulazimishana katika dini.”
Sharia imeishi vipi?
Allah, ambaye ameipa mbegu uwezo wa kuwa mti na ambaye ameupangilia kuzaa maatunda, ameweka baadhi ya hali za utambuzi wake. Mkusanyiko wa hali hizo unaitwa Sharia ya kimaumbile. Mbegu hiyo inahitaji kupata udongo wake, kukutana na maji na kupata jua ili iwe mti.
Maumbile ya mwanadamu ni kama mbegu hiyo, mbegu inayoweza kuleta uhai Peponi. Sharia ni mkusanyiko wa sheria ambazo mwanadamu anahitajika kutii ili astahiki kuingia Peponi, ambapo ni mahali pa furaha ya maumbile ya mwanadamu.
Akili inaweza kumjua Allah kama itafikiria ndani ya mipaka aliyoiweka Allah. Ulimi unakuwa mteuliwa kwa ajili ya kutamka maneno matukufu katika ardhi hiyo ya milele kwa kusema maneno mema na ya manufaa. Mwili unastahiki kupata manufaa yanayotokana na neema za mali za ardhi hiyo ya furaha kwa sababu ya kujichosha kwake kwa ajili ya Allah.
Kutokana na hisia kama vile upendo, hofu na huruma kwenye jicho, sikio, mkono na mguu, kila kitu kinaboreka, kinanyanyuka na kwenda kwenye ulimwengu wa juu zaidi kama tu vitafanya kazi kulingana na amri za Allah. Sharia ni jina la njia ya kuuendea ukweli. Maana yake katika kamusi ni “njia iliyofuatwa ili kupata maji kutoka katika chanzo cha maji”.
Yunus, mshairi wa kisufi, ameeleza kwa muhtasari njia ya kumfikia Allah na kupata ukweli kama ifuatavyo katika shairi: Sharia na tariqah ni njia kwa ajili ya wanaoweza, tunda la ukweli limo ndani mwake.
Kikomo cha safari hakitaweza kufikiwa bila ya kutembea njiani. Madai ya kuufikia ukweli bila ya Sharia ni hadaa isiyo na lolote isipokuwa kuwavuruga wanaodai umakini wa mwenye kumiliki.
Tariqah ni alama ya ibada ya sunna (nafilah). Ni kitendo cha mafunzo yanayopaswa kufanyika ili kuweza kutembea kwa uimara katika njia ya Sharia na kuwa na nguvu zaidi dhidi ya nafsi na shetani. Ni njia ya mja kujisogeza karibu na Mola wake Mlezi. Inamsaidia mtu kuizoeza nafsi yake kwa ufanisi zaidi.
Kwa kifupi, ni muhimu kutii amri za Allah kwa usahihi na kuendeleza ibada za sunna ili kuufanya moyo wa mtu uwe thabiti na roho yake iwe na nguvu zaidi. Hebu tumsikilize imamu Rabbani:
“Ni Sharia kuuzuia ulimi usiseme uongo na useme ukweli. Kama mtu ataondosha fikra ya kuongopa kutoka moyoni mwake kwa kujibidiisha, ni tariqah; kama ataifanya bila ya shida yoyote, ni haqiqah (ukweli).”
Je, hatuyafahamu yafuatayo kutokana na mfano mzuri wa imamu huyo mashuhuri? Kusema ukweli muda wote. Ni maadili ya juu ambayo Allah ameridhika nayo, ambayo ni haqiqah. Mja kwanza anatakiwa atii amri ya Sharia, “usidanganye” ili kufikia haqiqah hiyo; auepushe ulimi wake mbali na dhambi hiyo. Kisha, anaanza kutibu roho yake ili hali ya kutaka kudanganya isijitokeze moyoni mwake. Anaanza kujitahidi kuitambua. Mwishowe, moyo unaanza kuchukia kusema uongo bila ya kuulazimisha au kufanya bidii. Kutokea hapo na kuendelea, uongo hautaukaribia moyo huo. Anapozungumza, kwa hakika atasema ukweli kirahisi. Mtu huyo anazingatiwa kuwa amefikia haqiqah ya kusema ukweli.
Inafahamika kutokana na kauli ya imamu mashuhuri kuwa inawezekana kupata mwisho mwema bila ya tariqah. Mtu anaweza kupata fursa ya kupata haqiqah moja kwa moja kutoka katika Sharia. Hata hivyo, ni hakika kuwa fursa hiyo haitaweza kuwepo bila ya Sharia.
Sitaki kufanya uchambuzi wa tasawwuf (usufi) hapa. Nimeandika sentensi kadhaa hapo juu ili kueleza kuwa haitakuwa timilifu kufahamu kanuni za Uislamu tu kuhusu sheria ya adhabu pindi dhana ya Sharia inapotajwa. Kutokuongopa pia ni Sharia. Mtu asiyedanganya, hasengenyi, haingilii mali, maisha na wake wa watu yuko katika njia ya Sharia na haqiqah. Kama mtu wa namna hiyo atapinga Sharia, atakuwa anajipinga mwenyewe.
Msingi wa dini umeegemea katika kuumbwa kwa mwanadamu. Kuwepo kwa ulimwengu wa viumbe visivyo hai. Kila chembe, nyota, hewa, udongo, maji, mwangaza, kwa kifupi, kila kitu kinategemea utashi enevu wa Allah. Vinashughulika kulingana na sheria ya Allah aliyoiweka. Kila kitu kinatii Amri Zake kulingana na utashi Wake. Ulimwengu wa malaika unatoa uoni mwingine wa ukweli. Viumbe hao, walioumbwa ili kufanya ibada, kumtukuza na kumsifu Allah, hawana utashi kama wanadamu walivyo. Wanatimiza amri zote za Allah.
Ama kuhusu mwanadamu, analeta mtazamo tofauti kabisa katika rangi ya maumbile. Kila seli na kiungo cha tunda la hisia la ulimwengu linalomtukuza Allah linadumu katika kumtukuza na kumwabudu Allah. Usimamizi wao haumtegemei mwanadamu. Yeye mwenyewe hawezi kulifanya ini lake lifanye kazi; hawezi kuifanya damu mwilini mwake izunguke kwa kufuata utashi. Sultani huchaguliwa katika nchi ya mwili ambaye humtii Allah pamoja na seli zake zote: Roho hupewa utashi kama Baraka kubwa na mtihani.
Mwanadamu ana hiari na utashi. Anaweza kuashiria upande wowote autakao kwa kidole; anaweza kugeuza uso wake upande wowote anaoutaka. Anaweza kutumia hisia zake zote alizonazo kadiri atakavyo. Anaweza kwenda popote anapotaka, kula chochote anachotaka na kuepuka chochote asichokipenda.
Utashi huo unakabiliwa na zawadi na mtihani, na hatimaye ni Peponi na Motoni.
Hivyo, Sharia ni mfululizo wa amri na makatazo yanayoamuru utashi wa binadamu kubakia ndani ya mipaka ya eneo analoliridhia Allah na yanayouonya utashi wa binadamu kujiepusha na eneo asiloliridhia Allah. Mja ameamrishwa ashikamane na kamba ya Allah.
Kuna maeneo mawili mbele ya utashi wa binadamu. Moja ni dunia, na jingine ni ahera. Hata hivyo, kuna sheria na kanuni zilizowekwa kwa ajili ya mambo yote ya kidunia. Kama mja atazitii, atazingatiwa kuwa ameabudu na ataendesha maisha yake ya kidunia kirahisi zaidi na kwa furaha.
Tunaona kuwa mijadala kuhusu Sharia kwa kawaida hufanyika katika kundi la pili. Kundi hilo la pili limegawanyika katika sehemu mbili: mahusiano ya kijamii na adhabu. Kitovu cha mijadala inayohusu Sharia ni sehemu ya mwisho. Kwa hakika kuna hukumu nyingi sana zilizowekwa na Uislamu kuhusiana na sheria ya adhabu. Hizo ni sehemu ya Sharia hiyo na ni muhimu kuziamini. Mtu asiyezitii atawajibika kama amri na hukumu zingine. Kutokutii amri hiyo kunamfanya mtu awe mwenye dhambi kama uasi huo una namna ya usugu na kumwasi Allah. Kama mtu huyo atakana na kukataa amri hiyo ya Allah, kuwa hukumu inayotokana na Quran na sheria, anakuwa kafiri. Hata hivyo, Uislamu si hukumu hizo pekee na dini haina amri hizo peke yake. Ili kushughulikia jambo hilo peke yake katika uwanja huo itakuwa tathmini potofu na ufahamu usio sahihi.
Hukumu za Kiislamu zimegawanyika katika makundi matatu makuu yafuatayo. La kwanza ni majukumu ya mtu kwa nafsi yake. La pili ni majukumu yake kwa familia yake. Na la tatu ni majukumu yake katika maisha ya kijamii. Kuna vigezo na hukumu ambazo Sharia imezileta kuhusu wao. Inazingatiwa kuwa ni ukafiri kuikataa yoyote ile na ni dhambi kutokuitii yoyote katika hizo. Hata hivyo, lenye kipaumbele ni majukumu ya mtu kwa nafsi yake. Na jukumu muhimu zaidi kuliko yote ni ibada. Kuna hukumu zinazohusu wajibu wa mtu kwa nafsi yake na familia yake katika vitabu vitukufu vyote. Ibada imeamrishwa kwao wote, na kuyaepuka madhambi kunazingatiwa kuwa ni lazima.
Kuna tofauti kadhaa katika umbo, muda na kiasi cha ibada lakini haiwezekani kuonesha dini isiyoamrisha ibada na maadili ya juu. Hata hivyo, kanuni za kijamii, hususani hukumu zinazohusu usimamizi wa dola zipo kikamilifu katika Uislamu, ambayo ni dini kamilifu na ya mwisho.
Tunapaswa kueleza hususani yafuatayo: Lengo la kuumbwa kwa mwanadamu lipo katika dini zote. Kusudio ni kueleza kama ifuatavyo katika aya iliyo katika Quran: “Sikuwaumba majini na wanadamu isipokuwa waniabudu”. Pia kuna baadhi ya amri na makatazo yanayozingatia utambuzi wa hali kadhaa. Mojawapo ni hukumu zinazohusu sheria ya adhabu. Hukumu hizo zinategemea mazingira. Waislamu wanaoishi Ujerumani, Uingereza, Ufaransa hawana uwezo wa kutumia amri hizo. Na hawawajibiki nazo.
Katika mijadala inayohusu jambo hilo, itakuwa ni uonevu kumwonesha muumini kama mtu asiyekubali baadhi ya amri za Uislamu na kumkosoa. Ni muhimu kuepuka tuhuma za namna hiyo zinazoharibu undugu wa Kiislamu na ambazo adhabu zake ni kali huko ahera.
Fikiria nchi ambayo watu wake ni masikini. Je, unaweza kuwatuhumu watu wa nchi hiyo kwa kutokutimiza wajibu wa zaka? Bila ya shaka hapana. Hali hiyo si sawa na ya Muislamu anayeamini sheria za adhabu ya Kiislamu lakini hawezi kuzitumia? Ni wajibu wa dola kuzitumia. Kwa hivyo, mtu mmoja hana jukumu lolote kuhusu jambo hilo.
Kanuni za msingi za Uislamu ni amri za Allah ambazo mtu anapaswa kutii bila ya kujali mahali alipo.
Hukumu zinazohusu usimamizi wa dola ni amri za Allah, pia; ni wajibu kwa kila muumini kuziamini lakini hana wajibu wa kuzitumia.
“Sharia inahusiana na maadili, ibada, ahera na inafaidisha 99%. Inahusiana na siasa 1%. Watawala wanapaswa waifikirie.” Badiüzzaman.
Ningependa kutaja vigawanyo vya hukumu za Kiislamu. Hukumu za Allah zimegawanyika katika sehemu mbili: baadhi yake ni hukumu zinazotumika kwa ajili ya Waislamu tu; zingine ni hukumu zinazotumika kwa kila mmoja anayeishi nchi ya Kiislamu. Sehemu ya pili ni hukumu na sheria zinazohusu mahusiano ya kijamii na adhabu. Kama asiye Mwislamu atalipa jizyah (kodi ya kichwa inayotozwa kutoka kwa ambao hawakusilimu, lakini wanataka kuishi chini ya himaya ya Uislamu), anakuwa chini ya hukumu zote zinazohusu mahusiano ya kijamii na adhabu kama raia wa nchi hiyo. Kama ataiba kitu, atakatwa mkono wake; kama atamkashifu mtu kuhusu uzinifu, ataadhibiwa. Baadhi ya watu wanatathmini jambo hilo kinyume na wanasema maneno yaliyovurugika yanayowafanya wawajibike kama vile, “haina maana kuswali na kufunga katika nchi ambayo sheria ya Kiislamu ya adhabu haitumiki”. Wanawatuhumu Waumini wanaowapinga kwa kutozingatia baadhi ya hukumu za Allah.
Kwa hakika, dai hilo linakuwa halali kwao. Wanafanya kosa kwa kupuuza hukumu zainazounda asilimia tisini na tisa ya Sharia na ambazo ni misingi ya dini na kwa kuzipa umuhimu zaidi hukumu na sheria za mahusiano kijamii na adhabu zinazotumika kwa kila mmoja, awe Muislamu au asiye Muislamu, na zinazohakikisha amani na furaha ya jamii.
Muumini anayesoma surat al-Fatiha katika kila rakaa ya swala na kumwomba Allah amwongoze kwenye “njia iliyonyooka” anapaswa awe makini. Kila namna ya msimamo mkali, iwe kwa kupuuza au kuzidisha, inamwondoa mtu kutoka katika njia iliyonyooka.
Je Sharia inafaa katika karne yetu?
Tutataja namna mbili za msimamo mkali kuhusu jambo hilo hapa. Huku baadhi ya watu wakidai kuwa haiwezekani kutawala kwa sheria za Uislamu katika karne hii, wengine wanamlaumu kila asiyetawala kwa sheria za Uislamu kwa ukafiri bila ya kuzingatia nia zao. Kundi moja linakichofanya ni kupuuza na jingine linachokifanya ni kuzidisha kiasi. Maana yake, yote mawili yana msimamo mkali; wamekengeuka kutoka katika njia iliyonyooka.
Tunataka tuanze kutaja kosa la kwanza. Kuna kanuni mashuhuri. “Kama jambo limeamuliwa, linakuwa limeamuliwa pamoja na namna ya kulifikia, vifaa na zana.” Tunapotaja mkono, vidole huukamilisha. Hutaweza kuufikiria mkono bila ya vidole. Hutaweza kunufaika kutokana na mkono bila ya vidole. Tunapotaja uso, hutaweza kutenganisha macho kutoka usoni. Uso bila ya macho ni kitu kisicho kamili. Huwezi kutenganisha weupe wa macho mbali na weusi wa macho, pia. Kidole ni sehemu inayokamilisha mkono; jicho ni ukamilisho wa sehemu ya uso na mboni ya jicho ni ukamilisho wa sehemu ya jicho. Sheria za Kiislamu ni kama hivyo pia. Lazima ziwe fikra kwa ukamilifu wake. Ni hapo ndipo inaweza kumboresha mtu mmoja na jamii na kuwaongoza kwenye amani na furaha.
Katika jamii ambapo misingi ya Uislamu inapuuzwa na maisha ya mtu mmoja mmoja na familia yanaegemea juu ya kanuni zilizo potovu, kutumia tu sheria zinazohusu maisha ya kijamii na adhabu hazitakuwa na manufaa yoyote. Pengine isiwezekane kutumia sheria hizo katika jamii ya aina hiyo. Hata kama itawezekana, watu wengi watazitii bila ya kuziamini na bila ya kutaka, kwa kuangukia katika unafiki. Mtu anaonekana kama Muislamu lakini anaishi kama adui wa Uislamu.
Ningependa kutoa mfano kuhusu ukweli kuwa Sharia lazima zitathminiwe kuwa ni kitu kamili. Katika Uislamu, riba ni haram, imekatazwa. Ni muhimu kuzingatia aya inayohusu riba pamoja na aya ifuatayo, “Waumini si vinginevyo bali ni ndugu”. Kisha, ukweli ufuatao utadhihirika: “Muumini anapomkopesha mali nduguye aliye katika haja muhimu na anayemwomba mkopo, hatataka arudishiwe na ziada. Hiyo haiendani na undugu.”
Katika jamii ambapo undugu wa Kiislamu umedhoofika, ambapo mtu anajaribu kumhadaa nduguye na ambapo mali ya dola inaporwa pasi na huruma, kama makatazo ya riba hayawezi kutumika, ni kosa la muundo potofu, si kosa la dawa au chakula.
Ama kuhusu dai la pili linalovuka mipaka ya unyoofu, si haki kumwita ni kafiri mtu asiyeutumia Uislamu kikamilifu na asiyetawala au hawezi kutawala kulingana na Uislamu. Imani ni kinyume cha ukafiri. Kama mtu anatoa hukumu kinyume na Uislamu au anatumia lililo kinyume na Uislamu, atakuwa ni kafiri kama tu atalifanya hilo kwa kuukataa Uislamu. Vinginevyo, dhambi yake au dhuluma inaweza kutajwa na si ukafiri wake. Kuna sharti la nia na utashi katika imani na ukafiri. Mtu anazingatiwa kuwa ni kafiri kama tu atasema, “hukumu za Kiislamu kuhusu jambo fulani ni kadhaa lakini halikubali na kulifanya”. Kama hana nia au utashi kama huo na kama hukumu yake potofu inakuja kutokana na ujinga wake au udhaifu wa utashi wake na kama anajua kuwa anachokifanya si sahihi, haiwezekani kumwita kafiri kwa mujibu wa hukumu ya Ahl Sunnah. Wakhawariji tu, ndio wanaoamuru kuwa mwenye kutenda madhambi makubwa anakuwa ni kafiri, na Mutazilah, wenye rai kuwa mtu wa aina hiyo yuko baina ya imani na ukafiri, wanaweza kudai hivyo. Wanazuoni wote wa Ahl Sunnah wanaafikiana kuwa Wakhawariji na Mutazilah wamekengeuka kutoka katika lililo sahihi.
Lazima tuwe makini sana. Tunaweza kukengeuka kutoka kwenye lililo sahihi na wakati huo huo tunadhania kuwa tunautetea Uislamu.
Maswali juu ya Uislamu